Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

TBL WATEMBELEA KAMBI YA WASANII WA FIESTA DAR

$
0
0
MAOFISA Waandamizi kutoka kampuni ya Tanzania Breweries Lmited (TBL Group),iliyopo chini ya kampuni ya kimataifa inayoongoza kutengeneza vivywaji ya ABInBev, wamefanya ziara ya kutembelea kambi ya wasanii watakaoshiriki katika tamasha la Fiesta 2018 iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo walipata fursa ya kuongea na wasanii hao na kuwapiga msasa kuhusiana na sera ya kampuni hiyo inayohimiza unywaji wa kistaarabu na kujadili masuala mengine ya kuendeleza sanaa sambamba na kutangaza biashara mbalimbali.

Meneja wa chapa ya bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli alisema “TBL Group Kama kampuni kubwa ya biashara za vinywaji tunalo jukumu la kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii ,kama ambavyo tumekutana na wasanii kwa kuwa tunaamini wao ni kioo cha jamii,hivyo tumeweza kubadilishana nao mawazo mbalimbali ya kukuza Sanaa sambamba na kuwapatia mawaidha ya kufanikisha kazi zao na utumiaji wa vinywaji kistaarabu.
Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo,akiongea wakati wa ziara hiyo.
Meneja wa Masoko ya Biashara wa TBL na ABInbev Afrika Mashariki, Edith Bebwa, akiongea wakati wa ziara hiyo.
Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, akifafanua jambo kwa wasanii
Wasanii wakimsikiliza Meneja wa Masoko ya Biashara, Edith Bebwa kuhusu shindano la kuonja bia.
Baadhi ya wasanii wakishiriki kuonja bia.
MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva Chege Chigunda, (kulia) akipongezwa na Meneja Masoko na Biashara wa TBL, Edith Bebwa, kwa kuibuka mshindi wa shindano la kuonja bia lililofanyika kwenye kambi ya wasanii watakoshiriki Fiesta.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 20.09.2018

KATIBU HAMASA UVCCM HASSAN BOMBOKO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

uchaguzi wa chama cha Baiskeli Tanzania CHABATA wasuasua

$
0
0
Afisa Habari wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Najaha Bakari akikumbushia uchukuaji wa fomu za uchaguzi wa chama cha Baiskeli Tanzania CHABATA unaotarajiwa kufanyika tarehe 6 Oktoba, 2018 jijini Dodoma,ambapo mpaka sasa hakuna mgombea ata mmoja amefika ofisini kuchukua fomu hizo na kurudisha.

Serikali Yafuta Baadhi ya Tozo za Kikanuni zilizokuwa Zikitozwa na OSHA Kuvutia Wawekezaji

TANZIA: GWIJI WA MUZIKI WA REGGAE NCHINI JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari usiku huu zinasema kwamba gwiji wa muziki wa reggae nchini Jah Kimbute (pichani) amefariki dunia nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam, mshirika wa karibu wa marehemu David Msitta Manju, amethibitisha.
Akiongea nasi kwa njia ya simu kutoka Mwanza aliko kikazi, Manju amesema amepata habari usiku huu kwamba Jah Kimbute amefariki dunia Alhamisi jioni nyumbani kwake.
Amesema kwamba amepata taarifa hizo toka kwa mkewe aliyeko jijini Tanga na kwamba mipango ya mazishi itajulikana leo asubuhi baada ya ndugu kukusanyika.
Mke wa marehemu pia alithibitisha habari hizo akiwa Tanga, na kusema kila kitu kitafahamika baada ya ndugu wa Jah Kimbute kukutana.
Amesema marehemu alikuwa akiishi na mwanae nyumbani kwake Msasani na kwamba jana jioni alipokwenda chumbani kwake alimkuta amefariki.
"Hizi habari tumezipata usiku huu na sasa ndugu wa marehemu ambao wengi wako Lushoto wanakusanyika tayari kwa safari ya Dar es salaam kesho kukamimlisha mipango yote.
Jah Kimbute, ambaye jina lake halisi alikuwa Samwel Mleteni, alitamba sana katika anga ya muziki na kuitwa Mfalme wa Reggae wa Tanzania miaka ya 80 akiwa na kundi lake la Roots and Culture lililokuwa na makaazi yake jijini Dar es salaam.

