Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MATAIFA ZAIDI YA 75 YASHIRIKI KONGAMANO LA MAFUTA NA GESI, SERIKALI YATOA NENO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SERIKALI imesema imejipanga vema kuhakikisha sekta ya nishati na hasa ya mafuta na gesi inawanufaisha Watanzania wote na kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano January Makamba wakati anafungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya mafuta na gesi wakati anamwakilisha mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Kongamano hilo limehudhuriwa na zaidi ya wadau 200 kutoka mataifa zaidi ya 75 duniani na moja ya ajenda ni kuangalia fursa ambazo zinaweza kupatikana katika sekta ya mafuta na gesi huku pia kongamano hilo likijita kuangalia fursa ambazo watanzania watanufaika nazo kutokana na uwepo wa miradi mikubwa inayoendelea nchini.

Hivyo Waziri Januari Makamba amesema ujumbe wa Waziri Mkuu katika kongamano hilo ni kwamba nchi imefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kunufaika na sekta ya gesi na mafuta.

"Pia Serikali imeweka maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuandaa rasilimali watu, miundombinu, watalaamu na mambo mengine muhimu kwa lengo la kuhakikisha sekta hiyo inawanufaisha Watanzania wote,"amesema Januari Makamba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano January Makamba akizungumza wakati akifungua kongamano la pili la wadau wa sekta ya mafuta na gesi jijini Dar es Salaam leo kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.
Waziri wa wizara ya Ardhi, nyumba, maji, nishati na mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.
Naibu waziri wa wizara ya nishati, Subira Mgalu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kongomano la wadau wa mafuta na gesi.
Muandaaji wa kongamano la mafuta na gesi ambaye pia ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi nchini Tanzania Abdulsamad Abdulrahim akifafanua jambo.

TADB, TUME YA UMWAGILIAJI WAJIPANGA KUCHAGIZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

$
0
0
Katika kutekeleza kwa vitendo jukumu la kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Tume ya Umwagiliaji ya Taifa (NIRC) ili kuchagiza kilimo cha umwagiliaji nchini.

Akizungumza wakati wa utiaji wa saini wa makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema benki imejipanga kuchagiza tasnia ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo.

“Ili kuninua uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo nchini benki imejipanga kuwekeza mtaji wa kutosha katika kilimo cha umwagiliaji,” alisema.

Bw. Justine aliongeza kuwa mpaka sasa TADB imeshatoa mkopo katika miradi 9 mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere alisema tasnia ya umwagiliaji ina mchango mkubwa katika kunyanyua uzalishaji nchini hatahivyo muitikio finyu wa wadau umekuwa ukirudisha nyuma tasnia hiyo.

Mhandisi Dkt. Matekere ameishukuru TADB kwa kuwa taasisi ya kwanza ya kifedha kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji.

“uwekezaji huu wa pamoja utasaidia kuongeza uzalishaji hali itakayowaongezea kipato wakulima nchini na hivyo kusaidia kupunguza umaskini wa kipato kwa wakulima hasa wanaolima kwa kutegemea mvua,” alisema.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini. anayemsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia).
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine.
 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto) akiongea wakati wa kikao hicho. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Sheria ya TADB, Bibi Neema Christina John.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TADB wakifuatilia kwa makini utiaji saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini.  
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) wakitia saini makubaliano yanayolenga Kuimarisha Uendelezaji wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere (kulia) wakionesha makubaliano hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA STIEGLER"S GORGE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge wakisimama kwa dakika kadhaa kuwakumbuka marehemu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Ukara wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza Septemba 20, 2018. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanza kwa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge pamoja na wataalamu wakati wa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.

