Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AWAHUTUBIA WANANCHI WA TARIME MKOANI MARA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tarime mjini mara baada ya kuwasili akitokea katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
 Kwaya ya Chuo cha Ualimu Tarime ikitoa burudani mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili Tarime mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanakwaya ya Chuo cha Ualimu Tarime mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano Tarime mjini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tarime vijijini wakati akitokea katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Tarime mjini mara bada ya kuwahutubia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondary Ingwe iliyopo Nyamongo Wilayani  Tarime Monica Benard kiasi cha Shilingi milioni tano kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya shule hiyo kutokana na vipaumbele vyao.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ingwe ya Nyamongo Tarime mkoani Mara Monica Benard akionesha kiasi cha Shilingi milioni tano alizokabidhiwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya maendeleo ya shule yao. Pia Rais Dkt. Magufuli aliendesha Harambee ya papo kwa hapo ambapo zilipatikana jumla ya Shilingi milioni 26 kwa ajili ya maendeleo ya Shule hiyo. PICHA NA IKULU

TANZANIA YAIKABIDHI SEYCHELLES UONGOZI WA MAPAMBANO DHIDI YA UTAKASISHAJI FEDHA HARAMU NA UFADHILI WA UGAIDI MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM, Mahe, Seychelles

TANZANIA imekabidhi uongozi wa mwaka mmoja wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) kwa nchi ya Seychelles, huku ikijivunia mafanikio makubwa ya kuhakikisha kuwa nchi wanachama wa umoja huo zinakuwa na sera, sheria, taasisi na mifumo imara inayowezesha mapambano dhidi ya vitendo vya utakasishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekabidhi uongozi huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwa Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja huo, uliofanyika Mjini Mahe, nchini Seychelles na kushuhudiwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Danny Faure.

Miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, ni kufanyika kwa tathimini ya mifumo ya kudhibiti utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi wa nchi tatu wanachama wa umoja huo za Mauritius, Madagascar na Seychelles, na kwamba zoezi la kuzitathmini nchi nyingine mbili za Zambia na Malawi, linaendelea.

“Rasilimali za nchi zetu zinahitaji kutumika vizuri, kwa sababu zinapotumika vibaya zinapunguza uwezo wa nchi zetu kuchochea maendeleo haraka, pale zinapo hatarisha sekta yetu ya fedha, matumizi adili ya rasilimali hizi na usalama wa nchi zetu” alisema Dkt. Mpango

Aidha, Dkt. Mpango amesema kuwa utakasishaji wa fedha haramu unazuiwa kwa sababu unamadhara makubwa kiuchumi, kijamii na kiusalama kwa nchi wanachama.“Fedha ambazo zinakuja kuja tu hivi! Hujui kama zinakwenda kugharamia ugaidi, au ni fedha za wananchi wetu lakini wanazitorosha ambapo badala ya kuzitumia ipasavyo wanazitumia kufanya mambo haramu” aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini Mwa Afrika ESAAMLG, Dkt. Elliawony Kisanga amesema kuwa tangu umoja huo uanzishwe miaka 19 iliyopita, yamekuwepo mafanikio makubwa na kazi iliyopo mbele ya uongozi mpya ni kuanza na kuendelea kufanyika kwa tathmini ya mifumo ya udhibiti ya nchi za Zambia, Malawi na Tanzania.

Mwenyekiti Mpya wa ESAAMLG, Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, ameipongeza Tanzania chini ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kwa uongozi wake mahili na kuuwezesha umoja huo kutekeleza majukumu yake ipasavyo na msukumo wake utakuwa kuwezesha nchi wanachama kuendelea kusimamia utekelezaji wa sheria.

Aidha Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa ESAAMLG ulitanguliwa na Mkutano wa 36 wa Kikosi Kazi cha Maafisa waandamizi wa ESAAMLG, ambapo Bw. Onesmo Makombe alikabidhi kwa niaba ya Tanzania Uenyekiti wa Kikosi Kazi hicho kwa Bw. Philip Moustache wa Jamhuri ya Seychelles.

