Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

TBS YAKANUSHA UWEPO WA VIDONGE VYENYE DAWA KWENYE CHUPA ZA CHAI


Wateja wa Jumia kulipia bidhaa kwa Masterpass

0
0
Wateja wa Jumia kulipia bidhaa kwa Masterpass
Kurudishiwa 10% ya kiasi cha pesa watakacholipia bidhaa walizoziagiza.

Ni salama, rahisi na salama zaidi ambapo wateja hawatakiwi kulipia kwa pesa taslimu.

Dar es Salaam: Septemba 25, 2018. Katika jitihada za kurahisisha huduma za manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandao nchini, Jumia imewawezesha wateja wake kulipia bidhaa zozote watakazonunua kwenye mtandao wake kwa kutumia huduma ya Masterpass.

Maboresho haya ya kufanya malipo yamekuja ikiwa ni njia ya kuwarahisishia wateja kuwa na machaguo salama, rahisi na haraka zaidi kulipia bidhaa zao. Lengo la Jumia ni kuhakikisha Watanzania wanafanya huduma zao kwa kidigitali ili kurahisisha maisha yao ya kila siku. Na huduma ya Masterpass ambayo haimuhitaji mteja kubeba kiwango cha fedha ni suluhisho tosha kwa nyakati hizi za maendeleo ya sekta ya fedha kidigitali.

Akizungumzia juu ya huduma hii mpya ya njia ya malipo ambayo imetambulishwa na Jumia, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Albany James amebainisha kuwa, “huu ni mwendelezo wa Jumia katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanaweza kufanya manunuzi kwa usalama na urahisi mahali popote walipo. Kabla ya kuja na njia hii mpya ya malipo kwa kutumia huduma ya Masterpass, wateja wanalipia kwa Tigo Pesa au pesa taslimu. Tunaamini njia hii imekuja kufanya mapinduzi kwa wateja ambao wanakwenda na wakati kwa kuhifadhi fedha zao kidigitali.”

“Sio kila mtu anapenda kutembea na pesa taslimu siku za hivi karibuni. Ukiachana na sababu za kiusalama kwa wateja kutembea na kiwango kikubwa au kwa wafanyakazi wetu ambao hupokea malipo hayo kwa niaba ya kampuni, lakini njia hii mpya hurahisisha mchakato mzima. Hii ina maana kwamba badala ya mteja kutoa pesa, mteja atatumia simu yake ya mkononi kufanya malipo kwa ‘QR Code’ ya Jumia ndani ya muda mfupi tu!” alifafanua zaidi Bw. James.

Huduma hii mpya ya njia ya malipo imekuja wakati ambapo Jumia inaendesha kampeni ya ‘Electroshock.’ Kampeni hii ni ya kipekee ambayo inatoa fursa kwa wateja kununua bidhaa mbalimbali za vifaa vya umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ofisini, shuleni, na binafsi. Lakini pia wateja wanapatiwa vocha za punguzo la bei mpaka shilingi 50,000 pamoja na ofa ya kupelekewa bidhaa zao mpaka mahali walipo kwa zitakazozidi shilingi 200,000 na kuendelea kwa jijini Dar es Salaam pekee!



“Jumia imekuja kufanya mapinduzi katika namna ambayo Watanzania wanafanya manunuzi yao ya kila siku. Kwa miaka mingi wamekuwa wakipoteza muda na gharama kwenda na kurudi madukani kufuata bidhaa, muda ambao ungepaswa kuelekezwa katika shughuli zingine za maendeleo. Katika kulipatia ufumbuzi suala hili, sisi tumekuja na suluhisho kwa kuyakusanya maduka yote na kuyaweka sehemu moja mtandaoni. Hii inamrahisishia mteja kuweza kuperuzi bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara tofauti ndani ya wakati mmoja mahali na muda wowote alipo na kisha kufanya manunuzi na kupelekewa bidhaa zake mpaka pale alipo. Kwa mfano, wakati huu wa kampeni ya ‘Electroshock’ mteja anaweza kuperuzi bidhaa zaidi ya 1000 za vifaa vya umeme,” alihitimisha Meneja Masoko wa Jumia Tanzania.