LUGOLA AIBUKIA KITUO CHA POLISI KATORO, AWAHOJI WATUHUMIWA MAKOSA YAO WAKIWA WAMEPANGA FOLENI MAHABUSU, AWATAKA POLISI KUTOKUNYANYASA WANANCHI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi nje ya Kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, ambao walifika kituoni hapo kuripoti matukio mbalimbali. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo,ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Wapili kulia ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akihoji makosa ya watuhumiwa mbalimbali (hawapo pichani) waliopo katika mahabusu ya Kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, leo. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Katikati ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akiyaangalia kwa makini orodha ya majina ya watuhumiwa na makosa yao ambao wapo mahabusu ya kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, leo, wakati askari polisi wa kituo hicho, Janeth Shushu alipomletea kitabu cha taarifa mbalimbali za makosa yaliyoripotiwa kituoni hapo. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Katikati ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro.
Askari wa usalama barabarani wa Kituo cha Polisi Katoro, Mkoani Geita, Alau Mawanda (kushoto) akimuonyesha risiti Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), ambayo askari huyo alimkatia Dereva wa gari ndogo (hayupo pichani), baada ya kuvunja sheria za usalama barabani. Lugola akiwa njiani kuelekea Mkoani Kigoma, alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho ili kujua utendaji kazi wa askari polisi wa kituo hicho na pia kujua makosa ya watuhumiwa wote waliopo katika kituo hicho. Kulia ni Mkuu wa Kituo hicho, ASP Steven Kimaro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI JAFO ATOA SIKU MBILI KWA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA BAGAMOYO KUJIBU SAKATA LA VYOO KUFUNGWA SIKU TATU KATIKA STENDI YA MABASI

$
0
0
Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI )Selemani Jafo akizungumza na baadhi ya madereva na makondakta wanaofanya kazi zao katika stendi ya mabasi ya Wilayani Bagamoyo wakati wa alipofanya ziara yake ya kikazi ya kushitukiza kwa lengo la kusikiliza changamoto ya miundombinu ya vyoo inayowakabili na kuwalazimu kujisaidia katika mifuko ya plastiki pamoja na vichakani .

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

WAZIRI wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amefanya ziara ya kushitukiza katika stendi ya mabasi ya Wilayani Bagamoyo na kubaini kufungwa kwa choo kwa zaidi ya siku tatu bila ya kutumika kutokana na shimo lake kujaa maji  na kupelekea baadhi ya madereva,makondakta pamoja na abiria kupata usumbufu mkubwa na kuamua  kujisaidia katika mifuko ya plastiki aja kubwa na ndogo  na kwenda kuitupa kandokando  ya barabara  na wengine kujisaidia vichakani.

Jafo aliweza  kubaini kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema kwamba katika eneo la stedi hiyo ya mabasi kuna mapugufu mengi katika suala zima la miundombinu ya vyoo,pamoja na kuwepo kwa  miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuwa na  mashimo hivyo kuwapa wakati mgumu madereva katika utekelezaji wa majukumu yao.

Pia waziri Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa maafisa wa mazingira pamoja na afya wa Wilayani Bagamoyo kumwandikia barua ya maelezo kuhusiana na saakata la  kukithiri kwa uchafu huo sambamba na  kumwagiza  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kuunda tume kwa ajili ya kuweza kuchunguza kwa kina kuhusiana na baaadhi ya watu ambao wanafanya hujuma na kusababisha upotevu wa fedha za ushuru wa mabasi katika stendi hiyo.

“Kwa kweli hii hali mimi siwezi kuivumilia kabisa hata kidogo maana nimepata taarifa kwamba stedi hii inachangamoto mbali mbali lakini kubwa zaidi ni kufungwa kwa choo kwa zaidi ya siku tatu kutokana na kuwa ni kibovu, kwa hiyo sasa watu wanaangaika kweli kweli mpaka wanaamua sasa kwenda kujisaidia vichakani na kama haitoshi wengine wanatumia mifuko ya plastiki alafu wanakwenda kitupa hii sio sahihi hata kidogo,”alisema Jafo.

Kadhalika Jafo aliongeza kuwa kutokana na kukithiri kwa uchafu katika stendi hiyo ya mabasi kunaweza kusaababsiha mlipuko wa magonjwa mbali mbali hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka kwa wataalamu wa afya pamoja na mazingira zinafanyike haraka san ili kuweza kukabiliana na hali hiyo ambayo imekuwa ni kero kwa wananchi.

