Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

MADEREVA BODA WANAOPORA SIMU KUKIONA -SSP MAGOMI

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
WILAYA ya kipolisi Chalinze, mkoani Pwani, haitakuwa na muhali na madereva pikipiki (boda boda) ambao wamekuwa na tabia za kupora simu za watu kisha kutokomea kusikojulikana .

Aidha madereva hao wameaswa kufuata sheria za usalama barabarani bila kuzikiuka ili kujiepusha na migongano inayojitokeza baina yao na askari wa usalama barabarani kutokana na kukaidi kuzifuata sheria hizo.

Mkuu wa polisi wilaya ya kipolisi Chalinze, SSP Janeth Magomi alitoa rai hiyo, wakati wa kikao cha polisi jamii kilichohusisha madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa, maafisa tarafa, viongozi wa dini, wananchi na madereva pikipiki.

Alifafanua , jeshi hilo limejipanga kuhakisha wenye tabia hizo wanadhibitiwa kwani wamejipanga kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi kuweza kuwakamata bodaboda wote wenye tabia hizo.

SSP Janeth , alitakiwa madereva bodaboda  pia kujisajili katika ofisi za serikali za mitaa ili waweze kutambuliwa kisheria kutokana na huduma ya usafiri wanayoitoa kwa jamii.

"Iwapo madereva pikipiki watafanya kazi zao kwa kufuata sheria na kutambulika kila mmoja kijiwe anachopaki pikipiki yake, ni rahisi kuweza kuzuia uhalifu"

Alisema sheria wanazijua na wengine wanapewa elimu hivyo wazitii ili kuondokana na kukamatwa kwa makosa mbalimbali na usumbufu.

"Nyie mtakuwa ni wenye kuzuia watu wasiofahamika kupaki kwenye vijiwe vyenu na wale wenye nia ovu ya kutenda matukio ya uhalifu kuweza kudhibitiwa"alisema SSP Janeth.

Hata hivyo, SSP Janeth alisema, kwa kufanya hivyo itasaidia pale tukio la uhalifu linapotokea mhusika aweze kubainika kwa wepesi na kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mwenyekiti wa kamati ya amani alhaji Nasoro Hamisi ,aliomba jeshi la polisi kudumisha amani na usalama wa wananchi wa Chalinze .

Alitoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa pamoja na jeshi la polisi kuwa na kumbukumbu za madereva bodaboda wanaokesha katika vijiwe mbalimbali ikiwepo kuweka picha zao katika ofisi hizo ili waweze kutambulika.

Kwa upande wake ,ofisa wa polisi jamii mkoa wa Pwani (ASP) Grase Salia aliwataka wenyeviti wayatumie madaftari ya wakazi kujaza taarifa za wageni wanaoingia kwenye maeneo yao.

Alibainisha,  jambo hilo litaweza kusaidia kuwa na taarifa za wakazi wa eneo husika na iwapo patatokea uhalifu inakuwa rahisi kufanya ufuatiliaji.
 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chalinze SSP Janeth Magomi (wa tatu kulia) akifuatilia changamoto za wananchi wakati wa kikao cha polisi jamii huko Chalinze(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chalinze SSP Janeth Magomi akikagua paredi huko Chalinze. (picha na Mwamvua Mwinyi

Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
Baruapepe: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Nukushi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Uteuzi wa Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa unaanza leo tarehe 20 Septemba, 2018.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

20 Septemba, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA BALOZI ALI IDI SIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI YA NSSF

WAZIRI MKUU AIONYA BOHARI YA MADAWA (MSD)

$
0
0
*Akerwa na tabia ya kupokea fedha na kutopeleka vifaa, dawa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hataki kuona tabia ya kupokea fedha na kuchelewa kupeleka vifaa inayofanywa na Bohari ya Madawa (MSD) ikiendelea.

“MSD ninawatahadharisha wasirudie kosa la kupokea fedha na kutopeleka dawa na vifaa tiba. Ofisi zao ziko hapo Dodoma mjini, ni kwa nini mnachelewa kuleta vifaa hivyo,” amehoji.

Ametoa onyo hilo leo mchana (Alhamisi, Septemba 20, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mauno, wilayani Kondoa ambako alienda kukagua ujenzi wa kituo cha afya na kuelezwa kuwa MSD imekuwa ikichelewa kuleta dawa. Waziri Mkuu leo ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma.

Amesema Serikali ilitoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na kwamba baada ya ukaguzi ameridhika na kazi inayofanyika. Hata hivyo, amemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na madiwani wahakikishe wanatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili za wagonjwa wa kawaida wa kike na wa kiume.

“Hapa mna kituo cha afya, hospitali ya wilaya iko Kondoa mjini ambako ni km.62 kutoka hapa. Tengeni fedha za kujenga hizo wodi ili watu walazwe hapahapa. Halmashauri mnao uwezo wa kujenga hizo wodi mbili. Nataka nione mnaanza na nipate taarifa kuwa mmeanza ujenzi huo,” amesisitiza.

“Mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani kaeni na mfanye hiyo kazi. Nikisema muanze maana yake ni kuanza. Tunataka wana-Mauno watibiwe hukuhuku na hakuna haja ya kuwasumbua wananchi kwenda hadi Kondoa mjini. Mkimaliza ujenzi, mtuambie, tutaleta sh. milioni 250 za kununua vifaa vya ndani.”

