Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

BODI YA KOROSHO YASHAURIWA KUZITUMIA TAASISI ZA KIJESHI ZA JKT MGAMBO NA JKT MARAMBA MCHAKATO WA UZALISHAJI WA MICHE YA KOROSHO

$
0
0
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya Tasnia ya zao la korosho kwa kipindi cha msimu wa miaka mitatu katikati ni  Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa na kulia ni Mrajisi Msaidizi vyama vya Ushirika Mkoa Tanga Jacklin Senzige
 Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa katika mkutano huo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza katika mkutano huo.
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Gwakisa Kasongwa katikati akiwa na wakuu wa wilaya wa wilaya za Kilindi Sauda Mtondoo kushoto kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa anayaafuata ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
BODI ya korosho Mkoa Tanga imeshauriwa kuzitumia taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba ili ziweze kusaidia katika mchakato wa uzalishaji wa miche ya mimea hiyo ya korosho.

Hayo yamezungumzwa  na Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella kwenye mkutano wa wadau wa zao la korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya Tasnia ya zao la korosho kwa kipindi cha msimu wa miaka mitatu.

Shigella alisema ili bodi hiyo iweza kukabiliana na uhaba wa miche katika Halmashauri zinazolima zao hilo lazima ifike wakati taasisi hizo ziweze kutumika kukabidhiwa mbegu kwa ajili ya kuzalisha miche hiyo.

“Jaribuni kuwasiliana na taasisi hizio za kijeshi ambazo wanawataalamu wa kuandaa vitalu wanaweza kuwasaidia kuzalisha miche mingi na iliyo na ubora unaotakiwa”Alisema Shigella.

Mbali na hilo pia alizitaka Halmashauri zote zinazolima zao hilo kuhakikisha zinatenga bajeti mapema ndani ya mwezi huu wa Sept kwa ajili ya ununuzi wa mbegu toka katika Taasisi ya Utafiti wa kilimo(Naliendele) kwa ajili ya uzalishaji wa miche ambayo inatarajiwa kusambazwa mwakani kwa wakulima wote
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

MWAKILISHI WA PAPA AWATEMBELEA JIMBO KUU LA TABORA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akizungunza na  Balozi wa Vatican nchini ambaye ni Mwakilishi wa Papa, Askofu Mkuu Marek Solczynski( wa pili kutoka kushoto) na  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Mhashamu Paul Ruzoka(katikati) wakati kiongozi huyo wa kiroho alipomtembelea Ofisi kwake jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwene koti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Vatican nchini ambaye ni Mwakilishi wa Papa, Askofu Mkuu Marek Solczynski( pembeni yake kutoka kulia) na  ,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Mhashamu Paul Ruzoka(wa pili kutoka kulia) na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wakati kiongozi huyo wa kiroho alipomtembelea Ofisi kwake jana.

 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora Mhashamu Paul Ruzoka(  )  akizungunza na  viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora mara baada ya Balozi wa Vatican nchini ambaye ni Mwakilishi wa Papa, Askofu Mkuu Marek Solczynski( pembeni ya Mkuu wa Mkoa) alipomtembelea Ofisi ya Mkoa huo jana.

Wananchi wa Mkuranga wanufaika na Kilimo

$
0
0
Na Emmanuel Massaka,Global ya jamii
WILAYA ya Mkuranga ni moja ya wilaya saba zilizopo mkoani pwani wakazi wake  wakijishughuisha sana na shughuli za kilimo ilikujipatia kipato.

Wilaya ya Mkuranga inalima mazao  mbalimbali ya biashara na ya chakula ikiwemo Mihogo,Mbaazi,Korosho Machungwa Ufuta Mananasi pamoja na Nazi.

Pia wananchi wa Mkuranga wanategemea sana kilimo katika uchumi wao ambapo moja ya zao lililoshika kasi ni korosho,wanasomesha watoto kupitia korosho pamoja na kukuza pato la mtu mmoja mmoja.

Akizungumza wilayani Mkuranga mkoani Pwani Umri  Manage  mkulima wa mihogo na bamia alisema kuwa  kilimo kimemsaidia kwani ndio kinachoendesha Maisha yake"mimi nalima bamia linaniongezea kipato changu cha kila siku pia namsaidia mume wangu baadhi ya majukumu"amesema.

