Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

INTERNATIONAL YOUNG FASHION DESIGNERS SHOWCASE TOUR IN TANZANIA

$
0
0
*Talented Young Fashion Designers Gathered in Enchanting Africa

After the shows in Iceland and Panama, “International Young Fashion Designers Showcase Tour” set off her journey to Dar es Salaam as its third stop. A gala fashion show held at Hyatt Regency of Dar es Salaam on Sept 28 featuring the collections of the participating international young fashion designers.

To support the Belt and Road Initiative (BRI) launched by the Chinese Government to promote trade, infrastructure and networking strategy among countries, the “International Young Fashion Designers Showcase Tour” is organized aims to provide a platform for the young fashion designers to showcase their works globally.

This project is initiated by Dr. Annie Wu, SBS, JP, initiator of the showcase tour and the Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong and Macau, to boost her relationship between China and Africa.

It is honored that Hon. Mizengo Peter Pinda, Former Prime Minister of Tanzania was present as the Guest of Honour. He officiated the catwalk show together with Dr Annie Wu and Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist Board. 

They were joined by Mrs Pinda, Hon Angela Kairuki, Minister of Minerals, United Republic of Tanzania, Ambassador Ramadhani Mwinyi, Deputy Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs, Mr Joseph Kahama, Secretary General of Tanzania China Friendship Promotion Association, Ms Angel Hon, Curator of “Belt and Road International Young Fashion Designers Showcase Tour”, Mr Xu Chen, Minister Councellor of the Embassy of China in Tanzania and Mr Matindi, CEO of Air Tanzania.
Group photo from left: Ms Angel Hon, Curator of International Young Fashion Designers Showcase Tour, Ambassador Ramadhani Mwinyi, Deputy Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs, MrsPinda, Dr Annie Wu, Honorary Consul of the United Republic of Tanzania to Hong Kong and Macau, Hon MizengoPinda, Former Prime Minister of Tanzania Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist BoardHon Angela Kairuki, Minister of Minerals, United Republic of Tanzania, Mr Joseph Kahama, Secretary General of Tanzania China Friendship Promotion Association and Mr Matindi, CEO of Air Tanzania.
Opening speech by Ms Devotha Mdachi, Managing Director of Tanzania Tourist Board.
Belt and Road Collection specially designed for the Tour by Tony Vergara from Panama.
Group photo of all attended designers and models.


BENKI YA i&M YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUZINDUA PROMOSHENI YA JIDABO

$
0
0
Benki ya i&M imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kuzindua Promosheni inayojulikana kama JIDABO na i&M Bank.

Promosheni hiyo itawezesha Wateja wa Benki hiyo kupata akiba mara mbili katika Akaunti zao, Promisheni itakayodumu kwa kipindi cha Miezi mitatu kuanzia Oktoba Mosi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa i&M Bank, Ndabu Swere amesema Wiki ya Huduma kwa Wateja wanaipa kipaumbele kwa kuwashukuru Wateja, na kuangalia vitu vya kuboresha katika Benki.

Ndabu amesema Promosheni ya JIDABO na i&M Bank itakuwa kwa Wateja wa ndai na Wateja watarajiwa.

