Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Wabunifu wa Tehama wa kilimo na Afya wahitajika kutatua changamoto zilizopo

$
0
0
SEKTA ya Kilimo ya Afya inatakiwa kuwa na wabunifu mbalimbali katika kuweza kutatua matatizo yaliyopo katika sekta hizo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha wabunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) Mtafiti Mwandamizi katika Idara ya Utafiti wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Rodgers Msuya amesema vijana wabunifu katika teknolojia wanahitajika katika kutatua changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali nchini.
Amesema kuwa wabunifu hao wanaweza kufanya ubunifu kwa kuweza kutengeneza sauti ya kukimbiza Mbu bila ya kuacha madhara kwa binadamu kisha tatizo la Malaria kuisha.
Msuya amesema kuwa warsha hiyo kati ya Tanzania na Afrika Kusini ni ushirikiano katika mradi wa utafiti katika sekta ya Kilimo na Afya na baadaye timu ya watu wawili katoka nchi ya Tanzania na Afrika Kusini  hiyo kuleta shuluhisho ya matatizo yanayokabili sekta hizo.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech)  Dkt Amos Nungu amesema kuwa warsha hiyo imekuja katika wakati serikali iko katika uchumi wa viwanda hivyo lazima kuwepo kwa wabunifu kuweza kutatua changamoto.
Amesema kuwa vijana wabunifu bado wanahitajika katika kufanya ubunifu ambao utakuwa suluhisho katika matatizo yanayobili sekta mbalimbali.
 Mtafiti Mwandamizi katika Idara ya Utafiti wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Rodgers Msuya akizungumza katika warsha ya wabunifu wa Tehama kati Afrika Kusini na Tanzania ,warsha hiyo imefanyika katika ukumbi wa Costech Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dkt Amos Nungu akizungumza kuhusiana na uhitaji wa wabunifu katika sekta mbalimbali katika warsha ya wabunifu wa Tehama iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijibni Dar es Salaam.
 Baadhi ya  wadau wa utafiti na ubunifu wa Tehama walioshiriki warsha hiyo kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Picha ya pamoja wabunifu wa Tehama katika warsha uliyokutaanisha Tanzania na Afrika Kusini.

Madereva wasio na vyeti waaswa kuchangamkia fursa za mafunzo VETA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMANDA wa kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Fortunatus Musilimu amewataka madereva nchini kuchangamkia fursa za mafunzo ya udereva bora katika vyuo mbalimbali ikiwemo vyuo vya VETA.

Akizungumza wakati wa mahafali ya mafunzo ya muda mfupi katika Chuo cha VETA Dar es Salaam Kamanda Musilimu alisema zoezi la ukaguzi wa vyeti kwa madereva litafanyika kama ilivyopangwa ambapo baada ya miezi mitano iliyotolewa na Jeshi la Polisi kwa madereva kurudi shuleni na kupata vyeti kumalizika, hakutakuwa na mjadala tena bali hatua stahiki zitachukuliwa.

“Nawakumbusha madereva kuwa mwezi mmoja umeisha katika ile miezi mitano iliyotolewa…. Nawasihi tena kutumia vizuri muda uliobaki wakasome…”Alisema

Alisema vyeti vyote vitatakiwa kuwa na sahihi ya Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa ili kuhakikisha hakuna udanganyifu katika upatikanaji wa vyeti hivyo.

Kamanda Musilimu aliwaasa vijana waliohitimu mafunzo katika chuo cha VETA kuhakikisha wanatumia vyema ujuzi walioupata kuanzisha shughuli zao za kujiingizia kipato kulingana na fani walizosoma.

Naye Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Stella Ndimubenya aliwataka vijana kutumia vyema fursa zinazopatikana katika Halmashauri zao kuwa kuna fungu maalum kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufanya shughuli za ujasiriamali wakiwa kwenye vikundi.

Awali, Mkuu wa Chuo hicho Douglas Kipokola alisema chuo chake kwa kushirikiana na chuo cha VETA Kihonda wamejipanga vyema kutoa mafunzo ya udereva bora kwa madereva wote wataohitaji kupata mafunzo hayo.

Alisema hivi karibuni chuo hicho kimeanza kutoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa/malori yanayobeba mizigo na kwamba mtaala wake umeshapitishwa ambapo mafunzo hayo yameanza kutolewa tarehe 3 Septemba mwaka huu huku kukiwa na madereva 30 wanaopata mafunzo kwa wamu ya kwanza.