Nao baadhi ya madereva hawakusita kutoa kilio chao  kwa Waziri Japo ambapo wamedai kuwa wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa pindi wanapohitaji huduma ya kujisaidia na kwamba kwa sasa wapo katika mazingira hatarishi ya kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kukithiri kwa watu kujisaidia ovyo katika maeneo ambayo sio rasmi.

Aidha katika hatua nyingine Waziri Jafo katika ziara yake hiyo ya kikazi aliweza  kutembelea hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo n akuonyesha masikitiko yake makubwa kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji, na kutoa  muda wa siku 30 kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha  anatekeleza agizo lake alilolitoa la hospitali zote nchini kufunga mfumo wa kielekitroniki wa ukusanyaji wa mapato  unaofahamika kwa jina la Got Homis.

STENDI ya mabasi ya Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani imekuwa ikilalamikiwa kwa kipindi kirefu kutokana na kuwepo kwa changamoto mbali  mbali zinazoikabili ikiwemo kuwepo kwa miundombinu mibovu ya vyoo,ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji hususan madereva,makondakta pamoja na abiria  na kupelekea kuamua kujisaidia katika maeneo ambayo sio rasmi.

Tazama video fupi kuhusu ujenzi wa SGR TANZANIA Kipande cha Kwanza cha Reli kikitandikwa

WAZIRI MKUU AWATAKA WANANCHI KUWA WATULIVU KIPINDI HIKI CHA MAJONZI

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI


Senior Officials of SADC Ministries for ICT and Information meet in Namibia and observe a minute of silence for the lives lost in Tanzania ferry disaster

$
0
0

The Communications Technology (ICT) and Public Information from the Southern African Development Community (SADC) Member States are meeting on 24 – 25 September 2018, in Windhoek, Namibia. 
 The SADC Secretariat Deputy Executive Secretary for Regional Integration (DES-RI) Dr. Thembinkosi Mhlongo is leading the SADC Secretariat Team at the meetings which will review and prepare documents for the joint meeting of Ministers responsible for ICT, Information, Transport and Meteorology scheduled for 27, September 2018. 
The Senior Officials for the Transport and Meteorology sectors will be meeting on 25 – 26 September 2018, at the same venue. 
 The meeting was officially opened by the Deputy Minister in the Ministry of ICT in the Republic of Namibia Hon. Engel Nawatiseb, who noted that while significant progress has been made in implementing decisions aimed at achieving the SADC Regional Integration goals in the area of ICT, Telecommunication and Public Information, there was still much more to do for the well-being of the of SADC Citizens. 
 Hon. Nawatiseb highlighted the important role of the ICT and Information sectors noting that they are critical enablers of innovation, sustainable socio-economic development and catalysts to facilitate national priorities in all respects of the people in the SADC region. 
On Friday the delegates will be taken on a tour of two regional projects implemented in Namibia, namely the Swakopmund Submarine Landing Station, and the Port of Walvis Bay, which aim to facilitate access to affordable Internet and movement of goods, respectively. 
 In the SADC spirit of solidarity, the Deputy Minister invited delegates to observe a minute of silence in remembrance of the lives lost in the United Republic of Tanzania last week, during a ferry accident that led to the loss of more than 200 lives. 
The ferry was traveling from Bugolora to Ukara Island when it capsized 200 meters (about 650 feet) from its destination. The SADC meetings of Senior Officials provide a technical advisory role and review documents in preparation for the Sectoral Ministers’ meetings.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 24.09.2018

VIONGOZI WA DUNIA WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA MAAFA YA MV NYERERE

