Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

DONGE NONO KUTOLEWA KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MITA ZA MAJI JIJINI MWANZA

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) imesema itatoa zawadi nono kwa wananchi watakaofanikisha kukamatwa kwa wezi wa mita za maji jijiini humo. Akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Mwanza hapo jana, Meneja Msaidizi- Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Mohamed Saif alibainisha kwamba kumekuwepo na wimbi la wizi wa mita za maji kwenye maeneo mbalimbalii jijini humo.

Saif alisema jitihada mbalimbali zinaendelea kuwasaka wanaojihusisha na matukio hayo ya wizi na alibainisha kwamba mwananchi atakayefanikisha kuwabaini na kuwafichua wezi hao atapewa zawadi nono. Hata hivyo, Saif hakuweka bayana zawadi itakayotolewa lakini alimthibitishia mwandishi wa habari hii kwamba Mamlaka imeandaa zawadi nono ambayo mtoaji wa taarifa itakayofanikisha kuwakamata wezi hao ataifurahia.

“Ninawathibitishia kwamba mwananchi atakayefanikisha kuwafichua hawa wanaojihusisha na matukio haya ya wizi. Mamlaka itamzawadia zawadi nzuri ambayo naamini ataifurahia,” alisema.

Alilaani matukio hayo ambayo yanaendelea kushamiri kwenye maeneo mbalimbali Jijini humo ambayo alisema yanaipotezea mapato makubwa Serikali na pia yanasababisha upotevu mkubwa wa maji kwenye maeneo husika.

"Wahujumu hao huwa wanafungua mita za maji na kuziiba huku nyuma wakiacha mabomba yanamwaga maji mengi ambayo kimsingi yanapotea na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa maji suala ambalo linaisababishia hasara kubwa Serikali," alisema.

Saif alisema ndani ya kipindi cha Mwezi mmoja kuanzia Agosti hadi Septemba mwaka huu, idadi ya mita za maji zilizoibiwa jijini humo imefikia mita 170. Aliongeza kuwa upotevu wa maji unaotokana na wizi wa mita unasababisha kuzorota kwa huduma ya usambazaji majisafi kwani gharama inayopaswa kutumika mahali pengine ikiwemo uboreshaji wa huduma na pia kuunganishia wateja wapya inatumika kwenye ununuzi na ukarabati wa miundombinu hiyo iliyoibiwa au iliyoharibiwa wakati wa matukio hayo ya wizi.

Aidha, alisema MWAUWASA kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama imejipanga kuhakikisha hujuma hizo zinakomeshwa na aliwaasa wananchi kutoa ushirikiano katika hilo na pia aliziomba Serikali za Mitaa kuimarisha ulinzi shirikishi katika mitaa yao kwa lengo la kudhibiti wimbi la wizi wa mita za maji kwenye maeneo yao.

MICHUZI TV LIVE: ''SIRI YA USHINDI WA CCM KATIKA UONGOZI WA AWAMU YA 5''

Mafundi washauriwa kuwa waaminifu

$
0
0
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Wazazi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Edson Fungo kwenye tai nyekundu akioneshwa jinsi injini ya gani inavyofanya kazi na mwanafunzi aliyehitimu Mussa Ally.
Na Mwandishi WETU

WANACHUO wa Bruno Vocational Training Centre (BVTC) wameshauriwa kutumia ujuzi walioupata kufanya kazi za ufundi kwa bidii na waaminifu.

Hayo yalisemwa jana na Mjumbe wa Kamati ya Wazazi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam na diwani Mstaafu wa Kata ya Ilala, Edson Fungo kwenye mahafali ya 25 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana.

'Kazi za ufundi zinahitaji ujiaminishe mwenyewe kwa sababu kadri fundi unapokuwa mkweli na kutengeneza gari kwa uaminifu ndipo unapoletewa kazi nyingi' alisema Fungo.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imejikita kwenye ujenzi wa viwanda hivyo ametaka vijana waliomaliza mafunzo yao ya ufundi kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda lifanikiwe.

Fungo alimpongeza Mkurugenzi Chuo hicho, Bruno Ndege kuanzisha mafunzo ya ufundi na udereva katika eneo la watu maskini la Buguruni ambao vijana wengi ambao hawapati nafasi ya kuendelea na masomo wanajiingiza kwenye vitendo viovu vya wizi na uhalifu.
Alisema Chuo hicho kimekuwa kikisaidia Serikali kuwaandaa vijana kujitegemea na kuwafanya kuwa mafundi stadi wenye uwaledi katika fani hiyo.