Tanzania ilipokea uongozi wa Umoja huo Septemba 7 mwaka jana wakati wa Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika uliofanyika Zanzibar, ikipokea majukumu ya uongozi huo kutoka nchi ya Zimbabwe ambapo Umoja huo unaundwa na nchi 18 ambazo ni Angola, Botswana, Eswatini, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Rwanda, Seychelles, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.


Mwenyekiti wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), aliyemaliza muda wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia), akiwa Meza Kuu na Mwenyekiti mpya wa umoja huo, Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles, Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa mkutano wa 18 wa Umoja huo uliofanyika, Mahe-Seychelles.
Mwenyekiti wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), aliyemaliza muda wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia), akipongezana na Mwenyekiti mpya wa umoja huo, Waziri wa Fedha, Biashara, Uwekezaji na Mipango ya Kiuchumi wa Seychelles, Balozi Maurice Lousteau – Lalanne, wakati wa Mkutano wa 18 wa Umoja huo uliofanyika, Mahe-Seychelles. Kulia ni Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Maafisa Waandamizi wa ESAAMLG aliyemaliza pia muda wake kutoka Tanzania, Bw.  Onesmo Makombe. 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa (kushoto) na Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, Bi. Mwanahija Almas Ali, wakifuatilia kwa makini Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) uliofanyika Mahe, Nchini Seychelles.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi zaidi ya 19 za Afrika, wakifuatilia kwa makini Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG) uliofanyika Mahe, Nchini Seychelles, ambapo Tanzania imeikabidhi Seychelles uongozi wa Umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja ukiwa ni utaratibu wa nchi wanachama kupokezana uongozi.

Makamu wa Rais wa Seychelles, Mhe. Vincent Meriton, akifungua Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAMLG), mjini Mahe, Seychelles ambapo nchi hiyo imekabidhiwa kijiti cha kuongoza Umoja huo kwa mwaka mmoja (2018/2019) ukiwa ni utaratibu wa nchi wanachama kukabidhiana uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango, Seychelles.


KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA

$
0
0


 Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akifuatilia kwa makina taarifa ya mkoa wa Tanga kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmanuel Lwinga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7,2018.
PIX 2
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya maafisa wa ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na gereza la Mahabusu Tanga  mara alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Maweni jijini Tanga akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
PIX 3
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye “microphone” ) akizungumza na maafisa na askari wa vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na Gereza la Mahabusu Tanga (hawapo pichani) kwa pamoja katika bwalo la Gereza Kuu Maweni Tanga alipofanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmauel Lwinga, wa tatu kulia ni Mkuu wa Gereza Kuu Maweni Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Felichism Masawe na wa kwanza kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Marakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Hamis Mbwana.
PIX 4
Baadhi ya maafisa na askari  wa vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga,  waliokusanyika kwa pamoja katika bwalo la gereza Kuu Maweni  wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani)  alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo leo Septemba 7, 2018. Katika hotuba yake CGP ametilia mkazo suala la kubadili mtazamo wa kiutendaji, kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kufanikisha majukumu yetu kama serikali na jamii nzima inavyotarajia kutoka kwetu.
PIX 5
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi askari wa magereza wa kike mkoani Tanga alipofanya ziara ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
PIX 6
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) walioko mkoani Tanga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.Picha zote na Jeshi la Magereza.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 11 katika ajali Jijini Mbeya

JKCI yaibuka mshindi wa kwanza katika utoaji wa huduma ya upimaji na kutoa elimu ya magonjwa ya moyo katika mkutano wa wahandisi

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeombwa kuwafikia wananchi wengi zaidi wakiwemo wafanyakazi ili waweze kufanyiwa vipimo vya moyo pamoja na kupata elimu ya jinsi ya kuepukana na ugonjwa huo. Ombi hilo limetolewa leo na washiriki wa mkutano wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar es Salaam.

