Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Makamu wa Rais ameyasema haya leo wakati wa sherehe za kusimikwa wakfu wa Askofu Mkuu Msaidizi pamoja na Maaskofu wane wa majimbo wa Kanisa la Pentekoste Motomoto, Mwanga mkoani Kigoma.
“Serikali imeweka mazingira rafiki kwa madhehebu ya dini nchini kuweza kutoa huduma za kijamii hususan elimu na afya” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kanisa kujiepusha na migogoro ya kiutawala ndani ya Kanisa na pia liepuke kuchanganya dini na siasa,
“Kazi kubwa ya Kanisa iwe kuhubiri Amani kwa waumini wake na wananchi kwa jumla” alisema Makamu wa Rais huku akinukuu neno la Mungu katika Waebrania 12:14, ambalo linasema “tafuteni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote”.
Aidha, Eneo jingine ambalo Serikali inalitegemea Kanisa ni katika kujenga maadaili mema ya jamii, hivyo Makamu wa Rais alilitaka Kanisa kusaidiana na Serikali katika kupiga vita tamaduni mbaya za nje ili kujenga Taifa lenye maadili ya Kitanzania, pia Serikali inalitegemea Kanisa katika kupiga vita rushwa na ufisadi ambavyo ni adui wa maendeleo ya nchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Kanisa la Pentekoste Motomoto Jimbo la Tanganyika tayari kwa sherehe ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu Msaidizi pamoja na Maaskofu wa Majimbo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa sherehe ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu Msaidizi pamoja na Maaskofu wa Majimbo wa Kanisa la Pentekoste Motomoto ,Mwanga mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Motomoto Baba Askofu Ezra Enock Mtamya (kushoto), Askofu Mkuu Msaidizi Bwani J. Mathias na Maaskofu wengine wa Majimbo mara baada ya sherehe ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu Msaidizi na Maaskofu wa Majimbo kumalizika katika Kanisa la Pentekoste Motomoto Jimbo Kuu la Tanganyika Mwanga mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mmoja wa waumini wa Kanisa la Pentekoste Motomoto Jimbo la Tanganyika mara baada ya kumalizika sherehe ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu Msaidizi pamoja na Maaskofu wa Majimbo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA