Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Matumizi ya ARV hupunguza maambukizi kwa mtu mwingine

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu  akiendelea na matembezi katika moja ya banda lililokuwa katika viwanja vya maji maji Songea mkoa wa Ruvuma wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu Mkoa wa Ruvuma.

Na WAMJW-SONGEA,RUVUMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa mtu akitumia ARV kwa usahihi na kikamilifu anapunguza ewezekano wa kuambukiza VVU kwa mtu mwingine  kwa takribani Asilimia 60.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo wakati akizindua Kampeni ya FURAHA YANGU, PIMA, JITAMBUE, ISHI katika  viwanja vya Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma. 

“Kwa mujibu wa Wataalamu wa Afya ikiwemo Wanasayansi imedhihirika kwamba mtu akianza mapema kutumia Dawa anapunguza uwezekano wa kupata magonjwa nyemelezi, pia anaongeza muda wa kuishi na anapunguza uwezekano wa kuwaambukiza watu wengine”  alisema Waziri Ummy Mwalimu.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu aliselebuka na kikundi cha Bendi cha JKT Mlale wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha Yangu mkoa wa Ruvuma katika viwanja vya maji maji Songea.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa mtu akigundulika kuwa na maambukizi ya VVU na UKIMWI ataanzishiwa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi mara moja badala ya kusubiri hali yake kuwa mbaya zaidi. 

Waziri Ummy alisema kuwa wakati Takwimu za Kitaifa zikionesha maambukizi ya VVU yamepungua kutoka Asilimia 5.7 hadi Asilimia 4.7, bado maambukizi mapya yameendelea kuwepo, takribani vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 sawa na Asilimia 40 wanaambukizwa VVU.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa Asilimia 52 ya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wanajifahamu kuwa wana VVU,  katika kila watu 100 Watu 48 wenye maambukizi ya VVU hawajui kuwa wana VVU jambo ambalo ni hatari kwenye kaya zao na Taifa kwa ujumla .

Mbali ya yote Waziri Ummy aliwaagiza watoa huduma  kupitia Kampeni hiyo kwamba  watu wote wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU vizuri kwa kuzingatia masharti wapewe dawa za miezi mitatu badala ya mwezi mmoja kama inavyofanywa sasa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wapili Kushoto) akiendelea na matembezi katika viwanja vya maji maji wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Furaha yangu mkoa wa Ruvuma.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme.

“Watu wote wanaotumia Dawa vizuri kwa kuzingatia masharti, wapewe dawa za miezi mitatu badala ya kila mwezi kwenda kuchukua dawa katika vituo vya kutoa huduma za afya, tunaamini kwamba hatua hii itachochea watu wengi zaidi kwenda kupima na kujiandikisha kupata huduma za dawa” alisema Waziri Ummy.


MEYA WA DAR ES SALAAM AZINDUA MASHINDANO YA MASHAIRI

$
0
0
MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amezindua mashindano ya mashairi jijini Dar es Salaam leo yenye lengo la kukuza lugha ya kiswahili hapa nchini mashindano hayo yenye kauli mbiu  isemayo " Lugha yetu fahari yetu"

Mashindano hayo mgeni rasmi atakuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hasan Mwinyi washiriki wa mashindano hayo ni 51 ambapo mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni moja, mshindi wa pili atapata shilingi lakitano, mshindi wa tatu atapata shilingi laki tatu na mshini wa nne mpaka kumi watapata shilingi laki moja moja.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa mashairi ameomba lugha ya Kiswahili itumike barani Afrika kwa ujumla na Hapa nchini itumike kama Lugha ya kufundishia.Amesema kuwa mashindano hayo hayataishia jijini Dar es Salaam tuu pia anategemea kuanzisha na mikoa mingine ya Tanzania. "Mashindano haya hayataishi jiji la Dar es Salaam tuu pia tutayaanzisha na mikoa mingine ya Tanzania"

Pia ameomba Lugha ya kiswahili iweze kurasimishwa katika nyanja za kisheria. kiafya pamoja kielemu kwa shule za msingi na sekondari pamoja na chuo kikuu ili mwanafunzi akifundishwa aelewe lugha na kitu anachofundishwa ili ajengewe uwepo wa kuelewa vizuri.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya taaruma za Kiswahili wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Ernesta Mosha amesema kuwa vitabu vya kufunsihia kidato cha kwanza mpaka cha nne vimeshatayarishwa kwaajili ya kufundishia ila bado havijalasimishwa tuu kutumika vitabu hivyo ni pamoja na Bayilojia, Hisabati, Jeografia na Historia ambavyo vimeandiskwa kwa lugha ya kiswahili fasaha bila kutohoa(translation)

Amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa kikwazo cha Istilahi sio tatizo kabisa kwa sababu mtu anajifunza kuanzia shule ha msingi mpaka chuo kikuu na lugha ya kiingereza iwe kama ya kujifunza ili kuwezesha mawasiliano ya kawaida.
 Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mashairi ambayo yanaendelea katika ukumbi huo ambayo yameshirikisha washiriki 51 kutoka Dar es Salaam pekee.

