Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA ASKOFU MKUU WA KANISA LA ANGIKANA TANZANIA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Maimbo Willium Mndolwa (kulia) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Viongozi mbali mbali wa Kanisa hilo, Septemba 10, 2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania ulioongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dkt. Maimbo Willium Mndolwa (wa nne kushoto) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Viongozi mbali mbali wa Kanisa hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania ulioongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dkt. Maimbo Willium Mndolwa (wa tatu kushoto) babada ya mazungumzo wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Viongozi mbali mbali wa Kanisa hilo. Picha na Ikulu, Zanzibar.

SPIKA NDUGAI AZINDUA FILAMU ILIYOANDALIWA NA TAKUKURU KUELIMISHA JAMII JUU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) wakionesha kwa Waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) CD za Filamu ya ‘Bahasha’ mara baada ya kuizindua. Filamu hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akikata utepe kuzinduzi Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wakwanza kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia uzinduzi Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. PICHA NA BUNGE

WATAALAM WA AFYA KUTOKA MAREKANI WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (kushoto) akizungumza na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani Dkt Deborah Stith. 

Wataalam wa Afya kutoka Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa hospitali hiyo lengo likiwa ni kushirikiana katika utoaji wa huduma za afya. 

Ujio huo wa wataalam 9 umeongozwa na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani, Dkt. Deborah Stith akiwa na wataalamu hao wakiwemo madaktari wa macho, mfumo wa mkojo na meno. Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema lengo la ugeni huo ni kuangalia jinsi ambavyo pande hizi mbili zinavyoweza kunufaika kwa kujenga mahusiano katika ufundishaji ,kuboresha huduma pamoja na utafiti. 

“Ushirikiano ambao tunautafuta hasa ni katika nyanja ya ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuwaongezea ujuzi madaktari wetu katika sehemu tulizokuwa tunafikiri kutoa huduma ambazo tulikuwa hatutoi awali” Amesema Prof. Museru. 

Aidha Dkt. Deborah Stith amesema wako tayari kushirikiana kwa karibu na Muhimbili kwa kubadilishana wataalam kwa manufaa ya jamii.
Wataalam kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani pamoja na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini katika mkutano huo.  
Baadhi ya wakurugenzi wa (MNH) wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo Mkuu wa Idara ya Macho Dkt. Mtemi Baruani (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo (kulia). 

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 10.09.2018

MICHUZI TV DIRA YA KITAA : TOFAUTI YAMPIGA PICHA NA PHOTOGRAPHER...

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU SEPTEMBA 10, 2018

WANAFUNZI WATANO WAIBUKA KIDEDEA SHINDANO LA ANDIKA CHALLENGE

$
0
0

Taasisi ya Dr Ntubayaliwe imepongezwa kwa Kubuni shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi, kitendo kinachosaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi nchini.

Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga ametoa pongezi hizo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la Andika Challenge la kutunga hadithi zenye maana kwa wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za Kinondoni na Ubungo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi. Jacquiline Mengi amesema baada ya kuendesha shindano hilo kwa manispaa mbili za Dar es salaam kwa mafanikio makubwa, sasa shindano hilo litawashirikisha  wanafunzi wa shule za msingi za Tanzania nzima.

Amesema shindano hilo litadumu kwa miezi mitatu na washiriki wanatakiwa watume hadithi  kupitia sanduku la barua 163, Dar es salaam, huku kila mshiriki aandike jina lake, jina la shule yake, wilaya na mkoa atokao, na mwisho wa kuwasilisha hadithi ni mwezi Novemba mwaka huu. Hadithi zitakazoshinda zitachapishwa kwenye vitabu na kusambazwa katika maktaba mbalimbali za shule.

