Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live

MGENI RASMI MECHI YA SIMBA NA YANGA SPIKA JOB NDUGAI

$
0
0
 Mgeni rasmi katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akiwa ameongozana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakwembe pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinzia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakiingia uwanjani kwa ukaguzi wa vikosi hivyo, kabla ya kuanza kwa mchezo, uliopigwa jioni ya leo kwenye Dimba ya Taifa, jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa sare ya 0-0.

NEWS ALERT: KIPINDI KIPYA KUTIKISA TANZANIA, NI "STUKA" CHENYE UCHESHI NA ELIMU.

$
0
0
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kipindi kipya chenye mahadhi ya pranks (kumstua mtu huku ukimrikodi anavyostuka, bila yeye kufahamu), kinaanza mwezi Oktoba. 
 Katika mahojiano maalum na mwasisi na mendeshaji wa kipindi hicho, mwanahabari wa kimataifa wa Tanzania Joseph Msami, ambaye hivi karibuni alikuwa mtayarishaji wa vipindi wa Idhaa ya Kisahili ya Umoja wa Mataifa mjini New York, amesema STUKA ni kipindi amabacho kitawaelimisha watanzania kaika Nyanja mbalimbali kama za kijami, kiuchumi kwa kutumia mbinu za burudani. 
 Msami amesema kipindi hicho ambacho hutumia mbinu ya kamera isiyo hadharani na kuwanasa wakazi katika pitapita zao za kila siku, hakimlengi mtu maalum wala kumuandaa yeyote (Reality Show) na kitatoa burudani ya kutosha kutokana na maadalizi yaliyofanywa na timu ya STUKA kwa zaidi ya miezi mitatu. 
 Amesema timu hiyo inayojumuisha wataalamu wa maudhui ya habari, picha na sauti imekuwa katika mafunzo maalum yaliyolenga kuhakikisha umma unapata elimu na burudani kwa kuzingatia weledi. Kipindi chicho kitakachorushwa na kituo cha televisheni ya TVE katika muda ambao watazamaji wengi huangalia runinga (Prime Time ), na kurudiwa mara kadhaa ili kutoa fursa kwa watazamaji kuona uhondo huo kwa wingi.

NEWS ALERT: WAZIRI LUGOLA AAMURU POLISI WATOE DHAMANA SIKU ZOTE ZA WIKI, SAA 24 BILA WANANCHI KUOMBWA RUSHWA

$
0
0
 Na Felix Mwagara, MOHA-Kasulu 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi kutoza fedha kwaajili ya huduma ya dhamana kwa watuhumiwa waliopo mahabusu katika vituo vya polisi nchini. 
Waziri Lugola pia alisema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko. 
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, leo, Waziri Lugola alisema ni marufuku kwa askari yeyote atakayeshindwa kutoa dhamana kwa kosa ambalo lina dhamana. 
“Hii tabia sijui imetoka wapi ambayo imejengeka kwa baadhi ya askari polisi, eti mtu akiingia mahabusu ya polisi siku ya Ijumaa ikifika siku ya Jumamosi na Jumapili hawatoi dhamana wakisema dhamana mpaka Jumatatu, hii tabia sio sahihi na ife haraka iwezekananavyo,” alisema Lugola. Lugola aliwataka wananchi nchini kuhakikisha wanaripoti matukio ambayo yanavunjwa na baadhi ya polisi hao ambao wengi wao wanatengeneza mazingira ya rushwa. 
“Kuna tabia ambayo imezoelewa katika jamii, eti kuingia polisi ni bure ila kutoka ni fedha, hii kauli nataka ife, kwasababu nawajua polisi na hawanidanyi kwa lolote, hivyo ole wao ambao watawanyanyasa wananchi kuwaomba fedha,” alisema Lugola. 
Lugola alisisitiza kuwa, dhamana ni haki ya mtu endapo hilo kosa linadhaminika hivyo mwanachi yeyote atakaeombwa fedha anapaswa kuripoti tukio hilo kwa viongozi wa polisi ili polisi achukuliwe hatua za kinidhamu. 
Aidha, Waziri Lugola aliwataka maaskari wa usalama barabarani kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi na si kuwaandikia makosa madereva kwa kuwakomoa endapo magari yao yanamakosa. “Gari likiwa na kosa liandikiwe faini, hilo sina shida nalo, lakini utakuta baadhi ya askari wanaandika makosa mengi ili watengeneze mazingira ya rushwa, hii ssi sahihi ” alisema Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza mwananchi wa Kijiji cha Basanza Wilayani Uvinza, mkoa wa Kigoma, alipokua aamuuliza maswali, baada ya Waziri huyo kuwataka wakazi wa kijiji hicho kutoa kero mbalimbali zinawakabili wilayani humo. Lugola pia alisema dhamana hizo zinapaswa kutolewa saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko alipokua anatoa taarifa yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya.  Lugola aliwataka Polisi nchini watoe dhamana saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwa sababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko (kushoto) alipokua anatoa taarifa yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Katika hotuba yake kwa maafisa wa Wilaya hiyo, Lugola aliwataka Polisi nchini watoe dhamana saa 24 na siku zote za wiki na sio vinginezo kwasababu vituo vya polisi nchini vinafanya kazi muda wote zikiwemo siku za mapumziko. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI ALLY ALIVYOPAMBA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MSONDO NGOMA... OOHH BWANA WAZIRI, WAZIRI....

