Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

CHANGAMOTO YA KUPUNGUA KWA MAJI MTO MARA KUPATIWA UFUMBUZI

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amewakumbusha watendaji wa Wilaya ya Serengeti wajibu wao wa kipekee wa ulinzi katika hifadhi ya mbuga ya Serengeti kwakuwa Wilaya yao imebeba jina linalojulikana duniani kote ikiwa ni pamoja na eneo maalumu la wanyama aina ya Nyumbu ambao huvuka kwenda upande wa pili na kuwa miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo Wilayani Serengeti mara baada ya kufanya ziara ya kikazi Wilayani hapo kujionea uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira na kutembelea eneo la mto Mara eneo ambalo ni muhimu sana ki-ikolojia.

Katika kikao na viongozi wa Wilaya hiyo, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Bw. Wiliam Mwakilema aliainisha kuwa mtiririko wa maji katika Mto Mara kutoka chanzo chake kikuu katika Milima ya Mau nchini Kenya kimepungua kutokana na shughuli za kibinadamu na matumizi mengine yasiyoendelevu jambo linalohatarisha kupungua kwa mtiririko wa maji katika Mto Mara kwa kipindi kirefu, eneo ambalo ni kivutio pekee cha wanyama wanaohama dunia.

Katika kutatua tatizo hilo Waziri Makamba amesema kuwa masuala ya mazingira ni mtambuka hivyo Ofisi yake yenye dhamana na kusimamia hifadhi ya Mazingira nchini itafanya ziara ya kikazi nchini Kenya kwa lengo la kujadiliana na kupata ufumbuzi wa haraka juu ya jambo hilo.

“Sisi na wenzetu wa Kenya tumeingia mkataba mwaka 2013 wa matumizi sahihi ya rasilimali katika Mto Mara na kutunza ikolojia yake, kwa kushirikiana na Mawaziri wenzangu wa Maji na Maliasili na Utalii, tutafanya ziara nchini Kenya ili kwapamoja tupate ufumbuzi wa jambo hili ikiwa ni pamoja na Ziwa Chala, Ziwa Jipe na Ziwa Natroni ambayo yote yako pande mbili yaani Tanzania na Kenya.”

Waziri Makamba amesema Serikali itahakikisha maslahi ya Nchi yanalindwa kwa njia za ki-diplomasia na kuhakikisha Mto Mara unatiririsha maji kipindi chote cha mwaka. Waziri Makamba amehitisha ziara yake Mkoani Mara na amewasili Mkoani Arusha ambapo atakuwa na vikao wa wadau wa hoteli mbalimbali na kambi za uwindaji kwa lengo la kuweka mikakati ya kuhifadhi mazingira maeneo ya mbugani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akiwa amesimama pemebezoni mwa Mto Mara eneo la ‘Kogatendo’ na kupata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Serengeti Bw. William Mwakilema juu ya kupungua kwa maji katika Mto huo. Waziri Makamba ameahidi kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo mapema iwezekanavyo.
Bw. William Mwakilema (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba mara baada ya kutembelea Mto Mara eneo maalumu ambalo wanyama aina ya nyumbu huvuka kwa makundi na kuwa kivutio kikubwa cha utalii.
Eneo la Kogatendo katika Mto Mara ni miongoni mwa maeneo ambayo wanyama aina ya nyumbu huvuka kwa makundi na kuwa kivutio cha utalii. Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira January Makamba ametembelea eneo hilo ili kuhakikisha hatua zinachukuliwa kurejesha ikolojia ya mto huo katika hali ya awali.

BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, Mkoani humo.

Ujenzi unaondelea wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa Km 49.7 kwa kiwango cha lami unatarajiwa kufungua mkoa wa Simiyu na mikoa jirani ya Mara, Mwanza na Shinyanga hivyo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe mkoani Simiyu wakati akikagua barabara hiyo inayojengwa na mkandarasi wa kampuni ya CHICO na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo toka ulipoanza mwezi Oktoba mwaka 2017.

"Nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa na nina imani mkandarasi atamaliza mapema mradi huu",amesisitiza Waziri Kamwelwe. Aidha, ameupongeza uongozi wa mkoa huo na Wakala wa Barabara (TANROADS), kwa kusimamia mradi huo usiku na mchana na kuwataka kutoa taarifa muda wowote endapo kutakuwa na changamoto zinazoweza kukwamisha mradi huo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent, akimuoesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, nyumba za Mhandisi Mshauri zilizojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya CHICO katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.

Akizungumzia kuhusu Kiwanja cha Ndege cha Simiyu, Mhandisi Kamwelwe amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa hatua za awali zinaendelea katika kuhakikisha kiwanja hicho kinajengwa ili kufungua mkoa huo katika sekta za usafirishaji na uwekezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ameishukuru Serikali kwa kujenga kipande cha barabara hiyo baada ya ile ya Mwigumbi-Maswa kukamilika kwa kiwango cha lami kwa kuwa imekua ni kichocheo cha kuunganisha nchi yetu na nchi za maziwa makuu ambazo ni Uganda, Burundi, Rwanda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakikagua kokoto zitakazotumika katika ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, Mkoani humo.

Naye, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent amemueleza Waziri huyo kuwa mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 20 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka 2019.

Mhandisi Kent ameongeza kuwa kazi zilizofanyika mpaka sasa ni mkandarasi kuanza ujenzi wa madaraja makubwa mawili ya Banhaya na Simiyu na ameshamaliza kujenga madaraja madogo 9 kati ya 12 na makalvati 36 kati ya 58.

Mradi wa Maswa-Bariadi unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 86. Kukamilika kwa mradi huo kutakamilisha ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa- Bariadi-Lamadi yanye jumla ya urefu wa KM 171.8.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akioneshwa na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent, kazi zinazoendelea katika ujenzi wa daraja la mto Simyu, wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, Mkoani humo.
Muonekano wa kazi za ujenzi zikiendelea kwenye daraja la mto Simiyu katika barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7, Mkoani Simiyu.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA CHINA JIJINI BEIJING

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China, wakati akizungumza nao leo jijini Beijing ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli, katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania waliopo nchini China kuhudhudhulia Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China,mara baada ya kuzungumza nao leo jijini Beijing ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili. Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli, katika mkutano huo.
Balozi wa Tanzani chini China, Mbelwa Kairuki akimtambulisha mmoja wa wafanyabiashara wa China kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumza nao leo jijini Beijing, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping kesho jumatatu Septemba 3, 2018 ambapo utafanyika kwa siku mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Godfrey Mwambe akibadilishana kadi na baadhi ya Wafanyabiashara wa nchini China.

WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME

0
0
 Profesa Marjorie Mbilinyi akizungumzia simulizi ya hadithi yake  Jijini Dar es Salam katika viwanja vya ofisi ya TGNP mtandao  jinsi alivyofanikiwa  kupambana kupiga vita mfumo dume usimtawale katika kutimiza ndoto zake.
 rofesa Ruth Meena kushoto akimsikiliza kwa makini profesa Marjorie Mbilinyi  Jijini Dar es salaam wakati wa kusimulia hadithi ya harakati za mapambano ya kujikwamua kuondokana mfumo dume.
Profesa Ruth Meena akiwa  anawasimulia hadithi  Wanafunzi wa vyuo vikuu  Mbali mbali na wageni waalikwa  Jijini Dar es Salaam namna alivyokuwa mwanaharakati wa kukataa kudidimizwa  katika kujikwamua Kama mwanamke katika kujiendeleza  kimasomo  huku akiwa na majukumu ya kuangalia familia,pamoja na kufanya kazi.

Na Agness Francis,blogu ya jamii.
KATIKA harakati za ukombozi wa mwanawake,wanawake wametakiwa kuwa kipaumbele katika kuondokana na mfumo dume uliotawala katika jami yetu.

Ambapo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuukataa  na kupiga vita ukatili wa kijinsia,utabaka pamoja na ubeberu uliokithiri hasa kwa zile familia ambazo bado zinadhana  potofu ya kumdidimiza mwanamke katika kupata Elimu na uongozi.

Amesema hayo  Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TGNP mtandao  Profesa  Marjorie Mbilinyi  wakati wa kilinge cha simulizi za hadithi za maisha yake alivyopambana mpaka hapo alipofikia pamoja na misuko suko yote aliyopitia akipindi akiwa binti mdogo lakini alihakikisha anaepukana na janga la kukandamizwa Kama mwanamke.

Profesa mbili ambaye ni mwanaharakati wa mabadiliko ya  ukombozi wa mwanamke kimapinduzi  wakati wa simulizi amesema kuwa hakuna utofauti sana wa ubaguzi huo hapa nchini kwetu na ulaya.

"Isipokuwa  wanawake wa nchi za nje wamepiga hatua katika kujikomboa kuondokana na utabaka,ubepari,hivyo na sisi tujifunze kutoka kwao" amesema Profesa Mbilinyi.

Aidha mwanaharakati profesa Ruth Meena wakati wa simulizi wa hadithi yake amesisitiza kuwa  wanawake wapige vikali vita ya  mfumo huo wa unyonywaji na amewataka kusimama imara  kupigania maendeleo na kutimiza ndoto zao.

