Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SARATANI SHINGO YA KIZAZI INAONGOZA KWA KUUA, BENKI YA BARCLAYS YATOA ELIMU KWA WAFANYAKAZI WAKE NAMNA YA KUJIKINGA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya saratani nchini Dk.Dominista Kombe amesema saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoongoza kwa kuua na kwamba kwa siku wagonjwa 80 wa aina mbalimbali  za  saratani hufariki dunia.


Ameishauri jamii na hasa  wanawake kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua iwapo wana tatizo la saratani au la huku akifafanua changamoto kubwa wagonjwa wengi wanafika hospitali wakiwa wamefikia hatua ya tatu au ya nne.


Dk.Kombe ambaye kwa sasa ni mstaafu na ameamua kuanzisha Dar es Salaam Oncological Care Clinic amesema hayo leo wakati anazungumza na wafanyakazi wa Benki ya Barclays kabla ya kuanza kuwapima saratani ya matiti.


Amefafanua ugonjwa wa saratani nchini umeshika kasi na saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoshika nafasi ya kwanza na nafasi ya pili ni saratani ya matiti.


Amesema kibaya zaidi idadi kubwa ya wanaosumbuliwa na saratani hizo ni watu wenye umri chini ya miaka 60 na ipo haja ya kuchukua hatua mbalimbali ili kuepuka ugonjwa huo.


Amefafanua ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa  kupima afya mara kwa mara ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa elimu ya namna ambavyo mwanamke anaweza kupima saratani ya matiti.

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (kulia), akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF).  
 Mshauri na mtaalamu wa masuala ya afya magonjwa ya saratani, Dk. Dominista Kombe (kulia) akionyesha jinsi ya kuangalia viashiria vya ungonjwa wa saratani ya matiti kwa baadhi ya wafayakazi wa Benki ya Barclays katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), jijini Dar es Salaam leo.
 Mratibu kutoka Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), Kisa Mwakatobe (kulia), akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki ya Barclays kwa wafanyakazi wake kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na taasisi hiyo.
 Mmoja wa waratibu kutoka Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), Gloria Kida (kulia), akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyougua ugonjwa huo pamoja na matibabu aliyoyapata wakati wa semina hiyo.

Wadau wakoshwa na mafaniko ya benki ya Benki ya Azania

$
0
0
WANAHISA wa benki ya Azania wameonyesha kuridhishwa na mwenendo, ufanisi pamoja na mafanikio ya benki hiyo licha ya uwepo wa changamoto kadhaa zinazoikabili sekta ya benki hapa nchini, huku wakionesha kuridhishwa zaidi na namna benki hiyo ilivyoweza kukabiliana na changamoto ya mikopo isiyolipika.(Non- performing Loans) 

Wakizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, wadau hao wamesema baada ya kupitia ripoti ya mwaka ya mwaka 2017 kuhusu mwenendo wa biashara wa benki hiyo wamebaini kuwa benki hiyo imepiga hatua kubwa kwenye nyanja kadhaa ikiwemo ongezeko la rasilimali (asset growth), kukidhi matakwa ya sheria za kibenki pamoja na kufanikiwa kukwepaji changamoto ya mikopo isiyolipika.

“Kwa mujibu wa ripoti hii ongezeko la rasilimali yaani asset growth ni asilimia 15 na zaidi kinachovutia zaidi ni kuona kwamba benki yetu imejitahidi sana kukabiliana na tatizo la mikopo isiyolipika kwa kuwa na asilimia 8 tu ya mikopo na wito wangu kwa uongozi wa benki ya Azania ni kuhakikisha asilimia hizi zinashuka hadi kufikia chini ya asilimia 6,’’ alisema mmoja wa wanahisa hao Bw Misheck Ngatunga.

