Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli avunja Bodi ya TEMESA


POLISI MBEYA YAMSHIKILIA MWANAFUNZI KWA TUHUMA ZA KUTUPA MTOTO CHOONI

$
0
0
 KUTUPA MTOTO – JIJINI MBEYA. 

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la INES MTUNDU [19] Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari SEBAMA iliyopo ndani ya majengo ya Ottu, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya kwa kosa la kumtupa chooni mtoto mchanga wa masaa kadhaa. 



Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.09.2018 majira ya saa 09:53 asubuhi huko maeneo ya Isengo – Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mjamzito na mara baada ya kujifungua chooni ndipo alimtupa mtoto huyo. 


Mara baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi, jitihada za haraka zilifanyika kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo akiwa hai. Mama na mtoto huyo wote wapo Hospitali ya Wazazi – Meta wakipatiwa matibabu. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani. 


KUPATIKANA NA BHANGI – KYELA. 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la GOLIATH EMANUEL [43] Mkazi wa Kasumulu Wilaya ya Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi debe sita nyumbani kwake. 
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 22.09.2018 majira ya saa 23:47 usiku huko Kasumulu, Kata ya Ngana, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela katika msako uliofanyika maeneo hayo. Mtuhumiwa alikuwa ameificha bhangi hiyo katika mifuko ya salfeti nyumbani kwake. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani. 

MAUAJI – CHUNYA. 

Mnamo tarehe 22.09.2018 majira ya saa 15:00 alasiri huko katika kitongoji cha kasisi, kijiji cha nkwangu, kata ya upendo, tarafa ya kipembawe, wilaya ya chunya, mtu mmoja aitwaye LUTONJA LUKELESHA [33] Mkazi wa Kasisi alifariki dunia akiwa anajipatia matibabu kienyeji nyumbani kwake. 

Inadaiwa kuwa marehemu alipigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kukanyagwa kwa miguu kifuani na tumboni siku ya tarehe 12.09.2018 majira ya saa 12:09 mchana huko kijiji cha Kasisi na kaka yake aitwaye MASANILA LUKELESHA [45] Mkazi wa Kasisi akiwa na wenzake wawili. 

Chanzo cha tukio hili ni tuhuma za wizi wa radio ndogo yenye thamani ya Tshs 15,000/= ya mmalila mchoma mkaa ambaye jina lake halisi bado kufahamika. Mtuhumiwa mmoja MASANILA LUKELESHA amekamatwa na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili waliokimbia unaendelea. 

Katika kudhibiti ajali za barabarani, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na doria katika maeneo ya mlima nyoka [barabara kuu ya Mbeya-Njombe-Iringa], mlima iwambi [barabara kuu ya Mbeya – Tunduma], mlima Igawilo [barabara kuu ya Mbeya – Tukuyu] na Kawetele [barabara kuu ya Mbeya – Chunya]. Aidha katika operesheni ya kukamata bajaji zinazokiuka sheria za usalama barabarani ndani ya Jiji la Mbeya kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2018 jumla ya bajaji 170 zimekamatwa, madereva 31 wamefikishwa Mahakamani na bajaji 91 zimelipa tozo sawa na Tshs.2,730,000/= na bajaji 75 bado zipo kituoni kwa hatua zaidi za kisheria na watuhumiwa 14 wapo rumandewakiendelea na mashauri yao. 

Imesainiwa na: 
[ULRICH O. MATEI - SACP] 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MGALU ATHIBITISHA GATI LA NYAMISATI HALIHAMISHWI,LINATARAJIWA KUGHARIMU BIL.14

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI .

NAIBU Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu amethibitisha kuwa serikali inaendelea kujenga gati la Nyamisati, Kibiti, mkoani Pwani na haina mpango wa kulihamisha ambapo linatarajiwa kugharimu sh. bilioni 14 hadi kukamilika kwake. 

Amewatoa shaka hiyo wananchi ambao walikuwa wakidai ujio wa ujenzi wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto Rufiji, Hydro Power (Stigilers Gorge )unaweza kusababisha athari za ujenzi wa gati hilo kwenda kisiwa cha Mafia. 