ASILIMIA 11 YA WATANZANIA KUWA WAZEE IFIKAPO 2050

$
0
0
Na Mwandishi Wetu -Arusha
Tanzania inakadiliwa itakuwa na wazee 11% ya watu wote nchini ifikapo mwaka 2050, kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka kwa kasi kutokana na kuendelea kuboreka kwa huduma za Afya hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Huduma za Afya kwa Wazee kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Edward Mung’ong’o wakati akiwasilisha mada kwenye kongomano lililofanyika leo Jijini Arusha kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee, amesema kuwa Mwaka 2002 idadi ya Wazee ilikuwa milioni 1.4, ikiwa ni sawa na 4% ya watu wote yaani Milioni 33.5. 

Aidha Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa kwa sasa idadi ya Wazee hapa nchini inakisiwa kuwa milioni 3 sawa na 5.6% ya watu wote ambao kwa takwimu za sasa Tanzania ina Watu milioni 55.

Akizungumzia mafanikio ya serikali katika kuboresha huduma za Afya kwa Wazee Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la HelpAge International imepitia na kuboresha Mtaala wa kufundishia Wauguzi ngazi ya kata ili wapate mafunzo yatakayowawezesha kuhudumia Wazee kwa ufanisi.

 Aidha Dkt. Mung’ong,o  aliongeza kuwa kwa kushirikiana na HelpAge International pia serikali imeandaa Mwongozo kwa ajili ya watoa huduma wa kuwaelekeza jinsi ya kutibu magonjwa ya kawaida yanayowasibu Wazee.

Wakati huo huo Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt. Naftali Ng’ondi akifungua Kongamano hilo kwa niaba ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alisema Wazee watatumia fursa hiyo kujadiliana juu ya utekelezaji wa Sera na Miongozo ya kuboresha hali na Maisha ya Wazee nchini kwa kuzingatia utambuzi wa wazee katika Halmashauri, upatikanaji wa huduma za Afya kwa wazee na ushirikishwaji wa wazee.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ng’ondi akielezea lengo la kongamano kwa wazee waliohudhuria kongamano la wazee kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wazee yatakayofanyika  Jijini Arusha Oktoba Mosi.
 Mwenyekiti wa Kongomano la Wazee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee Tanzania Mzee Sebastian Bulegi akiongoza Wazee walioshiriki katika kongomano la wazee kwa lengo la kujadili changamoto wanazokabiliana nazo wazee nchini wakati wa kongamano la wazee kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wazee yatakayofanyika  Jijini Arusha Oktoba Mosi.
 Mratibu wa huduma za Afya kwa Wazee kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Edward Mung’ong’o akiwasilisha mada wakati wa kongomano kuelekea  Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo Jijini Arusha.
  Kamishana wa Polisi akieleze kuhusu hali ya mauaji ya wazee nchini na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo katika kupambana na vitebdo vya ukatili kwa wazee wakati wa kongomano kuelekea  Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo Jijini Arusha.
Wazee walioshiriki Kongamano la Wazee wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa katika Kongamano hilo ikiwa ni moja ya shighuli zinazofanyika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yatakayofanyika Jiji la Arusha Oktoba Mosi. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU ATAKA WACHIMBAJI WADOGO WAENDE BENKI WAKAKOPE MITAJI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wachimbaji wadogo wa madini waende Benki wakakope mitaji kwa sababu wana uhakika wa kudhaminiwa na Benki Kuu.

