Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

DC CHATO AAGIZA SHULE ZOTE KULIMA PAMBA

$
0
0
Na Richard Bagolele – Chato 

Serikali Wilayani Chato imeziagiza shule zote kuanzia msimu ujao kuhakikisha zinalima zao la Pamba na Mtama kuanzia ekari mbili kwa kila shule. 

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon wakati akiongea na walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu wa elimu kata za Chato kwenye hafla fupi ya ugawaji wa pikipiki 23 zilizotolewa na serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi, na ufundi stadi hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato. 

“Tunahitaji shule na taasisi zote ni lazima muwe na ekari zisizopungua mbili za pamba na zinatakiwa kusimamiwa na wagani waliopo huko vijijini” amesisitiza Mkuu wa Wilaya. 

Mkuu wa Wilaya amesema fedha zitakazopatinaka kutokana na zao la pamba ziwe na lengo la kumnufaisha mwanafunzi kwa kuwaandalia chakula ili kumpunguzia mzigo mzazi ambao wamekuwa wakichangia huduma ya Chakula kwa wanafunzi. Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya amewataka waratibu wa elimu kata kuzitembelea shule zilizopo maeneo yao mara kwa mara na si kusubiri wakati wa mitihani tu kwani sasa wamepata usafiri. 

Mkuu wa Wilaya pia amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji kutenga bajeti kwa ajili ya kununua pikipiki za watendaji wa kata kwa awamu ili nao waweze kutimiza malengo yao sambamba na kuwafikia wananchi kilahisi. 
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon akiongwa na walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu wa elimu kata za Chato
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Semeon (kulia) akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mratibu elimu kata ya Bwanga Venance Bahati
3 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke akiongea na wakuu wa shule, walimu wakuu na waratibu elimu kata za Chato
Mkuu wa Wilaya ya Chato (katikati) akiwasha pikipiki kama ishara ya kukabidhi pikipiki hizo kwa waratibu wa elimu kata 23 za Wilaya ya Chato.


WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU

$
0
0
NEC – Dodoma.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini, Monduli na kwenye Kata 23 za Tanzania Bara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni wakati wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi huo mdogo jijini Dodoma.

Jaji Kaijage amewataka Wasimamizi hao  kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili wapunguze na kuondoa malalamiko yanayojitokeza wakati wa uchaguzi.

Amesema  Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

 “ Tunakutana hapa kwa muda wa siku tatu (3) ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi,” Amesema Jaji Kaijage.

Aidha, amewataka Wasimamizi hoa waepuke madhara yanayotokana na ukiukaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi  na akisisitiza kwamba katika kipindi hiki chaguzi  zinafanyika katika mazingira ambayo yana hamasa kubwa ya Kisiasa, kutoaminiana na wakati mwingine hutawaliwa na mihemko ambayo imekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

Jaji Kaijage amewaeleza Wasimamizi hao kwamba wameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo za usimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wajiamini na kujitambua.

Amaetoa wito kwa Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi na kuhakikisha kwamba wanawatumia vizuri wasaidizi walio nao katika maeneo yao kwa matokeo bora.

“Mjue mna jukumu la kuimarisha imani ya wananchi pamoja na wadau wote wa uchaguzi kwa Tume. Hivyo mfanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, bila kuegemea upande wowote. Kufanya kazi kwa uhuru na kwa uwazi kutasaidia kudumisha amani katika maeneo yenu ya Uchaguzi” Amesisitiza.

Kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi huo mdogo Septemba 16 mwaka huu,  Jaji Kaijage amesema kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura 292, ni jukumu la Tume kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi.

Amesema kwa nyakati tofauti Tume imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini na Monduli.

Pia amefafanua kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa, Sura, 292 alitoa taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 23 kutoka katika Halmashauri 15 zilizopo katika Mikoa 10 ya Tanzania Bara.

