Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live

Tanzania Remix kuchukuriwa hatua za kisheria

0
0
 Naibu waziri wa Wizara ya UchukuziMhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa haabri jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelea eneo la viwanja vilivyonunuliwa na serikali kwaajili ya wananchi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege, Richard Mayongela akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kutembelea Viwanja vilivyopo Luhanga Kata ya Msongola Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam na kukubali bila kinyongo kutekeleza agizo la  Naibu waziri wa Wizara ya UchukuziMhandisi Atashasta mara baada ya kutoa agizo hilo.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TANZANIA Remix kuchukuliwa hatua za kisheria kulingana na mkataba unavyosema.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelea viwanja vya fidia vya wananchi Waliopisha upanuzi wa Uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.

 Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege  (TAA) Richard Mayongela amesema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Tanzania Remix na zitatekelezwa bila kuogopa.

 Pia amesema kuwa "Tanzania Remix tumieni wiki hii moja mliyopewa kwaaajili ya kutekeleza agizo hilo la sivyo mtachukuliwa hatua za kisheria bila kuogopwa"


Pia amewaomba wananchi wawe wavumilivu kwani haki ya Mtu haiwezi kupotea bure ili wananchi waweze kufurahia matunda yao.

 Kiwango cha uvumilivu kwa mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) umefikia mwisho na sheria zitachukuliwa.

TBL YAADHIMISHA SIKU YA UNYWAJI BIA KISTAARABU DUNIANI KWA VITENDO

0
0
KAMPUNI ya Tanzania Breweries Limited (TBL Group), chini ya kampuni mama ya ABInBev, mwishoni mwa wiki iliadhimisha siku ya Unywaji wa  Pombe Kistaarabu  diniani kwa kushiriki kampeni mbalimbali za kuhamashisha matumizi ya vinywaji vizuri kwenye jamii.

Mbali na uhamasishaji huo uliofanyika katika mikoa mbalimbali nchini ambako kampuni inaendesha biashara zake pia kampuni ilitoa vifaa vya kupima kiwango cha ulevi kwa madereva kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani.

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika hafla iliyofanika mwishoni mwa wiki,Afisa Mawasiliano wa TBL, Amanda Walter alisema kuwa  kupitia sera ya kampuni ya Smart Drinking Goals,siku zote itahakikisha inahamasisha matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kiafya na burudani na sio kuleta athari kwa jamii.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi (SACP), Fortunatus Muslim, (watatu kutoka kulia) akiongea wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupima ulevi kwa madereva vilivyotolewa na TBL Group katika maadhimisho ya Siku ya Unywaji bia kistaarabu,mwishoni mwa wiki, wengine pichani (wa nne kutoka kulia ) ni Afisa Mawasiliano wa TBL, Amanda Walter na Maofisa wengine kutoka Jeshi la Polisi. 3.Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda Walter akiongea wakati wa hafla hiyo. Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi (SACP), Fortunatus Muslim katika picha ya pamoja na askari waliohudhuria hafla hiyo pamoja na Afisa Mawasiliano wa TBL,Amanda Walter.

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAKABIDHIWA KUKU MKURANGA

0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii

MWENYEKITI  wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga mkoani Pwani Mariam Ulega  mwishoni mwa juma amekabidhi msaada wa kuku 4000 ambao watatolewa kwa wanawake wajasiriamali 400 ambao wamehudhuria mafunzo ya ujasiriamali.
 Akizungumza wakati akikabidhi kuku hao kwa wajasirimali ,amesema kuwa kwa hicho kidogo wakitumie katika kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla na amewataka wawe na ushirikiano ili wafiikie malengo yao.

Kwa upande wa baadhi ya akina mama hao wameshukuru kwa  kupewa msaada huo na kuahidi kuwatunza kuku hao na kueleza kuwa kuku hao watakuwa chanzo cha miradi mikubwa zaidi.

Akiongea na Globu ya Jamii baada ya Mama Ulega kukabidhi vifaranga hao, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya AKM Glitters Company Limited, Bi. Elizabeth Swai, amesema amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Jukwaa la wanawake la Mkuranga na kwamba kwamba kampuni yake itakuwa mstari wa mbele kusaidia wanawake hao elimu ya namna ya kuendesha ufugaji bora wa kuku.
Bi. Swai, ambaye kampuni yake ndiyo iliyodhamini msaada huo, ameeleza kuwa AKM Glitters ni kampuni iliyojizatiti kukuza ufugaji wa kuku na ukulima wa kisasa kwa njia ya uzalishaji bora na matunzo.
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza na wanajasiriamali kuhusu kuwatunza kuku waliopewa ili kujiongezea kipato.
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga,Mariam  Ulega  akiwakangua kuku kabla ya kuwakabidh wananchi walilaya hiyo kwajili ya kufunga iliwaweze kujikwamua kiuchumi.
 Mwenyekiti wa jukwaa la la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam  Ulega akiwakabidhi wananchi kuku 3000 kwa ajili ya kufunga ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza pato la Taifa, ambapo kila mwananchi alipewa kuku 10 (picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

MAANDALIZI YA UTANDIKAJI WA RELI KUFANYIKA JUMANNE HII, TAZAMA RELI ZIKISHUSHWA SOGA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 17.09.2018

CHAMA CHA MIELEKA KUFANYA UCHAGUZI WAKE OKTOBA 27, 2018

0
0


Baraza la mchezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi wa Viongozi wa Shirikisho la Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2018 katika ukumbi wa msasani Beach Club, jijini Dar es Salaam.