Mkurugenzi wa Taasisi ya taaruma za Kiswahili wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Ernesta Mosha akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya ushairi yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 1,2018.
 Wanafunzi wa shule za sekondari walikuja kuangalia mashindano ya mashairi yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mashindano ya mashairi ambayo yanalengo la kukuza Lugha ya kiswahili nchini Tanzania.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

SERIKALI YAJIPANGA KUBHIBITI UCHELEWESHAJI WA KUPAKUA SHEHENA YA MAFUTA BANDARINI

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwele, wa pili kushoto akiangalia moja ya nondo zilizoshushwa bandarini kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya bandari na kituo cha kushushia mafuta cha KOJ. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko.  
 Mkandarasi wa mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam (DMGP) kutoka Kampuni ya China Habour Engineering, LV Wei, kushoto akitoa maelezo ya mradi huo ulipofikia kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwele, wa pili kulia na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya bandari na kituo cha kushushia mafuta cha KOJ.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwele, kushoto akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya bandari na kituo cha kushushia mafuta cha KOJ.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kwamba Serikali imejipanga kubhibiti ucheleweshaji wa kupakua shehena ya mafuta bandarini ili kubhibiti upandaji bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la ndani.

Waziri Kamwelwe ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea bandari ya Dar es Salaam katika eneo la Kurasini Oil Jet (KOJ), na kubaini kuwa wakati wa zoezi la upakuaji kunakuwa na tatizo la ucheleweshaji mbalo mwisho wa siku huchangia kuongezeka bei ya mafuta. 

Mh. Kamwele amesema kwamba wamegundua kuwa uwezo mdogo wa pampu za meli za kupakulia mafuta pamoja na uhaba wa matenki ya kuhifadhia mafuta kwa waagizaji wa bidhaa hiyo pamoja na kuvuja kwa mabomba ya mafuta ndio chanzo kikubwa cha kupanda bei.  

“Tumegundua kuwa tatizo lingine linalochangia kuongeza bei ya mafuta kuwa ni ucheleweshaji wa kupakua shehena hiyo ya mafuta kwani baadhi ya meli hazina pampu zenye wezo wa kusukuma bidhaa hiyo kwa nguvu inayotakiwa,” amesema waziri Kamwele.

WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA BIL 2.5/-KUJENGA CHOO CHA MFANO KWA MAJIMBO YOTE NCHINI

$
0
0

 Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa benki ya CRDB wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Anne Makinda akipokea hundi kutoka kwa wawakilishi wa benki ya NBC wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

wakati wa harambee ya uchangiaji wa fedha kwaajili ya kujenga choo cha Mfano katika majimbo yote hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

*Spika mstaafu Makinda ashangazwa… atoa neno 
*Dk.Tulia asema ili kufanikisha lengo zinahitaji Bil 3.5/- 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Wabunge Wanawake wa Bunge la Tanzania wamefanikiwa kukusanya Sh.milioni 800 kwenye harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo kitakachojengwa katika majimbo yote nchini.

Fedha hizo zimekusanywa jana kwenye harambee iliyofanyika Mliman City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi kwenye harambee hiyo alikuwa Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda.

Tayari wabunge hao wanawake wamefanikiwa kukusanya jumla ya Sh.bilioni 2.5 kwani kabla ya harambee ya jana tayari walishafanya harambee nyingine ya kukusanya fedha jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo Spika wa Bunge Job Ndugai amesema wanatambua umuhimu wa kuunga mkono jitihada za wabunge wanawake katika kuhakikisha wanatimiza lengo la ujenzi wa choo.

“Tumekutana hapa kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.Lengo ni kujenga vyoo nchi nzima kwa maana ya majimbo yote,”amesema Ndugai.

Kwa upande wa mgeni rasmi Spika mstaafu wa Bunge Makinda amesema uamuzi ambao umefanywa na wabunge wanawake na kuungwa mkono na wabunge wanaume katika kufanikisha fedha zinapatikana ni wa kihistoria.

“Tunatambua changamoto ambazo wanafunzi wanazipata na hasa kwa mtoto wa kike kutokana na maumbile yake.Hivyo ujenzi wa choo cha mfano kitasaidia kuwafanya wanafunzi hao kufurahia mazingira yatakayokuwamo kwenye choo hicho.