Amesema Serikali inaimarisha huduma za afya kwa kujenga zahanati na kuimarisha vituo vya afya ambapo hadi kufikia Agosti mwaka huu, jumla ya vituo vya afya 209 vilikuwa vimekwishajengwa hapa nchini.

Amesema kila mwezi, Serikali inapeleka wilayani humo sh. milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa dawa kuanzia hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati na akawaonya waganga na wauguzi wasiziguse dawa hizo kwa sababu zimelenga kuwasaidia wananchi.

Mapema, akizungumza na wananchi hao, Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kondoa, aliishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha huduma za afya wilayani humo ambapo katika kipindi cha miaka mitatu, wameweza kuwa na vituop vya afya vitano.

“Katika kipindi cha miaka 40, tulikuwa na vituo vya afya vitatu tu lakini ndani ya miaka mitatu, tumefikisha vituo vya afya vitano. Alivitaja vituo hivyo kuwa ni Mauno, Busi, Bereko, Kalamba na Thawi.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Kondoa ambako atazungumza na wananchi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

M- BET KUTIMIZA NDOTO ZA WATEJA WAKE

$
0
0

Na Agness Francis globu ya jamii
KAMPUNI ya mchezo wa kubahatisha M- Bet imeendelea kutoa zawadi kwa wateja wao ambao wamekuwa waotumia fursa ya kubeti mchezo wa kubahatisha.

Ambapo leo M Bet wametoa  hundi ya Sh. milioni 7.7 kwa mshindi ambaye ni wa 2  kwa mwezi huu wa droo  ya Perfect 12 .Mshindi huyo ametajwa kwa jina la  Given Mgale Mkazi wa Kagera.

Akizungumza leo Ofisa Habari wa M- Bet David Malley amesema baada ya ushindi huo na kukabidhi zawadi Serikali itachukua kiasi cha asilimia 14  ambayo ni kodi na mshindi wao atakabidhiwa  zaidi ya Sh.Milioni 56.

Hata hivyo Malley amewaomba watu watumie fursa ya kujaribu bahati zao  katika kushiriki droo hiyo kwa shilingi 1000 tu kwa kutumia njia ya Simu kwa kupiga *149*19#  na kwa wenye smartphone waingie tovuti ya www.m-bet.co.tz kisha kwenda sehemu yenye mchezo wa  perfect 12.

Kwa upande wake Mshindi huyo amesema haikuwa rahisi kwake kushinda kwani alijaribu kubeti mara nyingi zaidi na  hakukata tamaa kwa kuamini ipo siku ndoto zake zitatimia.

"Safari ya kushinda fedha hizo ilikuwa ndefu kidogo kwangu, lakini sikukata tamaa mpaka nilipotangazwa mshindi wa M-Bet droo ya perfect 12 September 17  na sasa ndoto zangu za kujenga nyumba na kufanya biashara  zimetimia.Nawashukuru vijana wenzangu watumie fursa wasikate tamaa,"amesema Given.
Afisa Habari wa kampuni ya M-Bet, David Malley(kushoto)akikabidhi hundi ya shilingi milioni 70.7  Mshindi wa M-Bet, Given  Mgale (katikati)   leo jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa  mshindi wa 2 kwa mwezi huu katika  droo ya 17 ya perfect 12.

Bikosports yampa bonasi ya sh milioni 5 mkazi wa Kigamboni

$
0
0
MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Salum Juma, ameibuka kidedea baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 5 kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya bikosports, baada ya mdau huyo wa michezo ya kubahatisha kutabiri michezo 11 ya mpira wa miguu duniani, jambo lililowavutia Bikosports na kuamua kumpa bonasi kama sehemu ya kuwajali wachezaji wa bahati nasibu yao.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Biko sports, Jeff Lea alisema kitendo cha shabiki huyo kubashiri michezo 11 kimewafanya waone haja ya kumpa bonasi, akiamini kuwa haitawavunja nguvu wasahiriki wao badala yake itawapa mwamko katika kushiriki mbio za kuwania Sh Milioni 97 kwa mtu atakayeibuka shujaa wa kubashiri michezo 13 kama droo yao kubwa inavyotaka.

Leya alisema licha ya wadau mbalimbali kuendelea kuvuna fedha mbalimbali kwa kubashiri na Kampuni yao ambayo namba ya kampuni ni 101010, ambapo mchezo huo unaweza kuchezwa kwa kutuma jamvi kwa *149*89# bila kusahau kwa kuingia kwenye mtandao wao moja kwa moja kujionea mpangilio mzima wa mchezo wao unaoweza kuchezwa bila kuwa na akaunti huku ushindi ukipatikana moja kwa moja kwenye simu ya mkononi.

“Biko Sports tunawajali sana wateja wetu ndio maana leo tumeamua kwa dhati kabisa kumpa bonasi ya Sh Milioni tano ndugu yetu Juma kwa sababu amejitahidi kwa kubashiri michezo 11, akishindwa miwili tu ili avune Sh Milioni 97 kutoka kwetu, ambapo bikosports ina machaguo Zaidi ya 125.

“Biko Sports ni rahisi kubashiri na kushinda bila kusahau jinsi tunavyojali wateja, hivyo kwa pamoja tunaamini watanzania wataendelea kubashiri kwakupitia kampuni yetu kwa sababu tumeboresha mno huduma zetu na fedha zetu zinalipwa muda mfupi tu baada ya kufanikiwa kushinda kwenye jamvi husika,” Alisema.