Fomu zimeanza  kutolewa katika Ofisi za Baraza na pia kupatikana katika tovuti ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz kuanzia tarehe leo tarehe 17 Septemba, 2018, ambapo mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 19 Oktoba, 2018.

Aidha, usaili utafanyika tarehe 26 Oktoba kuanzia saa 3:00 asubuhi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo siku inayofuata ha na mahali mtafahamishwa kabla ya kufika tarehe hizo.

Nafasi zinazogombewa ni; 
Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhasibu Mkuu


Afisa Habari na Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa












SIFA ZA WAGOMBEA;-.



.Awe mwanachama wa shirikisho la mieleka nchini (TAWF).


.Awe na umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.



.Asiwe amewahi kupatikana na kosa la jinai.


.Kwa nafasi ya Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Msaidizi, awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea pamoja na uwezo wa kuandika na kusoma kingereza na Kiswahili kwa ufasaha.


.Awe na akili timamu.



.Mhasibu Mkuu na Msaidizi awe na cheti cha uhasibu, stashahada au zaidi ya hapo. 


.Sifa za wajumbe wa kamati mbalimbali wawe na uzoefu wa mchezo wa mieleka, wanaojua sheria za mchezo wa mieleka au wawe wameshawahi kuwa viongozi katika ngazi ya vilabu, wilaya, mkoa na Taifa.
.Asiwe amewahi kucheza,kuongoza au kushiriki kwa namna yoyote ile mieleka ya kulipwa.

BMT linatoa wito kwa wenye nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo huu, kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi stahiki ili kuendeleza shirikisho pamoja na kuiletea sifa nchi. 

Fomu zilipiwe katika Akaunti ya Baraza kwa jina la National Sports Council Ac. No. 20401100013 na kuwasilishwa risiti iliyolipiwa Benki pamoja fomu zilizojazwa kwa usahihi.






Kwa wa rais na makamu wake 
Ada ya fomu ni sh. 50,000/= na kwa nafasi zingine zilizisalia 

Ada ya fomu itakuwa ni sh. 30,000/

WAZIRI MBARAWA AZINDUA MRADI WA MAJI WA KIWALANI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
*Awataka Dawasa wawaunganishie 
maji wananchi walipe kidogo kiodogo

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amezindua mradi wa maji wa Kiwalani  na kuwataka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) kuhakikisha wanawaunganishia wananchi wa eneo hilo maji kwa mkataba ili walipe kidogo kidogo kwakuwa serikali imetumia fedha nyingi sana kufanikisha mradi huona Malengo ya Serikali ni kuona watanzania wanapata maji kwa asilimia 90.


Amezungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliokuwa umekamilika tayari na wananchi wa Kiwalani wakianza kupata maji safi na salama kuitia vizimba vitano vilivyokuwa vimeshajengwa tayari.


Profesa Mbarawa amesema, kumalizika kwa mradi huu ni moja ya ahadi ya serikali ya kuhakikisha kila mwananchi na eneo la Kiwalani wana zaidi ya miaka 30 hawajawahi kuwa na maji safi ya Dawasa  na wamekuwa wanatumia  chumvi katika kipindi chote hicho.

Amesema Profesa Mbarawa, ukiachana na mradi huo mpaka sasa serikali bado ina miradi mingine ikiwamo mradi wa Bilioni  133.2 ambao ni mradi wa kutoka Benki ya dunia na maji yatakayozalishwa hapo yatapatikana maeneo ya Dar es Salaam na Bagamoyo.

Amesema, Mradi mwingine ni wa Usambazaji maji wa Kiluvya, Salasala, Kimara na Goba utakaogharimu Bil 74.46, huku akisisitiza zaidi katika miradi ukiwamo mradi wa maji taka wenye thamani ya Bil 156.64 ambao yote kwa amoja ikikamilika itahakikisha inaleta manufaa kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.

"kuna Visima 21 katika  mradi wa Kimbiji Mpera tayari vimeshakamilika  na kabla ya 2020 maji yatapatikana kwa maeneo yote ikiwamo Kigamboni ambapo kumekuwa na changamoto ya maji safi kwa muda mrefu sasa,".