Wahandishi hao pia wamewashauri wafanyakazi kutenga muda wa kupima afya zao na kufanya mazoezi ambayo yatawasaidia kiafya. Mhandisi Alex Kalanje alisema kama Taasisi hiyo itawafikia watu wengi zaidi kwa kwenda katika mikusanyiko mbalimbali kutawasaidia watanzania wakiwemo wafanyakazi ambao kutokana na majukumu yao ya kazi wanakosa muda wa kwenda kupima afya zao kupata huduma ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo.

“Wafanyakazi wengi wanakosa muda wa kwenda Hospitali kupima afya zao, lakini kama kutakuwa na utaratibu wa kuwepo kwa wataalam wa afya katika mikutano mbalimbali kutawasaidia kupata muda wa kupima kirahisi zaidi kuliko wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi”, alisema Mhandisi Kalanje..

Kwa upande wake Mhandisi Dkt. Gemma Modu aliwashauri watanzania kutenga muda wa kupima afya zao kwa kufanya hivyo kutawasaidia kujuwa kama wanamatatizo au la na kama wanayo wataweza kupata matibabu mapema.

Aidha Dkt. Gema pia aliwasihi kinamama kubadilika na kuhamasisha familia zao kwenda kupima na ikifika muda wa kupima waende wao na waume zao pamoja na watoto.

Akizungumza wakati wa kufungwa kwa mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim James Yonazi aliipongeza Taasisi ya Moyo kwa huduma ya kijamii iliyoitoa ya upimaji na kutoa elimu ya lishe pamoja na mazoezi na kusema kuwa kazi waliyoifanya ni kubwa.

Taasisi hiyo ilishika nafasi ya kwanza ya mtoa huduma za kitaalam kwa kutoa huduma za upimaji wa vihatarishi vya magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora na mazoezi, kueleza kwa kina huduma zinazotolewa na Taasisi, kutoa dawa bure kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo na kutoa rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa waliokutwa na matatizo ya moyo yaliyohitajika kupewa rufaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea cheti cha nafasi ya kwanza ya mtoa huduma za kitaalam kutoka kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa kutokana na Taasisi hiyo kushiriki katika kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwenye mkutano wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dorica Burengelo akimpima ugonjwa wa kisukari mhandisi aliyetembelea banda la hiyo kwa ajili ya kupima afya na kupata elimu ya lishe na mazoezi wakati wa mkutano wa 16 wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Mushi akimpima msukumo wa damu (PB) mhandisi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima afya na kupata elimu ya lishe na mazoezi wakati wa mkutano wa 16 wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hussein Mube akimpa ushauri wa kiafya mhandisi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima afya na kupata elimu ya lishe bora na mazoezi wakati wa mkutano wa 16 wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa upimaji afya, utoaji wa elimu ya lishe bora na mazoezi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kupokea cheti cha kushika nafasi ya kwanza ya mtoa huduma za kitaalam kwenye mkutano wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

KUIONA SIMBA NA AFC LEOPARDS BUKU TANO TU UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Afisa habari wa Simba Haji Manara. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU ya Simba inashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na AFC Leopards ya Kenya kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea tena wiki ijayo utakaochezwa jioni ya leo katika dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mchezo huo, Afisa habari wa Simba Haji MAnara amesema katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa wa klabu ya Simba na AFC Leopards ya Kenya utakaofanyika Jumamosi kiingilio kitakuwa ni Sh. 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

Manara ametaja viingilio vingine katika mchezo huo utakaoanza Saa 12:00 jioni vitakuwa Sh. 15,000 kwa jukwaa la VIP A na Sh. 10,000 kwa jukwaa la VIP B na mchezo huo utakuwa ni kwa ajili ya kuwapima wachezaji wake kabla ya kuendelea na mtanange wa ligi kuu.