KAMPUNI YA SUKARI KILOMBERO SASA KUUZA PAKETI NDOGO ZA SUKARI, BEI NAFUU

$
0
0
 Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na wananchi wa Mbagala siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya 'Bwana Sukari' inayozalishwa na kiwanda hicho. Paketi hizo zitauzwa kwa shillingi 500/- na shillingi 1000/-.
 Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akimkabidhi paketi mpya za Bwana Sukari mkazi wa Mbagala Zena Athumani siku ya uzinduzi wa bidhaa hiyo uliofanyika viwanja vya Mabagala Zakeem hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Sukari ya Kilombero Sugar, Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari siku ya uzinduzi wa paketi ndogo za sukari ya Bwana Sukari itakayouzwa kwa shillings 500/- and shillingi 1000/-. 

Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Sukari ya Kilombero (KSC) imezindua paketi ndogo za sukari yake ijulikanayo kama ‘Bwana Sukari’, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanamudu kununua sukari hiyo kutokana na unafuu wake wa bei.

Paketi mpya za sukari chapa ya ‘Bwana Sukari’ zinapatikana kwa ujazo wa gramu 350 maarufu kama ‘Robo Plus’ na paketi za gramu 160 maarufu kama ‘Booster’. 

Paketi za ‘Robo Plus’ zitauzwa shilingi 1,000/ kwa kila paketi, na paketi za ‘Booster’ zitauzwa kwa shilingi 500/-kwa kila paketi.

Uzinduzi wa paketi mpya za ‘Bwana Sukari’ uliofanyika maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya KSC kuhakikisha sukari yake inawafikia watanzania wa hali mbalimbali za kiuchumi. 

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Chama cha Wazalishaji wa Sukari Tanzania (TSPA), viongozi na wafanyakazi wa KSC.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Biashara wa KSC, Fimbo Butallah alisema kampuni ya sukari ya Kilombero imekua ikipanga mikakati ya kuhakikisha bidhaa ya ‘Bwana Sukari’ inawafikia watanzania wengi zaidi hapa nchini.

“Sukari ni moja ya bidhaa muhimu kwa matumizi ya kila siku ya nyumbani na sukari ya Bwana Sukari ni moja ya sukari inayopendwa zaidi na watumiaji wengi, tunawashukuru wateja wetu kwa kuikubali bidhaa yetu na kuifanya ifanye vizuri sokoni, kuonyesha shukrani zetu tumeamua kuwaletea paketi hizi ndogo ili wateja wetu wawe na uhuru wa kuchagua ujazo upi utawafaa kwa matumizi yao,” alisema Fimbo.

Akiongeza kuwa, paketi mpya za ‘Bwana Sukari’ zitakidhi mahitaji ya watumiaji wengi zaidi, “kwa mfano paketi za ‘Booster’ ambazo zitauzwa kwa shilingi 500/-zitawafaa zaidi wale wanaohitaji sukari lakini kwa wakati huo hawana uwezo wa kumudu kununua paketi kubwa au kwa wale wenye familia ndogo.”

“Kwa ufupi, kupitia paketi hizi ndogo za Bwana Sukari tunawapa wateja wetu uhuru wa kununua sukari ya ujazo mdogo lakini iliyofungwa kwa hali ya usafi na usalama kabisa na kwa bei nafuu.”

Kwa kuanzia, paketi mpya za ‘Bwana Sukari ’zitapatikana katika maduka yote ya rejareja mkoani Dar es Salaam na wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati KSC inaendelea kufanya mikakati kuhakikisha bidhaa hii inasambaa nchini kote siku za usoni.

TRA: WAFANYABIASHARA MSISUBIRI TAREHE ZA MWISHO KUOMBA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto-Tabora
WAFANYABIASHARA wenye malimbikizo ya madeni ya kodi wametakiwa kutuma maombi ya msamaha maalumu wa riba na adhabu kwenye malimbikizo hayo mapema kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018 ili waweze kunufaika na msamaha huo ambao umetolewa kwa lengo la kutoa unafuu kwa kuwapa fursa ya kulipa kodi ya msingi  ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara, wadau na washauri wa wafanyabiashara kuhusu msamaha huo iliyofanyika leo mkoani Tabora. 