Waziri Mbarawa ameeleza kuwa, anatambua kuna baadhi ya maeneo yana changamoto ya maji na baadhi ya maeneo hayo ni Gongo la Mboto, Pugu,Kinyerezi na maeneo ya karbu  na kwa namna Dawasa mpya inavyofanya kazi kwa kasi inaonesha changamoto ya maji itakuwa ni historia ndani ya Mkoa wa Dares Salaam na Pwani.

Amemalizia kwa kuwaasa wananchi kununua maji ya Dawasa yenye gharama nafuu  na kuchana kununua maji ya maboza wanayouziwa kwa ei kubwa tofauti na Dawasa anbao wanauza Unit moja sawa na  lita 1000 kwa sh 1664 na sasa kununua maji ktk magari umekwisha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi  na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa miradi yote itakapokamilika wakazi wa Dar es Salaam na Pwani watapata maji ya uhakika.

Luhemeja amesema kuwa, ndani ya siku 100 za Dawasa Mpya watahakikisha miradi inakamilika na mingine wakandarasi wakiingia kazini ili kufanikisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wote na wakitimiza hitaji la kuongeza wateja wapya 200,000 kutokana na miradi hiyo  ya maji.

Pamoja na hilo, Luhemeja amesema kuwa moja ya mkakati mwingine wa Dawasa  mya ni kuona wanaongeza ukusanyaji wa mapato kwa kufikia Bilioni 12 ikiwamo kuwafuatilia wale wote wenye madeni.


Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema kuwa mradi wa Kiwalani ni Km 13.32 ukiwa na vizimba vinane lakini mpaka sasa tayari wameshajenga vizimba vitano na karibuni watamalizia vitatu. na ukiwa umekamilika mwishoni  wa mwezi wa nane.

Amesema mradi huo mpaka sasa umeweza kuata Wateja wapya 450  na waliounganishwa ni  246 ila wakati wa ujenzi wa mradi huu waliata Changamoto kubwa sana kwa kuwa eneo hilo lina mkondo wa maji  wakati wa umewakaji mitaro mitaro 

Amemalizia kwa kusema mradi huo una awamu tatu, na tayari awamu ya kwanza na ya pili umekamilika kwa  asilimia 100 limekamilika. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa (wapili kushoto) kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah  Kaluwa (wakwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa wakifungua  mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, kuzungumza  wananchi wa Kiwalani  Bom Bom leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame  Mbarawa, (wapili kushoto), akionyeshwa ramani ya mradi wa maji  katika kata Kiwalani Bom Bom na  Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akiwa ameambatana na watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa),wananchi wa Kiwalani Bom Bom wakielekea sehemu ya mradi wa maji.  (Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

DIRA YA KITAA : UNAKULA WAPI KATI YA HAWA...??


WAZIRI JENISTA MHAGAMA AZIAGIZA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI ZINAPOSAIDIA JAMII ZIKUMBUKE MAHITAJI YA MAKUNDI MAALUM

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kulia), Naibu Wake, Mhe. Stella Ikupa (wakwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (mwenye miwani), wakiangalia jinsi wanafunzi wasioona wanavyotumia mashine maalum za kuandika nukta nundu, kwenye chou cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam Septemba 17, 2018. Waziri Jenista amepokea mashine hizo maalum Braille Machines, 11 zilizotolewa na WCF ikiwa ni utekelezaji wa sera ya kusaidia jamii (CSR) ili zitumike kwanye taasisi za wanafunzi wasioona.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (pichani), ameziagiza taasisi za umma na binafsi nchini zinapotoa fedha za kusaidia jamii (CSR), zikumbuke kuna kundi maalum la walemavu nchini ambao nao wanahitaji huduma maalum kama wanavyohitaji wengine.

Mheshimiwa Waziri aliyasema hayo jioni ya Septemba 17, 2018 wakati akipokea mashine maalum za kuandika kwa wanafunzi wasioona (Braille Machines) kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye chuo cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam.


“Tunapoona kwenye shule za msingi wanahitaji madawati, tukumbuke kwamba, wapo wanafunzi kwenye vyuo, wapo wanafunzi kwenye shule za msingi, ambao ni wenye ulemavu ambao pengine badala ya madawati, wao wanahitaji viti vya kuwaongezea mwendo, au kama tunatoa computer mpakato, tukumbuke kwamba tunazo shule na vyuo watoto wetu, vijana wetu wanasoma wenye ulemavu wangehitaji mashine hizi zenye kuandika nukta nundu ili kuwasaidia wenye ulemavu ili na wao wafaidike na elimu katika nchi yetu ya Tanzania.” Alisema Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama wakati akihutyubia kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo.
Mhe. Waziri Jenista Mhagama (kushoto), akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia masuala ya wenye ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, wakati akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mhe. Stella Ikupa, (Kulia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba.

