Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RC HAPI KUTEMBELEA JUMLA YA MIRADI 55 KATIKA ZIARA YA TARAFA KWA TARAFA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ziara ya tarafa kwa tarafa ambayo anatarajia kuianza siku ya kesho katika wilaya ya Mufindi kwa lengo la kuijenga Iringa mpya yenye maendeleo.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi anatarajia kuanza ziara ya kikazi kwa kuzitembelea tarafa zote 15 za wilaya zote 3 za mkoa wa Iringa lengo likiwa ni kufanya jumla ya mikutano 37 na kutembelea jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi 78,138,549,216 ambayo itausisha ukaguzi,uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mh: Hapi alisema kuwa anatarajia kutembea jumla ya kilometa 2,611 wakati wa ziara hiyo ya kikazi kwenye mkoa wote wa Iringa.

“Nitatembea tarafa tano za wilaya ya Mufindi ambazo ni Ifwagi,Malangali,Kibengu,Sadani na Kasanga,wilaya ya kilolo nitatembelea tarafa tatu ambazo ni Mazombe,Kilolo na Mahenge na kumalizia wilaya ya Iringa yenye tarafa saba ambazo ni Kalenga,Ismani,Pawaga,Idodi,Mlolo,Kiponzelo na Iringa mjini hapo ndio nitakuwa nimemaliza ziara yangu ya tarafa kwa tarafa” alisema Hapi

Hapi alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuijenga Iringa mpya katika dhana ya kuboresha utendaji wa serikali,kuimarisha sekta za kilimo,ujenzi wa viwanda,utalii,miundombinu,biashara,huduma za afya,maji,elimu,utatuziwa kero za wananchi na kutengeneza fursa zilizopo katika mkoa wa Iringa.

Aidha Hapi alisema kuwa atafanya mikutano mikubwa kumi na saba na midogo 20 ambapo mikutano kumi na tano itafanyika katika tarafa kumi na tano kwa kuambatana na wataalam mbalimbali kutoka idara zote za serikali na taasisi za UMMA.

“ Katika ziara yangu zitatoa sana fursa kwa wananchi kuuliza maswali na kutoa kero zao kwa lengo la kutatua matatizo ambayo yanawakumba wananchi na nitawaeleza muelekeo wa kujenga Iringa mpya” alisema Hapi

Hapi aliwataka viongozi wote wa mkoa kuanzia wakuu wa wilaya haviongozi wa chini kuiga mfano wake wa kwenda kutatua kero za wananchi na wasipofanya hivyo hatakuwa na msamaa kwa viongozi wote wazembe na ambao hawatatui kero za wananchi.

Naomba kumalizia kwa kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yangu na kuhumiza viongozi wanatakiwa kuwepo kwenye ziara yangu bila kukosa.

CHAMA CHA USHIRIKA SIMIYU CHAFANYA UCHAGUZI VIONGOZI, WAASWA KUENDESHA USHIRIKA KISASA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu- Simiyu Co-Operative Union (SIMCU) kimefanya Uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Chama hicho kufanya Mkutano wake Mkuu, tangu kuanzishwa kwake baada ya Simiyu kujitoa Uanachama kwenye Vyama vya Ushirika vya NYANZA na SHIRECU.

Katika Mkutano huo uliofanyika Mjini Bariadi Septemba 04, 2018, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi waliochaguliwa kuendesha ushirika wa kisasa ambao utakuwa wa tofauti huku akihimiza SIMCU kuwekeza katika maendeleo ya elimu, afya na ujenzi wa vitega uchumi.

“Viongozi vaeni mawazo ya kisasa muendeshe Ushirika kisasa, ningependa kuona Chama chetu cha Ushirika cha mkoa(SIMCU) kinajipambanua kwenye maendeleo hasa elimu na afya; wekezeni katika kujenga vitega uchumi, haiwezekani mkusanye zaidi ya bilioni moja kutokana pamba kwenye AMCOS halafu mkashindwa kujenga vitega uchumi” alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Titus Kamani amewaasa viongozi wa SIMCU pamoja na vongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) kusimamia ushirika mkoani humo kwa uadilifu na kuiacha historia ya zamani ambayo baadhi ya viongozi walichukulia ushirika kama mahali pa kupiga dili na mali isiyo na mwenyewe.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU), Bw. Charles Madata, amesema atahakikisha SIMCU inafanya mambo ya maendeleo kama Mkuu wa Mkoa huo alivyosema, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika elimu, afya, kujenga vitega uchumi na kusimamia Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ili vijiendeshe kibiashara.

Aidha, Madata amebainisha mikakati yake mingine kuwa ni kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha na mali za Ushirika, kutafuta soko la pamba ndani na nje, ili bei ya pamba iweze kupanda na kufikia zaidi ya shilingi 1500/= na kuwahamasisha wakulima kujiunga na ushirika ili kuboresha maisha yao.