Subira aliyasema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa Nyamisati,  mara baada ya kutembelea ujenzi wa gati hilo .Alisema  mradi wa ujenzi wa gati hilo umefanyiwa utafiti wa kina na kubaini  hautakuwa na athari zozote za kimazingira .

Subira alieleza, baadhi ya watu wanadai kuwa eneo hilo la gati kina cha maji kitapungua suala ambalo sio la kweli ."Wataalamu wa mradi wa Hydro Power na gati walikaa kubadilishana uzoefu, na ripoti yao inaonyesha hakutakuwa  na athari za kimazingira "
  Naibu waziri wa nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Nyamisati wilayani Kibiti.

Naibu waziri wa nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kulia)  akimuelekeza jambo meneja wa ujenzi wa mradi wa gati la Nyamisati kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Erick Madinda (kushoto) kabla ya waziri huyo kuzungumza na wananchi wa Nyamisati wilayani Kibiti.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

NEWZ ALERT:MBUNGE WA MTAMA NAPE NNAUYE ANASURIKA KIFO BAADA YA GARI ALIYOKUWA AKISAFIRIA KUPATA AJALI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi Blog

MBUNGE wa Mtama Nape Nnauye(CCM) amenusurika kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali.

 Nape amepata ajali hiyo leo asubuhi katika Kijiji cha Kibutuka akiwa njiani kuelekea Liwale kwa ajili ya kushiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa.

Taarifa ambazo Michuzi Blog imezipata asubuhi zinaeleza kuwa ndani ya gari hiyo Nape alikuwa ameambatana na watu wengine wanne ambao wote ni wazima na hamna aliyedhurika. 
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi amepata ajali akiwa safarini kuelekea wilayani Liwale kushiriki kikao cha kamati kuu ya siasa ya mkoa wa Lindi ikiwa ni pamoja na kuungana  na ziara ya Katibu mkuu wa CCM Taifa Bashiru Ally anayoifanya wilayani Liwale. Katika ajali hiyo hakuna kifo
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kibutuka wakilitazama Gari lenye namba za usajiri T 349 DEL likiwa limepinduka  

MAGAZETI YA LEO JAMATATU SEPTEMBA 24, 2018

MWILI WA MAREHEMU WAFUKULIWA BAADA YA MUMEWE KUKIRI KUMUUA NA KUMFUKIA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

MWILI wa marehemu Celina Sulubu, mkazi wa Lubambawe wilayani Mkuranga,mkoani Pwani umefukuliwa kwa taratibu za kisheria baada ya mumewe Selemani Hija Usumba kukiri kumuua mkewe huyo. 

Mnamo septemba 21 Usumba inadaiwa alifika kituo cha polisi Mkuranga na kuripoti kuwa mkewe Celina ametoweka nyumbani kwake tangu septemba 13 mwaka huu. 

Kamanda wa polisi ,mkoa wa kipolisi Rufiji ,Onesmo Lyanga alisema baada ya kupokea taarifa hiyo mkuu wa upelelezi wilaya ya Mkuranga alifungua jalada la uchunguzi na kumshikilia kwa mahojiano na uchunguzi zaidi . 

Alieleza ,katika mahojiano ya awali alikiri kumuua mkewe kwa kumkaba shingoni na kumsababishia kifo mkewe.Lyanga alisema ,baada ya kutenda kitendo hicho aliamua kuchimba shimo kwenye shamba la jirani ambalo alikabidhiwa kulilinda na kisha kumzika . 

"Mnamo septemba 22 timu ya makachero ikiongozwa na mkuu wa upelelezi wilaya ya Mkuranga pamoja na mashahidi mbalimbali wa tukio hili walifika eneo la tukio kwa kuongozwa na mtuhumiwa " alifafanua Lyanga. 