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeendelea kupokea salamu za rambirambi kutoka kwa marais, mawaziri wakuu wa mataifa mbalimbali duniani kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea kwenye Ziwa Victoria, Mkoani Mwanza tarehe 20 Septemba, 2018 na  kusababisha vifo, majeruhi na upotevu wa mali.
Baadhi ya salamu zilizopokelewa ni pamoja na kutoka kwa Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, Rais wa Urusi, Mheshimiwa Vladmir Putin, Rais wa China, Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier, Rais wa Saharawi, Mheshimiwa Brahim Ghali, Mtawala wa Kuwait, Mtukufu Sheikh Sabah Al-Ahmad al Jaber Al-Sabah, Baba Mtakatifu, Papa Francis, Rais wa Italia, Mheshimiwa Sergio Mattarella, Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Finland, Mheshimiwa Sauli Niinistö, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange na Rais wa Jamhuri ya Sudan, Mheshimiwa Omar Hassan Ahmed Al-Bashir.  
Viongozi wengine ni Waziri Mkuu wa Israel, Mheshimiwa Benjamin Netanyahu, na Waziri Mkuu wa Sweden, Mheshimiwa Stefan Löfven. Viongozi hao wameeleza kusikitishwa kwao na taarifa za vifo vilivyosababishwa na  ajali hiyo na kuwatakia majeruhi kupona haraka.

African Court Judges mourn victims of ill-fated MV Nyerere ferry

$
0
0
The African Court Judges observed a minute’s silence before the start of their Ninth Extra-Ordinary Session  in Arusha in the memory of over 220 Tanzanians who drowned in the ill-fated MV Nyerere ferry last Thursday in Lake Victoria.

UONGOZI WILAYA YA SAME WARIDHISHWA NA MRADI WA KILIMO HIFADHI UNAVYOTEKELEZWA WILAYANI HUMO.

$
0
0
UONGOZI wa Halimashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro umeonyesha kuridhishwa kwake na namna Mradi wa Kilimo Hifadhi unaotekelezwa wilayani humo na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania ulivyoweza kuwasaidia wakulima kwa kupata mavuno mengi ukilinganisha na hapo awali. 

Kauli hiyo imetolewa Jana na Kaimu Mkurugenzi wa halimashauri hiyo John Nnko,Wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) waliofika wilayani humo kujionea utekelezaji wa Mradi wa kilimo Hifadhi unaotekelezwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania.

Alisema kuwa mpaka sasa kumekuwa na mwikitio mkubwa wa wakulima kutaka kujifunza zaidi namna ya kulima kilimo hifadhi hasa katika mazao ya mahindi na maharage ambapo alilishukuru Baraza la Kilimo kwa kutekeleza Mradi huo wilayani Same ambao unawafanya kupata mavuno mengi na kutokuwa na hofu ya ukame.

“Mpaka sasa Mradi huu wa Kilimo Hifadhi umekwisha kuwafikia zaidi ya wakulima 1,300 na uko katika vijiji tisa pekee, lakini tunaona mwitikio wa wakulima unazidi kuwa mkubwa wa kutaka kujua namna ya kulima kwa kutumia teknolojia hii, kwakweli ACT tunawashukuru sana kwa sababu pia hata watalaamu mmetuletea nyie” Alisema.

Miongoni mwa vijiji vinavyotekeleza mradi huo wilayani humo ni pamoja na Saweni, Hedaru,Kisiwani, Njiro, Mpirani na Ishinde ambapo wakulima waliueleza ujumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya ACT iliyofika katika mashamba yao kuwa tangu mradi huo wa Kilimo hifadhi ulipoanza mwaka 2011 vipato vyao vimeimarika huku gharama za uandaaji wa mashamba zikipungua.

Bw. Paul Mtango ambaye ni Mkulima wa Kijiji cha Mpirani Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) mfumo alioutumia kupanda Maharage katika shamba lake kwa kutumia Kilimo hifadhi, mfumo unaowafanya wakulima kupata mazao mengi tofauti na walivyokuwa wakilima awali.
Bw. Paul Mtango ambaye ni Mkulima wa Kijiji cha Mpirani Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania waliofika shambani kwake kujionea namna anavyonufaika na mradi wa kilimo hifadhi unaoratibiwa na ACT/TAP ambapo amewaeleza kwa kutumia Kilimo Hifadhi anaweza kupata gunia 12 za maharage kwa heka moja tofauti na awali alipokuwa akipata gunia 3 kwa hekari..
Bw. Paul Mtango ambaye ni Mkulima wa Kijiji cha Mpirani Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) waliofika shambani kwake kujionea namna anavyonufaika na mradi wa kilimo hifadhi unaoratibiwa na ACT/TAP, kuhusu namna kilimo hifadhi kinavyohifadhi ardhi vizuri kwa kizazi kijacho.