Katika kunogesha kampeni ya ‘Electroshock‘ ambayo inatarajiwa kufika kikomo Oktoba 7, Jumia imewapatia Watanzania ambao ni wapenzi wa mchezo ‘Playstation’ kununua bidhaa mpya ya ‘FIFA19’ ambayo haijaingia sokoni bado ikitarajiwa kuzinduliwa mnamo Septemba 28 duniani kote. Kupitia mtandao wa Jumia wateja wanaweza kuweka oda ya bidhaa hiyo na kuwa wa kwanza kuimiliki mara tu ikiingia sokoni. Lakini kama hiyo haitoshi kuna simu za bure ambazo zitakuwa zinashindaniwa kwenye mtandao huu kwa kupitia programu yao ya simu ya ‘Jumia App.

WAZIRI WA NISHATI AELEZA NAMNA AMBAVYO SERIKALI IMEWEKA MIKAKATIMADHUBUTI SEKTA YA MAFUTA NA GESI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Nishati Dk. Medradrd Kaleman amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha Watanzania wanakuwa wanafuika namba moja katika miradi mikubwa inayoendelea nchini.

Pia amesema katika kuhakikisha sekta ya nishati na gesi inawanufaika Watanzania wa makundi yote Serikali imeweka sera na mikakati madhubuti itakayosimamia vema maslahi ya nchi.


Waziri Kalemani amesema leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzungumza kwenye Kongamano la Pili la mafuta na gesi ambapo wadau zaidi 300 kutoka mataifa 75 duniani wameshiriki na kutoa maoni yao.


Akifafanua zaidi kuhusu namna ambavyo Serikali imejiandaa katika kuhakikisha sekta ya mafuta na gesi Waziri Kaleman amesema kikubwa ambacho wanahamasisha ni wananchi kushiriki katika sekta hizo na hasa miradi mikubwa inayoendelea ili waweze kunufaika.


“Tumewaambia wawekazaji wote ambao wamefika hapa na wale ambao wanayo miradi mikubwa wanayoendelea kuitekeleza kuhakikisha wananchi wetu wanashirikishwa na kunuifaka.


“Kuna kazi ambazo hazina sababu ya kufanywa na watu wa nje.Tunafahamu Watanzania wamesoma kwa viwango tofauti lakini kila mmoja lazima ashiriki kwa nafasi yake na anufaike na uwepo wa miradi inayoendelea nchini,”amesema Waziri Kalemani.


Amefafanua katika kushiriki huko ni matarajia ya Serikali kuwa kampuni ambazo zinahusika na chakula basi vitauza chakula, kampuni za kisheria basi nazo zitatoa ushauri wa kisheria na kwamba kila kampuni, kikundi au mtu mmoja mmoja lazima ashiriki na tayari Serikali imeweka mazingira mazuri.


 Pia amezungumzia hisa ya asilimia 25 kwa ajili ya wazawa na kwamba muwekezaji yoyote ambaye anataka kuja kuwekeza nchini katika gesi na mafuta basi lazima asilimia 25 ya uwekezaji iwe ya watanzania.


 Amewahakikisha Watanzania kuwa Serikali imejipanga vema kuhakikisha rasilimali zilizopo nchini zinawanufaisha.