 Jumla ya hadithi 1,202 kutoka wanafunzi wa shule za msingi 137 za manispaa za Kinondoni na Ubungo zilipokelewa na kushindanishwa, ambapo  Mshindi wa kwanza alikuwa  Nurath Komba kutoka shule ya msingi Tandale Magharibi.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Agnes Charles wa shule ya msingi Uzuri, huku Arsernia Charles akishika nafasi ya tatu, na Zulfa Miraji wa shule ya msingi Mtangani, na Aisha Hialai wa shule ya msingi Londa wakishika nafasi za nne na ya tano. Washindi wote na shule wanazotoka walikabidhiwa zawadi mbalimbali, zikiwemo kununuliwa sare za shule na vitabu kwa mwaka mzima, kufunguliwa akaunti ya benki.
Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi wa washindi wa shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi lililohisisha wilaya mbili za jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi. Jacquiline Mengi akitoa historia ya taasisi ya Dr Ntuyabaliwe pamoja na shindano la shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi lililohisisha wilaya mbili za jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kwenye shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi, Nurath Komba kutoka shule ya msingi Tandale Magharibi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi. Jacquiline Mengi.
Baadhi ya wanafunzi walioingia kwenye tano bora ya shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi wakipokea zawadi zao zilizodhamniwa na taasisi ya Dr Ntuyabaliwe lilihusisha wilaya ya Kinondoni na Ubungo.
Meza kuu ingiongozwa na Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha  Kusaga akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi watano walioibuka kidedea kwenye shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi lililoshirikisha shule mbalimbali zilizopo kwenye wilaya mbili za jijini Dar es Salaam.
Walimu wa shule zilizotoa washindi watano wa shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuumara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

FARU WAWEKEWA ULINZI KWA KUFUNGWA VIFAA VYA UTAMBUZI

$
0
0
Na Lusungu Helela
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amesema kutokana na kukua kwa teknolojia ya Kisasa, Maafisa wanyamapori watakuwa na uwezo wa kuwaona faru popote walipo wakati wakiwa wamekaa ofisini hali itakayosaidia kuwalinda wanyamapori hao ambao wapo hatarini kutoweka.

Pia amesema Maofisa hao watakuwa na uwezo wa kufuatilia mienendo ya wanyama hao pale walipo na popote wanapoenda ili kujua kama wanaumwa au wanatatizo lolote hali itakayosaidia kwenda kutoa huduma ili wanyama hao waendelee kuishi. 

 Mhe. Hasunga amezungumza hayo alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mara baada ya kushuhudia zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
 Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu sana kwenye uhifadhi wa wanyamapori hali itakayopelekea majangili kukamatwa hata kabla hawajamuua faru. 

 Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa faru katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Phillibert Ngoti amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa zoezi hilo la uwekaji alama za vifaa vya kisasa unafanywa katika Hifadhi hiyo kwa kushirikina na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA) Frunkfurt Zoological Society( FZS) pamoja Friedkin Conservation Fund ( FCF) .

 Bwana Ngoti amefafanua kuwa zoezi la uwekaji wa vitambuzi hivyo kwenye faru unafanyika kwa namna mbili, kuna vitambuzi vinavyowekwa ndani ya pembe za faru na pia kuna vitambuzi vinavyowekwa kwenye mguu mmoja wa mbele wa faru ili kusaidia kujua popote pale walipo. 

 Kwa upande wake, Kiongozi wa Mradi wa Uhifadhi kutoka FZS, Rian Habuschagne amesema mradi huo umefadhiliwa na Frunkfurt Zoological Society kwa kushirikiana na Friedkin Conservation Society. 

 Bwana Habuschagne ameeleza kuwa, wameweza kusaidia helkopta, mahema, kumlipa rubani, chakula kwa askari wanyamapori pamoja na magari na hadi kukamilika kwa mradi huo unaweza kugharimu zaidi ya bilioni moja. 