Manage  alitoa wito kwa wanawake wote nchini kuacha kujibweteka na kuacha utegemezi masala yake wajishughulishe katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
 Mfanyabiashara na Mkulima wa Bamia,Umri Manage akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana Kilimo.Wananchi wakivuna Mihogo   kama walivyokutwa na kamera yetu

Wananchi  wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wakivuna Mihogo   kama walivyokutwa na kamera yetu.
Picha na Emmaniel Massaka wa Global ya jamii)

MWEZI MMOJA WA KAMPENI YA USAFI MILIONI 346 ZAPATIKANA, MAKONDA ALAANI MGAMBO KUPIGA RAIA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa taarifa ya kampeni ya usafi iliyoanza takribani mwezi mmoja uliopita katika kikao kilichohusisha wadau ya afya na mazingira.

Akizungumza katika kikao hicho Makonda amesema kuwa tangu kuanza kwa kampeni hiyo zaidi ya watu 1,0000 wamekamatwa, watu 4443 waliachiwa huru, 376 walipata dhamana na takribani watu 6577 walilipa faini iliyofikia shilingi milioni 346 na laki 6 ambapo nusu ya fedha hizo ilikuwa ni malipo kwa mgambo wanaosimamia usafi na hadi sasa watu 6 bado wapo mahakamani.

Aidha amesema kuwa yeye na wakuu wa Wilaya wamelaani kitendo cha mgambo wa kusimamia usafi kumpiga raia katika eneo la Bunju na wamefatilia na hadi sasa watuhumiwa wapo katika gereza la Segerea na amewataka mgambo hao kufanya kazi kwa kufuata na kusimamia sheria kwani hakuna sheria inayorusu kupiga raia.

Aidha amewashukuru wadau na wananchi hasa wale wanaofanya usafi bila shuruti na kuwataka Wakandarasi kufanya kazi kulingana na mikataba yao na kwa kampuni zilizodanganya katika mikataba yao wajiandae kulipa gharama hizo kwa serikali.

Sambamba na hilo Makonda amewataka wanajamii wa jiji la Dar es salaam kushiriki katika shughuli za usafi na kila mmoja wa nafasi yake ashiriki suala hilo na wao kama serikali ni wasimamizi na wawezeshaji na amewataka wafanyabiashara na wenye viwanda kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.

Pia Mkuu wa Mkoa ameeleza changamoto za mchakato huo ni pamoja na uchache wa watendaji na uchache wa mashine za EFD na ameeleza kuwa zoezi hilo ni endelevu katika kuhakikisha jiji linakuwa safi.

Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Abubakar Kunenge amesema kuwa suala la usafi ni wajibu wa kila mmoja na hakuna chaguo zaidi ya kuhakikisha jiji linakuwa safi na usafi ufanyike bila shuruti na uwe tabia ya kila mmoja na amewaomba wadau wa afya na mazingira kuhamasisha katika suala zima la mazingira.

Mkutano huo umeshirikisha wadau na taasisi mbalimbali za mazingira na kujadili namna ya kuweka jiji katika hali bora zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es SalaamPaul Makonda akizungumza leo na wadau mbalimbali wa usafi katika ukumbi wa Anatoglo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

 Sehemu ya wadau mbalimbali wa usafi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)

HALMASHAURI YA MKURANGA YARUDISHA ENEO LA DUNDANI

$
0
0
HALIMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani imelirudisha eneo la Dundani ililolichukua kwa madhumuni ya kufanya shughuli za uwekezaji wa viwanda na kulirudisha mikononi mwa wananchi.

Eneo lililorudishwa ni lenye ukubwa wa hekari 325 ambalo lilifanyiwa utahmini kati ya hekari 700 zilizochukuliwa na Halmashauri hiyo kwa lengo la kulifanya kuwa eneo la uwekezaji.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Dundani, ambao maeneo yao yalichukuliwa na Halmashauri hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga alisema kuwa nia ya serikali ilikuwa njema sana na sulala hilo liliangaliwa kwa umakini na viongozi wa Halmashauri hiyo.