Amesema ili kushiriki Promisheni hiyo Wateja wote wenye Akaunti za Akiba, Biashara na Watoto wanaweza kushiriki katika Promosheni hiyo
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa i&M Bank, Ndabu Swere akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa I&M Bank kuhusu kuanzishwa kwa promosheni  mpya ya JIDABO na i&M Bank iliyoanza leo katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja wa benki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Wateja na wafanyakazi wa i&M Bank Tawi wa Oysterbay wakikata keki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam
Wateja wa i&M Bank tawi la Kariakoo wakikata keki wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam
Maneja  wa i&M Bank Tawi la Kariakoo, Asheri Warioba akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa  I&M Bank katika tawi ilo kuhusu huduma wanazozitoa wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa i&M Bank, Ndabu Swere akimsikiliza mmoja wa wateja wa  I&M Bank  Tawi la Main wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam.
Meneja wa  Tawi la Main Imran Walliakimlisha mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa i&M Bank, Ndabu Swere akilishwa keki na mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam.
Maneja  wa i&M Bank Tawi la Kariakoo, Asheri Warioba akimlisha mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam
Meneja wa  Tawi la Oysterbay Abbasali Remtulla akimlisha mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja wa jijini Dar es Salaam
Meneja wa  Tawi la Oysterbay Abbasali Remtulla akilishwa na mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam .
Meneja Masoko naUhusiano wa I&MBank, Emmanuel Kiondo(kulia) akizungumza jambo na Meneja wa  Tawi la Oysterbay Abbasali Remtulla
wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, aliyekuwa Lilongwe, Malawi
TAASISI zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mikopo kutoka kwa wanufaika na hivyo kuongeza uwezo wa taasisi hizo kutoa mikopo kwa wahitaji wengi zaidi.

Bw. Alex Twinomugisha, Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya TEHAMA ya Intel, amewaambia wiki iliyopita (Sept 27, 2018) Watendaji Wakuu wa taasisi hizo na wadau wengine wanaokutana mjini Lilongwe kuwa matumizi ya TEHAMA hayana mjadala katika kuongeza ufanisi.

Mkutano huo umeandaliwa na Shirikisho la Taasisi za kiserikali zinazotoa Mikopo ya Elimu ya Juu Afrika ambazo (AAHEFA).

Taasisi zilizoshiriki mkutano huo zinatoka katika nchi za Malawi, Botswana, Ghana, Kenya na Lesotho. Nchi nyingine zilizoshiriki ni Rwanda, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Tanzania.

“Swali mnalopaswa kujiuliza kila mara ni – mnafanya nini tofauti na mwaka jana au miaka iliyopita kuhusu matumizi ya TEHAMA?”, aliuliza na kuongeza kuwa taasisi hizo zinapaswa kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kutoa huduma bora kabla ya wateja wao hawajalalamika.

“Zaidi ya asilimia 50 ya kazi hivi sasa zinahitaji matumizi ya TEHAMA na katika baadhi ya nchi zenu, kama Kenya, kwa mfano, takribani theluthi moja ya makusanyo ya mikopo iliyoiva yanapatikana kupitia huduma ya simu za mkononi… ni huduma rafiki na rahisi,” amesema Bw. Twinomugisha wakati akiwasilisha mada iliyoitwa ‘Mapinduzi ya Nne ya Soko la Ajira: Elimu ya sasa inawezaje kutatua?”.

Katika mkutano huo, washiriki pia walipata fursa ya kusikiliza na kujadili mada iliyohusu ‘Kuunganisha Mifumo ya Taasisi za Mikopo ya Elimu ya Juu ili Kuimarisha Makusanyo – Kuongeza Matumizi ya Kidigitali’ iliyowasilishwa na Bw. Charles Odour, mtaalamu kutoka kampuni ya ushauri ya Ernest & Young.

Katika mada yake, Bw. Odour alizungumzia umuhimu wa taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu kuanzisha mifumo itakayohakikisha kila mnufaika wa mkopo anapatikana kwa urahisi na kuanza kurejesha bila kujali mahali alipo duniani popote.

“Dunia hivi sasa inaendeshwa kidigitali, tunawasiliana na wateja kidigitali … na nyie mna taarifa nyingi kuhusu wateja wenu, mnachotakiwa kufanya ni kuanzisha mifumo itakayobaini wanufaika ili waanze kurejesha,” amesema Bw. Odour.

Akichangia mada ya Bw. Odour, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Kenya Bw. Charles Ringera amesema ili taasisi za zinazotoa mikopo ya elimu ya juu ziweze kukusanya mikopo kwa ufanisi, hazina budi kuhakikisha kanzidata zao zinaunganishwa na mifumo mingine ya wadau muhimu.

