Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI

$
0
0
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu kabla ya kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi huo,  pia kujifunza shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu  wakati wa kikao baina yao kilicholenga kuboresha uhusiano kati ya Bunge na Ubalozi, nakujifunza shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. kikao kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu baada ya mazungumzo yaliyofanyika  leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

DC ahimiza jamii za wafugaji kusomesha watoto wa kike hadi chuo kikuu

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Simanjiro
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania Chaula amezitaka jamii za wafugaji kuanza kuchukua hatua dhidi ya Mila potofu zinazoendelea kumkandamiza Uhuru wa mtoto wa kike na kumfanya ashindwe kusoma kwa maslahi ya wazazi wake

Aidha ameitaka jamii hiyo ya kabila la kimasai kubadilika na kuanza kusomesha watoto wa kike hadi vyuo vikuu ili kuwapatia elimu itakayosaidia kuielimisha jamii hiyo ili kuachana na mila potofu zikiwemo ndoa za utotoni na ukeketaji .

Kauli hiyo ameitoa mapema jana katika kijiji cha Namalulu,wilayani Simanjiro,Mkoa wa Manyara wakati  alipohudhulia   sherehe za Kimika za kusimikwa kwa viongozi wakuu wa kabila la Kimasai alimaarufu Laigwanani.,Ambapo  Mzee Meshack Toreto na Lucas Kisongira walisimikwa kuwa viongozi wakuu wa Kimila katika jamii hiyo.

"Jamii za kifugaji lazima zianze sasa kumwandaa mtoto wa kike kwa ajili ya kumpatia Elimu bora ili aje kuikomboa jamii hiyo ambayo baadhi yao bado wanaendekeza mila potofu zilizopitwa na wakati''Amesema chaula

Mhandisi Chaula alisema serikali inaunga mkono mila na destuli za makabila mbalimbali na aliahidi kushirikiana na viongozi wa kimila  na kuwataka kufuata taratibu na sheria za nchi ikiwemo kuhamasisha maendeleo na kujiepusha na tamaduni zinazokinzana na sheria za nchi.

Ameipongeza jamii huyo ya kimasai kwa  hatua hiyo ya kuendelea kudumisha mila na tamaduni zao jambo linaloendelea kulipa sifa taifa katika nyanja za kimataifa kwani kwa hapa nchini ni kabila pekee linalotambulika kimataifa katika utamaduni wao unaoleta tija kimataifa.

Awali katibu wa viongozi wa kimila Ilaigwanak, Mchungaji Yohana ole Tiamongoi amesema kupitia viongozi hao wa kimila wamefanikiwa kuziondoa mila mbalimbali potofu katika jamii yao kupitia maadhimio mbalimbali kwenye vikao vyao.

Katika sherehe hizo za kusimikwa viongozi hao wa kimila katibu huyo amewataka wafugaji wa jamii hiyo kuanza kuwekeza kwa mtoto wa kike kwa kumpatia Elimu hadi  chuo kikuu.

Mmoja wa Laigwanani aliyesimikwa ,Meshack Toreto alisema kuwa kazi yao kubwa ni kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii yao ikiwemo migogoro ya Ardhi ili kuisaidia serikali kupunguza msongamano wa mashauri mahakamani yanayotokana na migogoro ya jamii hiyo.

"Sisi hatupingi watu wetu kwenda kwenye vyombo vya kisheria ila tunataka zaidi mambo yetu kuyamalize wenyewe na hii itasaidia hata serikali kupunguza mzigo wa wa kuendesha kesi mahakamani''Amesema Toreto

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Mhandisi Zephania Chaula (kushoto) akimkabidhi rungu maalumu mmoja ya wazee wakubwa, Meshack Toreto aliyesimikwa kuwa Laigwanani wa kabila la wamasai katika kijiji cha Namalulu, wilayani Simanjiro jana.

PROF. MKUMBO AWASHAURI WAHANDISI KUWA NA MAJIBU KABLA YA WANASIASA KUWAULIZA MASWALI KUHUSU MIRADI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewashauri wahandisi nchini kujenga utamaduni wa kuandaa mipango ya miradi ya maendeleo ya maji na kuwa na majibu kabla ya kukutana na maswali ya viongozi wa kisiasa.

Profesa Kitila ametoa ushauri huo leo wakati akiwasilisha mada yake inayohusu maendeleo ya maji kwa wahandisi ambao wapo katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa Bodi ya Usajili Wahandisi wa Tanzania (ERB) yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Hivyo wakati anatoa mada hiyo pamoja na mambo mengine amewaambia iwapo watakuwa na mipango inayoonesha gharama za miradi mbalimbali inayotekelezwa itakuwa rahisi kujibu maswali ya viongozi wa kisiasa bila kuchelewa badala ya kusubiri kuulizwa.

