Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

PRINCE WILLIAM ATEMBELEA HIFADHI YA MKOMAZI, AJIFUNZA NAMNA FARU WEUSI WANAVYOTUNZWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Elizabeth II Prince Willium ametembelea hifadhi ya Mkomazi iliyopo Tanga na hii ni katika ziara yake ya siku 7 kwa nchi za Tanzania, Kenya na Namibia. 
 Akiwa katika hifadhi hiyo Prince alifanikiwa kujionea namna faru weusi wanavyolindwa na kuongezeka zaidi, ambapo imeelezwa kuwa aina hiyo ya wanyama hupungua kutokana na ujangili na ongezeko la watu nchini. 
 Pia amejifunza namna faru hao wanavyoongezeka kwa kuzaliana na hadi sasa kuna takribani ya faru wasiopungua 50 katika hifadhi hiyo na wataalamu mbalimbali wamesema kuwa wanapiga vita na kuimarisha sekta ya ulinzi ili kuweza kukomesha ujangili unaopunguza wanyama mbugani. 
Prince Willium ametembelea Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika akiwa Rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya "United for Wildlife" na "Tusk Trust" na akiwa nchini alipokelewa Ikulu na Rais Dkt. John Magufuli na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala.
Aidha katika ziara hiyo katika hifadhi hiyo Prince ameshuhudia namana watoto wanavyopewa elimu kuhusiana na utunzaji wa wanyama na baadaye kujiunga katika timu za ulinzi kwa wanyama.



Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Elizabeth II Prince Willium aakiwa na faru alipotembelea  hifadhi ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya siku nne nchini.
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Elizabeth II Prince Willium akiwa mwenye furaha baada ya kushuhudia ongezeko la  faru alipotembelea  hifadhi ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya siku nne nchini.

Dkt. Pancras Bujulu ateuliwa kuwa Mkurugezi Mkuu VETA

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 1, 2018

You Alone (God) - Regina Avit (Official Audio)

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUKUZA UELEWA WA SHUGHULI ZA JUMUIYA HIYO KWA WANANCHI WAKE

$
0
0
Zamaradi Kawawa, MAELEZO, Windhoek, Namibia 

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC zinatakiwa kukuza uelewa wa shughuli za SADC kwa wananchi wake kwa kufundisha mashuleni historia ya ukombozi wa nchi hizo pamoja na kutumia wimbo wa SADC na bendera yake kwenye shughuli za kitaifa na kimataifa.

Baraza la SADC la Mawaziri wa nchi wanachama wanaoshughulikia sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na Uchukuzi walikubaliana hayo katika kikao kilichofanyika Septemba 27,2018 Windhoek, Namibia baada ya kufunguliwa na Waziri wa Madini na Nishati wa Namibia Mheshimiwa Tom Alweendo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilisema wananchi wa SADC wanatakiwa kuelimishwa kuhusu SADC kwa kufahamu historia yake na ukombozi wa nchi wanachama, alama za SADC zikiwemo bendera, nembo, wimbo na itifaki yake kwa kuhusisha elimu hiyo kwenye mtaala wa elimu kwa nchi wanachama.

Akifungua kikao hicho, Waziri wa Madini na Nishati wa Namibia Mheshimiwa Alweendo alisema kuna taarifa nyingi nzuri za kuwaeleza wananchi wa nchi wanachama kuhusu SADC hivyo ni jukumu la Serikali za nchi za SADC kuelimisha na kuwaeleza wananchi wake wakati chombo hicho kkiendelea kujiimarisha.

Kikao hicho cha siku moja kilichokutana kwa lengo la kupitia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi wanachama kwenye maeneo ya sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na uchukuzi kilisimama kwa dakika moja kabla ya kuanza ili kuonyesha masikitiko yao kwa vifo vya watanzania zaidi ya 200 vilivyotokana na ajali ya MV Nyerere Ziwa Victoria, Mwanza.

Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bi. Susan Mlawi kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambaye kwa niaba ya Serikali alipokea salamu za pole kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo kufuatia vifo vya watanzania zaidi ya 200 vilivyotokana na ajali ya MV Nyerere kwenye Ziwa Victoria mkoani Mwanza hivi karibuni.

