Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live

SPIDI YA KUPITA KATIKA BARABARA ZA JUU (FLYOVER) TAZARA NI 40 TU, KUTEMBEA KWA MIGUU, BODABODA NA BAISKELI MARUFUKU

$
0
0
 Magari yakipita katika barabara za juu (flyover) iliyopo eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam ambapo  spidi ni  Km 40 kwa saa tu kama inavyoonekana katika picha. Pia waenda kwa miguu na waendesha vyombo vya magurudumu mawili kama vile baiskeli na pikipiki na maguta nia marufuku.
 Magari yakipita katika barabara za juu (flyover) iliyopo Tazara jijini Dar es Salaam wakati wa usiku.
 Magari yakipita katika barabara za juu (flyover) iliyopo Tazara jijini Dar es Salaam wakati wa usiku. Bustani nzuri inaandaliwa sehemu hiyo ya katikati
Magari yakipita katika barabara za juu (flyover) iliyopo Tazara jijini Dar es Salaam wakati wa usiku. Bustani nzuri inaandaliwa sehemu hiyo ya katikati

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA NA TTB WATANGAZA KUANZA RASMI KWA SAFARI ZA AIR TANZANIA MJINI MUMBAI

$
0
0
Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania na Shirika la Ndege Tanzania umeandaa Maonesho Maalum ya Utalii na kutambulisha rasmi kuanza kwa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania zitakazofanyika Mjini Mumbai nchini humo kuanzia mwezi Novemba, 2018. 
 Maonesho hayo ambayo yatafanyika kwenye miji mikubwa mitatau ya India yaani New Delhi, Ahmedabad na Mumbai yanalenga kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nnchini. 
 Akizungumza wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Hoteli ya Roseate, Aerocity jijini New Delhi, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda alisema kuwa anaona fahari kubwa kushiriki maonesho hayo muhimu kwa Tanzania na India.
Alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi kuanza wa safari za kwanza za ndege ya shirika la ndege la Tanzania mjini Mumbai. Balozi Luvanda alisema kuwa safari za ndege hiyo nchini India ni fahari kubwa kwa Tanzania kutokana na ukweli kwamba nchi hizi mbili zina mahusiano ya kihistoria kwani mbali na kuunganishwa na Bahari ya Hindi, Tanzania na India ni marafiki na zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja mbalimbali zikiwemo biashara, utamaduni na mawasiliano ya mtu mmoja mmoja. 
 Mhe. Balozi Luvanda alisisitiza kuwa, safari za ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania nchini India hususan katika mji wa Mumbai zitaimarisha sekta ya utalii nchini kwa kuongeza idadai ya watalii kutoka nchini humo ambao kwa sasa takribani watalii 40,000 kutoka nchini humo wanatembelea Tanzania kwa mwaka. 
 Pia zitarahisisha safari za wanafunzi wa kitanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali vya India ambao idadi yao imeongezeka na kufikia 2500 kwa mwaka. 
 “Ninayo furaha kubwa kuwajulisha kuwa shirika letu la ndege yaani Air Tanzania limefufuka. Na kuthibitisha hilo Shirika litaanza safari zake mjini Mumbai mwezi Novemba, 2018. Nawaomba msisite kutumia ndege yetu kwa safari zenu za utalii, biashara hata kwenda kusalimia ndugu zenu waliopo Tanzania na wale waliopo Tanzania kuja kusalimia ndugu huku India” alisisitiza Balozi Luvanda. 
 Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wageni walioshiriki maonesho hayo ushirikiano, amani na usalama pale watakapokuwa Tanzania na kwamba Tanzania ni chaguo sahihi kwa utalii na wasisite kuja kwa shughuli mbalimbali za manufaa kwa nchi hizi mbili.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akizungumza wakati wa maonesho maalum ya utalii yaliyofanyika  katika Hoteli ya Roseate, Aerocity jijini New Delhi, India tarehe 17 Septemba, 2018. Mhe. Balozi Luvanda pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kutangaza kuanza rasmi kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania mjini Mumbai mwezi Novemba 2018. maonesho hayo yatafanyika kwenye miji mingine miwili ya India ambayo ni Ahmedabad na Mumbai.
Mhe. Balozi Luvanda akitangaza rasmi kuanza kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania nchini India huku  picha ya Ndege ya Shirika hilo aina ya Dreamliner ikionekana. Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Bi. Devotha  Mdachi ambaye yupo nchini India kushiriki maonesho hayo aliyoshiriki kuandaa anaonekana akichukua kumbukumbu ya tukio hilo
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devotha Mdachi naye akizungumza wakati wa maonesho yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Bodi hiyo.