Awali, akisoma taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Charles Itembe alisema ufanisi wa benki hiyo umethibitishwa zaidi mwaka huu baada ya kutoa gawio la kiasi cha Sh. Mil 633 kwa wanahisa wake ikiwa ni mara ya kwanza tangu benki hiyo ianzishwe mwaka 1995. Alisema mafanikio hayo ya kiutendaji yameiwezesha benki hiyo kupata faida baada ya kodi kiasi cha Sh Bilioni 1.81 kutoka hasara ya sh. Bilioni 6.04 iliyoikumba benki hiyo mwaka 2016.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw Charles Itembe, (kushoto) akizungumza na wadau wa benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki ya Azania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja naMakamu Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi wa benki hiyo, Bw  Eliudi Sanga (katikati) na Mkurugenzi wa Masuala ya kisheria wa benki hiyo Bw Charles Mugila.
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi wa benki ya Azania Bw  Eliudi Sanga (kushoto) akizungumza na wadau wa benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki ya Azania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw Charles Itembe.
 Baadhi ya wadau wa benki ya Azania wakifuatilia mkutano huo. 

RAIA WA MALAWI AFIKISHWA MAHAKAMANI YA KISUTU KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
RAIA wa Malawi, Edward Banda (38), amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi kuwepo nchini bila kibali,kutoa taarifa za uongo kwa maofisa wa serikali na kujipatia kitambulisho cha mpiga kura kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hati ya mashtaka leo Septemba 22, wakili wa serikali Mwandamizi, Veronika Matikila, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,, Wanjah Hamza amedai Septemba 18, mwaka huu katika kituo cha Daladala eneo la Kawe Wilaya ya Kinondoni mshtakiwa  alikutwa akiwa hana nyaraka za kumuwezesha kuwepo nchini.

Pia imedaiwa, kati ya Januari na Oktoba 2015 katika shule ya msingi Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa serikali kuwa yeye ni mtanzania ili aweze apate kitambulisho cha mpiga kura.

Imeendelea kudaiwa, mshtakiwa katika kipindi h cha kati ya Januari na Oktoba 2015, huko katika eneo la shule ya Msingi ya Mbezi Beach kwa udanganyifu aliwadanganya maofisa wa Tume ya Uchaguzi (NEC) waweze kumuamini na kumpatia kadi ya mpiga kura namba 1-1001-8940-587-6.

Hata hivyo, mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake hayo, hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Hata hivyo wakili huyo aliwasilisha hati kutoka kwa  (DPP) mahakamani hapo kwa Kuzuia dhamana ya mshtakiwa huyo.


Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Oktoba 4, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

OSC kupunguza gharama za kufanya biashara

$
0
0
 Naibu Meneja wa Bandari  Utekelezaji, Ahmed Mchalaganya, kulia akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba jinsi TPA inavyohudumia shehena ya mizigo inayopita bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba akitoa maelekezo kwa maofisa wa kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo hicho bandarini. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini.
 Afisa Mkaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo bandarini, Bw. Deogratias Mosha, kulia akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba jinsi kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo kinavyofanya kazi zake bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo hicho kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo,  Omary Mgumba akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na baadae kufanya ziara bandarini kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. 

Na Leonard Magomba
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mh. Omary Mgumba amesema kwamba kuanza kufanyakazi kwa kituo cha kuwaweka wadau wa bandari pamoja (One Stop Centre) kutapunguza gharama za kufanya biashara nchini.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejenga kituo cha kuwaweka wadau wa bandari pamoja (One Stop Centre) ili kurahisisha utendaji kazi na kupunguza urasimu wa utoaji wa mizigo bandarini.


Akizungumza wakati wa ziara yake kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao katika Bandari ya Dar es Salaam, Waziri huyo amesema kwamba kuna haja ya wadau wote kuanza kukitumia kituo hicho ili kuboresha huduma.

TRA YAENDELEA KUWAPIGA MSASA WATUMISHI WAKE

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa elimu ya maadili na namna bora ya kuhudumia wateja kwa watumishi wake nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao na kuwaongezea weledi katika majukumu yao ya kila siku.

Akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika ofisi ya TRA Moshi mkoani Kilimanjaro, Afisa Maadili Mwandamizi wa mamlaka hiyo Adelaida Rweikiza amesema kuwa  ni wajibu wa watumishi wote wa TRA kuwahudumia wateja kwa usawa na kwa kiwango cha hali ya juu.