Nao wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ambavyo ndivyo vinavyounda Chama cha Ushirika cha Mkoa(SIMCU) wamesema, wana matumaini makubwa na Chama hicho na wanaamini kitawasaidia katika kuboresha bei ya zao la pamba, kama ilivyoanza kuonekana katika baadhi ya AMCOS wakati wa msimu wa mwaka 2018.

“Tunaimani SIMCU itatusaidia kuimarisha bei ya pamba , mwaka huu bei elekezi ilikuwa 1100/= lakini kupitia mpango wa wenye makampuni kununua kupitia AMCOS baadhi ya maeneo bei iliongezeka ikafikia 1250/=, tunajua viongozi watasimamia tutapata bei nzuri na wakulima tutanufaika kupitia ushirika” alisema Magima Mageme mwanachama kutoa Itilima

“Ushirika ukisimamiwa vizuri unawasaidia wakulima mambo mengi, mwaka huu wakulima walikuwa wanapewa hela zao cash(taslimu) na wanunuzi wa pamba wa makampuni maana hela zote zilikuwa zinaletwa kwenye AMCOS, viongozi wetu tuliowachagua leo watusaidie kusimamia ushirika vizuri” alisema Nkumbamboi Mchunga wa Budalabujiga.

Naye Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahim Kadudu, amesema Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU), kitakuwa na wanachama (Vyama vya Ushirika vya msingi (AMCOS) 379, huku akibainisha kuwa AMCOS hizo hadi sasa zimezalisha takribani kilo milioni 100.4 za zao la pamba.

Bw. Kadudu amesema kutokana na uzalishaji huo wa kilo milioni 100.4 za zao la pamba AMCOS zimepata bilioni 3.3 kutokana na ushuru ambao AMCOS inapata shilingi 33/= kwa kila kilo moja ya pamba na Chama cha Ushirika cha Mkoa (SIMCU) kitapokea shilingi Bilioni moja na milioni 40 kutokana na ushuru wa shilingi 10/= katika kila kilo moja ya pamba.

Viongozi wa SIMCU waliochaguliwa ni pamoja na Charles Madata(Mwenyekiti), wajumbe wngine ni Mabula Bwire, Emmanuel Mboi, Simon Magoma, Kulwa Bupuma, Filimoni Sambe na Tuma Magagi.
 Baadhi ya wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU), uliofanyika Septemba 04, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kupata viongozi wa chama hicho.
 Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Titus Kamani (kulia) akiteta jambo na Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahim Kadudu (katikati) mara baada ya Mkutano Mkuu wa kwanza wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU), uliofanyika Septemba 04, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kupata viongozi wa chama hicho.
 Baadhi ya wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu(SIMCU), uliofanyika Septemba 04, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kupata viongozi wa chama hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa huo(SIMCU) katika Mkutano Mkuu wa kwanza, kwa lengo la kuchagua viongozi wa Chama uliofanyika Septemba 04, 2018 Mjini Bariadi, (wa tatu kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Titus Kamani na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU), Bw. Charles Madata .

Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma

$
0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kujali usalama wa wanafunzi kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya uchoraji kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo.Amesema tangu mwaka 2013, kampuni hiyo ilipoanzisha kampeni ya usalama barabarani ambayo imekuwa na lengo la kupunguza ajali za usalama barabani na sasa mafanikio yanaonekana.

“Tangu ilipozinduliwa kampeni hii tunaona kuna mafanikio na katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya wanafunzi 9,152, wamepewa mafunzo usalama barabarani ikiwamo kushiriki katika michoro hongereni sana Puma.“….na la kufurahisha zaidi ni hatua ya kuzishirikisha na shule za wanafunzi wenye ulemavu ikiwamo ya shule mojawapo ya Mkoani Ruvuma,” amesema Mavunde.

Awali Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwaelimisha wanafunzi kuhusu usalama barabarani tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kampeni hiyo.“Tangu ilipoanza kampeni hii tumetoa mafunzo kwa wanafunzi wapatao 68,000 katika shule 63 za mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Geita, Kilimanjaro na Ruvuma,” amesema .
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakiwasaidia kuvuka kwenye kivuko wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakikabidhi mfano wa cheki yenye tahamani ya shilingi milioni tano kwa mwalimu Mkuu wa wa shule ya msingi Upanga Ailika Yahya mara baada ya shule hiyo kuibuka mshindi katika shindano hilo lililoshirikisha wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba katika shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde akimkabidhi zawadi za mshindi wa kwanza Mwanafunzi wa shule za msingi ya Maktaba Francisco Salvatory kwa mwakilishi wake Elisha Msafiri katika hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya Upanga Ailika Yahya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti pamoja na majaji wengine wakichambua picha za wanafunzi walioshinda katika shindano hilo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

WALIOFARIKI AJALI YA MAGARI MBEYA WAFIKIA 15

$
0
0
Na EmanuelMadafa, Globu ya Jamii , Mbeya

WATU 15 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matano ikiwemo gari dogo la abiria aina Hiace katika eneo la mteremko wa mlima Igawilo Kasoko Nje kidogo mwa Jiji la Mbeya.