Lyanga alisema ,baada ya kufika eneo hilo mtuhumiwa alionyesha eneo alilozika mwili wa marehemu na kuanza kuufukua mwili huo kwa taratibu za kisheria. Kamanda huyo alibainisha ,mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi . Lyanga alisema ,chanzo cha tukio hili bado unachunguzwa. 

Aliwaonya wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani nao hawatasalimika.
Mwili wa marehemu Celina Sulubu, mkazi wa Lubambawe wilayani Mkuranga,mkoani Pwani ukifukuliwa kwa taratibu za kisheria baada ya mumewe Selemani  Usumba kukiri kumuua mkewe huyo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi) 

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA-ZANZIBAR

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Baozi Seif Ali Idd (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi (kulia) wakiwa wamesimama kwa dakika moja kama ishara ya kuwaombea marehemu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu Maalumcha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi mabati ya kisasa kwa ajili ya tawi la CCM Urusi lililopo Jang'ombe kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa kwenye ziara yake mapema mawaka huu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SHULE YA QUEEN’S KUJENGA MAABARA YA SAYANSI KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NA AWALI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema kuanzishwa kwa maabara ya sayansi kwa ngazi ya shule za msingi kutasaidia upatikanaji wa wataalamu wa fani hiyo nchini badala ya wataalamu hao kutokana nje ya nchi. 


Mjema amesema hayo jijini Dar es salaam Septemba 22 wakati wa akiweka  jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya kompyuta, ukumbi na mkataba ya shule katika shule ya msingi na awali Queen's pamoja na mahafali ya nane kwa wanafunzi wa awali na darasa la saba. 

Amesema si Mara nyingi sana shule za awali na msingi wakawa na maabara watoto wanaanza wakiwa wachanga watakapofika sekondari watakua wazuri sana ukizingati tuko katika serikali ya uchumi wa viwanda. 

" Tunaanza kuwajenga watoto sasa hivi sisi tunataka kama serikali wataalamu hawa watakua Wahandisi na marubani ambao watatumika maeneo mbalimbali ya viwanda watatoka hapa hapa nchini na hatutaweza kuwategemea wataalamu kutokana nje ya nchi waje hapa" amesema Mjema. 

Aidha ameongeza kuwa wao kama serikali wameunga mkono jitihada hiyo, hivyo shule nyingi zitaanza kuiga mfano wa shule ya msingi ya Queen's ya kuwa na maabara kwa ngazi ya awali na serikali wanampango wa kuanzisha programu hiyo. 

" Serikali tuna mipango mingi tukipata wadau kama nyinyi ambao mtatusaidia hilo litakua jambo pekee sana kwetu" ameongeza Bi Mjema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule ya Msingi na awali Queen's Bi Lilian wasira amesema wako hawako kibiashara, shule ipo kwa akili ya kuendeleza elimu kwa jamii wanataka kutengeneza kizazi cha taifa la kesho 

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza katika mahafali ya Nane katika Shule ya Msingi na Awali ya Queen’s iliyopo Ukonga Tabata jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Shule ya Msingi na Awali ya Queen’s Anna Mwalongo akizungumza kuhusiana na shule hiyo kufanya vizuri katika matokeo kwa wanafunzi wanaosoma hapo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikata Keki kwa ajili ya wahitimu na wazazi katika shule ya Queen’s.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Queen’s Samweli Mwakipesile akizungumza kuhusiana na ujenzi wa Ghorofa kwa ajili ya mabara ya komputa katika shule hiyo.
 Wanafunzi wa Shule ya Queen’s wakitupwiza katika mahafali ya Nane ya Shule hiyo. 
Mkurugenzi wa Shule ya Queen’s Lilian Wassira akiwa amenyanyua mkono kwa ajili ya kuwashukuru walimu wa shule hiyo katika picha hiyo ya pamoja.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA SHUGHULI ZA UOKOAJI MV NYERERE