Wakati huo huo amesema mkutano huo umedhihirisha namna ambavyo sekta binafsi wanashirikiana na Serikali katika kutoa muelekeo kuhusu sekta hiyo.
Waziri wa Nishati Dk.Medrard  Kalemani akifafanua jambo baada ya kuzungumza leo jijini Dar es Salaam  kwenye Kongamano la Pili la mafuta na gesi ambapo wadau zaidi ya 300 wameshiriki.
Mwaandaji wa Kongamano la pili la gesi na mafuta ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la  Watumiaji Huduma za Mafuta na Gesi(ATOGS) Abdulsamad Abdulrahim akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar  es Salaam kuhusu ajenda zilizojadiliwa kwenye kongamano hilo

Wachimbaji madini watakiwa kuzingatia utekelezaji mpango wa usimamizi wa mazingira

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WANANCHI wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini katika hifadhi za misitu nchini wametakiwa kutii sheria za uhifadhi na kujiepusha na vitendo viovu vya uharibifu wa mazingira vinavyosababisha kupotea kwa uoto wa asili na kutishia nchi kuwa jangwa.

Hayo yamesemwa Septemba 23, 2016, Mkoani Geita na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Professa Dos Santos Silayo wakati akizungumza na viongozi wa migodi ya dhahabu iliyopo katika Shamba la miti Biharamulo mkoani humo.

Alieleza kuwa vitendo hivyo vya uharibifu wa mazingira ni pamoja na ukataji wa miti hovyo, kilimo, uchungaji holela wa mifugo, uanzishaji makazi na shughuli zingine za kibinadamu katika shamba hilo linalotarajiwa kuwa shamba la pili kwa ukubwa nchini likifuatia kwa shamba la miti la Sao Hill lililopo Mafinga mkoani Iringa.
"Uharibifu wa misitu mnaofanya mgodini hapa unatisha! Uchimbaji wenu unateketeza miti lakini mbaya zaidi mnatumia tekinolojia duni inayowalazimu kutumia miti mingi mnayovuna kinyume na taratibu kuzuia mmomonyoko wa udongo katika mashimo mnayochimba madini.
“Endapo mkiendelea na kasi hii mtaigeuza nchi kuwa jangwa, na hili hatuwezi kulifumbia macho! Tekelezeni mpango wa usimamizi wa mazingira, na hili linawezekana, jana nilipita katika msitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ‘Council’ ambapo uchimbaji madini unafanyika na wachimbaji wadogo. Kazi nzuri wanaifanya na mwekezaji anatekeleza vizuri mpango wa usimamizi wa mazingira. Miti bado imesimama na mashimo hufukiwa baada ya utafutaji kukamilika,” anasema Professa Silayo.

Katika utekelezaji na usimamizi wa sheria hizo za uhifadhi, aliwataka watumishi wa TFS kusimamia sheria hizo kila siku na kuendesha utekelezaji wake kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama za Wilaya na Mikoa ili kuimarisha utekelezaji wa sheria hizo na kuweka uwazi katika utendaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Injinia Mtemi Msafiri Simion
 alisema wilaya yake inakabiliwa na uhaba wa ardhi uliosababishwa na ongezeko kubwa la watu waliovutiwa na shughuli za kiuchumi hasa uchimbaji wa madini ambapo kwa namna moja ama nyingine imekuwa ni changamoto kubwa katika uhifadhi wilayani humo.

“Wachimbaji wadogo wa madini wanakata miti, wanakatwa hasa lazima sasa tuweke sheria kali kuhakikisha wamiliki wa migodi hawaruhusiwi kufanya shughuli zao pasipo kuwa na shamba ya miti na wakati wakingoja miti yao kufikia umri wa kuvunwa lazima waeleze walikovuna miti wanayotumia kufanikisha uchimbaji wao kuthibiti uharibifu wa misitu,” alisema

Shamba la miti Biharamulo ni miongoni mwa mashamba manne ya Serikali yaliyoanzishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika mwaka wa fedha 2017/18 likiwa na ukuwa wa hekta 69,758 ambapo jumla ya miche 495,506 ilipandwa kwenye hekta 446 mwaka 2017, ikiwa ni mwaka wa kwanza wa upandaji katika Shamba hilo.
Mtendaji Mkuu wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Professa Dos Santos Silayo akitazama moja kati ya mashimo yanayochimbwa madini ya dhahabu katika Shamba la Miti Biharamulo jana. Mashimo hayo yanatumia magogo mengi ya miti yanayovunwa kinyume na taratibu kuzuia udongo kumong’onyoka hali inayohatarisha uhifadhi nchini.