Katika risala ya wanachuo hao waliomba serikali iendelee kukaza kamba ya utekelezaji wa kazi iliyoanzisha ya kukagua madereva wasiopitia shule ya udereva ili kupunguza ajali za barabarani.

Mkurugenzi wa BVTC, Ndege alisema kutoka chuo hicho kuanzishwe kimetoa wahitimu 11,041 katika kipindi cha miaka 25 ambao wengi wao wamejiriwa katika sekta mbalimbali na taasisi za serikali na binafsi.

Alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za utoro wa wanafunzi watukutu na wazazi kushindwa kuwalipia ada watoto wao.

MNAIGERIA KIZIMBANI KWA SHTAKA LA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
RAIA wa nchini Nigeria, Martine Ike (46) mfanyabiashara na Mkazi wa Mbezi Salasala, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusafirisha gramu 647.7 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Wakili wa Serikali, Faraja Nguka akisoma hati ya mashtaka, leo Septemba 18,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile amedai kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Julai 6,2018.

Imedaiwa, siku ya tukio, mshtakiwa huyo akiwa katika ofisi ya basi la kampuni ya Tahmeed iliyopo Mwembe Tayari Mombasa nchini Kenya, alikamatwa akisafirisha dawa hizo za kulevya zenye uzito wa gramu 647.7.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shtaka lake, hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Septemba 26 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

MICHUZI TV LIVE: IBADA YA KUAGWA MWILI WA MISANYA BINGI

Tigo na Clouds Wazindua Msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote kupata vibali kutoka kwa baraza hilo. Tigo Fiesta 2018 inatarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) .

Tamasha la kusisimua zaidi la muziki na utamaduni Afrika Mashariki na Kati, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Lama Lote sasa lipo tayari kukonga mioyo na 100% mziki wa nyumbani katika mikoa 15 ya nchi. Kauli mbiu ya Tigo Fiesta 2018 ni Vibe Kama Lote, ikiashiria burudani maridhawa na ladha ya kumbukumbu zisizofutika zinazoendana na msimu huu nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alibainisha kuwa, msimu wote wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote utashuhudia burudani 100% kutoka kwa wasanii wa kitanzania, kufuatia mafanikio makubwa ya mfumo uliotumika mwaka jana. Shangwe zinatarajiwa kuanza mjini Morogoro siku ya Jumamosi tarehe 29 Septemba.

‘Muziki ni nguzo muhimu ya kampuni yetu, kwa hiyo Tigo Fiesta 2018 itadumisha asili yake ya kuvumbua na kukuza vipaji vya Kitanzania. Lengo letu kuu ni kukuza tasnia ya muziki na kutoa fursa za ajira kwa vijana na jamii yote kwa ujumla’ William alisema. Naye Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Gardner G. Habash alisema kuwa katika historia yake ya miaka 17, Tigo Fiesta imekuwa jukwaa la kukuza muziki wa nyumbani. ‘Tigo Fiesta inawapa fursa wasanii kuonesha uwezo wao na kuongeza idadi ya mashabiki ndani na nje ya nchi. Kuna maelfu ya mashabiki wanaohudhuria matamasha yenyewe au kufuatilia matukio kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,’ alisema.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) .

Mbali na kutoa burudani ya uhakika, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote pia itaibua fursa nyingi za kujiongezea kipato kwa wasanii pamoja na wakaazi wa maeneo mbali mbali yatakayoshuhudia shamrashamra za msimu huu.

Pia katika msimu huu wa burudani, Tigo inatoa tiketi za watu mashuhuri (VIP) za kuhudhuria Tigo Fiesta 2018 kwa wateja ambao watanunua vifurushi vya Tigo VIP Pack ambavyo vinawapa wateja huduma bora zaidi za sauti, SMS na data kuanzia TSH 30,000/-. Vile vile, wateja wote wa Tigo pia watapata nafasi ya kujishindia zawadi kem kem kama vile pesa taslim na simu janja kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta Chemsha Bongo ambapo watatakiwa kujibu maswali yanayohusu Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote.
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es salaam katika uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati). 

‘Wasanii wenyewe pamoja na jamii yote kwa ujumla katika mikoa 15 itakayotembelewa na msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote watapata fursa kubwa za kiuchumi zinazoendana na msimu wenyewe,’ William alisema. Wafanya biashara mbali mbali ikiwemo wamiliki wa hoteli, migawa, kumbi za starehe, mama niitilie, wauzaji wa nguo na wamiliki wa vyombo vya usafiri huongeza kipato kutokana na biashara zao kuchangamka kutokana na idadi kubwa ya wateja wanaohudhuria matamasha ya Tigo Fiesta.