Kipokola alisema katika mahafali hayo,jumla ya wanafunzi 1125 wamehitimu mafunzo ya muda mfupi na katika fani mbalimbali ikiwepo Udereva, Uendeshaji wa hiteli, uhazili, umeme, compyuta, mapishi, Nywele na urembo na ufundi wa magari.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani , Fortunatus Muslimu akizungumza katika mahafali ya Chuo cha Veta Changombe yaliyofanyika Chuoni hapo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Stella Ndimubenya akizungumza katika mahali ya Chuo cha VETA Changombe kuhusiana na VETA katika uimarishaji katika utoaji wa Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Mkuu wa Chuo VETA Chang’ombe Douglas Kipokola akitoa historia ya chuo katika uandaji wa nguvu kazi ya taifa yenye ujuzi.
 Picha mbalimbali za matukio katika mahafali ya Chuo cha VETA Chang'ombe.

MAMLAKA HALI YA HEWA YATANGAZA UWEZEKANO WA KUNYESHA MVUA JUU YA WASTANI,WATABIRI MAGONJWA YA MLIPUKO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imeeleza uwepo wa uwezekano mkubwa wa kunyesha mvua nyingi za wastani hadi juu ya wastani katika msimu wa mvua za vuli kipindi cha Oktoba Dsemba mwaka huu.

Pamoja utabiri huo TMA pia imetoa  athari na ushauri wa mvua hizo ikiwemo kuwepo kwa hali ya unyevunyevu wa udongo na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajia kuimarika katika maeneo mengi ya ukanda wa nyanda za juu Kaskazini Mashariki na Pwani ya Kaskazini.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA ,Dkt Agnes Kijazi ametangaza utabiri huo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari.

Amefafanua kwamba  mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa  inaonesha kuwepo kwa mkubwa wa mvua za vuli kuwa za wastani katika maeneo mengi ya nchi.

 Ameongeza mvua za vuli kipindi cha Oktoba hadi Desemba ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

“Mvua za Vuli 2018 zinatarajiwa kuanza mapema katikati ya Septemba na mwanzoni mwa Oktoba 2018 katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua.

"Ambapo kwa mikoa ya Kagera ,Geita na wilaya ya kibondo mvua inatarajia kunyesha wastani hadi chini ya wastani,”amesema Dk.Kijazi

Wakati katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki pamoja na maeneo ya mashariki na kusini mwa ziwa Viktoria inatarajia kunyesha mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Ameeleza  mvua zinatarajia kuanza mapema kati ya wiki ya pili na ya tatu ya Septemba mwaka huu katika maeneo ya mkoa wa Mara na kusambaa katika mikoa ya Shinyanga ,Simiyu,Mwanza ,Geita na Kagera ifikapo wiki ya tatu ya Oktoba mwaka huu.

 Pia amesema katika ukanda wa Pwani wa kaskazini katika mikoa ya Dar es Salaam ,Tanga,Pwani ,Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro mvua zinatarajia kuanza mapema wiki ya nne ya Septemba ambapo itanyesha mvua ya wastani hadi juu ya wastani,”alisema Dk. Kijazi

Akielezea zaidi utabiri huo amesema katika maeneo ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara mvua inatarajia kunyesha kati ya wiki ya pili ya Oktoba mwaka huu  na inatarajiwa kunyesha wastani hadi juu ya wastani.

Dk.Kijazi amesema mazao yasiyohitaji maji mengi yanaweza kuathiriwa na hali ya unyevunyevyu wa kupitiliza na maji kutuama.

Pia amesema magonjwa ya wanyama na upotevu  wa samaki kutokana na uharibifu wa miundombinu ya kufugia samaki vinaweza kujitokeza kutokana na mvua za juu ya wastani zinazotarajiwa katika maeneo hayo.

Ameongeza upande wa sekta ya afya  kutakuwa na uhaba wa maji salama kwa shughuli za binadamu ikiwemo usafi katika maeneo yanayotarajia kupata mvua za chini ya wastani  huku milipuko ya magonjwa inaweza kujitokeza.

Hivyo amesema menejimenti za maafa zinashauriwa kuandaa mkakati wa kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za vuli .

"Hivyo zinapaswa kuandaa mbinu za kukabiliana na mafuriko pamoja na majanga yatokanayo na mafuriko," amesema.

Pamoja na mambo mengine amewaomba wananchi kuchukua tahadhari iwapo mvua zitanyesha juu ya wastani.

TBA WAKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA BUNJU, WANANCHI WAKARIBISHWA KUZINUNUA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Elias Kwandikwa amefanya ziara katika mradi wa nyumba zinazojengwa kupitia wakala wa majengo nchini (TBA) katika eneo la Bunju jijini Dar es salaam na kushauri wanananchi kujitokeza kununua nyumba hizo.

Akiongea baada ya kukagua nyumba hizo Kwandikwa amesema kuwa amekagua mradi huo na kuridhishwa na unavyoendelea kwa kuwa hadi sasa nyumba 279 kati ya nyumba 851 ambazo zipo kwenye malengo zimekamilika.

Kwandikwa amesema kuwa wananchi na wafanyakazi wajitokeze kununua nyumba hizo na kama serikali wanasimamia ili waweze kupata kilicho bora.

Aidha ameeleza kuwa heka 650 zilizopo Dodoma zitaanza kufanyiwa mradi huo mapema ili kuweza kuongeza makazi ya kutosha jijini humu katika wakati huu ambapo idara nyingi zimehamia Dodoma.

Pia amewataka wakala wa majengo nchini kutoa matangazo ili wananchi wajue kuna nyumba nzuri na bora zilizokamilika ili waweze kununua.

Na amewataka wafanyakazi wa wakala hiyo kufanya kazi kwa weledi na amewashauri waharakishe mradi wa ujenzi wa nyumba Dodoma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TBA  Idara ya miliki Baltazari Kimangano ameeleza kuwa kuna nyumba za viwango vyote  na hadi sasa nyumba 105 zimekamilika  na wateja bado wanauhitaji na kwa wafanyakazi wanaweza kulipia miaka 7 kwa nyumba hizo.

Pia amesema kuwa wateja wanaweza kupata mikopo kupitia benki za CRDB, NBC, BOA na wanamazungumzo na benki ya Zanzibar ambazo zitatoa mkopo kwa riba nafuu kwa wateja wao ili kuweza kupata nyumba hizo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh. Elias Kwandikwa (katikati)akiwa na viongozi wa wakala wa majengo nchini (TBA) wakati alipofanya ziara ya kukagua nyumba za umma zilizojengwa na TBA zilizokamilika huko Bunju.
 Mkurugenzi wa Idara ya umiliki wa  mamlaka ya majengo nchini Bartazari Kimangano (kushoto) akimuongoza naibu waziri kukagua baadhi ya nyumba hizo.
Baadhi ya nyumba  zijulikanazo kama Villa ambazo zimekamilika na zipo tayari kwa makazi.

DC SOPHIA MFAUME AHIMIZA WADAU WA MAENDELEO KUWEKEZA WILAYANI NAMTUMBO

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sofia Mfaume amesema kuna kila sababu ya sekta binafsi na sekta za umma kushirikiana kuhakikisha Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla inapiga hatua kimaendeleo.

Amesema sekta hizo zikishirikiana katika kutatua changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Namtumbo wananchi watapiga hatua kubwa kimaendeleo huku akiomba sekta binafsi kuwekeza ndani ya wilaya hiyo.

Mfaume amesema hayo leo wakati wa mkutano kati ya sekta binafsi na sekta za umma wilayani Namtumbo.

Amesema lengo la mkutano huo ni wadau wa maendeleo kupitia sekta hizo kujadili na kuweka mikakati ya kutatua changamoto na kisha kufanya maendeleo.

Amewaambia wadau wa maendeleo ni vema wakatambua Wilaya ya Namtumbo kuna fursa nyingi ambazo zikitumika vizuri kutakuwa na maendeleo.

“Wilaya yetu ya Namtumbo tunayo ardhi ya kutosha na yenye rutuba inayokubali mazao ya kila aina.Wananchi wanaitumia vema ardhi iliyopo katika kujiletea maendeleo.

“Ombi langu kwa wadau wa sekta zote hizi tushirikiane katika kuleta maendeleo na kwetu tutafurahi tukiona viwanda vinajengwa zaidi na hasa vya kuongeza thamani ya mazao ya wakulima,”amesema Mfaume.

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Namtumbo ambao wamepata nafasi ya kuuzungumzia mkutano huo wamesema unaonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa maendeleo ndani ya wilaya yao na zaidi wanampongeza Mkuu wao wa Wilaya kwani amekuwa chachu ya maendeleo ya wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume akizungumza wakati wa mkutano kati ya sekta binafsi na sekta za umma uliofanyika wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma leo

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA KAZI GABRIEL MALATA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna wa Kazi, Bw. Gabriel Malata (wa kwanza kulia). (Kushoto ni) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakimsikiliza Kamishna wa Kazi Bw. Gabriel Malata (hayupo pichani).
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza jambo walipomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Ofisini kwake Jijini Dodoma, (kulia ni) Kamishna wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Gabriel Malata. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

KATIBU MKUU UVCCM AWATAMBULISHA WAKUU WA IDARA WAPYA KWA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU UVCCM LEO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl.Raymond Mwangwala (MNEC) akizungumza na watumishi wa Makao makuu wakati akiwatambulisha wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walioteuliwa na Kuthibitishwa na baraza kuu la UVCCM Taifa lililoketi jijini Dodoma wiki iliyopita
o
 Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Siasa Ndg Peter Kasela akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg.Hassan Bomboko  akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Kamana Juma Simba  akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Uchumi na Uwezeshaji Ndg.Nelson Lusekelo akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM



Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja

$
0
0
Na Greyson Mwase, Dodoma
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amemwagiza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kuhakikisha wanakipatia kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini kijulikanacho  kwa jina la “Hapa Kazi Tu” kinachoendesha shughuli za uchimbaji wa madini aina ya sunstone katika kijiji cha Suguta wilayani Kongwa mkoani Dodoma leseni ya uchimbaji madini ndani ya mwezi mmoja kwa kufuata kanuni na sheria za madini.

Profesa Kikula alitoa agizo hilo tarehe 05 Septemba, 2018 katika  machimbo ya madini hayo yaliyopo katika kijiji hicho kwenye ziara yake ya siku mbili katika wilaya za Kongwa na Mpwapwa yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo, kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.

Katika ziara hiyo, Profesa Kikula aliambatana na Makamishna wa Tume, Profesa Abdulkarim Mruma na Haroun Kinega, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya pamoja na waandishi wa habari.

Mara baada ya kusikiliza kero za wachimbaji wadogo hao Profesa Kikula mbali na kutoa  agizo hilo alimwelekeza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, kuhakikisha anasaidia kikundi cha wachimbaji wadogo hao katika taratibu zote za usajili wa kikundi  kabla ya kuanza kushirikiana na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma katika upatikanaji wa leseni ndani ya mwezi mmoja.

Aidha, Profesa Kikula alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasaidia wachimbaji hao katika usajili kwenye vyama vya  wachimbaji madini Tanzania pamoja na utafutaji wa masoko na bei elekezi kwenye masoko ya kimataifa.

“Kutokana na kuwa na mtandao mkubwa na uelewa kwenye masoko na bei elekezi za madini kwenye masoko ya kimataifa, nakuelekeza kama Mwenyekiti wa wachimbaji kuhakikisha unawasaidia wachimbaji hawa hususan kwenye maeneo ya masoko na bei elekezi ili uchimbaji wao uwanufaishe wao na Serikali kupata mapato stahiki,” alisema Profesa Kikula.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
 Kutoka kushoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya, Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Deogratius Ndejembie na Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) na Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma (kulia) wakiangalia moja ya mawe ili kubaini madini yaliyomo kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (mbele) pamoja na msafara wake wakiendelea na ziara kwenye kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Mmoja wa watendaji wa migodi ya shaba ya Rays Metal Corporation na Tambi Minerals Resources iliyopo katika kijiji cha Tambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati). Kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega.

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APOKEA ALBUM YA GOLD YA BARNABA CLASSIC WODINI MOI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla amempongeza msanii nyota wa kizazi kipya nchini Bongo flava, Elias Barnaba maarufu kama Barnaba Classic kwa hatua yake ya kutoa albam ya Gold ambayo itasaidia kumtangaza zaidi kwenye medani za muziki ndani na nje ya nchi.

Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo mapema leo Septemba 6,2018 wakati alipotembelewa na msanii huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4, na kumkabidhi rasmi CD ya album yake ya GOLD ambayo imeingia sokoni 31 August mwaka huu. Katika hatua hiyo Waziri alimshukuru kwa kumtembelea ambapo pia alimpatia ushauri namna bora ya kuiuza albam hiyo ya GOLD ikiwemo soko la kimataifa.

