Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MARUFUKU MGAMBO KUNYANYASA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO - DC ARUMERU

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro amewaondoa Askari wa Jeshi la Akiba (MGAMBO) Waliokuwa katika Soko la Tengeru kutokana na Mgambo hao kutuhumiwa Kunyanyasa Wafanyabiashara Ndogo Ndogo wakiwemo kina Mama wanaouza bidhaa mbalimbali Sokoni Hapo.

Dc Muro ambae alifanya Ziara ya Kustukiza Sokoni Hapo amesikiliza Kero mbalimbali zikiwemo za Kuporwa bidhaa zao na kuvunjiwa mbao wanazotumia kupanga bidhaa zao jambo linalowapa wakati mgumu wa kufanya biashara zao ambazo wamekuwa wakizitumia kuongeza Vipato na kuhudumia Familia zao.

Kutokana na Malalamiko Hayo DC Muro amelazimika kuwaondoa Mgambo hao kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili, na Kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Ndugu Emmanuel Mkongo kupeleka Mgambo wengine mpaka hapo watakapomaliza Uchunguzi wa tuhuma Zao.

Katika Ziara hiyo pia Dc Muro amewataka kina Mama kuendelea kupanga bidhaa zao pembeni ya Soko kutokana na Miundombinu ya Soko kutomudu idadi Kubwa ya wafanyabiashara kwa wakati Mmoja jambo ambalo linasababisha Wafanyabiashara wengine kufanyiwa biashara zao kienyeji na kupelekea Halmashauri kukosa Mapato jambo lilionekana kumkera sana Dc Muro na kutoa maelekezo kwa wafanyabiashara hao kupanga biashara zao pembeni ya soko ili Halmashauri iweze kukusanya mapato yake ipasavyo. 

Soko la Tengeru linahudumia zaidi ya Wananchi elfu kumi na mbili kwa siku na kimekuwa sehemu ya chanzo kikuu cha Mapato ya Ndani kwa Halmashauri ya Wilaya Ya Meru.

Kwa upande wao Makundi ya wafanyabiashara ndogo ndogo mbali na kumshukuru Dc Muro kwa kuwaondolea kero hizo wamempongeza Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteu Dc Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambae ameendelea kugusa kero za Makundi mbalimbali ya Kijamii.

WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI

0
0
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewataka wananchi kupata taarifa sahii kutoka wizara yake na kuacha mara moja kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kupotosha jamii.

Ameyasema hayo leo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni ya umezeshaji wa dawa za kingatiba dhidi ya Kichocho na Minyoo ya tumbo nchini.Amesema waathirika wakubwa wa Kichocho na Minyoo ya tumbo ni watoto wenye umri wa kwenda shule,yaani watoto wenye umri kati ya miaka 5 na 14 ambao wanakuwa katika shule za msingi.

“Tunachotoa ni KINGATIBA na sio Chanjo,dawa hizi ni salama na zimethibitishwa ubora wake na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) pamoja na Shirika la Afya Duniani(WHO) pia zimesajiliwa kulingana na taratibu za nchi na mamlaka husika.

Amesema dawa hizo huimarisha afya ya mtoto na hivyo kujenga taifa lenye afya bora,nguvu ya kutosha ili kuleta maendeleo.
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na sintofahamu iliyozuka miongoni mwa jamii kuhusu utumiaji wa dawa kinga za minyoo na kichocho jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo juu ya matumizi ya dawa kinga za minyoo na kichocho ambazo zinatolewa hivi sasa katika jamii na kuwatoa hofu wananchi juu ya dhana potofu kuwa dawa hizo zina madhara.
Baadhi ya waandishi wa habari wakipata dawa kinga za minyoo na kichocho kutoka kwa Meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini (NTD) Dkt. Upendo Mwingira baada ya kikao kilichomuhusisha Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto na waandishi wa habari kuzungumzia dhana potofu iliyotanda katika jamii kuhusiana na madhara ya dawa hizo.
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akionesha dawa kinga za minyoo na kichocho zinazotolewa katika jamii hivi sasa na kuwataka wananchi wasihofu kumeza dawa hizo ambazo hazina madhara yeyote kiafya, wakati akifanya mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha ITV.

NEWZ ALERT:Rais Magufuli amteua Kamishna wa Polisi Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

NZEGA WAISHUKURU SERIKALI

0
0

Wananchi na viongozi wa wilaya ya Nzega wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuifanyia ukarabati mkubwa wa hospitali ya wilaya ya Nzega.

Shukrani hizo zimetolewa wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea wilayani hapo kuangalia maandalizi ya ukarabati wa hospitali hiyo ya wilaya.