MWILI WA MHANDIRI WA CHUO KIKUU DKT MISANYA BINGI WAAGWA NA KUSAFIRISHWA DODOMA KWA MAZISHI

$
0
0
MWILI wa aliyekuwa mtangazaji mahiri nchini na Mhadhiri wa Shule ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) iliyo chini ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi (47) umeagwa leo katika Kanisa Katoliki la Makongo Juu liliopo Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Miuji jijini Dodoma kwa ajili ya mazishi siku ya kesho.

Dkt Misanya Bingi alifariki dunia siku Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wa uhai wake alifanya kazi kwenye kituo cha Radio One ambapo alitangaza vipindi mbalimbali.

Hadi umauti unamkuta alikuwa akifundisha SJMC, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. na kabla ya hapo Misanya Bingi alikuwa mtangazaji kwenye kituo cha Radio One mwaka 1996.
Misa ikiendelea

Familia ya aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi wakiaga mwili wa mpendwa wao.



Ndugu, marafiki na jamaa wakitoa heshima zao za mwisho kwenye jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika kanisa Katoliki la Makongo Juu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi mara baada ya kuagwa katika kanisa Katoliki la Makongo Juu jijini Dar es Salaam.
Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi likiondoka kanisani mara baada ya kuagwa katika kanisa Katoliki la Makongo Juu jijini Dar es Salaam.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 18.09.2018

HABARI KUTOKA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK MAREKANI LEO

RELI TV: KUMEKUCHAA..TAZAMA KIPANDE CHA VIDEO KIKIONESHA UTANDIKAJI WA RELI,HISTORIA IKIANDIKWA TANZANIA

WAZIRI LUGOLA AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA YAKE, AWATAKA WACHAPE KAZI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na watumishi wa Wizara yake (hawapo pichani), kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi. Lugola aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii pamoja na changamoto zote zinazowakabili na atashirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), wanatatua changamoto za watumishi hao. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Veta, jijini Dodoma, leo.
Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo (mstari wa mbele) wakiwa na watumishi wengine wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati alipokua akizungumza na watumishi hao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza wizara hiyo. Katika hotuba yake, Lugola aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, pia aliwahidi watumishi hao atashirikiana na Katibu Mkuu kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utendaji wao. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha veta, jijini Dodoma, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akiandika mafanikio na changamoto zilizokuwa zinatolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Issa Ng’imba (kulia), katika mkutano wa watumishi wa Wizara hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima na kushoto ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serkali na Afya (Tughe), tawi la Wizara, Obeid Mbaga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu alipokua anawasili katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KUMBUKUMBU YA MIAKA MITANO YA MAMA FORTUNATA JOSEPH MSOKA

$
0
0
MPAKA TUTAKAPOKUTANA TENA KWENYE MAHALI PENYE ENZI NA UTUKUFU


 Mama Fortunata Joseph Msoka; tunakumbuka muda wote tulipokuwa nawe tukifurahi pamoja. Tunatamani Mungu angetupa upendeleo ukarudi hata kwa muda tu tukakaa na kuzungumza kama ulivyokuwa ukifanya; ukitufundisha mema, kushika Imani na kuwapenda ndugu na marafiki. 

Kwa hakika ulikuwa mtu pekee sana katika maisha yetu sisi watoto wako. 

Ni miaka mitano sasa lakini bado hatujaamini kweli umeondoka kwenye maisha yetu. Kila tukikuita hauitiki, tukija nyumbani haupo; ni ukweli ambao ni mchungu kumeza na maumivu yasiyoisha. Daima utadumu kwenye mioyo yetu watoto wako Paul na Constatine Msoka, Jackiline na Rose Mdami. 