"Nilipata mwaliko wako wa uzinduzi wa albam ya Gold. Bahati mbaya sikuweza kufika kutokana na ajari. Lakini naendelea vizuri na nashukuru kwa kufika kuja kuniona na kunikabidhi rasmi..natambua wasanii pia ni nguzo katika kukuza Utalii wetu ikiwemo kuutangaza kupitia ala na mashahiri yenu na ndio maana mwezi huu wa Septemba tunakuja na tamasha la Urithi ambalo Wasanii wamepewa nafasi ya kipekee" alieleza Waziri Dkt.Kigwangalla.

Kwa upande wake Barnaba alimshukuru Waziri Dkt Kigwangalla kwa kuipokea Album hiyo ambayo imezingatia vigezo vyote na ubora wa hali ya juu. "Kwanza nikupe pole kwa ajari. Naamini wasanii na wadau wote tunakuombea upone haraka na urejee kwenye majukumu yako ya kila siku ya kukuza Maliasili zetu na Utalii kwa ujumla na upokee albam hii ya Gold ikuburudishe unapoendelea kuuguza majeraha, Asante Sana" alisema Msanii huyo wakati wa kumkabidhi Albam hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa Mxcater amesema albam hiyo iliyosheheni nyimbo Bora na kali zikiwemo Chausiku, Lover Boy na nyingine nyingi inapatikana katika maduka ya mtandao yaani (Online) kupitia Boomplay Music."Kwa watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia App ya BoomplayMusic_tz na wataipata moja kwa moja" alisema Mxcater.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa  na msanii  huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4 mwaka huu. Kulia kwa Waziri ni Meneja wa Msanii huyo Michael Mlingwa 'Mxcater'.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla akipokea CD ya albma ya Gold kutoka kwa msanii nyota wa Bongo flava Elias Barnaba 'Barnaba Classic' mapema leo Septemba 6, 2018, wakati alipotembelewa  na msanii  huyo katika wodi ya Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto aliopata ajari Agosti 4 mwaka huu.
Habari na picha na Andrew Chale

RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWENYE MABWAWA NA VIZIMBA KATIKA KAMBI YA JESHI 27KJ MAKOKO-MUSOMA MKOANI MARA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka ,Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka , Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa kuashira uzinduzi rasmi wa Mabwawa 9 na Vizimba vya kufugia samaki aina ya Sato katika Kambi ya Jeshi YA 27 KJ Makoko Mkoani Mara.Wengine ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina,Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt.Frolence Turuka ,Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima,Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.Modestus Kimbilimba.Septemba 6,2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima mara baada ya kukata kuzindua rasmi mradi wa ufugaji wa Samaki wa kwenye mabwawa katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mradi wa ufugaji wa Samaki wa kwenye mabwawa wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mradi huo katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.

 Askari wa Jeshi la kujenga Taifa wakiwawekea samaki chakula katika Mabwawa ya kufugia samaki hao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018.
 Askari wa Jeshi la kujenga Taifa wakiwvua samaki katika Mabwawa ya kufugia samaki hao wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kambi ya Jeshi 27KJ Makoko Musoma Mkoani Mara.Septemba 6,2018. (PICHA NA IKULU)

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MAKUTANO-NYAMUSWA-SANZATE –NATA-IKOMA GATE KM 135 SEHEMU YA MAKUTANO-SANZATE 50KM, BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Maria Nyerere mke wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara bada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiimba na kucheza pamoja na vijana wa Kambi ya  JKT Rwamkoma iliyopo mkoani Mara mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Butiama(hawaonekani pichani) kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Makutano-Nyamuswa- Sanzate-Nata-Ikoma gate km 135 katika sehemu ya Makutano-Sanzate km 50 katika sherehe zilizofanyika Butiama mkoani Mara.
Mzee Joseph Butiku akiwa amekaa na Mwanasiasa mklongwe Stephen Wassira pamoja na viogozi wengine wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Magufuli katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi Butiama mkoani Mara. 
 Kikundi cha ngoma za asili cha Engubha cha kabila la wakabwa wenyeji wa Butiama mkoani Mara kikitumbuzia katika sherehe hizo. PICHA NA IKULU

WAKAZI WA LUMUKI WAPATA SHIDA KUTOKANA NA KUKOSA KIVUKO

$
0
0
 
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

BAADHI ya wakazi wa mitaa ya Lumumba ,Muheza na Kidimu (LUMUKI) wilayani Kibaha ,mkoani Pwani ,wanahitaji serikali iwasaidie kuwajengea daraja ama kivuko kwenye mto Mpiji ili kunusuru maisha yao. Wakazi hao kwasasa wanapata shida ya kuvuka kwenda mtaa wa Kibwegere kata ya Kibamba ,wilaya ya Ubungo ambako ndipo wanategemea kupata huduma za kijamii. 