Aidha alisema kwua viwanda vingi vilivyojengwa  katika wilaya hiyo vilijengwa kiholela hivyo kusababisha usumbufu na madhara kwa wakazi wa maeneo hayo ikiwemo kutiririsha maji machafu ya viwandani na kukosa njia za kupita.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na kamati teule ya wananchi wenye maeneo na wataalamu waliopo ofini kwake wataandaa barua ambayo itakabidhiwa kwa wenye maeneo kabla ya mwisho wa mwezi Septemba.

Sanga alisema serikali wilayani humo iliamua kulichukua eneo hilo ili kuepuka uwekezaji holela uliokuwa ukifanyika kwa kasi kutokana na wamiliki wa maeneo hayo kuyauza kwa kasi, kasi ambayo anasema hata hivyo kwa sasa imepungua sana.
Hata hivyo aliwaomba wamiliki wa eneo hilo kuepuka uwekezaji  wa kiholela pale watakapokabidhiwa rasmi maeneo yao.


Awali alijitokeza Muwekezaji kutoka nchini Misri aliyefika kaetika eneo hilo na kuahidi kurudi lakini hakufanya hivyo kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo mnamo mwaka 2014/2015.
Mwekezaji mwengine alitoka nchini China, yeye alitaka kuwepo kabisa miundombinu ya bara bara na umeme  vitu ambayo hata hivyo ilikuwa ngumu kwa serikali kwa sababu hata fidia ilikuwa haijatolewa kwa wenye maeneo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mshamu Munde alisema kuwa fidia ya kuwalipa wamiliki wa eneo hilo ni kiasi cha shilingi bilioni 7.9 huku mapato ya ndani ya Halmshauri kwa mwaka ni shilingi bilioni 3.8 hadi 4.3.
Mkurugenzi anasema awali wananchi walifikiri halmashauri ingekopa na kisha kuwafidia lakini hiyo suala hilo lisingewezekana kutokana na ufinyu wa mapato ya halmashauri.
akielezea matumizi ya mapato hayo ya ndani ambayo yanatokana na bidhaa za madini ikiwemo mchanga, bidhaa za kilimo, korosho, ufuta na bidhaa za misitu na ushuru wa viwandani.
matumizi ya wilaya hiyo ni pamoja na asilimia kumi kwa (Wanawake, vijana na walemavu), asilimia 60 inaenda miradi ya amendeleo vijijini, asilimia 20 mgao wa vijijini, asilimia 10 inatumiwa kwenye ufuatiliaji huku Akiba inayobaki ndio pengine ingelipa mkopo ambayo isingewezekana.

Akizungumzia uamuzi huo wa seikali Said Mohamed, mmoja wa wamiliki wa eneo hilo alisema uamuzi wa serikali hakuridhsiwa nao kwa vile maeneo hayo yamechukuliwa muda mrefu na kuahidiwa kulipwa fidia lakini leo wanaelezwa kuwa watarudishiwa.
Sande kauli imemvunja moyo na kumkatisha tamaa sababu wakati maeneo hayo yalipokuwa yanachukuliwa hakupenda, lakini kwa ushawishi wa serikali alikubali na kuahidiwa kulipwa Fidia baada ya miezi sita lakini sasa zaidi ya miaka minne wanaambiwa kuwa wanarudishiwa Ardhi kwa asilimia 100 hajafurahishwa nao.

KIDOMOLE FC YAICHAPA VIKAWE FC BAO 1-0

$
0
0
 Vikosi vya Timu za Vijiji vya Kidomole pamoja na Vikawe vikiwa katika picha ya pamoja na Mdhamini wao, Tippo Athuman a.k.a Zizzou (kati) kabla ya mtanange wao ulipigwa jana jioni katika uwanja wa Shule ya Msingi, Kidomole, Bagamoyo mkoani Pwani. Mchezo huo uliokuwa na mvuto wa waina yake, ulikuwa na leongo la kuunganisha undugu baina ya wanakijiji hao. Mchezo huo ulimalizika kwa Timu ya Kidomole kutoka kifua mbele kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0.
 Mdhamini wa Mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Kidomole FC na Vikawe FC, Tippo Athuman a.k.a Zizzou akitoa mawaidha kwa wachezaji wa timu zote mbili, kabla kabla ya mtanange wao ulipigwa jana jioni katika uwanja wa Shule ya Msingi, Kidomole, Bagamoyo mkoani Pwani. 
 Picha mbalimbalia za mchezo kati ya Timu ya Kidomole FC na Vikawe FC, ulipigwa jana jioni katika uwanja wa Shule ya Msingi, Kidomole, Bagamoyo mkoani Pwani. Mchezo huo uliokuwa na mvuto wa waina yake, ulikuwa na leongo la kuunganisha undugu baina ya wanakijiji hao. Mchezo huo ulimalizika kwa Timu ya Kidomole kutoka kifua mbele kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA DARAJA LA MTO SIBITI LINALOUNGANISHA MKOA WA SIMIYU NA SINGIDA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Mawaziri, Viongozi wa dini na Chama akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti lenye urefu wa mita 82 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 25 katika eneo la mto Sibiti Mpakani mwa Simiyu na Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Mawaziri, Viongozi wa dini na Chama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo itakayotumika katika mradi huo wa ujenzi wa Daraja la mto Sibiti.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Sibiti, Maswa na Singida katika eneo la mto Sibiti kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti lenye urefu wa mita 82 pamoja na barabara zake unganishi zenye urefu wa km 25.
 Wanachi mbalimbali kutoka Singida, Maswa, Sibiti wakishangilia wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Sibiti mpakani mwa mikoa ya Simiyu na Singida.
 Kikundi cha ngoma cha Lusanya kutoka Singida kikitumbuiza katika sherehe hizo.
Sehemu ya Daraja la mto Sibiti lenye urefu wa mita 82  upana mita 10.5 linalounganisha kati ya mikoa ya Simiyu na Singida kama linavyoonekana ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 70. PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI UVINZA MKOANI KIGOMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kigoma ambapo ametembelea Wilaya ya Uvinza.

Akiwa Wilayani Uvinza, Makamu wa Rais aliweza kutembelea mwalo wa Muyobozi uliojengwa kwa gharama za shilingi milioni 482 na kuzungumza na wananchi waliojitokeza kumlaki.

Pia alikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa Kituo cha Afya Uvinza ambapo shilingi milioni 400 zimetolewa kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Upasuaji, Jengo la X-Ray, Jengo la Wazazi, Maabara na Nyumba ya Mtumishi.

Mradi huu unalenga kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wote wa Wilaya ya Uvinza hasa kwa akina Mama Wajawazito na Watoto na unatekelezwa kwa kutumia njia ya “Force Account”.

Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Ruchugi kitongoji cha Kibaoni, Makamu wa Rais aliwataka wananchi wa Kigoma kuzingatia lishe bora kwa watoto kwani mkoa una chakula cha kutosha.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amewahimiza wananchi wa mkoa wa Kigoma kupima afya zao haswa wanaume pia aliwataka wananchi hao kutoa taarifa za wageni wanaonyesha kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya kuchakata dagaa kutoka kwa mmoja wa wachakataji Bi. Mwajuma Bakari Shingo wakati alipotembelea mwalo wa Muyobozi uliopo wilayani Uvinza mkoani Kigoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Athuman mwenye umri wa wiki mbili aliyelazwa katika kituo cha afya cha Uvinza, aliyembeba mtoto ni mama wa mtoto Esil Amour, Makamu wa Rais alitembelea kituo cha afya cha Uvinza ambapo kuna mradi wa upanuzi wa ujenzi wa kituo hicho. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Ruchugi kitongoji cha Kibaoni ikiwa sehemu ya ziara yake wilayani Uvinza mkoani Kigoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WATANZANIA WAOMBWA KUSHIRIKI SIKU YA MAZINGIRA SEPT 15, 2018

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Tanzania itashiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi tarehe 15 Septemba, 2018. Tukio hili litafanyika chini ya kauli mbiu ya “Let’s Do It”.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mjasiriamali na Mtoleaji (Volunteer) Kampeni ya Let’s Do it Tanzania, Fortunatus Ekklesiah amewaomba Watanzania kujitolea kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini na kujumuika na watu zaidi ya milioni 20 katika nchi 150 duniani kusherekea Siku ya Usafi Duniani ya kwanza kwa kusafisha maeneo mbalimbali ya umma hususani fukwe, njia za maji na mito.