SPEED YA KUPITA KATIKA BARABARA ZA JUU (FLYOVER) TAZARA NI 40 TU

0
0
 Magari yakipita katika barabara za juu (flyover) iliyopo eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam ambapo  speed ni  40 tu kama inavyoonekana katika picha (Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Magari yakipita katika barabara za juu (flyover) iliyopo Tazara jijini Dar es Salaam.

WAZIRI KALEMANI AVIWASHIA UMEME VIJIJI VINGINE ZAIDI

0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), akikata utepe, kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Nyijundu, Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, jana Septemba 17, 2018. Kulia kwake (mwenye kofia) ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na kushoto kwake ni Mbunge wa Nyang’hwale, Hussein Kassu.

Na Veronica Simba – Geita

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasha umeme katika vijiji kadhaa vya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita na Kwimba mkoani Mwanza; hivyo kuendelea kuongeza idadi ya vijiji vyenye umeme nchini.

Alifanya kazi hiyo jana, Septemba 17, 2018 akiwa katika ziara ya kazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini. Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, alipofika kumweleza nia ya ziara yake mkoani humo; Waziri Kalemani alisema kuwa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza, unatarajiwa kusambaza umeme kwenye vijiji na vitongoji zaidi ya 220 pamoja na kuunganisha wateja wapatao 12,944.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kanegele, Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita, jana Septemba 17, 2018; katika hafla ya uwashaji rasmi wa umeme kijijini hapo.

Aidha, alisema kuwa; kukamilika kwa Mradi husika, kutafanya Mkoa wa Geita kuwa na ongezeko la asilimia 45 ya wateja, kutoka 28,483 waliopo sasa hadi kufikia idadi ya wateja 41,427 hapo mwakani. Akifafanua zaidi kuhusu faida za Mradi huo unaotarajiwa kukamilika Juni 2019, Waziri alisema kuwa, utafanya jumla ya vijiji 372 kati ya 499 vilivyopo kuwa na nishati ya umeme, ambavyo vitakuwa ni asilimia 75 ya vijiji vyote vya Mkoa wa Geita.

“Matarajio yetu ni kuwa, mzunguko wa pili wa Mradi, unaotegemewa kuanza Julai 2019, utamalizia vijiji vilivyobaki na kufanya vijiji vyote vya Mkoa wa Geita kuwa na nishati ya umeme kwa asilimia 100,” alisema. Akizungumzia kuhusu Wilaya ya Nyang’hwale ambako alifanya ziara na kuwasha umeme katika vijiji vya Kanegele na Nyijundu, Waziri Kalemani alieleza kuwa, mzunguko wa kwanza wa Mradi utapeleka huduma ya umeme kwenye vijiji 30 ambapo jumla ya wateja 1,288 wataunganishwa.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika moja ya nyumba za wakazi wa Kijiji cha Kanegele, Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita, kuashiria uwashaji rasmi wau meme katika eneo hilo, jana Septemba 17, 2018.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel, mbali ya kupongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo; aliwataka wananchi kutambua kuwa maendeleo hayaji kwa siku moja, bali ni hatua kwa hatua. Akifafanua kuhusu kauli yake, Mhandisi Gabriel alieleza kuwa, anatambua kiu kubwa ya umeme waliyonayo wananchi na kwamba wangependa kuona vijiji vyote vinapatiwa nishati hiyo kwa mkupuo. Hata hivyo, aliwataka waiamini Serikali yao kuwa itahakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, kazi inayofanyika hatua kwa hatua.

Kwa upande wake, Mbunge wa Nyang’hwale, Hussein Kassu, aliipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuwapelekea wananchi wa Jimbo lake, hususan walioko vijijini nishati ya umeme. Aliiomba Serikali iendeleze jitihada zaidi ili kuwafikishia huduma hiyo muhimu wananchi wote hivyo kuwezesha maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza, wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) na wananchi wa Kijiji cha Nyijundu, jana Septemba 17, 2018. Waziri Kalemani aliwasha rasmi umeme katika Kijiji hicho.

Katika ziara hiyo, Waziri Kalemani pia alitembelea Kijiji cha Sanga kilichopo wilayani Kwimba, Mkoa wa Mwanza, ambako aliwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Akizungumza katika hafla hiyo ya uwashaji umeme, Waziri alisema kwamba Serikali imedhamiria kupeleka umeme katika vitongoji vyote 137 vya Wilaya hiyo; vikiwemo vitongoji vyote Tisa vya Kijiji cha Sanga.

Waziri Kalemani anaendelea na ziara yake ya kazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia), akimkabidhi Kifaa cha Umeme Tayari (UMETA), Mbunge wa Nyang’hwale, Hussein Kissu kwa ajili ya kuwagawia wananchi wa Kijiji cha Kanegele, wakati wa hafla ya uwashaji rasmi wau meme kijijini hapo, jana Septemba 17, 2018. Waziri alitoa jumla ya vifaa hivyo 20 bure kama motisha kwa wananchi ili wachangamkie huduma ya kuunganishiwa umeme.