"Nachukua fursa hii kutoa wito kwenu wafanyabiashara kutuma maombi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi ambapo mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huu ni tarehe 30 Novemba, 2018," alisema Mahendeka. 

Mahendeka aliongeza kuwa "Mara nyingi wafanyabiashara huwa mnajitokeza mwishoni kabisa mwa tarehe zinazoonyesha mwisho wa kulipa, kuwasilisha au kutuma maombi fulani suala linalosababisha foleni na msongamano mkubwa katika kutoa huduma katika ofisi zetu. Nachukua fursa hii kuwaomba msisubiri tarehe za mwisho kuleta barua za maombi ya msamaha huu wa riba na adhabu ya madeni ya kodi na naomba mjue kwamba, huu ndio muda muafaka wa kila mwenye malimbikizo ya madeni kutuma maombi Ofisi ya TRA katika mkoa wake kikodi."

Naye, Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo Chama Siriwa alisema muombaji wa msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya kodi anapaswa kutoa maelezo na vielelezo vya ukweli na uhakika wakati wa uwasilishaji wa maombi yake.

"Kila muombaji anatakiwa kutoa taarifa za ukweli wakati anaomba msamaha huu na endapo itabainika kuwa muombaji ametoa taarifa za udanganyifu, Kamishna Mkuu anayo haki kisheria kubatilisha na hivyo kupelekea muombaji kupoteza sifa za kufaidika na  msamaha huu, " alifafanua Siriwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mihayo iliyopo mkoani hapa inayomilikiwa na Taasisi ya Dini ya Kanisa Katoliki Padri Salvatory Maganga, ameishukuru TRA kwa kutoa Elimu ya msamaha wa riba na adhabu ya madeni ya malimbikizo ya kodi na kuomba elimu hii iendelee kutolewa kwa wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali nchini.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa elimu ya msamaha huu hususani kwa wafanyabiashara, wadau na washauri wa wafanyabiashara kwa lengo la kuwahamasisha kutuma maombi ya msamaha huu kabla ya muda uliopangwa haujamalizika ambao ni tarehe 30 Novemba, mwaka huu. 
 Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka akitoa elimu juu ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali (hawapo pichani) iliyofanyika mkoani Tabora kwa lengo la kuwahamasisha wafanyabiashara hao kutuma maombi ya msamaha huo kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.

RUBANI WA ATCL: ATCL ILILIPIA GARAMA ZA MATENGENEZO YA NDEGE ILIYOKODISHWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
RUBANI wa kampuni ya ndege ya Tanzania, (ATCL), Sadiki Jabez, ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, ATCL ililipia garama za matengenezo ya ndege iliyokodishwa licha ya kwamba matengenezo hayo yalifanywa na kampuni iliyowakodisha.

 Jabez ambaye pia ni mkurugenzi muendeshaji wa ATCL na  shahidi wa tisa wa upande mashtaka ameeleza hayo leo Agosti 29 wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. Bilioni 71, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustino Rwenzile.

Mattaka anadaiwa kusababisha hasara hiyo kutokana na kusaini mkataba wa kukodi ndege bila kufuata Sheria ya manunuzi ya umma pamoja na ushauri wa kiufundi.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Timon Vitalis, amedai, mwenye jukumu la kutengeneza ndege pale inapokuwa inahitaji marekebisho  hujulikana kutokana na jinsi mkataba ulivyoingiwa lakini hakuwahi kuuuona huo mkataba.

Shahidi Jabez amedai mwaka 2007, ATCL ikiwa chini ya mkurugenzi David Mataka ilikuwa na ndege moja, 737 boing.
 Amedai, baadae ATCL waliazimia kukodisha ndege airbus 320 kutoka kampuni ya Wallis.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

KIKOSI CHA YANGA VS RAYON SPORTS CAF CONFEDERATION

$
0
0
Kikosi cha Yanga.