Amesema mchezo huo utazikutanisha timu hizo baada ya miaka miwili toka wakutane mara ya mwisho kwenye tamasha la Simba Day, Agosti 8 mwaka 2016 Uwanja wa Taifa pia na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa golo 4-0.

Mbali na hilo, Manara amewataka mashabiki wa Simba na watanzania wote kwa ujumla kuipa sapoti Taifa Stars ambayo inacheza kesho dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON 2019.

Manara amesema watanzania kwa ujumla wanatakiwa kuwa wamoja kwa ajili tawashangaa mashabiki baadhi wa Simba ambao wataipa sapoti Uganda kutokana na kuondolewa kwa wachezaji wake 6 kwenye kikosi cha Stars kutokana na kuchelewa kufika kambini akieleza kuwa ni sababu ambayo haina maana.


Manara amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho ambapo timu yao itakuwa inacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya majira ya saa 12 jioni.

Sanjari na kujitokeza Uwanjani, mashabiki hao pia ambao watawahi watapata fursa ya kuutazama mchezo wa Uganda dhidi ya Stars ambao utarushwa mbashara kupitia kituo cha ZBC 2.

Dkt . Kalemani atoa mwezi mmoja kwa Vijiji vyote vya Jjiji la Arusha kupata umeme

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) akizungumza na wakazi wa Kimondolosi, wilaya ya Arusha mjini, wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (katikati) ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini (REAIII) wilayani humo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wakazi Kijiji cha Kimondolosi Kata Olasiti Wilaya ya Arusha mjini.
Wakazi wa Kata ya Olasiti, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani aliyekuwa akizungumza kuhusu kuwapatia huduma ya umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani (wa Tatu kushoto) akikagua nguzo za umeme katika Kata ya Terati, zitakazotumika kuwapatia Umeme wananchi wa eneo hilo mkoani Arusha. Wa Pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Na Zuena Msuya, Arusha.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa mwezi mmoja kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa vijiji vyote vilivyopo katika Jiji la wa Arusha vinaunganishwa na huduma ya umeme. Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo jijini Arusha baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA III) katika Vijiji vilivyopo jijini humo na kujionea hali ya ukosefu wa nishati ya umeme.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, Wananchi hawafurahii kucheleweshewa kupata huduma ya umeme hali ya kuwa wengine walikwishalipia huduma hiyo.

" Haipendezi na haifurahishi machoni mtu kajitahidi kujibana na kujenga nyumba yake nzuri na ya kisasa, lakini anakosa umeme wakati uwezo wa kumuunganishia upon a vifaa vipo, sasa kwa nini asiunganishwe.?," alihoji Dkt. Kalemani. Kutokana na hali hiyo, aliwataka TANESCO kuunda vikosi kazi mbalimbali vitakavyosaidia kazi ya kusambaza umeme kwa wananchi kwa haraka.

Aidha, alimwagiza mkandarasi anayesambaza umeme jijini humo, kampuni ya Nipo Group, kuhakikisha kuwa anawafungia umeme wananchi wa Kimondorosi katika Kata ya Olasiti mkoani Arusha na kuhakikisha kuwa kila siku anatoa ripoti ya utekelezaji wa mradi kwa mtendaji wa mtaa huo hadi atakapomaliza kuweka umeme kwa wananchi . 

Alisema kuwa, mkandarasi huyo anapaswa kufanya kazi hiyo ili kuwaondolea kero ya ukosefu wa umeme wananchi hao ambao wamekaa kwa muda mrefu bila kupata huduma hiyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alimshukuru Waziri wa Nishati kwa kutoa agizo hilo litakalopelekea wananchi hao kupata umeme kwani wananchi hao walishamlalamikia kuhusu kukosa huduma hiyo.

Vilevile, mmoja wa wananchi katika Kata hiyo, Clementina Mushi alimuomba Waziri wa Nishati kuhakikisha kuwa umeme huo unafika kwa wananchi wote bila kurukwa.