Akizungumza Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mbeya, Petro Siame, alisema hospitali hiyo jana ilipokea miili ya marehemu 13 na majeruhi 15 ambao kati yao wanne walitibiwa na kuruhusiwa.

Siame amesema kuwa alisema, kuwa majeruhi wawili walipoteza maisha wakati wakipatiwa matibabu hivyo idadi ya vifo kuongezeka na kufikia 15 ambapo miili ya watu 12 imetambulika.

‘Jana tulipokea miili ya watu 13 na majeuri 15 lakini kati ya hao wanne wamepatiwa matibabu lakini wawili wamefariki wakati wakiendelea na matibabu hivyo kufanya vifo kuwa 15 na mmoja yupo chumba cha wagonjwa mahututi ICU” alisema Siame

Amesema, majeruhi ambao wanaendelea kupata matibabu wengi wao wamepata majeraha makubwa vichwani na kuvunjika kwa mifupa ya viungo mbalimbali vya mwili ikiwemo mikono na miguu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, akizungumza mara baada ya kuwatembea majehurui waliolazwa katika Hospital ya Rufaa alisema watu 15 kupoteza maisha ni tukio kubwa sana tena kwa ajali ya aina ile ile licha ya serikali kuendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Mashuhuda wa ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne katika eneo la Mteremko wa Igawilo wakitazama moja ya Roli lililopata ajali katika eneo hilo la tukio.
Muuguzi Mkuu Hospital ya Rufaa Kanda ya Mbeya Petro Seme akizungumzia taarifa ya Majeruhi wa ajali.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) akimpa pole mmoja wa madereva wa malori kampuni ya (Asasi) Sabu Mohamed ambaye amelazwa katika hospital ya rufaa Mbeya anako patiwa matibabu.

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YATUMA RAMBIRAMBI KWA WAFIWA WA AJALI ILIYOTOKEA JIJINI MBEYA JANA

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inatoa pole kwa familia zote ambazo zimepoteza ndugu na jamaa zao na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matano, iliyotokea katika eneo la Igawilo Mjini Mbeya siku ya tarehe 7 Septemba, 2018 na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi wengine.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Kangi Alphaxard Lugola, (MB), kwa masikitiko makubwa anatoa pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao na kuwatakia majeruhi wote ahueni ya haraka ili warejee katika hali zao za kawaida na kuendelea na shughuli zao za kujenga nchi.

“Natoa pole nyingi kwa Watanzania wenzangu waliowapoteza wapendwa wao katika ajali hii na nawatakia majeruhi wote afya njema na wapate ahueni haraka ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida”.

“Ni wakati muafaka kwa Watanzania wenzangu, Wasimamizi wa Sheria za Usalama Barabarani na Madereva kutokatishwa tamaa na ajali hii na badala yake changamoto hii iwafanye waongeze umakini barabarani, kuongeza umadhubuti katika usimamizi wa Sheria ya Usalama barabarani kwa kuchukua hatua kali zaidi kwa madereva wazembe na askari wasiotimiza wajibu wako wa kuhakikisha magari mabovu hayaruhusiwi kutembea barabarani”.

Mwenyezi Mungu azipe roho za ndugu zetu pumziko la amani. Amina

Imetolewa na:

Meja Jenerali Jacob G. Kingu, ndc 
KATIBU MKUU

NAMA International Conference & Exhibition kuzikutanisha asasi za kiraia

$
0
0
TAASISI ya Kimataifa ya Mikutano na Maonesho, NAMA International Conference and Exhibition - NICX inatarajia kufanya kongamano kubwa ambalo linalenga kuziunganisha asasi za kiraia kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi kuongeza tija katika shughuli zao. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mratibu wa NICX kwa mwaka 2018, Bw. Shaban Mlongakweli amesema matarajio katika kongamano la mwaka huu ni pamoja na kuwatambulisha wataalamu kwenye nyanja za asasi za kiraia, elimu na maendeleo ya vijana.
Alisema kongamano la mwaka huu ambalo linatarajia kukusanya zaidi ya vijana 250 kutoka katika taasisi zaidi ya 100 litaitambulisha NAMA kama mbia wa maendeleo ambaye anafadhili na kuwaandaa wataalamu kutumika kwa ufanisi.

"NAMA Foundation ya Malaysia inaamini ufanisi wa asasi za kiraia unatokana na rasilimali zilizopo pamoja na elimu bora. Hivyo kuna wataalamu walioandaliwa kwenye nyanja mbalimbali za kiuongozi wa asasi kwenye maendeleo ya elimu na maendeleo ya vijana...pia NAMA tunaunga mkono juhudi za asasi za kiraia kwa kudhamini miradi mbalimbali za asasi hizo," alisema Bw. Mlongakweli.

Aidha aliongeza kuwa NAMA ina wataalamu wa ushauri, wabobezi wa elimu, wataalamu wa malezi kwa vijana pamoja na wataalamu wa kujitolea hivyo kuzitaka asasi za kiraia kujitokeza kwa wingi na kujadiliana kwa kina namna ya kuwatumia wataalam hao kwa maendeleo na pia kupanga namna bora ya ushirikiano utakaoleta tija kwa asasi hizo na taifa kwa ujumla.

Alibainisha kuwa kongamano hilo litakalofanyika Septemba 15, 2018, Serena Hotel ya jijini Dar es Salaam kwa siku moja kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Taasisi ya NAMA inafanya kazi kupitia washirika na kwa nchini Tanzania inajumuisha washirika An-Nahl Trust, Pamoja Foundation, TAMSYA, TAMPRO na UKUEM.

MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI KIGOMA TAYARI KWA ZIARA YA SIKU 4

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 4. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na vijana wa Skauti mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku 4.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi vya ngoma vikitoa burudani wakati wa mapokezi mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku 4. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TAARIFA: WCF KUHAKIKI MICHANGO KWA NJIA YA MTANDAO


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU.SEPTEMBA 8,2018

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Septemba, 2018 ameendelea na ziara yake katika Kanda ya Ziwa ambapo ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Lamadi na kufungua barabara za Mji wa Lamadi katika Wilaya ya Busega, amefungua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, na ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Maswa – Bariadi. 

Mradi wa maji wa Lamadi utakaozalisha lita Milioni 3.3 za maji kwa siku ambayo ni mara mbili ya mahitaji ya lita Milioni 1.8 ya wakazi wa mji huo kwa sasa, utatatua kero ya miaka mingi ya uhaba wa maji kwa wakazi hao ambao kwa sasa wanapata maji kwa asilimia 23 tu ya mahitaji yao. 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa mradi huo ambao umepangwa kukamilika mwezi Mei 2019 utagharimu shilingi Bilioni 12.83 na ni sehemu ya mpango wa uboreshaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira wa ziwa Victoria (LV WATSAN) unaotekelezwa katika miji ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Magu, Misungwi na Lamadi kwa gharama ya shilingi Bilioni 276, fedha ambazo zimetolewa kwa mkopo nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Serikali ya Tanzania. 

Ujenzi wa barabara za Mji wa Lamadi zenye jumla ya kilometa 6.26 umegharimu shilingi Bilioni 9.192 ambapo barabara hizo zimewekewa taa, mifereji, njia za waenda kwa miguu na eneo la kuegesha magari lenye ukubwa wa meta 900. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa pamoja na barabara hizo Serikali itajenga kituo cha mabasi na kilometa nyingine 1.5 ya barabara, kununua gari la taka na kuandaa ramani ya mpango mji katika Mji wa Lamadi kwa gharama ya shilingi Bilioni 6.47, na kwamba mradi kama huo unatekelezwa katika miji mingine 17 hapa nchini kwa gharama ya shilingi Bilioni 561 ikiwa ni fedha za mkopo nafuu ktoka Benki ya Dunia. 

Jengo la wagonjwa wa nje la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu limejengwa katika eneo la Nyaumata kwa ghamara ya shilingi Bilioni 1.8, na ni sehemu ya mradi mzima wa ujenzi wa miundombinu ya hospitali hiyo uliopangwa kugharimu shilingi Bilioni 11. Gharama za ujenzi huo zimepungua kutoka makadirio ya awali ya shilingi Bilioni 46 baada ya Mhe. Rais Magufuli kutembelea mradi huo mwaka juzi na kutoa maelekezo ya kutaka zipunguzwe ili ziendane na gharama halisi za ujenzi. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mojawapo ya wgonjwa aliyepumzishwa katika chumba cha mapumziko katika hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuifungua rasmi hospitali hiyo,Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi mara baada ya kuifungua rasmi hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018. 
   Sehemu ya jengo la wagonjwa wa nje (OPD)la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu lililofunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Bariadi Mkoa wa Simiyu.Septemba 8,2018.. PICHA NA IKULU

Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kuendelea Kufadhili Miradi zaidi Mkoani Geita.

$
0
0
Jumamosi Septemba 8 2018, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi . Robert Gabriel amezindua awamu nyingine ya miradi inayofadhiliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGML) pamoja na Halmashauri za Wilaya na Mji wa Geita   chini ya Mpango wa fedha za Miradi ya huduma kwa jamii kwa mawaka 2018.
Uzinduzi wa Miradi katika awamu hii unahusisha ujenzi wa Kiwanda cha Alizeti, Zahanati,madarasa manne na nyumba  nne za watumishi wa Afya kwenye vijiji vya Nyakabale, Manga, Ikulwa , Ihanamilo, Buhalala,Magaenge pamoja na Kasota ndani ya Wilaya ya Geita.