Mengi akubali kuilea Serengeti Boys

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
MLEZI wa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’, Dk. Reginald Mengi, amesema kuwa kikosi hicho kina kila sababu ya kufanya kweli katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kufanyika hapa nchini Aprili mwakani.
Mengi aliyasema hayo jana baada ya kutambulishwa rasmi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa mlezi wa timu hiyo, hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa TFF, Walace Karia, makamu wake, Athuman Nyamlani na Katibu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidau.
Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya IPP, alisema kuwa amefurahi mno kupewa nafasi hiyo ya kuwa mlezi wa Serengeti Boys, ukizingatia ni miongoni mwa wadau wa soka la vijana, akiwa ameifuatilia mno timu hiyo kwa muda mrefu.
“Hakuna sababu ya Serengeti Boys kutokuwa washindi, tunaamini tunaweza na timu hii itailetea Tanzania heshima kubwa. Shakira (mwanamuziki wa Colombia) aliimba ‘This time is for Africa’ wakati wa Kombe la Dunia 2010, na sisi tunasema ‘This time is for Tanzania (safari hii ni zamu ya Tanzania).
“Tuna kila kitu cha kutufanya tuwe washindi, wanachotakiwa vijana kufanya ni kujiamini. Tutafanya kila tunaloweza kuhakikisha timu inapata maandalizi ya kutosha ili iweze kufanya vizuri,” alisema.
Alimtaka kila Mtanzania kujivunia timu hiyo ya Serengeti Boys huku akiahidi kutowaangusha watanzania kutokana nafasi hiyo.
“Nawahakikishia Serengeti Boys itashinda mechi zote na kutwaa ubingwa,” alisisitiza Dk. Mengi.
Kwa upande wake, Karia alisema: “TFF tunafarijika kwa ndugu Mengi kukubali kuwa mlezi wa timu hii ya Serengeti Boys na tunaamini kwa pamoja tutaifanya timu hii kuwa msingi mzuri katika maendeleo ya ustawi wa soka la vijana.”
Alisema kuwa mkakati wao ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vema katika michuano hiyo ikiwa kama mwenyeji, lakini pia kukinukisha kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Peru Oktoba mwakani na hata zile za mwaka 2026 nchini Mexico na Peru.
“Tunawaomba wadau wa soka nchini na viongozi mbalimbali kumuunga mkono Dk. Mengi katika majukumu yake hayo kwani itakuwa ni fedheha kwa Taifa kama wenyeji wa michuano iwapo ubingwa utatoka nje ya Tanzania,” alisema.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd. Dk. Reginald Mengi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za IPP ya kutambulishwa rasmi na TFF kuwa mlezi wa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Wallace Karia. 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumtambulisha rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd. Dk. Reginald Mengi (kulia) kuwa mlezi wa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za IPP jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari za Michezo Clouds TV, Jacob Mbuya (wa pili kushoto) akiuliza swali kwa mlezi wa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) kuhusiana na malezi ya vijana hao ndani ya kambi na nje ya kambi wakati wa hafla fupi ya TFF kumtangaza rasmi kwa vyombo vya habari kuwa mlezi wa timu hiyo iliyofanyika katika ofisi za IPP jijini Dar es Salaam.


MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 21, 2018


IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya kamii

IMEELEZWA kuwa hadi sasa jumla ya miili ya maiti ya watu 44 imetolewa ndani ya maji ya Ziwa Victoria huku pia watu waliokuwa hai 37 wameokolewa baada ya kutokea ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani y
Ukerewe mkoani Mwanza.

Hata hivyo juhudi za kuendelea kuokoa watu waliokuwa ndani ya kivuko hicho ambacho kilizama ziwani jana mchana zinaendelea huku vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wadau wengine wa ukoaji wakiendelea kufanya jitihada za kutafuta miili na watu waliomo ndani ya kivuko hicho.

Akizungumza asubuhi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Jonathan Shana ameiambia Michuzi Blog kwamba wanaendelea nq juhudi za kuokoa watu waliokuwa wanasafiri na kivuko hicho na kazi inakwenda vizuri.

Alipoulizwa idadi ya watu ambao wamefainikiwa kuokolewa hadi sasa wakiwa hai amejibu idadi yao imefikia watu 37 na juhudi zinaendelea.