“Kwa Kenya, tumeunganisha mfumo wetu na mingine muhimu kama ile ya mamlaka ya mapato, mfumo wa bima ya afya, wa mamlaka ya usafiri na mingine … kwa hiyo ikitokea mnufaika wa mkopo anahudumiwa na taasisi moja, na sisi tunapata taarifa na kuanza kumdai iwapo hajaanza kurejesha,” amesema Bw. Ringera ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Taasisi za Serikali zinatoa mikopo ya Elimu ya Juu Afrika (AAHEFA).

Akichangia mada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Tanzania (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru amesema HESLB inatambua umuhimu wa TEHAMA katika kuboresha ufanisi na kuwa hivi sasa ipo katika maboresho makubwa na mifumo yake ya ndani ili iweze kuunganishwa na mifumo ya nje na hivyo kuongeza ufanisi.

“Hivi sasa tunaboresha mifumo yetu uombaji, upangaji na ukusanyaji wa mikopo na baada ya hapo, itaweza ‘kuongea’ na mifumo ya nje ya wadau wengine na hivyo kutoa huduma bora kwa wateja wetu,” amesema Bw. Badru.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu wa Mutharika na umefungwa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Malawi Bw. Justin Saidi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Abdul-
Razaq Badru akiongea katika mkutano uliojumuisha Watendaji Wakuu, maafisa na wadau wa taasisi
zinazotoa mikopo ya elimu barani Afrika hivi karibuni mjini Lilongwe, Malawi.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa taasisi zinazotoa mikopo ya elimu Afrika katika moja ya vikao vya mkutano ulioshirikisha taasisi hizo hivi karibuni mjini Lilongwe, Malawi.

CHIFU WA ENDONET AWAONGOZA WAKENYA KUCHANGIA UJENZI KITUO CHA POLISI TANZANIA

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Katika hali ya kujenga mahusiano ya nchi jirani pamoja na kutoa kipaumbele kwa suala zima la ulinzi na usalama bila kujali utaifa, Chifu wa eneo la Endonet, Count ya Kajiado ya nchini Kenya Bw. Jacob Lemunge aliwaongoza baadhi ya wananchi wa Kenya kuchangia ujenzi wa kituo kipya cha Polisi cha Kamwanga kilichopo wilaya ya Longido.

 Chifu Lemunge aliwaongoza wananchi wa Kenya ambao wanaishi mpakani mwa eneo hilo, kuchangia kituo hicho kipya wakati wa harambee iliyoongozwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi
 Chief Lemunge alisema kwamba wameamua kufanya hivyo kwa kuwa suala la usalama ni muhimu kwa pande zote huku ikizingatiwa kwamba jamii zote za Wakenya na Watanzania zinaishi mpakani na kunapotokea tatizo la kiusalama upande mmoja, basi wanaoathirika ni wote.

 Akizungumza mara baada ya harambee hiyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi licha ya kuwashukuru wananchi wa Kamwanga na majirani zao upande wa Kenya kwa kushikamana, alisema kwamba kitu cha kwanza katika maisha ya binadamu ni ulinzi na usalama.Alisema bila kuwepo kwa usalama katika eneo lolote hakuna shughuli zozote za maendeleo zitakazofanyika na kuongeza kwamba hata eneo hilo linahitaji uimarishaji wa ulinzi kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi. 

 “Eneo lolote linapopiga hatua kiuchumi na kama hakuna ulinzi wa kutosha basi litakuwa linashawishi kuwepo au kuongezeka kwa uhalifu, hivyo nami sitataka kusikia eneo hili ambayo ni himaya yangu linatawaliwa na wahalifu”. Alifafanua Kamanda Ng’anzi. 

