Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

Mastercard na M-Pesa wazindua kadi inayowezesha kufanya manunuzi mtandaoni

$
0
0

 Kwa mtu yeyote aliyewahi kufanya manunuzi ya kitu chochote bila kuinuka kitini ama kutoka nyumbani kwake anaweza kuelezea urahisi na wepesi wa kufanya manunuzi mtandaoni, lakini hii imekuwa ni ndoto kwa Watanzania walio wengi, mpaka sasa ambapo Mastercard wameungana na Vodacom na BancABC kutengeneza kadi ya kwanza itakayowezesha manunuzi mtandaoni – M-Pesa Virtual Card.

“Huduma ya M-Pesa kutoka Vodacom ina wateja Zaidi ya milioni 8.2 huku ikiwa na Zaidi ya wakala laki moja waliotapakaa nchi nzima, hii inawezsha upatikanaji wa uhakika wa huduma za kifedha, lakini imekuwa ni ngumu pale linapokuja suala la kulipia manunuzi mtandaoni haswa kupitia tovuti za kimataifa. Uzinduzi na ufanyaji kazi wa Virtual Card kupitia M-Pesa utaleta mapinduzi katika kuwezesha Watanzania kufanya manunuzi mtandaoni na kuondosha vikwazo ikiwamo kuwa na akaunti ya benki na pia hatari ya mteja kuweka taarifa zake za kibenki mtandaoni,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Hisham Hendi.

Inategemewa kwamba uunganisho wa intaneti kwa bara la Afrika itaongezeka sana ikiwa ni matokeo ya upatikanaji wa simu janja (Smartphone) na pia ukuaji wa utoaji huduma yenye kasi zaidi ya intaneti kutoka kwa watoa huduma kama Vodacom. Ongezeko hili la upatikanaji wa huduma ya intaneti litaongeza uhitaji wa maudhui ya kidijitali, mitandao ya kijamii, M-Commerce, elimu ya mtandaoni na pia malipo mtandaoni kurahisishwa na kuongezewa usalama zaidi.

Kadi hii itawawezesha wateja wa M-Pesa kufanya malipo ya aina yeyote kwa tovuti za kimataifa au za hapa nyumbani, ama kwa kutumia zana (App) yeyote ambayo inatumia na Mastercard kwa malipo, bila kuhitajika kuwa na akaunti ya benki au kadi ya mkopo (Credit Card). Wateja wanaweza kutengeneza virtual card kupitia menyu ya M-Pesa ama kupitia App yetu ya M-Pesa (huduma hii tutaiongeza hivi karibuni) na kuijaza pesa kupitia mfumo wetu wa M-Pesa. Kadi hii inakuwa tayari kwa matumizi mara tu baada ya kujazwa pesa.


Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (Kati), Raisi wa Kusini mwa Sahara wa Mastercard, Raghay Prasad (kushoto) na Mkuu wa hazina na kitengo cha soko la kimataifa wa Banki ABC, Barton Mwasamengo (kulia) wakionesha ushirikiano kati ya M-Pesa na Mastercard uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (Kati), Raisi wa Kusini mwa Sahara wa Mastercard, Raghay Prasad (kushoto) na Mkuu wa hazina na kitengo cha soko la kimataifa wa Banki ABC, Barton Mwasamengo (kulia) wakionesha ushirikiano kati ya M-Pesa na Mastercard uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.


BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI

$
0
0
Na. WFM
Serikali imezitaka Benki zote zinazotoa mikopo ya kilimo Tanzania Bara na Zanzibar kuhakikisha zinatoa mikopo kwa kuzingatia vigezo vya ukopeshaji vikiwemo kuangalia historia ya mkopaji ili kuondoa mikopo Chechefu (NPL).

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bububu Mhe. Mwantakaje Haji Juma, aliyetaka kujua utaratibu unaotumika kutoa mikopo kwa wakulima wa Zanzibar kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Dkt. Kijaji alieleza kuwa kabla ya kutoa mkopo ni lazima Benki ijiridhishe na aina ya mradi wa mkopaji ikiwa utaleta faida itakayomuwezesha mkopaji kurejesha mkopo huo kwa wakati ili kuzuia ukuaji wa Mikopo Chechefu.

Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo aliyetaka kujua ni wananchi wangapi wanaonufaika na mikopo ya Kilimo kwa upande wa Zanzibar, Dkt. Kijaji alisema kuwa jumla ya wananchi 3,000 wamenufaika na mikopo ya Benki ya TADB hadi kufikia Julai 31, 2018.