“Tunafahamu binti wa kike anapovunja ungo akiwa shuleni kuna mabadiliko yanaanza kutokea na anapokuwa kwenye tarehe yake wengine wanatega shuleni kwa kuona hawako salama.Choo kitakachojengwa kitamfanya binti kutokuwa na wasiwasi hata akiwa kwenye tarehe za hedhi,”amefafanua.
Makinda ametoa ombi kwa Watanzania kokote walipo kuchangia ujenzi wa choo hicho kwani lengo na kumuondolea adha mwanafunzi na hasa mwanafunzi wa kike.

PROFESA JAY, NAPE WACHUANA, MLINGA AENDESHA KIGARI JUKWAANI

$
0
0
WABUNGE WAAMSHA SHANGWE UKUMBI WA MLIMANI CITY DAR
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 
BUNGE limesheheni vipaji katika fani ya Sanaa na burudani!Hivyo ndivyo unavoweza kuelezea baada ya wabunge kutoka majimbo mbalimbali kuonesha umahiri wao katika fani hiyo. 

Wabunge hao wamedhihirisha hili jana usiku kwenye ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo cha mfano. 

Hivyo kabla ya kuanza kwa shughuli ya harambee hivyo, wabunge waliamua kuteka sekta ya Sanaa na burudani kwa kuonesha umahiri wao. 


Wapo wabunge ambao wameonesha umahiri katika mchezo wa sarakasi huku wengine wakishindana kucheza Singeli.


Pia wabunge wengine walishiriki kuimba nyimbo maalum kwa ajili ya harambee hiyo na wapo walioimba kwaya pamoja na kucheza nyimbo za kabila la Wanyamwezi. 


Hata hivyo baada ya burudani hiyo kupamba moto jukwaa likatawaliwa na ushindani mkali kati ya Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule a.k.a Profesa Jay. 

Wakati Nape ameamua kuimba nyimbo za zamani(Zilipendwa) Profesa Jay yeye aliamua kuimba muziki wa kizazi kipya. 

Hata hivyo hakukuwa na mshindi kwani kila mmoja alionesha umahiri mkubwa wa kushika kipaza sauti na kuteka mashabiki ambao wengi wao walikuwa wabunge wenyewe pamoja na wageni waalikwa. 

Haikushia hapo kwani wabunge hao katika kuthibitisha hakuna ambacho hawakijui wapo ambao wao walionesha umahiri wa kulitawala jukwaa kwa kuonesha mitindo ya mavazi. 

Mbunge Geita Vicky Kamata na Mbunge Mathar Mlata wao walithibitisha ubora wa sauti zao walipokuwa wanongoza wabunge wengine kuimba. 

Naibu Spika Dk.Tulia Akson yeye alipanda jukwani kuimba wimbo wa Subalkere Mpenzi akiwa mtoto wake(Gudlucky Mlinga) aliyekuwa anaendesha kigari . 

Baadhi ya wageni waalikwa ambao wamezungumzia namna ambavyo wamebunge hao wameonesha umahiri katika eneo la burani wamesema wanastahili kupongzwa. 



kwani wamethibiwa Viti Maalum Mkoa wa Samua kutoa na kuchezea , kucutoa buruWABUNGE mbalimbali wameonesha.
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye akitumbuiza wabunge na wageni waalikwa wakati wa harambe ya kuchangia ujenzi wa choo cha mfano kitakachojengwa kwenye kila jimbo hapa nchini ambapo choo kimoja kitakuwa na matundu 10.


Mbunge wa Mikumi Joseph Haule a.k.a Profesa Jay 
akitumbuiza wabunge na wageni waalikwa wakati wa harambe ya kuchangia ujenzi wa choo cha mfano kitakachojengwa kwenye kila jimbo hapa nchini ambapo choo kimoja kitakuwa na matundu 10.


Naibu Spika Dk.Tulia Akso, Mbunge wa Kindondoni, Maulid Mtulia na Mbunge wa Ulanga anayeendesha kigari jukwaani, Goodluck Mlinga wakiwa  jukwani wakiimba wimbo wa Subalkere Mpenzi

wakati wa harambe ya kuchangia ujenzi wa choo cha mfano kitakachojengwa kwenye kila jimbo hapa nchini ambapo choo kimoja kitakuwa na matundu 10.