Msemaji wa BIKOSPORTS Tanzania, Jeff Lea kulia, akikabidhi hundi ya sh Milioni 5 kwa mshiriki wa bahati nasibu ya kubashiri matokeo ya michezo ya mpira wa miguu, Salum Juma wa pili kutoa kulia, aliyepewa bonasi ya kiasi hicho baada ya kubashiri mechi 11 badala ya 13 ambayo ndio droo kubwa ya sh milioni 97 hali iliyowavutia biko sports kumpa bonasi hiyo kama sehemu ya kuwajali wateja wao. Wengine ni Maulid Kitenge Balozi wa Bikosports pamoja na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Saleh wakati kushoto kwake ni Meneja Uendeshaji wa Bikosports Tanzania Lucas Kiangi. 

WAZIRI LUGOLA AWASILI TABORA AKIELEKEA MKOANI KIGOMA KIKAZI

$
0
0




Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akipokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Emmanuel Nleyi (kushoto) alipowasili mkoani humo, leo. Waziri Lugola yupo safarini akielekea mkoani Kigoma kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Emmanuel Nleyi (kulia), pamoja Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, SP Nestory Didi. Waziri Lugola yupo safarini akielekea mkoani Kigoma kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA MIRADI 37 YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI 15.7 MANYARA

$
0
0
MWENGE wa uhuru umepokelewa Mkoani Manyara ambapo utatembelea miradi 37 yenye thamani ya sh15.7 bilioni kwenye Halmashauri saba za mkoa huo. 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, akizungumza jana wakati wa kupokea mwenge huo kutoka Mkoani Arusha alisema utatembea miradi mbalimbali ya maendeleo, kwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi. 

Mnyeti alisema gharama ya miradi ya halmashauri ya wilaya ya Babati ni sh3.490 bilioni, Babati mji sh1. bilioni, Mbulu Mji sh1.1 bilioni, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu sh3.4 bilioni, Hanang sh1.5 bilioni, Kiteto sh6.9 bilioni na Simanjiro sh1.1 bilioni.

"Tunawakaribisha kwenye mkoa wa Manyara ambapo wananchi wana hamu kubwa ya kuona mwenge wa uhuru na kusikiliza ujumbe wa elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu," alisema Mnyeti. 

Mkuu wa Wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu alisema kwenye halmashauri ya Wilaya hiyo mwenge wa uhuru utatembea miradi mitano ya thamani ya shilingi bilioni 3.4. 

Kitundu alisema mwenge wa uhuru utaweka jiwe la msingi kituo cha afya Nkaiti, bweni la wavulana shule ya msingi Mbugwe na kupanda miti ya kumbukumbu.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kaimu mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta, ukiwa mkoani Manyara mwenge wa uhuru utatembelea miradi 37 yenye thamani ya shilingi bilioni 15.7.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akisoma taarifa ya mkoa huo baada ya kupokea mwenge wa uhuru kutoka Mkoani Arusha, ambapo utatembelea miradi 37 yenye thamani ya shilingi bilioni 15.7 kulia kwake ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Charles Kabeho.  
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2018 Charles Kabeho akisoma jiwe la msingi la bweni la shule ya sekondari Mbugwe, Wilayani Babati, baada ya kuizindua, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo Elizabeth Kitundu. 
  Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Elizabeth Kitundu akipanda kwenye ukiwa katika halmashauri ya Wilaya ya hiyo mwenge wa uhuru umetembelea miradi mitano ya thamani ya shilingi bilioni 3.490.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu mwenge wa uhuru baada ya kupokea kutoka Mkoani Arusha eneo la Minjingu madiwani. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEWZ ALERT;TAARIFA YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV NYERERE.

MAHAKAMA YAWAACHIA KWA DHAMANA ASKARI MGAMBO WALIOMPIGA RAIA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
BAADA ya kusota rumande kwa takribani wiki mbili, leo Septemba 20.2018 askari mgambo wawili kati ya watatu wanaotuhumiwa kumpiga raia Robinson Olotu wameachiwa kwa dhamana baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa masharti ya dhamana.

Washtakiwa wawili  Goodluck Tarimo (30) na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo ya Bunju Ibrahim Mabewa (39) ndio wametimiza masharti ya dhamana huku mshtakiwa Kelvin Sawala akishindwa kutimiza masharti na kurudishwa rumande.

Hatua hiyo imekuja kufuatia wakili wa Utetezi Nassoro Mbilikira kuiomba mahakama iwapatie dhamana washtakiwa hao kwa sababu shtaka linalowakabili linadhaminika kisheria. 

Akisoma masharti ya dhamana,  Hakimu mkazi Mwandamizi Salum Ally amesema kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja anayetambulika kisheria atakayesaini bondi ya Sh. 500,000.

Mapema wakili wa serikali Nasoro katuga alidai mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa upelelezi bado haujakamilika. . 

Watuhumiwa  hao ni miongoni mwa watu waliokuwa wakisimamia operesheni ya usafi iliyoasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 30 mwaka huu maeneo ya Bunju Kinondoni jijini Dar es Salaam walimjeruhi kwa rungu Oloth.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 4 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

MRADI WA DALBERG 3D WA MAPINDUZI YA KILIMO WAIVUTIA SERIKALI

$
0
0
SERIKALI imeridhishwa na mradi wa mapinduzi katika sekta za kilimo na mifugo baada ya mradi huo unaotekelezwa katika halmashauri nne za Mkoa wa Mwanza kuonyesha mafanikio na tija kwa wakulima na wafugaji.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari wilayani Misungwi hivi karibuni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais(TAMISEMI) John Cheyo alisema baada ya kukutana na wakulima walikiri kuwa mradi huo una tija.