Aidha, Kikao hicho kiliipongeza Tanzania kwa kupata tuzo ya dunia ya usalama wa anga baada ya kufaulu kwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na Baraza la usafiri wa anga duniani vinavyohusu uhakika wa usalama wa anga.Wakati wa kikao hicho cha baraza la SADC la Mawaziri wa sekta za Mawasiliano, Habari, Ujenzi na Uchukuzi, Bi Mlawi alieleza nia ya Tanzania ya kupeleka mgombea kwenye nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na kuomba ushirikiano wa nchi wanachama wa SADC wakati wa uchaguzi ukifika.

Alimtaja mgombea huyo kuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr Agnes Kijazi, mwanamke msomi wa ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD) mwenye uzoefu wa miaka 30 kwenye masuala ya hali ya hewa kutoka nchi za SADC.Mheshimiwa Alweendo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho alisema nchi wanachama wa SADC zimepiga hatua kubwa kwenye masuala ya hali ya hewa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya satellite iliyoimarisha kwa kiasi kikubwa matokeo ya utabiri wa hali ya hewa hivyo kuwezesha nchi kukabiliana na majanga ya ukame, mafuriko na moto yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr. Agnes Kijazi ambaye pia alitambulishwa katika kiako hicho aliiambia Idara ya Habari-MAELEZO kuwa Tanzania inajipanga kutekeleza miradi miwili mikubwa ya SADC ikiwemo uboreshaji wa chuo cha yaifa cha hali ya hewa kilichopo Kigoma pamoja na uwekaji wa miundo mbinu ya kisasa ya utabiri wa hali ya hewa itakayoimarisha huduma za utabiri wa hali ya hewa kwa nchi ili kupunguza umaskini. 

Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC ina nchi wanachama 16 zikiwemo Namibia ambaye ni mwenyekiti na Tanzania ni Makamu mwenyekiti wa Jumuiya hiyo. Nchi nyingine ni Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika Kusini, Botswana, Angola, Msumbiji, Eswati, Lesotho, DRC, Mauritius, Comoro, Seychelles na Moroco. 

MSANII WA BONGO MOVIE RADO ALIPOZUNGUMZA NA WANA HABARI LEO JIJINI DAR

NEWS ALERT: Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akaribishwa rasmi ofisini kwake

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB  Bw. Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles. Kimei (kulia) wakati alipowasili rasmi kazini kwa siku ya kwanza leo Oktoba 1, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Bw. Ally Laay.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akipokea vitendea kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles Kimei wakati alipowasili rasmi kazini kwa siku ya kwanza, Oktoba 1, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, Dkt. Charles Kimei (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, (wa pili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji,

TIGO FIESTA 2018 – VIBE KAMA LOTE YAACHA GUMZO MOROGORO

$
0
0
Msanii wa Bongo Flava - Ben Pol akitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii.

Msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote, umeanza kwa kishindo katika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro huku wasanii wa nyumbani wakifanya onesho bab-kubwa lililoacha gumzo midomoni mwa maelfu ya mashabiki waliofurika kushuhudia tamasha hilo la kila mwaka. 

Milango ilifunguliwa saa kumi na mbili kamili na kushuhudia wasanii wanaochipuka walioshiriki katika shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota wakifungua jukwaa. Wasanii hao wachanga kutoka mjini Morogoro waliongozwa na washindi Supa Nyota kimkoa, Michael Yusufu (Belly 255) na Abdul Michael (V Dax). 

Shangwe kubwa zaidi zililipuka wakati kundi linalokuja kwa kasi la Mesen Selekta pamoja na msanii Whozu anayetambaa na wimbo wake wa Huendi Mbinguni walipopanda jukwaani na kusababisha vumbi kutifuka miongoni mwa mashabiki huku wengi wakisikika wakinongona kuwa vijana hao ni moto wa kuotea mbali katika tasnia ya sasa ya bongo flava.
Msanii wa Bongo Flava - Dogo Janja akitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii.