Wabunge wakionesha burudani.Mbunge akicheza Singeli jukwaani.
Wabunge wakipita jukwaani wakionesha mavazi ya mitindo mbalimbali.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya jamii



TCU yatangaza wenye sifa ya kujiunga vyuo vikuu 2018/2019

$
0
0
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
TUME ya Vyuo Vikuu  Nchini (TCU) imetangaza maombi ya wanafunzi watakaojiunga vyuo vikuu katika mwaka wa masomo 2018/2019.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charle's Kihampa amesema kuwa jumla ya waombaji wa awamu ya kwanza walikuwa 74,113.

Amesema wanafunzi waliodahiliwa na vyuo vikuu awamu ya kwanza 43,005 katika dirisha la awamu ya kwaza. Profesa Kihampa amesema kuwa wanafunzi waliokosa kudahiliwa katika dirisha hilo ni wanafunzi 31,108.

Amesema katika uhakiki wa maombi hayo wamepata wanafunzi 39,812 ndio wenye sifa ya kujiunga na Shahada ya kwanza.

Amesema walioidhinishwa na TCU 22,743 huku waombaji 16,507 wameomba vyuo zaidi ya kimoja ambapo watatumiwa namba ya siri ya kuwa na chuo kimoja atachosoma shahada hiyo.

Kati ya maombi hayo ni wanafunzi 3,193 hawana sifa ya kujiunga na shahada ya kwanza huku waombaji waliodahiliwa miaka ya nyuma ni 562 na baadhi ya majina ya waombaji 102 yanakasoro.
Amesema dirisha la awamu ya pili litafunguliwa Septemba 6 na kufungwa Oktoba 6 mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) Profesa Charle's Kihampa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na wanafunzi wanaopaswa kudahiliwa katika shahada ya kwanza katika mwaka masomo 2018/2019.

DK.KEBWE ATAKA ELIMU YA USM ISAMBAZWE NCHINI

$
0
0
NA Suleiman Msuya,Morogoro 
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Steven Kebwe amesema elimu ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM) ikisambazwa nchini kote misitu itakuwa endelevu na kuepusha nchi kuingia katika jangwa. 

Dk. Kebwe aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 18 wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) uliofanyika mkoani Morogoro. 

Alisema iwapo elimu ya USM itasambaa kwa kila mwana jamii ni dhahiri rasilimali misitu itakuwa salama kwa muda mrefu hivyo ni imani yake kila kiongozi atatoa kipambele. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema uhifadhi misitu ni jambo ambalo haliepukiki hasa katika kipindi hiki kwa kuwa madhara yakutohifadhi yameshaonekana jwa sasa. 

“Napenda kutumia nafasi hii kuziomba mamlaka husika ili elimu ya USM ifikie kila kiongozi katika nchi kwani takwimu za kuharibiwa kwa hekta 469,000 kila mwaka ni dalili za jangwa na Morogoro pekee inaharibu hekta 150,000 sawa na asilimia 48 ya uharibifu wote,” alisema. 

Alisema iwapo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) itaweka taratibu ambazo zitaelekeza njia mbadala ya kukabiliana na uvunaji wa miti kwa sababu ya kaa hali itakuwa salama. 

Dk. Kebwe alisema kinachoonekana kwa sasa ni kukosekana kwa maelekezo sahihi ambayo yatasababisha sheria kusimamiwa kikamilifu. 

Alisema katika mkoa wake atahakikisha wasaidizi wake wanasimamia rasilimali misitu kwa weledi huku ikifaidisha jamii zaidi ambayo inazungukwa na misitu hiyo. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema iwapo kila mkoa utatembea na dhana ya kuhakikisha jamii inanufaika na rasilimali hiyo ni wazi kuwa ulinzi utakuwepo na dhana ya uchumi wa viwanda itaonekana moja kwa moja. 

Mwenyekiti wa Mjumita Taifa, Revocatus Njau alisema wao wamejikita katika kutoa elimu ya usimamizi shiriki wa misitu baada ya kugundua jamii kubwa haina uelewa. 

Njau alisema pamoja na elimu pia wanahakikisha jamii inamiliki misitu inanufaika nayo kwa kufanya shughuli za kiuchumi kwa kufuata sheria za nchi. 

“Kwa miaka 18 tumekuwa tukitoa elimu ya utunzaji na unufaikaji kupitia rasilimali misitu, ila ipo changamoto kwa baadhi ya watendaji wa vijiji na kata kushirikiana na waharibifu wa misitu hali ambayo inatudisha nyuma,” alisema. 

Kwa upande wake Ofisa Misitu Mwandamizi kutoka Tamisemi Rogasian Lukoa alisema Serikali inajipanga kuhakikisha elimu ya USM inasambaa kwa kila mwanajamii ili kuwa mlinzi sahihi wa rasilimali hiyo. 