 Ameongeza kuwa utaratibu wa uwekaji vitambuzi kwa faru umekuwa pia ukifanyika nchini Afrika Kusini hali iliyosaidia sana katika kuwalinda faru. Aidha, Daktari wa Wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Alex Muse anayeshiriki katika zoezi hilo amesema kuwa zoezi la uwekaji vitambuzi kwa faru lina changamoto zake lakini kwa vile kuna timu nzuri kwa ajili ya kazi hiyo hivyo imekuwa kazi nyepesi kwao.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akishiriki katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akishiriki katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akiwa na wataalamu na askari wa wanyamapori baada ka kushiriki katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 
Faru akipozwa na maji katika zoezi la uwekaji wa vifaa vya utambuzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa faru waliopo katika Hifadhi hiyo. 


Serikali yafikia hatua za mwisho kukamilisha Sera ya Michezo - Dkt. Mwakyembe

$
0
0
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Serikali imefikia hatua za mwisho za kukamilisha rasimu ya Sera ya   Maendeleo ya Michezo baada ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau ndani na nje ya nchi na ni matarajio ya wizara kukamilisha zoezi hili ndani ya muda mfupi.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge Rashid Shangazi wa Mlalo (CCM) aliyeuliza kuwa ni lini serikali itakamilisha Sera ya Michezo.
“Zoezi la kupitia upya Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 ni zoezi ambalo limehusisha ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa michezo na   tayari rasimu kamili ya Sera hiyo imefikia hatua nzuri.”Alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha Mhe. Mwakyembe ameongeza kuwa  Sera ya Michezo itakapokamilika itasaidia kuleta mabadiliko mengi ya kisera ikiwemo kuibuka kwa michezo ya kulipwa,mahitaji ya shule na vyuo mahususi vya michezo mbalimbali  kwa lengo la kulea vipaji toka utotoni pamoja na uhitaji wa viwanja vizuri na vya kutosha ngazi za shule za msingi,sekondari, vyuo na sehemu za kazi.
Pamoja na hayo katika swali la nyongeza la Mbunge huyo wa Mlalo lililohoji kuhusu ushirikishwaji wa wabunge katika uandaaji wa Sera hiyo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa wizara itaandaa utaratibu wa kuweza kuwashirikisha wabunge katika kutoa maoni yao.
Mheshimiwa Mwakyembe ameongeza kuwa Sera mpya itasaidia kuleta mabadiliko chanya katika tasnia ya michezo nchini ikiwa ni pamoja na kubadili sheria iliyoanzisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili iweze kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa michezo nchini pamoja na kuanisha vyanzo rasmi vya mapato katika michezo.

Hata hivyo Waziri huyo mwenye dhamana na michezo nchini  ametoa wito kwa Taasisi,Mashirika ya Umma,Vilabu na vyama vya michezo kutunza na kufanyia ukarabati viwanja vyote vinavyomiliki ili viwe na ubora unaotakiwa katika michezo
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo   Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza leo Bungeni Jijini Dodoma.

Kwa Simu Toka London- Na Freddy Macha: Vitabu Mahiri Vya Kiswahili

$
0
0
Mwandishi nguli wa Kiswahili - Mohammed S Mohammed- aliwahi kupata tuzo mbalimbali na kuzawadiwa na Mwalimu Nyerere (1970) na Kenyatta (1973). Ingawa alichapisha vitabu vitatu tu Mohammed S Mohammed yumo ndani ya kundi la wanafasihi majabali - Shaaban Robert, Adam Shafi, Said Ahmed Mohammed, Euphrase Kezilahabi, nk. Baada ya zaidi ya miaka 40 vitabu vyake vipya vimetolewa upya na shirika la uchapishaji vitabu Nairobi, Sasa Sema Vitabu hivi ni Kiu, Nyota ya Rehema na Kicheko cha Ushindi ... Tungependa kufahamu yu wapi?

Mikocheni veterans kushiriki katika michezo ujirani mwema nchini Rwanda

$
0
0
Timu ya Mikocheni veterans ya jijini Dar es salaam (pichani) itashiriki katika tamasha maalum ya ujirani mwema lililopangwa kufanyika Kigali, Rwanda,  kuanzia Septemba 22. 

Timu hiyo inatarajia kuandoka nchini Septemba 19, ikiwa na wachezaji na mashabiki 23 kwa ajili ya safari hiyo kwa mujibu wa Seneta wa timu hiyo, Yassin Ally Yassin.