Gardner aliongeza kuwa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote utajumuisha miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

CAF YATAJA WAAMUZI MECHI YA TANZANIA NA CAPE VERDE

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Mali kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Cape Verde na Tanzania katika Uwanja wa Estadio National  Oktoba 12,2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Boubou Traore akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Drissa Kamory Niabe, Mwamuzi msaidizi namba 2 Baba Yomboliba na Mwamuzi wa akiba Gaoussou Kane na Kamishna wa Mchezo anatokea G. Equatorial Tadeo Nsue Onva.

Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Djibouti

Mwamuzi wa katikati atakuwa Souleiman Ahmed Djama, na Mwamuzi msaidizi namba 1 Farhan Bogoreh Salime, Mwamuzi msaidizi namba 2 Rachid Waiss Bouraleh na Mwamuzi wa akiba Bilal Abdallah Ismael.

Kamishna wa mchezo anatokea Malawi Maxwell Mtonga, Mtathmini waamuzi anatokea Rwanda Michael Gasingwa.

KUELEKEA MICHEZO YA MAJESHI SANLAM LIFE INSURANCE YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA JESHI LA MAGEREZA

$
0
0
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Augustine Mboje(kushoto) akipokea vifaa vya michezo toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa SANLAM LIFE INSURANCE Bw. Khamis Suleiman,(wa tatu toka kulia) ni Meneja Uhusiano Mkuu wa SANLAM LIFE INSURANCE, Bw. Kileo Rishia.
Mkurugenzi Mkuu wa SANLAM LIFE INSURANCE Bw. Khamis Suleiman pamoja na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Augustine Mboje(kushoto) wakikagua vifaa vya michezo kabla ya makabidhiano rasmi, leo Septemba 18, 2018 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa SANLAM LIFE INSURANCE Bw. Khamis Suleiman (meza kuu) akizungumza na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Augustine Mboje (wa pili kushoto) pamoja na ujumbe kutoka Jeshi la Magereza katika Ofisi za SANLAM LIFE INSURANCE Makao Makuu, leo Septemba 18, 2018 jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Augustine Mboje akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa SANLAM LIFE INSURANCE Bw. Khamis Suleiman mara baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya michezo katika ofisi za SANLAM LIFE INSURANCE Makao Makuu, leo Septemba 18, 2018 jijini Dar es Salaam.(Picha na Jeshi la Magereza).

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKABIDHIWA KANDARASI YA KUJENGA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA EWURA DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio na wafanyakazi wengine wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa ndani ya ofisi za NHC Dodoma.
 Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na Wale wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dodoma wakikagua eneo la mradi. 
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio akikabidhiana nyaraka na Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Injinia Nyirabu Musira wakati viongozi walipokabidiana eneo la Ujenzi la Ofisi ya Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dodoma, Shirika la Nyumba limepewa kandarasi ya kujenga jengo hilo lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10.8 ambalo litakuwa makao makuu ya Mamlaka hiyo nchini. NHC imepewa dhamana ya kuusanifu, kujenga na kuusimamia mradi huo. 

WAZIRI KAMWELWE: SINA IMANI NA MHANDISI MSHAURI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ameuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora kujiridhisha kwa kuyapima tena madaraja na makalvati yaliyoanza kutengenezwa kwenye ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kama yanakidhi ubora na viwango kwa kuwa mchanga uliotumika haufai.

Waziri Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa hata eneo ambalo mkandarasi anasaga mawe kuna vumbi jingi kulinganisha na kokoto zinazozalishwa hii kitaalamu ina maanisha kwamba mwamba huo wa mawe ni dhaifu.

Ameyasema hayo katika kijiji  cha Ipole wilayani Sikonge wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo na kusema kuwa hana imani na mhandisi mshauri kutoka kampuni ya LEA International Ltd katika usimamizi wa mradi huu.

"Sijaridhishwa na madaraja na makalvati haya Mhandisi wa Mkoa kushirikiana na Mhandisi Mshauri na Mkandarasi mkayapime tena ubora kwenye Maabara ya Taifa na kama hayafai muyaondoe maramoja na kutengeneza mengine",amesema Waziri Mhandisi Kamwelwe