MDAIWA SUGU WA USHURU JIJI LA ARUSHA ANASWA

0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni akiwa ndani ya duka la mmoja wa wafanyabiashara wa stendi dogo ya Jiji la Arusha akikagua leseni ya biashara pamoja na risiti za ushuru wa kibanda leo Tarehe 17 Septemba 2018.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni (wa kushoto) alipokuwa akifanya operesheni ya kukusanya mapato ya jiji la arusha leo Tarehe 17 Septemba 2018.

Na. Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni  amemnasa mfanyabishara Bw. Mouris Makoi na kumfungia vibanda 69 kutokana na kudaiwa ushuru wa shilingi milioni 85.  

Hatua ni katika muendelezo wa operesheni ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na Dkt. Madeni ambapo amefungia vibanda  zaidi ya vibanda 90 vikiwemo vya Bw. Makoi katika stendi ndogo Jijini Arusha kwa kuwa na malimbikizo ya madeni na kukwepa ushuru wa vibanda hivyo pamoja na kutokuwa na leseni za biashara .

Dkt. madeni amesema kuwa Bw. Makoi ni mdaiwa sugu na amekuwa akikwepa kulipa kodi ya Serikali kwa mda mrefu kitendo kinachopelekea kuinyima mapato Halmashauri na ameagiza alipe deni lote ama ajisalimishe ofisini kwake kabla hatua nyingine za kisheria hazijachukuliwa dhidi yake.

Pia Dkt. Madeni amesikitishwa na baadhi wafanyabiashara wanaojificha chini ya miamvuli ya vyama vya siasa ili kukwepa kulipa kodi ya Serikali na kuwaasa wawe mfano bora katika kuhamasisha zoezi la ulipaji kodi.

“Kuna wafanyabiashara wanajificha kwenye vyama Fulani ili kukwepa kulipa kodi ya Serikali, nawaasa kuacha mara moja mazoea hayo kwani Serikali ya awamu hii imejikita katika kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali dini, kabila wala itikadi za vyama” alisema Dkt. Madeni

“Pia kuna wenye mikataba ya Halmashauri lakini wamepangisha watu wengine na kuwachajisha kodi ya juu kinyume na sheria  kwa mfano  kuna baadhi ya vibanda vinapaswa kulipiwa laki moja lakini wenye mikataba wanachukua laki mbili mpaka tatu kwa wapangaji wao kitu ambacho ni unyonyaji na ukatili wa hali ya juu hivyo nimeamuru wafutiwe mikataba yao na wapewe wapangaji ili wawe wanalipa ushuru moja kwa moja katika Halmashauri” aliongeza Mkurugenzi huyo.

WAZIRI MBARAWA AZINDUA MRADI WA MAJI WA KIWALANI LEO JIJINI DAR

0
0
*Awataka Dawasa wawaunganishie maji wananchi walipe kidogo kidogo

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amezindua mradi wa maji wa Kiwalani na kuwataka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) kuhakikisha wanawaunganishia wananchi wa eneo hilo maji kwa mkataba ili walipe kidogo kidogo kwakuwa serikali imetumia fedha nyingi sana kufanikisha mradi huona Malengo ya Serikali ni kuona watanzania wanapata maji kwa asilimia 90.

Amezungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliokuwa umekamilika tayari na wananchi wa Kiwalani wakianza kupata maji safi na salama kuitia vizimba vitano vilivyokuwa vimeshajengwa tayari.

Profesa Mbarawa amesema, kumalizika kwa mradi huu ni moja ya ahadi ya serikali ya kuhakikisha kila mwananchi na eneo la Kiwalani wana zaidi ya miaka 30 hawajawahi kuwa na maji safi ya Dawasa na wamekuwa wanatumia chumvi katika kipindi chote hicho.

Amesema Profesa Mbarawa, ukiachana na mradi huo mpaka sasa serikali bado ina miradi mingine ikiwamo mradi wa Bilioni 133.2 ambao ni mradi wa kutoka Benki ya dunia na maji yatakayozalishwa hapo yatapatikana maeneo ya Dar es Salaam na Bagamoyo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa (wapili kushoto) kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa (wakwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa wakifungua mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, kuzungumza wananchi wa Kiwalani Bom Bom leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa, (wapili kushoto), akionyeshwa ramani ya mradi wa maji katika kata Kiwalani Bom Bom na Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi leo jijini Dar es Salaam.