Lukoa aliwataka watendaji wa Serikali kuanzia ngazi za vijiji kushirikiana na taasisi kama Mjumita, Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Jamii Tanzania (TFCG) na wengine ili kuhakikisha misitu inakuwa endelevu.

MAKONTENA YA MAKONDA KUENDELEA KUNADIWA


TRENI YA KIFAHARI DUNIANI YALETA WATALII 64 NCHINI KUPITIA RELI YA TAZARA

$
0
0
 Fatma Salum- MAELEZO

TRENI ya kifahari inayojulikana kwa jina la ROVOS ambayo ni miongoni mwa treni tatu bora duniani imewasili jijini Dar es Salaam kwa kutumia reli ya Tazara ikiwa na watalii 64

Watalii hao wamekuja Tanzania kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii hapa nchini ikiwemo mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea watalii hao iliyofanyika stesheni ya TAZARA Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa TAZARA Tanzania, Fuad Abdallah alieleza kuwa treni hiyo iliondoka mji wa Cape Town nchini Afrika ya Kusini Agosti 18, mwaka huu.

“Watalii mbalimbali huja nchini mara tano kwa mwaka kwa kutumia ROVOS kupitia reli ya TAZARA na nchi yetu hunufaika na ujio huu hasa faida za kiuchumi,” alisema Fuad.

Aidha alibainisha kuwa treni ya ROVOS ni miongoni mwa treni tatu bora duniani, hivyo ujio wa treni hiyo na watalii unatokana na vivutio bora vya utalii na miundombinu mizuri ya reli ya TAZARA.

“Treni hii inatumia reli ya TAZARA kuleta watalii kwa sababu nchi yetu imekidhi vigezo vya utalii na reli yetu imekidhi vigezo vya usalama na mawasiliano ya uhakika,” aliongeza Fuad. 

Alisema kuwa katika safari hiyo ya treni watalii hao pia walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania na kuona wanyama mbalimbali wanaopatikana kwenye hifadhi hiyo.

Wakizungumza kwa furaha ya kuwasili Tanzania, watalii hao wa kijerumani walisema kuwa wamefurahia sana safari hiyo na mapokezi mazuri ya watanzania na kuahidi kurudi kwa mara nyingine.

Kwa upande wake mfanyakazi wa treni ya ROVOS, Monica Rieder mwenye asili ya Ujerumani alisema kuwa amewahi kufika Tanzania mara 14 na anavutiwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanyika hapa nchini siku hadi siku.

TAZARA ni shirika la reli ya pamoja ya Tanzania na Zambia iliyoanza mwaka 1976 na inamilikiwa kwa asilimia 50 kila upande.


 Meneja Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Fuad Abdallah (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari katika makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kabla ya kuwasili kwa treni ya kitalii ya ROVOS kutoka Afrika ya Kusini.
 Baadhi ya watalii kutoka Ujerumani wakifurahia buradani ya bendi ya Polisi baada ya kushuka kutoka kwenye treni ya ROVOS moja kati ya treni ya kifahari duniani, watalii hao wamekuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali.
 Mama wa Kijerumani Linde Erdmann (katikati) akifurahia kuwasili Tanzania kwa mara ya kwanza akitokea Afrika ya Kusini kwa kutumia treni ya ROVOS kupitia reli ya TAZARA.
Moja ya mgahawa unaopatikana katika treni ya kifahari ya ROVOS iliyowasili leo hapa nchini ikitokea Afrika ya Kusini kupitia reli ya TAZARA.
(Picha na Paschal Dotto- MAELEZO).

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA OFISI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI MKOA WA SINGIDA

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia kwa karibu Uwasilishwaji wa Taarifa ya Ukaguzi katika Mkoa wa Singida walipotembelea Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Singida.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akifuatilia Uwasilishwaji wa Taarifa kutoka kwa Naibu wa Mdhibiti Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ndg. Wendy Massoy katika Kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida hii leo, Kamati hiyo ipo katika Ziara Mkoani humo.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa George Simbachawene wakiwa katika kikao na Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida hii leo Kamati hiyo ilipofanya ziara yake Mkoani humo.

MAADHIMISHO YA WIKI YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KITAIFA YAFUNGWA JIJINI DODOMA.

$
0
0

Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola (Mb) Agosti 29, 2018 katika Uwanja cha Jamhuri Jijini Doodma na kufungwa jana Agosti 31, 2018 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa mwaka huu ni “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA KUFUNGA VING’AMUAMOTO VIWANDANI”

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye, akitoa taarifa ya Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi toka Makao Makuu wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, jinsi wanavyoweza kufanya maokozi kwenye majengo marefu pindi ajali inapotokea, alipotembela Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini humo jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, akipokea zawadi ya kizimia moto cha awali (Fire Extinguisher) kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto Philibert Chaki, alipotembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini Dodoma jana.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akimkabidhi cheti mwakilishi wa TCRA, ambaye jina lake halikupatikana kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyoanza Agosti 29, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.