Alisema usafi utafanyika katika maeneo 70 kwenye mikoa 16 hapa nchini ikiwemo Dar es salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Morogoro, Mwanza, Mtwara, Simiyu, Mbeya, Shinyanga na baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar.

Usafi utafanyika katika maeneo 33 yaliyopo katika manispaa zote za jiji la Dar es salaam na maeneo 37 yatafanyiwa usafi katika mikoa mingine. Baadhi ya maeneo ambayo yatafanyiwa usafi jijini Dar es salaam ni pamoja na Tandale Kwa Tumbo, Mto Mbezi, Mwembeyanga, Tabata Magengeni, Soko la Mikindu, na Mto Mlalakuwa.

“Let’s do It! Ni kampeni ya usafi ya kidunia iliyolenga kuondoa taka kutoka kwenye mazingira ya asili. Ni mpango mkubwa zaidi wa watu kufanya shughuli ya kiraia kwa kujitolea kuwahi kufanyika duniani. Wazo hili lilizaliwa nchini Estonia mwaka 2008 na Tanzania inashiriki katika kampeni hii kwa mara ya kwanza mwaka huu,” alisema Ekklesiah.
 Mjasiriamali na Mtoleaji (Volunteer) Kampeni ya Let’s Do it Tanzania, Fortunatus Ekklesiah (Katikati) akiwaomba Watanzania kujitokeza siku ya mazingira duniani September 15, 2018 katika maeneo yapatayo 33 ya Tanzania. Pembeni ni waratibu wa Nipe Fagio, Catherine Nchimbi (kulia) na Navonaeli Kaniki (kushoto). Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATAALAM WA AFYA KUTOKA MAREKANI WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (kushoto) akizungumza na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani Dkt Deborah Stith. Wataalam kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani pamoja na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini katika mkutano huo.

INTRODUCING "FASHIONISTA" BY CLICKER FT. MR BLUE

BASI LA MWENDOKASI LAPATA AJALI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Wananchi wakiangalia ajali ya basi la mwendo kasi lenye namba za usajili, T 967 DGV  iliyohusishwa na ajali ya barabarani na gari dogo lenye namba za usajili  T 584 DLA kwenye makutano ya Barabara ya Morogoro na Umoja wa Mataifa eneo la Faya Jijini Dar es Salaam, ambapo mwenye gari dogo inasemekana alikuwa akielekea Hospitali ya Taifa Muhimbili akimpeleka mgonjwa na wote wakitokea upande mmoja wa Faya na basi la mwendokasi likitokea Gerezani kueleke Ubungo.  Madereva na abiria wa magari yote mawili walisalimika
 Askari wa Usalama Barabarani (kulia) akikagua  ajali hiyo akiwa na wananchi wakiangalia ajali ya basi la mwendo kasi lenye namba za usajili, T 967 DGV  iliyohusishwa na Gari lenye namba za usajili T 584 DLA kwenye makutano ya Barabara ya Morogoro na Umoja wa Mataifa eneo la Faya Jijini Dar es Salaam

 Askari wa Usalama Barabarani (mwenye kofia nyeupe) akipiga simu kuomba gari maalumu ya kuvuta gari lililokuwa limegonga Basi la Mwendokasi eneo la Faya.

Gari lenye namba za Usajili T 584 DLA baada ya ajali kutokea eneo la Faya
Basi la mwendoa kasi baada ya kugongwa.  
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Article 1

TANGAZO LA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA DHAHABU MKOANI GEITA.

Taarifa ya hali ya Mfumuko wa Bei nchini kwa mwezi Agosti, 2018

$
0
0
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo akitangaza hali ya Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2018 leo jijini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa Habari walioshiriki kwenye ‘Press Conference’ ya kutangazwa kwa hali ya Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2018 leo jijini Dodoma.

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA GARI LA KUBEBA MBAO ROMBO

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Rombo.

WATU wanne wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Isuzu kuacha njia na kwenda kugonga ngema katika eneo la Kikelelwa wilayani Hai.