“Tulipokutana na wakulima maeneo mbalimbali ya mradi walikiri una tija na hivyo tukiuhamisha na kuupeleka katika mikoa mingine kunaweza kuwa mabadiliko makubwa zaidi kwenye kilimo. Ili kuongeza uzalishaji wakulima wanatakiwa kusaidiwa utaalamu na ushauri wa kupanda mbegu kwa nafasi na matumizi bora ya pembejeo,” alisema Cheyo.

Alifafanua kuwa mradi huo unafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Mwanza kwenye maeneo manne kujaribu zao la alizeti huko Buchosa na Sengerema ambako lilikuwa halijaanza ili wawasaidie wakulima walime kibiashara na kuongeza kipato, pia  Dalberg inajaribu kuongeza nguvu kwenye zao la pamba liwe na tija zaidi.

Mradi huo pia unawajengea uwezo maofisa ugani na mifugo kwa kuwapa kompyuta, vifaa vya kazi na  usafiri ili kufuatilia na kukusanya taarifa, kutunza takwimu na kumbukumbu kwa kutumia kompyuta.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi Dalberg Tanzania Steve Kisakye alisema kuwa mwaka 2016 serikali kupitia sekta ya kilimo na mifugo ilianza kufanya kazi na Dalberg 3D ikijikita kwa kutoa mafunzo na ufadhili wenye tija kwenye kilimo na ufugaji katika kuongeza uwezo kwenye sekta hiyo.
 Baadhi ya wakulima wilayani Sengerema wakiwa katika moja ya shamba darasa la zao la pamba walilolianzisha baada ya kupata elimu kwa ufadhili wa mradi wa Dalberg 3D.
 Afisa Mfugo Wilaya ya Misungwi  Dk. Chrispine Shami (mbele), Mratibu wa Dalberg wilayani humo Ines Muganyizi wakimuongoza  Mkurugenzi wa Uratibu (TAMISEMI)Dk. Andrew Komba (wa tatu nyuma)kukagua mashamba ya mfano ya  utekelezaji wa mradi wa Dalberg  3D wilayani humo.
 Mfugaji  wilayani Misungwi ambaye jina lake halikupatikana mara akiswaga ng’ombe wake kuingia ndani ya josho kwa ajili ya kuwaogesha dawa ya kuua wadudu. Josho hilo ni moja kati ya majosho yaliyofufuliwa kwa ufadhili wa mradi wa Dalberg 3D unaotekelezwa katika halmashauri nane za Mkoa wa Mwanza ambapo wameanza kuzingatia elimu ya ufugaji wanayopewa na wataalamu wa mifugo kupitia mradi huo. 
 Mkurugenzi wa mradi wa Dalberg Tanzania Steve Kisakye (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais(TAMISEMI) John Cheyo (katikati)kabla ya kukabidhi pikipiki za usafiri kwa maofisa ugani na mifugo katika Wilaya ya Sengerema.Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Alfred Kipole.
 Mkurugenzi wa Dalberg Steve Kisakye (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais (TAMISEMI) John Cheyo pikipiki kwa ajili ya usafiri wa maofisa Kilimo (ugani) na Mifugo katika Wilaya ya Sengerema  ili ziwarahisishie usafiri wa kwenda vijijini kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji pamoja na kukusanya taarifa.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

Mawaziri watatu wakutana na jumuiya ya wafanyabiashara kujadili changamoto za biashara

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JUMUIYA ya Waanyabiashara Kariakoo imekutana na mawaziri wa watatu kutoa changmoto zao biashara wanazokutana nazo na kufanya biashara zao kuwa ngumu.

Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa kukutana wa wafanyabiashara hao ni kutaka kujua changamto na kufanyia kazi ili serikali iendelee kupaata mapato.

Amesema kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa wafanyabiashara hivyo ni lazima kwa vongozi wenye dhamana kufanya kazi ya kukutana na wafanyabiashara kujua changamoto za biashara zinazotokana na mifumo ya kiutendaji serikalini.

Nae Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa wafanyabiashara wanahitajika sana katika maendeleo ya nchi kwani miradi inayotekezwa yanatokana na mapato ya ndani.

Amesema kuwa kuombaomba kunadharisha hivyo wafanyabiashara ndio nguzo ya maendeleo ikiwa ni kusoma bure kunatokana na hizo kodi ambazo ni za watanzania.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charle’s Mwijage amesema kuwa vitu vyote vilivyozuiliwa kwa ajili ya ukaguzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kufanya ukaguzi bidhaa za wafabiashara kuanzi leo hadi kesho na kuma havikidhi mahitaji ya mlaji vitekezwe.

Hata hivyo Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema kuwa kuna mchezo wa kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kuchezea mashine za Kielektroniki ambapo wanashughulikia wote wanaofanya hivyo.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo katika biashara kupitia mamlaka za kiserikali..
 Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Charles Kichere akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara kuhusiana na ukusanyaji wa mapato na hatua ambazo wanazichukua kwa wafanyabiashara wasiofuata utaratibu.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akizungumza na Jumuiya ya wafanyabiashara kwa kuwataka kufuata taratibu katika mamlaka zilizowekwa katika usimamiaji wa biashara hizo.
Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na jumuiya ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam leo.

TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki

$
0
0
Wiki hii TatuMzuka imezindua jackpot ya Jumatano ikiwa ni jackpot ya pili ndani ya wiki moja. Watanzania sasa watapata fursa ya kuwa washindi wa jackpots mara mbili na hivyo kutengeneza washindi wengi zaidi kupitia jackpots.Jackpot ya jumatano ambayo itahusisha wachezaji wote waliocheza tangu jumapili itakuwa inaonyeshwa saa 3 usiku kupitia Clouds TV na EATV.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Bwana Sebastian Maganga alisema kampuni ya The Network ambao ni wamiliki wa mchezo wa namba wa TatuMzuka imekuwa ikiangalia namna ya kuongeza nafasi za Watanzania kushinda kwa wingi na kwa kiasi ambacho kinabadilisha maisha yao.

“Tangu tulipoanza mwaka mmoja uliopita tumetoa jackpot ya kihistoria ya milioni 300, na sasa kwa kuongeza jackpot ya jumatano watanzania hawatahitaji kusubiri wiki nzima kushinda, itakuwa sasa jumatano na jumapili” Alisisitiza Maganga

Baada ya uzinduzi huu, Tatumzuka sasa itaondoa jackpot ya kila siku ya Mzuka Deile na kuibadilisha na droo za vipindi maalumu ndani ya siku moja. Droo hizi zitatengeneza mamilionea wengi kwa haraka na kuufanya TatuMzuka kuwa mchezo unaotengeneza mamilionea wengi zaidi kuliko mchezo mwingine katika soko.

Akiongea wakati wa uzinduzi, balozi wa TatuMzuka Mussa Hussein (pichani) alisema hii ni fursa kubwa kwa watanzania kubadili maisha yao kupitia jackpots mbili kubwa kila wiki.

“Kwa tiketi moja ya shilingi 500 sasa Watanzania watakuwa wanasubiri kwa siku 3 tu kushinda kupitia jackpot za jumatano na jumapili. Hii itakata kiu ya wachezaji wetu wapendwa ya kusubiri muda mrefu kushinda kiasi kikubwa” Aliongeza Hussein

Ili kuongeza nafasi ya watanzania wengi kutazama shoo za jackpots Bwana Maganga alisisitiza kwamba The Network imeiongeza TBC1 kati ya vituo vitakavyokuwa vinaonyesha mubashara shoo ya jackpot ya jumapili.

WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea msaada wa dawa na vifaa tiba wenye thamani ya Sh.Bilioni mbili kutoka Serikali ya India.

Msaada huo wa dawa na vifaa tiba wa Serikali ya India umekabidhiwa kwa Waziri Mwalimu na Balozi wa India nchini Tanzania na kwamba dawa na vifaa tiba hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imedhamiria kuboresha sekta ya afya.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo Waziri Mwalimu ameishukuru Serikali ya India kwa kutoa msaada huo ambao umetokana na ombi la Rais Dk.John Magufuli kwa Waziri Mkuu wa India ambaye alikuja nchini.

"Wakati Waziri Mkuu wa India alipokuja nchini,Rais Dk.John Magufuli alitoa ombi la kuomba dawa muhimu na vifaa tiba.Hivyo tunatoa shukrani kwa Serikali ya India kwa msaada huu.Tunatoa shukrani kwa Waziri Mkuu wa India," amesema Waziri Mwalimu.

Akizungumzia zaidi msaada huo,Waziri Mwalim amesema miongoni mwa dawa ambazo zimetolewa na Serikali ya India  ni dawa aina ya Amoxline kwa ajili ya watoto na zipo dozi 19800.
Pia kuna dawa ya kuzuia wajawazito kuvuja damu baada ya kujifungua na kwamba kuna dawa za chanjo ya homa ya ini.
Waziri Mwalim amesema kuwa dawa na vifaa tiba vitapelekwa kwenye Hospitali za umma na kwamba pamoja na msaada huo Serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ikiwemo ya kuongeza dawa na vifaa tiba.

"Dawa ambazo zimetolewa zitatolewa bure.Hii imedhihirisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania na India.Kwa kukumbusha tu baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani tumekuwa tukinunua dawa kutoka viwandani badala ya watu binafsi.

" Tunaomba Balozi wa India uendelee kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba waliopo India kuja kuwekeza nchini kwa kujenga viwanda vya dawa,"amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Wakati huo huo Waziri Mwalimu amezungumzia namna ambavyo Serikali imefanikiwa kuongeza dawa muhimu nchini ambazo kwa sasa zipo za kutosha.