"Wahandisi wengi wamekuwa wakisubiri maelekezo kutoka kwa wanasiasa hali ambayo inachelewesha maendeleo ya miradi ya maji hasa vijijini.Ni vema wahandisi wakawa mbele kwa.majibu na hiyo itawezekana kwa kuwa na mipango endelevu," amesema.

Ameongeza kuwa "Wahandisi wanatakiwa kuwa mbele ya wanasiasa kwa kuwa mipango ya maendeleo na hasa miradi ya maji ili kuepuka maelekezo ambayo sio ya kitaalamu," amesisiza na kueleza maji na maendeleo na maendeleo na maji.

Prof.Kitila amewasisitiza wahandisi nchini kiwa ili miradi ya maji kuwa na tija wana kila sababu ya kuwa wabunifu kwa kubuni miradi mipya na kubwa ni kutatua changamoto zilizopo .

"Ni wajibu wa wahandisi kuhakikisha wanabuni miradi ya maji,kwa mfano wanaweza kubuni mradi wa maji wa kuondoa changamoto Singida kwa kutumia maji yaliyopo Ziwa Victoria," amesema.

Amefafanua  kwa kufanya  hivyo hata akitokea kiongozi akazungumzia utatuzi wa maji mkoani Singida tayari wahandisi walishakuwa na majibu na kinachobaki ni utekelezaji.
  
Kuhusu mikakati ya Serikali katika sekta ya maji nchini, Profesa Mkumbo amesema kuna mpango wa miaka mitano ambao utagharimu zaidi ya Sh.Tril 10.4 kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa maji.

Akizungumzia kiasi cha maji kilichopo nchini Profesa Mkumbo Kuhusu kiasi cha maji kilichopo Kitila alisema hali bado ni nzuri ambapo pamoja maji kupungua Tanzania ina ujazo wa trilioni 92.

Pia ametoa mwito kwa kila mwananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo huku akiwasisitiza wahandisi kutambua dhamana walinayo katika maendeleo ya nchi.

VYUO VIKUU VIWE NA BODI ILI KULINDA MASLAHI YA WANAFUNZI NA WAHADHIRI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa Manonga Mh. Seif Gulamali amependekeza kuwepo kwa bodi maalumu itakayowaongoza wahadhiri wa vyuo vikuu kiutendaji na kinidhamu.

Akichangia katika mjadala wa kupitisha muswada wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  kuhusiana na uanzishwaji wa bodi ya kitaalamu ya walimu nchini ambayo itakuwa na majukumu ya kuinua viwango vya utaalamu wa Ualimu kwa lengo la kuhakikisha walimu wanakuwa na viwango stahiki kitaaluma na kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya ualimu.

Gulamali ameunga mkono muswada huo na kuongeza kuwa isiwe kwa walimu pekee bali ilenge kwa wahadhiri pia ambao  wana wana umoja wao kama UDOMASA kwa wahadhiri wa Chuo kikuu cha Dodoma na UDASA kwa chuo kikuu cha Dar es saalam.

Ameeleza kuwa vyuo vyenye umoja huo lazima kuwe na bodi moja ambayo itawaongoza na majukumu ya bodi iwe ni pamoja na kusajili wataalamu hao kwa ngazi za shahada, uzamili na uzamivu na kujua idadi yao ili kuweza kuwa na takwimu sahihi za idadi ya wataalamu hao.

Pia ameshauri kuwa bodi hiyo iwe na kazi ya kutambua uwezo wao kitaalama sambamba na kusimamia nidhamu hasa malalamiko ya wanafunzi hasa wakike juu ya wahadhiri kwa manyanyaso ya kijinsia.

Aidha amesema kuwa bodi hizo zitakuwa na maslahi kwa pande zote mbili  wawezeshaji na wawezeshwaji katika elimu ili kuweza kuzalisha wataalamu wengi na bora zaidi.

Muswada huo uliopita Bungeni utawalenga walimu katika ngazi zote waliohitimu katika vyuo vinavyotambulika kwa ngazi ya Shahada, stashahada na astashahada na utashirikisha taasisi na wizara mbalimbali zikiwemo Utumishi wa Umma, Chama cha Walimu, Maafisa elimu, Wizara ya mambo ya ndani na Ofisi ya Waziri Mkuu.

ISBAH ENTERTAINMENT YAANDAA SHOW YA KIBABE JIJINI DAR ES SALAAM

SIFA YA TRENI YA UMEME, IKIWA DEREVA ATAENDESHA KWA KASI KINYUME NA UTARATIBU

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WASAINI MKATABA WA MKOPO WENYE RIBA ZIRO NA BENKI YA DUNIA

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WIZARA ya Fedha na mipango kwa niaba ya serikali imesaini mkataba Mkopo wa fedha kati ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na benki kuu ya dunia jijini Dar es salaam leo kwaajili ya kusafirisha, kuzalisha na kusambaza nishati ya umeme na maji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wizara ya fedha na Mipango, Dotto James amesema kuwa mkataba huu wa mkopo huu utahusisha usambazaji wa maji katika maeneo ya vijijini katika mikoa 17 ya Tanzania pamoja na umeme. Pia Katibu Mkuu wizara ya fedha na mipango amewashukuru benki ya dunia kwa kutoa mkopo usio na riba kabisa.