Wasanii wengine waliofanya kazi kubwa kukonga mioyo ya mashabiki ni pamoja na kundi la Rostam linaloundwa na wasanii Roma na Stamina, , Fid-Q aliyeambatana na msanii wa kike wa mziki wa kufokafoka Rosaree, Ben Pol, Mr Blue Kabayser, Dogo Janja, Maua Sama , Nandy, pamoja na Belle 9 ambaye ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda jukwaani kama msanii mwenyeji wa Morogoro. Wasanii wote walionesha uwezo mkubwa wa kuimba na kumiliki jukwaa, huku wote wakiwa wamejiandaa kikamilifu pamoja na wacheza dansi waliokuwa wamevalia sare za kuvutia.  

Msanii mkongwe ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi – Professor Jay ambaye aliambatana na wasanii wengine wakongwe ikiwemo Black Rhino waliwashangaza mashabiki ambao hawakutegemea ujio wa wasanii hao wakongwe kwa kufanya onesho la kukata na shoka, na kuwafanya hata wale waliokuwa wameanza kutoka uwanjani kurudi ndani na kukesha hadi jogoo wanawika.
Msanii wa Bongo Flava - Nandy akitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii.

Akizungumza katika onesho hilo lililoshirika 100% wasanii wa nyumbani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe alisema kuwa mbali na shamrashamra za mwanzo wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, msimu huo ulikuwa umeibua fursa nyingi za biashara katika mji huo. 

‘Tunatambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Bali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa wetu, pia imeongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,’ alisema mkuu huyo wa mkoa.  

Kuendana na msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo pia inaendesha promosheni za kusizimua kwa wateja wake ikiwemo ile ya kutoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha tiketi kilichotangazwa kwa kila mkoa husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888. 
Wasanii wa Bongo Flava - Roma (kushoto) na Stamina (kulia) wanaounda kundi la Rostam wakitumbuiza katika ufunguzi wa matamasha ya mwaka huu ya Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi usiku. Tamasha hilo linahamia katika mji wa Sumbawanga mwisho wa wiki hii. 

Wateja wa Tigo pia wanapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi za thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH 10 milioni. Kushiriki wateja wanapaswa kujiunga kwa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia. 

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu litashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam. 


TTCL NA MKOA KWA MKOA TOUR

BENKI KUZITAMBUA HATI ZA HAKIMILIKI ZA KIMILA

$
0
0
Mratibu wa Mradi wa kuwezesha umilikishaji ardhi (LTSP) akitoa taarifa fupi ya mradi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na wafadhili wa mradi mjini Ifakara kabla ya kuanza ziara ya uwandani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya (kulia) wakitia saini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi ya kijiji cha mbuyuni ambapo pamoja na viongozi hawa, wafadhili wa mradi na wafanyakazi wa LTSP walishiriki katika ziara hii.
Afisa Ardhi mteule wa Wilaya ya Kilombero Syabumi Mwaipopo (alioyeshika karatasi) akiwaelezea Naibu katibu mkuu pamoja na wafadhili mchakato mzima wa kuipata hati ya hakimiliki ya kimila inavyopatikana.
Mmoja wa watumishi wa LTSP akiwaonesha wageni jinsi kazi ya kupima vipande vya ardhi inavyofanyika uwandani.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kukagua majina yao kama yapo sawasawa kabla ya hati kuchapishwa. Hili ni zoezi muhimu katika kuhakikisha hakuna makosa katika hati itakayochapishwa.

SERIKALI  imedhamilia kuunda mpango mkakati utakaoziwezesha benki nyingi nchini ziweze kutambua hati miliki za kimila ili kuwawezesha  wananchi kujikwamua kiuchumi wakitumia hati zao kama dhamana ya mikopo. Azma hiyo imekuja baada ya kuona mafanikio ya kupima na kurasimisha Ardhi katika Wilaya tatu za mfano za Kilombero,Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro kulikofanywa na wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP).