ACACIA YAONESHA MBINU BORA ZA UCHIMBAJI MADINI KWENYE MAONESHO YANAYOENDELEA GEITA

0
0
Kampuni ya Acacia Mining PLC kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imeshiriki maonyesho ya Teknolojia Bora ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Kalangalala Mkoani Geita.
Akizungumzia Ushiriki wa Migodi ya Acacia ya Bulyanhulu na Buzwagi Mhandisi wa Uchenjuaji wa Bulyanhulu Emmanuel Muchunguzi amesema katika Maonyesho hayo wamejipanga kuielimisha jamii kuhusu uchimbaji wa madini chini ya ardhi, hatua za Uchenjuaji wa Dhahabu, masuala ya Mazingira, Afya, na usalama mahala pa kazi.
 Muchunguzi amewakaribisha wadau mbalimbali waweze kutembelea banda la Maonyesho la Acacia ili wajifunze masuala mbalimbali hasa ya kuhusu uchimbaji na Uchenjuaji salama kwani usalama ndiyo nguzo muhimu ya Uzalishaji wa Dhahabu. Maonyesho hayo yameandaliwa na Mkoa wa Geita.
 
Wakazi wa Geita wakiwa katika banda la Kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia kwenye maonyesho ya Teknolojia Bora ya Uzalishaji Dhahabu kwa Maendeleo ya Kijamii na Uchumi wa Viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Kalangalala Mkoani Geita.Picha zote na Mary Lupamba - Acacia

RAIS SHEIN AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU TAKUKURU

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisis ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  Kamishna wa Polisi  Diwani Athumani (katikati) alipofika kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar akifuatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya kuzuia Rushwa na uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) Nd,  Mussa Hassan Ali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi  Diwani Athumani alipofika kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi  Diwani Athumani baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar alipofika kujitambulisha.(Picha na Ikulu).

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AWAASA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA NIDHAMU YA HALI YA JUU

0
0
LUSUNGU HELELA-DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ametoa rai hiyo leo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu na kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu

Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi ameelezea kufurahishwa kwake na ushirikiano alioupata kutoka kwa watumishi wa Wizara hiyo na kuelezea kuwa, ndio umemwezesha kuiongoza vema wizara hiyo kwa kipindi alichokuwepo madarakani na kupelekea mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Wanyamapori, Utalii, Misitu na Nyuki na Malikale.

Ameongeza kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii imepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya ujangili ambayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri uliopatikana kutoka kwa watumishi wa Wizara, wananchi, Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa Wanyamapori.

“Katika Kipindi tulichokuwa pamoja, kuna mambo mengi tumeyakamilisha. Nimefanya kazi nanyi na kila mmoja wenu alikuwa akinisaidia ili Wizara yetu iweze kusonga mbele. Hakuna hata mmoja aliyeonyesha kutaka kunikwamisha. Ninawashukuru sana”Amesema Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa UDOM jijini Dodoma na kuhudhuriwa na watumishi wapatao 113 wa Wizara hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aloyce Nzuki, amempongeza Meja Jenerali Mstaafu, Milanzi kwa kustaafu rasmi jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( kulia) akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati akiwaaga leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu ambapo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki.
 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili wakiwa wamesimama kwa muda wa dakika moja mara ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara kabla ya kuzungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kwa ajili ya kuwaaga leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu. .
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( kushoto) akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) mara baada kumaliza kuwaaga Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( wa pili kushoto) akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki (wa kwanza kushoto) akiwasili kwa ajili ya kuwaaga Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini Dodoma kufuatia kustaafu kwake rasmi Jeshini na kwa mujibu wa sheria kama Katibu Mkuu mnamo tarehe 16 Septemba mwaka huu ambapo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Wengine ni Wasaidizi wake. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TABORA WAWAOMBEA WANANCHI WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA MV NYERERE

0
0
NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wamekutana kwa ajili ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha yao  baada ya kuzama meli ya MV Nyerere tarehe 20 Mwezi huu katika Kisiwa cha Ukara mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa maombi hayo jana jioni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema Taifa limepoteza nguvu kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi na kuwaacha wananchi wakiwa katika simanzi kubwa.