Na Zainab  Nyamka,Globu ya Jamii.
Yanga imeshuka dimbani leo kumenyana na Rayon Sports ya nchini Rwanda mchezo utakaoanza majira ya saa 9 alasiri.

Mchezo huo wa kukamilisha ratiba wa kundi D kombe la Shirikisho utachezwa katika Mji wa Kigali.

Beno Kakolanya
Abdala Shaibu 'Ninja'
Gadiel Michael 
Andrew Vicent 'Dante'
Kelvin Yondani
Pius Buswita
Raphael Daud
Deus Kaseke 
Ibrahim Ajib
Matheo Anthony
Heritier Makambo



Hiki ndicho kikosi cha Rayon Sports 
Bashunga Abuba 
Ange Mutsinzi 
Rutanga Eric
Abdul Rwatubyaye 
Mugabo Gabriel 
Mugisha Francois 
Nyandwi Saddam 
Prosper Donkor 
Bimenyimana Caleb 
Muhire Kelvin 
Manishimwe Djabeli

WAZIRI WA ARIDHI AFANYA KIKAO NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO

$
0
0
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiiongoza Wizara yake kutoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi alipokuwa akitoa majibu ya hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

MSAJILI NGOs AWAHIMIZA WADAU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUTILIA MKAZO UTEKELEZAJI WA SERA ZA MAENDELEO

$
0
0
Na WAMJW Dodoma

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba ameyataka wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutilia mkazo katika kutekeleza Sera za Maendeleo zilizopo katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) ili kufanikisha juhudi za Serikali katika kuletea wananchi Maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo Jijini Dodoma.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa Mashirika hayo yanapaswa kuwasilisha mipango yao kwa Msajili ili kuweza kuwa na Mpango mkakati mmoja wa kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa suala la Maendeleo ni mtambuka na linapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Wadau na wananchi ili kufanya shughuli za Maendeleo kuwa endelevu.

 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Idara Kuu Maendeleo ya Jamii pamoja na wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa kuhusu ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Serikali katika kikao cha ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza Sera zinazosimamiwa na kuratibiwa na chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MARAFIKI WA NMF WAIPA SURA MPYA WODI YA WATOTO YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA NANYUMBU, MTWARA

$
0
0
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Nathan Mpangala Foundation (NMF), kupitia programu yake ya Wafanye Watabasamu, hivi karibuni ilishirikisha marafiki wa programu hiyo kubadilisha mwonekano wa wodi ya watoto na chumba cha daktari wa watoto katika Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara toka kuta nyeupe na kuwa zenye michoro mbalimbali.

Mwenyekitio wa taasisi hiyo, Nathan Mpangala alisema lengo la kazi hiyo ya siku tano mbali na kuichukulia kama ibada pia ililenga kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuipa wodi ya watoto ya hospitali hiyo mazingira rafiki kupitia sanaa ya uchoraji, kurudisha kidogo walichonacho kwa jamii na kuhamasisha umuhimu wa matumizi ya sanaa ya uchoraji kwenye maeneo yanayotoa huduma ya afya.

“Zahanati, vituo vha afya na mahospitali uhudumia wagonjwa. Mara nyingi huwa na maumivu, uchovu, upweke na msongo wa mawazo. Sehemu hizo zinapokosa michoro ukutani ambayo ingeweza kuwasahaulisha maumivu, hali huwa ngumu zaidi kwao. Sanaa si kwa ajili ya wagojwa tu, ni muhimu pia madaktari, wauguzi na wote wanaohusika na huduma ya afya. Kama maofisini, kumbini, sebuleni, hotelini tunaning’iniza sanaa iweje zinakosekana sehemu nyeti kama mahospitalini?”  alihoji Mpangala.

Mpangala anaishukuru Toyota Tz, Shule ya Msingi ya Catton Grove ya Uingereza na marafiki mbalimbali wa NMF kwa kuwezesha tukio hilo  na kwamba ametoa wito kwa wadau na wananchi kujitokeza kushirikiana na taasisi yake. “NMF ina mtandao mkubwa wa wachora nchini na wako tayari kujitolea kwa kushirikiana na wananchi au vikundi vilivyo tayari kujitolea.