Akizumgumza baada ya kutembelea Wilaya za Kilombero na Ulanga akiambatana na wafadhili Wa mradi Wa LTSP ili kuona hatua za utekelezaji Wa mradi,Naibu Katibu Mkuu Wa wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mathias Kabundugulu amesema Mradi huo umetekeleza kwa vitendo Sera ya wizara ya miaka mitano. Amesema kwa kipindi cha miaka miwili toka kuanzishwa kwa mradi Wa LTSP mwaka 2016 mafanikio makubwa yameonekana kwa zoezi kwenda kwa haraka zaidi na wananchi wengi kupata hatimiliki za kimila na za vijiji na hiyo ni kutokana na kwenda na teknolojia mpya ya upimaji ya kutumia simu tofauti na teknolojia waliyoanza nayo ikiwemo ya kutumia GPS.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa pia amebaini  wananchi katika Wilaya hizo wameupokea vizuri mradi na wameonyesha matumaini na imewapanua kiakili hasa baada ya kuelewa kuwa hati hizo wanaweza kuchukulia mkopo baada ya baadhi ya benki kuanza kuzipokea na kuwapatia mikopo. Hata hivyo Kabundugulu ameonyesha kufurahishwa baada ya kuona akinamama wengi kumiliki hati na kusema kuwa serikali wanajivunia kwani wanaweza kumiliki nguvu ya kiuchumi.

Akizungumzia Mpango Wa wizara kulitunza Bonde LA mto Kilombero,Kabundugulu amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya Maliasili na utalii wiki ijayo watatuma timu ya wapimaji na kuweka kambi katika vijiji vyote vyenye muingiliano Wa mipaka na eneo la hifadhi ili kuweka mipaka na kuwaondoa wavamizi wote ili kunusuru eneo hilo ambalo asilimia 65 ya Maji yake yanaingia katika mto Rufiji.

Naye Mkuu Wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya amesema mradi umekuwa na faida kwa wananchi Wa Wilaya yake kwani umemaliza migogoro ya wakulima na wafugaji sambamba na kupunguza migogoro ya mipaka baina ya kijiji na kijiji.

Kwa upande wake Mratibu Wa mradi Wa LTSP Godfrey Machabe amesema toka kuanza kwa mradi wamejaribu kutumia teknolojia tofauti ili kuendana na kasi ya kupima na kuwapatia hati wakazi Wa Wilaya hizo na teknolojia  ya kutumia simu ndio imekuwa na mafaniko makubwa na ana imani ikiendelea kutumika itasaidia kurahisisha upimaji katika maeneo mengi nchini. Machabe ametaja mafanikio ya mfumo Wa kutumia simu kuwa toka waanze kuutumia takribani kwa siku katika wilaya hizo wanazalisha vipande vya Ardhi 1800 tofauti na zamani walipotumia mifumo mingine walikuwa wakizalisha vipande vya Ardhi 400 tu kwa Siku.

TTCL INAKULETEA MKOA KWA MKOA TOUR NDANI YA KAHAMA NA TABORA

MAPATO SIMBA NA YOUNG AFRICANS MILIONI 404,549,000

$
0
0
Mchezo namba 72 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara(TPL) kati ya Simba na Young Africans uliochezwa Jumapili Septemba 30,2018 Uwanja wa Taifa umeingiza mapato ya jumla ya shilingi milioni 404,549,000.

Mchezo huo ulioanza saa 11 jioni umeingiza jumla ya Watazamaji 50,168.

Mgawanyo wa mapato hayo ni kwenye upande wa VAT,Selcom,TFF,Uwanja,Simba,TPLB,gharama za mchezo,BMT na DRFA.

Kati ya fedha hizo VAT ambayo ni asilimia 18 ni shilingi milioni 61,710,864.41,Selcom milioni 17,901,293.25.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) milioni 16,246,842.12,Uwanja milioni 48,740,526.35.