Wajukuu wamekosa wa kumtania wamebaki kulibeba jina lako kwenye nyoyo zao. Hakika upendo wako hauta sahaulika kwa watu wote ulioshi nao; majirani, marafiki, WAWATA Parokia ya Ukonga na wanafunzi wako. 
Tunasema Buriani uendelee kulala usingizi wa Amani na Mungu Mwenyezi akaitulize roho yako na ya Baba yetu mahali pema Mbingun - Amina 

 Ufunuo 21:4 “ naye atafuta kila chozi katika macho yao wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena, kwakuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 19, 2018

KAMWELWE AZINDUA RASMI KAZI YA UTANDIKAJI RELI YA KISASA SOGA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (aliyeketi kushoto) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyechuchumaa) wakizindua kazi ya kutandika reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga, Pwani. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati) akikagua kipande kilichotandikwa reli ya kisasa ya SGR, Soga mkoani Pwani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa tatu kulia) akipata maelezo ya namna ya kutengeneza mataruma ya reli ya kisasa ya SGR kwenye kIiwanda cha Soga, Pwani. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa na wa kawanza kushoto ni Farid Munir Abdallah, Mhandisi Mzalishaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa nne kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) namna kazi ya utandikaji reli ya kisasa ya SGR inavyofanyika kwenye eneo la Soga mkoa wa Pwani 
Mmoja wa mafundi wakiendelea na kazi ya kutengeneza mataruma ya kujengea reli ya kisasa ya SGR kwenye iwanda cha Soga kilichopo mkoa wa Pwani


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua rasmi kazi ya utandikaji wa reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga lililopo mkoani Pwani ambapo reli hiyo inajengwa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa umbali wa kilomita 300 na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa.

Kamwelwe amesema kuwa reli hiyo yenye jumla ya kilomita 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ni kwa ajili ya njia ya reli ambayo itakuwa na umbali wa kilomita 205 na kilomita 95 ni kwa ajili ya reli kupishana ambapo reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo kiasi cha tani milioni 17,000 kwa mwaka ambapo nchi yetu imeingia mkataba wa kujenga reli hiyo na kampuni ya Yapi Merkezi ya kutoka nchini Uturuki na kusimamiwa na mshauri mwelekezi wa kutoka nchini Japan kwa kushirikiana na kampuni ya kizalendo ya hapa nchini kwetu. Reli hiyo itaendeshwa kwa kutumia umeme na itakuwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa.

Ameongeza kuwa Serikali inazalisha mataruma kwenye kiwanda chake yenyewe kilichopo Soga mkoa wa Pwani na vifaa vingine vya ujenzi wa reli hiyo kama vile sementi, mchanga na kokoto vyote vinapatikana hapa nchini. Amefafanua kuwa Serikali iliagiza reli peke yake kutoka nchini Japan ambapo kiasi cha tani 7,250 ziliingizwa nchini katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo reli hizo zitatumika kujenga reli hiyo ya kisasa ya SGR kwa ukubwa wa kilomita 60. Amesema kuwa itafika siku ambapo nchi itachimba chuma kutoka kwenye mgodi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga kwa ajili ya kujenga reli ya kisasa ya SGR badala ya kuendelea kuagiza reli kutoka nje ya nchi

Serikali yatoa muda wa siku 43 kumalizwa kwa ujenzi wa barabara ya daraja la Nyerere

$
0
0
Serikali imekubali kuongeza muda wa siku 43 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya daraja la nyerere kiunganishi cha barabara ya Kivukoni Kibada wenye urefu wa kilomta mbili ikiwemo kukubaliana na hatua iliyochukuliwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF kumkata asilimia 0.01 mkandarasi wa kampuni ya China Railway construction engeneer Group katika malipo ya makubaliano ya ujenzi huo kutokana na uzembe wa kuchelewesha kukamilika kwa kazi ya ujenzi.

Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Ajira,vijana,sera bunge na wenye ulemavu) Mh Jenister Mhagama ameridhia wakandarasi hao kuongeza muda huo wa ujenzi kutokana na changamoto za kifusi ambacho awali kilishindikana kupatikana kutokana masuala kadhaa ikiwemo uharibifu wa mazingira katika eneo la Mbutu lilipo Kigamboni .

“Nimekubali ombi hilo kutokana na changamoto ya kifusi ambapo sasa kimepatiwa ufumbuzi na uongozi wa wilaya ya Kigamboni hivyo nataka katika muda huu niliuongeza barabara hii ikamilike haraka na wakazi wa kigamboni waweze kuondokana na changamoto hii ya barabara”alisema Mh Mhagama.