Hospitali hiyo imepokea sh. milioni 800 ili kujenga majengo kwa ajili ya huduma zote za uzazi pamoja na ukarabati na ujenzi wa wodi ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Katika Ziara hiyo Waziri Jafo amezielekeza Halmashauri ya wilaya ya Nzega na ya Mji Nzega kuunda timu ya pamoja ya usimamizi wa ujenzi huo ili mradi huo ukamilike ndani ya miezi mitano.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua maeneo ambapo majengo mapya yatajengwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega.
 Viongozi wa Nzega wakimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
Wananchi wa Nzega wakisubiri huduma katika hospitali ya wilaya ya Nzega.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akitembelea kukagua miundombinu ya hospitali ya wilaya ya Nzega

RC HAPI AKUTANA NA WAMACHINGA IRINGA,AWAAHIDI KUENDELEA KUWA MTETEZI WAO

0
0
Awaahidi kuwa serikali itaendelea kuwa mtetezi wao siku zote
Wampa tuzo ya Rais Magufuli kwa utekelezaji wa ilani, kuwatetea

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekutana na kuzungumza na wamachinga wa Mkoa wa Iringa ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya makundi mbalimbali ya jamii mkoani humo.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara hao maarufu Machinga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameeleza mikakati ya serikali ya mkoa ya kuwatetea na kusimamia maslahi ya wamachinga ili watambuliwe na kusaidiwa kufanya shughuli zao vizuri.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watendaji wote wa Mkoa wa Iringa kutowahangaisha machinga na badala yake kuwatengea maeneo mazuri ya biashara, kuanzisha magulio, kuwapanga vema machinga na kuwawekea utaratibu mzuri wa kuchangia maendeleo ya nchi yao jambo ambalo machinga wameeleza kuwa tayari kulifanya.

Aidha Hapi ameeleza kutoridhishwa na manispaa ya Iringa kushindwa kukusanya mapato kikamilifu kutoka kwa machinga wote ambao wamekuwa na utayari wa kuchangia mapato.Kati ya machinga zaidi ya 2000 waliopo, taarifa za manispaa ya Iringa zinaonesha ushuru unakusanywa kwa machinga 353 pekee.Mkuu wa Mkoa ameagiza jambo hilo kurekebishwa haraka.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Machinga umemkabidhi RC Hapi hati maalum ya shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kwa jinsi serikali yake ilivyokuwa mtetezi wa wamachinga wakati wote.

Mikutano hii ni utangulizi wa ziara kubwa ya Mkuu wa Mkoa ijulikanayo kama IRINGA MPYA tarafa kwa tarafa inayotarajiwa kuanza tarehe 8 septemba wilayani Mufindi na kisha wilaya za Kilolo na Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi aakifafanua jambo awakati akizungumza na Wamachinga wa Mkoa wa Iringa, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya makundi mbalimbali ya jamii mkoani humo.Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara hao maarufu Machinga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameeleza mikakati ya serikali ya mkoa ya kuwatetea na kusimamia maslahi ya wamachinga ili watambuliwe na kusaidiwa kufanya shughuli zao vizuri.
Baadhii ya Wafanyabiashara hao a.k.a Wamachinga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Ally Hapi alipokutana nao na kuzungumza nao mambo mbalimbali

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS SEPTEMBA 6, 2018

VETA KUJENGA CHUO CHA UFUNDI STADI MKOANI RUKWA

0
0
Na David Edward, VETA.
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule amesema kuwa Mkoa wa Rukwa ulikuwa na uhitaji wa Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuwazesha wanannchi wa mkoa huo kupata ujuzi wa ufundi kwa maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla.


Dkt Halfan Haule aliyasema wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa katika hafla ya makabidhiano uliofanyika wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, amesema vijana wa Mkoa wa Rukwa ni fursa kupata mafunzo ya ujuzi na kuweza kujiajiri au kujiariwa.

Amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Pombe Magufuli kutatua tatizo upatikaji wa chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi mkoani humo.

Amesema vijana watapata ujuzi wa kusindika mazao mbalimbali na maendeleo yatapatikana kupitia usindikaji ambao utaogeza thamani ya mazao.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akizungumza katika Hafla ya kukabidhiana eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu naMafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Adelina Macha akitoa taarifa za kuhusiana na mipango ya ujenzi ya Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa VETA Kanda VETA Makao Makuu na Viongozi mbalimbali wa Mkoa.
Kaimu Mkurugenzi wa Soko la Ajira VETA, Hildergardis Bitegera akikabidhi mchoro wa ramani ya Jengo la Chuo VETA Rukwa kwa Mkandarasi atakayejenga Chuo hicho.