 Marafiki wa Wafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Karim Mchaka, Athuman Said, Nathan Mpangala na Ndalo Kalua wakijadiliana jambo wakati wa zoezi la usafi wa jumla katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
 Wanawafanye Watabasamu, kutoka kushoto, Athuman Said, ndilo Kalua na Winny Majuva wakihamisha vitanda kutoka katoka wodi ya watoto ili kupisha uchoraji hivi karibuni.
 Kutoka kushoto, George Nyandiche, Neema Loth, Asteria Malinzi na Masoud Kibwana wakiendelea na uchoraji katika wodi ya watoto ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
 Wazazi pamoja na watoto wao wakifurahia muonekano mpya wa wodi ya watoto ya Hospitali ya  Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hamis Dambaya (mwenye shati mikono mirefu) akiwa katika picha ya pamoja na Wanawafanye Watabasamu na baadhi ya viongozi mara baada ya kukamilika kwa uchoraji katika wodi ya watoto Hospitali ya Halmashauri ya Nanyumbu, Mtwara. (Picha zote na NMF)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAKUTANA KUJADILI USALAMA WA CHAKULA NA MASOKO KWA WAKULIMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka ACT Bw Timothy Mmbaga akichangia mada kwenye Mkutano wa wadau wa Kilimo uliokuwa ukijadili usalama wa Chakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana mjini dodoma.
Katibu Tawala Msaidizi Sekta za Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akichangia Mada kuhusu Nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha Usalama wa Chakula, Bei za vyakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana Mjini Dodoma
Mratibu wa taifa wa ubia wa kilimo Tanzania TAP, Bw. Mark Magila akichangia mada wakati wa mkutano wa wadau wa kilimo uliokuwa ukizungumzia usalama wa chakula na masoko kwa wakulima ulioandaliwa na baraza la kilimo Tanzania chini ya mradi wake wa TAP na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo uliofanyika mjini Dodoma jana. 
Sehemu ya washiriki wa warsha ya wadau wa kilimo nchini wakifuatilia kwa ukaribu mjadala wa nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha usalama wa chakula bei za vyakula na masoko ya wakulima, ulioandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania ACT, Chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania TAP, uliofanyika jana mjini Dodoma.
Afisa Sera kutoka Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Bi Laetitia Wiliam akisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa Mada ya iliyokuwa ikihusu Nafasi ya NFRA na CPB katika kuimarisha Usalama wa Chakula, Bei za vyakula na Masoko kwa wakulima, katika walisha iliyoandaliwa na ACT chini ya Mmradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana Mjini Dodoma. 

Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utetezi kutoka ACT Bw Timothy Mmbaga akiwa katika Picha ya pamoja na baada ya kumalizika kwa Mkutano wa wadau wa Kilimo uliokuwa ukijadili usalama wa Chakula na Masoko kwa wakulima ulioandaliwa na Baraza la Kilimo chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania (TAP) uliofanyika jana mjini dodoma.

Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba

$
0
0
Na Nuru Mwasampeta, Dodoma
Imeelezwa kuwa Bandari ya Mtwara itapokea mafuta tani za ujazo 8000 (lita milioni 9.6) ifikapo mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni mara ya Pili kupokea shehena hiyo ya mafuta kutoka yaliposhushwa kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Agosti, 2018 na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mjiolojia Erasto Simon, alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Wizara ya Nishati kuhusu uanzishwaji wa gati la kupokelea mafuta katika bandari ya Mtwara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua waliwaongoza Watendaji mbalimbali wa Wizara na Taasisi zake katika utoaji wa taarifa na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza.

“ Kiasi cha tani za ujazo 8,000 kinatarajiwa kushushwa katika Bandari ya Mtwara ifikapo mwezi Septemba ambapo tani 5,000 kati ya hizo zitakuwa ni mafuta ya dizeli na tani 3,000 zitakuwa ni petroli,” alisema Simon.