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watu walionusurika  katika  ajali ya kivuko cha MV Nyerere wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Bwisya  kisiwani humo Septemba 24, 2018. Wengine ni mwananchi ambao bado wamepotelewa na  ndugu na jamaa katika ajali hiyo wakisubiri kutambua miili endapo itaonekana. 
 Gari la wagonjwa  likiwa limeegeshwa kwenye jengo la Kituo cha Afya cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani  Ukererwe ili kuteremsha mwili wa mtoto  ambao waokoaji  waliupata katika kivuko cha MV Nyerere Septemba  24, 2018. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea kituo hicho leo asubuhi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akikabidhi  kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isaack Kamwelwe mchango wa sh. milioni 10 zilizotolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia katika  ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  kilichozama ktika kisiwa cha Ukara wilayaniu Ukerewe, Septemba 20, 2018.  Makabidhiano hayo yalifanyika  katika kijiji cha Bwisya kisiwani Ukara, Septemba 24, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Venance Mabeyo  baada ya kumkabidhi jukumu kuwa msimamizi mkuu wa operesheni ya uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Septemba 24, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati)  na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustine Kamuzora kwenye kijijii cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe baada ya Waziri Mkuu kutembelea eneo kilipozama kivuko cha  MV Nyerere kijijini hapo Septemba 24, 2018.

ELIMU YA MSAMAHA WA KODI YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA MANYARA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto Manyara.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi kwa wafanyabiashara, washauri wa wafanyabiashara na wakaguzi wa hesabu mkoani Manyara ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wale wote wenye madeni ya kodi yanayotokana na riba na adhabu kuomba msamaha kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.



Akiwasilisha mada kuhusu msamaha huo, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla amesema kuwa, lengo la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha kwamba, kila mfanyabiashara mwenye malimbikizo ya madeni ya kodi anapata taarifa na kufuata taratibu za kuomba msamaha huo.

"Mpaka sasa TRA imeshatoa elimu hii ya msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi katika mikoa mingi nchini na lengo letu ni kuwahamasisha wafanyabiashara wote wenye malimbikizo hayo kuomba msamaha ili waweze kupata unafuu na kulipa kodi ya msingi tu isiyo na riba wala adhabu," alisema Masalla.

Aidha, pamoja na washiriki hao kupewa elimu ya msamaha wa riba na adhabu ya kodi, pia wameelimishwa kuhusu Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Afisa Maadili Mwandamizi wa mamlaka hiyo Adelaida Rweikiza akizungumza na washiriki hao wakati akiwasilisha mada ya maadili amesema kuwa, ni haki ya wateja wote wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhudumiwa vizuri na kwa usawa bila upendeleo.
 Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akitoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika leo mkoani Manyara.
 Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika leo mkoani Manyara.
 Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Manyara Nicodemus Massawe akijibu baadhi ya maswali ya wafanyabishara wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika leo mkoani Manyara.

Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada mbalimbali wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika leo mkoani Manyara. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SALAMU ZA POLE

DKT. RWAKATARE ACHAGIZA UCHUMI WA VIWANDA

HESLB yajipanga kuchota mbinu kutoka kwa wadau Lilongwe

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru
Na Omega Ngole, Lilongwe,
TAASISI za kiserikali zinazotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu Afrika zinakutana kwa siku nne kuanzia kesho (Jumatatu, Septemba 24, 2018) mjini Lilongwe, Malawi katika mkutano ambao Bodi ya Mikopo ya Tanzania (HESLB) ikisema imejipanga kuchota mbinu za kuongeza ufanisi.

Mkutano huo wa kimataifa utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu wa Mutharika na umeandaliwa na Shirikisho la Taasisi hizo linalofahamika kwa kifupi kama AAHEFA. Washiriki zaidi ya 160 kutoka nchi 11 na wadau mbalimbali kama Benki ya Dunia, USAID wanatarajiwa kushiriki.

Washiriki hao ni maafisa wa Serikali, Watendaji Wakuu wa taaasisi hizo zinazotoa mikopo na wageni waalikwa kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda, Ghana, Uganda and Zambia. Wengine wanatoka Botswana, Lesotho, Namibia, Afrika Kusini na wenyeji Malawi.