Mkopo huo kutoka Benki ya dunia kiasi cha shilingi trilioni 1.04 ambapo itatumika katika mradi wa umeme na maji kwa mikoa ya kusini ambayo ni Iringa Kisada,Tunduma, Mbeya hadi mpaka wa Zambia.

Nae Katibu Mkuu wizara ya Maji safi na maji taka, Kitila Mkumbo amesema kuwa fedha hizo zitatumika kikamilifu katika lengo lililopangwa na serikali kwa mikoa 17 katika usambazaji wa maji maeneo ya vijijini.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji uwekezaji wizara ya Nishati na Madini, Khalid James amesema kuwa kwa upande wa Nishati ya umeme wataweza kuunganisha gridi ya Taifa kwa mikoa ambayo haijafikiwa na gridi ya taifa.
Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 7,2018 kabla ya kusaini Mkataba wa mkopo wa fedha kwaajili ya usambazaji wa maji vijijini na uboreshaji, utengenezaji na kuzalisha umeme hapa nchini.
Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (Kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird (Kushoto) wakisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu na wenye riba ziro kwaajili ya uboreshaji na utengenezaji mifumo ya umeme na maji katika maeneo ya vijijini hapa nchi.
Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (Kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird (Kushoto) wakibadilishana Mkataba wa mkopo jijini Dar es Salaam leo, Septemba 7,2018 wenye masharti nafuu na wenye riba ziro kwaajili ya uboreshaji na utengenezaji mifumo ya umeme na maji katika maeneo ya vijijini hapa nchi.
Katibu Mkuu wa wizara ya maji safi na maji taka (DAWASO), Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mpango waliojiwekea katika kuboresha na kusambaza maji hapa nchini katika maeneo ya vijijini. Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI YAPATIWA MAFUNZO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mtaalamu wa masuala ya Jinsia, Bajeti kwa Mtazamo wa kijinsia na Haki za Binadamu, Ndg. Gemma Akilimali (aliesimama) akitoa mada kwa Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti katika semina iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia mada iliyowasilishwa na Mtaalamu wa masuala ya Jinsia, Bajeti kwa Mtazamo wa kijinsia na Haki za Binadamu, Ndg. Gemma Akilimali (aliesimama) wakati wa semina iliyohusu Bajeti kwa Mtazamo wa Kijinsia leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akizungumza jambo wakati kamati hiyo ikipatiwa semina iliyohusu Bajeti kwa Mtazamo wa Kijinsia, leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Husna Mwilima. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA MTO MARA, AHUTUBIA WANANCHI WA NYAMONGO MKOANI MARA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Nyamongo mkoani Mara wakati akitokea Mugumu Serengeti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua daraja hilo la mto mara lenye urefu wa mita 94 linalounganisha katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyansura Serengeti mara baada ya kukagua mradi wa daraja la mto mara lenye urefu wa mita 94 linalounganisha katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Nyambura Nyamarasa ambaye alikuwa na kero ya kulishiwa na shamba lake na mfugaji mmoja huko Mugumu Serengeti mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa shilingi milioni moja Nyambura Nyamarasa ambaye alikuwa na kero ya kulishiwa na shamba lake na mfugaji mmoja huko Mugumu Serengeti mkoani Mara.

Sehemu ya Daraja la mto mara mita 94 ambalo ujenzi wake unaendelea na litaunganisha kati ya katika ya Wilaya ya Serengeti na Tarime mkoani Mara. PICHA NA IKULU

Job Opportunity in Tanzania: COMMISSION SALES REPRESENTATIVES

$
0
0
We are a group of companies currently looking to expand and now we are looking for Commission based sales representatives in Dar es salaam (4) who will be placed in different territories.
The ideal candidates will possess high energy levels, outgoing personality, confident, smart, must be results oriented with demonstrated success in sales or have the ability to sale, ready to learn.  A go getter on the whole.

QUALIFICATIONS 

 • 1 or more years of successful commission based sales experience or if you feel you are born to sale with no experience you may apply.
 • Customer service, Meeting sales goals, closing skills, territory management
• cold calling, market research  and securing sales from small/big business accounts that you were be allocated.
• Capable of seeking out and participating in local networking events. 
• Identifies prospects, customers, and referral sources and ready to do research as per target areas .
• Strong interpersonal and communication skills (oral, written, presentation) in English and Kiswahili.
• Must be highly organized and self motivated 
•Positive and energetic attitude
 •Knowledge of Word, Outlook, Excel.
•Ethical and trust worthy character.

 On-going sales training will be provided. 

NB: This is a commission based position with a possibility of making over 2 million plus for the serious go getter .