“Msihofu kukopa, kukopa ni jambo la kawaida sana. Nenda mkakope ili mpate mitaji ya kununua mitambo ya kuchenjua dhahabu na madini mengine,” amesema.

Ametoa wito leo (Jumapili, Septemba 30, 2018) wakati akifunga maonesho ya mkoa wa Geita ya dhahabu, madini, teknolojia ya madni na uwekezaji yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita. Maonesho hayo yalianza Septemba 24, mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema, wakati akikagua mabanda ya maonesho kwenye viwanja hivyo, ameelezwa kwamba gharama ya mtambo unaohitajika kwa wachimbaji wa kati inafikia sh. milioni 10. “Naomba niwaeleze wanaGeita kwamba mnakopesheka, nendeni mkaombe mikopo ili mnunue mitambo ya kuchenjua dhahabu,” amesisitiza.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewaeleza wana-Geita kwamba siri kubwa ya kufanikiwa kupata mikopo ni kwa wao kuunganisha nguvu kwa kujiunga kwenye vikundi ili wawe na malighafi ya kutosha mitambo hiyo.

“Wakuu wa wilaya za Mkoa huu simamieni zoezi hili kwa sababu wilaya zenu zote zinachimba madini. Simamieni uundaji wa vikundi na mwende mkawasemee benki pale wanapokwama.”

Akielezea kuhusu makusanyo ya fedha kutokana na mauzo ya dhahabu kwenye mkoa huo, Waziri Mkuu amesema tangu Aprili mwaka huu, mapato yanayotokana na madini yameongezeka kutoka sh. milioni 400 na kufikia sh. milioni 850 Agosti, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wazazi wawapeleke watoto wao kwenye vyuo vya ufundi vya VETA ili wakajifunze taaluma ya uchongaji wa madini na vito kama eneo jipya la ajira nchini.
 Mwanafunzi wa mwaka pili katika chuo cha VETA Moshi, Careen Vedasto akiendesha kifaa cha kuchimbia madini kilichobuniwa na wanafunzi na walimu wa chuo hicho mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimuuliza maswali mwanafunzi wa VETA Moshi, Jesca Jonathan (mwenye rasta), kuhusu utaalamu wa kuchonga vito na madini alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Wa pili kulia ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kifungashio cha kopo la kahawa aina ya AMIMZA alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Kulia ni Afisa mauzo wa TANICA PLC, Revina Peter akitoa maelezo. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea maelezo ya mtambo wa kuchenjua madini unaoweza kumilikiwa na wachimbaji wa kati alipotembelea mabanda kwenye maonesho ya dhahabu, madini, teknolojia ya madini na uwekezaji, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kalangalala, mjini Geita, Septemba 30, 2018. Anayetoa maelezo ni Katibu Msaidizi wa UMUMAGE, John Ngenda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAWAAGIZA WENYEVITI WA VIJIJI KUSIMAMIA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Na Veronica Simba – Lindi
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza Wenyeviti wa Vijiji nchini kote, ambako miradi ya umeme vijijini inatekelezwa, kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo ili wakamilishe kazi kwa wakati.
Alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti Septemba 27 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi katika vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Lindi ambako aliwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi.
Katika kuhakikisha maagizo yake yanatekelezwa, Waziri Kalemani aliwataka wakandarasi kuripoti kila siku asubuhi kwa wenyeviti wa vijiji husika, ambako wanatekeleza miradi ili kujiridhisha kuwa wapo kazini.
Aidha, Waziri aliwataka wenyeviti hao kujiridhisha kuwa wakandarasi husika hawaajiri vibarua kutoka nje ya maeneo yao bali watoke katika vijiji husika. “Mwenyekiti ukigundua kuwa Mkandarasi kaajiri vibarua kutoka nje, mtaarifu Mkuu wa Wilaya mara moja ili achukue hatua stahiki.”
Vilevile, aliwaagiza Mameneja wa TANESCO wa Kanda na Wilaya kuongeza nguvu katika zoezi hilo la kuwasimamia wakandarasi ili kuhakikisha wanafanya kazi ipasavyo.
Akiwa mkoani Lindi, Waziri kalemani aliwasha umeme katika vijiji vya Chipande (Lindi Vijijini), Luchelegwa (Luangwa) na Legezamwendo (Liwale).
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akikata utepe katika Jengo la Kituo cha Afya kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Luchelegwa, Wilaya ya Luangwa, Mkoa wa Lindi. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.