WAKULIMA WADOGO WA MKONGE WAIPINGA KAMPUNI YA KATANI MBELE YA WAZIRI WA KILIMO WATAKA MFUMO WA SOKO HURIA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Tanga

Wakulima wadogo wa zao la mkonge Wilayani Korogwe mkoa wa Tanga, wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuanzisha soko huria kwa ajili ya ununuzi wa zao hilo ili malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha tani 100,000 kwa mwaka yafikiwe.

Wakulima hao wameilalamikia Kampuni ya Katani Ltd. kwamba inachukuwa asilimia 54 na kumuachia mkulima asilimia 46 jambo walilodai ni unyonyaji unaofanywa na kampuni hiyo kinyume na utaratibu wa kiutendaji.

Wakulima hao wametoa malalamiko yao mbele ya waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza na wananchi katika maeneo tofauti wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili kutekeleza maagizo aliyopewa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ya kutembelea mashamba ya Mkonge mkoani humo na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.

Katika mkutano huo pia wakulima hao walijadili suala la bei na namna ambavyo sera iliyowekwa na serikali inayoelekeza kuwa kila mwaka mkonge uzalishwe tani 100,000 na kwamba sera hiyo haisimamiwi ipasavyo kwani endapo kama ikisimamiwa ipasavyo zao hilo litaingia kwenye zao kuu la kibiashara nchini.
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi katika Wilaya ya Korogwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK, Tanga)
Kikao kazi wakulima wa zao la Mkonge na Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba kilichofanyika katika kijiji na kata ya Makuyuni Wilaya ya Korogwe wakati wa ziara ya waziri huyo ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga, jana tarehe 24 Septemba 2018. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akitoa maelezo mafupi Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba kuhusu zao la Mkonge mkoani humo mbele ya wakulima wakulima katika kijiji na kata ya Makuyuni, Wilayani Korogwe jana tarehe 24 Septemba 2018. 
Wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi wilaya ya Korogwe wakifatilia kwa makini mkutano wa Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba wakati wa mkutano wa pamoja kujadili zao la Mkonge Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi wilaya ya Korogwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018.

Introducing VIDEO Ya WIMBO Mpya Wa Akil The Brain "Mashallah"


MEJA JENERALI MASANJA AMEVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI TABORA KWA MSHIKAMANO

$
0
0
Na Tiganya Vincent
Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wa Serikali Mkoani Tabora kwa kufanya kazi zao kwa ushirikiano ambao umesaidia kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao.

Alisema vyombo hivyo vinapaswa kuwa kitu kimoja jambo ambalo litawasaidia kubadilishana taarifa ili kufichua vikundi vya kihalifu kwa ajili ya kuhakikisha amani na salama miongoni mwa wananchi.

Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Masanja alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Viongozi wa Serikali , Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania alipotembelea Ofisi ya Mkoa wa Tabora.

“Sio kila chombo kiende njia yake lazima kuwepo na umoja na mshikamano katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi” alisema.

Aliongeza kuwa na kila  Wananchi analo jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi kwa kuchukua hatua za kutoa taarifa juu ya  vikundi vya uhalifu katika maeneo yao ambazo zitaviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kuzuia uhalifu.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akimkaribisha Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja ili aweze kuzungumza na viongozi mbalimbali na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora. 
 Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja akizungumza na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya(kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(kulia) na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora. 
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya akuzungumza na viongozi mbalimbali na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati wa Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora wakisikiliza Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja (hayupo katika picha) wakati alipotembelea Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 Mkuu wa Utumishi Jesheni Meja Jenerali  Blasius Kalima Masanja akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komaya( wa tatu kutoka kushoto) , Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( wa tatu kutoka kulia) na Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa mara baada ya kutembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA LIWALE NA UDIWANI KATIKA KATA 37