Uzinduzi huo utahusisha pia ukabidhiwaji wa Kituo cha Polisi Jamii katika kijiji cha Nyakabale pamoja na Trekta jipya kwenye kikundi cha ushirika cha NYABUSAKAMA kinachoundwa na vijiji vya Saragulwa Nyakabale, Bugulula, Saragulwa, Kasota pamoja na Manga.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Bwana. Richard Jordinson amesema kuwa uzinduzi wa kuanza kwa  ujenzi wa Miradi hiyo ya kihistoria ni mwanzo wa maendeleo ya jamii mjini Geita na kwamba shughuli za uchimbaji zinazofanywa na Kampuni hiyo ni kwa ajili ya kuchochea maendeleo endelevu ya uchumi kwa faida ya wakazi wa  Mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujumla.
"Tunafurahi kuona kwamba, GGML kama Kampuni raia,inaendelea kuleta manufaa kwa jamii inayozunguka Mgodi. Utekelezaji wa miradi hii ni moja ya ushuhuda wa wazi kwamba GGML, Serikali na Jamii  inayotuzunguka inaweza kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha miundombinu na huduma bora za jamii, "alisema.
Bw Jordinson ametambua na kupongeza mchango na ushirikiano unaotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na Serikali za mitaa katika utekelezaji wa miradi ya CSR, akielezea: "Kampuni ingependa kutoa Shukrani zake za dhati kwa Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wote wa Halmashauri ya Mji na Wilaya  kwa msaada na uongozi wao katika utekelezaji wa Miradi hiyo.”
Gharama yote katika utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na GGML chini ya Mpango wa CSR kwa mwaka 2018, ni shilingi za Kitanzania  bilioni 9.2 ambazo zitatekeleza miradi mingi ikiwemo ufungaji wa taa za barabarani zinazotumia mwanga wa Jua katika barabara kuu za mji wa Geita, ujenzi wa mnara katika makutano ya barabara za Mji wa Geita pamoja na ujenzi wa soko la kisasa katika Mji wa Geita.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel(kulia) akichanganya mchanga na saruji kuashiria ujenzi wa Shule ya Kiingereza katika eneo la Bomba Mbili Mjini Geita.Akishiriki Zoezi hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita Bw Richard Jordinson
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel(kulia) akichanganya mchanga na saruji kuashiria ujenzi wa Shule ya Kiingereza katika eneo la Bomba Mbili Mjini Geita.Akishiriki Zoezi hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita Bw Richard Jordinson

ZOEZI LA KUSAJILI WAKAAZI WA ZANZIBAR KATIKA MFUMO WA KIELEKTRONI (E-ID CARD) LAANZA

$
0
0
 Zoezi la uandikishaji wananchi wa Zanzibari katika mfumo wa kidigitali limeanza rasmi leo Sept 8, 2018 katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja. Ambapo idadi kubwa ya wananchi imejitokeza kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho ya kielektroniki (E-ID CARD). Mapema wiki hii rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein alizindua Vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar na Uzinduzi wa Uimarishaji Mfumo wa Usajili kielektroniki hafla iliofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
Wananchi wakiendelea kuandikishwa.
Mwitikio wa wananchi ulikuwa ni mkubwa sana.
Wananchi wakingoja foleni ili kuingia katika chumba cha kuandikishwa.

QUEEN ELIZABETH ASHINDA TAJI LA MISS TANZANIA 2018

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kinyang'anyiro cha kumpata mrembo wa Miss Tanzania 2018 limefanyika jana usiku na Mrembo kutoka Kinondoni Queen Elizabeth amefanikiwa kuondoka na taji hilo katika shindano lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Saalaam.

Katika shindano hili, Mshindi wa pili ni Nelly Kazikazi na mshindi wa tatu ni Sandra Giovinazzo., nafasi ya nne ikienda kwa Teddy Nkenda na wa tano ni

Baada ya kuibuka na ushind wa taji la Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth ameweka wazi mwanzo mwisho kile kilichopelekea kushinda taji hili la U-Miss kwa walikuwa wanashindana na warembo wengi halafu wazuri.
 “Nafurahia kushinda taji hili la Miss Tanzania 2018, najisikia vizuri sana napenda kuwashukuru majaji kwa kuweza kuona nafaa kuiwakilisha nchi nasema asante Tanzania, ukiwa kama mrembo lazima ujiandae kama unavyoona warembo ni wazuri sio kwamba ni wazuri kumuonekano tu hata kichwani pia wako vizuri” Queen alisema

Katika shinda no hilo Queen Elizabeth amewashinda warembo wengine 19 waliokuwa wakiliwinda taji hilo kubwa kabisa nchini katika tasnia ya urembo.