Waliofariki dunia wametambulika kwa majina ya Emanual Josephat Silayo (28) ,Viviano silayo (35) wakazi wa Mbomai Juu,Juma Idd (20) maarufu kama mwarabu na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Deolla .

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah aliyefika eneo la tukio amethibitisha kutokea kwa ajalo hiyo na kwamba dereva wa Lolri hilo lililokuwa limebeba mbao alikimbia kusiko julikana baada ya ajali..

"Jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kupoteza muelekeo kwa Lori hilo na baadae kugonga Gema ndipo watu waliokuwa wanekaa mbele walichomoka na kwenda kupigiza vichwa katika Gema na kupasuka"alisema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema gari hilo likiwa na shehena ya mbao lilikuwa likitokea eneo la West Kilimanjaro ,eneo maarufu kwa uchanaji wa mbao na kwamba lilikiwa likielekea Rombo kupitia njia ya Rongai.

"Ni gari la kubeba mbao lilikua linatoka West Kilimanjaro kupitia njia ya Kikelelwa wilayani Rombo ,Gari aina ya Isuzu likiwa na namba za usajili T 889 ACN lilimshinda dereva na kuacha njia na baadae kugonga ngema iliyosababisha watu wanne waliokuwemo katika gari hilo kufa papo hapo." alisema Kamanda Issah.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya ya Rombo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah akiangalia gari hilo wakati alipofika kwenye eneo la tukio.

RAIS MAGUFULI ATOA SALAMU ZA POLE KWA MAJERUHI SITA WA AJALI SIMIYU, WAKIWEMO WAANDISHI WATANO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akikabidhi salamu za pole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa Mwandishi wa habari wa AZAM TV, Bi Rehema Evance ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Septemba 09, 2018 wilayani Meatu, wakati Mhe.Rais akiwa ziarani mkoani humo.
Kutoka Kushoto Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dk t. Joseph Chilongani na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera wakimjulia hali, Mwandishi wa habari wa AZAM TV, Bi Rehema Evance ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Septemba 09, 2018, wakati Mhe.Rais akiwa ziarani mkoani humo.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa pole kwa waandishi wa habari watano wa Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani waliopata ajali katika wilayani Meatu, wakati akiwa ziarani wilayani humo, salamu ambazo zimewasilishwa kwa niaba yake  na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, ambaye aliwatembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu walikokuwa wakipatiwa matibabu.

Akiwasilisha salamu za Mhe.Rais,  jana jioni Mhe. Mtaka amesema magari matano ya Simiyu ya Serikali na gari binafsi yaligongana na watu sita wakajeruhiwa wakiwemo waandishi watano na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani  na kusisitiza kuwa Mhe. Rais ameguswa na jambo hilo, hivyo ametoa shilingi laki tano kwa kila majeruhi ili iwasaidie katika matibabu.

“...magari ya waandishi wa habari lakini kulikuwa na gari binafsi, baada ya msafara wa Rais kwa sababu ya vumbi,  dereva mmoja katika yale magari alisimama kutaka kuona njia vizuri, magari yaliyokuwa yakifuatana  matano yakagongana kwa nyuma, watu sita wakapata majeraha miongoni mwao walikuwepo waandishi wetu watano na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani”

“Mhe. Rais anatoa salamu zake za pole kwa majeruhi wote,  ameguswa sana na jambo hili hasa pale aliposikia kuwa sehemu ya majeruhi ni waandishi ambao tumekuwa nao pamoja katika ziara hii, wakafanya kazi kubwa ya kuuhabarisha Watanzania,  akaomba mimi kama Mkuu wa Mkoa nifikishe salamu zake za pole kwa niaba  yake kwa watu hawa sita” alisema.

Ameongeza kuwa Mkoa utaendelea kuchukua tahadhari kupitia jeshi la polisi hasa katika misafara ya viongozi na kuhakikisha kuwa wanajenga uelewa wa pamoja kwa madereva wakati wa maandalizi ya safari juu ya namna ya kuchukua tahadhari.

Rehema Evance ambaye ni mwandishi wa Azam TV amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua na kuona awape mkono wa pole ambao amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia katika kugharamia matibabu.