Wenyeji wa mchezo Simba milioni 194,962,105.41,TPLB milioni 29,244,315.81,gharama ya mchezo 22,745,578.96,BMT milioni 3,249,368.42 na DRFA milioni 9,748,105.27

SUKOS KUTOA ELIMU JINSI YA KUJIKINGA NA MAAFA, MAJANGA KWENYE JAMII

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii

TAASISI isiyo ya kiserikali SUKOS inayomilikiwa na Kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova imezinduliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kova Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2014  ambayo inatoa , huduma ya uokoaji,usimamizi,uhamasishaji wa jamii kuhusiana na namna ya kukabiliana na maafa ya aina mbalimbali ikiwa ni harakati za kuunga mkono juhudi za Serikali kukabiliana na maafa na majanga .

Kova ameeleza mabadiliko ya nchi yetu kwa sasa   haiwezi kuepukana na majanga na kutokana na uzoefu na  utendaji wake wa kazi na Jeshi la Polisi lilitoa msaada wa hali na mali kuhakikisha wananchi wanarudi Kwenye maisha yao ya kila siku.

 Kova ameyataka  kwa mashirika yasiyo ya Serikali  kusaidia wananchi wanaofikwa na kadhia hiyo ili kupata hifadhi kwa muda pamoja na chakula.Hata hivyo  ametoa pole kwa  ajari iliyotokea Mkoa wa Mwanza kwa kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere mkoani Mwanza Katika Wilaya ya Ukerewe  na kusababisha athari kubwa ya kimaisha na mali katika jamii.

Aidha, amefafanua kazi ya taasisi hiyo ni  kutoa elimu kuhusu namna ya kujiokoa katika maafa ikishirikiana na kampuni ya CocaCola,Taasisi ya Mpango wa Taifa ya Damu salama,na Cops Security.Pia amesema tarehe sita kutakua na  mbio za mwendopole ambazo zitafanya katika Uwanja Taifa kuelekea viwanja vya Jakaya M. Kikwete saa moja asubuh pamoja na tukio la uchangiaji wa damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa hospitalini.

Kova ametoa rai kwa wananchi kujitokeza Oktoba  6 ili kujifunza vingi likiwemo suala la kujikinga na kujiokoa kwenye majanga na maafa yatakayotokea mahali popote .
 

TAIFA STARS YAANZA KAMBI KUJIANDAA DHIDI YA CAPE VERDE KUFUZU AFCON

$
0
0
Kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaanza rasmi leo kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Africa mwakani dhidi ya Cape Verde.

Kambi hiyo inayoanza leo itaanza na wachezaji wanaocheza ndani kabla ya kuungana na wale wanaocheza nje ya Tanzania.

Mazoezi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager yanatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye Uwanja wa JKM Park,MNAZI Mmoja.Maandalizi yatakuwa chini ya Kocha Mkuu Emmanuel Amunike,Wasaidizi Hemed Morocco na Emeka Amadi.

Madaktari Dr Richard Yomba na Gilbert Kigadya

Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 12,2018 kwenye mji wa Praia huko Cape Verde na mchezo wa marudiano utachezwa Oktoba 16,2018 Uwanja wa Taifa.

Kikosi kilichoitwa

Aishi Manula (Simba)
Salum Kimenya(Tz Prisons)
Frank Domayo(Azam FC)
Salum Kihimbwa(Mtibwa),
Kelvin Sabato(Mtibwa)
David Mwantika(Azam FC) 
Ally Abdulkarim Mtoni(Lipuli)
Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )
Beno Kakolanya (Young Africans)
Hassan Kessy (Nkana,Zambia)
Gadiel Michael (Young Africans)
Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini)
Aggrey Morris (Azam FC)
Andrew Vicent (Young Africans )
Himid Mao (Petrojet,Misri)
Mudathir Yahya (Azam FC)
Simon Msuva (Al Jadida,Morocco)
Rashid Mandawa (BDF,Botswana)
Farid Mussa (Tenerife,Hispania)
Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium)
Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan)
Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania)
Yahya zaydi(Azam FC)
Kelvin Yondan (Young Africans)
Paul Ngalema (Lipuli)
Jonas Mkude (Simba)
John Boko (Simba)
Shomari Kapombe (Simba)
Feisal Salum (Young Africans)
Abdallah Kheri (Azam FC)

MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MFANYABIASHARA, Hafidhi Jonggradgorn amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kukiri kutenda makosa wawili likiwemo la kukutwa na madini ya Coloured Gemstones yenye usurp Wa kilogramu 67.76 na thamani ya USD 105.757.