 Kamanda Ng’anzi aliahidi kukipandisha daraja kituo hicho kutoka daraja” C” mpaka kufikia daraja “B” sambamba na kuongeza idadi ya askari pindi tu kitakapokamilika. Kwa upande wa mhamasishaji wa ujenzi wa kituo cha awali ambacho kinatumika mpaka hivi sasa Mzee Hendry Daniel maarufu kwa jina la Sawaki alisema kwamba mwaka 1998 aliamua kuhamasisha wananchi wa eneo hilo kujenga kituo kwa kuwa kulikuwa na matukio ya kijinai yaliyokuwa yanatokea lakini hapakuwa na sehemu ya kushtaki.

 “Tulikuwa tunapata tabu sana na tulikuwa tunaishi kama wanyama yaani ukifanyiwa kosa hakuna hata sehemu ya kushtaki labda uende Tarakea ambapo ni mbali zaidi kutoka hapa”, Alisema Mzee Sawaki. 

 Harambee ya ujenzi wa kituo hicho kipya ambacho kilianza kujengwa mwaka 2010 ililenga kupata fedha kwa ajili ya umaliziaji, ambapo wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Enduimeti walijitolea kutoa fedha taslimu huku wengine wakitoa ahadi ya fedha na vifaa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akikagua jengo la kituo kipya cha Polisi ambacho kilijengwa toka mwaka 2010 lakini bado hakijamalizika, kushoto kwake ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Longido Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joswam Israel Kaijanante
 Jengo la kituo kipya cha Polisi Kamwanga ambacho kimejengwa kwa nguvu ya wananchi toka mwaka 2010 ambacho kikikamilika kitaongeza idadi ya askari ambao watahudumia katika eneo hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akiongea na wananchi wa kata ya Kamwanga wilayani Longido mara baada ya kufanya harambee ya kuwezesha umaliziaji wa ujenzi wa kituo hicho.
Chifu wa eneo la Endonet Count ya Kajiado nchini Kenya Bw. Jacob Lemunge akiongea na wananchi waliohudhuria katika shughuli ya harambee ya kuchangia umaliziaji wa ujenzi wa kituo kipya cha Polisi Kamwanga kabla ya kuongoza wananchi wa Kenya kuchangia, pembeni yake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng'anzi. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha) 

MICHUZI TV: MWASELELA AZUNGUMZIA MIAKA MITATU YA JPM KATIKA SEKTA YA ELIMU

MICHUZI TV: MALULU KUFANYA ONESHO KUBWA LA MICHORO LA MWARONI

MICHUZI TV : RADO WA BONGO MOVIE AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI


MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WAZEE JIJINI ARUSHA

INTRODUCING "UMENIBAMBA" BY KINGSURE FT. MAPANCH

Rais Magufuli akutana na Wajasiriamali wa Feri Jijini Dar es Salaam na awachangia shilingi Milioni 20

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01 Oktoba, 2018 ameahidi kutoa shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya wajasiriamali wa eneo la Feri katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na ameahidi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao.

Mhe. Rais Magufuli amekutana na Wajasiriamali hao ambao wanajumuisha Wavuvi Wadogo na Mamalishe wakati akiwa katika mazoezi ya jioni pamoja na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli ambaye pia amewachangia wajasiriamali wanawake shilingi Milioni 5.

Pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli, wajasiriamali hao wameomba awasaidie wasifukuzwe na Manispaa ya Ilala katika eneo hilo, na badala yake wawekewe utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao.

Pia wameomba waondolewe ushuru unaotozwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kwa mitumbwi ya wavuvi wadogo wa samaki, kama ambavyo Serikali imewaondolea ushuru wakulima wanaopeleka sokoni mazao yasiyozidi tani moja.

Aidha, Wajasiriamali hao wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kuiongoza nchi na kushughulikia kero za Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwatembelea na kuwasikiliza kwa mara ya pili.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameahidi kufanyia kazi maombi ya Wajasiriamali hao na amewapongeza kwa juhudi zao za kujitafutia kipato.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam



01 Oktoba, 2018

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 01.10.2018

BEI YA KITOWEO KATIKA SOKO LA KIWALANI

$
0
0
Mfanyabiashara wa kuuza Kitoweo katika soko la Kiwalani  akiandaa kwa ajili ya kukaanga kuku na kuuza kwa wateja wanaotoka sehemu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, ambapo kipande cha kuku huuzwa kati ya shilingi 1500 mpaka 2000. (picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Wanfanyabiashara wa kuku katika soko la Kiwalani jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi.