Amefafanua  kuwa taarifa ya Bohari ya Dawa nchini(MSD) ni kwamba kuna ongezeko kubwa la  dawa muhimu hadi  kufikia asilimia 85 kutoka asilimia 36 huko nyuma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YAO KWA WANANCHI MBALIMBALI NA WASHIRIKI WA SEMINA JIJINI MOROGORO

$
0
0
Afisa Masoko na uhusiano wa UTT AMIS Ndg.Waziri Ramadhani akitoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyo andaliwa na TAGLA katika ukumbi wa JKT Umwema-Morogoro
Afisa Masoko na uhusiano wa UTT AMIS Ndg.Waziri Ramadhani akitoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyo andaliwa na TAGLA katika ukumbi wa JKT Umwema-Morogoro
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba apeleke wataalamu kwenye kituo cha utafiti kilichopo Makutupora, Dodoma ili wazalishe mbegu bora za ufuta kwa ajili ya mikoa ya kanda ya kati.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Septemba 20, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mauno, wilayani Kondoa ambako alienda kukagua ujenzi wa kituo cha afya. Waziri Mkuu leo ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma.

Alikuwa akijibu ombi la mbunge wa viti maalum, Bi. Mariam Ditopile ambaye alisema mkoa wa Dodoma ni wa pili kwa uzalishaji wa ufuta hapa nchini lakini aina ya ufuta inayozalishwa ni ya daraja la chini kwa sababu hawana mbegu za ufuta mweupe.

“Ili mradi mikoa ya kanda ya kati inazalisha ufuta, ninamuagiza Waziri wa Kilimo ahamishe watumishi kutoka kokote ili wakae Makutupora na kuwasaidia wakulima wawe na mbegu bora zenye kutoa mafuta mengi,” alisema.

Amesema kila mwaka Serikali inatumia zaidi ya dola za Marekani milioni 267 kuagiza mafuta ya kula kutoa nje ya nchi na kwamba hivi sasa imeamua kufufua mazao ya mbegu za mafuta ili mafuta ya kula yazalishwe kwa wingi hapa nchini.

 “Sasa hivi tumeanza kufufua mazao ya mbegu za mafuta ni nilianza mkoa wa Kigoma kwa kuhimiza kilimo cha michikichi. Sasa hivi niko Dodoma nahimiza ufuta na alizeti na nitaenda Singida kwa ajili ya zao hilo la alizeti,” amesema.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.  
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mauno Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

 Wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chumba cha kuhifadhia maiti, wakati alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Mauno Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk. Ikaji Rashid.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TIDO MHANDO AELEZEA MCHAKATO WA KUITOA TBC KWENYE ANALOGI,AMTAJA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
ALIYEKUWA  Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amedai mchakato wa kuitoa TBC kwenye analogy kuingia kwenye digital ulifanywa na Bodi ya shirika hilo na kupata baraka za Bodi ya zabuni. 

Amedai mchakato huo ulitokana na maelekezo ya Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete ya kumtaka alibadilishe shirika  hilo lifikie katika hadhi inayostahili.

Mshtakiwa Tido, amedai hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alipokuwa akijitetea dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi mabaya ya madaraka.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.Milioni 887.1.

Amedai kuwa Serikali imewalipa Sh. Milioni hiyo 887.1 watu wasiojulikana badala ya mawakili kama inavyodaiwa  na upande wa Jamhuri

Akiongozwa na Wakili wake wa utetezi, Dk.Ramadhani Maleta Tido amedai, mwaka 2006 Rais Kikwete alimuita kuja kuiongoza TBC ambapo majukumu yake yalikuwa ni kulibadilisha shirika hilo liwe lenye uwezo na kuheshimika duniani. 

Amedai, tuhuma anazotuhumiwa nazo zimemuumiza sana kwa sababu alikuwa na ndoto ya kuifikisha TBC mbali ,ifikie kutoa gawio kwa Serikali na siyo serikali kutoa fedha kwa TBC.

Kuhusu kuisabishia Serikali hasara ya Sh.Milioni  887.1, Tido amedai kuwa, hakushirikishwa kwa namna yoyote katika malipo hayo na kwamba  angeshirikishwa angeweza kunusuru fedha hiyo isilipwe.

Alidai mwaka 2012 aliitwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru)  kutoa maelezo  na kwamba maalipo yanaonesha kufanyika mwaka 2015 wakati yeye akiwa tayari ni mtuhumiwa na hakuwahi kuitwa mahali popote kuulizwa kuhusu mchakato mzima wa mradi, kabla maalipo hayo hayajafanyika angeweza kushauri.

Tido amedai kwa taaluma yake ya uandishi wa habari kwa miaka 50 sasa, waliufahamu muda mrefu na kwamba wahusika wakubwa walikuwa ni TCRA na TBC kama shirika la Umma walikuwa mstali wa mbele katika utekelezaji wake.

Amedai,  walishirikishwa katika vikao mbali mbali vya awali na kwamba wakati huo walipewa ishara ya maandalizi ya kuhakikisha wakati rasmi ukifika utekelezaji wa kuingia kwenye mfumo wa analogia unaanza ipasavyo.

Akiendelea kujitetea Tido alidai kuwa kwa kuangalia maeneo mengine shida kubwaza nchi za Afrika  nilikuwa ni kuwapatia watu kwenye uwezo wa kutekeleza mradi huo.

Amedai kutokana na ukubwa wa huo mradi, TBC ndiyo ilitegemewa kuwa inaongoza mradi huo hivyo iliruhusiwa kutafuta mmbia Mwenyekiti uwezo wa kifedha kusubiri kila na naye  kuendesha mradi huu.

Tido alidai kuwa walitakiwa 2015 wahamie katika mfumo huo mpya wa digitali na kuwa  TBC  ili kufanikisha hilo walianza kuzungumza na watu  mbali mbali ambapo kampuni za kimataifa yaliyokuwa na hadhi ambayo walikuwa wakiitaka yalikuwa machache na walikuwa na malengo ya kupata faida.