Ameongeza kuwa, Serikali iliamua kutumia rasmi Bandari ya Mtwara kupokea mafuta ili kupunguza msongamano wa magari ya kusafirisha mafuta kwenda mikoa ya Kusini na nchi jirani.

Amebainisha kuwa, kwa mara ya kwanza mafuta yalipokelewa katika bandari ya Mtwara tarehe 28 Juni, 2018 ambapo kiasi cha tani 8,339 kilishushwa bandarini hapo na kupokelewa kwenye maghala ya kuhifadhi mafuta yanayomilikiwa na kampuni za GM & Company /Oryx na Oilcom Tanzania.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakiwa katika kikao kilichojadili taarifa mbili za utekelezaji wa majukumu ya  Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (wa Pili kushoto) wakiongoza Ujumbe wa Wizara pamoja na Taaisisi zake katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JWTZ KUTIMIZA MIAKA 54 SEPTEMBA 1, LAHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
Na Angess Francis Blogu ya Jamii

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza na kushiriki kwa wingi katika kufanya shughuli za usafi wakati maadhimisho ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kutimiza miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.

JWTZ linatarajia kufikisha miaka 54 ifikapo Septemba 1 mwaka huu.Jeshi hilo lolianzishwa mwaka 1964.
Akizungumzia sherehe hizo Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano  wa JWTZ Kanali Ramadhani Dogoli amesema katika maadhimisho hayo ya mwaka huu jeshi limeanza kufanya  shughuli mbalimbali za kijamii  pamoja na kujishughulisha katika michezo.

“Itakumbukwa kila mwaka  inapofika tarehe hiyo bada ya kubadilishwa  jina kutoka Tanganyika Rifle (TR)  kuwa Jeshi la Ulinzi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

"Na sherehe hizo kila mwaka tumekuwa tukifanya shughuli za kijamii kwa kufanya usafi  kwenye maeneo ya kambi zote za jeshi na kushiriki katika michezo,”amesema.
Amefafanua michezo inayoendelea kuchezwa ni mpira wa miguu,Pete,wavu, golf na mingine na kwamba timu za jeshi na za uraiani ndizo zinashiriki michezo hiyo.
Kanali Dogoli amefafanua shughuli hizo zilianza kufanyika  Agosti 27  mwaka huu na kwamba zitaendelea hadi siku kilele cha sherehe hizo.

Hivyo limesisitiza umuhimu wa watanzania wote wenye mapenzi mema kungana kuadhimisha siku  hiyo kwa kujitokeza kufanya usafi katika maeneo yao wanayoishi na  kuyaweka katika hali ya usafi.

Article 18

SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti , Mhe. Goerge Simbachawene akiongoza Kikao cha Kamati hiyo kilichokutana leo  katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mashimba Ndaki . Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018.
 Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. George Simbachawene ikiwa katika kikao cha Kamati leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018.

Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. George Simbachawene ikiwa katika kikao cha Kamati leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.Kamati hiyo ilikuwa ikipitia na kuchambua Muswada wa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018

VIONGOZI WA DINI WAWE SEHEMU MUHIMU KATIKA MIKAKATI YA KUJIKINGA NA EBOLA.

$
0
0
Na Editha Karlo,wa blog ya jamii Kigoma

VIONGOZI wa dini zote wametakiwa kushirikishwa kwenye maandalizi ya mapambano ya ugonjwa wa ebola ambao umetaatifiwa upo nchi jirani ya Jamhuri ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo endapo itatokea utaingia nchini Tanzania ili kuweza kuutokomeza kabisa.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi wakati alipotembelea Mkoa wa Kigoma akiongozana na timu yake ya wataalam kwa ajili ya ukaguzi wa nyenzo na afua mbalimbali zilizowekwa ili kupambana na ugonjwa wa ebola leo Mkoani humo.