WANAHABARI KUPEWA UBOBEZI WA HABARI ZA NISHATI JADIDIFU

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KATIKA kukuza na kuendeleza sekta ya nishati nchini Kampuni ya Nukta Afrika kwa kushirikiana  Energy Change Lab pamoja na Hivos wameandaa mafunzo rasmi na endelevu kwa  wanahabari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kuhabarisha habari za nishati jadidifu  ambayo ni muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda na kupunguza gharama za umeme unaotoka katika gridi ya taifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa  Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri(TEF)  Deodatus Balile ameeleza kuwa mafunzo hayo kwa wanahabari yatatolewa na wabobezi na mada zitakazotolewa na pamoja na namna ya kufanya tafiti kuhusiana na nishati na kuthibitisha/kutetea  maandiko yao.

Amesema  kunauhitaji mkubwa wa nishati jadidifu  nchini kwani sekta zote hutegemea nishati licha ya tafiti kuonesha kuwa nyumba 3 kati ya 4 hutumia kuni au mkaa na kuna maeneo ambayo yapo nje ya gridi ya taifa kama vile visiwa vya Ukara ambako ni ngumu kupeleka nguzo kwa ajili ya umeme ila matumizi ya sola yanaweza kutatua changamoto hiyo na wananchi kupata huduma stahiki.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Nukta Afrika Nuzulack Dausen amesema kuwa jukwaa hilo lililowahusisha wanahabari ni kwa malengo ya kuwaongezea ufanisi kwa kuwa sekta ya nishati hugusa kila mtu hasa katika sekta za afya na viwanda.

Pia amesema kuwa kupitia mafunzo hayo endelevu wanaamini idadi ya wawekezaji katika sekta hiyo itaongezeka ili kuweza kuokoa maisha ya watu hasa akina mama wanaojifungua katika maeneo ya vijijini.

Kwa upande  Mratibu wa The Energy Change Lab Sisty Basil amesema kuwa jukwaa hilo kwa waandishi litakalotoa mafunzo kwa muda wa miezi 6 ni endelevu na litawajengea  uelewa pindi wanaporipoti habari  kuhusu nishati.

Ameeleza kuwa mahitaji na huduma katika sekta ya nishati kwa sasa ni ya kuridhisha kwani asilimia 90 ya malengo yamefanikiwa katika kuwaunganishia wateja huduma hiyo huku serikali ikiwa na malengo ya kufika asilimia 70 katika sekta ya nishati. 
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) Deodatus Balile akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya waandishi wa habari kuhusiana na uhabarishaji wa habari za Nishati Jadidifu  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Nukta Afrika  Nuzulack Dausen akizungumza kuhusiana na mtaumizi ya habari za takwimu katika uandishaji habari katika eneo la habari za Nishati Jadidifu , uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa The Energy Change Lab Sisty Basil akizungumza kuhusiana na matumizi ya nishati zilizopo nchini kwa takwimu wakati uzinduzi wa mafunzo ya waandishi wa habari katika eneo la matumizi ya nishati mbadala .
Picha ya pamoja waandaji wa mafunzo pamoja na wahariri wa habari pamoja na waandishi wa habari

ZANZIBAR YAADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA WAZEE DUNIAN

$
0
0
 : Waziri  wa Fedha na Mipango Dkt. Khalid Salum Mohammed akizungumza na Wazee katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wazee duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Bakharesa Fumba Wilaya ya Magharib ‘B’ Zanzibar.
 Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Maudline Castico  akimkaribisha Mgeni rasmi Dkt. Khalid Salum Mohammed katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wazee duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Bakharesa Fumba Wilaya ya Magharib ‘B’ Zanzibar.
 Baadhi ya Wazee waliohudhuria katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wazee duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Bakharesa Fumba Wilaya ya Magharib ‘B’ Zanzibar.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