Tulifanikiwa kupata kampuni tatu kampuni ya Uswiss, kampuni ya Channel 2 group ya Dubai na kampuni ya Stertimes nao walikuwa na matakwa yao mbalimbali.

Amedai, kampuni ya Uswiss walionesha mapema tayari wamepata nafasi nzuri Afrika Magharibi katika nchi za Nigeria na Ghana wakajiondoahata walipopelekewa mwaliko hawakujibu.

"Kampuni ya Channel 2 group wao walitaka kuhakikishiwa  kama watashirikishwa katika mchakato na kwamba wafanye makubaliano ya awali hivyo waliandikishana na kuwaambia utakapofika wakati wa mchakato wasiwe na wasiwasi.


Tido amedai, waliandikishiana na  katika maandishi hayo yeye alisaini na kwa upande wa Channel 2 group alisaini mmiliki wake Sethi Dubai na kwamba alifanya hivyo kwa kuzingatia  hayo ni makubaliano ya mwanzo.

Aliendelea kudai  wakati wa kushiriki katika mchakato ulipofika kampuni hizo mbili zilishirikishwa na kuwasilisha michanganuo yao na hatimaye kupatikana mshindi Star times.

Amedai wakati wa mchakato wote huo ukiendelea a bodi ya TBC haikuwahi kulalamika  wala kutoa lawama zozote badala yake waliunga mkono jitihada hizo.

" Huu ulikuwa mradi wa mkubwa wa  kimataifa kwa hiyo bodi ya TBC waliamua kuuchukua mchakato mzima na kuendesha na kuuondoa katika bodi ya zabuni ambayo inashirikisha wafanyakazi wa TBC, pia ilipata ushauri wa PPRA,"ameeleza Tido mahakamani hapo.

Pia ilishirikisha taasisi nyingine kama TCRA, TIC, Wizara ya Mawasiliano, UDSM, Wizara ya Habari na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia,yalialikwa kwa kuleta wajumbe.

Alidai wataalam hao na kamati ya ufundi walikana kwa siku mbili Bagamoyo kuchambua michanganuo iliyowasilishwa na kampuni za Channel 2 group na Star time kwa kina ili waweze kufanya maamuzi sahihi.

Baada ya kupitia kwa kina  makampuni hayo waliridhika wamejieleza inavyopaswa, na kwamba baadaye walipeleka majibu yao kwa bodi ambayo iliamua mbia wa TBC awe Startimes .

Tido amedai waliendesha vikao vingi ikiwamo kuandaa rasimu ya mkataba  ambayo walimpatia mwakilishi wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG) akaipitie neno kwa neno kama inakubalika na baadaye aliwaarifu inakubalika.

Alieleza kuwa Tanzania ilikamilisha mradi huo mwaka 2015 na kuwa nchi ya pili katika bara la Afrika na wataalam toka nchi mbalimbali wamekuwa wakijua kuona imewezekanaje na hadi hivi sasa bado kuna nchi za Afrika bado zina suasua.

"Tangu nimekaa TBC sijawahi kupokea malalamiko yoyote toka kwa mmiliki wa Channel 2 Group Sethi, "ameongezaTido.

Akiendelea kutoa ushahidi wake, amedai, mkataba wake na TBC ulimalizika mwaka 2010, mchakato wa mabadiliko ya kutoka mfumo wa analoji kwenda digitali ulianza 2009 na kwamba hadi anaondoka alihakikisha umesimama kikamilifu.

Akiongozwa na Wakili  Matunda, Tido alioneshwa kielelezo kilichowasilishwa na upande wa mashtaka kwenye kesi hiyo ambacho kilioonyesha kuwa TBC, Serikali, AG na Wizara ya Habari waliipa kazi  kampuni ya uwakili ya Uingereza katika kesi ambayo ilikuwa ifunguliwe nchini humo.

Hata hivyo Wakili Matunda alimuonesha Tido vielelezo hivyo vya upande wa mashtaka  na risiti za malipo zilionesha mawakili hao wa Uingereza walitaka kulipwa Euro 280,603.57 huku TBC wakionesha mawakili hao walipwe Euro 434,226.21.

Tido amedai fedha hizo zinazodaiwa kulipwa kwa mawakili hao wa Uingereza na kusababisha hasara zililipwa kusiko julikana .

Hakimu Shaidi  aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9 mwaka huu

INASIKITISHA!KIVUKO CHA MV.NYERERE CHAZAMA ZIWA VICTORIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya kamii
KIVUKO cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani 
Ukerewe mkoani Mwanza kimezama ziwa Victoria.

Inadaiwa kwamba kivuko hicho kimezama kikiwa na abiria ambapo hata hivyo bado haijafahamika idadi ya abiria waliokuwemo ingawa taarifa za awali zinadai kilikuwa na abiria zaidi ya 90.

Kwa mujibu wa baadhi ya waliozungumzia kivuko hicho wamedai sema kilikuwa kinatokea Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye ghati ya Ukara.

Kwa mujibu wa nashuhuda wamedai kuwa ghafla kilianza kutitia kwenye maji kwa nyuma kulikokuwa na mzigo na kuwezesha abiria waliokuwa mbele kurukia majini na kuogelea na mitumbwi iliyokuwa pale kufanya kazi ya kuwaokoa abiria waliorukia majini.