Walifikisha kero hiyo ,walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi la ujenzi wa nguzo kwa ajili ya kuvusha watu . Mwenyekiti wa ujenzi wa daraja hilo la LUMUKI, Iddi Chamale alisema ,changamoto kwenye eneo hilo ni kubwa .

Aidha , wamekuwa wakiweka vivuko vya muda ambapo huweka mabanzi kwa ajili ya kuvuka ambapo wakati wa mvua kubwa yanasombwa na maji hayo. “Kivuko kikisombwa shida ndipo zinapoanza kwani hubidi watu wavushwe kwa kubebwa ambako kuna mamba wengi na ni hatari kwani maji yakiwazidia ni hatari watu wanapoteza maisha,” alifafanua Chamale. 

“Makao makuu ya wilaya ya Kibaha ni mbali lakini kwa kuvuka mto ni karibu hivyo inatubidi twende Kibwegere, tumetenganishwa na mto Mpiji lakini kinachotusumbua ni sehemu ya kuvuka ” alisema Chamale.

Nae Neema Zawadi alisema , kipindi cha mvua ni taabu kwani mawasiliano hukatika na watu hupoteza maisha wanapojaribu kuvuka huku wajawazito hujifungulia njiani kabla ya kuvuka mto. “Wanafunzi hushindwa kwenda shule wazazi huogopa wasivushwe,wafanyakazi huwabidi wakae ngambo hivyo kutorudi nyumbani hivyo hata ndoa zetu zinayumba”alisema Neema. 
 
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Pangani iliko mitaa hiyo Agustino Mdachi ,alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema jitihada wanazofanya ni kujenga vivuko lakini havidumu . Alielezea, amekuwa akiwasilisha changamoto hiyo halmashauri lakini tatizo ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kujenga daraja. Mdachi alisema atawasiliana na wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili walishughulikie suala hilo. 

Diwani wa kata ya Pangani Kibaha mkoani Pwani, akielezea kero ya kivuko kwa wakazi wa eneo la Lumumba na Kidimu. Picha na Mwamvua Mwinyi 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

NDUGULILE ATOA SIKU 14 KUKAMILISHWA KWA MASHINE YA X RAY HOSPITALI YA RUFAA DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kitabu cha taarifa mbalimbali za hospitali wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, kulia kwake ni katibu wa afya wa hospitali hiyo Mwanaisha Hassan.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kuhakikisha mashine ya kutolea huduma za X-ray  inafanya kazi ndani ya siku 14. 

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kuangalia na kujiridhisha na hali ya utoaji huduma za afya  katika Hospitali hiyo leo jijini Dodoma. 

"Ifikapo Septemba 21 nataka kuona mashine ya kutolea huduma za X-ray na vifaa vingne viwe tayari kutoa huduma kwa wananchi wa Dodoma na maeneo yanayoizunguka kwani Hospitali hii ni tegemezi kwa wakazi wa mkoa huu la sivyo hatua stahiki zitachukuliwa bila ya kumuonea mtu haya" alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha,Dkt. Ndugulile ametoa siku 30 kwa uongozi wa hospitali hiyo kukarabati jengo la bima ya afya baada ya kukagua na kutoridhishwa na muonekano wake kwani linaleta kero kwa wateja wanaokwenda kupata huduma Hospitalini hapo. 

Mbali na hayo Dkt.  Ndugulile ameonekana kukerwa na uzembe  wa watendaji wa Hospitali  hiyo na kusababisha kuwakemea vikali na kuhaidi maagizo aliyoyatoa yasipotekelezwa kwa wakati hatua za kinidhamu zitakuchululiwa kwa vitendo.

Wakati huo huo dkt.Ndugulile ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuwarudishia fedha wagonjwa walizotumia kununua dawa pamoja na sindano kwenye maduka yaliopo nje ya hospitali hiyo ilihali wana vifaa hivyo  takribani ya kutosha miezi sita kwenye stoo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikagua maboksi ya sindano katika stoo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wagonjwa waliokua wanasubiri huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali hiyo.