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi  ilitangaza tarehe 13 Septemba 2018 kuwa siku ya uteuzi wa wagombea Ubunge  katika jimbo la Liwale Mkoani Lindi  na tarehe 21 Septemba 2018  kuwa siku ya uteuzi kwa wagombea Udiwani katika  kata 37 zilizopo katika Hamashauri ishirini na saba na mikoa kumi na tatu ya Tanzania Bara.  
Hata hivyo, baada ya uteuzi huo Tume imepokea malalamiko kupita vyanzo mbalimbali  juu ya kutotendewa haki kwa baadhi ya wagombea Udiwani katika baadhi ya maeneo yenye chaguzi hizo.
Tume, imefanya ufuatiliaji na kupokea taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya  wasimamizi wa uchaguzi kwenye maeneo  yanayolalamikiwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya wasimamizi hao wagombea ambao hawakuteuliwa ni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuwekewa pingamizi, kutorejesha fomu siku ya uteuzi, kujitoa baada ya kuteuliwa na baadhi kutotimiza masharti ya  uteuzi ambayo ni ujazaji wa fomu za uteuzi kikamilifu na kutotimiza idadi ya wadhamini inayokubaliwa kisheria.
Maeneo ambayo wagombea wake wamewekewe Pingamizi na wagombea wenzao ni pamoja na kata ya Kibutuka  Halmshauri ya wilaya ya Liwale, Kata ya Ruvu Halmashauri ya Wilaya Kibaha, Kata ya Njianne Halmasahuri ya wilaya Mkuranga, Kata ya Jibondo na Kilindoni Mafia na  Kata ya Ikwiriri  Halmashauri ya Rufiji, ambapo ni Wagombea wa CUF waliowekewa Pingamizi.
Aidha, katika Halmashauri zote ambazo wagombea wa CHADEMA walichukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya udiwani hawakurejesha fomu hizo kwa ajili ya uteuzi.
Vile vile, Baadhi ya  wagombea mfano Mgombea wa CUF kata ya Ruaruke, Wagombea ACT WAZALENDO na CUF katika  kata ya Mailimoja  na Mgombea wa ACT WAZALENDO katika kata ya Mbwawa zote kutoka Halmashauri ya Mji wa Kibaha hawakuteuliwa kwa sababu hawakurejesha fomu za uteuzi.
Wengine ambao hawakurejesha fomu ni mgombea wa CUF kata ya Kisiju Halmshauri ya Mkuranga, mgombea wa CUF na mgombea TLP  kata ya Mjimwema Halmashauri ya Kigamboni.
 Aidha, katika kata  ya  Kagando wagombea wa CUF,TLP NCCR-MAGEUZI  na ACT WAZALENDO na  Kata ya Hamugembe Mgombea wa CUF wote wa  Halmashauri ya  Manispaa ya Bukoba hawakurejesha fomu ili wateuliwe.
Vile vile, katika Halmashauri ya Kakonko kata ya Rugenge mgombea wa CUF hakurejesha fomu na mgombea wa NCCR-MAGEUZI Katika Halmashauri ya Sumbawanga kata ya Ikozi hakurejesha fomu pia.
Katika Halmashauri ya wilaya ya Geita wagombea wa Vyama CCK na ADC hawakurejesha Fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi kata ya Nyankumbu, wakati huo huo wagombea wa CUF na NCCR-MAGEUZI kata ya QURUS hawakurejesha fomu za uteuzi. Wakati katika Halmashauri ya Monduli Mji mgombea wa ACT WAZALENDO hakurejesha Fomu.
Baadhi ya wagombea  hawakuteuliwa kwa kuwa hawakujaza fomu za uteuzi kikamilifu ikiwemo kutotimiza idadi ya wadhamini  na wengine kutodhaminiwa na Vyama vyao vya Siasa. Mfano; Wagombea wa CUF katika kata za Jibondo na Kilindoni Halmashauri ya wilaya Mafia, wagombea wa CUF na ACT WAZALENDO Kata ya Mabatini Halmashauri ya Nyamagana hawakuteuliwa kutoka na mapungufu haya.
Vile vile, kuna baadhi ya wagombea waliojitoa baada ya uteuzi, hili limejitokeza katika Halmashauri ya Babati mji ambapo mgombea wa CUF kata ya Sigino alijitoa baada ya kurejesha fomu kabla ya muda wa uteuzi kumalizika, na pia Halmashauri ya Geita Mji kata ya Nyankumbu ambapo wagombea wa ACT WAZALENDO na CUF walijitoa pia baada ya kuteuliwa.
Kwa ujumla hiyo ni taarifa ya awali katika zoezi la uteuzi wa wagombea Ubunge na Udiwani katika kata 37 uliofanyika katika  maeneo mbalimbali yenye uchaguzi. Katika Uchaguzi huu vyama vya ACT WAZALENDO, CCM, CUF, DP, NCCR –MAGEUZI, NRA na SAU vitashiriki kwa kuwa vimesimamisha wagombea.
Taarifa kamili kuhusu  zoezi la uteuzi ikiwemo matokeo ya rufaa  itatolewa hapo baada  mchakato wote kukmilika.