Hata hivyo mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mlimani  Sliyvia Sostenes baada ya  simulizi hiyo amesema kuwa watakuwa mabalozi wazuri katika kuwaelemisha wengine ambao wapo katika janga hilo ili kuleta ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.

JWTZ laahimisha miaka 54 tangu kuanzishwa kwake

0
0
JESHI la Wananchi wa Tanzania JWTZ Leo limeadhimisha miaka 54  tangu kuanzishwa kwake.

Maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dar es salaam chini ya Mkuu wa Majeshi Generali Venance Mabeyo akiwa na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, kwa kufanya usafi katika eneo la kambi ya Jeshi Lugola na  baadaye kufuatiwa na michezo iliyofanyika katika eneo la Uwanja wa Jeshi mwenge vinyago .

Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amelipongeza Jeshi hilo kwa kudumisha usafi na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuiga mfano wa Jeshihilo kutumia mazingira kwa usafi na kupanda miti katika maeneoyao.

Aidha Makonda ameelezeakusikitishwa kwake na kitendo cha mgambo wanaosimamia usafi katika jijini la Dar es salaam kwenda kinyume cha sheria katika kusimamia zoezi hilo kwakupiga wananchi na kusema kuwa hajawatuma kufanya hayo  na ametoa amri wakamatwe .

''Sheria zipo hakuna hata mmoja inayosema adhabu ya kukutwa na uchafu ni kupigwa bali sheria imeongelea faini, nimeagiza tangu jana walihusika na hilo tukio wakamatwe na hatua za sheria zichukuliwe dhidi yao" alisema. 

Kwa upande wake mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wanajeshi kudhibiti usalama wa kambi  kwa kutoruhusu raia kukatisha  katika maeneo ya Jeshi  na kuahidi kujenga ukuta katika eneo la jeshi kambi ya Lugalo na  Mwenge na kuhiza usafi kuwa endelevu.
 Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Tanzania jenerali,Venance Mabeyo akizungumza viongozi mbalimbali pamoja na wanajeshi la JWTZ  katika maazimisho ya miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.
 Mbwa wa jeshi akimdhibiti adui.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

K-VANT WAJA NA MUONEKANO MPYA NA LADHA YAKE HALISI YA SIKU ZOTE

0
0
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Mega Beverage Company Limited,ya mkoani Arusha, inayotengeneza pombe kali chapa maarufu ya K Vant, imezindua chupa mpya za kinywaji cha K-Vant zenye mwonekano tofauti na chupa za awali.Mabadiliko hayo hayakubadilisha ladha halisi ya kinywaji hicho na wateja wake wataendelea kuifuahia ikiwa katika ladha yake halisi ya siku zote.

Lengo kubwa la kubadilisha chupa za pombe ya K-Vant, ni mkakati wa kampuni wa kupanua masoko yake ya ndani na nje ambapo imelenga kuwa katika mwonekano bora zaidi bila kuathiri ladha halisi ya kinywaji hicho ambayo inapendwa na watumiaji wengi wa pombe kali nchini na nje ya mipaka ya Tanzania

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh.Antony Mavunde.

Mh.Mavunde,alipongeza hatua ya kampuni kubuni mkakati wa kuongea soko la bidhaa na kuongeza kuwa masoko yakiongezeka ndivyo mapato ya serikali yanaongezeka kupitia kulipa kodi sambamba na kuongeza wigo wa ajira kutokana na kuhitajika nguvu kazi zaidi.

“Serikali ya awamu ya tano inao mkakati wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda,tutazidi kuboresha mazingira zaidi kwa wawekezaji katika sekta hii ili lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hii lifanikiwe haraka sambamba na kupunguza changamoto ya tatizo la ajira kwa vijana “,alisema.

Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Beverage Company Limited, Marco Maduhu alisema, “Kauli mbiu yetu ya kinywaji cha K-Vant katika mwonekano mpya ni ’Ni Halali Yako’ kampuni imejipanga kuimarisha usambazaji wa bidhaa ya pombe ya K-Vant katika sehemu zote nchini ili watanzania waendelee kufurahia ubora wake kikiwa katika mwonekano wa chupa mpya na katika ladha ileile waliyoizoe kuipata siku zote”.