Meli ya Kwanza iliyobeba Tani 7,250 za Reli za SGR kutoka Japan yawasili nchini

$
0
0

Meli ya Kwanza iliyobeba Tani 7,250 za Reli za SGR kutoka Japan imetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na kazi ya kupakua reli na kupeleka eneo la ujenzi imeanza jana Septemba 06, 2018 tayari kwa ajili ya kutandika reli. Meli nyingine ya Reli za SGR inatarajiwa kufika mwezi Oktoba 2018.

Meli iliyobeba Tani 7,250 za Shehena ya Reli za SGR ikiwa katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.

Kazi ya kupakia Shehena ya Reli za SGR ikiendelea katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.


Tani 7,250 za Shehena ya Reli za SGR zikipakuliwa kutoka kwenye Meli katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.
Kazi ya kupakia Reli kwenye mabehewa ikiendelea katika Bandari ya Dar es Salaam Septemba 06, 2018.

Kongamano la Watanzania wanaoishi Marekani chini ya DICOTA lafanyika Seattle

$
0
0
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson M. Masilingi, akizungumza wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa, aliyekuwa amealikwa kufungua Kongamano la Watanzania wanaoishi Marekani, lililoandaliwa na DICOTA (Diaspora Council of Tanzanians in America) tarehe 31 Agosti, 2018 hadi tarehe 2 Septemba, 2018 Seattle, Marekani.
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba John Kabudi, akiwasilisha hotuba yake kuhusu tulipotoka baada ya Uhuru, tulipo sasa, tunapoelekea, mafanikio na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Washiriki wa Kongamano la Diaspora, Marekani wakishangilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoshehini mafanikio na mipango kabambe ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Washiriki katika Kongamano la Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani lililoandaliwa na DICOTA (Diaspora Council for Tanzanians in America), wakifuatilia Hotuba hiyo katika Hoteli ya Seattle Marriott Belleview, Seattle, Washington, Marekani tarehe 31 Agosti 2018 hadi tarehe 2 Septemba 2018.
Picha ya pamoja ya Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Kongamano la Diaspora, Seattle, Washington, Marekani na viongozi wa DICOTA wenyeji wa Kongamano hilo.

WAFANYABIASHARA MNARANI WAKINZANA NA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA KATIKA KODI

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA.

MADUKA ya baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mnarani, Loliondo, halmashauri ya Mji wa Kibaha, Pwani, yamefungwa kwa siku tatu baada ya kushindwa kulipia kodi kwa zaidi ya mwaka sasa. Kufuatia kufungwa kwa maduka hayo, wameiomba ofisi ya mkuu wa mkoa huo iingilie kati suala hilo kwani wanatakiwa kulipa sh.8,000 kwa mita za mraba kiasi ambacho ni kikubwa kwao.

Mfanyabiashara aliyefungiwa duka lake ,Henry Makundi alisema wamehamishiwa kutoka Maili Moja stendi na kupewa maeneo Loliondo ili wajenge maduka na fedha zao watafidia kwenye kodi.  Alieleza, walikuwa wanataka kuwe na mafungu matatu ya malipo moja ya tatu mkurugenzi na moja ya tatu mfanyabiashara na moja ya tatu iwe ya mfanyabiashara kama wawekezaji moja ya tatu iwe kama faida.

Makundi alielezea ,halmashauri inataka asilimia 50 na mfanyabiashara 50 ili kurudisha gharama jambo ambalo hawakubaliani nalo.

Nae mwenyekiti wa soko hilo ,Ramadhan Maulid alishangaa kuona maduka yanafungwa. Alisema kwamba,kulikuwa na makubaliano walipe mita za mraba 4,000 huku akiwepo mkurugenzi na mbunge wa mji huo hivyo wanashangaa kuambiwa walipie sh 8,000.

Maulid alifafanua, kutokana na hali hiyo wanaendelea na mazungumzo na katibu tawala wa mkoa ili kuangalia namna ya kulishughulikia suala hilo .
Akijibu hoja za wafanyabiashara hao mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Jeniffer Omolo alisema ,walikubaliana kuwa wafanyabiashara wajenge maduka kwa gharama ya sh .milioni tano na halmashauri walitoa ardhi lakini hawajalipa kodi zaidi ya mwaka sasa.