Mh Mhagama amesema kuwa barabara hiyo itakapokamilika itaweza kuongeza mapato zaidi kwa daraja na hivyo kukuza uchumi wa nchi kutokana na uwekezaji wa viwanda vingi katika eneo la kigamboni uliopo na unaoendelea kwa hivi sasa.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ndugu William Erio alimtaka mkandarasi kufanya kazi kulingana na mkataba na kwamba wataendelea kukata tozo ya adhabu ya kutokamilisha mradi kwa wakati na kwamba gharama zote zilizo nje ya mkataba hazitalipwa.

“Kama shirika tumeamua kumkata mkandarasi huyu kutokana na kushindwa kumaliza kazi kwa wakati kama ilivypangwa awali na kuwa nitahakikisha nafuatilia hatua kwa hatua hadi ujenzi huu ukamilike ndani ya muda uliongezwa”alisema Erio.

Pia Mkurugenzi huyo wa NSSF alisema kwa sasa shirika hilo litaweka mfumo wa utambuzi wa vyombo vya usafiri kutoka kwa wakala wa serikali ili kuhakikisha mapato ya daraja yanaongezeka kutokana na uhalisia wa tozo halisi ya magari na kuachana na mfumo wa utambuzi kwa kutumia na njia ya kuhisi kwa kutumia macho. Ambapo amesema kuwa mfumo huo utaunganishwa moja kwa moja na mamlaka ya mapato TRA ili kuhakikisha kila gari linatozwa tozo kulingana na thamani ya gari.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kigamboni wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana. 
 MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana.


Meneja Mradi wa Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) Jamal Mruma akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana, kushoto ni MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (aliyevaa kitenge) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana .


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni mapema jana , kulia ni MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio.

 Eneo la kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni likiendelea na ujenzi wakatio Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni mapema jana .Picha na MAELEZO.





CCM YAAMUA KUWEKA HADHARANI SABABU ZA KUSHINDA UKONGA, MONDULI

$
0
0
*Yatangaza kuanzia mwaka huu vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 kupatiwa elimu ya ufundi bure

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewashukuru Watanzania kwa namna ambavyo wameendelea kukiamini huku kikieleza mambo makubwa yanayofanywa na Rais Dk.John Magufuli watu wanaona na ndio siri ya ushindi wao.

Pia kimetangaza kwamba kuanzia mwaka huu vijana wenye kuanzia umri wa miaka 18 hadi miaka 35 watapatiwa elimu ya ufundi bure na hiyo  ni fursa kwa vijana.Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Humphrey Polepole wakati anatoa sababu za ushindi wa kishindo ambao Chama hicho wameupata katika uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga ,Monduli pamoja na Kata zote ambazo uchaguzi mdogo umefanyika.

Kuhusu kuaminiwa Polepole amesema kutokana na mambo makubwa ambayo yanafanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais Dk.John Magufuli wananchi wanaona na ndio maana kimeendelea kuaminika na kupata ushindi wa kishindo"Yanayofanyika ndani ya nchi yetu watu wanaona.Tumeshinda Jimbo la Ukonga na Monduli.Tumeshinda Kata 23 na kati ya hizo 12 tumepita bila kupingwa.

"Siri ya kuendelea kuaminika na kushinda chaguzi ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM chini ya uongozi madhubuti wa Rais.Dk.John Magufuli," amesema Polepole.Amefafanua kwamba unapozungumzia kupita bila kupingwa kuna sababu mbalimbali na kwamba uchaguzi unasimamiwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na hasa sheria za uchaguzi.

"Hivyo wanaoshiriki chaguzi wanatakiwa kuzingatia sheria na taratibu za uchaguzi na kinyume na hapo unapoteza sifa," amesema.Akifafanua zaidi kuwa wanaojiita wapinzani kwa sasa wamebaki na siasa za kubeza mazuri yanayofanyika.Polepole ameeleza pamoja na mambo makubwa yanayofanyika ya kimaendeleo CCM pia imetoa maagizo na maelekezo  kwa mawaziri kushughulika na shida za Watanzania.nakwamba ni marufuku kwa viongozi kujifungia maofisini badala yake watoke kwenda kutatua kero za watu huko waliko.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

NFRA YASISITIZA HAITONUNUA MAHINDI YASIYOKUWA NA UBORA

$
0
0

Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma


IKIWA msimu wa kununua mazao umeanza, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia  Zikankuba amewataka wakulima kuhakikisha wanazingatia ubora wa mahindi.