Imetolewa na,
Mkurugenzi wa Habari na Elimu kwa Umma Tume ya Taifa ya uchaguzi

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WAENDELEA NA KIKAO CHA BARAZA HILO ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheiri akifafanua baadhi ya maswala yalioulizwa ndani ya kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Chukwani Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Maalim akijibu maswali ndani ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
 Naibu Waziri Wizara ya Biashara na Viwanda Hassan Hamis Hafidh akijibu maswali ndani ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
 Naibu Waziri Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdalla akijibu maswali ndani ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar..
 Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohamed Raza akiwa ndani ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi akisikiliza michango mbalimbali inayotolewa na wajumbe katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Chukwani Zanzibar.
 Muakilishi wa Jimbo la Chake chake Suleiman Sarahan Said kushoto akibadilishana mawazo na Muakilishi wa Jimbo la Pangawe Khamis Juma Mwalim ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico akiwa na wageni wake Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Mahotelini na Majumbani CHODAU nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani  Zanzibar . PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

LUGOLA ATAKA ASKARI POLISI, UHAMIAJI WASIOKUA WAAMINIFU VIZUIZINI KUDHIBITIWA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Kakonko
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanawadhibiti baadhi ya askari Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya kujihusisha na vitendo vya rushwa, kunyanyasa wananchi katika vizuizi pamoja na maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Lugola pia aliitaka kamati hiyo kushirikiana na vyombo vya dola mkoani humo katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa shughuli za Wizara yake anayoiongoza ni mtambuka.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Lugola alisema vyombo vya dola vifanye kazi kwa weledi na kuwezesha utekelezaji  wa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano, hasa katika kuwezesha Tanzania ya viwanda.
“Vyombo vyetu vya dola visikwamishe shughuli za watu wengine na taasisi nyingine zisitumie vyombo hivyo kukwamisha bali kuwezesha,” alisema Lugola na kuongeza kuwa;
“ Kamati hii ya Ulinzi na Usalama ya mkoa akikisheni mnawasimamia vizuri viongozi wa vyombo katika kudhibiti askari wachache wanaoharibu sifa za Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na wengineo kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na kunyanyasa wananchi,” alisema Lugola.
Aidha, Waziri Lugola aliwataka askari wa usalama barabarani wasimamie sheria na wawe wakali na wasitishwe na mtu ila wasionee wananchi.
Lugola, pia aliwataka Makamanda wa Mkoa huo wahakikishe magari yanakaguliwa, madereva wanapimwa vilevi na askari wa usalama barabarani wawe wakali katika kusimamia sheria bila kuangalia cheo wala wala hadhi ya mtu ila akasisitiza wasionee mtu.
Waziri Lugola ameanza ziara yake ya kutembelea mikoa yote nchini kwa kuanzia Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.
 Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Julius Samwel, akimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) Jengo la Wilaya hiyo, alipowasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Simon Mando.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Wilaya ya Kakonko (upande wa kushoto) pamoja na Kamati ya Mkoa (upande wa kulia) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, leo. Lugola aliwataka wajumbe hao kuwadhibiti baadhi ya askari Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya kuomba rushwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika vizuizi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, Julius Samwel (kushoto) alipokua anatoa taarifa ya Wilaya ya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, leo. Lugola aliwataka wajumbe wa Kamati hiyo pamoja naya Mkoa huo kuwadhibiti baadhi ya askari Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya kuomba rushwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika vizuizi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (aliyeshika kitabu) akitoka katika ofisi ya Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, akielekea katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kwa ajili ya kufanya kikao na Wajumbe wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Wilaya ya Kakonko pamoja na Kamati ya Mkoa, leo. Katika kikao hicho, Waziri Lugola aliwataka wajumbe hao kuwadhibiti baadhi ya askari Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya kuomba rushwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika vizuizi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