"Afua muhimu ya mkoa wowote katika kupambana na ugonjwa huu ni kuwashirikisha vizuri viongozi wa dini zetu pamoja na viongozi wa kimila na jamii kwani ndio wanaokutana na wanajamii kwa muda mwingi zaidi hivyo kuwashirikisha kwao elimu juu ya kujikinga na Ebola itakuwa kubwa zaidi na hatimae tutafanikiwa kujikinga na ugonjwa huu" alisema Prof. Bakari.

Aidha Prof. Bakari Kambi amesema kuwa Mkoa wa Kigoma upo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa Ebola kwa kuwa kuna mipaka mingi iliyo wazi ambayo inaingiza wageni kutoka Burundi na Congo ambapo ugonjwa huo umetaarifa upo maeneo ya nchi ya Congo.

Mbali na hayo Prof. Bakari Kambi ameuoingeza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa jitihada na mikakati waliyoiweka na kuifanyia kazi ili kuweza kudhibiti ugonjwa wa Ebola endapo utaingia Mkoani humo. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote amesema kuwa Kigoma amesema kuwa hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola katika maeneo yote ya Mkoa huo. 

Mganga Mkuu wa serekali Prof.Mohammed Bakari akitoka kukagua moja ya mabanda yaliyopo katika bandari ya Kigoma ambayo yatatumika kumpumzisha mgonjwa mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebola mara baada ya kushuka katika bandari ya Kigoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt.Paul Chawote akitoa taarifa ya ugonjwa wa ebola kwa Mganga Mkuu wa Serekali prof.Bakari Kambi kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkoa wa Kigoma.


MATUMIZI YA POMBE YANA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII

$
0
0
MTANDAO wa Kudhibiti Madhara ya Matumizi ya Pombe (TAAnet) umeeleza kuwa matumizi makubwa ya pombe ni chanzo kikubwa cha matatizo hasa ugomvi na mifarakano katika familia.

Aidha mtandao huo umesema asilimia nne ya vifo vitokeavyo duniani na asilimia nne ya magonjwa yasitoambukizwa usababishwa na matumizi makubwa ya pombe yanayofanika kwa sasa.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam Jana na Mjumbe wa bodi katika mtandao huo, Dk. Mashombo Mkamba wakati wa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu madhara ya matumizi ya pombe.

Alisema licha ya pombe kusababisha matatizo hayo pia inaelezwa kuwa ni moja ya visababishi vikubwa vya aina mbalimbali ya saratani zinazotesa baadhi ya watu nchini na duniani kwa ujumla.

"Najua ni vigumu kwa baadhi ya watu wanaotumia pombe kuacha Ila upo uwezekano wa kuiacha kama utaamua kwani hakuna faida yoyote inayotokana na unywaji wa pombe," alisema na kuongeza kuwa.

"Licha ya pombe kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya serikali duniani kote,lakini usababisha ajali nyingi zinazosababisha vilema  na kupoteza maisha ya watu wengi," alisema.

Aidha alisema inakadiliwa katika kila mwaka lita 2.4 bilioni za pombe za kienyeji utengenezwa na kunywewa hapa nchini na kusema hiyo ni idadi kubwa ya pombe inayonywewa na watu.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa TAAnet Sophia Komba alisema yapo magonjwa zaidi ya 120 usababishwa na matumizi ya pombe hivyo ameitaka jamii kubadilika kuacha matumizi ya vilevi kwani havina maendeleo wala faida yoyote.
Waandishi wa habari wakiwa katika semina ya siku moja inayohusu madhara ya matumizi ya pombe.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaombwa kuondoa kero ya kukosekana kwa vifaranga wa kuku bora nchini

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu MIZENGO PINDA ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuondoa adha ya kukosekana kwa vifaranga wa kuku bora nchini, sambamba na uhaba wa upatikanaji wa chakula bora cha kuku.