BODI YA PAMBA TANZANIA YATEMBELEA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHEMBA

$
0
0
Na Shani Amanzi,

Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania Ndg.James Shimbe amesema wakulima wakiweka kipaumbele kulima zao la pamba litaleta kipato kikubwa kwa Taifa kwani zao la Pamba nje ya nchi linauzwa kwa 80% na 20% ndani ya nchi ambapo mahitaji makubwa yanaenda Viwandani. 
 

Shimbe aliyazungumza hayo alipokuwa kwenye Kikao kazi cha Baraza la Madiwani tarehe 31/9/2018 kama mgeni mualikwa kuelezea zao la Pamba linavyoweza kulimwa katika wilaya ya Chemba kwa kuwa ardhi iliyopo inafaa kwa kilimo hicho.

Aidha Shimbe amesema “nchi yetu inapata mapato makubwa kwa kuuza pamba nje ya nchi katika nchi za China, India, Pakistan na Indonesia na tunapaswa kuuza kwa wingi katika Viwanda vyetu ili vitengeneze nguo na kuepuka nchi kuagiza nguo za mitumba nje ya nchi kama ilivyo sasa ”.
Shimbe amesema, uzalishaji wa pamba kwa ekari moja ni kilo 560-912 katika mikoa ya Iringa, Manyara,Tanga,Singida ,Katavi,Geita ,Mwanza, Shinyanga na tunapaswa kuzidi kuwahimiza wakulima wetu walime pamba kwa wingi kwani Pamba ni dhahabu nyeupe inayohitajika kwa wingi zaidi katika soko la dunia.

“Katika utafiti tulioufanya katika wilaya ya Chemba kilimo cha pamba tutaanza kuwawezesha wakulima wa kata ya kidoka, gwandi,Lahoda, na mrijo kwa kuwapatia pembejeo za kilimo cha pamba na msimo wa kilimo unaanza mwezi wa novemba 2018 na mvuno ni mwezi wa aprili, 2018”. Alisema Ndg. Shimbe.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amewapongeza wageni kutoka bodi ya Pamba kwa kuja wilayani Chemba na ameahidi watashirikiana na Wataalam wa kilimo, Wahe. Madiwani na Wananchi ili kuweza kurahisisha kuwaelimisha wakulima umuhimu wa zao la pamba ili kuwainua .

“Tunaelewa katika kilimo kunachangamoto ikiwemo uwezo mdogo wa vyama vya ushirika,mabadiliko ya tabia nchi,kuwepo Maafisa ugani wachache ,wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo na mtazamo hasi wa zao la pamba lakini nawaahidi tutajitahidi kukabiliana nazo ili uzalishaji wa zao la pamba uwe tegemeo kubwa kama ilivyo zao la alizeti”aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Mashimba.

MGODI WA BULYANHULU WATILIANA SAINI MAKUBALIANO NA HALMASHAURI YA NYANG'HWALE KUCHANGIA VIFAA VYA UJENZI

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Bi Mariam Chaurembo katika ukumbi wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Mkoani Geita baada ya kusaini na kubadilishana hati za makubaliano ya mchango wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati za vijiji 32 vya Halmashauri ya Nyanghwale, Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyanghwale Aloyce Mussa Lumambi, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi, Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Hamim Gwiyama, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Japhet Simeo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi Benedict Busunzu akizungumza wakati wa zoezi la utiaji saini makubaliano.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Mariam Chaurembo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale Bi Mariam Chaurembo akizungumza.
Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Hamim Gwiyama, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi Bwana Benedict Busunzu.

MICHUZI TV: Dkt. Tizeba atoa tathmini ya ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Sukari

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA SEPTEMBA 07, 2018

AJALI: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA

$
0
0
Na Emanuel Madafa- Fadhiri Atick Globu ya Jamii, MBEYA.