“Kati ya wanufaika hao 3000, idadi ya wanaume walionufaika ni 1800, wanawake 900 na vijana wa kike na kiume ni 300”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa jumla ya mikopo ya shillingi bilioni 6.50, imetolewa kwa wananchi hao wa Zanzibar hadi kufikia Julai 31, 2018.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi. Hamad Masauni, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Peter Serukamba, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.

6 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mbunge wa Chalinze Rizwani Kikwete, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Septemba 11, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza kikao cha sita cha mkutano wa kumi na mbili cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akijibu maswali Bungeni, jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi  akieleza mipango mbalimbali ya jeshi la kujenga Taifa katika kuanzisha mafunzo ya stadi za kazi kwa Vijana waliojiunga na jeshi ilo kwa kujitolea ili waweze kuajiriwa na taasisi zingine za Serikali,Sekta binafsi au kujiajiri wenyewe.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, akizungumza Bungeni jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt Philip Mpango akisoma Muswada wa Sheria ya marekebisho ya sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi wa mwaka 2018 leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Mhandisi Isack Kamwelwe akitolea ufafanuzi juu ya changamoto za kivuko cha Mv Mafanikio katika kusaidia dharura zinazojitokeza kwa wagonjwa hasa akina mama wajawazito kuhudumiwa wakati wa usiku leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Mhandisi Stella manyanya akielezea mipango  mbalimbali ya Serikali katika kufanikisha azma nzuri ya uchumi wa Viwanda nchini leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Mwalimu Joyce Solomon wa Shule ya Tumaini Mission kutoka Arumeru akifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge pamoja na wanafunzi wa shule hiyo leo Jijini Dodoma.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.

MASENETA KUTOKA BUNGE LA UFARANSA WAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SPIKA WA BUNGE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (kushoto) akizungumza na Masaneta kutoka Bunge la Ufaransa walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wakwanza toka kulia ni Seneta Ronan Dantec, Seneta Cyril Pelleah na Seneta Bernard Jomier.
   Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier (kushoto) akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (katikati) wakati yeye pamoja na Masaneta kutoka Bunge la Ufaransa walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wakwanza toka kulia ni Seneta Ronan Dantec, Seneta Cyril Pelleah na Seneta Bernard Jomier.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (katikati) akiwaelezea jambo Masaneta kutoka Bunge la Ufaransa na Balozi wa Ufaransa nchini wakati alipowatembeza ndani ya Ukumbi wa Bunge, wakwanza toka kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier, Seneta Ronan Dantec, Seneta Cyril Pelleah na Seneta Bernard Jomier.
 
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (katikati) ndani ya Ukumbi wa Bunge katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier, (wakwanza toka kulia) Seneta Ronan Dantec, Seneta Cyril Pelleah na Seneta Bernard Jomier.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (katikati) nje ya  Ukumbi wa Bunge katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier, (wakwanza toka kulia) Seneta Ronan Dantec, Seneta Cyril Pelleah na Seneta Bernard Jomier.
PICHA NA BUNGE

WAMBURA AWAONYA WAAMUZI, LIGI KUENDELEA WIKIENDI HII

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
LIGI kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena mapema wikiendi hii kwa timu zote 20 kuanza kukamilisha  mzunguko wa nne  wa ligi huku timu za Simba, Yanga na Azam ratiba zao za zikitafutiwa ratiba nyingine.

Akizungumzia ratiba ya ligi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi  Boniface Wambura amesema mzunguko wa nne wa ligi utaanza wikiendi hii baada ya kumalizika kwa ratiba ya michezo ya kimataifa ya kirafiki ya FIFA iliyochezwa tarehe 3 hadi 11 Septembe.

Amesema kutokana na kalenda ya FIFA, kuna baadhi ya mechi za Simba, Yanga na Azam zuki zilizoondolewa kwa ajili ya kupisha ratiba hiyo na wao kuwa na mechi pungufu baada ya  wachezaji wao kwenda katika timu za taifa na kupelekea kuhairisha mechi zao.

Wambura amesema kuwa, kwa timu zilizokuwa hazijakilimisha mzunguko wa pili na wa tatu watapangiwa tarehe ya kucheza mechi zao kwani kwa sasa kutakuwa na ligi ndefu ,mechi nyingi 380 na hiyo ni  kutokana na timu kuwa nyingi.

"timu ambazo hazijafanikiwa kufikisha idadi ya mzunguko wa mechi zao na watapangiwa ratiba ili kucheza mechi hizo, ila kwa sasa ligi itakuwa ndefu na itahitaji umakini mkubwa kutokana na timu kuwa nyigi,"amesema Wambura.

Akizungumzia kuhusu waamuzi wa ligi kuu kutokuwa makini katika maamuzi yao uwanjani, Wambura amesema kuwa waamuzi waliofanya makosa katia mzunguko wa kwanz ana wa pili tayari wameshawachukulia hatua na kuwataka waamuzi wengine kuchezesha mpira wa kutumia kanuni 17 za mpira.