"Ni wajibu wetu sisi watumishi wa TRA kuhakikisha tunatoa huduma bora pamoja na kutumia lugha nzuri kila tunapowahudumia wateja wetu," alisema Rwikiza.

Rweikiza ameongeza kuwa, maadili katika Utumishi wa Umma  ni jambo la msingi hivyo amewasisitiza watumishi hao kuwa waadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa na mienendo mibaya ambayo inaweza kuharibu taswira ya TRA.

Naye, mmoja wa watumishi hao ambaye ni Afisa wa Kodi Robert Mlay amefurahishwa na kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoa elimu kwa watumishi wake na kufafanua kuwa, elimu hiyo itawasaidia katika kuongeza ufanisi na kutimiza malengo ya mamlaka.

"Nimejisikia vizuri sana kupata elimu hii ya maadili na namna bora ya kuwahudumia wateja kwasababu itatusaidia sisi kama watumishi wa TRA kutoa huduma kwa haki bila upendeleo wowote," alieleza Mlay.
 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro Msafiri Mbibo akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao.
  Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao.
  Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akijadiliana jambo na Afisa Kodi Mwandamizi wa mamlaka hiyo Shaban Makumlo wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi hao iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KALEMANI AMUONDOA MENEJA WA TANESCO MEATU KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani amemuondoa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae katika nafasi ya umeneja baada ya kushindwa kusimamia usambazaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme vijijini (REA) wilayani humo na amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kumpangia kazi nyingine.

Waziri KALEMANI amechukua hatua hiyo katika mkutano wa hadhara mjini Meatu  akiwa katika ziara yake ya kukagua  kazi zinazofanywa na wakandarasi wa mradi wa Umeme vijijini REA awamu ya tatu Septemba 20, 2018, ambapo anaanzia katika uzinduzi wa mradi wa umeme  katika ofisi ya kijiji cha Dakama wilaya ya Meatu.

Dkt. Kalemani ameoneshwa kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi anayesambaza umeme wilayani Meatu ambaye ni kampuni ya White City, kutokana na kutokuonekana katika vituo na kutokuwa na vifaa vya kutosha na vituo vya kutosha.

“Kasi ya mkandarasi hapa ni mbovu niliteegemea nione wakandarasai wanachakarika maana kote nilikotoka nimekuta wanachakarika, pili nilitegemea nione yadi ya vifaa vya wakandarasi wetu”

“Huyu meneja ndiye msimamizi wa wakandarasi, namuuliza anasema hajui leo wakandarasi wako wapi sasa anasimamia nini? Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO pokea maelekezo, kuanzia sasa huyu Meneja wa TANESCO Wilaya mtoe, weka Meneja mwingine kuanzia kesho hapa, wananchi wanataka umeme hapa” alisema Dkt. Kalemani.

Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani amewahakikishia wananchi wa vijiji 36 vya wilaya ya  MEATU kupata umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya tatu na akawasisitiza kuwa umeme utakapowafikia wautumie kwa ajili ya maendeleo.
 Aliyekuwa Meneja wa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kulia), wakati wa ziara yake wilayani humo Septemba 20, 2018.
  Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwaonesha wananchi wa Kata ya Mwamishali kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA , alipozungumza nao wakati wa ziarayake wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
 Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu wakishangilia baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuwatangazia kuwa vijiji vyote katika wilaya yao vitapata umeme kupitia mradi waWakala wa Nishati  Vijijini (REA) Awamu ya tatu, baada ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu, Septemba 20,2018.

NSSF NA NBC KUENDELEZA MAHUSIANO MAZURI YA KIBIASHARA

$
0
0

Uongozi wa Benki ya NBC umetembelea Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu yenye lengo la kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo baina ya Benki na shirika hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bwana Theobald Sabi katika mazungumzo alisema benki hiyo ni miongoni mwa taasisi ambayo serikali imeweka hisa zake na inajivunia kufanya kazi na NSSF,kwani alisema Benki yake inaendeshwa kisasa zaidi ambapo katika kuhakikisha wanahudumia wananchi kwa haraka NBC wana huduma ya “mobile banking” inayoweza kuwafikia wananchi wengi waliopo vijijini wakiwemo wastaafu wa NSSF.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio aliishukuru NBC kwa kuifanya NSSF kuwa mteja wake mkubwa zaidi katika huduma za kibenki na kuwashukuru kwa kuwa tayari kutoa ushauri wa kitaalamu utakaohitajika na Shirika kwa sasa katika boresha huduma zao.