VYUO VIKUU SABA VYAZUILIWA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA

$
0
0
*Vingine vyaamriwa kusitisha utoaji wa mafunzo
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
VYUO Vikuu saba nchini vimezuiliwa kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika programu zote.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Charles Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi huo.

Wakati huohuo vyuo vitano vimeamriwa kusitisha utoaji wa mafunzo na kwa wanafunzi na wanaoendelea na masomo kuhamishwa mara moja.

Pia vyuo vingine viwili vimeamriwa kuwahamisha wanafunzi wote wanaoendelea na masomo kwani tume hiyo imefuta vibali vya vyuo hivyo.

Akifafanua zaidi Kihampa amesema Vyuo hivyo saba ambavyo vimezuiliwa kudahili wanafunzi wapya ni pamoja na Chuo kikuu cha Kimataifa cha kampala nchini Tanzania (KIUT), Chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo kikuu kishiriki cha Marian (MARUCO), Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Kadinali lugambwa CARUMUCo na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKUMU).

Pia Chuo kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania kituo cha Mt. Marko (SJUT- St. Mark's c3ntre ) na Chuo kikuu cha umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) . 

Wakati vyuo vilivyoamriwa kusitisha utoaji mafunzo na kuamriwa kuhamisha wanafunzi wote ni pamoja na Chuo Kikuu cha Mlima Meru (MMU),Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo Kikuu cha ECkernforde Tanga (ETU), 

Chuo kikuu cha kilimo cha na Teknologia cha Jomo Kenyatta-Kituo cha Arusha (JKUAT) Kituo cha Arusha na Chuo kikuu Kishiriki cha Josiah Kabira. (JOKUCo).

Kihampa amesema kuwa baadhi ya vyuo vipo katika uangalizi wa Tume ya vyuo kikuu Tanzania na vinaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazo zote za masomo kuanzia Astashahada, Stashahada, Shahada, Shahada ya Uzamili, hadi shahada ya Uzamivu kwa programu zote mpaka vitakapoamriwa.

Pia tume ya vyuo vikuu Tanzania imevitaka vyuo vyote kuzingatia na kutekeleza maagizo waliyopewa na inawaarifu wanafunzi wote wanaotakiwa kuhama kuwasiliana na vyuo vyao kwaajili ya maelekezo kuhusu kuhama na vyuo wanavyotakiwa kuhamia.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Bodi ya Mikopo Tanzania Deus Changala amesema kwa wanafunzi waliokuwa na mikopo katika vyuo hivyo wasiwe na wasiwasi mikopo yao wataendelea kuipata wakati wakiwa kwenye vyuo watakavyohamia.
Mtendaji wa Mkuu wa Tume ya Vyuo vikuu Tanzania Charles Kihampaakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kusitisha utoaji wa mafunzo katika vyuo mbalimbali pamoja na kuamru wanafunzi wanaoendelea na masomo kuhamishwa katika vyuo vyao na kuhamia vyuo vingine.Kushoto ni Mwakilishi wa bodi ya mikopo, Deus Changala.
Mtendaji wa Mkuu wa Tume ya Vyuo vikuu Tanzania Charles Kihampaakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>