MKUU WA OPERESHENI MAALUM JESHI LA POLISI AKITOA ELIMU JUU YA KUKABILIANA NA UHALIFU KATIKA KIJIJI CHA MASUGURU MKOANI MTWARA.

$
0
0

Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akisalimiana Kamandani Jawapi mwanakijiji wa Masuguru wilayani Masuguru mkoani Mtwara baada ya kumalizika mkutano na wananchi wa eneeo hilo.( Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akizungumza na wanakijiji cha Masuguru wilayani Masuguru mkoani Mtwara juu ya kukabilina na kuwafichua wahalifu wanaokimbilia kijijini hapo wakitokea nchini Msumbiji.( Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, akizungumza na wanakijiji cha Masuguru wilayani Masuguru mkoani Mtwara juu ya kukabilina na kuwafichua wahalifu wanaokimbilia kijijini hapo wakitokea nchini Msumbiji.( Picha na Jeshi la Polisi)

IN LOVING MEMORY

$
0
0
IN 8 YEARS MEMORY OF JOYCELYN MKAMSURI SAWAYA MAWALLA MAREALLE

Our mother you left to us beautiful memories your love is still our guide although we cannot see you physical  your always in our side. In life we loved you dearly in death we loved you still in our heart you hold a place no one could ever fill. Days will pass and turn into years but we will always remember you with silent tears.

Deeply remembered by you Beloved children Emmy and Leonard Marealle. Mpora Caroline Marealle and Grand children Vanessa Benne, Joyceline and Eve Marealle Brothers and Sisters from Mawalla and Marealle families. 

MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEFARIKI KWA KUPIGWA VIBOKO NA MWALIMU WAKE WAZIKWA WILAYANI MULEBA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Sinkamba Kandege akitoa heshima za mwisho kwa Mwlili wa Mwanafunzi Marehemu Sperius Eradius aliyefariki dunia Agosti 27, 2018 baada ya kupigwa viboko na Mwalimu wake wa nidhamu katika Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba.

Na ALLAWI KABOYO, MULEBA

Mwlili wa Mwanafunzi Marehemu Sperius Eradius aliyefariki dunia Agosti 27, 2018 baada ya kupigwa viboko na Mwalimu Respicius Mtazangira ambaye alikuwa Mwalimu wa nidhamu katika Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba umeagwa  na kusafirishwa Wilayani Muleba Kata Mubunda Kijiji Kitoko nyumbani kwa baba yake mzazi Eradius Petro na kuzikwa leo Agosti 31, 2018.

Katika mazishi hayo Serikali iliwakilishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Sinkamba Kandege ambaye alitoa salaam za Serikali katika msiba huo kwa kuwahakikishia familia, ndugu, jamaa wa marehemu pamoja na wananchi waliojumuika kumuaga Sperius Eradius kuwa lazima Serikali isimamie haki mpaka ipatikane kwa waliohusika katika tukio la mauaji ya mwanafunzi huyo.
“Sisi tunawaacha watoto wetu waende shule kama sehemu salaama tukiamini kuwa ndiyo sehemu salama na ya kujifunzia na siyo chuo cha mafunzo ya viboko. Jambo hili haliwezi kuachwa likapita  hivi hivi tuseme inatosha na iwe fundisho kwa wengine.” Alisisitiza Mhe. Naibu Waziri Kandege.

Pia Mhe. Naibu Waziri Kandege  aliiomba familia ya marehemu kuwa na subira kwa wakati huu mgumu wa kupoteza mpedwa wao Sperius Eradius na kusema kuwa msiba si wao tu bali ni msiba wa taifa zima. Aidha, aliishukuru Serikali ya Mkoa ilivyoshughulikia tukio hilo tangu lilipotokea Agosti 27, 2018 hadi kuupumzisha mwili wa Mwanafuzi Marehemu Sperius Eradius nyumbani kwa baba yake mzazi Eradius Petro. 

Baba yake mlezi Mchungaji Justus Balilemwa akitoa historia ya Mwanafunzi Marehemu Sperius Eradius alisema kuwa mtoto huyo alizaliwa Mei 2005 na mara baada ya kuzaliwa mama yake aliaga dunia na Sperius Eradius kuchukuliwa na kupelekwa Ntoma katika Kituo cha kulelea watoto yatima na baada ya mwaka mmoja alimchukua mtoto huyo na kuanza kuishi na kumlea kama mtoto wake hadi mauti yalipomkuta Agosti 27, 2018 akiwa na umri wa miaka 13 Shuleni Kibeta Manispaa ya Bukoba.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Sinkamba Kandege akizungumza katika mazishi ya Mwanafunzi Marehemu Sperius Eradius aliyefariki dunia Agosti 27, 2018 baada ya kupigwa viboko na Mwalimu wake wa nidhamu katika Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba.