Aidha Mahakama imeamuru madini hayo yataifishwe na wapewe Tume ya Madini. 

Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori kumsomea mashtaka mshtakiwa huyo na alikiri makosa yote.

Akisomewa hati ya mashtaka, imedaiwa Kati ya Januari Mosi 2017 na June 3 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, nchi za Falme za Kiharabu na India mshtakiwa akiwa si mtumishi wa umma kwa makusudi alifadhili biashara ya mchongo wa jinai kwa lengo la kujipatia faida. 

Katika shtaka la pili, Wakili Nyantori amedai Juni 3 mwaka huu maeneo ya Mikocheni A mtaa wa Chwaku mshtakiwa huyo alikutwa na vito vya madini ya Coloured Gemstones Kilogramu 67.76 yenye thamani ya Dola za Marekani USD 105.757 bila ya kuwa na leseni na uhalali wa kuwa na madini hayo.

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo Wakili Nyantori aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali itakayokuwa fundisho kwa wengine wanaofanya makosa kama hayo. Pia ameiomba Mahakama kutoa amri ya kutaifisha madini hayo kwa mujibu wa sheria na kuelekeza yawe chini ya Tume ya madini.

Katika utetezi wake, wakili wa Utetezi Habibu Mwenye anayemtetea mshtakiwa ameiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwani anafamilia inamtegemea na kuwa Mtejatu wake huyo tangu alipoingia nchini mwaka 1989 hakuwahi kufikishwa Polisi wala mahakamani mpaka siku ambapo aliletwa kwa mashtaka hayo, hana rekodi ya uharifu. 

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mashauri alisema mshtakiwa anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine hivyo katika shtaka la kwanza anamuhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni mbili au jela miaka miwili na katika shtaka la pili anamuhukumu faini ya Sh. Milioni tatu au kwenda jela miaka mitatu. 

Hakimu Mashauri amesema Mahakama pia imetoa amri ya kuyataifisha madini hayo na kuyapeleka Tume ya madini. Hata hivyo mshtakiwa huyo alilipa faini na kuachiwa huru.

SPIKA AINDIKIA TUME YA UCHAGUZI KUHUSU KUJIUZULU KWA MBUNGE WA JIMBO LA SERENGETI.

MV MBEYA KUTATUA CHANGAMOTO ZA USAFIRI ZIWA NYASA

$
0
0

Na Leonard Magomba

Kukamilika kwa ujenzi wa meli mpya ya abiria ya MV Mbeya II kunatarajiwa kutatua changamoto za usafiri wa abiria na mizigo katika mwambao wa Ziwa Nyasa.

Meli hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 80, itakuwa meli ya kwanza ya kisasa ya abiria ambayo itaunganisha mikoa mitatu ya Mbeya, Njombe na Ruvuma pamoja na nchi jirani za Malawi na Zambia.

Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa, Bw. Abed Gallus amesema kwamba ujenzi wa meli hizo ambao unafanywa na kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine, ni moja ya juhudi zinazofanywa na TPA kuboresha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo majini. “Ujenzi wa meli hii ya abiria, ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa meli tatu za TPA katika Ziwa Nyasa zilizolenga kutatua changamoto za usafiri wa abiria na mizigo majini,” amesema Gallus.

Bw. Gallus amesema kwamba TPA, ilianzisha mradi wa meli tatu zikiwemo mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja na moja ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 200. Amesema kwamba miradi hiyo ilitekelezwa kwa awamu mbili tofauti ambapo awamu ya kwanza ilihusisha meli mbili za mizigo, MV Ruvuma na MV Njombe ambazo ujenzi wake ulikamilika mwezi Julai, 2017.