Pia inadaiwa abiria wengi waliokuwa ndani ya Mv Nyerere hawakuweza kutoka na kuwa wamezama.

Mmoja ya waliozungumzia kiazama kwa kivuko hicho amedai idadi yaabiria waliopanda haijulikani ingawa uwezo wa kivuko ni kubeba abiria 150.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo hazikifanikiwa kwani simu yake haikuwa hewani.

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada y kupigiwa simu ya mkononi alisema yupo kikaoni.

Hivyo tutaendelea kuwajuza kinachoendelea na idadi kamili ua abiria waliokuwamo kwenye kivuko hicho.

Wakati huo huo Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ambayo chini ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano umesema unasikitishwa na tukio la kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere.

Kivuko hicho kimekuwa kinatoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya Ukara na Bugolora wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari naKitengo cha Habari na Mawasiliano  cha TEMESA imesema wanasikitishwa na ajali hiyo na inawaomba wananchi wote kuwa na subira wakati taarifa zaidi kuhusu tukio hilo la kusikitisha zikiendelea kutolewa.

Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
Baruapepe: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Nukushi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Uteuzi wa Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa unaanza leo tarehe 20 Septemba, 2018.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

20 Septemba, 2018

TUME YA UCHAGUZI YA TAIFA YAKANUSHA TUHUMA ZA CHADEMA

$
0
0
 
Na Idara ya Habari-NEC

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (pichani) amekanusha Tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe dhidi ya Tume kutokana na uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Monduli na Ukonga.
Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Monduli, Mkaoni Arusha na Ukonga Jijini Dar es Salaam ulifanyika Tarehe 16, Septemba mwaka huu pamoja na Kata 23 za Tanzania Bara.
Dkt. Kihamia akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo (20.09.2019) amesema tuhuma zilizotolewa na Mbowe dhidi ya Tume na dhidi yake binafsi hazina ukweli wowote.
Dkt. Kihamia aliwathibitishia waandishi wa habari kwamba tuhuma kwamba kulikuwa na vituo ‘fake’ 16 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ukonga ni za uongo na kwamba vituo vilivyotumika ni 673 ambavyo ni vilevile vilivyotumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
“Vituo vilevile 673 vilivyotumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ndio hivyohivyo vilivyotumika kwenye uchaguzi mdogo wa Septemba 16 Jimbo la Ukonga. Hakujapunguzwa kituo hata kimoja wala kuongozwa kituo hata kimoja…,” alisema.
Dkt. Kihamia aliongeza kwamba wakala wa Chadema wa kujumlisha matoke, Bi. Asia Msangi ambaye pia alikuwa mgombea wa chama hicho Jimbo la Ukonga alisaini fomu ya matokeo jambo ambalo linaonyesha kwamba chama hicho kiliridhia mchakato huo.
Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi alisisitiza kwamba ni vyema chama hicho kikawaeleza wananchi ukweli juu ya sababu zilizowapelekea kushindwa kwenye chaguzi hizo badala ya kuizushia Tume uongo kila mara.
“Watanzania wasipotoshwe, wanasiasa wasitafute sababu za kushindwa kwa kuzungumza mambo yasiyokuwa na ukweli na kama tuhumu za Chadema ni za ukweli basi ni bora wakaenda mahakamani. Hizi ni tuhuma za uongo zenye lengo la kujiosha,” alisema.
Kuhusu Monduli na tuhuma kwamba kuna mawakala wa Chadema waliozuiliwa, Dkt. Kihamia amesema kwamba wapo watu wasiokuwa mawakala wanaotambulika kisheria walitaka kukiwakilisha chama hicho na hivyo walizuiliwa.
“Sio kweli kwamba mawakala walikataliwa na kutolewa nje ila kilichotokea ni kwamba wapo watu ambao walifika kituoni kwenye vituo vinne tofauti wakidai kwamba ni mawakala wakati hawajaapa kufanya kazi hiyo kwa hiyo watu kama hao hawawezi kuruhusiwa,” alisema.
Mkurugenzi aliongeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwatuma Makamishna na Maofisa wake kwenye maeneo yote ambayo yalikuwa yanafanya uchaguzi ili kufuatilia mwenendo wa uchaguzi kwa hiyo Tume ina taarifa za uhakika juu ya yale yote yaliyojiri.
Kuhusiana na kujitokeza kwa wapiga kura wachache, Dkt. Kihamia alisema kwamba kwa kawaida chaguzi ndogo huwa hazina msisimko mkubwa kwa wapiga kura kwa hiyo idadi ya wapiga kura waliojitokeza sio ya kushangaza.
“Ukifanya utafiti duniani kote utagundua kwamba chaguzi ndogo huwa hazina wapiga kura wengi, kwa hiyo hili sio jambo la kushangaza,” alisema.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kihamia alimtaka, Mhe. Mbowe kumuomba radhi kwa kumtuhumu kuwa yeye ndio anahusika na mambo yaliyokinyume na sheria ndani ya Tume.
“Mhe. Mbowe sijawahi kukutana naye na yeye hajawahi kukutana na mimi, kwa maana hivyo hatujawahi kugombana, hivyo anatakiwa achague maneno ya kusema…..mimi sipendi kulumbana na wanasiasa na wanasiasa wengine wote waelewe hivyo, nipo hapa kuhakikisha kwamba Tume inatimiza wajibu wake,” alisema.



Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images