Wambura amesema, waamuzi wanatakiwa waangalie mechi zao zilizopita pamoja na kufanya mazoezi kwa sana na hii inatokana na idadi ya mechi 
na msimu huu watakuwa wamepata mechi nyingi za kuchezesha.

Amesisitiza kwa sasa wana waamuzi makini wakiwa wanasimamiwa vizuri na kamati ya waamuzi na hawatasita kwuachukulia hatua wale ambao watashindwa kuchezesha kwa sheria 17 za soka.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi  Boniface

MAHAFALI YA SEKONDARI YA JOHN BAPTIST YAFANA

$
0
0
Shule ya Sekondari ya wasichana ya John Baptist imefanya mahafali ya kidato cha nne na kushuhudia jumla ya wanafunzi 32 wakihitimu kidato cha nne.Shule hiyo pia ilitumia mahafali hayo kuzindua rasmi masomo ya kidato cha tano na sita kwa wasichana.
Akizungumza kwenye mahafali hayo mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Chemba ya Biashara Tanzania Octa Mshiu alisema " wasichana ni nguzo kuu ya maendeleo ya Taifa letu, tunawaomba muende kutumia maarifa mliyoyapata hapa na muhimu zaidi ni kuendelea kukumbuka kuwa hakuna litakalowezekana bila ya kutilia maanani nidhamu na kufanya kazi kwa bidii".
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Jalia Mayanja alisema shule ya John Baptist imenuia kusaidia wasichana kufikia malengo yao kutumia elimu na kutilia mkazo nidhamu. Aliwakaribisha wazazi kutumia shule hiyo kwa ajili ya masomo ya watoto wao kwa kidato cha tano na sita yaliyoanzishwa. Shule hiyo inayotoa michepuo ya ECA, HKL na HGE na iko Boko Jijini Dar es salaam.

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA KIGOMA

$
0
0
Mradi wa Kuwawezesha vijana wa kike na wanawake kiuchumi kupitia Tasnia ya Urembo na Vipodozi ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wamemaliza mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma Yaliofanyika kwa wiki mbili kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Kigoma. Mafunzo hayo yaliyotolewa bure yamewanufainsa wanawake 20 kutoka Mkoani Kigoma na vitongoji vya jirani. 
Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. Awamu ya pili walipata ujuzi jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi salama vya LuvTouch Manjano.
Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba ili waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara zao wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea. Taasisi ya Manjano imefanikiwa kuwawezesha zaidi ya wanawake 500 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Kigoma na Unguja - Zanzibar
. Wengi wa wahitimu wa mradi wa Manjano Dream-Makers wamefanikiwa kuanzisha biashara zao na kuwa mawakala wa bidhaa za LuvTouch Manjano. Kwa mwaka huu taasisi ya Manjano wanajipanga pIa kumalizia kwa kuwawezesha kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wa kike na wanawake wa Mkoa wa Tabora..

SEPTEMBA 11, OSAMA BIN LADEN ALIVYOONGOZA SHAMBULIO LA KIGAIDI MAREKANI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
LEO Septemba 11 dunia inakumbuka miaka 17 tangu kutokea kwa shambulio la kigaidi lililotekelezwa na kundi la kigaidi maarufu kama Al Queda dhidi ya Marekani kwa kulipua miji miwili na kusababisha mauaji na hasara kubwa.

Shambulio hilo ni moja kati ya mashambulio manne makubwa kuwahi kutokea, na shambulio hilo linafahamika zaidi kama Septemba 11 lilotokea asubuhi ya siku ya jumanne ya tarehe 11/9/2001 ambapo magaidi hao waliteka ndege 4 na kuzitumia kama silaha kwa kuzigongesha kwenye majengo makubwa ya kibiashara (World Trade Centre) katika majiji Newyork na Washngton DC.

Shambulio hilo lililofanyika asubuhi ilisababisha vifo zaidi ya watu 2996, majeruhi zaidi ya 6,000 na hasara ya uharibifu uliokadiriwa kufikia dola za kimarekani bilioni 10 na baadaye wengi wakagundulika na kuwa na matatizo katika mifumo ya upumuaji na saratani.

Ndege tatu zilifanikiwa kugonga majengo makubwa ya kibiashara na ndege moja ilitwaliwa na abiria na ikaangua katika mji wa Pennsylvania na magaidi 19 wa shambulio hilo walifariki.

Baada ya shambulio  Marekani walilaani shambulio hilo  na kuanza vita dhidi ya ugaidi ambapo kiongozi na mwanzilishi wa kundi hilo la Al Queda Osama Bin Laden alikimbilia nchini Afghanistan na kujificha.