Aidha, amesema nchi inachakula cha kutosha na kusisitiza kuwa katika msimu wa kwanza wa ununuzi wa mahindi bei ya NFRA ni wastani wa Sh 380 hadi Sh 400 kwa kilo.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Dodoma, Zikankuba alisema NFRA haitaweza kununua mahindi mabovu na kusisitiza wakulima kuwa na mahindi yenye ubora ambayo yatawasaidia kupata masoko ya nje pia.

" Haiwezekani NFRA itumia fedha za Serikali kununua mahindi yasiyokidhi viwango vya ubora na machafu kutoka kwa wakulima. Hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha mahindi kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyokidhi vigezo vya soko..


Aliongeza: “Lazima chakula tunachonunua kizingatie ubora. Tunataka tubadilishe taswira ya NFRA kwa sababu awali kulikuwa na tatizo la chakula kuharibika kwa kipindi kifupi.”


Zikankuba alisema ili kuhakikisha mahindi ya wakulima yanaweza kukidhi viwango vinavyotakiwa NFRA tayari imekwishatoa elimu kwa wakulima kupitia vikundi na kwenye vyombo vya habari.Alibainisha kuwa baada ya elimu hiyo wakala umefanikiwa ambapo wakulima kutoka maeneo ya Makambako, Sumbawanga na Mpanda wameanza kuzalisha na kuuza mahindi yenye ubora kwa NFRA.

“Changamoto iliyopo ni kwa baadhi ya wakulima wachache ambao bado wamekuwa wagumu kubadilika na wale ambao wanaamini wakitumia nafasi zao wanaweza kuuza mahindi yasiyo na ubora,"Alisema kwa mkulima kuwa na mahindi yenye ubora unatoakiwa utasaidia katika kupata soko la NFRA, pia katika taasisi zingine zinazonunua nafaka hiyo za ndani na nje ya nchi.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia  Zikankuba.

DC SOPHIA KIZIGO AELEZEA SABABU ZA KUFANYA ZIARA KATIKA KATA ZOTE ZA WILAYA YA NAMTUMBO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Mfaume Kizigo ametoa ufafanuzi kuhusu ziara ambayo ameifanya katika wilaya zote za wilayani humo huku akieleza namna ambavyo imesaidia kusikia changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya huyo ni kwamba ziara hiyo  ilikua na malengo makubwa matatu  ambayo yalitofautiana kulingana na kata husika. Akizungumzia ziara hiyo leo amesema utofauti ulikuja kwasababu kuna kata ambazo alikuwa tayari  ameshazitembelea, hivyo ziara hiyo ilikua wakimpokea kwa mara ya pili.

Wakati kwa Kata zingine alikuwa akipokelewa kwa mara ya kwanza.Ametaja malengo ya  yake  ya ziara hiyo ni kwamba kwa kata ambazo ziara hiyo ni kwa mara ya kwanza,lengo namba moja ilikuwa kujitambulisha. Pia kuhamasisha uhifadhi huku akifafanua alikuwa ameambatana na  wakuu wa idara muhimu kama kilimo, ardhi, ufugaji na uvuvi, misitu, sheria,sanaa utamaduni na michezo pamoja na kamati yote ya ulinzi na usalama ya wilaya.

Wakuu wa idara za kilimo, ardhi, mifugo na OCD walipata nafasi ya kutoa somo fupi kuhusu uhifadhi. Kila mtaalamu kwa kitengo chake alieleza njia bora zaidi za kufanya shughuli mbalimbali bila kuathiri uhifadhi hasa wa mazingira na hifadhi za misitu tulizonazo.Ameongeza lengo la tatu lilikuwa kusikiliza kero na Changamoti za wananchi.

 "Kero karibu zote zilijibiwa palepale kwani wakuu wa idara zote na kamati ya ulinzi na usalama walikuwepo."Kwa kata ambazo nilikua nimekwenda kwa mara ya pili, lengo namba moja lilikua kuhamasisha uhifadhi na lengo namba mbili lilikua kujibu kero na changamoto za wananchi walizotoa katika mkutano uliopita ambazo hazikuwa zimetolewa majibu ya moja kwa moja.