Amesisitiza kuwa fedha za kujengea barabara hiyo zimefedhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika  (AfDB) na tutalazimika kuzilipa hivyo ni lazima thamani ya fedha inaonekana katika mradi huu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International Bw. Sanjeev Gupta (kushoto) anayesimamia ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, wakati akikagua hatua za ujenzi wa barabara hiyo na kutoridhishwa na madaraja na makalvati yaliyotengenezwa katika mradi huo, mkoani Tabora.
Fundi Mchundo Bw. Fadhili Amiri, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa pili kushoto) kuhusu kazi anazozifanya  wakati alipokuwa akikagua hatua za ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua mchanga unaotumika kutengenezea madaraja na makalvati katika ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, na kutoridhishwa na ubora wake, mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International Bw. Sanjeev Gupta anayesimamia ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, wakati akikagua kokoto zitakazotumika katika mradi huo na kutoridhishwa nazo, mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa kwanza) akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAMOTA Bw. Abdallah Salim, kuhusu kukamilisha mradi huo kwa wakati, mara baada ya kukagua hatua za maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28, Mkoani Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

LUKUVI ALILIWA ZUMBA /SOGA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI BAINA YA WANANCHI NA MWEKEZAJI

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, ameingilia kati mgogoro wa ardhi kati ya kampuni ya Mohammed Enterprises na kijiji cha Zumba ,Mpiji Stesheni ,Soga na Kipangege huku akimuomba Waziri mwenye dhamana kutatua mgogoro huo.

Aidha ,amelazimika kuunda kamati ndogo ya watu 12 ,itakayofuatilia jambo hilo ili haki itendeke .

Akizungumza na wananchi hao ,Jumaa alisema, ifikie hatua ya wataalamu na viongozi wenye dhamana kukutana na wananchi ,kuwaeleza jitihada zinazochukuliwa na serikali kutatua malalamiko yao bila kukaa kimya .

"Tatizo hili nimelikuta ,katika kipindi changu ni miaka saba sasa ,2015 niliongea na waziri na kuja na kamati ya ardhi ,na kutolewa maelekezo mbalimbali lakini bahati mbaya ,wakati wa uchaguzi ule waziri husika hakuweza kufika "

"Mkuu wa wilaya ya Kibaha aliwahi kufika kuongea na wananchi ,na mkoa wa Pwani ulifikishiwa hatua zinazochukuliwa walitumwa wataalamu kufanya tathmini na kujua mapungufu ya ardhi ya wananchi wanayohitaji ." alisema Jumaa.

Jumaa alieleza ,tangu hapo hakuna taarifa ya hatua hizo zilipofikia lakini amejipanga kufuatilia suala hilo kwa kushirikiana na kamati iliyoundwa .

"Mh Lukuvi ni mwelewa na ana hekima , naamini atalitatua tatizo hili bila kuangalia upande wowote ,ili kuondoa dhana ya wananchi kuwa mwekezaji kaiweka serikali mfukoni " alifafanua Jumaa.


Hata hivyo ,Jumaa alikemea tabia inayofanywa na meneja wa mwekezaji huyo aitwae Mndeme kunyanyasa baadhi ya wananchi na wengine kupigwa na kupelekwa polisi bila hatia .
 Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ,akizungumza na wananchi kijiji cha Zumba kuhusiana na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na kampuni ya Mohammed Enterprises.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mpiji Stesheni ,Saidi Abdallah akizungumza katika mkutano na wananchi kuelezea mgogoro wa ardhi.
 (Picha na Mwamvua Mwinyi)

WATANZANIA WATEULIWA NA CAF KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI ZA KUFUZU AFCON

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini Tanzania kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 Cameroon kati ya Seychelles na South Africa utakaochezwa Uwanja wa Stade Linite Oktoba 16,2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Mfaume Ali Nassoro akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Ferdinand Chacha, Mwamuzi msaidizi namba 2 Alli Kinduru na Mwamuzi wa akiba Elly Sasii. Mtathmini waamuzi anatokea Uganda Ronnie Kalema na Kamishna wa mchezo anatokea France Yves, Jean-Baptiste Etheve. 

Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) limemteua Bwana Ahmed Idd Mgoyi kuwa kamishna wa mchezo wa Kufuzu kucheza AFCON 2019 Cameroon, mchezo ambao utazikutanisha Malawi na Cameroon mchezo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 
Kamuzu Stadium katika Mji wa Blantyre.


Naye Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathmini Waamuzi mchezo utakaowakutanisha Congo DR na Zimbabwe utakaochezwa Kinshasa Complexe OmniSports Stade Des Martyrs Oktoba 13,2018.

WAZIRI MHAGAMA AWAAGIZA WAJUMBE WA CWT KUTEKELEZA HOJA ZA CAG

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amewaagiza wajumbe wa baraza la chama cha walimu Tanzania kutekeleza hoja zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Hayo ameyasema hii leo wakati wa kikao cha dhararu kilichowakutanisha wajumbe hao kujadili hoja zote zilizotolewa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) katika taarifa yake ya mwaka 2016/2017.