 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chipande, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, akiwa katika ziara ya kazi Septemba 27, 2018 ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika eneo hilo.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme katika Jengo la Kituo cha Afya cha Rondo, Lindi Vijijini, Septemba 27, 2018 kuashiria uwashaji rasmi wau meme katika eneo hilo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi wakiongozwa na Mbunge na Waziri Mstaafu Benard Membe.
 Mbunge na Waziri Mstaafu Benard Membe, akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Chipande, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini. Tukio hilo la kuwashwa rasmi umeme katika eneo hilo lilifanywa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye shati la bluu-walioketi), Septemba 27, 2018.

 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akizungumza na wananchi wa Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.
 Wananchi wa Kijiji cha Legezamwendo, Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi wakishangilia mara baada ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 27, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wafanyakazi nchini

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.
Serikali imewahimiza wafanyakazi  kote nchini kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kujiletea maendeleo  na kuchangia katika ujenzi wa Taifa. 
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokuwa akiongea na viongozi wanawake wa Mkoa wa Morogoro kutoka vyama vya wafanyakazi ikiwemo TAMIKO, CWT, TUICO, TALGU, TULGE, TPAWU na CHODAWU.
Waziri Mhagama amebainisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imelenga kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa wafanyakazi kwa kuhakikisha wanashirikishwa kwenye dhana ya uchumi wa viwanda. Lengo likiwa ni kuwawezesha wafanyakazi wanashiriki katika mipango ya maendeleo ya taifa kwa kufuata kanuni na taratibu ya dhana nzima ya uchumi wa viwanda.
"Mnao uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na mkawa chachu ya maendeleo ya viwanda kwenye uchumi wa taifa letu, kwa kuweza kutoa ajira, vilevile kuwasaidia ninyi kupiga hatua za maendeleo kwa kufanya kazi kwa uzalendo na weledi kwa kutumia sera ya viwanda" ameeleza Waziri Mhagama.
Aidha, aliongeza kuwa, Sera ya uchumi wa viwanda iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ni jambo jema linalolenga kuboresha maisha ya watanzania.
“Mheshimiwa Rais amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza azma ya kujenga Tanzania ya viwanda, hivyo nitafurahi sana kama Waziri mwenye dhamana ya wafanyakazi kuhakikisha tunaleta mabadiliko chanya ya kiuchumi kwa wafanyakazi.” Alisema Mhagama.
Alitoa rai kwa viongozi wanawake kuhakikisha wanaratibu na kusambaza ujumbe huu wenye habari njema kwa wanawake nchi nzima waliopo kwenye sekta ya ajira kuchangamkia fursa hii kwa kuanzisha miradi mbalimbali itakayowawezesha kuwakomboa kiuchumi.
Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa alifafanua juu ya sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambayo imelenga kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa mitaji ili kuwawezesha wananchi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Viongozi wanawake kutoka vyama vya wafanyakazi Mkoani Morogoro kuhusu kuwahimiza wafanyakazi kuchangamkia fursa za shughuli za kimaendeleo zilizopo nchini.  
 Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamuhoke akielezea jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokutana kwa lengo la kuzungumza na Viongozi Wanawake kutoka kwenye Vyama vya Wafanyakazi Mkoani Morogoro.  
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa akizungumzia Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa viongozi kutoka vyama vya wafanyakazi walipokutana Mkoani Morogoro.
 Baadhi ya viongozi kutoka kwenye Vyama mbalimbali vya Wafanyakazi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipokutana nao kuzungumzia ushirikishwaji wa wafanyakazi kwenye dhana ya uchumi wa viwanda. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Kilwa Jazz Band - Napenda nipate lau nafasi

SONGAS yatoa rambirambi ya milioni 50 kwa wafiwa kufuatia tukio la ajali la MV Nyerere

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Issack Kamwelwe (wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 50 kutoka kwa Meneja wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Uzalishaji Umeme nchini Songas Limited, Bi. Agatha Keenja (wa pili kulia) ikiwa ni kama rambirambi kwa ajili ya kusaidia shughuli za kuhudumia wahanga wa ajali pamoja na mkono wa pole kwa wafiwa kufuatia tukio la ajali la MV Nyerere. Hafla hiyo imefanyika  mwishoni mwa juma visiwani Ukerewe jijini Mwanza. Wengine katika picha kulia ni Meneja Miundombinu wa kampuni ya Uzalishaji Umeme ya Songas Limited, Bw. Goronga Kasaka.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) na wadau wa SONGAS mara baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa juma visiwani Ukerewe jijini Mwanza.