" Lengo la tatu lilikua kusikiliza kero na changamoto nyingine za wananchi,"amefafanua.Ameeleza kuwa kuna kero ambazo zilitolewa majibu katika ziara iliyopita na kuna nyingine zilihitaji ufuatiliaji ikiwamo ya mgambo na wakulima wa korosho ambapo aliwapatia majibu.

Kuhusu mgambo Mkuu wa Wilaya Kizigo amesema wananchi wa Magazini katika kijiji cha Magazini walilalamika kwamba wao hawafanyiwi mafunzo ya mgambo hivyo kusababisha wakati wa kazi mbalimbali kama usimamizi wa mitihani wanakosa nafasi hizo. Majibu ndio hayo
 MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akiwasili kwenye moja ya kata wakati wa ziara yake alioyoifanya hivi karibuni wilayani humo,nana kutoa ufafanuzi kuhusu ziara hiyo ikiwemo kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo (wa tatu kulia) alipokuwa akizungumza nao kwenye moja ya mkutano wake wa hadhara,katika kuzisikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

BENKI KUU YATAKA FEDHA ZA NOTI,SARAFU ZIHESHIMIWE

$
0
0

*Yaonya wanaozichezea ,yataka ziheshimiwe na kila mmoja wetu

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imewataka Watanzania wote kuhakikisha wanatunza fedha zetu kwani ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu.

Pia fedha ni alama ambayo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwa mfano Bendera  ya Taifa. 

 Taarifa ya BoT kwa vyombo vya habar ambayo wameitoa leo inasema utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji."Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, kifungu cha 26, BoT ndiyo taasisi pekee yenye mamlaka ya kutoa noti na sarafu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," imesema taarifa hiyo.

 Pia imesema noti na sarafu hizo zina alama muhimu inayolitambulisha taifa la Tanzania ambayo ni nembo ya Bwana na Bibi. Imefafanua alama hiyo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwamfano Bendera 
ya Taifa.

Pia noti na sarafu zote zimetengenezwa kutoa thamani ya kisheria (legal 
tender) kama ilivyoandikwa juu ya noti au sarafu husika na pia Benki Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuharibu noti na sarafu.

Taarifa hiyo imefafanua kuhusu hilo kupitia kifungu cha  28 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006."Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi kuzitunza fedha zetu kwa kuwa ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu. 

"Vilevile, utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji," imesema taarifa hiyo ya BoT.Imesisitiza kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, kifungu cha 26, Benki Kuu ya Tanzania ndiyo taasisi pekee yenye mamlaka ya kutoa noti na sarafu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Pamoja na mambo mengine imesisitiza umuhimu wa alama hiyo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwamfano Bendera ya Taifa. Na kwamba Noti na sarafu zote zimetengenezwa kutoa thamani ya kisheria (legal tender) kama ilivyoandikwa juu ya noti au sarafu husika.

"Na pia Benki Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuharibu noti na sarafu (kifungu cha 28 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006) ," amesema.

RC MAKONDA AWATAHADHARISHA WANANCHI WA DAR KUHUSIANA NA UTAPELI WA NYUMBA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameutahadharisha umma wa jiji la Dar es salaam kuhusiana na utapeli wa nyumba hasa kwa baadhi ya watu kutumia hati wasizo na miliki nazo kuomba mikopo mikubwa katika benki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Makonda amesema "baadhi ya watu hukopa fedha na kuacha hati zao za nyumba kama bondi lakini wale walioachiwa hugeuka na kutumia hati hizo kwa kuomba mikopo mikubwa katika mabenki na wakishindwa kulipa watu wasiohusika na madeni hayo huusishwa hasa kwa nyumba zao kuuzwa" amesema Makonda. Sambamba na Makonda amempongeza Waziri ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi kwa kusimamia suala la hati za kidigitali ambazo huweza kutambua hati kieletroniki.

Aidha ameeleza kuwa wale wote wenye mikopo wasiyoielewa katika mabenki mbalimbali kuanzia jumatatu wakaripoti kwenye ofisi za wakuu wa Wilaya na baadaye Seeikali ya Mkoa itakutana benki zote 56 na kujadili suala hilo ambalo linaibia mabenki na kupoteza mali na haki za makazi kwa wananchi.