WATU 11 wahofiwa kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne ikiwemo gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace iliyotokea eneo la Mlima Igawilo Kasoko Jijini hapa.

Kwa majibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa kumi na moja za jioni ambapo chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli kwa Lory lenye namba T334 DJN lililokuwa limebaba ndizi likitokea Wilayani Rungwe.

Amesema, hadi sasa taarifa waliyoipata ni kwamba vifo vya watu ni 11 na idadi ya majeruhi bado haijapatikana kwani watu waliokuwepo kwenye magari hayo walikimbizwa hospital kwa ajili ya matibabu.
“Kwa sasa taarifa tuliyonayo ni kwamba vifo ni watu watano idadi ya majeruhi bado haijajulikana kwani asilimia kubwa wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa matibabu, hivyo tunategemea taarifa ya hospitali ili kupata ripoti sahihi ya vifo na majeruhi,”alisema.

Aidha amesema baada ya Lory namba T334 DJN likitokea Tukuyu, kufeli breck hivyo kugonga Dogo ya abiria Hiace namba T883 ABS ambalo nalo liligonga Lory lingine lililopakia ndizi nalo kugonga Lory la mafuta. Amesema , majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajli ya matibabu huku miili ya marehemu watano imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika hospitali hiyo.
 Baadhi wa mashuhuda wa ajali hiyo, walisema kuwa dereva wa lory lililosababisha ajali alifanya makosa kwani alipoona gari hilo limeferi brek alikuwa na uwezo wa kulichepusha pembeni ili kuepusha ajali hiyo ambayo ni kubwa.

“Dereva alikuwa anakuja mwendokasi alipofika kwenye mteremko huu wa mlima Igawilo ndipo aliposhtuka na kuanza kuingiza gia ambazo zilifeli na kusababisha gari kuserereka lakini alikuwa na uwezo wa kuliegesha gari hili pembeni,”alisema Jamali Ismaili.
Hata hivyo Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya ilifika eneo la tukio.

MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI AELEZA SABABU ZA KUMUONDOA MKURUGENZI WA TAKUKURU

SAFARI YA BIASHARA NCHINI CHINA

KAMPUNI YA KITANZANIA YA NALA YASHINDA TUZO YA ECOBANK FINTECH CHALLENGE

$
0
0
SHINDANO la Ecobank Fintech Challenge lenye lengo la  kuonesha na kushirikiana na  miradi yenye mafanikio zaidi ya Fintech Katika bara zima la Afrika limemalizika huku Tanzania kupitia Kampuni ya Nala kupitia mradi wake wa Nala Money(Nala App) chini ya Mkurugenzi na mwanzilishi Benjamin Fernandes wakiibuka na kuwa washindi,

Shindano hilo limelenga  kusaidia kupitia ushirika wa kibiashara ili kukua na kujitanua kwenda kwenye mafanikio ya kikanda na biashara ya kimataifa.

Mradi wa malipo ujulikanao kama Nala hapa Tanzania umetajwa kuwa mshindi wa mwaka wa shindano hilo la Ecobank Fintech Challenge na kufanikiwa kuibuka na zawadi ya dola za kimarekani 10,000.

Nala inawasaidia watumiaji wa miamala ya simu kujihusisha na nakala za USSD kupitia njia rahisi kama vile Venmo app, iliyotoa ufumbuzi pamoja na miradi (startups) mingine ipatayo 10 katika sherehe za 30 agosti katika makao makuu ya kimataifa ya Ecobank huko Lome Togo.
Nigeria wallet, imekuwa ya pili na kujishindia dola za kimarekani 7,000 wakati Virtual Identity ya Afrika ya Kusini ilikuwa mshindi wa tatu na kupata dola za kimarekani 5,000. Washiriki wengine ni Lypa ya Kenya, Litee ya Benin, SESO Global ya Afrika ya Kusini, InvestED  ya Sierra Leone, Eversend ya Ufaransa, Seca pay ya Nigeria, Moji pay ya Togo na Awamo ya Uganda.