Yassin alisema kuwa mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Karibu Sports Club ya Rwanda Septemba 24 na mechi nyingine zitafuatia.
Aliwataja wachezaji wanaondoka kuwa ni Adam Mohamed Mselem, Fumu Mahamud, Dornad Mtoka, winchande  Chambuso, Ally Salim, Adnan Juma, Omary Mkuku, Jumanne Mnkumbu na Hamis Kisukari.
Wengine ni Agapiti Manday,  Fikir  Muhango, Belanus  Komba, Eric Frederic , Ian Balegele, Timothy Kipilimba, Abdul Hamis Said, Suleima  Masatu, Nassoro Abdul  Mwinchui,  Hassan Mbegu Mohamed, Neema Visent Msema na Witness David Mbingi.
Viongozi ambao wataambatana na timu hiyo ni Chriss Chale ambaye ni Mweka Hazina, Adam Mselem (Seneta) na Aidan Mshani ambaye ni kocha. Alisema kuwa wamejiandaa vilivyo na wanatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki ili kujiandaa na tamasha hilo.
“Mpaka sasa tumejiandaa vilivyo na maandalizi ya safari yetu yanakwenda vizuri, morali ya wachezaji ipo juu na tunatarajia kupata ushindi huko Rwanda,” alisema Yassin.
Alisema kuwa mbali ya kushiriki tamasha la Rwanda, pia timu yao ina mipango ya kushiriki katika matamasha mengine ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ili kujifunza mambo mbalimbali na kudumisha ushirikiano na wadau wa soka.

TAA, MANISPAA YA ILALA, TANZANIA REMIX WAWALIPA FIDIA YA VIWANJA WANANCHI WA KIPUNGUNI B

$
0
0
Zoezi la upimaji likiendelea ili kuweza kuonyesha mawe ya upimaji kabla ya kumkabidhi Mwananchi husika mapema leo katika Mtaa wa Kidole kata ya Msongola.
Mmoja wa Wananchi kutoka Kipunguni ambaye ameoneshwa eneo lake akiwa amepiga picha katika eneo hilo  Mtaa wa Kidole kata ya Msongola mapema leo.
Baadhi ya Wananchi wa Kipunguni Mashariki na Kipunguni A wakiwa na Maofisa wakisubiri kupimiwa maeneo yao katika Mtaa wa Kidole kata ya Msongola mapema leo.
Picha na.
Wapima ardhi Masasu Magenyi (Manispaa ya Ilala) na Hemedi fundi (Tanzania Remix) wakisoma ramani za eneo hilo wakati wa kugawa maeneo hayo kwa Wananchi Mtaa wa Kidole Kata ya Msongola Wilaya ya Ilala mapema leo

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Manispaa ya Ilala,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Kampuni ya Tanzania Remix  imeanza kutekeleza agizo la Naibu Waziri Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi)  Mhandisi Atashasta Nditiye juu ya ulipaji wa fidia ya Viwanja kwa Wananchi wa Kata ya kipunguni A na Kipunguni mashariki.

Agizo hilo alilotoa Agosti 30 mwaka huu limeanza kutekelezwa leo  kwa Wananchi watokao Kipunguni Mashariki na Kipunguni A kwenda  mtaa wa Kidole na Luhanga kupewa viwanja 537 ndani ya kata ya Msongola ili kupisha mradi wa upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius  Nyerere(JNIA).

Awali Mhandisi Nditiye alitoa maagizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege  Bw, Richard Mayongela kushirikiana na Manispaa ya Ilala ,Mkuu wa Wilaya na Kampuni ya Tanzania Remix ambayo ilihusika na upimaji wa maeneo hayo kuhakikisha inawagawia Wananchi viwanja hivyo na kuhakikisha viwanja hivyo vina ubora.