Kuhusu watu waliokufa kutokana na ajali hiyo ,Kamanda amejibu kuwa wamefanikiwa kupata miili ya watu 44.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu idadi ya watu waliokuwa wakisafiri na kivuko hicho ambacho kimepata ajali ,amejibu kwamba kwa sasa ni ngumu kupata idadi yao na kikubwa ambacho wanaendelea nacho ni kuendelea na ukoaji ambalo ndilo muhimu kwa sasa."Tunaendelea na ukoaji wa watu ambao wamezama ,hivyo suala la idadi ya watu tuliweke kando.Tunachoweza kueleza tunaendelea na ukoaji ikiwamo kuwaondoa watu waliokuwa ndani ya meli(kivuko).

Hata hivyo wakati Kamanda akielezea kinachoendelea ikiwemo juhudi za ukoaji,baadhi ya mashuhuda wamedai kivuko hicho kilikuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na mizigo.Imedaiwa kuwa idadi ya watu ndani ya kivuko ni zaidi ya 150 huku wengine wakidai walikuwa watu zaidi ya 200.Mbali ya idadi ya watu pia kulikuwa na mizigo mingi hali iliyosababisha kivuko kuzidiwa na kuelemea upande mmoja.

Kivuko cha Mv.Nyerere kabla ya kuzama ziwani inaelezwa kiliondoka Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye ghati ya Ukara.

Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea katika shughuli za uokoaji.Pia inaungana na Watanzania wote katika kutoa pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wananchi wa Mkoa Mwanza ,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na tukio hilo ambalo limesababisha kupoteza roho za Watanzania wenzetu.
Juhudi za uokoaji zilipokuwa zikifanyika hapo jana kufuatia Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kuzama.

RC SHIGELLA AWAONYA WANANCHI WA KIPUMBWI KUHUSU UINGIZWAJI WA DAWA ZA KULEVYA, BIASHARA ZAMAGENDO

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewaonya wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wanaojishughulisha na uingizwaji wa dawa za kulevya ,wahamiaji haramu na biashara za magendokuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawajakumbana na mkono wa sheria huku akiwataka wananchi kuwafichua watu hao.


Eneo la Kipumbwi limekuwa likitajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo kumekuwa bandari bubu ambayo imekuwa ikitumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kuingiza bidhaa za magendo, wahamiaji haramu jambo ambalo alisema linapaswa kukomeshwa.

Shigella aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara wilayani Pangani ambapo alisema Bandari hiyo bubu zimekuwa tatizo kwenye kutumika kwenye matumizi ambayo yasiyokuwa salama.

“Hapa Kipumbwi mmekuwa na tatizo kubwa la bandari bubu ambayo imekuwa kutumika kwenye matumizi yasiyosalama biashara haramu ya kupitisha wahamiaji, dawa za kulevya ama kusafirisha wahamiaji haramu lakini wapo  baadhi yenu wanadhamira njema ya kuleta bidhaa kutoka maeneo mengine  ikiwemo mkoani Tanga wakati mwengine kivuko kikiwa kimefungwa.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yake ambapo aliwataka kuacha kushiriki kwenye vitendo vya biashara haramu za magendo na uingizaji wa dawa za kulevya.
 Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwl Hassani Nyange akizungumza katika ziara hiyo.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani  (CCM) Jumaa Aweso.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikilizaa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.


TADB Board meets African Development Bank Delegation

$
0
0
The Tanzania Agricultural Development Bank’s Board of Directors has met with the delegation from African Development Bank (AFDB), which is in official engagements pertaining to AFDB’s projects supervision in the country.

During the visit the delegation met with TADB’s Board Chairperson, Madam Rosebud Kurwijila, board members and management team of the Bank, which was led by Acting Managing Director, Mr. Japhet Justine.

The delegation was led by AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda.
 TADB’s Board Chairperson, Madam Rosebud Kurwijila (centre) chairs a joint meeting between TADB and AFDB. The meeting held at TADB’s Board Room, Dar es Salaam.
 TADB’s Board Chairperson, Madam Rosebud Kurwijila insists on something while talking with members of the visiting delegation AFDB (not in picture), during a joint meeting between TADB and AFDB.
 AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda (second left) elaborates something during a joint meeting between TADB and AFDB. Others in picture are AFDB’s Senior Investment Officer, Trade Finance, Mkola Tambwe-Mlima (left), TADB’s, Acting Managing Director, Mr. Japhet Justine (right) and second right is Bank’s Head of Legal Service, Neema Christina John.
 TADB’s Acting Managing Director, Mr. Japhet Justine makes a point during a joint meeting between TADB and AFDB. The meeting held at TADB’s Board Room, Dar es Salaam.
 AFDB’s Senior Investment Officer, Trade Finance, Mkola Tambwe-Mlima (left) talks during the meeting with TADB’s Board of Directors. Looking on are AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda (centre) and TADB’s Head of Legal Service, Neema Christina John.
The delegation from African Development Bank (AFDB) having a group photo with TADB’s Board of Directors and Bank’s management.