EXCLUSIVE:Makubwa yaibuka Nai kuacha video vixens kisa hiki hapa

MICHUZI TV: NAVY KENZO Kusajiliwa WCB wafunguka Haya..

MICHUZI TV: DIAMOND atanioa ni mwanaume anayenifaa, Mrembo Irene

MICHUZI TV: MBOSSO afunguka ishu ya kushindanishwa na ASLAY

MICHUZI TV: Aunty Ezekiel kumuacha Mose Iyobo, siwezi kumuhusisha Cookie na Film


MICHUZI TV: Queen Darleen Utamu wake katika Mapenzi, Mbosso sababu ya kutoboa

DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wameendelea kuboresha huduma ya maji sehemu mbalimbali ikiwemo kuongeza maji ya kutosha katika bandari ya Dar es Salaam.

Mkakati huo umeanza kutekelezwa rasmi  na Mkoa wa Dawasa Ilala kwa kuanza zoezi maalum la kuunga Bomba kubwa la kipenyo nane ili  kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini.

Meneja wa mkoa Ilala Judith Singinika  amesema kuwa zoezi linatekelezwa kulingana na agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Makame Mbarawa  alilolitoa alipotembelea mamlaka hiyo ya Bandari.

Amesema kuwa, kukamilika kwa zoezi la kuunga bomba hilo kutaongeza wingi wa maji katika bandari hiyo ya Dar es salaam na kuhakikisha kuwa mahitaji ya huduma ya maji kwenye eneo lote la Bandari yanafikiwa. 

Aidha kazi hii itawezesha pia meli zote za abiria na mizigo zinazotia nanga katika bandari hii kibwa kuliko zote nchini zinapata maji safi na kukidhi mahitaji.

Hapo awali, Bandari walikuwa wananunua maboza kutoka nje kwa ajili ya matumizi ya meli zinazotia nanga na Profesa Mbarawa alipiga marufuku na kuwataka watumie maji ya Dawasa kwa usalama zaidj.

Kazi hii ni utekelezaji wa  agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.
Ujenzi wa kuunga bomba kubwa la maji lenye kipenyo nane ili  kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini ukiendelea kufuatia agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.

TETEMEKO LAUA 832 INDONESIA, VIFO VYAHOFIWA KUONGEZEKA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

IDADI ya vifo vilivyosababishwa   na tetemeko la ardhi na tsunani nchini Indonesia vimefikia  832  huku vifo vingi zaidi vikihofiwa kuongezeka kadri maeneo yanavyofikiwa na waokoaji.

Mamlaka husika imetangaza kuwa wataanza kuzika miili hiyo iliyopatikana katika makaburi ya umma kwa kuhofia mlipuko wa magonjwa.

Aidha idadi kubwa ya watu wanasadikika kuwa hai chini ya vifusi, na katika mji wa Palu wamehitaji vifaa maaalmu ili kuweza kuwaokoa manusura waliokwama katika maduka na hoteli ambapo pamehofiwa kuhusu usalama kwa waokoaji hao.

Kwa upande wake wakala wa majanga nchini humo Sutopo Nugroho amevieleza vyombo vya habari kuwa ugumu katika vifaa (mashine za uokoaji) na mawasiliano ni changamoto kubwa ukilinganisha na idadi ya majengo yaliyoporomoka.

Tetemeko lenye ukubwa wa 7.5 lililikumba taifa hilo ikiwa ni miezi miwili tangu kutokea kwa tetemeko jingine na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Rais wa nchi hiyo  Joko Widodo amekuwa akitembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika na kusaidia katika shughuli ya uokoaji na amekubali msaada wa kimataifa wa majanga kutokana na tetemeko hilo.
 Sehemu ya makazi ya watu yalivyoathiriwa na tetemeko hilo kwa kiasi kikubwa.