Mkutano huo utafunguliwa kesho (Jumatatu, Sept 24, 2018) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Malawi Bw. Bright Msaka.

Akiongea mjini hapa kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru ingawa HESLB imepata mafanikio makubwa karika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, bado kuna nafasi kubwa ya kujifunza kutoka kwa nchi nyingine hususan za kiafrika ambazo zinakutana na changamoto kama za Tanzania.

“Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita tumekusanya zaidi ya TZS 298 bn kati ya TZS 398 bn zilizokusanywa tangu kuanzishwa kwa HESLB mwaka 2005 … na kwa miongozo tunayopata kutoka Serikalini, tumefanikiwa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kwa kiasi kikubwa… ni lengo letu kutenda bora zaidi,” amesema Bw. Badru katika mkutano na wanahabari mjini Lilongwe leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MTANGAZAJI WA CLOUDS SHAFII DAUDA AFIKISHWA KORTINI,APEWA DHAMANA

$
0
0


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MTANGAZAJI wa Clouds na mmiliki wa mtandao wa Shafii Dauda,  Shafii Dauda Kajuna na Benedict Kadege  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.

Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka akisaidiana na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono wamewasomea washtakiwa shtaka lao mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina


Akiwasomea hati ya mashtaka Wakili Kombakono amedai kuwa  kati ya Juni 14 hadi Septemba mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda, washtakiwa kinyume cha sheria walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Hata hivyo, baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa hao wamekana huku upande wa mashtaka ukidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo Wakili Jebra Kambole anayewatetea washtakiwa hao aliomba Wateja wake hao wapewe dhamana kwa sababu shtaka wanaloshtakiwa nalo linadhaminika.

Wakili Kweka amedai kuwa hawaping kutoa dhamana bali kama mahakama itaridhia kutoa dhamana izingatie kifungu cha 148 (6)(7) cha sheria ya makosa ya jinai.

Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Mhina alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kwenye kitambulisho vya kuwatambulisha na barua ambazo zinatambulika.

Pia kila mdhamini alitakiwa kusaini bondi ya Sh .milioni 15 na hawaruhusiwi kusafirisha nje ya Tanzania bila kupata kibali cha mahakama.

Pia wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafirisha mahakamani Oktoba 8 mwaka huu.

Washtakiwa wamefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi imeahirishwa hadi Oktoba 8 mwaka huu.
 Baadhi ya watuhumiwa wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakiwa wameficha sura zao wamefika mahakamani hapo kwaajili ya kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.
 Gari la Jeshi la Polisi likiwafikisha watuhumiwa wa makosa mbalimbali ikiwemo ya watumiaji wa maudhui ya matandao bila kibali. 
 Baadhi ya watuhumiwa wakiwa wameficha nyuso zao baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kwa  kujibu tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.

Chuo Kikuu Mzumbe Chatakiwa Kutumia Matokeo ya Tafiti Mbalimbali Katika Sekta ya Afya

$
0
0
Na Beatrice Lyimo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekitaka Chuo Kikuu Mzumbe kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali katika sekta ya afya kuleta matokeo chanya yanayokusudiwa na Serikali.

Dkt Ndugulile ameyasema hayo leo  Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Pili la Tathmini na Ufutiliaji lililloandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Calfonia  cha Marekani likilenga kujadili na kuweka mikakati ya namna bora ya kutumia matokeo ya tafiti za sekta ya afya kufanya tathmini na ufuatiliaji ili kuimarisha huduma zinazotolewa.