Women are highly encouraged to apply.
Send your CV only to  kccsm@turkysgroup.co.tz  
Deadline 14.9.2018

Viwanja vya ndege vyaaswa kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa kuambikiza-TCAA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga (TCAA)  imesema kuwa viwanja vya ndege na wadau wengine katika usafiri wa anga wanatakiwa kuwa na mikakati ya kukubiliana na magonjwa ya kuambukiza ili kufanya usafiri wa anga kuwa salama kwa abiria pamoja na mizigo.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa usafiri wa anga uliofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka hiyo  , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Redemptus Bugomomola amesema viwanja vya ndege vinatakiwa kuwa na huduma za Afya kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza ili kuweza kulinda jamii kutoka sehemu kwenda nyingine.

Bugomola amesema kuwa baada ya kuwepo magonjwa ya kuambukiza kwa watumiaji usafiri wa anga Shirika la Usafiri wa Anga (ICAO) liliunda chombo cha kuratibu masuala kukabiliana na magonjwa ya  kuambukiza katika Viwanja vya Ndege CAPSCA  ambapo nchi za Afrika bado ziko nyuma katika kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza.

Amesema kuwa TCAA kwa kushirikiana na wadau kunahitajika kuwepo na mikakati ya kila mmoja kutambua umuhimu wa kufanya kazi katika kukabiliana magonjwa ya kuambukiza kutoka ndani au kwenda nje pamoja na wa nje kuangalia wasiweze kuambikiza wanapingia nchini.

Nae Mkuu wa Vituo vya Afya Mipakani wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Remidius Kakula amesema kuwa kupitia ICAO  imeweka viwango vya viwanja vya ndege kuwa mazingira ya kuweza kukabiliana na maginjwa ya kuambikiza.

Amesema kuwa kila kiwanja cha ndege kinatakiwa kuwa na chumba maalumu pale anapobainika kuwepo kwa mgonjwa ili kuweza kupata huduma haraka ndani ya  uwanja ndege ikiwemo na huduma ya Thermo ya kupima kiwango cha joto pamoja na kuwa gari ya wagonjwa kwa kila kiwanja cha ndege..

Amesema katika mkutano huo watajadiliana mbinu mpya ya kukabiliana magojwa ya kuambukiza kwa magonjwa yaliyotishio kama vile Ebola , Homa ya Ini, Mafua ya Nguruwe pamoja na Mafua ya Ndege.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Redemtus Bugomola akizungumza katika mkutano wa wadau wa anga kuhusiana na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika viwanja vya ndege uliofanyika katika ukumbi wa TCAA, jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Daniel Malanga akizungumza kuhusiana na masuala mbalimbali ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza katika viwanja vya ndege.
Baadhi ya wadau wa usafiri wa anga katika mkutano wa kujadilia namna ya kukabiliana na magonjwa kuambukiza

KAMBI YA TIMU YA YAIFA YA SOKA LA UFUKWENI KUVUNJWA JUMAPILI

$
0
0
kIkosi cha timu ya Taifa ya soka la Ufukweni wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya soka ya ufukweni (Beach Soccer) Boniface Pawasa amesema kuwa kwa sasa anavunja kambi rasmi siku ya Jumapili kwa ajili ya wachezaji kurudi nyumbani baada ya wapinzani wao Afrika Kusini kujiondoa kwenye mechi ya kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON  Nchini Misri.

Akizungumza leo, Pasawa amesema kuwa kambi waliyokuwa wameweka na wakiendelea na mazoezi kwenye Fukwe za Coco Beach ilikua ni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ho na Afrika Kusini ambapo wamejitoa tayari.

"Lengo letu la kwanza ilikuwa ni mechi dhidi ya Afrika Kusini lakini wamejitoa tayari ambao ulikua  ni mchezo wa kufuzu kwenda Mataifa Afrika (AFCON) na tutawalipa wachezaji wote stahiki zao ili warejee majumbanu," amesema Pawasa.

Amesema, katika maandalizi yajayo kwa ajili ya michuano ya  kuwa wameshatuma maombi kwa  timu ya Taifa ya Oman  kwa Kocha Talib Hilal  kwa ajili ya kuweza kupata kambi ya wiki mbili kabla ya kwenda nchini Misri kuchuana katika michuano hiyo ya AFCON.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Soka la Ufukweni wakiwa katika mazoezi Fukwe za Coco Beach.

"Wenzetu Oman ni wazoefu wameweza kucheza hata mashindano ya dunia kwahiyo kupata nafas ya wiki mbili nchini mwao itakuwa ni nafasi nzuri sana kwetu kwa maandalizi ya AFCON, ukiangalia Oman na Misri sio mbali,"amesema.