IMANI POTOFU-ZIMBABWE -BAADHI YA WAGONJWA WA UKIMWI WANAAMINI UKISHIRIKI TENDO LA NDOA NA ALBINO UNAPONA .

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga.

IMANI haba na zile za kishirikina zimeendelea kushika kasi kwa nchi za Afrika huku  watu wenye ulemavu wa Ngozi “Albino” wakiwa waathirika wakubwa kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa kuuawa na kisha kunyofolewa viungo kwa imani za kishirikina.

Matukio haya yanatajwa kuendelea kukithiri katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, ambapo nchini Zimbabwe ipo imani ya kwamba muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi akishiriki tendo la ndoa na mwenye ulemavu wa ngozi "Albino " atakuwa amepona .

Lissa Marange ni miongoni mwa washiriki 25 kutoka nchi zaidi ya nane walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kupeleka ujumbe maalumu kwa viongozi wa Afrika kuongeza nguvu katika mapambano ya vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye Ualbino.
 Pichani wa pilia kulia ni Lissa Marange ambaye ni miongoni mwa washiriki 25 kutoka nchi zaidi ya nane walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kupeleka ujumbe maalumu kwa viongozi wa Afrika kuongeza nguvu katika mapambano ya vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye Ualbino.
 Baadhi ya washiriki 25 kutoka nchi zaidi ya nane walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kupeleka ujumbe maalumu kwa viongozi wa Afrika kuongeza nguvu katika mapambano ya vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye Ualbino.

PROFESA NDALICHAKO 'AWATUMBUA' WAWILI WIZARANI KWAKE

$
0
0

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

WAZIRI Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaondoa kwenye vyeo vyao Mratibu wa Miradi na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu kwa kushindwa kusimamia majukumu yao na kupelekea baadhi ya miradi kushindwa kukamilika kwa wakati.

Aliwataja viongozi ambao wanatakiwa kuondolewa katika nafasi zao na kuondolewa katika Wizara hiyo ni Mratibu wa Miaradi kuwa ni Fredrick Shuma na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu Basiliana Mrimi.

Profesa Ndalichako alitoa kauli hiyo jana wilayani Nzega wakati akikagua mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu Ndala na kukutana miradi hiyo iko katika hali isiyoridhisha. Alisema utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa Chuo cha Ualimu cha Ndala hauridhishi na kusababisha kushindikana wanachuo wengi kuanza katika mwaka huu wa masomo.

Profesa Ndalichako alisema watendaji hao ni miongoni mwa waliosababisha vifaa kwa ajili ya vyuo vya ualimu vya sayansi kupelekwa katika vyuo ambavyo havifundishi sayansi na kupelekea baadhi kupitwa na wakati na kusababisha hasara kwa Serikali. o Aidha Waziri huyo ametoa onyo kwa Mhandisi wa Wizara hiyo George Sambali kwa kushindwa kukagua miradi ya ujenzi inayoendelea hadi wasubiri Waziri na Naibu wake watembelea ndio nao waonekana jambo ambalo linasababisha kujengwa kwa miradi ambayo sio mizuri na inachukua muda mrefu.

Alisema suala la kuhakiki ubora wa miradi ni kazi ya wataalamu na sio kungoja viongozi waendele ndio marekebisho yafanyike jambo linalosababisha baadhi ya miradi kuchelewa. Profesa Ndalichako alimwonya Mkuu wa Chuo cha Ualimu Ndala Abinego Ndikumwe kutopokea majengo yaliyokarabatiwa na United Builders ambayo yameonyeshwa huku yakiwa na mapungufu mengi.

Alisema kabla ya kuyapokea wahakikishe wahusika wamefanyia kazi mapungufu yote na kufikia Mwezi Novemba wakabidhi kazi ikiwa imekamilika. Kuhusu Kampumi ya Unite Builders ambayo inakarabati na kujenga baadhi ya majengo ameitaka kuhakikisha inakabidhi kazi ifikapo Novemba ikiwa katika hali nzuri na kuongeza nje hapo hawatapa kazi yoyote ya Serikali.

Alisema majengo ambayo watajenga lazima yaonyeshe thamani ya bilioni 3.1
Viewing all 110180 articles
Browse latest View live




Latest Images