“Kinachonisikitisha leo hii ni kuwa tulimchukua Sperius Eradius akiwa mzima lakini leo tumerudisha sanduku, haikuwa nia yetu tulitamani sana mtoto huyu atimize ndoto zake kwa kuwa alikuwa mchangamfu sana na alimjua Mungu kwa kuimba na kumtukuza Mungu katika Kwaya mbalimbali mfano kwaya ya Kagoma.” Alimalizia kwa uchungu mkubwa baba mlezi wa Sperius Eradius Mchungaji Justus Balilemwa.

Baba yake mzazi Marehemu Sperius Eradius, Eradius Petro akitoa neno kwa wananchi waliofika kumfariji katika mazishi hayo alisema yeye anamwachia Mungu kwa yaliyotokea bali anaishukuru Serikali kwa kulifuatilia tukio hilo kwa karibu sana. Pia na kutoa ushirikiano nyumbani kwa baba mlezi tangu tukio linatokea hadi kwenye mazishi ya Sperius Eradius.
Serikali ya Mkoa wa Kagera tangu kutokea kwa tukio hilo la mauaji ya Mwanfunzi Sperius Eradius (13) Agosti 27, 2018 imekuwa ikigharamia mahitaji yote katika familia ya baba mlezi na kugharamia jeneza la kumhifadhia marehemu pamoja na usafiri wa kusafirisha mwili wa marehemu, familia, ndugu na jamaa wa Sperius kutoka Kibeta kwenda Mubunda Kijiji Kitoko kwa ajili ya Mazishi. Aidha, Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kandege alitoa Shilingi Milioni mbili kwaniaba ya Serikali.

KAMATI YA LAAC YATEMBELEA MIRADI YA BARABARA MANISPAA YA MOROGORO

$
0
0
Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Mpinzile akitoa maelezo kuhusiana na mradi wa Barabara ya Maelewano iliyoko katika Manispaa ya Morogoro mbele ya Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC).kamati hiyo iko ziara Mkoani Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi ya maji na barabara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Vedasto Ngombale akizungumza na watendaji wa Manispaa ya Morogoro kabla ya Kamati hiyo kutembelea miradi ya Barabara katika Manispaa hiyo. kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Abdallah Chikota.

RAIS KARIA AIPONGEZA TWIGA STARS

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” kwa kurudi na Kombe la Ubingwa wa Jumuiya ya Africa Mashariki kutoka Burundi na kuwataka kudumisha nidhamu mpaka kwenye klabu zao.

Rais wa TFF Ndugu Karia amesema nidhamu ndio msingi wa mafanikio ambayo yanapatikana kwenye mashindano mbalimbali.

Amewataka kwenda na nidhamu hiyo mpaka kwenye ngazi ya klabu ambako wanarudi sasa baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa na waepukane na tabia hatarishi.

“Mafanikio mnayoyapata msingi wake ni nidhamu mliyonayo nashukuru sijawahi kusikia nidhamu mbaya katika timu hii,ni vyema pia mkajiepusha na tabia hatarishi” alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.

Wakati huohuo Rais wa TFF Ndugu Karia amesema Shirikisho litafanya mpango wa kutafuta mechi za kirafiki na mataifa yenye ushindani ili kuimarisha kikosi hicho cha Twiga Stars.

Amesema mechi hizo zitakuwa dhidi ya mataifa ambayo yamekuwa kikwazo kwa Tanzania.

Wachezaji wa kikosi cha Twiga Stars wameruhusiwa kurudi kwenye timu zao mpaka hapo watakapoitwa kwa maandalizi ya mechi mbalimbali.

MICHUZI TV: MIZENGO PINDA AFUNGUA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA UKONGA, ASEMA WAITARA ANATOSHA KWA JIMBO HILO

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda akizungumza kabla ya kumpandisha Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Ukonga , Mwita Waitara wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo hilo
 Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM, Mwita Waitara wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo.


Mbunge Mteule wa Chama Cha Mapinduzi anayegombea ubunge katika Jimbo la Ukonga , Mwita Waitara akiomba kura kwa wakazi wa jimbo hilo wakati wa uzinduzi wa kampeni za  uchaguzi mdogo katika Viwanja vya Kivule Shule.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

JAFO AAGIZA MKANDARASI WA JENGO LA HALMASHAURI YA PANGANI AONDOLEWE

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameagiza kuondolewa kwa Mkandarasi anayejenga Ofisi za halmashauri ya wilaya ya Pangani kutokana na kushindwa kukamilisha Ujenzi huo kama mkataba unavyoelekeza. Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya leo wilayani humo.