Hata hivyo Bwana Erio aliwahakikishia uongozi wa NBC kwamba ushirikiano uliopo utaendelea kuimarika chini ya uongozi wake na alissitiza kuhakikisha mifumo ya fedha za wananchama inaendelea kuwa salama na kutumika kwa maendeleo ya Taifa. Pia alishukuru NBC kwa kuendelea kutoa riba ya asilimia tano kwenye akaunti ya makusaanyo kutoka kwa wanachama wa NSSF.

NBC imekuwa Benki ya nne kuweza kutembelea katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo benki nyingine ni pamoja na CRDB,NMB na UBA ambazo wote kwa pamoja wamekutana na NSSF na kupanga namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na ujumbe wake (kushoto) akiwa na ujumbe wa Menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara nchini NBC(kulia) ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Theobald Sabi wakifurahia jambo kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika katika makoa makuu ya NSSF jijini Dar es salaam ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza mahusiano yao ya kibiashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) , Bwana William Erio( katikati) akiwa na Menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara,kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi na wajumbe nane wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo makuu ya NSSF jijini Dar es salaam.(Watatu kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa NSSF Bwana Gambamala Luchunga na wa kwanza kushoto ni Meneja kiongozi wa Masoko na Uhusiano wa NSSF Bi.Lulu Mengele.)

DEREVA BODABODA ASHINDA BAJAJI BAADA YA KUIBUKA MSHINDI WA DROO YA SPORTSPESA

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
DEREVA wa bodaboda aliyetambulika kwa jina la Msafiri mkazi wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga ameshinda bajaji baada ya kuibuka mshindi katika droo ya  Sportpesa.

Imeelezwa kuwa mshindi huyo ni wa kwanza baada ya Sportspesa kuzindua rasmi shindano la Shida zaidi na Sportspesa jana.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportspesa Abbas Tarimba ameeleza furaha ya kumpata mshindi huyo kwa mara ya kwanza  ambaye ametokea mkoani Tanga.

Tarimba ametoa rai kwa washiriki kuendelea kubashiri kwa wingi zaidi ili kujiwekea nafasi ya  kuingia kwenye droo na kubadilisha maisha yao kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Martin
Langarivo amempongeza mshindi huyo mwenye umri wa miaka 21.

Ametoa rai kwa  wengine kushiriki kwani ni mchezo ambao unafata masharti yote ya bodi pamoja na kutenda haki kwa washindi na hakuna mtu ambae anapangwa kama watu wanavosema .

Kwa mujibu wa Sportspesa ni kwamba baada ya bajaji hiyo kupata mshindi sasa zimebaki bajaji 99 ambazo zinasubiri washindi.

RAIS DR. SHEIN AWEKA WA JIWE LA MSINGI SKULI YA SEKONDARI KINUNI ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar sherehe zilizofanyika leo,akiwepo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pemba Juma.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Salem Construction LTD Nd,Aziz M.Qurban (katikati) alipokuwa akitoa maelezo baada ya kuweka  jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Magharibi leo ,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Wanafunzi   katika sherehe ya  uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Magharibi,sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma(kushoto)Waziri Kiomgozi Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kijito Upele Mhe.Shamsi Vuai Nahodha na Naibu katibu Mkuu CCM Zanzibar Dk.Juma Abdala Sadala(wa pili kushoto). 
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria katika sherehe ya uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa   Wanafunzi hao leo katika sherehe Skuli hapo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono  Wananchi na Wanafunzi mara baada ya kuweka   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Magharibi,sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,(katikati) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pemba Juma. 
 Baadhi ya madarasa mapya ya Skuli ya Sekondari ya Kinuni  Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Magharibi,yaliyowekwajiwe la msingi na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar. (Picha na Ikulu)

ULEGA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

NAIBU Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi mafunzo ya ufugaji wa kuku kibiashara katika jiji la Dar es salaam na kueleza mikakati ya Wizara inayolenga kuongeza uzalishaji wa sekta ya mifugo na uvuvi hasa katika kuangalia suala la chakula na lishe kwa mifugo ili kuweza kuinua kipato kwa wananchi.