“Mshirikiane na Tanzania Remix na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa kuwagawia Wananchi viwanja hivi vilevile  shirikianeni na  vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini  wafanyakazi wote wa TAA waliojiingiza kwenye mradi huu na kujipatia viwanja kinyume na utaratibu angali hawakuguswa na mradi huu wabainishwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria”alisema.

Safari Kishiwa na Evaline Malume ni miongoni mwa Wananchi walioanza kugawiwa viwanja hivyo nakuishukuru Serikali kutokana na maeneo hayo kuwa katika mazingira mazuri.
Wananchi hao walidai wanawashangaa baadhi ya wananchi wenzao walioathiriwa na mradi huo kukimbilia mahakamani kwasababu mbalimbali  zisizo na mashiko.

"Tuwaombe tu wenzetu wafute kesi waje wachukue viwanja viwanja hivi vipo kwenye mazingira mazuri tofauti na wanavyofikiri"walisema.

WATAALAM WA AFYA KUTOKA MAREKANI WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (kushoto) akizungumza na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani Dkt Deborah Stith. Wataalam kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani pamoja na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini katika mkutano huo. Baadhi ya wakurugenzi wa (MNH) wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo Mkuu wa Idara ya Macho Dkt. Mtemi Baruani (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo (kulia).

 Na Mwandishi Wetu.
WATAALAM wa Afya kutoka Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa hospitali hiyo lengo likiwa ni kushirikiana katika utoaji wa huduma za afya.

Ujio huo wa wataalam 9 umeongozwa na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani, Dkt. Deborah Stith akiwa na wataalamu hao wakiwemo madaktari wa macho, mfumo wa mkojo na meno.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema lengo la ugeni huo ni kuangalia jinsi ambavyo pande hizi mbili zinavyoweza kunufaika kwa kujenga mahusiano katika ufundishaji ,kuboresha huduma pamoja na utafiti.

“Ushirikiano ambao tunautafuta hasa ni katika nyanja ya ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuwaongezea ujuzi madaktari wetu katika sehemu tulizokuwa tunafikiri kutoa huduma ambazo tulikuwa hatutoi awali” Amesema Prof. Museru.

Aidha Dkt. Deborah Stith amesema wako tayari kushirikiana kwa karibu na Muhimbili kwa kubadilishana wataalam kwa manufaa ya jamii.

WATANZANIA WAOMBWA KUSHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA SEPT 15, 2018

$
0
0
 Mjasiriamali na Mtoleaji (Volunteer) Kampeni ya Let’s Do it Tanzania, Fortunatus Ekklesiah (Katikati) akiwaomba Watanzania kujitokeza siku ya mazingira duniani September 15, 2018 katika maeneo yapatayo 33 ya Tanzania. Pembeni ni waratibu wa Nipe Fagio, Catherine Nchimbi (kulia) na Navonaeli Kaniki (kushoto). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Tanzania itashiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi tarehe 15 Septemba, 2018. Tukio hili litafanyika chini ya kauli mbiu ya “Let’s Do It”.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mjasiriamali na Mtoleaji (Volunteer) Kampeni ya Let’s Do it Tanzania, Fortunatus Ekklesiah amewaomba Watanzania kujitolea kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini na kujumuika na watu zaidi ya milioni 20 katika nchi 150 duniani kusherekea Siku ya Usafi Duniani ya kwanza kwa kusafisha maeneo mbalimbali ya umma hususani fukwe, njia za maji na mito.

Alisema usafi utafanyika katika maeneo 70 kwenye mikoa 16 hapa nchini ikiwemo Dar es salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Morogoro, Mwanza, Mtwara, Simiyu, Mbeya, Shinyanga na baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar.

Usafi utafanyika katika maeneo 33 yaliyopo katika manispaa zote za jiji la Dar es salaam na maeneo 37 yatafanyiwa usafi katika mikoa mingine. Baadhi ya maeneo ambayo yatafanyiwa usafi jijini Dar es salaam ni pamoja na Tandale Kwa Tumbo, Mto Mbezi, Mwembeyanga, Tabata Magengeni, Soko la Mikindu, na Mto Mlalakuwa.