"Tuhakikishe rasilimali fedha inayowekezwa katika sekta ya afya inatumika vizuri ili kuleta matokeo chanya yanayotarajiwa na pia mfanye taafiti zitakazo saidia kuboresha na kusimamia sera na maamuzi ya Serikali" ameongeza Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt Ndugulile, amekiasa Chuo hicho kufanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wadau mbalimbali wanayojishughulisha na masuala ya afya kwa lengo la kuibua changamoto na  kufanya utafiti ili kutoa majibu ambayo Serikali na wadau wanayahitaji ili kutoa majawabu kwa kuchukua hatua stahiki.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kupeana uzoefu kuhusu umuhimu wa ufuatiliaji na tathimini katika sekta ya afya.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka  wakati wa Kongamano la pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali wakiwemo wanafunzi na Watafiti.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka  akizungumzia nafasi ya Chuo Kikuu Mzumbe katika kufanikisha programu mbalimbali za tafiti hasa katika sekta ya afya na kuzichakata taarifa zinazokusanywa ili zisaidie watunga sera katika kufanya maamuzi.
  Sehemu ya washiriki wa Kongamano  la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi  wa Chuo Kikuu Mzumbe  na Watafiti.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa Kongamano la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Watafiti.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RC SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AWAASA MADAKTARI KUTENDA HAKI

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka Madaktari wanaopatiwa mafunzo ya jinsi ya kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia au kuugua mahala pa kazi, kutenda kazi kwa weledi na kwa haraka ili kuharakisha utoaji wa fidia.

Mkuu wa Mkoa alitoa rai hiyo leo Septemba 24, 2018 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madakatari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Kigoma na Tabora kwenye chuo cha Uhasibu Singida.

“Katika kutoa fidia kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi hakuna njoo kesho….njoo kesho, bali ni kumhudumia Mfanyakazi huyo kwa haraka ili aweze kupata fidia yake kutokana na madhara aliyoyapata kwa wakati na ninyi madaktari ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha mnafanya kazi kwa weledi na kwa haraka.” Alisema.

Dkt. Nchimbi alisema, katika suala la utoaji fidia, Madaktari ni sawa na mahakimu, na wanayo dhamana kubwa sana kwani mapendekezo yao ndiyo yatatoa muongozo kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kuamua ni kiwango gani ambacho muathirika anapaswa kufidiwa au kutofidiwa kabisa.

“Kwa nafasi yenu Madaktari na kwa taaluma yenu mnafahamu sana namna ya kuwahudumia wahitaji wenu, lakini vile vile mnavyofanya katika tiba nyingine, huwezi kumtibu au kuwa na uhakika ni tiba ya namna gani mgonjwa anapaswa kupewa mpaka uwe na uelewa sahihi na ndio maana leo mko hapa ili muwe na uelewa sahihi, mtakapotoka hapa hatutarajii mseme sijui, sina uhakika, hayo siyo maneno ambayo tunataka yatoke kwenye vichwa vyenu baada ya mafunzo haya.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, (aliyesimama), akitoa hotuba wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya madaktari kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma kuhusu namna ya kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia au kuugua mahala pa kazi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF). Wengine pichani kutoka kulia ni Daktari bingwa na mbobezi wa magonjwa ya mifupi kutoak MOI, Dkt. Robert Mhina, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskazi Muragila, na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omary.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa neon la ukaribisho kwenye mafunzo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi, (kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati wa mapunziko ya mafunzo hayo. Kulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya mifupa, na kionbgozi w atimu ya wataalamu wa kutoa mafunzo hayo, Dkt. Robert Mhina.
Dkt. Pascal Magessa kutoka Idara ya Madai na Tathmini WCF, akizungumza na mmoja wa washiriki.
Mgeni rasmi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Singida.

SOUDY BROWN APATA DHAMANA MAHAKAMANI, ARUDISHWA KITUO CHA POLISI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MTANGAZAJI wa Clouds,  Soudy Peter  Kadio 'Brown' amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.

Akisomewa mashtaka na Wakili wa serikali Mkuu Faraja Nguka kwa kusaidiana na wakili Estazia Wilson amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile, kuwa kati ya June 11 na September, 2018 ndani ya Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shilawadu Tv mshtakiwa, alitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka (TCRA).

Hata hivyo, mshtakiwa Soudy Brown baada ya kusomewa shtaka hilo amekana na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Wakili Peter Kibatala anayemtetea mshtakiwa huyo aliomba mteja wake apewe dhamana kwa sababu shtaka linalomkabili linadhaminika.

Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu Rwizile amemtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh.Milioni 2, pia mshtakiwa mwenyewe naye asaini bondi ya Sh.Milioni 2.

Mshtakiwa huyo alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa. Kwa mujibu wa upande wa mashtka, wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi October 18, 2018.

RC MAKONDA ASAINI MKATABA WA LISHE ILI KUTOKOMEZA ASILIMIA 14.6 ZA UDUMAVU SUGU KWA WATOTO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesaini mkataba na wakuu wa Wilaya zote tano za jiji la Dar es salaam katika kuhakikisha suala la afya na ukuaji wa watoto.

Akizungumza katika hafla hiyo Makonda amesema kuwa mkataba huo uliosainiwa ufanyiwe kazi ili kupunguza asilimia 14.6 za watoto wenye udumavu sugu jijini humo.

Aidha amewataka makatibu tawala katika Wilaya zote kuhusisha suala la lishe katika vikao vyote vya Manispaa hasa kwa Wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala ambazo zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto ukilinganisha na Ubungo na Kigamboni.

Pia amewataka wananchi kuzingatia mlo kamili na usafi katika kuandaa mlo wa watoto kabla ya siku 1000 za mabadiliko kutoka kutokwa kutungwa kwa mimba hadi mtoto afikapo miaka miwili.

Kwa upande wake mratibu lishe kutoka TAMISEMI Mwita Waibe ameeleza kuwa hayo yote ni matekelezo ya makamu wa Rais na wakuu wa Mikoa kote nchini katika kuhakikisha suala la lishe linapewa kipaumbele ili watoto waweze kukua kiafya na akili.

Na amesema kuwa " Kuanzia mimba inapotungwa hadi mtoto kufikia miaka 2 takribani siku 1000 ni siku pekee za kumtengeneza mtoto hasa katika ubongo kwa kuzingatia lishe, na baada ya hapo  mtoto hataweza kuepuka udumavu alioupata" ameeleza. 

Aidha ameeleza kuwa Mikoa ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa chakula ndio inayoongoza kwa udumavu ikiongozwa na Rukwa yenye asilimia 50, Katavi, Ruvuma na Mbeya.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza leo na wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  wa wilaya tano za jijini Dar es salaam katika kuhakikisha suala la afya na ukuaji wa watoto(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda(kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iala Sophia Mjema(kushoto)  wakisani hati ya makubaliano ya lishe.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kulia) akimkabidhi hati ya mkataba wa lishe Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva  leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akimkabidhi  hati ya mkataba wa lishe Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema(kushoto)  leo jijini Dar es Salaam.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU ATANGAZA TUME YA KUCHUNGUZA AJALI YA MV.NYERERE ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU 224

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametangaza tume ya kuchunguza ajali ya kivuko cha MV Nyerere yenye wajumbe saba ambayo itaongozwa na Jenerali mstaafu, George Waitara.

Akitangaza majina hayo kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza leo (Jumatatu, Septemba 24, 2018), Waziri Mkuu amesema wajumbe hao wanapaswa kuikamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Amewataja wajumbe wengine kuwa ni Mbunge wa Ukerewe, Bw. Joseph Mkundi, Mhandisi Marcelina Magesa, Wakili Julius Kalolo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi. Queen Mlozi.

Wengine ni SACP Camillus Wambura na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu Hussein.Amemwagiza Mkuu wa Majeshi, Jenarali Venance Mabeyo asimamie uundaji wa tume hiyo na kuainisha ni mahitaji gani yanatakiwa kwa haraka na pia afuatilie utekelezaji wake. 

MV Nyerere ilipinduka na kuzama Septemba 20, mwaka huu ambapo hadi sasa jumla ya watu 41 wameokolewa na wengine 227 wamepoteza maisha baada ya miili mingine mitatu kupatikana leo asubuhi. Jana yalifanyika mazishi ya kitaifa ambapo miili tisa ilizikwa kwenye eneo la uwanja wa shule ya msingi Bwisya. Miili 214 ilitambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza itangazwe zabuni ya haraka ya kutengeneza kivuko kingine kipya chenye uwezo wa kubeba tani 50 za mizigo na abiria zaidi ya 200.