Akizungumza katika ufunguzi huo Ulega ameeleza ķuwa sekta ya ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli muhimu za kiuchumi zinazogusa wananchi wa mjini na vijijini na zaidi ya asilimia 72 ya kaya zote nchini hufuga kuku kwa malengo ya kuboresha lishe na kipato.

Na amewataka wanawake na vijana kujikita katika ufugaji wa kuku kwani huhitaji mtaji mdogo na sekta hiyo huchangia asilimia 53 ya kipato cha kaya za wafugaji wa kuku ukilinganisha na vyanzo vingine vya mapato.

Aidha kuhusiana na mada zitakazojadiliwa katika mafunzo hayo Ulega amesema yatakayojadiliwa ni pamoja na utengenezaji na matumizi ya vyakula vya kuku, uzalishaji na upatikanaji wa vifaranga bora, uthibiti wa magonjwa na matumizi ya dawa za kuku, ujasiriamali na masoko ya kuku na mazao yake.

Sambamba na hayo kutakuwa na fursa ya uanzishwaji vyama vya ushirika, majukwaa na mitandao ya wafugaji wa kuku nchini pamoja na upatikanaji wa mikopo hususani kupitia mfuko wa vijana, wanawake,wazee na wenye ulemavu katika halmashauri zote kama mpango wa serikali unavyoeleza.

Ameeleza kuwa baada ya mafunzo hayo maarifa ya wafugaji hao yataongezeka na kupelekea kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji wa kuku wa mayai hivyo hali ya kipato itaongezeka zaidi.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015-2020 pamoja na mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka mitano yaani 2015/206 hadi 2020/2021 na amewataka wafugaji watumie fursa ipasavyo na kulipeleka taifa kwenye uchumi wa kati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa kuku leo katika katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wafugaji hao yaliyoandaaliwa na Wizara hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa utafiti, mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Angello Mwilawa akizungumza na wafugaji wa kuku wakati ya utolewaji wa mafunzo hayo katika kuhakikisha sekta hiyo inakuwa bora zaidi.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwasikiliza na kujibu maswali ya wafugaji waliohudhuria mafunzo ya ufugaji wa kuku yaliyoandaliwa na Wizara hiyo.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

UJENZI BARABARA KIMARA KOROGWE KWENDA TABATA KUPITIA KIBANGU WAFIKIA PAZURI

$
0
0
 Sehemu ya madaraja yanayojengwa katika Barabara inayotoka kimara Korogwe kupitia Kibangu mpaka Tabata yakiwa katika hatua za Mwisho za kukamilika hili kupunguza foleni katika barabara ya Morogoro Road ambayo inajengwa kw anjia sita kwa sasa kutoka Ubungo mpaka kibaha hivyo njia hizi za mchepuko zitasaidia kwa kiasi kikubwa kugawa magari yanayokwenda Tabata, Vingunguti mpaka Temeke.
 Upande wa pili wa daraja hilo ukionekana huku gari ikibeba udongo usiohitajika katika pembezoni mwa daraja hilo.
 Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa Barabara ya Kimara Korogwe kupitia Kibangu Mpaka Tabata Kisukulu kwa kiwango cha zege kama ilivyojengwa barabara ya Mwendokasi
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa Barabara ya Kimara Korogwe kupitia Kibangu Mpaka Tabata Kisukulu kwa kiwango cha zege  kama ilivyojengwa barabara ya Mwendokasi huku upande uliokamilika vyombo vya moto.

DK NDUGULILE AZINDUA HUDUMA YA TB KUPITIA TEKNOLOJIA YA SIMU ZA MKONONI

$
0
0
Na Zanab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile amewataka Wizara ya Afya kuongeza idadi ya mikoa iliyopo katika programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi ili kila mwananchi aweze kupata huduma hiyo.