Pia amewataka Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam hasa wa Wilaya ya Kinondoni ambako kuna kesi zaidi ya 500 za watu kuuziwa nyumba zao bila kutokuwa na mikopo katika mabenki kutumia nafasi hiyo ili kuepuka kughudhibiwa na kufilisiwa mali zao na amewashauri wananchi kuwa makini kwa kutunza hati hizo.

Kuhusiana na uchaguzi wa marudio unaotarajia kufanyika kesho katika jimbo la Ukonga na kata 2 jijini humo Makonda amesema kuwa uchaguzi huo utakuwa wa amani kwani kamati ya ulinzi na usalama imejipanga vyema hivyo wananchi wasiwe na shaka wafuate taratibu na baada ya uchaguzi washangilie kwa amani bila fujo ili kulinda amani ya jiji ambalo ni kitovu cha biashara na utalii.

Wataalam wakutana ESRF kuzungumzia ukuaji wa miji Tanzania

$
0
0
Na Mwandishi wetu
IMEELEZWA kuwa katika mazingira ya sasa ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda ni lazima taifa litakuwa na mabadiliko katika makazi na kwamba miji mingi itachipuka.
Aidha serikali inapotekeleza mpango wake wa pili wa maendeleo  2016/17-2020/21 katika mpango wa muda mrefu wa maendeleo kwa lengo la kuwezesha mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu uwepo wa miji ni wa lazima.
Aidha mazingira duni ya maisha katika vijiji kunafanya watu kuhamia katika maeneo yenye shughuli mbalimbali na hivyo kukuza miji iliyopo.
Hayo yalisemwa na Dk Lorah Basolile Madete, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha kwenye mkutano wa mkutano wa 5 wa jukwaa la ukuaji wa miji Tanzania (Tanzania Urbanisation Laboratory - TULab) ulioambatana na uwasilishaji wa tafiti tatu zilizofanywa na TUlab kuanzia mwaka jana.
Pia alisema tofauti kubwa ya kipato iliyopo vijijini na mijini inafanya maeneo ya jirani na vijiji kubadilika na kuanza kuchukua muonekano wa miji.
“Ndio kusema ni lazima kujiandaa kwa mabadiliko hayo na kuwa na  mpangilio wa kudhibiti ukuaji wa miji, kinyume chake Tanzania haitaweza kuvuna faida katika uchumi, kijamii na kimazingira kama miji itakua ghafla bila mipango mathubuti” alisema Dk Madete.
Katika mkutano huo ilielezwa kuwa kudhibiti miji ni kitu muhimu ikiwa mataifa yanataka kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi na ustawi wa jamii.
Miji hiyo inatakiwa kupangwa na kukua kwa mujibu wa makubaliano ya dunia kama  yale ya Paris na maendeleo endelevu yaliyokubaliwa na Umoja wa Mataifa.
 Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),  Bw. Deodatus Sagamiko akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
 Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika Kusini akiwasilisha Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab)  na kuongoza majadiliano kuhusu athari za kisera katika tathmini ya kitaifa ya mabadiliko kuelekea miji (National Urbanization Transition Assessment -NUTA) wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Reshian W. Kanyatila akielezea masharti ya ushiriki katika shindano la utoaji huduma katika majiji.
 Mtafiti Msaidizi na Mratibu wa Miradi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Bw. Emmanuel Njavike (katikati) akiwasilisha waliyojadili katika kikundi kazi wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.

SHUKRANI KUTOKA ARUMERU

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro amewashukuru wananchi wote wa Wilaya ya Arumeru kwa kujitokeza kwa wingi wakati wa ziara ya Mbio za Mwenge Kitaifa 2018 ambapo Wilaya ya Arumeru ilipokea Mwenge Kuanzia  Tarehe 16/09/2018 na Kuukabidhi Kwa Wilaya ya ARUSHA Mjini Siku ya Jumanne tarehe 18/09/2018 .

Dc Muro Amewashukuru Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Arumeru pamoja na kuwashukuru Wakurugenzi, Watumishi wa Halmashauri Mbili Za Arusha Dc na Meru Dc ambazo ziko Wilaya ya Arumeru pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na Vyama Rafiki vya Siasa ambavyo Vilijitokeza na Kuunga Mkono mbio ZA Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao umezindua na Kuweka Mawe ya Msingi ya Miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 19 Kwa Mwaka 2018.