TAMASHA LA TULIA TRADITION DANCES FESTIVAL 2018

$
0
0
MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, akimtunza pesa msanii wa muziki wa kizazi kipya Hip Hop akapela, Meshack Ngemela, aliyetoa burudani katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
 WASANII wa kikundi cha ngoma cha Songela, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe. 
 WASANII wa kikundi cha ngoma cha Lupaso, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
 MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Ditto, akiimba jukwaani na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.

(Picha na Muhidin Sufiani)

MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA WAZIRI MKUU MKOANI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa Kata ya Pahi Wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kondoa, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kondoa, kwenye ziara ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza mwanafunzi wa kidato cha sita Veronica Sharma wa Shule wa wasichana ya Kondoa Mkoani Dodoma, alipotembelea shule hiyo Septemba 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipanda mti kwenye Shule wa wasichana ya Kondoa Mkoani Dodoma, alipotembelea shule hiyo Septemba 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya wasichana ya Kondoa Mkoani Dodoma, alipotembelea shule hiyo Septemba 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mti aliyoupanda mwaka 2012 kwenye Shule ya wasichana ya Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAANDAMANO YA KUMBUKIZI YA KIFO CHA IMAM HUSSEIN YAFANA

$
0
0
 Sheikh Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim (wa pili kushoto) akiongoza maandamano ya kumbukizi ya kifo cha Imam Hussein Ally wa dhehebu la kiislamu la Shia, jiini Dar es Salaam juzi jioni. Kushoto kwake ni  balozi wa Iran nchini, Mosa Farhang na anayefuatia ni Katibu wa kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Padri John Solomon.
Waumini wa dini ya kiislamu wa dhehebu la Shia wakiwa katika maandamano ya kumbukizi ya kifo cha Imam Hussein Ally, jiini Dar es Salaam jana

VIKUNDI 19 WALIOPOKEA MSAADA KUTOKA UBALOZI WA MAREKANI WAASWA KUSIMAMIA KIDETE

$
0
0
VIKUNDI 19 vilivyopokea msaada kutoka Mfuko wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania vimeshauriwa  kusimamia kidete ili fedha zinazotolewa zifanye kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo.

Hayo yamesemwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Immi Patterson amesema kuwa fedha hizo zitumike katika kutokomeza unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Akizungumza jijini leo Dar es Salaam Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Immi Patterson wakati wa ugawaji wa vyeti vya kufanikisha kupata msaada uliotolewa na Mfuko wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

 Amesema kuwa wanufaika wa msaada walituma maombi ya kupata fedha hizo zinazotoka katika mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na UKIMWI(PEPFAR) ikiwa ni mwitikio wa maombi ya kuwasilisha maandiko ya miradi inayolenga kusaidia miradi ya vikundi hapa nchini.

"Kwa mara ya kwanza katika historia ya zama za sasa tumepata fursa ya kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi bila chanjo". Amesema Immi Patterson.

Amesema kuwa jitihada za sisi sote zitasaidia kufika pale tunapotaka katika jitihada za kutokomeza Ukimwi hapa nchini.
Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Immi Patterson akizungumza na wanavikundi wanaosaidia mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI jijini Dar es Salaam leo. 
   Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Immi Patterson akitoa vyeti vyeti kwa wanavikundi ambao mfuko wa balozi wa Marekani wa kusaidia mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI unaosaidia makundi ya kijamii na watu waishio na virusi vya ukimwi kushughulikia Changamoto zao vikundi vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Immi Patterson akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa vikundi 19 ambavyo vitasaidia kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke.