Alisema miongoni mwa waliofariki kuna watoto huku watu wakipoteza wenza wao na hivyo kubaki wagane na wajane na kuzifanya baadhi ya familia kuanza maisha ambayo hawakuyatarajia.

Mwanri alisema ni kipindi kigumu lakini ni vema wakamshuku Mungu na waendelee kumutegea  yeye katika kipindi hiki kwaku ndiye msaada wao wa kwanza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Igunga,John Mwaipopo,aliwapongeza wananchi kwa kuendeleza mshikamano na umoja kwa vile baadhi ya watu walitoa maneno ambayo yangeweza kuyumbisha mshikamano na umoja uliopo.

Kwa pande wa  Askofu wa Anglikana Tabora,Elias Chakupewa alisema kuwa Biblia inasema siku za kuishi mwanadamu ni miaka sabini hadi themanini na zaidi ya hapo ni tabu na mateso makubwa na kusema kuwa baadhi ya waliofariki walipaswa kufikia miaka sabini lakini hawakufika umri huo na hivyo kuacha majonzi mengi.

Aliwataka wananchi ambao bado wako hai kutumia somo hilo la ajali hiyo kujiandaa kihoro kwani hajui watakufaje na lini.

Maombi ya Mkoa wa Tabora yaliwashirikisha viongozi wa Dini zote, wanafunzi, wananchi na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za wakazi wa Tabora wakati wa maombi ya kuombea marehemu wa ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.
 Shekh wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi akiongoza dua ya kuwaombea wananchi walipoteza maisha kwenye ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao..
 Askofu wa Anglikana Tabora,Elias Chakupewa akiongoza maombi ya kuwaombea marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao..

Viongozi mbalimbali mkoani Tabora wakiwa katika maombi maalumu ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha katika ajali ya MV Nyerere wakati wa maombi ya Mkoa ya kuwaombea marehemu hao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MSIMU WA PILI WA TUZO ZA SZIFF WAZINDULIWA, JOKATE AWA MLEZI WA TUZO HIZO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MSIMU wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu Nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zimezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es salaam na kumtangaza kwa  Mlezi wa tuzo hizo.

Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alitangazwa kuwa mlezi wa tuzo za SZIFF kwa msimu wa pili na kuahidi kuhamasisha vijana kujikita zaidi katika ubunifu wa sanaa ya uigizaji.

Akizindua maandalizi ya tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa anajivunia namna msimu wa kwanza wa tamasha la SZIFF lilivyoamsha ari na hamasa kwa waandaaji na wapenzi wa filamu nchini na fainali yake kufanyika 23 februari 2019.

Tido amesema, Hili ni tamasha la kwanza la Filamu Afrika kuonyeshwa kwenye televisheni , filamu zitashindanishwa kwenye vipengele tofauti huku ushindani ukiaminika kuwa mkubwa zaidi wa msimu uliopita kwakuwa moja ya vigezo vya filamu zitakazoshindanishwa ni kuwa lazima ziwe zimeandaliwa kati ya mwaka 2016 hadi 2018.