Alisema uzinduzi wa chupa mpya za K-Vant mbali na kufanyika katika mkoa wa Dar es Salaam pia utafanyika katika mikoa ya Arusha na Mwanza, pia usambazaji wa kinywaji hiki kwenye mwonekano mpya katika ladha yake halisi utaendelea kufanyika katika mikoa yote nchini kuanzia sasa.”Wateja wetu wowote popote mlipo tunawashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono nasi tutaendelea kuboresha huduma zetu za usambazaji na kuhakikisha kinywaji bora cha K-Vant kinawafikia popote mlipo kikiwa katika chupa mpya”alisisitiza

Maduhu, alioongeza kusema kuwa, kampuni ya Mega Beverage,itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo kupitia uwekezaji wake itahakikisha inaendelea kuchangia pato la taifa kupitia kulipia kodi mbalimbali, kunufaisha watanzania wengi kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, pia imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye jamii.Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (wa pili kulia) akionyeshwa na Meneja mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mega Beverages, Marco Maduhu, Chupa mpya ya K-Vant wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji cha K-Vant uliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Francis Kimaro.
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Mega Beverages, wazalishaji wa Kinywaji cha K-Vant ,Francis Kimaro(kushoto) na Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni hiyo ,Marco Maduhu, wakigongeana glasi ya K-VANT.
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Mega Beverages wakati wa uzinduzi huo.

UNLOCK CASTLE LITE YAZIDI KUWAPA RAHA WAKAZI WA JIJI LA DAR

0
0
ILE promosheni ya kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Castle Lite kwa lengo la kuwapatia burudani inayojulikana kama Unlock Castle Lite inazidi kusambaza furaha kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo mwishoni mwa wiki ilikuwa kata mti panda mti ndani ya baa ya 5N iliyopo maeneo ya Sinza.

Lengo kubwa la promosheni hiyo ni Kutangaza chapa na kuwashukuru wateja kwa kuendelea kufurahia EXTRA COLD CASTLE LITE!.

Tofauti na promosheni zilizozoeleka, promosheni hii imesheheni kila aina ya burudani ambapo inaweza kuwakutanisha ndugu, jamaa na marafiki pamoja na kupiga picha mbalimbali huku wakifurahia kinywaji bia ya Castle Lite wakiwemo wafanyakazi wa TBL ambao kwa sasa wameamua kutokana ofisini na kujumuika na wateja wao.

Unlock Castle Lite, ambayo inafanyika katika siku za Alhamisi na Ijumaa baada ya saa za kazi pia inawashirikisha wafanyakazi wa kampuni ya TBL ambao wanajumika pamoja na wateja na kuwapatia zawadi mbalimbali za promosheni. Tayari wakazi wa Kawe, Boko na Tegeta, Sinza,wamefikiwa na Unlock Castle Lite.
 Burudani za furaha ya Castle Lite zikiendelea
  Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakiwa na wateja waliojumuika pamoja katika burudani za furaha ya Castle Lite.
Furaha ya Castle Lite ilipamba kila mahali katika kiwanja cha maraha cha 5N kilichopo jijini Dar es Salaam.