Waziri Mhagama alieleza kuwa ripoti ya mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) imeelezea changamoto zilizokuwepo kwenye chama hapo awali ikiwemo masuala ya mapato na matumizi ya chama, mfumo wa uongozi na uwajibikaji, mikataba iliyoingiwa na chama ya uwekezaji, suala la utozaji ada kwa wananchana na mfumo wa sera ya malipo ya fedha.

“Wajumbe wa baraza hili mkishiriki kikamilifu katika kujadili na kufikia maamuzi ya pamoja ili kutimiza malengo ya chama na kutakuwa na utaratibu utakao saidia kuongeza uwazi na mshikamano miongoni mwa wanachama” alisisitiza Mhagama.

Aliongeza pia kwa kuyatekeleza hayo chama kitakuwa na utaratibu mzuri utakao heshimiwa na kila kiongozi wa chama na wanachama wote pamoja na namna bora ya kutunza na kutumia fedha za chama ili ziweze kutumika katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa manufaa ya wanachama wote.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipongezwa na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bi. Leah Ulaya (katikati) mara baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Kushoto ni Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Deus Seif.
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoke akizungumza wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG). (Wapili kutoka kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bibi. Leah Ulaya (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Walimu Wenye Ulemavu (CWT) Taifa, Mwl. Ulumbi Shani (katikati) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutoka mikoa ya Rukwa na Ruvuma mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho uliofanyika hii leo Jijini Dodoma.

VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi Kanda ya Dar es Salaam imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani zaidi ya sh.milioni 41 katika Chuo cha Ufundi Maalumu Yombo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga amesema kuwa vifaa hivyo vimekwenda kwa watu muhimu katika kuwaandalia maisha ya baadaye kwa vijana wenye ulemavy mbalimbali.

Amesema kuwa msaada huo sio mwisho kutokana na mahitaji ya Chuo hicho kutoa elimu kwa vijana wenye mahitaji maalum kwani serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda ambapo vijana wanaweza kuunda vikundi na kuanzisha viwanda na kuweza kujipatia kipato na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Dkt Mwesiga amesema vifaa hivyo lazima vitumike kwa malengo ualiyokusudia ikiwa ni kujifunzia wanafunzi hao na kupata ujuzi wanaohitaji pamoja na kanda ya VETA kufatilia vifaa hivyo na maendeleo ya wanafunzi katika Chuo cha Yombo.

“Nia ya serikali ni kuona watu wenye mahitaji maalumu wanapata ujuzi kutokana na ulemavu wao na hakuna kuachwa nyuma jamii hiyo na wala kubaguliwa kwa kuwakosesha elimu”amesema Dkt. Mwesiga.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam Florence Kapinga amesema kuwa maombi ya Chuo cha Yombo yalikuwa yanamkosesha usingizi kwa kutambua vijana waliopo wana mahitaji maalum ikilinganishwa na maombi mengine.

Picha ya Pamoja Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga pamoja Kanda ya VETA Dar es Salaam,Watumishi wa Chuo pamoja na wanfaunzi.
 Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga akizungumza wakati hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Maalum Yombo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Maalum Yombo, Mariam Chilangwa akitoa historia fupi ya chuo hicho katika hafla iliyofanyika Chuoni hapo o jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga akikabidhi moja kifaa cha msaada kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufiundi Maalum Yombo, Mariam Chilangwa katika hafla iliyofanyika Chuo hapo , jijini Dar es Salaam.

ZOEZI LA UZIBAJI MIVUJO TABATA LAKAMILIKA KWA ASILIMI 85- MHANDISI ARON

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamefunga zoezi la  siku tatu la uzibaji wa mivujo ya mabomba katika Mkoa wa Tabata na kufanikisha  kuziba mivujo 298 iliyokuwa sugu na mipya ikiwa ni mikakati ya siku 100 ya Dawasa mpya kuhakikisha wanaondoa tatizo hilo..

Zoezi hilo lililoanzia  Mkoa wa Dar es Salaam  katika maeneo ya Tabata zoezi limedumu kwa muda wa siku tatu na kufanikiwa kwa asilimia 85 kwenye kata zote 13.


Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa, zoezi hilo imeenda vizuri kwa mafundi wote kufanya kazi kwa ufanisi mzuri na kufanikisha kuziba mivujo yote 298 kwa asilimia 85 na tayari wameshakabidhi kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata.