Amesema kuwa, mbali na hilo kwa mwaka huu wameongeza vipenele vingine vitano na kufikisha idadi ya  tuzo zinazowaniwa kuwa 24, pamoja na mshindi kuondoka na tuzo hiyo pia atakabidhiwa kiasi cha fedha taslimu kulngana na nafasi alizowania na kushinda.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe na Mlezi wa Tuzo za SZIFF Jokate Mwegelo amesema kuwa anafurahi sana kupewa nafasi ya kuwa mlezi wa tuzo hizo kwani hata yeye alikuwa  katika tasnia ya filamu akiwa amecheza filamu mbalimbali.

Amesema kuwa, tuzo hizi zimeleta chachu ya wasanii kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa na kuhamasisha zaidi vijana kufanya kazi za sanaa kwani  inawapatia kipato wasanii wengi sana ila wanahitaji mtu wa kuwasaidia kuinua na tuzo hizi za SZIFF zimekuwa na mchango mkubwa sana.

Mkurugenzi wa Tamasha la SZIFF, Jacob Joseph amesema kuwa kiswahili ni miongoni mwa ligha kumi kubwa kuzungumzwa Barani Afrikla, matamasha mengi hayajakidhi kuwafikia watu wengi na kuwatimizia mahitaji yao kupitia sanaa.
fisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu Nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF)  na kumtangaza  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo  kuwa mlezi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo  akizungumza na wasanii waliojitokeza katika uzinduzi wa  msimu wa pili pili wa Tuzo za Sinema Zetu Nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) na kwuashukuru waandaaji wa tamasha hilo lwa kumpa nafasi ya kwua mlezi wao.
 Mratibu wa tamasha la Sinema Zetu Nchini (SZIFF), Sophia Mgaza  
 akivitaja vigezo na tuzo zitakazowaniawa katika msimu wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu.
Picha ya Pamoja ya waandaji wa Tuzo za Sinema Zetu, wasanii na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.

WAFAMASIA NCHINI WAASWA KUTOA HUDUMA BORA YA BIDHAA ZA DAWA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Utaratibu wa kubadilishana dawa kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mtu anayejisikia kuumwa hawaufai kwa afya badala yake anayejisikia kuumwa kupima.

Hayo ameyasema Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) Issa Hango wakati wa maadhimisho ya siku Wafamasia Duniani ambayo hufanyika Septemba 25 ya Mwaka.

Amesema kuwa katika kuadhimisha siku hiyo ni wito kwa Wafamasia kufanya kwa weledi katika kuangalia afya za wananchi katika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa.

Hango amesema kuwa kuna kuwa dawa za maji zikishafunguliwa zinatakiwa kukaa kwa muda wa mwezi mmoja.

Aidha Hango amesema kuwa uweledi mwingine ni pamoja kutoa ushauri dawa zingine zisitumike katika matumizi ya dawa za kulevya.
Amesema  maadhimisho hayo ni pamoja na kufanya tathmini kwa Wafamasia kilichopatikana katika utoaji wa huduma katika jamii.
"Hatuwezi kuacha jamii yetu iangamie katika matumizi ya dawa wakati tunauwezo wa kutoa huduma hiyo kutokana taaluma tulionayo"amesema Hango.

Mwakilishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Grace Shimwela amesema kuwa TFDA itaendelea kufanya tathmini katika katika Udhibiti wa bidhaa ya dawa ikiwa ni kuwalinda watumiaji wa bidhaa hiyo.
Shimwela amesema kuwa wakifanya tathmini hiyo ni pamoja kuangalia    njia sahihi katika uteketezaji bidhaa za dawa ambazo zimebainika kuwa na madhara.

"Tutaendelea kudhibiti bidhaa za dawa kwa uweledi ili kufanya wananchi wapate huduma bora ya bidhaa za dawa"amesema Shimwela.
 Mwakilishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Grace Shimwela akizungumza katika Siku ya Wafamasia kuhusiana na Mamlaka hiyo kujipanga katika Udhibiti wa bidhaa za dawa.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) Geofrey Yambayamba akizungumza kuhusiana na mikakati ya Wafamasia katika kutoa huduma bora ya bidhaa za dawa
 Picha ya pamoja
Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) Issa Hango akizungumza katika mkutano wa Wafamasia katika Siku ya Wafamasia Duniani.