DC CHAMWINO AMKARIBISHA OFISA TARAFA ALIYEKUWA MASOMONI CHINA, AMUAHIDI USHIRIKIANO

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Vumilia Nyamoga amempongeza Ofisa Tarafa wa Itiso Remidius Emmanuel.

Pia amemkaribisha tena  kuendelea na majukumu yake ya kutumikia Taifa ikiwa ni siku chache  tu baada ya kurejea nchini akitokea masomoni nchini China.

"Wilaya ya Chamwino inakutegemea sana na tunatarajia maarifa uliyoyapata yataleta tija zaidi,..Ninakuahidi ushirikiano popote pale utakapohitaji msaada zaidi nitakuunga mkono,"amesema Vumilia

Pia amemtaja Remidius kama Ofisa Tarafa machachali na mchapa kazi na kuwataka Viongozi, watendaji  wa tarafa ya Itiso kumpatia ushirikiano wakati ambo amerejea kwa ajili ya kuwatumikia.

Kwa upande wake Remidius, amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa namna ya kipekee kwa shauku ya mapokezi makubwa.

Amesema baada ya  kurejea kutoka masomoni amekuja kukutana na Kufanya mazungumzo na Mkuu wake wa kaziMkuu wa Wilaya.

Amesema amemueleza machache aliyojifunza na kwamba tayari ameanza kazi.

" Ninaahidi kuendelea kutumia uzoefu na maarifa ya kile nilichojifunza nchini China kwa ustawi na maendeleo ya Taifa langu  kupitia Tarafa ya Itiso,"amesema.

Katika hatua nyingine Remidius alimkabidhi Mkuu huyo Kitabu kinachoeleza historia na mifano kutoka baadhi majimbo nchini China  yalivyoweza  kujikwamua na janga la umasikini (The way Forward: Stories of Poverty Reduction in China) 
Amesema kuwa "Kitabu hiki kinaeleza namna ambavyo Taifa la China limeendelea kufanikiwa katika mapambano dhidi ya umaskini, mapambano hayo ndio ambayo hata sisi (Tanzania) tunaendelea nayo.

" Na sasa tunao mwelekeo wa kuufikia Uchumi wa wakati 2025 zote ni juhudi za kuondoa umasikini....naamini hii ni zawadi sahihi kwa mkuu wangu na yeye amefurahia sana, kupitia uzoefu uliomo naamini Chamwino itasonga mbele zaidi,"amesema Remidius

Juni 29 mwaka 2018  Chuo Kikuu cha Kilimo nchini China (China Agricultural University - CAU) kilimtunuku Cheti Maalum akiwa ni mwanafunzi pekee kutoka Afrika  katika chuo hicho kama "Outstanding Graduate "

Ikiwa ni kutambua juhudi zake katika kujituma na mtu mwenye bidii kwa kipindi chote akiwa masomoni.

Remidius  Emmanuel ambaye pia alikuwa ni katibu Mkuu wa Shirikisho la wanafunzi Watanzania nchini China aliweza kutembelea zaidi ya majimbo 15 katika taifa hilo na kujifunza mambo mbalimbali kutoka taifa hilo.

Mapema Julai mwaka 2018  alichaguliwa kushiriki katika kambi maalum ya Vijana nchini China ("Future Leader and  Youth Ambassador, International Social Practice Summer Camp") Julai 16 mpaka Julai 22 Julai,2018.

Ambapo ilihusisha vijana  wapatao 140 (International & Chinese Students) kwa uwakilishi wa vyuo vikuu jijini Beijing, China akiwa mtanzania pekee aliyeshiriki katika kambi hiyo iliyofanyika katika Jimbo la Hebei ( Eneo jipya la Xiongan)

Itakumbukwa  Aprili 1 mwaka  2017, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jiping (Kupitia Kamati kuu ya Chama cha Kikomunist cha China - CPC ) aliutangaza mji wa Xiongan (katika Jimbo la Hebei) kama eneo jipya " Xiongan New Area".

Mji ambao ifikapo mwaka 2035 utakuwa ndio mji wa kisasa zaidi ya miji ya Shenzhen (Jimbo Guandong) na Pudong (Jimbo la Shanghai) na China kwa ujumla kama Ukanda maalum mpya wa kiuchumi (New Special Economic  Zone).