Pawasa amesema kuwa mpaka sasa ameshaomba mechi za kirafiki kwa timu ya Malawi na Uganda kwa ajili ya kupata mchezo wa kirafiki kujiandaa na michuano ya AFCON miezi mitatu ijayo.

micAmeeleza kuwa  mbali na hilo atakuwa na programu ya kuweza kuwapata wachezaji wengi wa mchezo huo mwezi Oktoba mwaka huu na kuwataka wachezaji wa mpira wa miguu kuja kutafuta fursa baada ya kushindwa kuoata nafasi kwenye timu ya taifa ya mpira wa miguu.

Mbali na hilo, Pawasa amewaomba watanzania waweze kujitokeza kuisaidia timu ya taifa ya soka la ufukweni kwani ni timu inayowakilisha nchi na sio klabu, wasiwaachie majukumu yote Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kwani imechukua miaka takribani 30 kuweza kufuzu kwenda Michuano ya AFCON na malengo yakiwa ni kuhakisha wanapata nafasi ya kwenda Kombe la Dunia nchini Paraguay.



Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ya Tanzania imefuzu kucheza Fainali za Africa zitakazofanyika nchini Misri. 
 baada ya mpinzani wake Afrika Kusini kuwasilisha barua ya kujiondoa katika mashindano.  


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tayari wametuma barua hiyo ya kufuzu kucheza Fainali hizo za Afrika zitakaofanyika Misri mwaka huu kuanzia Desemba 9-Desemba 14,2018 na kushirikisha nchi Nane.

Timu ya  Soka la Ufukweni ilikuwa kambini kujiandaa na mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumapili Septemba 9,2018 na kambi hiyo itavunjwa rasmi Jumapili.

WANAFUNZI WATATU WA IFM WAPATA UFADHILI WA ADA YA MWAKA WA TATU

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Wanafunzi watatu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamepata ufadhili kusoma mwaka wa tatu kwa kulipiwa ada kupitia kampuni ya Bima ya Metropolitan.

Akizungumza wakati wa kupokea hundi ya sh.milioni 4.5 Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Immanuel Muzava amesema kuwa kampuni ya Bima ya Metropolitan kupitia Chama cha Mawakala wa Bima (TIBA) kimefanya jambo la kuigwa katika umuhimu wa kusaidia wanafunzi ambao wana uhitaji wa kuweza kuhitimu masomo yao.

Muzava amesema kuwa sekta ya Bima inakua kwa kasi nchini hivyo lazima kuwepo na watalaam wa kutosha.

Wanafunzi waliopata ufadhili huo Paschalina Msofe,Rhoda Maholy pamoja na Leonard Mahimbo.

Amesema wanafunzi hao walikuwa na changamoto ya kiuchumi ambayo ingewafanya wakwame kuhitimu mwaka wa tatu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar amesema kuwa wanajibu wa kufanya hivyo bila kulazimishwa.

Amesema kuwa watu wakipewa elimu kunaongeza tija kwa serikali katika kuwa na watalaam wataosaidia maendeleo ya uchumi.

Aidha amesema waliofadhiliwa sio wakihitimu wakafanye kazi katika kampuni hiyo bali watafanya sehemu yeyote ikiwa nia kutoa huduma ya bima katika maendeleo ya nchi.

Mmoja wa wanafunzi waliofadhiliwa Paschalina Msofe amesema kuwa kazi yao ni kusoma bidii na kutoa matokeo mazuri kwa kile walichosome katika utoaji wa huduma ya bima nchini.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar akizungumza wakati wa kupokea hundi ya wanafunzi waliofadhiliwa katika chuo hicho.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar akizungumza kuhusiana na kampuni hiyo kufadhili ada kwa wanafunzi.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Immanuel Muzava  akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar kwa ajili ya ada kwa wanafunzi kwa ada ya mwaka wa tatu.
 Mwanafunzi wa IFM Rhoda Maholy akitoa shukurani kwa niaba wanafunzi wenzake kuhusiana msaada kusoma mwaka wa tatu kwa ufadhili.
Wanafunzi wa IFM wakiwa na hundi ya mfano wa ada ya iliyotolewa na Kampuni ya Bima ya Metropolitan.

MTAANI : MAANDALIZI YA BIASHARA

$
0
0

 Mfanyabiashara wa Matunda akiendelea na biashara yake huku pembeni kukiwa na mtaro wa maji machafu katika eneo la Mwenge  jijini Dar as Salaam,jambo ambalo ni hatari kwa afya ya walaji.Wananchi wanaaswa kutunza mazingira yao na kuwa safi kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uchafu.(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
Wafanyabiara wa samaki katika kituo cha mabasi  Mwenge jijini Dar as Salaam wakiweka  samaki katika meza hukupembeni kukiwa na mtaro wa maji taka.

PROF KITILA MKUMBO AWATAKA WADAU WA MAJI KUTOA MAONI YA UTUNGAJI WA SHERIA MPYA YA MAJI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu wa  Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo amewataka  wadau wa maji nchini kushiriki katika utoaji wa maoni kuhusiana na utungaji wa sheria mpya ya maji ili kuweza kudhibiti upotevu wa maji.