“ Kwanza namshukuru Mungu kwa kutujalia tukapona,  lakini kipekee napenda kumshukuru Mhe. Rais kwa kuona kuna haja ya kutusaidia katika hili, kwa hiki alichotoa Mungu ambariki sana kitatusaidia kwenye matibabu, tunaahidi kuendelea kuwahabarisha Watanzania na kuhakikisha yale yote yanayotendeka ndani ya nchi yanawafikia” alisema.

Ajali hii iliyotokea wilayani Meatu Septemba 09, 2018 imesababisha majeruhi sita ambao ni waandishi watano Rehema Evance (AZAM TV), Belensi China(ITV), Aidan Mhando(Channel Ten), Phaustine Fabian(Mwananchi), Mpiga Picha Samson Masunga pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani na hakuna kifo kilichotokea..

Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Hospitaliya Wilaya ya Meatu ambapo waandishi wa habari Rehema Evance (AZAM TV), Phaustine Fabian(Mwananchi), Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dkt. Titus Kamani waliruhusiwa na Belensi China(ITV), Aidan Mhando(Channel Ten), na Mpiga Picha Samson Masunga walipewa Rufaa kwenda Bugando kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa majeruhi hao waliopelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando wote wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu na leo Septemba 10, 2018  wameruhusiwa. 

Mikocheni veterans ndani ya michezo ujirani mwema nchini Rwanda

$
0
0
Timu ya Mikocheni veterans itashiriki tamasha maalum ya ujirani mwema lililopangwa kufanyika Kigali, Rwanda kuanzia Septemba 22. Timu hiyo inatarajia kuandoka nchini Septemba 19, ikiwa na wachezaji na mashabiki 23 kwa ajili ya safari hiyo kwa mujibu wa Seneta wa timu hiyo, Yassin Ally Yassin.

Yassin alisema kuwa mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Karibu Sports Club ya Rwanda Septemba 24 na mechi nyingine zitafuatia.

Aliwataja wachezaji wanaondoka kuwa ni Adam Mohamed Mselem, Fumu Mahamud, Dornad Mtoka, winchande  Chambuso, Ally Salim, Adnan Juma, Omary Mkuku, Jumanne Mnkumbu na Hamis Kisukari.

Wengine ni Agapiti Manday,  Fikir  Muhango, Belanus  Komba, Eric Frederic , Ian Balegele, Timothy Kipilimba, Abdul Hamis Said, Suleima  Masatu, Nassoro Abdul  Mwinchui,  Hassan Mbegu Mohamed, Neema Visent Msema na Witness David Mbingi.

Viongozi ambao wataambatana na timu hiyo ni Chriss Chale ambaye ni Mweka Hazina, Adam Mselem (Seneta) na Aidan Mshani ambaye ni kocha. Alisema kuwa wamejiandaa vilivyo na wanatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki ili kujiandaa na tamasha hilo.

“Mpaka sasa tumejiandaa vilivyo na maandalizi ya safari yetu yanakwenda vizuri, morali ya wachezaji ipo juu na tunatarajia kupata ushindi huko Rwanda,” alisema Yassin.

Alisema kuwa mbali ya kushiriki tamasha la Rwanda, pia timu yao ina mipango ya kushiriki katika matamasha mengine ya nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ili kujifunza mambo mbalimbali na kudumisha ushirikiano na wadau wa soka.

Kwa Simu toka London: VItabu Mahiri Vya Kiswahili

$
0
0
Mwandishi nguli wa Kiswahili - Mohammed S Mohammed- aliwahi kupata tuzo mbalimbali na kuzawadiwa na Mwalimu Nyerere (1970) na Kenyatta (1973). Ingawa alichapisha vitabu vitatu tu Mohammed S Mohammed yumo ndani ya kundi la wanafasihi majabali - Shaaban Robert, Adam Shafi, Said Ahmed Mohammed, Euphrase Kezilahabi, nk. Baada ya zaidi ya miaka 40 vitabu vyake vipya vimetolewa upya na shirika la uchapishaji vitabu Nairobi, Sasa Sema Vitabu hivi ni Kiu, Nyota ya Rehema na Kicheko cha Ushindi ... Tungependa kufahamu yu wapi?

MICHUZI TV: DIRA YA KITAA : TOFAUTI YAMPIGA PICHA NA PHOTOGRAPHER

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images