Hayo yamesemwa leo wakati wa uzinduzi wa huduma ya TB kupitia kupitia teknolojia ya simu za mkononi unaojulikana kama TAMBUA TB  kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kufahamu kuhusu dalili za Kifua  pamoja na mpango labambe wa kudhibiti kifua kikuu nchini.

Dkt Ndugulile amesema kuwa pamoja na kuwa na programu hiyo lazima Wizara watoe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu ambapo inakadiriwa zaidi ya vifo 27,000 vinasababishwa na uginjwa huo.

Amesema, katika kuboresha na kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu, wameweka mifumo ya tambua ambapo imeongeza mashine 209 zinazoweza kutambua mgonjwa ndani ya masaa mawili.

Dkt Ndugulile amesema, kupitia Wizara mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano 2015-2020 lengo likiwa ni kupunguza maambukizi mapya ya TB kwa asilimia 20 na idadi ya vifo vinavyotokana na TB kwa asilimia 35.

Amesema, kuwa kutokana na mpango wa Wizara wamewekea mkakati wa kuboresha zaidi huduma  na kutoa rai ya kuongeza idadi ya mikoa kwani wananchi wote wanahitaji huduma hiyo ili kupunguza kasi ya maambukizi.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile  akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  uliojulikana kwa jimba TAMBUA TB akiwataka kuongeza  idadi ya mikoa ili wananchi wapate huduma hiyo nchini kote.
Meneja wa mradi wa ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  Dk Beatrice Mutayoba akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo akielezea namna mfumo utakavyosaidia kutambua wagonjwa kwa njia rahisi na kwuashauri kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya kupata matibabu.
Baadhi ya washiriki mbalimali wakiohudhuria uzinduzi wa programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  uliojulikana kwa jimba TAMBUA TB.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja madaktari kutoka sehemu mbalimbali na mashirika yalityosaidia kufanikisha mradi huo.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI MGALU ATOA PONGEZI KWA TPDC KUPITIA KAMPUNI YAKE TANZU YA GASCO KWA KUKAMILISHA UTOBOAJI WA BOMBA LA GESI- MKURANGA

$
0
0

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiongea na wanahabari mara baara ya kukagua eneo lilipokuwa inafanyika kazi ya utoboaji wa bomba la gesi asilia na kuweka toleo katika kijiji cha Mwanambaya Wilayani Mkuranga kwa ajili ya kuwasambazia wateja wa viwandani katika Wilaya hiyo. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Mkuranga.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akipata maelezo machache kutoka kwa Mhandisi wa Mitambo wa Kampuni Tanzu ya GASCO, Dominic Ngunyami mara baada ya kutembelea eneo la lilipofanyika kazi ya utoboaji wa bomba la gesi asilia na kuweka toleo katika kijiji cha Mwanambaya Wilayani Mkuranga kwa ajili ya kuwasambazia wateja wa viwandani katika Wilaya hiyo.
 Bomba likiwa limetobolewa.
Mafundi wakikamilisha ufungaji wa bomba hilo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

RAIS SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA SKULI MPYA YA SEKONDARI KINUNI

$
0
0


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amesema mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Elimu nchini yanatokana na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika Skuli ya Sekondari ya Kinuni iliyopo Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Unguja, amesema ujenzi wa skuli hiyo ya Ghorofa ambayo ni ya kisasa ni hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu.

Alisema CCM kupitia Ilani yake imeahadi kuimarisha Sekta ya Elimu kwa kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa elimu ikiwemo kujenga majengo ya kisasa yanayoendana na kasi ya maendeleo katika zama za sasa.
Alibainisha kuwa Serikali ya awamu ya saba inaendeleza kwa vitendo falsafa ya elimu bila ya malipo iliyoasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Aman Karume kwa lengo la kukuza kiwango cha elimu.

Alisema serikali ya ASP ilitangaza elimu bure kwa lengo la kuwakomboa watoto wa Waafrika waliokoseshwa fursa ya elimu kwa makusudi na utawala uliokuwa ukitawala kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964.Dk.Shein alisema pamoja na maendeleo yanayopatikana katika sekta za elimu bado zipo changamoto zinazoendelea kutatuliwa zikiwemo upungufu wa madarasa, madawati pamoja na upungufu wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi.