LUGOLA AKERWA MGAMBO KUMPIGA KIKATILI MWANANCHI JIJINI DAR ES SALAAM, ATOA ONYO KALI KWA WATU WANAOCHUKUA SHERIA MKONONI

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelaani tukio lililofanywa na Mgambo wa Jiji la Dar es salaam akisema ni la kihuni, kishenzi na kinyama na halipaswi kufumbiwa macho na wapenda amani, watetezi wa haki za binadamu na wananchi wote kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Lugola alisema Serikali inalaani vikali tukio hilo ambalo lililotokea wiki iliyopita jijini humo, na kutokana na unyama huo tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa.
“Jeshi la Polisi tayari limewakamata wahusika kama Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni tarehe 31 Agosti, 2018 ilivyoeleza. Natumia fursa hii kuwakumbusha tena Mgambo wote kuwa makini katika utekelezaji wa maagizo wanayopewa na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu,” alisema Lugola.
Pia kutokana na tukio hilo, Lugola alisema anazitaka Mamlaka za Majiji, Manispaa na Halmashauri kufikiria kuanzisha Huduma ya Polisi Wasaidizi (Auxiliary Police) katika maeneo yao kwa mujibu wa Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322 ili kuepuka matukio ya uvunjifu wa haki za Binadamu kama tukio la Mgambo watatu  jinsi lilivyo tokea.
Aidha, Lugola pia alizungumzia kuhusu baadhi ya matukio mengine ambayo watu  wanajichukulia Sheria mkononi na kuwaadhibu kwa kuwapiga watu wengine kwa sababu mbalimbali.
Aliyataja matukio hayo ni pamoja na ugomvi wa kifamilia ndani ya ndoa ambao huhusisha Wanaume kuwapiga wake zao au wake kuwapiga waume zao, pia  wananchi kuwapiga watu wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali, pamoja na walimu kuwapiga wanafunzi kinyume cha sheria.
Pia Lugola aliwaonya baadhi ya Askari Polisi ambao wanatumia nguvu isiyo ya kadiri kulingana na mazingira halisi wanapowadhibiti watuhumiwa.
“Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalaani vikali matukio ya kujichukulia Sheria mkononi na kupitia kwenu Wanahabari nawataka Watanzania kufuata sheria za nchi kwa kuacha vitendo vya kujichukulia Sheria mkononi. Vitendo hivi pamoja na kusababisha uvunjifu wa amani vinaweza kuleta madhara kwa watu ambao hawana makosa na kuichonganisha Serikali na wananchi wake,” alisema Lugola.
Kutokana na matukio hayo, Lugola aliwataka wanandoa wanakumbushwa kutumia Dawati la Jinsia katika Vituo vya Polisi kote nchini ili kuwasilisha malalamiko yao ya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya ndoa ili hatua stahiki zichukuliwe.
Pia aliwataka wananchi waendelee kuheshimu sheria za nchi na kuepuka kujichukulia unakuta mtu anapigwa hata haulizi anayepigwa amekosa nini nae anajiunga nao na kumpiga hali ambayo imesababisha majeraha, vilema vya kudumu na vifo kwa watu wasio na hatia.
Hata hivyo, Lugola aliwaonya walimu kwa kufanya matukio kujirudia kwa kuwaadhibu wanafunzi kwa kuwachapa na kuwapiga hovyo kiasi cha kusababisha maumivu makali, ulemavu na vifo.
“Natumia fursa hii kuwakumbusha Walimu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya Adhabu kwa wanafunzi ambayo imetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuepuka madhara yake, kuondoa hofu kwa wazazi na kufanya shule zetu kuwa mahali salama kwa watoto wetu,” alisema Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Mwanza leo. Katika hotuba yake kwa waandishi hao, Lugola alilaani tukio la askari mgambo wa Jiji la Dar es Salaam kwa kumpiga kikatili mwananchi eneo la Bunju, wilayani Kinondoni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

JUMLA YA WAHAMIAJI HARAMU 647 WAMEKAMATWA MKOANI PWANI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
IDARA ya Uhamiaji, Mkoani Pwani imesema, jumla ya wahamiaji haramu 647 wamekamatwa kwa kuingia nchini kinyume na sheria, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Aidha idara hiyo imetaja sababu kubwa inayosababisha wahamiaji hao, hasa wale wa nchi jirani kuingia nchini ni kutaka kutumia rasilimali za nchi na kupita kuelekea Afrika ya Kusini kutafuta maisha. 
Ofisa uhamiaji mkoa wa Pwani Naibu kamishna wa uhamiaji Plasid Mazengo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari,ofisini kwake. Alieleza ,kipindi cha mwaka 2016 walikamatwa wahamiaji haramu 362,mwaka 2017 walikamatwa 194 na Januari hadi Juni mwaka huu walikamatwa 91.
Mazengo alisema ,katika kipindi cha mwaka 2016 waliofukuzwa walikuwa 237,mwaka 2017 walifukuzwa 38 na Januari hadi Juni walifukuzwa 30 jumla 305.
"Mwaka 2016 waliofikishwa mahakamani walikuwa 162 mwaka 2017 waliofikishwa mahakamani walikuwa 194 na Januari hadi Juni mwaka huu waliofikishwa mahakamani walikuwa 91".
Alibainisha ,wengi wanavutiwa na rasilimali zilizopo zikiwemo za uvuvi,maliasili na kilimo huku wengine wakiwa njiani kuelekea Kusini mwa Afrika kwa ajili ya kutafuta maisha hasa Wasomali na Waethiopia. 
Aidha Mazengo alibainisha, katika kipindi cha wiki mbili zilizopita walifanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 26 kwa tuhuma za kuingia nchini bila ya kibali.
Kwa mujibu wa Mazengo, kati ya waliokamatwa ni pamoja na Warundi wanane,Wasomali watatu,Waethiopia wanne, Wakongo wawili,Mnyarwanda mmoja na wengine ni wakimbizi watano wa familia moja waliokimbia kambini.
Idara hiyo inaendelea na taratibu za kuwachambua kila mmoja na kosa lake ili waweze kufikishwa mahakamani au kurudishwa nchini kwao,  kwani wapo wengine wanadai kuwa ni watanzania lakini hawana utambulisho  kuwa ni watanzania. Hata hivyo, siku chache zilizopita jeshi la polisi mkoani Pwani liliwapa salamu wale wanaojihusisha na biashara ya kuingiza nchini wahamiaji haramu. 

Lilisema endapo atakamatwa mtu yeyote ama chombo cha usafiri kikiwasafirisha basi atachunguzwa na kutaifishwa mali zake ama kukitaifisha chombo hicho cha usafiri. 
Ofisa uhamiaji mkoa wa Pwani Naibu kamishna wa uhamiaji Plasid Mazengo akionesha baadhi ya wahamiaji haramu kutoka Ethiopia waliokamatwa hivi karibuni.