DAWA YA MATAPELI WANAOUZA NYUMBA NA MALI ZA RAIA KINYUME NA SHERIA YAPATIKANA

0
0
* MAKONDA AALIKA WANANCHI UZINDUZI WA FLYOVER 

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda leo amekutana na wawakilishi wa  benki, wenyeviti wa mitaa, madalali wa mahakama na kuweka mikakati madhubuti ya kudhibiti wizi na utapeli ambao umekuwa chanzo cha maumivu kwa wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho Makonda amewataka watu wa benki kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kujiridhisha kabla ya kutoa mkopo na hii ni baada ya kuibuka kwa utapeli wa watu kutumia hati za watu na kuchukuwa mkopo pasipo muhusika kujua jambo linalopelekea nyumba na Mali za watu kupigwa mnada na kuacha familia zikikosa makazi. 

Aidha  Makonda amewataka madalali wa mahakama na wale wa benki kuhakikisha wanatoa taarifa kwa mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa mtaa kabla ya kufanya mnada huku akiwaagiza kuhakikisha wamesajiliwa na kuwa ndani ya chama cha madalali ili kuondokana na uvunjifu wa amani wakati wa minada. 

Pamoja na hayo  Makonda amewataka wenyeviti wa mitaa kusimamia sheria na taratibu kwa kuhakikisha minada inafanyika pasipo uonevu wala uvunjifu wa amani. 

 Makonda pia amewaagiza watu wa benki kuhakikisha maafisa mikopo na wanasheria wao wanazingatia taratibu baada ya kubaini baadhi yao wamekuwa chanzo cha migogoro na utapeli.

Pia  Makonda amewapa mwezi mmoja watu wa benki, Wenyeviti wa mitaa, Madalali wa mahakama na benki kuandika changamoto na mapendekezo yao kisha kuyawasilisha kwake kwaajili kufanyiwa marekebisho  mwisho wa siku wawe na sheria nzuri inayomlinda mkopeshaji na mkopwaji.

Hata hivyo, Makonda amewataka wote wanaokopesha wananchi mitaani kienyeji pasipo kusajiliwa wala kuwa na vibali vya utambuzi kuacha Mara moja kwakuwa wamekuwa chanzo cha migogoro huku akiwataka madalali wa nyumba,viwanja na mashamba kuhakikisha wanasajiliwa na kutambulika na serikali.

Mwisho amewataka wananchi na viongozi mbalimbali bila kujali itikadi wala vyama wa Mkoa wa  kujitokeza kwa wingi siku ya Alhamisi katika makutano wa barabara ya Tazara kushuhudia uzinduzi wa Flyover itakayozinduliwa na Rais John Magufuli.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na  wanasheria,madalali wa Mahakama pamoja Benki  ambapo amewataka watu wa Benk kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kujiridhisha kabla ya kutoa mikopo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiangalia nyaraka mbalimbali.
Mkutano ukiendelea.

AZAM MEDIA WACHANGIA MILIONI 5 KWA AJILI YA KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO KISARAWE

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amepokea kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000) kutoka kwa uongozi wa Azam Media wakichangia katika kampeni ya Tokomeza Zero.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tdo Mhando amesema kuwa wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ya kuhamasisha wananchi kuchangia ili kutokomeza Zero kwenye Wilaya hiyo.
Tido amesema kuwa, wao kama uongozi wa Azam wanachangia kiasi ch Milioni tano (5,000,000) ili kusaidia kampeni hiyo na bado wataendelea kushirikiana katika nyanja zingine za kimaendeleo kwani huu ni mwanzo.