Amezungumza hayo katika Ofisi za Dawasa jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa sheria hii mpya itasaidia Mambo mengi ikiwa ni pamoja na udhibiti wa maji ambayo yamekuwa yakipotea kwa asilimia 44 mpaka sasa

Prof Mkumbo amesema wizara inapendekeza kuanzishwa kwa Taasisi maalumu  ya kushughulikia miradi ya maji mijini na vijijini yaani Rural Water Agency, Taasisi ambayo imekusudia kuimarisha Jumuia za watumiaji wa maji kwa ngazi za vijiji na miji ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa Taasisi mpya ya Dawasa

Kutunga kwa sheria hii mpya ya maji kutaongeza matamanio kwa watumiaji wa maji na kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama kwa uhakika  zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya DAWASA Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka wananchi wa Dar Es Salaam na Pwani kushirikiana na Dawasa katika ufanyaji kazi wake hasa kutoa taarifa punde inapobainika uvujaji wa maji, na kusisitiza kuhusu utungaji wa sheria mpya unapofanyika wananchi watoe maoni ili mchakato uwe na tija kwani sheria hii ina manufaa makubwa kwa wananchi.
Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Menejiment mpya ya Mamlaka ya Maji Taka na Maji Safi (DAWASA) inayoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) leo baada ya kukutana nao ofizi za DAWASA Jijini Dar es Salaam.

PPRA yawapa wahandisi ufafanuzi fursa ya ununuzi kwa njia ya mtandao

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imeendelea kuwapa wadau wake elimu na ufafanuzi kuhusu fursa na faida za kutumia mfumo wa ununuzi wa njia ya mtandao (TANePS).
Mamlaka hiyo imetumia fursa ya maonesho ya mkutano wa 16 wa mwaka wa Wahandisi yaliyoandaliwa na Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), yaliyofanyika Septemba 5 hadi 7 jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, PPRA ilikuwa inapokea maoni na kujibu maswali mbalimbali yaliyohusu mfumo wa ununzi kwa njia ya mtandao (TANePS) pamoja na masuala yanayohusu marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma yaliyofanyika mwaka 2016.
Katika maboresho ya sheria ya ununuzi wa umma, wahandisi walijikita zaidi katika marekebisho ya kanununi Na. 55A, 55B, 55C NA 55D, kama walivyoelezwa na mgeni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kuwa kupitia maboresho ya sheria ni vyema wakachangamkia fursa za miradi ya serikali kuliko kulalamika kila wakati kuwa wanakosa miradi hiyo na kupewa kampuni za nje ya nchi.
Akizungumziaa kuhusu mfumo wa ununuzi wa umma (TANePS), Mhandisi Mwanahamisi Ally wa kampuni ya Classic Plan alisema kuwa baada ya kujiunga na TANePS anaona mwanga wa kupungua kwa mianya ya rushwa na urasimu katika michakato ya manunuzi ya umma, hivyo akawaomba PPRA waendelee kutoa elimu zaidi kwa wahandisi na wazabuni kwa ujumla ili wasipitwe na fursa hiyo muhimu.
“Leo nimepata ufafanuzi zaidi zaidi kuhusu maeneo ambayo nilikuwa na maswali  zaidi baada ya kujisajili na kupata mafunzo ya kuutumia mfumo huu wiki kadhaa zilizopita,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kupata ufafanuzi, alitaka kufahamu ni lini fursa za zabuni zitaanza kutangazwa kwa njia hiyo ili aanze ‘kuchangamkia’ fursa hiyo muhimu isiyo na urasimu na inayohuisha uwazi.
Akitoa ufafanuzi kuhusu swali hilo, Afisa Tehama wa PPRA, Giftness David alisema kuwa kwa sasa baadhi ya taasisi zimeshawasilisha mpango wa manunuzi kwa njia ya TANePS, na kwamba kwa ujumla takribani wazabuni 1000 wamekwisha jiandikisha kwenye mfumo huo, hali inayoashiria utayari zaidi.
Aidha, Mhandisi Tumaini Msaki aliungana na idadi nyingine ya wahandisi kuuliza maswali ya sheria ya manunuzi ya umma, hususan kuhusu marekebisho ya sheria na kanuni ya mwaka 2016.
“Mimi nilitaka kufahamu ni kwa kiasi gani wahandisi wa ndani wanapewa nafasi ya kufanya kazi na Serikali kupitia zabuni mbalimbali ambazo makampuni ya nje yanakuwa yanashindania pia kwa kuwa wenzetu wana nguvu zaidi ya kifedha na mitambo,” alisema Mhandisi.
Aliongeza kuwa alijibiwa na kuoneshwa jinsi ambavyo sheria inatoa nafasi ya upendeleo kwa wazabuni wa ndani wanapokuwa wanashiriki zabuni zinazohusisha makampuni ya nje pia. Alisema kuwa sheria hiyo inatoa hadi upendeleo wa asilimia 10 kwa wazabuni wa ndani katika hali hiyo.
TANePS, ni mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao unaoratibiwa na PPRA kwa kushirikiana na taasisi za Serikali ambao ni wadau wa manunuzi. Mfumo huu ulizinduliwa rasmi Juni mwaka huu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa. 
 Afisa Tehama wa PPRA, Giftness David, akijibu maswali ya wahandisi kuhusu TANePS katika maonesho ya mkutano wa 16 wa mwaka wa Wahandisi yaliyoandaliwa na Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), yaliyofanyika Septemba 5 hadi 7 jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa PPRA, Nelson Kessy, na Afisa Tehama, Siganike Baruti wakitoa ufafanuzi kwa wazabuni kutoka kampuni ya Bizcyclone katika maonesho ya mkutano wa 16 wa mwaka wa Wahandisi yaliyoandaliwa na Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), yaliyofanyika Septemba 5 hadi 7 jijini Dar es Salaam.