TTB YAINADI “ 787-8 DREAMLINER“ NCHINI INDIA

0
0
Bodi ya Utalii Tanzania inaendele na mkakati wake wa kupenya katika masoko ya utalii ya Bara la Asia kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii kutoka katika bara hilo pamoja na kuwashawishi watalii kuifanya Tanzania kuwa ni chaguo namba moja la utalii barani Afrika ”Tanzania, the leading and preferred tourist destination in Africa”, ambapo TTB imetayarisha maonesho matatu yatakayowahusisha wadau mbalimbali wa utalii wa nchini India.

Katika maonesho hayo yaliyoanza leo tarehe 17/9/2018 Mijini Delhi, The Roseate Aero City yametoa fursa kwa wadau wa utalii wa India kuvijuwa vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na kutangaza safari mpya za shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa kutumia ndege yake aina ya 787-8 Dreamliner mwezi November, 2018 inatarajia kuanzaisha safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Mumbai nchini India.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Bi Devota Mdachi amesema “kupitia maonesho haya wadau wa utalii wa India watapata fursa ya kujuwa kwa kina kuhusu utalii wa Tanzania pamoja na kuweza kufanya biashara na wadau wa utalii wa Tanzania tuliyoambatana nao katika maonesho haya. Aidha, tunatarajia wadau hao wa India wataitumia ” 787-8 Dreamliner” ya ATCL kwa ajili ya kuwaleta watalii Tanzania, juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitika mashirika haya zitaongeza idadi ya watalii kutoka soko la utalii la India”.

Tarehe 19/09/2018 TTB itaendelea na maonesho hayo katika mji wa Ahmadabad, Crowne Plaza na tarehe 21/09/2018 maonesho yatafanyika mijini Mumbai, Hotel Orchid Mwaka 2017 Tanzania ilipokea idadi ya watalii 39,115 kutoka india.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa BOdi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi akikoa maelezo ya utalii wa Tanzania kwa wadau wa utalii wa India.
Wahishiriki wa onesho wakifuatika maelezo yanayotolewa ma mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi.
Mkurugenzi wa TTB, akitoa akifafanua jambo kwa wadau wa utalii wa India.

BancABC Tanzania partners with MasterCard and Vodacom to introduce online payment solutions

0
0
BancABC Tanzania, which is part of Atlas Mara a London listed entity, has made yet another step ahead of the market by partnering with MasterCard and Vodacom Tanzania through M-Pesa service to introduce online payment solutions – The Vodacom MasterCard Virtual card for both local and international purchases. The service will enable local businesses and merchants to accept interoperable digital payments, many for the first time. Consumers are now able to make quick, easy and secure payments with their mobile money wallets at any time. 

The virtual card will allow M-Pesa mobile wallet holders to make payments on any local or international website or app so long as MasterCard is accepted for payment without the need for a bank account or credit card. Customers can request the virtual card from the M-Pesa USSD menu or soon on the M-Pesa app and top the card up via the wallet. Once the card is topped up with funds, the virtual card is ready for use.

Speaking in Dar es Salaam during the launch of the Vodacom MasterCard Virtual card, the BancABC Tanzania Head of Treasury Barton Mwasamengo said currently we are living in a world where payments are processed every fraction of a second, financial institutions are increasingly challenged to improve the profitability of today’s business whilst they accommodate a steady stream of new transactions, channels and technologies. Due to that factor, BancABC is striving to expand the various channels of its transactions processing systems to new levels by collaborating with other partners in the market to increase its penetration with an objective of taping into the unbanked, Mwasamengo said.

Through partnerships like these, we will be able to accomplish our digital channels vision by providing tailor made solutions for our customers. The Vodacom MasterCard Virtual card is one of the many digital initiatives to be rolled out in the Country, added Mwasamengo.


Mkuu wa Kitengo cha Hazina BancABC Tanzania Barton Mwasamengo akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kuzindua huduma ya Vodacom MasterCard Virtual card. Huduma ya Vodacom Virtual Card ni maalum kwa kulipia huduma na bidhaa kwa kupitia M-Pesa kwa njia ya mtandao na itatumika ndani na nje ya nchi ikiwa ni ushirikiano baina ya BancABC, Vodacom Tanzania na MasterCard.

Mkuu wa Kitengo cha Hazina BancABC Tanzania Barton Mwasamengo (kushoto), Raghav Prasad Rais wa MasterCard Ukanda wa Sub African Sahara (kati kati) na Hisham Hendi Kaimu Mkurugenzi Vodacom Tanzania (kulia) wakipiga makofi baada ya kuzindua kuzindua huduma ya Vodacom MasterCard Virtual card jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Huduma ya Vodacom Virtual Card ni maalum kwa kulipia huduma na bidhaa kwa kupitia M-Pesa kwa njia ya mtandao na itatumika ndani na nje ya nchi ikiwa ni ushirikiano baina ya BancABC, Vodacom Tanzania na MasterCard.