Baada ya kupokea hundi ya Kiasi hicho, Mkuu wa Wilaya Jokate amewashukuru uongozi wa Azam kwa kuweza kuona umhimu wa kuungana nae kwa kushirikiana  na kumpatia kiasi hicho kitakachowasaidia kuhakikisha wanafunzi wanapata mahitaji yote kwenye kipindi hiki kuelekea mtihani wa kidato cha nne.
Jokate amesema wanafunzi wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wananchi mbalimbali kwa kiasi chochote walichonacho ikiwemo mahitaji muhimu kama unga, sabuni, mafuta na kadhalika, kwani katika kipindi hiki wapo wamekaa mahali wanajisomea na vitu vinavyopatikana vinawasaidia wao.
Amesema kwua, wanafunzi hao kwa sasa wanahudumiwa na serikali ya Wilaya ya Kisarawe  chini ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Twala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye ni Mbunge  wa Kisarawe Seleimani Jaffo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano (5,000,000) kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa ajili ya kampeni ya Tokomeza Zero.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA WAFUNGUA KITABU CHA MAOMBOLEZO

Introducing Dogo Janja's "Imani" Official Music Video

Introducing "KIZAU ZAU" by Isack Abeneko Ft Khadija Kopa (Official Video)


DC PANGANI AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE MAUAJI YA DEREVA WA BODABODA WILAYANI PANGANI

0
0
MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Mhe. Zainabu Abdallah ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina ufanyike ili kuweza kubainika sababu za mauaji ya dereva wa bodaboda Mohamed Ally alimaarufu kama Sharo aliyekuwa anafanya kazi zake Pangani mjini.  
Inadaiwa mauaji ya bodaboda huyo yalitokea jioni ya Septemba 22 mwaka huu na mwili wake kupatikana Jumapili na kuzikwa juzi mara baada ya kukodiwa na watu wasiojulikana ambao walitaka awapeleka Tanga mjini na walipofika njiani wakatekeleza mauaji hayo kwa kumnyonga hadi umauti ulipomkuta na kuchukua pikipiki yake kutokomea kusikojulikana. 
Akizungumza mara baada ya kuitembelea familia ya marehemu na kutoa pole, Mkuu huyo wa wilaya alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa na mshtuko wizi huo na mauaji hayo ya bodaboda ambaye ni kijana mjasiriamali. 
 “Kijana huyu mkazi wa Pangani ameuwawa kikatili sana kwa kunyongwa na watu wasiokuwa na utu na kuchukua pikipiki aliokuwa akifanyia biashara ….inaumiza kijana asie na hatia anayejitafutia riziki kujikwamua kimaisha ndoto zake zinakwamishwa”,alisema. 
 Aidha alisema wanalaani vikali vitendo hivyo huku akiviagiza vyombo husika kufanya uchunguzi wa tukio hilo haraka ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kwa kupelekwa kwenye vyombo vya kisheria. 
DC ZAinab alisema wanatarajia kukutana na kuongea na chama cha waendesha BodaBoda wilaya ya humo kuhusu jambo hili na mustakabali wao hasa kwenye masuala ya ulinzi na usalama.
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia akimfariji mama wa dereva wa bodaboda aliyeuwawa Mohamed Ally alimaarufu Sharo anayefanya kazi zake Pangani mjini ambaye inadaiwa alikodisha na watu wasiojulikana na kufanya mauaji hayo
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto akimpa pole mama wa bodaboda aliyeuwawa Mohamed Ally alimaarufu Sharo anayefanya kazi zake Pangani mjini ambaye inadaiwa alikodisha na watu
wasiojulikana na kufanya mauaji hayo
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah katikati akiteta jambo na ndugu wa marehemu kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Nyange Hassani katikati ni Afisa Tawala wa wilaya hiyo Gipson

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 25.09.2018

ALICHOZUNGUMZA DKT. KALEMANI KATIKA MKUTANO WA WADAU WA MAFUTA NA GESI

TRC yawapatia kifuta machozi ndugu wa marehemu walioridhia kuhamisha makaburi kupisha mradi wa SGR

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK MAREKANI

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images