Shindano la Miss Tanzania 2018 liliweza kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akiwa moja ya zao la Miss Tanzania 2006 na kuibuka namba mbili Jokate Mwegelo pamoja mbunge wa Segerea Bona Kaluwa.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa, mashindano ya mwaka huu yamekuwa na tija kubwa sana kutokana na waandaaji wa mwaka huu chini ya Basila Mwanukuzi  kujipanga na kushirikiana na serikali kuanzia hatua ya mwanzo mpaka kufikia tamati.


Warembo watano waliofanikiwa kuingia tano bora wamepewa ubalozi wa mwaka mmoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na  Wakala wa Misitu Nchini (TFS).

BOFYA HAPA KUONA ZAIDI

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA WILAYA YA ITILIMA NA KISESA MKOANI SIMIYU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Meatu mkoani humo. Picha na Ikulu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kisesa mkoani Simiyu wakati akiwa njiani kuelekea Meatu mkoani humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mwankoli(hawaonekani pichani) katika jimbo la Kisesa mkoani Simiyu. Picha na IKULU

SERIKALI YAWATAKA WANAOZUNGUKA HIFADHI YA MSITU WA KAZIMZUMBWI KUHESHIMU MIPAKA

$
0
0
 Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi akizungumza kwenye mkutano na wananchi hao katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam.
 Wananchi katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi

*Yawazungumzia pia waliofungua kesi na baadae wakashindwa 

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
SERIKALI imewataka wananchi wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi waliokuwa wamefungua kesi na baadaye kushindwa waendelee kuheshimu mipaka ya Msitu huo huku  Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikiangangalia namna bora ya kuwasaidia.

Hatua hiyo inakuja kutokana na wananchi waliokuwa na mgogoro wa ardhi ndani ya msitu kufungua kesi mwaka 2017,  kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na maamuzi ya shauri la madai ya ardhi kwenye msitu huo yaliipa serikali ushindi, baada ya wananchi hao  kushindwa kuonyesha ushahidi wa umiliki wa ardhi ikiwa ni ushahidi wa manunuzi na urithi wa ardhi hiyo katika  Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi, 

Akizungumza kwenye mkutano na wananchi hao katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi amewaambia wananchi hao kuwa  hawana  haki kwenye ardhi hiyo kwa mujibu wa hukumu iliyotoka, 

Aliongeza kuwa mipaka ya msitu huo ipo sahihi na si  vinginevyo hali iliyopelekea wananchi hao kushindwa  kukata rufaa.

 Hata hivyo  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  amejipa siku 30 kuangalia namna ya kuwasaidia wakazi wa Zingiziwa waliokuwa wamevamia  msitu huo


 Ameongeza kuwa  tayari ameshaunda kamati iliyopewa muda wa miezi miwili kutoa na tayari ishamaliza mwezi mmoja na hivyo itatoa majibu ndani ya siku 30 lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi hao ambao kisheria walishindwa kesi.

"Mgogoro huu ulishafika mahakamani na uamuzi ukatolewa kuwa mmevamia hilo lipo wazi na sisi hatupingani na uamuzi wa mahakama.
"Ila kwa kuwa nyie ni wananchi wetu, CCM imeamua kununua kesi, sio kwa maana ya kupinga mahakama Bali ni kwa kuangalia tunawasaidia vipi,"


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amesema wizara yake haina tatizo na wakazi hao zaidi ya kuhakikisha msitu huo uko salama.


Amesema katika kipindi ambacho msitu huo ulivamiwa athari kubwa zilijitokeza.

"Msitu huu tunaweza kusema ndio mapafu ya Dar, sasa ukivamiwa kwa kuwekwa Makazi au shughuli za kibinadamu mambo yanakuwa mabaya,”

"Tunategemea tupate hewa nzuri kutokana huku lakini wao walivamia na kutengeneza hewa chafu. Sisi tunachosimamia ni kuhakikisha msitu unatunzwa na kubaki kuwa msitu,"amesema.

Baadhi ya wawakilishi wa kundi hilo la wananchi  waliokuwa wamevamia msitu huo  wameeleza kuwa wanachotaka ni kuonyeshwa mipaka ya kitaalam ya unapoanzia msitu huo.


"Hatupingani na mahakama wala wizara sisi tunataka wataalam wa wizara ya ardhi waje wafanye vipimo na kutuonyesha kitaalam ilipo mipaka," amesema Jackson Rwehumbiza.

Kuhusu msitu huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo alisema, mwaka 1954 Serikali ilianzisha Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi wenye ukubwa wa hekta 4,860, kwa Tangazo la Serikali Na. 306 la mwaka 1954 na ramani Jb 196 ya mwaka 1954 kwa kutambua umuhimu wake.

Profesa Silayo anasema licha ya umuhimu wake Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na wananchi wanaoishi kuzunguka msitu huo na serikali ilifanya zoezi la kuwaondoa mwaka 1998,2003,3007,2011 na 2014.