Wengi wamemtaja kijana huyu kama sehemu ya vijana wachache ambao wanajituma kwelikweli na wenye hulka za uzalendo kwa Taifa.
Ofisa Tarafa wa Itiso, Remidius Emmanuel(kushoto) akifafanua jambo mbele ya Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga kuhusu Kitabu hicho kinachoelezea mapambano ya Umasikini kwa mifano ya baadhi ya maeneo nchini China alipokuwa masomoni nchini humo.

CHAMA CHA WAAJIRI WAANZA MAFUNZO KUNDI LA TATU LA PROGRAMU YA MWANAMKE WA WAKATI UJAO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wameanza kutoa mafunzo ya kundi la tatu kwa wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) wakishirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (Confederation Of Norway Enterpise NHO) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yatakayokuwa katika kozi tatu yanalenga zaidi katika kuwapa mwongozo bora wafanyakazi wa kike ili waweze kumudu nafasi zao za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa wameshasajili wafanyakazi wa kike 24 kutoka makampuni 11 ambayo yamefadhili mafunzo hayo na kundi hili ni la tatu toka waazne kutoa mafunzo hayo na tayari wanawake 60 wameweza kupata programu hiyo.

Dkt Mlimuka amesema mafunzo haya yatachochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya kampuni na yatawapa ujasiri wanawake kuomba nafasi za uongozi sehemu mbalmbali ikiwemo bodi ya wakurugenzi..

Amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano na katika maisha yao kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (
ESAMI) kwa muda wa siku 14 muda wa darasani kwa kozi zote tatu ndani ya miezi tisa na yatafanyika kwa mfumo wa kuunganishwa na shughuli za kila za muhusika mahali pake pa kazi.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya mwanamke wa wakati ujao (Female in future) yenye malengo ya kumpa fursa mwanamke 
juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano 

wakati akizindua leo Jijini Dar es Salaam. Chini akizungumza na wanahabari.




Mhadhiri mwandamizi wa




Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Apollonia Kerenge akizungumza na wanawake waliokatika mafunzo ya mwanamke wa wakati ujao (female in future) iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akiwa katika picha ya pamoja na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya wanawake wa wakati ujao (female in future) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam .

Puma Energy yajipanga kupeleka ‘Happy Hour’ nchi nzima

0
0




Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeahidi kuipanua zaidi kampeni yake ya ‘Happy Hour’ inayoendelea katika vituo vyake vya mafuta vilivyopo mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kuwafikia wateja wa kampuni hiyo kote nchini kufuatia muitikio mkubwa ulionyeshwa na wateja katika kuipokea kampeni hiyo.

Kampeni hiyo ambayo kwa sasa inahusisha vituo vya mafuta vya Puma vilivyopo vilivyopo mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, inamuhakikishia mteja rejesho la asilimia 5 ambalo ni sawa na Tsh 100 kwa kila Tsh 2,000 atakayotumia kununua mafuta kwa njia ya simu za mikononi au akaunti ya benki kupitia huduma Masterpass QR katika siku zote saba za wiki kuanzia saa 10:00 hadi 12:00 jioni.

Akizungumza kupitia taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw. Philippe Corsaletti amesema kwa sasa wateja wa kampuni hiyo wanaweza kufanya malipo kwa urahisi, haraka na kwa usalama zaidi kwa kutumia pesa zilizopo kwenye akaunti zao za simu au akaunti za benk.

“Kupitia kampeni hii tunashuhudia wateja wetu wakihamia kwenye ulimwengu wa kidigitali zaidi na kuungana na wenzao wengi ulimwenguni ambao tayari wapo huko. Aidha, ili kufanikisha hili tumewajengea uwezo wahudumu wetu waliopo kwenye vituo vyetu na sasa wapo tayari kuwasaidia wateja watakaopatwa na changamoto ya aina yoyote katika kufanikisha miamala yao,’’ alifafanua.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

StarTimes yaongeza kasi kupambana na UKIMWI

0
0
Kampuni ya StarTimes na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ugonjwa wa UKIMWI UNAIDS, wamekutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ushirikiano wao katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo. Mkutano huo uliopewa jina la “Thamani ya Taarifa kwa njia za kidigitali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI” ulihudhuriwa na Makamu Rais wa StarTimes Group Bi. Guo Ziqi, Mke wa Rais wa Malawi Bi. Gertrude Mutharika na Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS Bw. Michel Sidibe.