AIRTEL YAZINDUA MNARA WA MASAFA YA 3G MIKUMI, WATU ZAIDI YA ELFU 30 KUNUFAIKA WAKIWEMO WATALII

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua mnara wa mawaliano wenye uwezo wa kutoa huduma za Intanet kwa kiwango cha 3G kwa wakazi wa Kata ya Mikumi  ikiwa ni hatua ya Kampuni hiyo kurahisha huduma za masafa ya Mtandao kwa wateja wake na watalii wanaotembelea katika hifadhi ya taifa ya Mikumi.

Akizindua Mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mtandao kwa masafa ya 3G Diwani wa kata ya Mikumi Rivinus Mwawira amesema, Mbali na upatikanaji wa Masafa ya Mtandao lakini pia wakazi wake Zaidi ya elfu 30 watapata fursa mbalimbali za kimaendeleo kama kutuma na kupoke fedha kwa urahisi na pia huduma ya mawasiliano ya kawaida ya simu za mkononi.

“Mimi na wananchi wangu wa Mikumi tumekuwa na shauku kubwa ya kupata manara huu, lakini jambo kubwa zaidi ni upatikanaji wa Masafa ya 3G kwani utaturahisishia sana kazi zetu kwani ukiwa na Internet ya uhakika kila kitu kinakua rahisi”Amesema bw Mwawira

“Manufaa Mengine yanayopatikana kutokana na uwepo wa Mnara huu hapa kwetu ni pamoja na wanafunzi kujisomea kwa kutumia program mbalimbali zinazopatikana mtandaoni ikiwa ni pamoja na Masomo ya Ufundi ya VSOMO inayotolewa kwa ushirikiano baina ya Airtel na VETA” Amesisitiza Diwani huyo

Kwa upande wake Meneja mauzo wa Airtel Kanda ya Morogoro Gibson Renatus alielezea kuwa manufaa yanayopatikana baada ya kuzinduliwa kwa mnara huo katika eneo la mikumi ni pamoja na upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi, Huduma ya Airtel Money na huduma bora za mtandao za 3G.

Baadhi ya Wananchi wa eneo la Mikumi wameelezea furaha yao baada ya kuboreshwa kwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel katika eneo lao.

“Sasa hivi tunaweza kutuma na kupokea fedha kwa urahisi kupitia Airtel Money, tunapata internet yenye kasi ya 3G na pia hatupati tabu kupiga na kupokea simu tukiwa popote ndani nan je ya eneo letu la Mikumi” walieleza wananchi hao

Kuzinduliwa kwa mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano na mfumo wa Internet wa 3G utawawezesha wakazi Zaidi ya elfu 30 wa kata ya mikumi na maeneo ya jirani kutuma na kupokea fedha, kuwa na mawasiliano ya uhakika wakati wote, kutumia internet kupakua na kupakia taarifa mbalimbali na hivyo kurahisha shughuli zao za kila siku.

Diwani wa Kata ya Mikumi Rivanus Mwawira akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa kampuni ya simu ya Airtel  wenye uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano ya kawaida na masafa ya internet ya 3G katika eneo la Mikumi, Wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Wanaoshuhudia ni Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Morogoro Gibson Renatus mwenye Fulana Nyekundu na Maofisa wa serikali ya mtaa na kitongoji cha Mikumi Mjini
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Jackson Mmbando akitoa ufafanuzi kwa Diwani wa kata ya Mikumi Rivanus Mwawira mwenye Suti na Maofisa wengine wa serikali na watendaji wa kampuni ya  Airtel wakati wa hafla ya uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wenye uwezo wa wa kutoa huduma ya masafa ya 3G katika eneo la Mikumi, wilayni Kilombero mkoani Morogoro hivi karibu.