“Let’s do It! Ni kampeni ya usafi ya kidunia iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili. Ni mpango mkubwa zaidi wa watu kufanya shughuli ya kiraia kwa kujitolea kuwahi kufanyika duniani. Wazo hili lilizaliwa nchini Estonia mwaka 2008 na Tanzania inashiriki katika kampeni hii kwa mara ya kwanza mwaka huu,” alisema Ekklesiah.

Nae mratibu wa Nipe Fagio, Navonaeli Kaniki amesisitiza kuwaomba wananchi wote wajitokeze na kujumuika na sisi katika kufanya usafi katika maeneo ambayo yameathiriwa na taka nchi nzima.

“Ushiriki wa kila mmoja ni muhimu kwani mafanikio ya tukio hili yanatokana na jinsi watu watakavyojitolea kushiriki kutokana na mapenzi tuliyonanyo kwa mazingira yetu na Tanzania yetu,” alisistiza.

Lengo la Siku ya Usafi Duniani sio tu kufanya usafi bali pia kuongeza uelewa wa madhara ya tatizo la taka na uchafuzi wa mazingira kutokana na plastiki hapa nchini na kidunia. Vilevile siku maadhimisho ya siku hii yamelenga kuandaa jamii ya kizazi kipya cha viongozi wa jamii ambao wanaweza kufanya kazi kwa pamoja na kumaliza tatizo la taka.

MATUKIO YA BUNGENI SEPTEMBA 10,2018

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.
 Naibu Waziri wa Fedha,Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 10, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wakazi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao

$
0
0
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakazi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kujitambua na pia kutaisaidia Serikali kuwa na takwimu kamili za afya na kurahisisha utoaji huduma kwa waathirika.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano wa Kazuramimba, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.

Pia alihimiza wakina mama kuzingatia lishe bora kwa watoto kuepuka athari za udumavu “Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa uzalishaji chakula ni mkoa ambao hautuumizi kichwa katika kutafuta chakula cha Watanzania, unajitosheleza kabisa lakini kuna tatizo la lishe duni hasa kwa watoto”alisema Makamu wa Rais.

Takwimu zinaonyesha mpaka mwaka 2015 kiwango cha udumavu katika mkoa wa Kigoma ni asilimia 37.9

Makamu wa Rais amewaambia wakazi wa Kigoma kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa hasa kwa wageni wanaotoka nchi jirani ya Congo ili Taasisi za Serikali zifanye kazi yake haswa katika kuzuia waathirika wa ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

“Mgeni anapokuja semeni amekuja mgeni ili taasisi ya serikali zifanye kazi yake,kazi ya kuhakikisha mgeni aliyeiingia yupo msafi anakaa wapi, ataishi na nani, hatukatai wageni lakini toeni taarifa tuwajue na hii ni kwa faida yetu kama Taifa lakini yenu kama wana Kigoma, wana Uvinza ni kwa faida yenu wenyewe tunawalinda na maradhi, tunawalinda na uharamia,tunawalinda na mambo chungu mzima ya kiusalama wenu kwa hiyo ndugu zangu msifiche wageni wanapokuja tuambieni ili tuweze kuchukua zinazostahili”. Alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya awamu ya tano imeamua kutumia pesa zake za ndani kwenye vipaumbele vikubwa vya Kitaifa katika ununuzi wa ndege, umeme wa kudumu na uhakika, kupeleka maji kwa wananchi, elimu bure pamoja na kuboresha huduma za afya na kuhakikisha madawa yanapatikana kwa urahisi.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Kigoma aliwaambia wananchi wa mkoa huo kuwa Kodi zinazokusanywa na Serikali ndizo zinajenga miundo mbinu.Maelezo ya Picha:


10: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipungia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa mikutano tayari kuhutubia mkutano wa hadhara jana jioni katika kata ya Kazuramimba,wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SPIKA NDUGAI AZINDUA FILAMU ILIYOANDALIWA NA TAKUKURU KUELIMISHA JAMII JUU YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (katikati) akizungumza na Waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wa pili  kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza  kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akikata utepe  kuzinduzi Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wakwanza kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza  kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) wakionesha kwa  Waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) CD za  Filamu ya ‘Bahasha’ mara baada ya kuizindua. Filamu hiyo imeandaliwa  na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa. Wa pili  kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt. Mst. George Mkuchika, wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jasson Rweikiza na Wakwanza  kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brig. Jen. John Mbungo.
Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia uzinduzi Filamu ya ‘Bahasha’ iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 11, 2018

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AMETIMIZA AHADI ALIYOITOA JWTZ KWAAJILI YA UFUGAJI WA SAMAKI MKOANI MARA

$
0
0
  Katibu wa Rais Ngusa Samike akikabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni 40 kwa Mkuu wa kikosi cha 27KJ Luteni Kanali Js Mshashi kilichopo Makoko mkoani Mara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa fedha hizo Septemba 6,2018 alipokuwa ziara Mkoani humo kwaajili ya kuongeza Vizimba 10 vya kufugia Samaki.Makabidhiano hayo yamefanyika Jijini Dodoma mbele ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.Septemba 11,2018. 
Katibu wa Rais Ngusa Samike akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kukabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni 40 kwa Mkuu wa kikosi cha 27KJ Luteni Kanali Js Mshashi kilichopo Makoko mkoani Mara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa fedha hizo Septemba 6,2018 alipokuwa ziara Mkoani humo kwaajili ya kuongeza Vizimba 10 vya kufugia Samaki.Makabidhiano hayo yamefanyika Jijini Dodoma mbele ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.Septemba 11,2018.
PICHA NA IKULU

BONGO STAR SEARCH YAZINDULIWA RASMI, KUONESHWA KURUKA STARTIMES SWAHILI

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MSIMU wa Tisa wa mashindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS) umezinduliwa rasmi ikishirikiana na Kampuni ya Startimes jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wanahabari Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wanawapongeza BSS kwa kukuza vipaji toka msimu wa kwanza mpaka msimu huu ujao ambao unatarajia kuruka hewani hivi karibuni kupitia Startimes Swahili .

Malisa ameeleza mipango yao kushirikiana na Bss kuhakikisha inakuza vipaji na kunyanyua vijana kuonyesha vipaji vyao,  pia kipindi hiki ni chenye maudhui na kinaweza kutazamwa na rika zote .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark production ambae pia ni Jaji Mkuu Ritta Paulsen ameiomba Serikali kuangalia na kutoa mchango kwenye sekta ya muziki kwani inaongeza Pato la Taifa na wasanii wamekua wakiendesha maisha yao kupitia muziki.

Hivyo  amesema katika  msimu huu wanaomba ushirikiano kwa watanzania wote kwani wanaamini hiki ni kipindi kinachofatiliwa na watu wengi sana kwa hiyo vijana wajitokeze kuonyesha vipaji vyao.

Kuhusu ratiba ya usahili itakua mikoa mbalimbali kamaMwanza, Dar es salaam,  Arusha, Mbeya na usahili huo utaanza  Septemba na kauli mbiu ikiwa ni Jiongeze piga hatua.

Wakati huo huo mmoja wa wasanii ambao wameibuka baada ya kuibuliwa na  BSS  Kala Jeremaya amewapongeza Benchmark kwa kulirudisha shindano hilo na kueleza mafanikio ambayo amepata.

Amesema  kwani amekua akishirikiana na watu wakubwa kutoka mashirika mbalimbali kutokana na fursa ambayo amepata kutoka kwenye shindano na kumtambulisha vizuri na kumpa fursa kujulikana kwa urahisi zaidi huku akiendesha maisha yake kupitia muziki wake.
Uongozi wa Startimes Tanzania pamoja na  uongozi wa Bongo Star Search wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa kwa
shindano ya kusaka vipaji vya muziki Bongo Star search (BSS).
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live




Latest Images