Katika mkutano huo ambao umefanyika mapema mwanzoni mwa wiki hii jijini Beijing, baadhi ya mambo yaliyoongelewa ni ongezeko la vifo vilivyosababishwa na UKIMWI kwa Vijana hii inatokana na kutofikiwa na taarifa juu ya maambukizi ya VVU/UKIMWI hivyo wanakosa ufahamu juu ya njia sahihi za kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huo.
Bw. Michel Sidibe akizungumza katika mkutano huo alisema “Tumejionea mwenendo mzuri katika nchi nyingi lakini changamoto tunayokutana nayo ni kukata tama. Vijana wengi hawana taarifa, hawana ufahamu, hivyo hawajilindi na maambukizi..kwa hiyo taarifa, ufahamu na elimu ni muhimu na ndio maana tunajivunia kufanya kazi na StarTimes katika hili.”
Michel aliongeza, “nataka tu kusema kwamba kupeana taarifa na kueleweshana juu ya UKIMWI ili kuwabadilisha vijana itakuwa ni hatua muhimu sana katika kutokomeza ugonjwa huu”. Pia alisema kwenye nchi nyingi za kiafrika zaidi ya asilimia 70 ya watu wote wana umri wa miaka 35 na hawapati taarifa kuhusu ugonjwa huu. “njia yetu ya kukabiliana nao itabadilisha kila kitu na pengine tutakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya UKIMWI”, aliongeza.
Kwa kupitia teknolojia ya mawasiliano ya intaneti kwenye simu barani Afrika na kwingineko duniani, mawasiliano yatakuwa muhimu zaidi katika mapambano haya.
“Kwa kulitambua hilo, StarTimes tulianzisha huduma ya kupata video za moja kwa moja kwenye simu barani Afrika, StarTimes App ambayo tuliizindua mwezi wa sita, na tayari miezi mitatu baadaye imepakuliwa na watu milioni 8 tunategemea watafikia milioni 15 kufikia mwisho wa mwaka”, aliseama Bi. Guo Ziqi.
Kwa sasa tayari StarTimes wanatoa huduma ya kustream maudhui yanayofahamika kama “Zero Discrimination” ikishirikiana na UNAIDS.
Naye mke wa Rais wa Malawi Bi. Gertrude Mutharika alisema, “Ushirikiano wa StarTimes na UNAIDS katika kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI umekuja kwa wakati sahihi kabisa ambapo Malawi na Afrika kwa ujumla tupo katika mapambano haya muhimu kwa bara letu”.
Viongozi wa Afrika walikuweko jijini Beijing kuhudhuria kongamano la vyama vya Kisiasa vya Africa na kile cha China FOCAC katika kuimarisha uhusiano wa Afrika na nchi ya China.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO AFUNGUA SEMINA YA UBIA KATI YA SEKTA BINAFSI NA UMMA

0
0
KATIBU Mkuu wa wizara ya fedha na mipango, Dotto James amefungua semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) cha makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango inayofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa semina hiyo itawajengea uwezo maafisa hao kutoka wizara na taasisi wanazooongoza ili waweze kutekeleza miradi ya PPP-(Public service Private partnership) yenye sifa.

James ametoa wito kwa washiriki wa semina wawe na utayari,uzalendo wad hat katika kuchangia, kuchambua kikamilifu miradi yenye sifa ili kuongeza ufanisi na wigo wa kutoa huduma za kiuchumi na kijamii.

“Matumaini yangu kuwa kila mmoja atashiriki kikamilifu katika semina hii muhimu na kupata uelewa wa mambo mhimu yatakayowezesha kuongeza jitihada za maandalizi ya mradi wa PPP.”Amesema James.

Nae Kaimu Mkurugezi wa mkondo wa chini wa shirika la mafuta na gesi (PTDC), Emmanuel Gilbert mradi wa PPP unatambulishwa kwa makatibu wakuu ili serikali na sekta binafsi waweze kushirikiana kikamilifu katika mradi huo.

Amesema kuwa katika uwekezaji katika usambazaji wa mafuta na gesi hapa nchini utasaidia kwa haraka wananchi kuweza kutumia gesi ya hapa nchini.

Amesema kuwa katika mradi huo wa kusambaza gesi utashirikisha waombaji watakao kidhi vigezo kwaajili ya usambazaji wa gesi hiyo ambapo kwa jiji la Dar es Salaam kutakuwa na vituo vitatu ambapo kitakuwa Ilala, Temeke na Kinondoni.
 Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango,Dotto James akizungumza  wakati wa kufungua semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) cha makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango inayofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
 Mtaalamu wa masuala ya ubia kati ya sekta za umma na sekta binafsi, Philip Kelly  akifafanua jinsi Mradi wa sekta Binafsi na sekta za umma wakati wa semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
Kaimu Mkurugezi wa mkondo wa chini wa shirika la mafuta na gesi (PTDC), Emmanuel Gilbert akizungumza na waandishi wa hanbari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
Picha ya Pamoja ya Makatibu wakuu wa taasisi na wakuu wa idara wa wizara ya fedha na mipango mara baada ya semina ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) iliyofanyika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2018.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