Dc Muro Mara ya Baada ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru Kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Daqarro Amewashukuru Sana Viongozi wa Mbio Za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambapo amesema Mbio ZA Mwenge wa Uhuru Kwa 2018 Zimekuwa tofauti kuliko miaka Mingine Kutokana na Umakini,Umahiri na Uweledi wa Wakimbiza Mwenge Wakiongozwa na Ndugu Charles Francis Kabeho ambao wamesaidia katika Kurudisha Heshima na thamani ya Mwenge wa Uhuru Kwa Kukagua na kutoa Maelekezo ambayo yamesaidia kuongeza umakini katika kusimamia Miradi ya Maendeleo pamoja na Fedha zinazotoka Serikali.

#ArumeruYetu #MwengeWetu #WakatiWetu

*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Arusha Tanzania *

19/09/2018
Pichani kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro

WAZIRI WA NISHATI ATAKA MITAMBO YOTE YA MADINI ITUMIE UMEME

$
0
0
Na Veronica Simba – Mara
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema Serikali kupitia Wizara anayoisimamia, imejipanga kuhakikisha wawekezaji wote katika sekta ya madini wanatumia umeme katika shughuli zao ili wazalishe kwa tija itakayowawezesha kulipa kodi stahiki kwa Taifa na hivyo kukuza uchumi wa nchi. 

Alitoa kauli hiyo, Septemba 18, 2018 mkoani Mara, wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa Adam Malima ofisini kwake, kabla ya kuanza ziara ya kazi katika Mkoa huo, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.

“Tunataka migodi izalishe kwa tija ili kusudi ilipe kodi, ushuru na tozo zote stahiki kwa Serikali hivyo kukuza uchumi wa nchi yetu.”

Kauli hiyo ya Waziri Kalemani, aliitoa kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa kuhusu kuupatia nishati ya umeme Mgodi wa Dhahabu wa Nyamongo uliopo mkoani humo; ambapo Waziri Kalemani alimhakikishia kuwa Wizara yake inakamilisha taratibu za kuunganisha umeme katika Mgodi huo ndani ya muda mfupi, baada ya mwekezaji huyo kukamilisha malipo.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika nyumba ya mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Nyakatende, Musoma Vijijini, ikiwa ni ishara ya uwashaji rasmi wa nishati hiyo katika eneo hilo. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Septemba 18, 2018 kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Mhandisi Emmanuel Kachewa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani humo, kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), alipowasili katika Mkoa huo kwa ajili ya ziara ya kazi Septemba 18, 2018.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bubombi, Wilaya ya Rorya mkoani Mara, muda mfupi kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Hafla hiyo ilifanyika Septemba 18, 2018.

Ziara ya kitabibu Wilayani Kondoa yazinduliwa

$
0
0
Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akihutubia kwenye uzinduzi wa ziara ya Madaktari Wauguzi kutoka taasisi binafsi ya Health Education Development (HEAD INC) ya watanzania waishio nchini Marekani ya kutoa huduma za kitabibu kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa. Dkt. Gwajima alitumia fursa hiyo kuwapongeza taasisi hiyo kwakuona umuhimu wa kuja nyumbani kutoa huduma za afya kwa watanzania wenzao. Dkt. Gwajima hakusita kuipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Idara ya Diaspora kwa kuwezesha kufanikisha Ziara ya Madaktari na Wauguzi hao kutoka Nchini Marekani ambapo inaonyesha namna mwitikio wa Watanzania waishio nje ya nchi katika kuchangia maendeleo nchini. Madaktari na Wauguzi hao watakuwa kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa siku nne (4) wakitoa huduma za Afya kwa wagonjwa mbalimbali. 
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makutta (wa kwanza kushoto), na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Anisa Mbega wakimsikiliza kwa makini Dkt. Gwajima alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa ziara ya Madaktari na Wauguzi kutoka (Head Inc).

Sehemu ya Watumishi kutoka wilaya ya Kondoa wakimsikiliza kwa makini Dkt. Gwajima alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Ziara ya Madaktari na wauguzi.

Viewing all 110026 articles
Browse latest View live


Latest Images