Baada ya kumsaka gaidi huyo kwa miaka 10, Bin Laden aliuawa na jeshi la wana maji la Kimarekani mnamo 5/2/2011.

ARUSHA UNITED YAPANIA KUPANGA LIGI KUU MSIMU UJAO

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MKIRUGENZI Mtendaji wa timu ya Arusha United Saad Kawemba amesema kuwa kwa sasa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kuanza ligi daraja la kwanza baada ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao lkilichorejea jana kutokea mkoa wa Lindi, Kawemba amesema walikuwa wamepanga kuweka maandalizi ya kikosi chao katika mikoa 2 ambayo ni Dar es Salaam na Tanga na kucheza mechi za kirafiki ila wakabahatika na kuongeza mkoa mwingine ambao ni Lindi.

Kawemba amesema kuwa, wameweza kucheza mechi sita za kirafiki na katika michezo hiyo walifanikiwa kushinda michezo miwili na kutoa sare moja na mitatu wakipoteza.

Amesema kuwa, walianza mechi ya kwanza ya kirafiki na Simba ambapo walipoteza mchezo huo, walicheza pia na Coastal Union ya Tanga na mechi zingine wakicheza Lindi na Dar es Salaam na mchezo mwingine watacheza alhamisi dhidi ya Namungo ya Arusha.

Kawemba amewataka wana Arusha kuwa na imani na timu kwani wana uhakika wa kuoanda ligi kuu msimu ujao kutokana na kikosi kuwa kizuri na ushindani, akielezea kuwa kupoteza mechi yoyote katika mchezo wa kirafiki sio kama wana timu isiyo ya ushindani bali mwalimu anakuwa anaangalia makosa yaliyopo ili aweze kuyafanyia kazi kabla ya kuanza kwa ligi.

"Tumecheza michezo sita ya kirafiki na Alhamisi tutacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Namungo na mechi hizo zimekuwa na mchango mkubwa sana katika kikosi chetu kwani zimeweza kumsaidia Mwalimu kuona makosa yaliyopo kabla ya kuanza kwa ligi na kupoteza mechi ya kirafiki haimaanishi kuwa kikosi ni kibaya ila tuna imani na timu yetu mwakani itashiriki ligi kuu Tanzania bara,"amesema Kawemba.

Akizungumzia udhamini wa timu yao, Kawemba amewataka wadau mbalimbali wanaopendelea soka na wasio wajitokeze kuidhamini timu hiyo kwani kwa sasa kwani itakapopanda ligi kuu msimu ujao thamani yao itapanda zaidi.

Arusha United iliyo chini ya kocha Fred Felix Minziro akiwa na historia ya kuzipandisha timu za ligi daraja la kwanza katika kipindi mitatu uongozi wa timu hiyo umekuwa na imani kuwa msimu ujao kuwa timu yao itaingia Ligi Kuu.Minziro amefanikisjha timu ya Singida United, KMC kupanda ligi kuu katika misimu miwili tofauti.
MkuruenziMtendaji wa timu ya Arusha United Saad Kawemba.

EMIRATES WAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA

$
0
0


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer amesisitiza kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wanaosafiri na ndege zao katika mataifa mbalimbali duniani.

Pia amezungumzia fursa zilizopo kutokana na uwepo wa safari za ndege zinazofanywa na Emirates kati ya Tanzania na nchi nyingine ikiwemo ya usafirishaji mizigo ya kibiashara kutoka Dar es Salaam ambako kumekuwa kituo kikubwa cha kibiashara kwa Afrika Mashariki.

Alfajeer amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari katika mazungumzo yaliyolenga kujenga uhusiano kati yake na vyombo vya habari kuhusu masuala ya kibashara na maisha.

“Emirates nia yetu ni kuendelea kuhakikisha wateja wetu wanakuwa wenye thamani bora kadri inavyowezekana,” amesema.

Hivyo wanaendelea kuwa wabunifu katika kutoa huduma bora zaidi. “Kila siku tumekuwa tukiangalia njia za ubunifu ili kuboresha huduma zetu kwa wateja ikiwa pamoja na kurahisi safari zao kati ya eneo moja ya jingine.”

Kuhusu mizigo amesema mingi kupitia Emirates kuna mizigo mingi ambayo inasafirishwa kutoka Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio na jinsi wanavyoliendesha shirika hilo. Pembeni ni mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo, Tununu Kasambala. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwandishi wa TBC1 Stanley Ganzel akiuliza swali. Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania (hayupo pichani).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Ndege la Emirates nchini Tanzania Rashed Alfajeer (wa sita kutoka kushoto) akiwa na wanahabari waliohudhuria mkutano wake. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAGOMBEA 21 WACHUKUA FOMU ZA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI KLABU YA SIMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kamati ya uchaguzi ya Simba imetangaza majina ya wagobea waliochukua fomu kuwania nafasi mbalimbali katika klabu hiyo uliokamilika Septemba 10 saa Kumi Jioni kama ilivyokuwa imepangwa.

Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya kamati, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa Kamati hiyo imetoa taarifa ya jumla ya fomu 21 zimechukuliwa na wagombea mbalimbali, fomu 2 zikizchukuliwa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo, fomu 2 zingine zimeenda kwa wagombea wanaowania nafasi ya wajumbe wanawake na fomu 17 ziliozosalia zmechukuliwa na wagombea wa kiumekwa nafasi ua ujumbe wa bodi.

Majina  ya wagombea hao ni kama yaliyoanishwa hapo chini

Wagombea Simba SC nafasi ya Mwenyekiti 
Mwenyekiti wa Bodi
1. Swedi Nkwabi
2. Mtemi Ramadhani


Wagombea nafasi ya wajumbe wanawake
1.Jasmeen Badou
2.Asha Baraka

Wajumbe wa Bodi 
1. Mwina Kaduguda
2. Iddi Kajuna
3. Said Tulily
4. Hussein Kitta Mlinga 
5. Ally Suru
6. Mohamed Wandi
7. Hamis Mkoma
8. Abdallah Migomba
9. Alfred Eliya
10.Juma Abbas Pinto
11.Abubakar Zebo
12.Seleman Said
13.Dr Zawadi Ally Kadunda
14.Christopher Mwansasu
15.Omar Mazola
16.Patrick Rweyemamu
17.Selemean Omar Seleman

Aidha kamati inapenda kwuakumbusha wagombea hao kuwa zoezi la urudishaji fomu limeanza rasmi leo Septemba 11 hadi Jumamosi Septemba 15 kuanzia saa 3 asubuhi hadi kumi jioni katika ofisi za makao makuu ya Kalbu hiyo Msimbazi Kariakoo na watahitajika kurudisha fomu hizo wao binafsi wakiambatanisha nakala za vyeti vyao vya elimu kama ilivyoanishwa kwenye fomu.

ULAJI USIOFAA UNAONGEZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemalishe duni pamoja na ulaji usiofaa na mitindo ya maisha vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususan kwa vijana na watu wazima, ambao ndiyo nguvu kazi kwa Taifa.

“Ni jambo lisilopingika kuwa hatua za kukabiliana na magonjwa ya kusendeka (mfano matatizo ya moyo, saratani, kisukari na shinikizo kubwa la damu) zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kasi ya maendeleo yetu kwani gharama za matibabu yake ni kubwa mno; si kwa kaya zinazoathirika tu bali kwa Taifa zima.”

Waziri Mkuu  ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 11, 2018),  wakati akifungua mkutano wa tano wa wadau wa masuala ya lishe, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema lishe iliyozidi inadhihirishwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha na ulaji usiofaa kama vile uzito uliozidi, viriba tumbo, shinikizo la damu pamoja na kisukari.

Amesema kasi ya ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza inapaswa kudhibitiwa kwa kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha. “Huu ni wakati wa kuangalia kwa pamoja kama jitihada zetu zinaleta matunda tunayotarajia.”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa mkutano wa tano wa kutathmini utekelezaji wa afua za lishe nchini, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Septemba 11, 2018. 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na washiriki wa mkutano wa tano wa kutathmini utekelezaji wa afua za lishe nchini, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Phaustine Ndugulile kushoto na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kulia, wakifuatilia mkutano wa tano wa kutathmini utekelezaji wa afua za lishe nchini, uliyofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Septemba 11, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kabla ya kufungua mkutano wa tano wa kutathmini utekelezaji wa afua za lishe nchini, kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Septemba 11, 2018.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HABIBU KYOMBO AREJEA NCHINI BAADA YA KUMALIZA MAJARIBIO AFRIKA KUSINI

$
0
0
Na Agness Francis,globu ya jamii
UONGOZI wa Singida United  wanategemea kukaa mezani na Mamelod  Sundowns  ya Afrika Kusini kwa ajili ya kufikia muafaka wa mchezaji Habibu Kyombo.

Mshambuliaji huyo kinara kwa ufungaji kwenye michuano ya Azam Sport Federation Cup aliekipiga  Singida United kwa msimu mzima uliopita 2017-18 amerejea nchini jana akitokea nchini humo.

Ambako alikuwa akifanya majaribio katika viwanja vya Schloorkop Mamelodi Sundowns kwa ajili ya majaribio kikosini hapo.