RC HAPI: MARUFUKU KUWANYANYASA MACHINGA KATIKA MAENEO WANAYOFANYIA AZI ZAO

0
0
 NA FREDY MGUNDA,IRINGA
MKUU wa mkoa wa Iringa amepiga marufuku wafanyabiashara wadogo wadogo kunyanyaswa katika mahali ambazo wanafanyia biashara kwa kuwa wanatoa kodi ambayo inachochea kuleta maendeleo ya watanzania hususani mkoani iringa tukielekea kuijenga Iringa mpya.


Akizungumza kwenye mkutano na wafanyabiasha wadogodogo wa manispaa ya Iringa mkuu wa mkoa Ally Hapi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo maarufu kama machinga wanatakiwa kufanya biashara zao kwa kufuta taratibu na sheria za nchi huku viongozi wakiancha kuwanyanyasa kwa kuwa nao ni wafanyabiashara.


“Toka nikiwa mkuu wa wilaya najua umuhimu wafanyabiasha wadogo wadogo kwa kuchangia katika kukuza uchumi wa eneo husika hivyo natangaza rasmi ni marufuku kuwanyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa” alisema Hapi


Hapi aliwataka polisi wanasimamia eneo lastand kuu kuacha mara moja kunyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wanaofanyia biashara katika eneo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto ambazo wanakabiliana katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuhakikisha wanaijenga Iringa mpya ambayo inatakiwa na wanairinga 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea wakati wa kikao cha wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga na mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga walijitokeza kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na kama ambavyo unawaona walivyokuwa makini kumsikiliza hapo

DKT. JANABI:VYAKULA VISIVYO NA AFYA HUSABABISHA MAGONJWA YA MOYO

0
0
Na Salome Majaliwa - JKCI
ULAJI wa vyakula visivyokuwa na afya ni moja ya sababu zinazosababisha watu kupata magonjwa  yasiyo ya kuambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akitoa mada kuhusu afya na mazoezi   kwenye  mkutano wa wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Katika mada hiyo ya afya na mazoezi Prof. Janabi alifundisha kuhusu ugonjwa wa shambulio la moyo na kiharusi, tezi dume, saratani, kukoma kwa hedhi na huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Prof. Janabi ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema hivi sasa  watu wanapenda kula vyakula ambavyo ni hatari kwa afya zao zikiwemo chips na bagger badala ya kula kwa wingi matunda na mboga za majani.

“Dhibitini vyakula mnavyokula hii ikiwa ni pamoja na kutokula vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo vinapelekea mishipa ya moyo kuziba kutokana na mafuta na kusababisha tatizo la kiharusi pia  fanyeni mazoezi ya mara kwa mara”, alisisitiza Prof. Janabi.

Alisema ugonjwa wa moyo ni moja ya magonjwa yanayoua watu wengi wakiwemo watoto ambao wasipopata chanjo za muhimu zinazotolewa chini ya umri wa miaka mitano pia mama mjamzito asipopata chanjo   kuna uwezekano mkubwa kwa watoto kuzaliwa na kupata magonjwa ya moyo.

Kwa upande wa  ugonjwa wa shambilio la moyo  alizitaja dalili zake kuwa ni maumivu kwenye kifua ambayo yanakwenda kwenye mgongo upande wa kulia na kushoto na kuwasihi wanapoona dalili kama hiyo wawahi  mapema kwa daktari.
 Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakitoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo  kwa wahandisi wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Pix 3 & 4: Baadhi ya Wahandisi wakiwa katika foleni ya kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo katika  banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi ulifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo ilishiriki kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya  moyo kwa wahandisi hao.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adela Martine akitoa ushauri kwa mhandisi aliyepata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi hiyo wakati wa mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada ya Afya na mazoezi kwa wahandisi wakati wa Mkutano wa 16 wa Wahandisi unaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.Picha na JKCI

WAKALA WA MANISPAA JIJI LA ARUSHA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA MIL 23/-KWA NJIA YA UDANGANYIFU

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
WAKALA  wa Manispaa ya Jiji la Arusha Robert Modu, leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kugushi, kutoa nyaraka za uongo na kujipatia zaidi ya Sh. milioni 23 kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hati ya mashtaka leo mahakamani hapo Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leornad Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Wanjah Hamza kuwa, mshtakiwa ametenda makosa hayo kati ya Desemba 4 mwaka 2013 na Julai 14 mwaka 2014 huko Kijitonyama.