Pamoja na mambo mengine Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alimpa taarifa Makamu wa Rais juu ya ziara ya Mwanamfalme William wa Uingereza, atakayewasili nchini wiki ijayo kwa ziara yake ya siku tatu yenye lengo la kujifunza mambo ya uhifadhi wa wanyamapori kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dunia unaohusu masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori utakaofanyika London, Uingereza mwezi Oktoba. 
Aidha Balozi Cooke alimjulisha Mhe. Makamu wa Rais utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Aprili 2018, jijini London, Uingereza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akimsikiliza  Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke(kushoto) alipokuwa anafanya mazungumzo naye leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Media Group (MMG) inaungana na watanzania wote kutoa salamu za pole na rambirambi kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv.Nyerere

NEWZ ALERT:IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAONGEZEKA KUFIKIA 86, WATU WALIO HAI 40 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE ZIWA VICTORIA

$
0
0
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh John Mongella  hadi leo saa 4 asubuhi Septemba 21,2018,jumla ya maiti 86 zimeopolewa.

Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),Mongella amesema Miili ambayo imeshaopolewa leo asubuhi pekee ni 42 wakati mingine 44 ilipatikana jana,kwa hiyo Jumla ni 86 na Watu 40 waliokolewa wakiwa hai .

Amesema kuwa pamoja na kupatikana idadi hiyo ya watu bado wanaendelea na shughuli ya uokoaji 

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN


WAZIRI AZITAKA TAASISI ZA FEDHA, WAENDELEZAJI MILKI BINAFSI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA NYUMBA

$
0
0
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anastazia Mabula amezitaka taasisi za fedha pamoja na waendelezaji milki binafsi kushirikiana na Serikali ili kutatua changamoto iliyopo ya uhaba wa nyumba na makazi nchini.

Akihutubia katika ufunguzi wa maonyesho ya nyumba yaliyoandaliwa na benki ya NMB jana na kufanyika katika viwanja vya Kambarage jijini Dodoma, Mabula amesema serikali inauhaba wa nyumba za watumishi hususani baada ya serikali kuhamia jijini Dodoma.

Amesemakuwa Tanzania inaupungufu wa nyumba 3,000,000, hivyo ili kutatua changamoto hiyo, kunatakiwa kujenga nyumba zaidi ya laki mbili kila mwaka hivyo hawana budi kuwashirikisha wadau kikamilifu kama benki ya NMB ilikuziba pengo hilo.

Akizungumzia upande wa Dodoma, Mabula amesema mahitaji ni kuwa na nyumba zaidi ya elfu 23 lakini zilizopo ni nyumba 1329 tuhivyo maonyesho hayo yaliyowakutanisha wateja wa benki ya NMB, waendelezaji milki pamoja na wauzaji wa vifaa vya ujenzi yana tija kubwa kwani yanalenga kuiunga mkono serikali katika suala la maendeleo.

“Makazi bora ni haki ya kila mwananchi, na tukiri kuwa tuna changamoto ya uhaba wa nyumba nchini, lakini kupitia maonyesho haya tunaweza kukutana na wadau mbalimbali kama vile taasisi za fedha waendelezaji miliki na pia wauzaji wa vifaavya ujenzi ili kumaliza changamoto hiyo,” Alisema Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho ya Nyumba day yaliyofanyika jana viwanja vya tawi la NMB Kambarage Jijini Dodoma. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo. 

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA KITUO CHA KIBIASHARA NMB

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

SERIKALI mkoani Morogoro imewahimiza Wafanyabiashara wakubwa eneo hilo kukitumia Kituo cha Biashara kilichofunguliwa na Benki ya NMB ili kutambua fursa zilizopo katika kituo hicho pamoja na kuunganishwa na masoko ya ndani na nje hatua itakayo saidia kukuza uchumi wa mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe alisema hayo wakati akizindua kituo hicho cha kibiashara mkoani Morogoro kilichoanzishwa na Benki ya NMB kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara wa mkoa huo.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, alisema NMB imeamua kuanzisha kituo hicho cha kibiashara baada ya Mkoa wa Morogoro kuwa na fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo shughuli za kilimo, uchimbaji madini na masuala ya kiutalii.

Alisema kuwa NMB kupitia fursa hizo imeona iwasaidia Wafanyabiashara wa Morogoro kwa kuanzishia kituo maalumu ambacho licha ya kupata elimu na kuunganishwa na masoko ya ndani na nje pia watapatiwa huduma anuai za mikopo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema kituo cha Biashara cha Morogoro ni kituo cha kumi nchini na kimeanzishwa mahususi kwa ajili ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro waweze kukuza uchumi wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza 

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live


Latest Images