Imeelezwa Kyombo alipewa siku 10 za majaribio na uongozi wa klabu ya Mamelod na  kuongezewa tena siku zingine 10 kwa ajili ya kufanya trial na senior team.

Siku 20 zilipokamilika kwa majaribio ya mshambuliaji huyo huku mamelodi wakikikubali kiwango chake na uwezo wake mkubwa aliouonyesha kwa siku hizo alizopewa.

Baada ya kukaa mezani uwongozi wa Singada United na Mamelod Sundown kujadiliana kubaki  mchezaji huyo kwa waajiri wake  wa msimu uliopita au kujiunga na kikosi cha Mamelodi.

RC MAKONDA ATOA SIKU 30 KWA KAMPUNI YA NYANZA KUMALIZA MIRADI WALIYOIANZISHA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii.

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Mkonda ametoa mwezi mmoja sambamba  na kutopewa kazi nyingine kwa  Kampuni ya Nyanza hadi pale watakapomaliza miradi walioianza.Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua miradi ya ujenzi wa barabara za halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja inatakiwa kukamilika ndani ya miezi 15 lakini hadi sasa ni miezi 11 ujenzi hauridhishi."Mkataba uliosainiwa ni wa miezi 15 hadi sasa ni miezi 11 mradi unasuasu na hauridhishi" amesema Makonda

"Nnaagiza kwa halmashauri zote kampuni hii ya Nyanza isipewe kazi yoyote kwenye Mkoa wangu hadi watakapokamilisha miradi mitatu waliyoianza," ameongeza.Mkurgenzi wa manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa kusuasua hivyo wajitathimini kwa kuwa kwenye halmashauri hiyo hawatapa nafasi.

"Nilipofika Temeke niliwaambia kwenye halmashauri yangu ujanjaujanja hakuna hivyo wajitafakari kwa kina kwani nnaweza kuvunja mkataba," amesema
 Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kutoa agizo la mwezi mmoja kwa kampuni ya Ujenzi ya Nyanza kukamilisha  miradi ya ujenzi barabara ya Chang`o wilayani Temeke jijini Dar es salaam(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mkuu wakoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambata na mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Mkurugenzi wa wilaya ya Temeke,Lusubilo Mwakabibi pamoja na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maji wa DAWASA, Mhadisi Aron Joseph wakikangua miradi mbalimbali inayojengwa na DMDP leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maji wa DAWASA, Mhadisi Aron Joseph akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ziara ya kukangua miradi mbalimbali inayojengwa DMDP wilaya ya Temeke.

Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi barabara 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA CHINI

MAKAMU WA RAIS AMALIZIA ZIARA YAKE WILAYA YA BUHIGWE MKOANI KIGOMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiuandaa mti kabla ya kuupanda kwenye shamba la miti la Buhigwe, kushoto anayemsaidia Makamu wa Rais ni Meneja Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kanda ya Magharibi Bw. Valentine Msusa
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu alioupanda kwenye shamba la miti la Buhigwe katika kijiji cha Munzenze wilaya Buhigwe mkoani Kigoma.
  Sehemu ya miche laki mbili na nusu iliyopandwa kwenye shamba la miti Buhigwe mkoani Kigoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wanaoishi jirani na  shamba la miti la Buhigwe katika kijiji cha Munzenze wilaya Buhigwe mkoani Kigoma.
 : Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Mbunge wa Jimbo la Buhigwe Mhe. Albert Obama wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Munzenze, Buhigwe mkoani Kigoma.
  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubiwa wananchi katika kijiji cha Munzenze, Buhigwe mkoani Kigoma.
Sehemu ya Wakazi wa kijiji cha Munzenze waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mwanafunzi Chuo Kikuu Iringa ashinda Milioni 239.4 za M-Bet

$
0
0
 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Ibrahim Pius Mbwilo (28) ameshinda Sh 239,417,800 kupitia mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na kampuni ya M-Bet.

Mbwilo ambaye anasoma shahada ya Utawala wa Biashara (Business Administration) akiwa mwaka wa pili, alibashiri kiusahihi mechi 12 za ligi mbalimbali za ulaya. Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa Mbwilo ambaye ni shabiki wa timu ya Simba na Chelsea ya Uingereza, amekuwa mshindi wa pili kupata fedha nyingi zaidi tokea kuanzishwa kwa droo ya Perfect 12. Mshindi wa kwanza alipata Sh 280 millioni.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwasaidia watanzania kubadili maisha yao kwa kutumia Sh1,000 tu. “Nawaomba Watanzania kuendelea kubashiri kwa kutumia michezo yetu,kuna nafasi kubwa ya kushinda na mpaka sasa tumepata jumla ya washindi 10 ambao wamefaidika na droo yao,” alisema Mushi.