Imedaiwa, siku ya tukio mshtakiwa Modu kwa nia ovu alitengeneza nyaraka ya uongo ya hati ya madai yenye kumbu kumbu RA/CC &ADV/VOL.1/1078 kwa madai kuwa hati hiyo ilitolewa na Manispaa ya Jiji la Arusha huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, tarehe hizo katika ofisi za Kampuni ya Sigara Tanzania iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa aliwasilisha hati hiyo ya madai ya uongo yenye kumbu kumbu namba hiyo hiyo, katika kampuni ya Sigara kuonesha kuwa hati hiyo imetolewa na Manispaa ya jiji la Arusha.

Aidha imedaiwa, kati ya Novemba 4 mwaka 2013 na Julai 14 mwaka 2014, katika kampuni ya Sigara ya Dar es Salaam akiwa Wakala wa Manispaa ya Mji wa Arusha kwa nia ya kudanganya alijipatia Sh. 23,273,632 kwa niaba ya manispaa hiyo ya Arusha.

Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alijipatia malipo hayo kuonesha kuwa yameizinishwa na Manispaa hiyo na kwamba fedha hizo alizipokea Kwa niaba ya Manispaa.
Hata hivyo. Mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo na huko nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Hakimu Hamza alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini Wawili wataosaini bondi ya sh. milioni 10 na mmoja kati ya wadhamini hao wametakiwa kiwasilisha fedha Sh. milioni 10 au hati ya mali isiyohamishika yenye kiasi hicho cha fedha.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 19 mwaka 2018.
 Wakala  wa Manispaa ya Jiji la Arusha Robert Modu akiingia katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu leo kabla ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kugushi na kutoa nyaraka za uongo na kujipatia zaidi ya Sh. milioni 23 kwa njia ya udanganyifu.
Wakala  wa Manispaa ya Jiji la Arusha Robert Modu akitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kugushi na kutoa nyaraka za uongo na kujipatia zaidi ya Sh. milioni 23 kwa njia ya udanganyifu.


NEWZA ALERT;Wenyeviti wa Vijiji 19 (Chadema) kutoka Wilayani Hai wajiondoa Chadema na Kujiunga CCM leo

0
0
 Baada ua kukabidhi barua zao kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohane Sintoo,waliamua kupiga picha ya pamoja
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohane Sintoo akipokea barua za baadhi ya Wenyeviti wa vijiji kati ya 20 walioamua kujivua vyeo vyao vyote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi mapema leo.


Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF

0
0
Jumla ya waendesha bodaboda 117 kutoka wilaya ya Temeke wamejiandikisha katika mfumo wa hiari wa kuchangia mafao kwenye Shirika la Tiafa la hifadhi ya Jamii NSSF. 

Hatua hii ni alama njema kwa wananchi kuendelea kutambua na kuona muhimu wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini jambo ambalo litasaidia wananchi kuweza kujiwekea akiba yao ya maisha ya baadae.

Afisa mwandamizi uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Abbas Cothema akizungumza na waendesha bodaboda wa wilaya ya Temke ambapo amesema wameitikia wito kwa wingi wa kujiandikisha na kujichangia wenyewe kwa hiari kwamba hivyo hii ni hatua kubwa wananchi kuelewa elimu kuhusiana na suala la hifadhi zao za baade.

Cothema amesema kuwa wanachama hao wapya wataweza kufaidika na mafao mbalimbali yakiwemo mafao ya matibabu ambapo mwananchama anapata matibabu ya bure kutokana na michango yake anayoichangia kwa kila mwezi ambapo atachangia kiwango cha kuanzia kiasi cha shilingi elfu ishirini.

‘Hii ni fursa pekee kwa wananchi ambao wapo kwenye sekta isiyorasmi kuweza kujiandikisha na kujiwekea akiba ambayo itawasaidia hivyo ni wakati wao sasa nao kufaidika na matunda ya jasho lao kwa kujichangia wenyewe” alisema Cothema.

Cothema amesema mpaka sasa wameshatoa elimu kwa mikoa zaidi ya kumi ambapo wananchi wameweza kuelimishwa umuhimu wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umuhimu wake.

NSSF imepewa jukumu la kuandikisha wanachama wapya watakaojichangia kwa hiari wenyewe. 


Afisa matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Abbas Cothema akitoa maelekezo kwa waendesha bodaboda wa wilaya ya Temeke wakati walipokuwa wakijiandikishai ili kujiunga kwenye mfumo wa Hiari wa NSSF katika kampeni ya Zamu yako maalumu kwa wananchi ambao wako kwenye sekta isiyorasmi.
Baadhi ya waendesha bodaboda wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kwenye mfumo wa hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF jana wilayani TemekeJijini Dar es salaam.
Afisa matekelezo Kassim Mfundo akiwaandikisha wanachama wapya kwenye mfumo wa Hiari hapo jana wilayani Temeke ambapo waendesha bodaboda 117 walijiandikisha.