Mkuu wa Kitengo cha Hazina BancABC Tanzania Barton Mwasamengo (kushoto), Raghav Prasad Rais wa MasterCard Ukanda wa Sub African Sahara (kati kati) na Hisham Hendi Kaimu Mkurugenzi Vodacom Tanzania (kulia) wakishikana mikono baada ya kuzindua kuzindua huduma ya Vodacom MasterCard Virtual card jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Huduma ya Vodacom Virtual Card ni maalum kwa kulipia huduma na bidhaa kwa kupitia M-Pesa kwa njia ya mtandao na itatumika ndani na nje ya nchi ikiwa ni ushirikiano baina ya BancABC, Vodacom Tanzania na MasterCard.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

KAMPENI YA 'LET'S DO IT' YAWAKUTANISHA PAMOJA WATANZANIA KUFANYA USAFI

0
0
 Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifanya usafi kwenye ufukwe wa Coco, Kinondoni Jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia kampeni ya ‘Let’s Do it’ iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili. #KINONDONI
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wadau mbalimbali wa Mazingira kwenye ufukwe wa Coco katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia Kampeni ya ‘Let’s Do it’ iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili. #KIGAMBONI
 Wadau mbalimbali wa Mazingira wakifanya usafi eneo la Ferry Sokoni, Kigamboni jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya usafi duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki kupitia kampeni ya ‘Let’s Do it’, iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili.
#MBEZI MWISHO - UBUNGO

UEFA CHAMPIONS LEAGUE is baack! KAMA SIO DSTV POTEZEA

0
0
 DStv tunauwasha tena Moto Jumanne hii ambapo msimu mpya wa UEFA Champions league unaanza rasmi, Na ni kwenye Supersport pekee ndipo utaweza kuipata Ligi hii ya Mabingwa wa Ulaya Mubashara!

Barcelona watatufungulia pazia kwa mechi kali dhidi ya PSV itakayochezwa saa 2 usiku na kuruka LIVE kwenye DStv kupitia Supersport 5. Inter Milan itacheza dhidi ya Tottenham Hotspur saa 2 usiku na utaipata mechi hii LIVE kwenye Supersport 6 kifurushi Compact Plus.

Borussia Dortmund wataenda Jan Breydel Stadium kukutana na Club Brugge mechi itakayorushwa LIVE kwenye Supersport 8 ya kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 saa 12 jioni. Mechi nyingine kali Jumanne hii ni kati ya Liverpool dhidi ya PSG itakayochezwa saa 4 usiku kwenye Supersport 5 kifurushi Compact Plus.

Mteja wa DStv, Hakikisha unalipia kifurushi chako kabla hakijakatika ili upate ofa ya kuongezewa chaneli za supersport za kifurushi cha juu kwa kipindi cha siku 7 buree na utaweza kufurahia msimu mpya wa UEFA Champions League.

Kumbuka ukiwa na Application ya DStv Now utaweza kuangalia mechi zote kupitia simu yako ya mkononi, Tablets, Laptop na hata Desktop ukiwa mahali popote wakati wowote bila gharama ya ziada.

DStv sasa inapatikana kwa sh.79, 000 tu unapewa na kifurushi cha mwezi mmoja Bomba buree, Kujiunga piga 0659 070707!

DStv Moto Hauzimi!

MADAKTARI MUHIMBILI WAPATA UFADHILI

0
0
Shirika Lisilo la Kiserikali Australia Tanzania (ATS) limetoa ufadhili kwa madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa upasuaji (plastic Surgery) kwa watu wenye tatizo la mdomo sungura pamoja na wale waliopata ajali za barabarani na ajali za moto. Lengo la kutoa ufadhili kwa Dkt. Ibrahim Mkoma na Dkt. Edwin Mrema kusoma katika chuo chochote duniani ni kuwajengea uwezo wa kufanya upasuaji kwa watu waliopata ajali za moto na wenye tatizo la mdomo sungura.

Mbali na ATS kutoa ufadhili huo shirika hilo kupitia Rafiki Surgical Missions na Muhimbili wamekuwa wakishirikiana kutoa elimu na kufanya upasuaji kwa watu wenye matatizo hayo nchini.

Mwenyekiti wa shirika hilo Didier Murcia amesema kuwa tangu mwaka 2004, Rafiki Surgical Missions imekuwa ikituma wataalamu kutoka Australia kwa ajili ya kubadilisha maisha ya watu kwa wale wenye tatizo la mdomo sungura na waliopata ajali.

“Kila mwaka wataalamu wetu wanakuja Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma kwa watu waliopata ajali na hadi sasa zaidi ya watu 2,500 wamefanyiwa upasuaji wakiwamo watoto na watu wazima,” amesema Murcia.

Murcia amesema kwamba Watanzania wengi wamenufaika kupitia huduma za upasuaji na hivyo watu waliozaliwa wakiwa na tatizo la mdomo sungura na waliopata ajali-baada ya upasuaji wamekuwa wakirejea katika hali zao za kawaida.