MHAGAMA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha sukari cha Mkulazi (Mbigili) Mkoani  Morogoro kujionea maendeleo ya Ujenzi wa kiwanda hicho kuelekea katika hatua ya kuanza uzalishaji.

Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Mhagama amewataka watendaji wa Mradi wa Ujenzi wa kiwanda hicho pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha wanatumia mradi huo kwa manufaa ya Taifa na kuwasisitizia wafanye kazi kwa weledi ili  kuendeleza kiwanda hicho wakizingatia uadilifu katika utendaji kazi wao.

"Lazima kila mmoja wenu atekeleze majukumu yake kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Serikali ili azma ya kuanzishwa kwa kiwanda hiki itimie, kwa kuwa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt John Magufuli ni kuhakikisha kuwa inajenga uchumi wa viwanda ambao ni jumuishi na unalenga kuwanufaisha wananchi wote na manufaa ya kiwanda hiki ni kwa wanachama". Alisisitiza Mhe Mhagama

Akifafanua Zaidi, amesema kuwa Kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji kitatoa ajira kwa watanzania wengi na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa letu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio  aliahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Waziri  Mhagama na kumhakikishia  kuwa watashirikiana na Bodi ya Wadhamini ya Shirika hilo kusimamia kwa uadilifu mkubwa mradi huo.

Pia alisisistiza kuwa wataendelea kufanya juhudi kubwa katika kutekeleza mipango yote itakayowezesha kuanza mapema iwezekanavyo kwa uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho.

Ziara hiyo ya Waziri Mhagama ililenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi pamoja na kukagau mashamba ya Miwa ya kiwanda hicho ili kujionea hatua iliyofikiwa katika kuelekea kwenye uzalishaji wa sukari na muelekeo wa uchumi wa viwanda nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio akimwelezea jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipotembelea kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Mbigili, Mkoani Morogoro alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akisisitiza jambo kwa watendaji wa kiwanda hicho na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. William Erio akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipotembelea mashamba ya miwa ya kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Mbigili, Mkoani Morogoro kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi Bw. Gerald Sondo akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) eneo la shamba walilopanda hekta 860 za miwa ambayo imekwa bila kutegemea umwagiliaji.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na watendaji wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kuhakikisha wanatumia mradi huu kuleta manufaa yanayotarajiwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Dkt. Mwakyembe avipa wiki mbili vilabu ya mchezo wa Kriketi kujisajili

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wiki mbili kwa vilabu vyote vya mchezo wa Kriketi nchini ambavyo havijasajiliwa  kufika Baraza la Michezo La Taifa kwa ajili ya kujisajili .
Akizungumza na wadau hao wa mchezo huo jana katika Ukimbi wa mikutano  uliopo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa ni wajibu wa kila kilabu cha mchezo nchini kufuata sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya michezo.
“Kama kuna kilabu chochote cha mchezo wa kikreti kipo na hakijasajiliwa, natoa wiki mbili  kuweza kufuata taratibu na sheria za usajili ili viweze kutambulika kisheria ” alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha aliongeza kwa kuutaka uongozi wa Chama cha Kriketi Tanzania kuhakikisha unatenga siku moja  kwa ajili ya mkutano na wanachama wake ili kupata nafasi ya kupitia vipengele vinavyounda katiba ya chama hicho kwa ajili ya maboresho mbalimbali.
Vilevile Waziri Dkt. Mwakyembe  alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali  zinazokikabili chama hicho cha mchezo wa Kriketi na kuhaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Kwa Upande wake Kaimu Katibu  Mtendaji wa Baraza la Michezo  la Taifa Bw.Makoye  Nkenyenge amewataka wanachama hao kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Dkt. Mwakyembe kwa kuhakikisha wanasajili vilabu vyote ambavyo havijasajiliwa.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na wadau wa mchezo wa Kriketi  alipokutana nao hapo jana katikati ukumbi wa mkutano uliopo Uwanja wa Taifa, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto) akieleza jambo kwa wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni  Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge. 
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge (kulia) akizungumza na  wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni  Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto). 
  Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania Bw. Taher Kitisa akizungumza wakati wa kikao kilichowahusisha wadau wa chama cha Kikreti pamoja na Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha), kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Mchezaji wa Kriketi ambaye pia ni Kocha wa mchezo huo Bw. Hussein Mohamedi akichangia jambo katika kikao kilichowahusisha wadau hao pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika Picha),katika kikao  kilichofanyika jana uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NFRA YAENDELEA KUSISITIZA UBORA WA MAZAO KUTOKA KWA WAKULIMA