TFS IMESABABISHA MACHO YA WASHIRIKI SHINDANO LA MISS TANZANIA 2018 KUYAONA AMBAYO HAWAJAWAHI KUYAONA .

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MOJA ya kauli ambayo nimeisikia zaidi ya mara moja ikitamkwa na washiriki wa Shindano la Miss Tanzania mwaka 2018 ni ile inayoonesha kutoa shukrani zao za dhati kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),

Warembo hao walioumbwa na Molla wao wakaumbika hawakuwa na shaka hata kidogo kupaza sauti zao tena kwa madaha na madoido wakisema Tanzania yetu, Misitu yetu, Fahari yetu, Urembo oyeee na kisha wanamalizia kwa kusema hivi TFS oyeeeeee..Nikwambie mapema nilikuwa nawasikia kwa masikio yangu.Ndio maana nakwambia nimewasikia.Niamini.

Unajua kwanini?Iko hivi TFS ambayo ipo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kwamba iliamua kuwapeleka warembo hao kwenye Hifadhi ya Mazingira ya Msitu Asili wa Amani iliyopo mkoani Tanga.

Hifadhi hiyo inapatikana katika Wilaya ya Muheza na ipo umbali wa kilometa 35 kutoka Muheza Mjini.Hivyo ni hifadhi ambayo haiko mbali saaana, lakini kwa vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo hata ingekuwa mbali kiasi gani ningekushauri ufike ujioonee mwenyewe. Na hivi TFS wanavyojua kutunza hifadhi zetu hadi raha.Nenda Mtanzania mwenzangu ukaone vilivyomo.
 Washiriki wa Shindano la Miss Tanzania mwaka 2018 wakishangilia baada ya kufika katika Mapango ya Amboni mkoani Tanga.
 Baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania 2018 wakiwa wamenyoosha mikono juu baada ya kufika katika Shamba la Chai lililopo katika hifadhi ya msitu wa asili wa Amani mkoani Tanga 
Washiriki wa Miss Tanzania 2018 wakiwa katika hifadhi ya msitu wa asili wa Amani mkoani Tanga baada ya kutembelea majiko banifu yanayotumiwa na wananchi wa vijiji vinavyozunguka msitu huo uliopo mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Miss Tanzania 2018 wakiwa katika moja ya  mlango wa pango la Amboni mkoani Tanga.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA SEPTEMBA 6, 2018

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Geogre Mkuchika akieleza umuhimu wa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) wakati wa kupitishwa kwa muswaada huo leo Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa  Sima akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha inatunza mazingira ya ziwa manyara ili kuondoa athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati akijibu hoja za wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kupitisha muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018).
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso akisisitiza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama kote nchini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi waliokuwa na akaunti katika iliyokuwa  Benki ya FBME  wanalipwa haki zao kwa mujibu wa sheria na Kanuni za utumishi baada ya Benki hiyo kufungwa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kuondoa mgogoro kati ya wananchi na Manispaa ya Mtwara Mikindani unaotokana na eneo la Mjimwema na Tangira lililopimwa kwa ubia kati ya Manispaa na Taasisi ya UTT-PID mwaka 2003.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akisisitiza kuhusu umuhimu wa wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Zungu akisisitiza jambo wakati wa kupitishwa kwa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018.(The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima, leo Bungeni Jijini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi)

CHAMA CHA WABUNGE MARAFIKI WA UTURUKI WAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI TANZANIA, BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Fatma Toufiq (kulia) akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (katikati) kwa lengo la kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi, kikao kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mwandishi Mwandamizi wa Taarifa Rasmi za Bunge, Ndg. Patson Sobha
 Wajumbe wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Fatma Toufiq (watatu kushoto) wakimsikiliza Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (wa pili kushoto) wakati wa kikao baina yao kilicholenga kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi, kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Fatma Toufiq (katikati) wakiwa katika mazungumzo na  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (wa pili kushoto) wakati wa kikao baina yao kilicholenga kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi, kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu (kulia) akizungumza na Wanachama wa  Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki walioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Fatma Toufiq (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kililenga kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi
Mjumbe wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki na Mbunge wa Chilonwa, Mhe. Joel Mwaka akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu na Wanachama wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Uturuki (hayupo kwenye picha) katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images