Ujenzi wa meli ya abiria ya MV Mbeya II ambao umefikia asilimia 80 unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Disemba, 2018 na umegharimu kiasi cha Tsh.9 bilioni za kitanzania. Asilimia 20 iliyobaki katika kukamilisha mradi huo wa meli inahusu ufungaji wa engine, generate, uwekaji wa vyumba na mambo mengine madogo madogo katika umaliziaji wa ndani na nje ya meli.

Meli hiyo ya abiria inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa watumiaji wa usafiri wa majini kutokana na ukweli kwamba itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo na abiria kwa wakati mmoja. MV Mbeya II inatarajia kufanya safari zake katika bandari mbalimbali kongwe na nyingine mpya zitakazoanzishwa na TPA katika mwambao wa Ziwa Nyasa ili kuleta ufanisi katika usafirishaji wa abiria na mizigo ziwani.

Meli ya MV Mbeya II ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake kwenye Bandari ya Kyela ambapo inatarajia kukamilika Mwezi Desemba Mwaka huu na itakuwa ikihudumia Abiria 200 na mizigo tani 200 kwenye Ziwa Nyasa. 
Baadhi ya mafundi wa ujenzi wa Meli ya MV Mbeya II wakiendelea na kazi hiyo kwenye Bandari ya Kyela Mkoani Mbeya,kukamilika kwa ujenzi wa Meli hiyo kutasaidia usafirishaji wa Mizigo tani 200 na Abiria 200 kwenye Ziwa Nyasa. 

MKUTANO MKUBWA WA UONGOZI KUFANYIKA OKTOBA 19 JIJINI DAR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kinatarajia kufanya Mkutano Mkubwa wa Kwanza wa Uongozi utakaofanyika tarehe 19 Novemba 2018 katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye atawakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama . 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka amesema lengo kuu la mkutano huo ulioandaliwa na ATE kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (Confederation of Norwegian Enterprise, NHO) unalenga kuwaleta pamoja viongozi wa mashirika mbalimbali wakiwemo wanawake na wanaume ili kujadili namna ya kuongeza idadi ya viongozi wanawake katika nafasi za juu kabisa za uongozi.

Dkt Mlimuka amesema kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu ya ‘Uongozi wenye Ufanisi kwa Mazingira yanayobadilika Kibiashara’ na katika utafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa taasisi na makampuni yaliyofanikiwa kuwa na wanawake katika nafasi za juu za uongozi yamepata matokeo chanya kama vile ongezeko la uzalishaji jambo ambalo Chama cha Waajiri wangependa kulifanikisha kwa wanachama wao na wasio wanachama pia katika kuunga mkono jitihada za kitaifa za kujenga Tanzania ya Viwanda ili kufikia Uchumi wa Kati ifikapo Mwaka 2025. 

Aidha amesema kuwa, jitihada hizi zinaendana na juhudi ambazo zinafanywa na Chama cha Waajiri Tanzania na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) kwa kutoa mafunzo ya Mwanamke wa wakati Ujao (Female Future) yaliyozinduliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshiwa Samia Hassan Suluhu mwaka 2016. Mpaka sasa jumla ya wanawake 66 wamepatiwa mafunzo haya ambapo awamu ya kwanza walikuwa 36 kwa mwaka 2016 na awamu ya pili walikuwa 30 kwa mwaka 2017. Sasa tupo kwenye awamu ya tatu ambapo wanawake 20 wanashiriki. 

Dkt Malimuka ameelezea kuwa, Programu hiyo imefanikiwa kuandaa wanawake kwa ajili ya nafasi za juu za uongozi na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye Bodi za Wakurugenzi na kushiriki katika kutoa maamuzi ambapo wanawake kadhaa waliohitimu tayari wamefanikiwa kupata nafasi za juu za uongozi na pia kuwa wajumbe kwenye bodi mbalimbali huku mchango wao ukionekana dhahiri. 