$
0
0

Na Mathias Canal, NFRA

Zoezi la kununua nafaka ya mahindi kwa ajili ya akiba ya Taifa ya Chakula unaendelea katika maeneo mbalimbali kote nchini ambapo wakulima kwa kiasi kikubwa wameitikia wito uliotolewa na Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi yasiyokuwa na ubora.

Pamoja na Ubora wa mahindi kuwa changamoto katika maeneo mengi nchini kutokana na hali ya msimu wa mwaka Jana kuwa na jua Kali na mvua za msimu jambo lilolopelekea Mazao kuharibika yakiwa shambani.

Katika hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya ununuzi ambapo hivi tarehe 1 Octoba 2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika kituo hicho.

Katika ziara hiyo ya Mtendaji Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma, Meneja wa Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya alieleza kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya kwanza ya ununuzi na hadi kufikia leo tarehe 1 Oktoba 2018 Kanda hiyo imeshanunua zaidi ya tani 6000. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akikagua mahindi wakati wa ununuzi katika kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma. 
Afisa ubora wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Masanja akikagua mahindi kwenye kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOPOTOSHA MIPAKA YA KIJIJI CHA MABWEGERE KILOSA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA

$
0
0
Na Munir Shemweta, Morogoro 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji saba vya wilaya hiyo na mpango wa utekelezaji wake na kuagiza wote waliohusika kupotosha mipaka ya eneo hilo akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Lukuvi alitoa agizo hilo leo mkoani Morogoro wakati akikabidhi taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Jaji wa Mahakama Kuu ambaye sasa ni jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacob Mwambegele kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe kuhusiana na mgogoro wa mipaka ya kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mambegwa, Mbigiri, Dumila, Matongolo na Mfulu vilivyopo Wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. 

“Wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika process yote ambayo kwa kiasi fulani imeigharimu serikali fedha nyingi na kuipa maumivu serikali katika suala hilo ni lazima wachukuliwe hatua kali” alisema Lukuvi. 

Taarifa ya uchunguzi ilibaini chanzo cha mgogoro ni kukosekana ushirikishwaji wa vijiji jirani katika kuainisha na kuweka mipaka ya kijiji cha Mabwegere jambo lililosababisha kijiji kiwe na eneo la ukubwa wa hekta 10, 234 kuliko hata kijiji mama cha Mfulu chenye hekta 1,717 jambo lililothibitishwa na ukweli kwamba mipaka ya kijiji hicho imeingia ndani ya mipaka ya kata tatu za Mbigiri, Msowero, na Kitete ingawa kiutawala kijiji cha Mabwegere kinaratibiwa na kata ya Kitete. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro kabla ya kuikabidhi taarifa hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (kulia). Wengine katika picha Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda (wa pili kushoto) na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa mkoa wa Morogoro pamoja na watendaji wa Wilaya ya Kilosa wakati wa kukabidhi taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. kulia ni mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Wengine katika picha wa pili kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Bi. Merry Mwanjelwa.

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda.

aadhi ya viongozi wa halmashauri za vijiji saba wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa kuwapa taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.

Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na viongozi wa halmashauri za vijiji saba kuhusu taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro. 


Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images