Alisema Zanzibar kwa sasa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu ikilinganishwa na kabla ya Mapinduzi kwani na skuli za msingi 62 na skuli za sekondari nne lakini kwa sasa idadi imekuwa ni kubwa hadi hatua ya kuwa na Vyuo vikuu vinavyozalisha wataalamu wa kada tofauti kila mwaka.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar sherehe zilizofanyika leo,akiwepo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pemba Juma,[Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
DSC_6117
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Salem Construction LTD Nd,Aziz M.Qurban (katikati) alipokuwa akitoa maelezo baada ya kuweka  jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo ,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar.
DSC_6388
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Wanafunzi   katika sherehe ya  uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma(kushoto)Waziri Kiomgozi Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kijito Upele Mhe.Shamsi Vuai Nahodha na Naibu katibu Mkuu CCM Zanzibar Dk.Juma Abdala Sadala(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.] 21/09/2018. 
DSC_6430
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria katika sherehe ya uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa   Wanafunzi hao leo katika sherehe Skuli hapo, [Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
DSC_6054
Miongoni mwa madarasa mapya ya Skuli ya Sekondari ya Kinuni  Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,yaliyowekwajiwe la msingi na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar.

NEWZ ALERT:RAIS DKT. MAGUFULI ATANGAZA SIKU NNE ZA MAOMBOLEZO KUANZIA LEO KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV NYERERE ZIWA VICTORIA

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusiana na ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake  kati ya kisiwa cha  Bugolora na Ukara katika ziwa Victoria  Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ambapo  watu 131 wanahofiwa kupoteza maisha. Pia Rais Dkt. Magufuli ametangaza siku nne za Maombolezo kuanzia leo tarehe 21 Septemba 2018. PICHA NA IKULU

CASSIUS MDAMI KWELI UMEENDA; ILA UMEBAKI KWENYE NYOYO ZETU

$
0
0
Cassius O. Mdami ni miaka miwili sasa tangu umetuacha familia yako; mke wako Rose Mdami; na watoto wako Martina, Grace, Gideon, Gonsalver na Gibson. 
Kila uchao hatuachi kuisikia sauti yako na kukumbuka ucheshi wako kila mara ulipokuwa nasi. Kifo kimetutenganisha nawe. 
 Mungu anajua maumivu yote na machungu tuliyopitia familia yako na tunayoendelea kuyapitia kwa kutokuwepo kwako. Machozi yanatudondoka na hakuna wa kuyafuta; ila tumaini tunalo ya kwamba iko siku moja tutaonana nawe katika makao ya Baba Mbinguni.
Mungu endelea kutufariji kama maneno yako yasemavyo katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 31:8 “ Naye Bwana ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike ”
 Pumzika kwa Amani Baba G4

H-TOWN OLD SCHOOL REUNION 2019, HOUSTON, TEXAS, LOADING......

$
0
0
H-Town Old School Reunion 2019 kufanyika March 22 na 23 Houston, Texas kaa mkao wa kula ikiwemo Bonanza la mpira wa kikapu na soka la Simba na Yanga inayosubiliwa kwa hamu Houston na vitongoji vyake.
 Timu ya Yanga
Timu ya Simba
Image result for OLD SCHOOL OHIO VIJIMAMBO
Timu ya mpira wa kikapu

RATIBA NI KAMA IFUATAVYO

Ijumaa March 22, 2019 ni *Karibu Night* Music policy ni *NEW SCHOOL* by Houston Dj’s 
Crystal Palace Party Hall
12450 Bissonnet #220
Houston, TX. 77099
Jumamosi March 23 Litaanza bonanza la kikapu na baadae mpira wa Simba na Yanga
Baadae Usiku kutakuwa na *Old School Party* usikose burudani kutoka kwa The Legendary DJs Luke Joeaka Mix Master Akishirikiana na DJ DENNIS FUNKHOUSE

Crystal Palace Party Hall
12450 Bissonnet #220
Houston, TX. 77099

Cover Charge
Sept - Dec
Fri $10
Sat $20
*Jan-March 22*
Fri $20 couple $30
Sat $30 Couple $50
Kulipia mlangoni
Fri $30
Sat $40
Lipia kupitia CashApp 
Luke Joe 301 661 6696 au Gloria Alex 336 214 0218-Tuma lisiti/jina kamili
*Stay tuned more details to come!!

VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YASHIKA KASI, MSIKILIZE KAMISHNA SIANGA...

Volunteers Summer 2018 Tanzania

$
0
0
Each year SHINA, Inc., is accompanied by volunteers who assesses projects to give an objective eye in Helping The Most Vulnerable. Thank you for your support and faith in what we do. Together we make a difference

TANESCO IHARAKISHE KUFIKISHA UMEME BANDARI KAVU -MGALU

$
0
0
 Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipowasili kutembelea mradi wa bandari kavu ,Kwala Kibaha Vijiji, Mkoani Pwani
 Meneja wa mradi wa bandari kavu mhandisi Raymond Kweka ,akitoa taarifa ya mradi wakati naibu waziri wa nishati Subira Mgalu hayupo pichani alipotembelea mradi huo.
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wakazi wa  kijiji cha Mperamumbi Kibaha Vijijini.
Picha na Mwamvua Mwinyi.

NAIBU Waziri wa Nishati,Subira Mgalu ameliagiza shirika la umeme (TANESCO) kuharakisha kufikisha umeme katika mradi mkubwa wa Bandari Kavu ,Kwala Kibaha mkoani Pwani  na wasiwe sehemu ya kuchelewesha mradi huo wa kimkakati wa kitaifa. 

Aidha amesema ,serikali ipo kwenye mpango wa kumpata mkandarasi wa mradi mpya wa Peri Urban ambapo anatarajiwa  kuanza kazi Novemba mwaka huu katika mitaa na vitongoji 182 na zimetengwa sh. bilioni 86 kwa ajili ya kazi hiyo. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea ujenzi wa Bandari Kavu na kuongea na wakazi wa Mperamumbi, Kwala na Msua alitaka nishati ya umeme ipatikane wakati mradi ukiendelea hadi ukikamilika. 

Subira alisema, mradi usikwame kwasababu moja wapo nishati anataka nishati ya uhakika ipatikane ili kazi iende haraka .

Alilitaka shirika hilo lijipange vizuri katika maeneo ya miradi mikubwa ya kimkakati na uwekezaji na viwanda na ,wakimbizane na  fursa hiyo. 

Subira alifafanua,  anaamini ukikamilika mradi huo sio fursa ya kitaifa bali na Tanesco kwani itakuwa ni mteja wao. 

"Mamilioni yanalala kwenye mradi huo ,mataluma ya reli yameanza kutandazwa kwenye mradi wa standard gauge, kwahiyo Tanesco msije mkawa sababu ya kucheleweshe suala hili "

Akizungumza na wakazi wa ,Msua na Mperamumbi aliwahakikishia kuwa umeme utafika kwenye maeneo hayo kupitia mradi wa Peri Urban. 

Subira aliwataka wakulima na wafugaji kuheshimiana,kuthaminiana na kufanya kazi pamoja .

Aliwaambia penye maendeleo panahitaji amani hivyo makundi hayo yanapaswa kuishi kwa upendo na sio visasi. 

Meneja mradi wa Bandari Kavu, mhandisi Raymond Kweka  alielezea, mkandarasi wa mradi  ni Suma Jkt na msimamizi ni mamlaka ya bandari Tanzania .

Alisema mradi upo kwenye awamu ya kwanza ya kuandaa na kuweka ukuta. 

Kwa upande wake, mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, alisema, endapo barabara ya lami ikikamilika italeta maendeleo chanya na kukuza uchumi wa Kwala. 

Akielezea kuhusu umeme ,Jumaa alieleza ni hitaji la wengi katika kijiji cha Mperamumbi, kitongoji cha Msua kata ya Kwala ambapo ikisogezwa huduma hiyo wananchi wataanza kuuza na kuhifadhi vitu vya biashsra na matumizi ya nyumbani. 
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images