Alisema kuwa Serikali imepata Sh 47 millioni kutokana na kodi kutokana na ushindi huo wa Mbwilo. Akizungumza baada ya kupokea hundi yake, Mbwilo alisema kuwa amefarijika sana kupata fedha hizo ambazo atazitumia kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo, kuwasomesha ndugu zake na kusaidia familia.

Mbwilo alisema kuwa pia atatumia fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza biashara yake ya kuuza matofali na kuanzisha biashara nyingine. Alisema kuwa yeye ni mtoto yatima na aliishi maisha ya mitaani huku akiokota taka na kuziuza kama mbolea (samadi) kwa akina mama ambao walikuwa wateja wake kwa lengo la kumsaidia.

“Niliishi mitaani, nilikwenda jalalani kutafuta matunda, taka, kutafuta taka na kuziuka kama mbolea, nilifanya hivyo baada ya kuachwa na mlezi wangu nikiwa kidato cha pili, naguswa na aina hiyo ya watoto yatima hiyo. “Tarehe 6 mwezi huu, nilitumia sh 1,000 kubashiri na kupata kiasi kikubwa cha fedha, namshukuru Mungu kwani wanaobashiri wengi, nitasaidia kituo cha watoto yatima kwa kunua magodoro, kuna kituo cha watoto yatima ambao hawana vitanda hata magodoro, nitafanya hivyo kwa sababu mimi mwenyewe nimetokea huko,” alisema Mbwilo.

 Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Ibrahim Mbwilo (28) ambaye ameshindia Sh milioni 239.4. Mbwilo ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Chuo Kikuu Cha Iringa. Picha: Mpigapicha wetu 

KAMATI YA MAADILI YA TAIFA YAITAKA CHADEMA KUTEKELEZA MAAMUZI YALIYOTOLEWA NA KAMATI YA MAADILI JIMBO LA UKONGA.

$
0
0

Kamati ya Maadili ya Uchaguzi Ngazi ya Taifa, imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiendelee kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo la Ukonga yaliyokitaka chama hicho kusahihisha makosa yaliyotendeka na kuomba msamaha hadharani kwa kosa la kimaadili walilotenda.

Uamuzi huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jaji Mst. Mary Longway baada ya kikao cha kamati hiyo kupitia na kujadili rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Maadili Jimbo la Uchaguzi Ukonga, iliyowasilisha na Chadema Septemba 5, 2018 ikiitaka kamati hiyo itengue uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Jimbo.

Alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyoambatishwa katika Rufaa hiyo, Kamati ya rufaa imefikia maamuzi ya kuwa rufaa hiyo imewasilishwa nje ya muda wa saa 48 kinyume na maelekezo ya kipengele cha 5.7 (b) cha Maadili tajwa.

“Rufaa iliyowasilishwa yenye Kumb. Na. CDM/ILALA/MAADILI/2018/28 ya tarehe 5 Septemba, 2018 iliyopokelewa Tume tarehe 7 Septemba..Imewasilishwa nje ya muda wa saa 48 kinyume na maelekezo ya kipengele cha 5.7 (b) cha Maadili tajwa. Hivyo, Kamati inaelekeza kuwa mrufani aendelee kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo.”, alisema Jaji Mst. Longway.

Kwa mujibu wa uamuzi wa Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo la Ukonga, Chadema kimeonywa kuhakikisha kuwa kinafuata Kanuni na Taratibu za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 na kutekeleza maamuzi hayo ndani ya saa 48 tangu kutolewa na adhabu hiyo.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga Jumanne Shauri mnamo Agosti 27, 2018 alipokea malalamiko na kupitia utetezi wa Chadema na kujiridhisha kuwa Chadema kilitumia kiongozi wa dini kumpigia kampeni mgombea wa chama hicho kinyume na kifungu cha 2.2 (k) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.

Msimamizi huyo wa Uchaguzi aliongeza kuwa “Dr. Makongora Mahanga akiwa kiongozi wa Chadema, siku ya kampeni tarehe 25/8/2018 alitumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji dhidi ya mgombea wa CCM, ikiwa pia ni kinyume na kifungu cha 2.2 (k) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015” aliongeza taarifa ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Jimbo hilo”

Mbali na uamuzi juu ya rufaa hiyo, Kamati hiyo pia imepitia barua ya tarehe 5 Septemba, 2018 iliyowasilishwa Tume tarehe 7 Septemba, 2018 kupinga maelekezo ya Kamati ya Maadili Jimbo la Ukonga yaliyokiagiza Chadema kuwasilisha ndani ya Saa 48 kuanzia tarehe 4 Septemba, 2018 vielelezo vilivyothibitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano na wataalamu wa lugha ya Kikurya ili kutoa maamuzi ya shauri husika.Akizungumzia barua hiyo, Jaji Mst. Longway alisema baada ya kupitia vielelezo na kujadili barua husika, imeamuliwa kuwa rufaa hiyo imekosa sifa kwa kuwa hakuna maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Maadili Jimbo la Ukonga.