“Msitu huu upo katika Wilaya ya Kisarawe na upande wa mashariki ndiyo mpaka kati ya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani na wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es Salaam.

KATIBU KAGAIGAI MGENI RASMI AKIMUWAKILISHA SPIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAMU NA HARAMBEE YA KWAYA YA UPENDO SIKONGE

$
0
0
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kushoto) akiwa katika uzinduzi wa albamu na Harambee ya Kwaya ya Upendo Sikonge kutoka Mkoa wa Tabora tukio lililofanyika leo katika kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini Jijini Dodoma. Wageni wengine ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Kakunda (kushoto), Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) na Mbunge wa Tabora Mjini, Mhe. Emmanuel Mwakasaka.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Kakunda akizungumza na viongozi mbali mbali wa kitaifa, wanakwaya wa kwaya ya Upendo Sikonge ya Mkoani Tabora na waumini wa kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini ya Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa albamu na Harambee ya Kwaya ya Upendo Sikonge tukio lililofanyika leo katika kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kushoto) akipokea risala aliyopatiwa na wana kwaya ya upendo kutoka kanisa la Moravain Sikonge kutoka Mkoa wa Tabora tukio lililofanyika leo katika kanisa la Moravian Jimbo la Kaskazini Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Kakunda, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, Mbunge wa Tabora Mjini, Mhe. Emmanuel Mwakasaka, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, Mhe. Richard Mbogo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula. Katika Shughuli hiyo Katibu wa Bunge alimuwakilisha Spika Ndugai.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza na wanakwaya na waumini wa kanisa la Moravian Iringa Road wakati wa uzinduzi wa Albamu na Harambee ya Kwaya ya Upendo Sikonge kutoka Mkoa wa Tabora iliyofanyika leo Jijini Dodoma. Katika Shughuli hiyo Katibu wa Bunge alimuwakilisha Spika Ndugai.

MEYA MWITA AISHAURI SERIKALI, JAMII KUWAKUMBUKA WATOTO WENYE ULEMAVU

$
0
0
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza n.a. wanafunzi wenye ulemavu wakati wa mahafli ya 45 ya shule ya msingi Wokovu iliyopo jijini hapa jana.

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameishauri serikali na Jamii kwa ujumla,Kuongeza jitihada za kuhakikisha kwamba watoto wenye ulemavu wanapata nafasi za kusoma  na kutambulika sehemu mbalimbali.


Meya Mwita ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki Wakati wa mahafali ya 45 ya darasa lasaba katika shule ya walemavu ya Jeshi la Wokovu iliyopo jijini hapa ambapo alisema kuwa watu wenye ulemavu wanaonekana hawafai,hawapati nafasi katika jamii na hivyo kushauri jitihada mahususi zitumike kuwatambua watu hao.


Aliongeza kuwa katika sekta ya elimu ,Taasisi mbalimbali pamoja na mashirikia ya dini ndio zimekuwa mstari wa mbele kutoa nafasi za kupatiwa elimu kwa makundi hayo na kutoa wito kwa jamii nyingine kujitoa kusaidia makundi hayo.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimkabizi zawadi mwanafunzi mwenye ulemavu wa miguu Ernest aliyemaliza darasa la Saba jana katika shule ya msingi Wokovu.

" Kazi mnayoifanya nyie jeshi la Wokovu ilitakiwa ifanywe na Serikali,lakini kwa nafasi yenu mmeweza ndio mana leo hii tuko hapa,mnapaswa kupongezwa ,nitumie nafasi hii kuwaawlika viongozi wa serikali, mashirika mbalimbali kujitoa ili kusaidia shule hii ambayo imeonyesha nia dhabiti ya kusaidia watoto hawa" alisema Meya Mwita.

Aidha katika hatua nyingine Meya Mwita aliwataka wazazi waliokuwa na watoto wao shuleni hapo kuwa mabalozi kwa wazazi wengine na hivyo kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu kama wengine.

"Niwapongeze wazazi wenye watoto wenu hapa,

mmeonyesha uthubutu mkubwa,hizi sio dhama za kuficha watoto,waambieni na wengine wasiwafiche waleteni wapate elimu ili iwasaidie huko badae, hawa ndio watakuja kuwa viongozi wa badae"alisema Meya Mwita.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ,Mkurugenzi wa shule hiyo ,Luteni Thomas Sinana mbali na kumpongeza Meya Mwita kuhudhuria mahafali hayo,alisema kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi 210 wenye ulemavu huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Alieleza changamoto hizo kuwa ni upungufu wa vitabu ,huku wanafunzi wengine wakishindwa kufika shuleni wakati wa likizo kutokana na kukosa Fedha za kuwasafirisha. Alifafanua kuwa shule hiyo inachukua wanafunzi kutoka mikoa  mbalimbali hapa nchini hivyo wakati mwingine huwawia vigumu wanafunzi hao kurudi shuleni kutokana na ukosefu wa Fedha hivyo kuiomba serikali kusaidia.