Mkandarasi huyo alianza kazi hiyo Novemba 2017 na alipaswa kukamilisha kazi hiyo juni 2018 lakini alishindwa kukamilisha na halmashauri kumuongezea muda hadi Agosti 31, mwaka huu.  Licha ya kuongezwa Waziri Jafo amekuta hakuna chochote cha maana kilichofanyika na hivyo kuagiza kuondolewa kwa Mkandarasi huyo ili kumpata mtu makini wa kukamilisha kazi hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu amethibitisha kwamba Mkandarasi huyo hana uwezo kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akikagua mradi huo na kutoa maelekezo lakini Mkandarasi huyo ameshindwa kutimiza wajibu wake. 

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ametembelea miradi mingine na na kukasirishwa na utekelezaji ubovu wa mradi wa Ujenzi wa madarasa na mabweni kwa shule ya sekondari Tongani ambao ulipatiwa Sh.Milioni 259 mwaka jana na serikali lakini mradi huo hadi sasa haujakamilika. Kufuatia hali hiyo, 

Waziri Jafo ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza wote waliohusika na kuwafikisha katika vyombo vya Dola. Hata hivyo Jafo amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuanza kuchukua hatua za uchunguzi juu ya watu waliohujumu mradi huo. Aidha, waziri Jafo amewataka wananchi wa wilaya hiyo kumuunga mkono Mbunge wao Jumaa Aweso kwa kuwa amekuwa akipigania upatikanaji wa miradi ya maendeleo kwenye jimbo hilo.

Kadhalika, amewataka wananchi wa Mwela pamoja na Mkaramo kushikamana na serikali ili kukamilisha ujezi wa vituo vya afya vilivyopata sh. milioni 400 kila kimoja kutoka serikali kuu.
Zoezi la ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika kituo cha afya Mwela
Wanafunzi wa shule ya sekondari Tongani wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea shuleni hapo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi na watendaji wa wilaya ya Pangani katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

KONGAMANO LA VIJANA NA WAZAZI KUFANYIKA DESEMBA 14 - 15, 2018 JIJINI DAR

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha atembelea Mazoezi ya timu ya Taekwondo Polisi Arusha

$
0
0
Wachezaji wa Taekwondo Polisi Arusha wakimuonesha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'anzi moja kati ya show ya Mchezo huo.

Na Gasto Kwirini wa Polisi Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi leo ametembelea mazoezi ya Timu  ya Taekwondo ya Polisi Mkoa wa Arusha yanayofanyika kila siku iioni katika Dojo lilipo Kambi ya Polisi New Line Arusha. 

Alipata fursa ya kuona sehemu ya Mazoezi (Gym), Onesho (Show) ya Taekwondo pamoja na changamoto zilizopo katika Timu hiyo. Aidha amewapongeza wachezaji wa timu hiyo walioshiriki katika Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (EAPCCO) yaliyofanyika  Mkoani Dar es Salaam na kupata Medali mbili ya Shaba na Fedha. 

‘‘Leo nimehamasika kuungana na mazoezi haya hasa kwa kuzingatia yanatija katika kazi yetu, Kwa sababu lengo la mchezo huu ni kujenga ukakamavu na kujilinda binafsi. Kuanzia wiki ijayo nitajumuika nanyi, mwisho wa siku na mimi nivae mikanda kama yenu’’. Amesema Kamanda Ng’anzi.

Pamoja na mambo mengine amehaidi kuzifanyia kazi changamoto walizo nazo hasa la vifaa na muda wa Mazoezi kuingiliana na Ratiba za kazi. Alisema atakaa na viongozi  wenzake kuona jinsi ya kutatua changamoto hizo.

Awali akitoa historia fupi ya Timu, Kocha wa Timu hiyo Shija Makoye alisema timu hiyo inahusisha jumla ya wachezaji kumi na tano (15) ambapo wanapata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za kujijengea ukakamavu na uwezo binafsi wa kujilinda pindi wanapokabiliana na Adui. Pia  alimweleza changamoto mbalimbali ambazo timu hiyo inakumbana nazo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akijaribu moja kati ya vifaa vya mazoezi vilivyo katika GYM ya Polisi Arusha. Kushoto kwake ni Kocha wa Timu hiyo Shija Makoye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akisisitiza jambo wakati akiongea na Wachezaji hao.
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images