MICHUZI TV: Mgambo wanaodaiwa kupiga raia virungu na Ofisa mtendaji Bunju wapandishwa kizimbani

$
0
0
Na Karama Kenyunko,blogu ya Jamii.

ASKARI Mgambo wawili na Afisa mtendaji wa kata ya Bunju, 
 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kumjeruhi kwa kutumia Rungu mkazi wa Bunju Robinson Olotho.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni askari Mgambo Kelvin Sawala (25) na Goodluck Tarimo (30) ambao wanashtakiwa pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Ibrahim Mabewa (39).

Wakisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde imedaiwa August 30, 2018 huko  Bunju Wilayani Kinondoni, washtakiwa hao walimpiga Olotho kwa kutumia rungu sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali

Hata hivyo washtakiwa wamekana kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya wakili wa serikali, Nassoro Katuga kuieleza mahakama kuwa, licha ya kesi hiyo kudhaminika lakini wanaiomba mahakama isubirishe dhamana ya washtakiwa hao kwa sababu kuu mbili.

Amezitaja sababu hizo  kuwa kuna suala la kiusalama ambapo washtakiwa walionekana kwenye video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, hivyo kama watapatiwa dhamana usalama wao utakuwa shakani kwa sababu wananchi na ndugu wa mjeruhiwa watakuwa na hasira.
Pia akadai sababu nyingine ni kwamba mjeruhiwa bado yupo hospitali na hali yake ya kiafya sio nzuri.

Hakimu Kasonde alipowauliza washtakiwa hao kuhusu hoja hizo walidai hali ya afya ya mjeruhiwa walionana naye jana na anaendelea vizuri wala hayupo hospitalini na kuwa suala la usalama wao liko vizuri, hivyo wanaomba dhamana, 

Hata hivyo, Hakimu Kasonde amesema mahakama imekubali hoja za upande wa mashtaka kuhusu usalama wa washtakiwa hao, hivyo wananyimwa dhamana hadi hapo itakapojiridhisha kuhusu usalama wao.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado hayjakamilika na imeahirishwa hadi September 20,2018.

KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya maafisa wa ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na gereza la Mahabusu Tanga mara alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Maweni jijini Tanga akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (mwenye “microphone” ) akizungumza na maafisa na askari wa vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Gereza Kuu Maweni na Gereza la Mahabusu Tanga (hawapo pichani) kwa pamoja katika bwalo la Gereza Kuu Maweni Tanga alipofanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmauel Lwinga, wa tatu kulia ni Mkuu wa Gereza Kuu Maweni Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Felichism Masawe na wa kwanza kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Marakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Hamis Mbwana.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akifuatilia kwa makina taarifa ya mkoa wa Tanga kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Emmanuel Lwinga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7,2018.
Baadhi ya maafisa na askari wa vituo vya ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga, waliokusanyika kwa pamoja katika bwalo la gereza Kuu Maweni wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo leo Septemba 7, 2018. Katika hotuba yake CGP ametilia mkazo suala la kubadili mtazamo wa kiutendaji, kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kufanikisha majukumu yetu kama serikali na jamii nzima inavyotarajia kutoka kwetu.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi askari wa magereza wa kike mkoani Tanga alipofanya ziara ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) walioko mkoani Tanga alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo leo Septemba 7, 2018. Picha zote na Jeshi la Magereza.

RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA MKOANI SIMIYU KESHO SEPTEMBA 08

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atafanya ziara ya siku tatu (03) Mkoani Simiyu, kuanzia kesho tarehe 08/09/2018 hadi tarehe 10/09/2018, Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthony Mtaka amesema Mhe. Rais akiwa mkoani Simiyu atapata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi, kufungua pamoja na kuzungumza na Wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Mtaka amesema siku ya Jumamosi tarehe 08/09/2018, Mhe. Rais atakagua na kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Lamadi uliopo wilayani Busega na baadaye, ataelekea wilayani Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo(kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mkutano kati ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Waandishi wa Habari, kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10, 2018.