Amewaomba wadau mbalimbali kushiriki katika Mkutano huu ili kujipambanua kama kampuni au taasisi zinazounga mkono jitihada za kuleta uongozi bora wenye kuleta maendeleo katika jamii nzima. Pia tumefungua milamgo kwa mashirika, makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo zitapenda kujitangaza kupitia mkutano huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano Mkubwa wa Kwanza wa Uongozi utakaofanyika tarehe 19 Novemba 2018  jijini Dar es salaam .

ZAIDI YA WATU 300 WAFANYIWA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO KIGAMBONI

$
0
0
Na Genofeva Matemu – JKCI

1/10/2018 Zaidi ya watu 300 wamefanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo pamoja na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo katika maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni.

Katika upimaji huo uliofanywa na madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) jumla ya watu 169 wakiwemo watoto walipimwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram ECHO) na 135 ambao ni watu wazima walipima kipimo cha kuangalia jinsi umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography-ECG).

Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyemamu alisema kwa upande wa watoto waliwaona 34 sita kati yao walikutwa na matatizo ya moyo na watu wazima 10 walikutwa na matatizo wote hao wamepewa rufaa ya moja kwa moja ya kwenda kutibiwa JKCI.

“Wananchi wengi tuliowaona na kuwafanyia vipimo wamekutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu ambapo tumewapa dawa za kwenda kutumia pamoja na ushauri na wachache kati yao tumewapa dawa za ugonjwa wa kisukari”, alisema Dkt. Rweyemamu.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smitha Bhalia akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa kwa mkazi wa Kigamboni wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani ambapo Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) walifanya upimaji bila malipo katika viwanja vya Hospitali ya Vijibweni iliyopo wilaya ya Kigamboni. Katika upimaji huo makampuni mbalimbali ya dawa za binadamu yaligawa dawa bure kwa watu waliokutwa na matatizo yaliyohitaji kutumia dawa.

KITUO CHA SANAA CHA URUSI NA TANZANIA WAMKUMBUKA ALIYEKUWA MCHORAJI NGULI MSAGULA

$
0
0
Na Agness Francis,globu ya Jamii

Kituo cha utamaduni cha Urusi na Tanzania wanaadhimisha wiki ya kumbu kumbu ya aliyekuwa mchoraji nguli hapa nchini Boniface Msagula.

Msagula aliyezaliwa 1939 kijiji cha ndanda wilayani masasi mkoa wa Lindi na kufariki 2005 anakumbukwa na kituo hicho kwa kuonyesha sanaa ya michoro yake ya aina ya tinga tinga alichora enzi ya uhai wake.

Akizungunza jijini Dar es Salaam aliyekuwa Mkurugenzi wa kituo hicho Rifat Pateev amesema maonesho hayo yameana jana katika hicho na kilele chake itakuwa Oktoba 6 mwaka huu.Amefafanua muda wa kuanza kwa maonesho hayo ni saa nne asubuhi na kumalizika saa 10 jioni na hakuna kiingilio,na watu waliokuwa wakijishuhulisha na Sanaa hapa jijini Dar es Salaam hasa Rifat Pateev aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Urusi na Tanzania. 

Akifafanua zaidi Rifat alisema alivutiwa Sana na viwango na uasili wa kazi za Sanaa za Msagula."Miongoni mwa wasanii wa kitanzania ambao nimezishuhudia kazi zao ni Damian Msagula ana michoro ya kipekee,rangi katika michoro na picha zake zilikuwa zikiendana vizuri na kwa uhakika,hiki kilikuwa ni kipaji muhimu kwake"amesema Rifat Pateev. 

Pia ametaja baadhi ya Maonyesho ya picha michoro na Sanaa aliyowahi kufanya Msagula katika sehemu mbali mbali ni mwaka 1976 New Africa hotel Dar es salaam, mwaka 1992 Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, mwaka 1993 Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, mwaka 1995 Telelom building Bonn, mwaka 1996 Dunia ya mizimu ya Msagula kituo cha utamaduni cha urusi na Dar es Salaam.Pia mwaka 1998 simulizi za Msagula kituo cha utamaduni cha urusi na Dar es Salaam,mwaka 1999 Tinga tinga na 2000 Msagula-Solo Exhibition. 

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images