Ecobank itawaandikisha washindi wote 11 katika ushirika wake wa Fintech. Ushirika huu utadumu kwa kipindi ya miezi 6. Katika kipindi hicho miradi hiyo (startups) itanufaika kutoka kwenye fursa hiyo  kwenda kwenye hatua kubwa Zaidi ya ushirika na ecobank group.
Mkuu wa kitenge cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu(kushoto) akimpongeza Mkurugenzi na mwanzilishi wa Kampuni ya  Nala, Benjamin Fernandes baada ya kuibuka mshindi wa Tuzo ya Ecobank Fintech challenge.

#ROSALINACHALLENGE By MASAKA KIDS UGANDA - Song by BM Congo

PROFESA KITILA MKUMBO AMEWATAKA WADAU WA MAJI KUSHIRIKI KATIKA UTUNGAJI SHERIA MPYAA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu wa  Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof esa Kitila Mkumbo amewataka  wadau wa maji nchini kushiriki katika utoaji wa maoni kuhusiana na utungaji wa sheria mpya ya maji ili kuweza kudhibiti upotevu wa maji.

Amezungumza hayo katika Ofisi za Dawasa jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa sheria hii mpya itasaidia Mambo mengi ikiwa ni pamoja na udhibiti wa maji ambayo yamekuwa yakipotea kwa asilimia 44 mpaka sasa

Prof Mkumbo amesema wizara inapendekeza kuanzishwa kwa Taasisi maalumu  ya kushughulikia miradi ya maji mijini na vijijini yaani Rural Water Agency, Taasisi ambayo imekusudia kuimarisha Jumuia za watumiaji wa maji kwa ngazi za vijiji na miji ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa Taasisi mpya ya Dawasa

Kutunga kwa sheria hii mpya ya maji kutaongeza matamanio kwa watumiaji wa maji na kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama kwa uhakika  zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya DAWASA Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka wananchi wa Dar Es Salaam na Pwani kushirikiana na Dawasa katika ufanyaji kazi wake hasa kutoa taarifa punde inapobainika uvujaji wa maji, na kusisitiza kuhusu utungaji wa sheria mpya unapofanyika wananchi watoe maoni ili mchakato uwe na tija kwani sheria hii ina manufaa makubwa kwa wananchi.
Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Menejiment mpya ya Mamlaka ya Maji Taka na Maji Safi (DAWASA) inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) leo baada ya kukutana nao ofizi za DAWASA Jijini Dar es Salaam.

WAFANYA BIASHARA WA VIPODOZI WA KARIAKOO: TUMECHOKA KUKAMATWA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU

$
0
0
 Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na wamiliki wa maduka ya vipodozi ya Kariakoo. Waliokaa toka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa za Dawa wa TFDA, Bw. Adonis Bitegeko (wa pili), Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya biashara wa Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Martin Mbwana (wa kwanza) na Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba, Vipodozi na Bidhaa Dawa, Bi Grace Shimwela
 Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa za Dawa wa TFDA, Bw. Adonis Bitegeko (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina elekezi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya biashara hao Bw. Martin Mbwana (aliyesimama)akizngumza wakati walipozungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo amesema kuwa "tumechoka kukamatwa mara kwa mara na vipodozi vyenye sumu, mitaji yetu inafilisika, sasa tunahitaji elimu  na kuzingatia matakwa ya kisheria”  anaongea,   wakati alipokuwa akichangia maada"
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya vipodozi ya Kariakoo wakifuatilia mojawapo ya maada.     

Na: James Ndege – Dar es Salaam
TFDA imetoa elimu kwa wafanya biashara wa vipodozi zaidi ya 30 wanaomiliki maduka ya jumla na rejareja wa eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaaam kwa lengo kuwakumbusha mambo muhimu ya kisheria ya kuzingatia katika kufanya biashara hiyo nchini.