Kutokana na jambo hilo, Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Taifa imekielekeza Chadema kuwasilisha vielelezo Kamati ya Maadili ya Jimbo la Ukonga kwa uamuzi kama ilivyoelekezwa na Kamati husika.

MKUU wa Dar es Salaam Paul Makonda atoa mwezi mmoja kwa kampuni ya Ujenzi ya Nyanza kukamilisha miradi ya ujenzi ya DMDP

$
0
0
 Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya agizo la mwezi mmoja kwa kampuni ya Ujenzi ya Nyanza kukamilisha  miradi ya ujenzi barabara ya Chang`ombe wilayani Temeke na kwamba ikishindwa kutekeleza agizo la serikali itasitsha mkataba na haitapewa tenda tena katika  Mkoa Dar es Saĺaam.
 Mkuu wakoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambatana  na mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva,Mkurugenzi wa wilaya ya Temeke,Lusubilo Mwakabibi pamoja na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maji wa DAWASA, Mhadisi Aaron Joseph wakikangua mira mbalimbali inayojengwa na DMDP leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maji wa DAWASA, Mhandisi Aaron Joseph akifafanua kambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ziara ya kukangua miradi mbalimbali inayojengwa na DMDP leo katika ziara ya kukangua miradi ya mbalimbali wilaya ya Temeke.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi barabara

Ukaguzi wa daraja
(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)


Mwanamuziki Abbu Omar aachia ' kitabu cha "Maisha yangu na Bendi za Wanyika” mkongwe Abbu Omar

$
0
0
Mimi ni Abbu Omar, mwanamuziki mkongwe aliyewaji kupiga Bendi za Simba Wanyika / Les Wanyika kutoka 1981 – 1992. Pia nilishiriki katika recordings za Album nyingi maarufu kama “Mwana sikia”,  “Sikujua kama utabadilika”, “Haleluya”, “Shilingi yaua”, “Baba Asia”, “Mapenzi ni Damu”, “Mapenzi ya Weekend” na kadhalika.
Hivi sasa  Abbu Omar ameandika kitabu cha historia ya bendi za Wanyika kinachoitwa “ Maisha yangu na Bendi za Wanyika” Kuanzia bendi ya Young Nyamwezi Jazz 1958 (Tanga), Jamhuri Jazz 1964, Arusha jazz 1972, Simba Wanyika 1973, Les Wanyika 1978, Super Wanyika By Issa Juma 1981, Hadi mwisho wa Les Wanyika wakati wa kifo cha John Ngereza  mwaka 2002.
Kitabu hiki chenye kurasa 248 na picha za matukio mbalimbali, Kinapatikana:
Zanzibar Bookshop – Kariakoo jijini Dar es salaam – Shule ya Uhuru, Karibu na Ghorofa Kubwa la China Plaza
Simu: 0713 3523248
Mtaa wa Samora Opposite J-Mall njia panda ya Samora na Morogoro Road jijini Dar es salaam.
Simu: 0715520701
Mtoni Kwa Azizi Ally: Round About, Yerusalem Stationary, jijini Dar es salaam.
Simu: 0782387838 George
Mtoni Kwa Azizi Ally- Internet, Katika Fremu iliyopo kwenye Nyumba ya Mzee King Kikii.
Sheikh Hando - Simu 0719 529292
Mwananyamala – Komakoma karibu na Biashara Complex / Kambi ya Akudo Impact band
Simu 0715681838 - Timothy
Kitabu cha "Maisha yangu na Bendi za Wanyika” cha Abbu Omar
Kitabu cha "Maisha yangu na Bendi za Wanyika” cha Abbu Omar
Ankal akiwa na mtunzi wa kitabu cha"Maisha yangu na Bendi za Wanyika” mkongwe Abbu Omar alipokuwa likizo jijini Dar es salaam mwaka 2010 akitokea nchini Japan alikokuwa akiishi na kufanya kazi
Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa na mumewe Bw. Khamsin (kushoto) na Keppy Kiyombile wa The Kilimanjaro Band Wana Njenje wakiwa na mtunzi wa kitabu cha"Maisha yangu na Bendi za Wanyika” mkongwe Abbu Omar alipokuwa likizo jijini Dar es salaam mwaka 2010 akitokea nchini Japan alikokuwa akiishi na kufanya kazi
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images