"Ndugu mgeni rasmini ,shule hii inachangamoto nyingi ,tunaomba utufikishie salam zetu kwa viongozi husika, awali serikali iliweka utaratibu wa kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kupatiwa fedha za kujikimu,lakini kwa sasa imeondoa,tunaomba utufikishie salam zetu huko" alisema Luteni Sinana.

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo Amnyuka Sam Eggington wa uingereza kwa KO

$
0
0
Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo mwenye umri wa miaka 23 amemtwanga bondia wa Uingereza Sam Egginton kwa K.O kwenye round ya 4  kwenye pambano lao la raundi 10 la kusindikiza mchezo baina ya  Amir Khan na  Samuel Vargas lililofanyika Jumamosi Septemba 8, 2018 katika ukumbi Arena Birmingham  (zamani Barclaycard Arena/NIA), mjini Birmingham kitongoji cha  West Midlands, Uingereza. Vyombo vya habari za ndondi vimeutaja ushindi wa kijana huyo wa Kitanzania kama wa kushtua  ikizingatiwa mpinzani wake ni bingwa wa mikanda kadhaa mikumbwa ya kimataifa. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

MENEJA WA BENDI YA VIJANA JAZZ JAMES ROCK MWAKIBINGA AFIWA NA BIBI YAKE

$
0
0
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa (MCC) comrade Kheri James (kulia) akizungumza jambo na Meneja wa Bendi ya Vijana Jazz ya CCM, Comrade James Rock Mwakibinga leo wakati alipofika kwenye Msiba wa Bibi Paulina Mwita ambaye ni Bibi yake na James Rock Mwakibinga, uliotokea leo Kawe Ukwamani, jijini Dar es salaam. Mazishi ya Bibi Paulina Mwita yatafanyika Siku ya Alhamisi Tarehe 13/9/2018  Saa 6 Mchana kwenye makaburi ya Kinondoni FM jijini Dar es salaam. 

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI

$
0
0


Na Deodatus Kazinja, Moshi
Wito umetolewa kwa Asasi mbalimbali za kiraia nchini kujitokeza kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazoweza kulikwamisha katika kutoa huduma muhimu za wafungwa magerezani  kutokana na ufinyu wa bajeti. 

Hayo yamesemwa leo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Phaustine Kasike katika hafla ya kupokea msaada wa Kibinadamu uliotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ  iliyofanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga mjini Moshi jana Septemba 8, 2018.

“Ni ukweli usiopingika kuwa Jeshi la Magereza limekuwa likishindwa kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa kutokana na ufinyu wa bajeti,” amesema CGP  Jenerali Kasike.
Huduma nyingine ambazo zimewezeshwa na Asasi hizo ni kuwa na vituo vidogo vidogo vya kujifunza kufanya mambo ambayo tayari yanafanyika ndani ya magereza kama vile uokaji mikate, ushonaji na kudarizi, ushonaji wa viatu, ukinyozi, useremala na uchomeleaji mchanganyiko.

Katika hafla hiyo Asasi ya Kidini ya New Life In Christ imekabidhi msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.2 ambapo wameahidi kuendelea kutoa misaada ya namna hiyo kwa kadiri Mungu atakavyowajalia. Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa leo imewalenga zaidi wafungwa walioko Mikoa ya  Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Mwanza.



Wakati huo huo,  Kamishna Jenerali Kasike amewaagiza wakuu  wote wa magereza yote ambayo vifaa hivyo vitapelekwa kuhakikisha wanavitunza na kuvitumia kwa uadilifu kama ilivyokusudiwa.

Jenerali Kasike ametoa wito kwa Asasi nyingine kuiga mfano uliooneshwa na New Life in Christ na Dorcas Aid International Tanzania zinavyoshirikiana na Jeshi la Magereza.

Asasi ya Kidini ya New Life In Christ  pamoja na Dorcas Aid International Tanzania kwa miaka 14 sasa tangu 2005 zimekuwa zikishirikiana na Jeshi la Magereza kwa kutoa misaada ya Kibinadamu na Kiroho yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.7 hadi hivi sasa.

Kwa kipindi chote hicho Asasi hizi zimekuwa zikitoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa semina za ushauri pamoja na mafunzo ya ufundi stadi kwa wafungwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Ndg. Charles Shang’a mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya wafungwa leo Septemba 8, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (wa pili kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kuchomelea akiwa ni sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ kwa ajili ya wafungwa vitakavyotumika kuwafundisha stadi mbalimbali za ufundi magerezani.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akipokea msaada wa vyerehani uliotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ leo Septemba 8, 2018 kwa ajili ya wafungwa. Hafla ya upokeaji wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga Moshi.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AREJEA NCHINI AKITOKA NCHINI CHINA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitoka nchini China, Septemba 9, 2018 alikomwakilisha Rais John Magufuli kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing hivi karibuni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images