Semina hiyo elekezi iliyoratibiwa na Mamlaka kwa kushirikiana na Uongozi wa wadau hao, imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Margareth Ndomondo-Sigonda uliopo TFDA Makao Makuu leo tarehe 7/9/2018.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa za Dawa wa TFDA, Bw. Adonis Bitegeko, alisema “TFDA kama Taasisi ya Umma, ni rafiki kwa wafanyabiashara wote wakiwemo wa vipodozi, na ipo tayari kusikiliza kushauri na kujenga mazingira rafiki ya kufanya biashara kwa lengo la kupata bidhaa salama, bora na zenye ufanisi ili kulinda afya ya jamii na kuleta maendeleo ya nchi”.

“Wafanya biashara wa vipodozi tuliopo Kariakoo na maeneo mengine, tumechoka kukamatwa mara kwa mara na vipodozi vyenye sumu, mitaji yetu inafilisika, tunapelekwa mahakamani sasa tunahitaji elimu ya namna ya kufanya biashara hii kwa kuzingatia matakwa ya kisheria na si vinginevyo” alisema Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanya biashara hao, Bw. Martin Mbwana wakati alipokuwa akichangia mada.

Kwa upande wake, Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba, Vipodozi na Bidhaa Dawa, Bi Grace Shimwela alisema, “Kwa mujibu wa Sheria, hairuhusiwi kuingiza vipodozi au bidhaa zinazodhibiwa na Mamlaka ndani ya nchi au katika soko bila ya kusajiliwa na TFDA. Kabla ya kuingiza bidhaa toka nje ya nchi,, hakikisha una kibali cha TFDA ili kuepusha kuingiza bidhaa ambazo si salama na bora ambazo zitaharibiwa au kurudishwa zilikotoka kwa gharama yako. 

Pia wakati wa kufuatilia maombi yenu TFDA hakikisheni mnawasilisha nyaraka stahiki, msighushi vibali wala kufanya udanganyifu wa kodi kwani mambo hayo yatasababisha shehena za mizigo yenu ishikiliwe na kufunguliwa kesi. Ninyi wamiliki mnatakiwa kuwasiliana moja kwa moja na TFDA mkipata changamoto zozote, chukueni tahadhari kwa baadhi ya mawakala wa mizigo wasiyo waaminifu mliowapa dhamana ya kufuatilia uingiaji wa mizigo ya biashara zenu”. 

Wafanya biashara hao waliishukuru Mamlaka kwa kuwapa elimu muhimu ambapo waliomba iwe endelevu na ishirikishe makundi mbalimbali ya wafanya biashara wakiwemo mawalaka wa mizigo nchini ili kuepuka kuingiza bidhaa zenye madhara kwa watumiaji. “Badala ya kutegemea bidhaa za nje ya nchi pekee, tumieni fursa iliyopo ya Serikali ya Awamu ya Tano, anzisheni viwanda vya vipodozi na TFDA itasaidia kutoa ushauri ili vikidhi vigezo vinavyotakiwa”, alisema Bw. Adonis Bitegeko.

PROFESA KITILA MKUMBO AZUNGUMZA NA WATENDAJI WA DCCA

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo ametembelea na kufanyamazungumzo na watendaji wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA)jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kikao  na Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, Domina Msonge akitoa taarifa fupiya Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kwa 2017/2018 mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kutembelea ofisi zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa  walipotembelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo jijini Dar es Salaam na kumsomea taarifa ya Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kwa 2017/2018.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, Domina Msonge (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa taarifa fupi ya Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kwa 2017/2018 mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kutembelea ofisi zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko, biashara naMahusiano wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, Egwaga Nungu
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


BENKI KUU YATOA MAFUNZO KWA WABUNGE

$
0
0
 Kushoto ni Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia kwa makini maelezo ya mwezeshaji katika Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza katika Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa Wabunge wote yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wabunge wakifuatilia Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa Wabunge wote yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images