Vanesa Mdee atumia mitandao ya jamii kushawishi kampuni ya Zola Tanzania kufunga umeme wa solar Arusha Girls

0
0
Na Ibrahim othman Jama, Arusha.

Msanii Vanessa Bdee amefanikiwa tumia mitandao ya kijamii katika shughuli zake kuhakikisha kuwa anamtafuta mfadhili wa kusambaza umeme wa solar power kwa shule ya bweni ya Arusha Girls iliyopo wilaya ya Arusha mjini. Tayari kampuni ya Zola Tanzania imefunga umeme wa solar shuleni hapo kwa guarantee ya miaka mitano. 

"Shukran za kipekee zimfikie Mkuu wa wilaya ya arusha mjini Mhe. Gabriel Daqaro pamoja na katibu tawala wilaya ya Arusha mjini ndugu David Mwakiposa kwa kusaidi kufanikisha hili.

"Tunamshkuru Mungu kwa hili na pia niwashukuru uongozi wa shule, afisa elimu wilaya na msanii vanessa mdee, kampuni ya zola ofisi ya mkurugenzi pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kuniamini kuratibu shughuli hii katika wilaya yetu na kuwa kiunganishi katika hili mpaka kuweza kutimiza jambo hili la kheri" amesema mratibu wa Zola Tanzania
Msanii Vanessa Mdee akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqaro pamoja na katibu tawala wilaya ya Arusha mjini ndugu David Mwakiposa na mwakilishi wa Zola Tanzania kuelekea kwenye mabweni ya shule ya sekondari ya Arusha Girls kuzindua mradi wa umeme wa Solar 
Msanii Vanessa Mdee akiongozana na Mkuu wa wilaya ya arusha mjini Mhe. Gabriel Daqaro wakijiandaa kukata utepe wakishuhudiwa na katibu tawala wilaya ya Arusha mjini ndugu David Mwakiposa na wawakilishi wa kampuni ya Zola Tanzania kwenye moja ya mabweni ya shule ya sekondari ya Arusha Girls wakati wa kuzindua mradi wa umeme wa Solar shuleni hapo.

MADHIMISHO YA MIAKA 54 YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA PAMOJA NA MIAKA 42 YA CHUO CHA KIJESHI(TMA)MONDULI

0
0
Madhimisho ya miaka 54 ya jeshi la wananchi na Miaka 42 ya chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) yaliadhimishwa Jumamosi  katika uwanja wa Bomani na kuongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta na Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi monduli Brigedia Jenerali Stephen Justice Mnkande. 
Mkuu wa wilaya Monduli na Brigedia jenerali Mnkande waliongoza mamia ya askari na Raia katika matembezi ya miguu kilomita nne katika mji wa Monduli  wakiwa  na brass band ya  jeshi.
Katika kuadhimisha Siku hiyo muhimu kwa jeshi la wananchi wa Tanzania waliadhimisha kwa kufanya michezo mbalimbali kama Mpira wa miguu,Netiboli,Kuvuta kamba na Mchezo wa kukimbiza kuku.
Mkuu wa wilaya akiongea amelishukuru Jeshi hilo kwa ushirikiano mkubwa wa mara kwa mara katika kujitolea katika shughuli za kijamii na kudumisha umoja wao kwani wanajeshi Monduli na raia ni wamoja.

 Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.  Idd Hassan Kimanta na Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi monduli Brigedia Jenerali Stephen Justice Mnkande wakiongoza mamia ya askari na raia katika matembezi ya miguu kilomita nne katika mji wa Monduli Jumamosi Agosti 2, 2018
  Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta na Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi monduli Brigedia Jenerali Stephen Justice Mnkande wakiongoza mamia ya askari na raia katika matembezi ya miguu kilomita nne katika mji wa Monduli 
  Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.  Idd Hassan Kimanta na Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi monduli Brigedia Jenerali Stephen Justice Mnkande wakiongoza mamia ya askari na raia katika mazoezi ya viungo baada ya matembezi ya miguu kilomita nne katika mji wa Monduli 
  Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.  Idd Hassan Kimanta akihutubia mamia ya askari na raia baada ya matembezi ya miguu kilomita nne katika mji wa Monduli 
 Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi monduli Brigedia Jenerali Stephen Justice Mnkande akiongea na mamia ya askari na raia baada ya matembezi ya miguu kilomita nne katika mji wa Monduli 
 Sehemu ya mamia ya askari na raia baada ya matembezi ya miguu kilomita nne katika mji wa Monduli 

Taasisi ya The Desk & Chair Foundation yatoa msaada wa madawati 60 na miche 630 ya miti kwa Shule ya Msingi Mabatini A wilayani Nyamagana, Mwanza

0
0
 Mwenyekiti wa The Desk & Chair Sibtain Megjee akizungumza na walimu (hawapo pichani) pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini A iliyopo Wilaya ya Nyamagana kabla ya kuwakabidhi msaada wa madawati 60 na miche 630 ya miti jana. Msaada huo umetolewa na taasisi hiyo ikishirikiana na Welfare Aid International ya Australia.

Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee amkimpa mkono Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mabatini A Bryson Kamonge ikiwa ni ishara ya kumkabidhi madawati 60 yalitolewa na taasisi hiyo ikishirikiana na Welfare Aid International ya Australia jana.
Na Baltazar Mashaka

  Mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi madawati na miche ya miti kwa Shule ya Msingi Mabatini A katika Wilaya ya Nyamagana Dk. Swalehe Maulid akimkabidhi miche ya miti Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bryson Kamonge (katikati).
Mmoja wa wafadhili wa visima vya maji Ali Hamdani akizungusha mkono wa pampu ya kuvuta maji kwenye kisima alichofadhili katika Kijiji cha Ikengele wilayani Magu. Anayeshuhudia kushoto ni Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee.

MISS TANZANIA WAPEWA UBALOZI WA KUHIMIZA UHIFADHI WA MISITU NA UTALII WA NDANI

HABARI ZA UN: Kijana Abdul wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ajivunia hatua zilizopigwa visiwani humo

WAITARA - MIMI SIO MSALITI NIMEFUATA MAENDELEO YA JPM

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mgombe Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwita Waitara  amesema yeye sio Msaliti bali amechagua CCM  ili aweze kumalizia alipoishia hususani swala la barabara , Umeme na Maji katika jimbo  hilo. Waitara amesema hayo leo katika Mkutano wake wa Kampuni uliofanyika katika Kata ya kitunda.
"Naomba niwaeleze ukweli kuwa nilikuwa natumia nguvu sana  katika kufanikisha mambo ya Maendeleo yenu huku  kutokana na sehemu niliyokuwa hivyo sasa nimehamia  huku na  kila kitu sasa ni mtelezo" alisema Waitara
Alisema kuwa alikuwa anapigwa marufuku kuongea na viongozi wa CCM lakini hao ndio wenye  mafungu ya Pesa na serikali jambo amblo mie nilikuwa kinyume nao kiasi cha kuanza kuniita Mimi Msaliti. Alisema kuwa hajaanza kuitwa msaliti leo  kwani walimuita msaliti tangu  alivyokuwa ya kuwasaidia   na kuwaletea maendeleo watu ambao  wamemwamini hili wapige hatua katika shughuli Zai za kila siku.
Alisema kuwa kwa  sasa unaweza kuzungumza na Waziri moja Kwa moja natayari Waziri wa Nishati  amemuakikishia kuwa Wakazi wote wa eneo hilo watapata  Umeme Kwa gharama za Rea.
Alisema kuwa katika swala la  barabara  na Maji tayari linqpatiwa ufumbuzi chini ya Serikali ya Chama Cha Mapunduzi.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Juu ya CCM  Livingstone Lusinde aliwataka watu wa ukonga wasifanye makosa kwani sasa wanachqgua Mbunge wa  jimbo atakayefanya kazi na serikali na sio uchaguzi Mkuu.
Alisema CCM peke yake ndio inatekeleza ilani Kwa kupewa dhamana ya kuongoza dola hivyo wakichahua mgombea kutoka vyama vingine watakuwa wamejitafutia matatizo wenyewe 
 Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara akizungumza Wakazi wa Kata ya Kitunda katika moja ya Mikutano yake ya Kampeni
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akimwaga sera za CCM Namna gani Ilanai inatekelezwa kwa Wakazi wa Kitunda wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo Jimbo la Ukonga
 Mbunge wa Jimbo la Segerea , Bonnaha Kaluwa akizungumza na wakazi wa kitunda kuwataka wadumishe ujirani kw akumchagua Waitara wa CCM
 Mbunge wa Ilala , Mussa Hazzan Zungu akizungumza na Wakazi wa Kitunda na kuwaomba wamchague waitara kwa kuwa ni Msikivu .
 Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia akiwambaia wakazi wa Kitunda Jimbo la Ukonga kuwa kuhama kwa Waitara sio shida kwnai akuanza yeye kutaka kufata Maendeleo yaliyopo CCM
 Mbunge wa Ilala , Mussa Hazzan Zungu Akiserebuka na wkaazi wa kitunda kabla ya kupanda jukwaani .
 Wabunge waliohudhuria Mkutano huo wakisakata rumba linalopigwa na Bendi ya TOT PLUS
  Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara  Akicheza Ngoma ya Litungu kutoka Mkoani Mara
 Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa Tiketi ya CCM Mwita Waitara  akiagana na wapiga kura waliojitokeza katika Mkutano huo.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO CHINA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio nchini China Kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 2, 2018. Pichani kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini China,Mh Mbelwa Kairuki.
Baadhi ya Watanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies Naima Mohamed Kiluwa,alipozungumza na Watanzania waishio China wakiwemo na wageni waalikwa kutoka Tanzania kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China Septemba 2, 2018. Pichani kati ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies Mohamed Kiluwa na kulia ni Mfanyabiashara maarufu kutoka Tanzania,Mh John Cheyo wakiwa sehemu ya wageni waalikwa kutoka nchini Tanzania.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China, Septemba 2, 2018. Kushoto ni Waziri wa Madini, Angela Kairuki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mke wa Balozi wa Tanzania nchini China na Waziri wa Madini, Angela Kairuki wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing China kuzungumza na Watanzania, Septemba 2, 2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio nchini China baada ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China Septemba 2, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki. 