Aron amesema,Tabata kulikuwa na changamoto kubwa sana ya Mivujo na wamefanikiwa kwa asilimia kubwa na kwa sasa wanahamia Ubungo kuanzia wiki ijayo na kuwataka mafundi waliofanikisha kuondoa changamoto ya mivujo Tabata kuwa ana imani watafanya kazi nzuri.


"Nina imani tunahamia Ubungo mafundi mtafanya kazi nzuri kama ya Tabata na hilo sina shaka, kwa takwimu Tabata kulikuwa kunaongoza kwa mivujo na hilo linatokana na kuwa na miundo mbinu chakavu ya muda nrefu na tumekabidhi kwa meneja wa Dawasa Tabata na tayari tumempa maelekezo kuwa mivujo yote itatakiwa kufanyika matengenezo ndani ya masaa 6,"amesema Aron.

Aliongezea na kusema, Dawasa mpya imeweka mikakati zaidi ya kuboresha miundo mbinu na  kuhakikisha ndani ya miaka mitatu miundo mbinu hiyo inabadilishwa ili wananchi wasikose maji na idara ya uzalishaji na usambazaji maji itahakikisha katika kipindi chote hicho watakuwa wanasimamia miundo mbinu hiyo ili kuondokana na uvujaji wa maji.

Akiongezea, Aron amewasihi wananchi kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapoona maji yanavuja kupitia namba yao ambayo haina malipo pia hata watakapowaona mafundi wa Dawasa wawape taarifa ili wakarekebishe eneo hilo.

Meneja wa Dawasa Tabata Victoria Masele baada ya kukamilika katika kata zake zote 13 za Tabata amesema kuwa, anatambua eneo la Tabata lilikuwa limeathirika sana kwa mivujo kwani miundo mbinu yake ni ya zamani toka enzi ya Mchina na ilikaa muda mrefu bila maji  kwahiyo zoezi hili limesaidia kuondoka kero kwa asilimia 85.

Victoria amesema kuwa, tatizo la mivujo linatokana na mtandao wa maji kuwa mdogo na maji yanakuja kwa kasi kubwa sana yanapelekea kupasuka kwa mabomba ya maji  hasa katika maeneo ya Kimanga na Segerea.

"Mafundi wamefanya kazi kubwa sana wakifanikiwa kuziba mivujo 298  sawa na asilimia 85 na hiyo ambayo imebaki itaendelea kushughulikiwa kwani tayari mafundi wangu niimeshawaambia wahakikishe mivujo mipya na ile ya zamani irekebishwe ndani ya miezi 6,"amesema Victoria.

Amesema baada ya zoezi hili kukamilika anaamini uuzaji wa maji kwa wateja wake  utaongezeka  na kuchochea ongezeko la mapato kwenye Mamlaka pamoja na kuongeza wateja wapya  ambapo ndani ya siku 100 watarajia wateja 4000 kujiunga kwenye mtandao wao.

Meneja wa Usambazaji maji Mhandisi Paschael Fumbuka amesema zoezi hili ni kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu ya maji kwa kuzuia upotevu wa maji kitu ambacho kinaathiri biashara ya maji maana kila tone la maji linahesabiwa na kwa sasa wanahamia Mkoa wa Ubungo mwishoni mwa wiki hii.

Fumbuka ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Dawasa kuwabaini watu wanaochafua miundo mbinu yao ikiwamo kutiririsha maji taka na hatua za kisheria zitachukuliwa juu yao.

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph akizungumza na mafundi waliofanikisha kurekebisha kwa mivujo 298 katika Mkoa wa Tabata uliofanyika kwa siku tatu na kuwapongeza kwa kazi kubwa sana  walioifanya na kuwataka wajipange kwa Mkoa wa Ubungo.
Meneja wa Dawasa Tabata Victoria Masele (kulia) akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Aron Joseph na kuahidi kurekebisha mivujo yote ndani ya saa 6 kama alivyoagizwa baada ya kufanikisha kwa zoezi la uzibaji mivujo ndani ya Mkoa wake wa Tabata.

PROFESA MBARAWA AMEWATAKA WAKAZI WAISHIO KWENYE MIUNDOMBINU YA MAJI KUONDOKA

$
0
0
Waziri wa maji na umwaguliaji profesa Makame Mbarawa

Na Agness Francis,Globu ya jamii.
WAZIRI wa maji na umwaguliaji profesa Makame Mbarawa amewata wakazi waliojenga na wanaoishi Katika miundombinu ya mabomba ya maji hapa nchini kuondoka maramoja.