“Hili ni agizo la Mheshimiwa Rais, na mimi ninamuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe aitishe zabuni hiyo haraka sana. Kazi hiyo ifanywe mara moja ili kivuko kipya kiweze kutengenezwa na kusaidia wananchi wa eneo hili kwa haraka,” amesema.

Amesema kivuko kipya kikikamilika, itabidi kipangiwe ratiba za safari nyingi zaidi badala ya kwenda mara moja kwa siku ili kuondoka kero ilikuwa ikiwakabili wananchi hao.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATATU, SEPTEMBA 24, 2018.

MC LUVANDA APANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU TUHUMA TATU

$
0
0
Mtuhumiwa Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa amejifunika usoni leo jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko,blogu ya Jamii.
MSHEHERESHAJI maarufu nchini,Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda pamoja na kampuni yake,amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kutumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.

Luvanda anashtakiwa pia kwa kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mbali na luvanda washtakiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo Leo Septemba 24 kwa makosa kama hayo mbele ya mahakimu watatu tofauti ni pamoja na Fadhili Kondo, Michael Mligwa na kampuni ya Luvanda ya Home of Company Limited.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yanayowakabili mahakamani hapo kwa nyakati tofauti mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, 
Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na Hakimu Mkazi Mkuu, Hamza Wanjah 

Akimsomea mashtaka MC Luvanda, wakili wa Serikali Mkuu, Tumain Kweka amedai mbele ya Hakimu Shaidi kuwa mfanyabiashara MC Luvanda na kampuni anayomiliki ya Home of Company Limited walitumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.

Amedai kati ya Februari 24 na Septemba 2018 katika jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alianzisha na kutumia mtandao wa www.mcluvanda.com ambao haukuwa na kikoa cha .tz.

Pia imedaiwa katika kipindi hicho mshtakiwa alianzisha na kutumia mtandao huo ambao haukuwa na kikoa cha .tz.
Aidha imedaiwa,mshtakiwa huyo alitoa Huduma ya online bila ya kuwa na kibali.

Mc Luvanda anadaiwa kuwa katika kipindi hicho alitoa huduma hiyo kupitia online TV ifahamikayo kama MC Luvanda pasipokuwa na kibali toka TCRA.

Mshtakiwa Luvanda amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Wakili Jebra Kambole anayemtetea mshtakiwa huyo aliiomba mahakama itoe dhamana kwa mteja wake kwa sababu shtaka linadhaminika.

Akisoma masharti ya dhamana, hakimu Shaidi alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja Mwenye barua na kitambulisho ambaye atasaini bondi ya Sh 5 milioni.

Mshtakiwa huyo alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru. 
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 23, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Kwa upande wa mshtakiwa, Michael Mlingwa ambaye ni mpiga picha amepandishwa katika kizimba cha mahakama ya hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akikabiliwa na shtaka la kutumia mtandao bila kusajiliwa na TCRA.

Akimsomea mashtaka mshtakiwa huyo Wakili wa Serikali, Faraja Nguka alidai kuwa mshtakiwa huyo katika kipindi hicho cha Februari 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinyume cha sheria alimiliki na kutumia mtandao wa WWW.Slidevisual. Com bila leni kutoka TCRA. 

Mshtakiwa amekana mashtaka na yuko nje kwa dhamana yenye masharti ya kuwa na wadhamini wawili, waliosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba nane kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa mwingine John Lusingu amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hamza Wanjah kwa shtaka la kutumia mtandao waWWW.magazetini.com bila leseni. 

Mshtakiwa amekana mashtaka hayo anayodaiwa kuyatenda Februari 24 na Septemba mwaka huu, yuko nje kwa dhamana hadi Oktoba. 5,mwaka huu
Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images