INTRODUCING "IOKOTE" by Maua Sama Ft. new kid on the block Hassan Banza Stone

MAGAZETINI LEO

Vodacom yatoa gari la Tisa la M-Pesa jijini Tanga katika sherehe ya kufana

0
0
  Mkuu wa kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen (kushoto) akikabidhi kadi ya gari kwa mkazi wa Tanga Adolf Mlay, huku mkewe Amina Urssa akishuhudia, hafla hiyo ya kusherehekea miaka 10 ya M-Pesa ilifanyika katika viwanja vya Commercial jijini Tanga, ili kushinda Mteja anatakiwa kufanya miamala mingi Zaidi na kutumia M-Pesa ili kujikusanyia points na kuongeza wigo wa kushinda.
  Mshindi wa gari ya tisa ya M-Pesa kutoka Tanga Adolf Mlay (wa pili kushoto) na wake wakionesha kadi ya gari wakati wa hafla ya kukabidhiwa gari katika viwanja vya Commercial jijini Tanga
Mshindi wa gari ya tisa ya M-Pesa kutoka Tanga Adolf Mlayakiingia kwenye gari lake mara baada ya kukabidhiwa na kampuni ya simu ya Vodacomkatika viwanja vya Commercial jijini Tanga
Mshindi wa gari ya tisa ya M-Pesa kutoka Tanga Adolf Mlay (wa pili kushoto) akiwa na familia yake wakati wa hafla ya kukabidhiwa gari katika viwanja vya Commercial jijini Tanga

GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameendelea na  ziara yake jimboni humo katika kukagua na kuangalia namna miradi ya  maendeleo  inavyoendelea kutekelezwa  kunufaisha wana Manonga.

Katika ziara ziara yake Gulamali alitembelea kituo cha afya Simbo sambamba na kukagua ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya sekondari Mwisi ambako ameridhishwa namna miradi hiyo inavyotekelezwa na kuwataka wasimamizi kwenda na kasi na kufanya kazi zilizo bora zaidi.

Aidha Mbunge huyo alipata wasaa wa kukutana na kamati ya Zahanati ya  Nkinga, viongozi wa CCM na wadau wengine na kuona namna ukarabati wa miundombinu katika Zahanati ya Nkinga unavyoendelea. 

Gulamali  ameahidi kutoa kiasi cha shilingi 430,000 kwa ajili ya kuvuta maji ya Uhakika kwenye Zahanati ya Nkinga ili kupunguza adha kwa wananchi wa wauguzi katika mchakato mzima wa kutoa na kupokea huduma.

Pia ameahidi kuongeza vitanda viwili vya kujifungulia katika wodi ya wazazi na kueleza kuwa suala la afya hasa ya mama na mtoto lazima ipewe kipaupele.

Gulamali alihitimisha ziara yake kwa  kufanya kikao na wachezaji pamoja na viongozi wa timu  ya Manonga Queens ambayo iliibuka kidedea kwa kuichapa  Singida Worrier kwa goli mbili, na  amekabidhi mipira miwili na  kuahidi jezi na vifaa vya michezo ambavyo ameshaagiza kwa ajili ya timu hiyo itakayowakilisha mkoa mzima wa Tabora kwenye michuano ya soka daraja la kwanza Tanzania bara kwa timu za wanawake.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali (katikati) akizungumza na kamati ya Zahanati ya Nkinga mara baada ya kuwasili.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images