Aidha, amesema Mhe. Rais akiwa katika Wilaya ya Bariadi, atafungua Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, atakagua na kufungua barabara za lami (kilomita 6.9) zilizojengwa chini ya mradi wa kuboresha Miundombinu ya Miji (ULGSP).

“Siku hiyo pia atakagua maendeleo ya Ujenzi wa  barabara ya Bariadi-Maswa inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi. Mhe.Rais atapokea salamu za Chama Cha Mapinduzi, salamu za Wilaya, Mkoa, taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara na baadaye kuzungumza na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania wote kwa ujumla, katika Mtaa wa Salunda kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Salunda.”
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ofisini kwake alipozungumza nao leo, kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambaye anatarajia kuanza ziara ya siku tatu(03) kuanzia Septemba 08 hadi Septemba 10,2018.

“Tarehe 09/09/2018 Mhe. Rais atazungumza na wananchi wa wilaya ya Itilima eneo la Makao Makuu ya Wilaya (Lagangabilili) na kuelekea wilayani Meatu. Akiwa njiani kuelekea Meatu Mhe. Rais atapata fursa ya kusalimia wananchi wa Kijiji cha Mwandoya na baadaye atafungua Miundombinu ya Uboreshaji wa Huduma za Afya Hospitali ya Wilaya ya Meatu na kuzungumza na wananchi katika Viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi” alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa Siku ya Jumatatu tarehe 10/09/2018 Mhe. Rais Magufuli atahitimisha ziara yake Mkoani Simiyu kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Mto Sibiti linalounganisha Mkoa wa Simiyu na Singida na baadaye  kuwasalimia wananchi.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote mkoani Simiyu hususani katika Miji ya Lamadi, Bariadi, Lagangabilili, Mwanhuzi na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Mhe. Rais Magufuli atapita na kufanya mikutano ya hadhara.

Programu ya Vodacom Tanzania ya mafunzo kwa wahitimu vyuo vikuu kufanikisha kupata viongozi wa baadaye

$
0
0
Programu nyingi za mafunzo kwa wahitimu wa vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi duniani kote, zimekuwa zinalenga kuwawezesha wasomi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuwa na dhamira ya kuajiriwa kwenye makampuni mbalimbali yanayohitaji wataalamu. Huwawezesha wahitimu hao kupata msingi na ujuzi kuhusiana na taaluma zao, sambamba na kuwaanda kuwa viongozi wa siku za mbele. 

Tofauti na programu nyingine za kuwafundisha wahitimu wa vyuo vikuu kazi,Programu ya Vodacom Tanzania (ambayo imeasisiwa na Vodafone Group) inajulikana kama ‘Gundua Vipaji vya Wahitimu wa Vyuo Vikuu). Humuwezesha mhitimu kufanya kazi kwenye vitengo muhimu vya kampuni.

Programu hii ya miaka 2 inalenga kuwapata viongozi wa baadaye wa kuendesha biashara za kampuni kutoka kwa wahitimu wa vyuo vikuu waliobobea katika fani mbalimbali.Kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya hapa nchini,lengo ni kukuza vipaji na kuwapata wataalamu ambao watafanikisha kuiwezesha Vodacom kwenda sambamba na mabadiliko katika sekta ya mawasiliano. 

Programu hii ya ‘Gundua vipaji vya wahitimu wa Vyuo vikuu’ nchini Tanzania, ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Julai,mwaka 2015 na ilianza kwa kupokea maombi ya wahitimu 10 kutoka vyuo mbalimbali ambao walichukuliwa katika awamu ya kwanza ilipoanzishwa. 

Ili kujiunga nayo,mhitimu anapitia mchakato mkali uliowekwa, kuhakikisha wanapatikana washiriki wenye sifa zinazostahili. Wahitimu wanafanyiwa tathmini kwa njia ya mtandao,kupitia uelewa wa majukumu watakayotekeleza,tathmini kwa njia ya makundi,uwezo wa kuwasilisha mada na kujieleza na mahojiano ya uso kwa uso.
Wahitimu wa programu ya kampuni ya Vodacom Tanzania wakikata keki kusherehekea kumaliza programu ya miaka miwili iitwayo 'Discover Graduate'. Programu hii iliyoanzishwa July mwaka 2017 inalenga kufunza na kusaidia wanafunzi bora kutoka vyuo mbalimbali nchini kuja kuwa viongozi bora wa kesho.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Perece Kirigiti akimkabidhi Gervas Mfubusa, moja kati ya watahitimu waliochaguliwa kuingia kwenye programu ya 'Discover Graduate'. Discover Graduates ni programu ya miaka miwili iliyodhamiriwa kufunza na kusaidia wahitimu bora kutoka vyou mbalimbali nchini kuja kuwa viongozi bora wa kesho. 

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images