“Mpango huu unanufaisha familia, jamii na Tanzania kwa ujumla. Lakini nipende kuwashauri wazazi kwamba watoto wanaozaliwa na tatizo la mdomo sungura wanatakiwa kufanyiwa upasuaji mapema ili kurejesha sura ya mtoto katika hali ya kawaida, watoto wasiachwe hadi wanakuwa watu wazima,” amesema Murcia.

Naye Dkt. Mkoma alishukuru ATS kwa kuwapatia ufadhili wa kwenda kusoma nje ya nchi na kwamba masomo hayo yatasaidia kuwaongezea utaalamu ambao watautumia kufanya upasuaji kwa watu mwenye matatizo hayo.

“Udhamini huu utasaidia kuongeza utaalamu katika upasuaji kwa watu wenye tatizo la mdomo sungura pamoja na wale walipata ajali ya moto,” amesema Dkt. Mkoma.
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Shirika Lisilo la Kiserikali Australia Tanzania (ATS), Didier Murcia akizungumza kwenye hafla ya kutoa ufadhili wa masomo ya upasuaji (plastic surgery) kwa madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Madaktari waliopatiwa ufadhili ni; Dkt. Ibrahim Mkoma na Dkt. Edwin Mrema wa hospitali hiyo.
Baadhi ya wageni walioudhuria hafla hiyo wakimsikiliza mwenyekiti huyo wakati akieleza jitihada za ATS na Muhimbili za kutoa huduma za upasuaji kwa watu waliopata ajali za moto, ajali za barabarani na wenye tatizo la mdomo sungura.
Dkt. Ibrahim Mkoma wa Muhimbili akipokea vifaa tiba vya upasuaji kutoka kwa mwakilishi wa Australia Tanzania Society (ATS).
Dkt. Baruani akipokea vifaa tiba kwa niaba ya Dkt. Edwin Mrema kutoka kwa mwakilishi wa Australia Tanzania Society (ATS), James Chialo.

KATIBU MKUU WA UVCCM KUZINDUA ALBAM YA MSANII MGEGO TAREHE 30 /09 /2018 MKOANI IRINGA

0
0
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
KATIBU mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) taifa kuwa mgeni rasmi katika uzindua albam ya nyimbo za injili ya msanii James Mgego wa mkoani Iringa inayoitwa “Achani Mungu Aitwe Mungu” na uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa HIGHLAND HALL uliopo mjini iringa tarehe 30 /09 /2018.

Akizungumzia uzinduzi huo msanii wa nyimbo za injili James Mgego alisema kuwa anatarajia kuzindua albam yenye nyimbo tisa zilizotengenezwa katika studio za Nice zilizopo mkoani Iringa.

Mgego alisema kuwa mgeni rasmi atakuwa katibu mkuu wa umoja wa vijana ndugu Raymond Mwangwala(MNEC) na viongozi wengi wa serikali na wakisiasa kutoka mkoani Iringa na nje ya mkuoa wa Iringa.

Katika uzinduzi huo kutakuwa na kwaya mbalimbali ambazo zitatumbuiza kama vile TAC kwaya Anglicana, Nuru kwaya Anglicana,TAG Mlandege,Mhimidini Mlandege,Kwaya ya vijana kanisa kuu,kwaya mkuu kihesa,uinjilisti KKKT Ipogolo, uinjilisti KKKT PHM frelimo,kwaya ya vijana kitwilu,RC Mshindo,ACT fellowship,Faith kwaya tumain, RC kichangani kihesa,Sayuni Anglican Ipogolo na Elishadai Anglican Ilula.

Aidha Mgego alisema kuwa kutakuwepo na waimbaji maalufu na mashuhuri wa nyimbo za injili ndani na nje ya mkoa wa Iringa watakuwepo kama vile DR Tumaini Msowoya,Nesta Sanga,Ntimiza Rwiza,Samson Kihombo,faraja kigula,Mwl Senje,mama masawe mwamvita,Petro Chetenge,Raymond Mwalisu,Tukuswiga Ikoso na wengine wengi.

Mgego alisema kuwa anawakabiribisha wananchi wote katika uzinduzi huo ambapo hakutakuwa na kiingilio chochote kile.

UVCCM MKOANI TANGA YAWEKA KAMBI UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA

0
0
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoani Tanga,Omari Mwanga akizungumza wakati wa  ghafla ya uzinduzi wa kambi ya Vijana wa chama hicho kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza ambapo  mgeni rasmi Mbunge wa Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema ushirikiano uliofanywa na vijana hao wa kushiriki katika mradi mkubwa kama huo ni jambo la
kuigwa nchi nzima.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tanga Omari Mwanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
VIJANA wa UVCCM Mkoani Tanga wakiendelea na ujenzi
 Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga Omari Mwanga.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live




Latest Images