Kwa mujibu wake ,wamegundua wengi wanaofanya biashara ni wapangaji na sio waliojenga maduka ambayo wanapangisha kuanzia sh.300,000 hadi sh.400,000 kwa mwezi.

Jennifer alibainisha ,kwa mwaka wanapata kati ya sh.milioni 3.6 - milioni 4.8 kwa miaka miwili anakuwa amerejesha gharama zake za ujenzi .

Mkurugenzi huyo aliwataka ,wale ambao gharama zimezidi ya waliyokubaliana waende ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo.

Jennifer alielekeza ,wafanyabiashara ambao hawajalipa kodi kulipa kwani kutolipa kodi ni kinyume cha sheria , ili waepukane na usumbufu.

KATIBU MKUU UVCCM AWATAMBULISHA WAKUU WA IDARA WAPYA KWA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU UVCCM LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) pamoja na wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walipowalisi katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya Makao Makuu UVCCM Upanga Dar Es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl.Raymond Mwangwala (MNEC) akizungumza na watumishi wa Makao makuu wakati akiwatambulisha wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walioteuliwa na Kuthibitishwa na baraza kuu la UVCCM Taifa lililoketi jijini Dodoma wiki iliyopita.
Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Kamana Juma Simba  akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) akiwaongoza wakuu wa Idara za Makao makuu ya Umoja wa Vijana wakati akiwatembeza maeneo mbali mbali ya Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam
(Picha na FahadiSiraji wa UVCCM).

MAHAKIMU WAANDAMIZI WAPONGEZA ELIMU WALIYOIPATA KUHUSU SHERIA YA FIDIA KWA MFANYAKAZI

$
0
0
 Waheshimiwa Mashakimu Wakzi wa Mikoa na Wilaya kutoka Mikoa mitano ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wakiwa kwenye mahakama ya mfano ili kujipima kuona uelewa wao kuhusu Sheria ya Bunge ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 5  [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] naada ya kushiriki mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na kuratibiwa kwa pamoja na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kufanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba 5-6, 2018.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

MAHAKIMU wakazi wafawidhi wa Mahakama za Mikoa na Wilaya kutoka mikoa mitano ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wamefurahishwa na mafunzo ya kuwajengea uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] ambapo jukumu lake kubwa ni kutoa fidia kwa wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya.
Kutokana na jukumu hilo la Mfuko, Chuo cha Uongozi wa Mahama Lushoto ambacho ndicho chenye dhamana ya kutoa mafunzo kwa watumishi waandamizi wa mahakama, kiliandaa mafunzo hayo ili kuwawezesha viongozi hao wa mahakama wa ngazi za mikoa na wilaya kuelewa vema Sheria hiyo ili iwe rahisi kwa wao kutoa maamuzi sahihi endapo mashauri yahusuyo fidia kwa wafanyakazi na shughhuli za Mfuko yatafika mbele yao. Amesema Mkuu wa Huduma za Sheria wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Abraham Siyovelwa.
Wakizungumza katika mahojiano baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele, alisema
“Nimefurahia sana kupata mafunzo haya, mimi nina nafasi mbili, kwanza kabisa kama mfanyakazi,  lakini pia kama mdau mkubwa wa Sheria ya Mfuko huu kama hakimu, nimefaidika sana na elimu hii kwani nimeelewa vitu vingi ambavyo hapo awali sikuwa nikivijua.”
Alisema, elimu aliyoipata kama mtumishi wa mahakama, ameelewa haki zake za msingi kuhusiana na Mfuko huo wa Fidia ameridhika na kufurahia kuwa anafanya kazi katika mazingira ya uhakika na akiamini pia hata wategemezi wake lolote likimtokea kutegemea na Mungu amepanga nini, basi wategemezi wake wanaweza kunufaika licha ya yeye mwenyewe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Chuom cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, (IJA), Mhe. jaji Dkt.Paul Kihwelo, akitoa nasaha zake kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya JIA na WCF. Aliyesimama kushoto ni mratibu wa mafunzo, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo hicho, Mhe. Lameck Samson.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, (wapili kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka, mwishoni mwa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo mahakimu wakazi wa mikoa na wilaya yaliyofikia kilele mkoani Morogoro Septemba 6, 2018. Wengine pichani ni Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa. na kulia ni Mhadhiri Msaidizi, Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Lameck Samson.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 7, 2018

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images