Profesa Mabrawa amesema hivyo ili kuweka usalama kwa wananchi hao kuondokana na adha ya kuhatarisha maisha ya wananchi hao.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari  ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuwa  mwananchi atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua  kwa  kuwaondoa wote waliojenga katika miundo mbinu hiyo, kwa kuwa sheria iko wazi na inajulikana

Aidha Waziri Mbarawa amesema kuwa  serikali ya Tanzania kupitia shirika LA maji safi na maji taka  Dawasa itahakikisha zoezi hilo linafanikiwa katika kuhakikisha wananchi hao wanafata maagizo hayo bila kukiuka.

Hata hivyo Mbarawa amewataka wananchi wote  kuwa waangalifu katika kuzuia upotevu wa maji ambapo amesema mpaka kufika 2020  tatizo a maji  litakwisha na huduma ya upatikaniani wa maji itainhezeka u kuwafikia wanachi wote wa mijini na vijijini.

Ambapo ameahidi kubadilisha utendaji wa kazi hasa katika utekelezwaji wa wakandarasi  wasio na vigezo vya ufanyaji kazi kwa ufanisi pamoja na wasimamizi kulega lega katika usimamizi wa majukumu yao.

Vile vile profesa Mbarawa amezungumzia  utungwaji wa  Sheria Mpya ya maji kuwa italeta mapinduzi ya upatukanaji wa huduma ya maji nchini kote kwa urahisi.

"Wanachi wote wanaruhusiwa kutoa maoni  yao kuhusu sheria  hiyo mpya itakayotungwa,kwa Kuwa sheria hiyo haitakuwa ni yakwangu bali ni ya sisi wote"amesema profesa Mbarawa.

WATU WENYE UALBINO 35 WA MATAIFA YA ULAYA NA AFRIKA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Jumla ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi 35 kutoka mataifa ya Ulaya na Afrika wanatarajia kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Septemba 21,2018 kwa ajili ya kuongeza uelewa wa jamii juu ya uwezo walio nao watu wenye ualbino katika jamii kufanya mbalimbali ya kijamii. 
Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumanne Septemba 18,2018 katika Ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Josephat Torner Foundation Europe,bwana Josephat Torner amesema lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro ni kuamsha uelewa wa jamii kuondokana na imani potofu za kishirikina juu ya watu wenye ualbino. 
“Safari hii ya kupanda Mlima Kilimanjaro yenye Kauli mbiu ya “Vunja ukimya,Linda watu wenye ualbino” pia inalenga kutangaza utalii wa nchi ya Tanzania,tunaamini kuwa nchi yetu ya Tanzania itanufaika kwa kuendelea kuutangaza mlima wetu kimataifa na kupata fedha za kigeni”,alieleza Torner. 
Aidha alisema baada ya shughuli ya kupanda mlima kwa muda wa siku nane, washiriki watatembelea mbuga ya wanyama Serengeti ili kujionea wanyama mbalimbali na mandhari nzuri ya mbuga hiyo. 
“Pamoja na lengo kuu la kujenga uelewa wa jamii juu ya watu wenye ualbino,pia tutaitumia shughuli hii kama sehemu ya ugemaji rasilimali ambapo kila mshiriki atachangia dola za Kimarekani 1,000 na fedha hizo zitatumika katika kuwahudumia watoto wenye ualbino kwenye masuala ya elimu hasa wanaotoka katika kaya maskini”,alisema Torner. 
“Nitoe wito kwa Umoja wa nchi za Afrika (AU) kuchukua hatua madhubuti kukomesha hali ya mauaji ya watu wenye ualbino yanayoendelea hivi sasa katika baadhi ya nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwa ni pamoja na Malawi,Msumbiji,Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Somali,Ghana,Rwanda na nchi nyinginezo”,aliongeza. 
Alitumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kuendelea na moyo wa kujitoa katika kuripoti matukio ya unyanyasaji,mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino na watu wenye ulemavu kwa ujumla. 
Taasisi ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) yenye makao makuu nchini Uholanzi na nchini Tanzania ofisi zake zipo jijini Mwanza ina njozi ya kutengeneza jamii yenye amani inayojumuisha watu wote ambapo watu wenye ualbino watafurahia maisha yao bila hofu katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Josephat Torner Foundation Europe,bwana Josephat Torner akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Vedastus Wilfred,kulia ni Maria Msuva 
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Josephat Torner Foundation Europe akielezea safari ya watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka mataifa mbalimbali duniani kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Septemba 21,2018 - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kushoto ni kijana Vedastus Wilfred mmoja wa washiriki wa upandaji Mlima Kilimanjaro akizungumza na waandishi wa habari leo.Wa Kwanza kulia ni Maria Msuva ambaye naye atapanda Mlima Kilimanjaro. Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

BODABODA, BAJAJI, TAXI KUSHINDWA KULETA HESABU NA KUKUSABABISHIA HASARA, NINI UFANYE KISHERIA.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub
Sio siri wengi waliowekeza kwenye biashara ya bajaji,bodaboda,taxi na hata daladala wamejuta kufanya hivyo. Wengi wameingia hasara na mambo hayakuwa kama walivyotarajia. Na niamini,waliomo leo kwenye hiyo biashara sio wale walioanza, bali ni wageni kwani walioanza walishaacha siku nyingi kuepuka kichwa kuuma.
Sasa yafaa tuzingatie mambo kadhaa ya kisheria ili kuona  namna gani unaweza kudhibiti biashara hii na hata ikikushinda isikushinde ukiwa mwenye kupoteza(looser).Katika kufanya hivyo tutizama mambo mawili, kwanza Mkataba, na pili Udhamini.
1.MKATABA.
Eneo la mkataba au makubaliano ni eneo muhimu  sana tangu unapowaza biashara hii. Mkataba ndiyo tafsiri ya uhusiano wako na huyo unayemkabidhi chombo. Popote, na wakati wowote mtakapotofautiana  rejea yenu ya kwanza ni mkataba. Mkataba ndio biashara yenyewe, na hivyo uimara wa mkataba utatambulisha uimara wa biashara, halikadhalika udhaifu wa mkataba huenda ukawa ndio udhaifu wa biashara.
Na uimara wa mkataba ni sehemu kuu mbili. Kwanza mfumo, na pili maudhui/vipengele. Mfumo ni lazima mkataba uwe katika muundo mzuri wa sheria. Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba, Sura ya 345 kinasema mkataba  mzuri ni ule ambao umefanywa na watu stahili kufanya mkataba(partie’s competence), wenye hiari huru(free consent), wakibadilishana vitu halali(lawful object and consideration ), na kile wanachokubaliana kiwe hakijakatazwa na sheria nyingine yoyote. Kwahiyo mfumo mzuri wa mkataba utategemea haya.                 KUSOMA ZAIDI NENDA sheriayakub.blogspot.com



JKT yatekeleza kwa vitendo ujenzi wa uchumi wa Viwanda - Dkt Hussein Mwinyi

Delegation from African Development Bank visits Bank of Tanzania

$
0
0
The delegation from African Development Bank’s (AFDB) has paid a courtesy call to the Bank of Tanzania Office in Dar es Salaam for official engagements pertaining to AFDB’s projects supervision in the country.
The delegation was led by AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda. While in BOT, they met with the Governor of the Bank of Tanzania, Prof. Florens Luoga.
 Tanzania Agricultural Development Bank, Acting Managing Director, Japhet Justine (right) chats with the Governor of the Bank of Tanzania, Prof. Florens Luoga (left) when he accompanied the visiting delegation from African Development Bank (not in picture) to the Governor’s Office in Dar es Salaam.
 The Governor of the Bank of Tanzania, Prof. Florens Luoga (left) welcomes the visiting delegation from African Development Bank’s (AFDB), who paid a courtesy call at his Office in Dar es Salaam. Right is AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda, Senior Investment Officer, Trade Finance, Mkola Tambwe-Mlima (second right) and Principal Investment Officer, Maureen Katuvesirauina (centre). The delegation was accompanied by Tanzania Agricultural Development Bank, Acting Managing Director, Japhet Justine (second left).
 The Governor of the Bank of Tanzania, Prof. Florens Luoga (left) chats with members of the visiting delegation from African Development Bank’s (AFDB), who paid a courtesy call at Governor’s Office in Dar es Salaam. Listening are AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda (right), Senior Investment Officer, Trade Finance, Mkola Tambwe-Mlima (second right) and Principal Investment Officer, Maureen Katuvesirauina (centre). The delegation was accompanied by Tanzania Agricultural Development Bank, Acting Managing Director, Japhet Justine (second left).
 The Governor of the Bank of Tanzania, Prof. Florens Luoga (centre) in a group picture members of the visiting delegation from African Development Bank.
The Governor of the Bank of Tanzania, Prof. Florens Luoga (second right) gestures  while talking with members of the visiting delegation from African Development Bank’s (AFDB), who paid a courtesy call at Governor’s Office in Dar es Salaam. Listening are AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda (right), Senior Investment Officer, Trade Finance, Mkola Tambwe-Mlima (second left) and Principal Investment Officer, Maureen Katuvesirauina (left). The delegation was accompanied by Tanzania Agricultural Development Bank, Acting Managing Director, Japhet Justine (centre).
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images