PINDA ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO amesema hayo leo Jijini DODOMA wakati chama hicho kikipokea msaada wa vifaranga vya kuku bora kutoka Kampuni AKM GLITTERS, ambapo amebainisha kuwa ukosefu wa vifaranga na chakula bora cha kuku imepelekea wafugaji kukosa ari ya kuendelea kufuga.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi ABDALLAH ULEGA amekiri kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa chakula bora cha kuku nchini na kusema kuwa suala hilo ni lazima lishughulikiwe ili kumaliza tatizo hilo kwa wafugaji wa kuku .Pia Naibu Waziri ULEGA amebainisha kuwa kukosekana kwa vifaranga bora nchini kumetokana na udhibiti wa uingizwaji holela wa vifaranga vya kuku na kubainisha kuwa hivi sasa tatizo hilo lipo katika hatua za utatuzi na kwamba hali ya upatikanaji wa vifaranga itarejea kama zamani.

"Tumekubaliana lazima kuwe na udhibiti wa utotoleshaji wa vifaranga kiholela na utengenezaji wa vyakula vya mifugo jambo litakalosaidia kuondoa tatizo la kuwa na vifaranga na vyakula visivyo na ubora" alisema Waziri Ulega.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjinj PATROBAS KATAMBI amewapongeza wafugaji hao na kusema kuwa kwa sasa sekta ya ufugaji inakua hivyo ni lazima changamoto zilizopo ziweze kutatauliwa. Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Mkoa wa DODOMA kimepokea msaada wa vifaranga elfu nne ikiwa ni awamu ya kwanza ya msaada huo.


Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi ABDALLAH ULEGA akimkabidhi Vifaranga bora mmoja wa wachama chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO mapema leo mjini Dodoma,kuku hao wametolewa na kampuni ya AKM GLITTERS,huku Mlezi wa Chama hicho CHAWAKUBODO Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akishuhudia
Makabidhiano ya Vifaranga bora kwa Chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO,yakifanyika kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho kutoka kwa viongozi wa mkoa wa Dodoma akiwemo mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh.Patrobas Katambi.
Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi ABDALLAH ULEGA,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh.Patrobas Katambi pamoja na Mlezi wa chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO wakionesha vifaranga bora kwa wanachama wa CHAWAKUBODO,vifaranga hivyo vimetolewa na kampuni ya AKM GLITTERS.

Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi (MB) Abdallah Ulega akizungumza mapema leo kwenye hafla fupi ya kukabidhi Vifaranga bora kwa wachama wa chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO mapema leo mjini Dodoma,kuku hao wametolewa na kampuni ya AKM GLITTERS

MWENYEKITI WA NEC AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza na baadhi ya Mafundi na  Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi alipotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Ofisi hizo eneo la Njedengwa leo jijini Dodoma. Wengine ni Wajumbe na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akikagua eneo linapojengwa ghala la kuhifadhia vifaa vya uchaguzi akiwa ameambatana Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka eneo la Njedengwa leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza na Wajumbe na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (kulia) mara baada ya kutembelea eneo la mradi la ujenzi wa Ofisi za NEC jijini Dodoma. Wengine (kushoto) ni Mafundi na  Wahandisi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo hilo kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi.
Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Muhandisi Geofrey Mushanyela akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi hizo kwa wajumbe na watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliotembelea mradi huo leo jijini Dodoma.

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakipita mbele ya jengo la Utawala la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Wahandisi wanaosimamia mradi huo kutoka TBA na Chuo Kikuu Ardhi. Jengo hilo la Ofisi za NEC linajengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma leo. PICHA/ TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA

$
0
0
MADIWANI watano wa vyama vya upinzani ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, CUF na ACT Mzalendo na viongozi wengine sita wamevikimbia vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani.

Madiwani hao ni pamoja na Ramadhan Lutambi aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja kupitia Chadema na Ramadhan Kombe aliyekuwa diwani  kata Mbwawa kupitia ACT. 

Wengine ni, Muharami Mkopi Cuf kata ya Ruaruke wilayani Kibiti,Seif Lwambo kupitia Cuf kata ya Beta,Muharami Mketo Cuf Kata ya Lukanga na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga.

Aidha viongozi waliojiuzulu kwenye vyama hivyo ni Ayubu Chapile ambae alikuwa katibu kata ya Mkuza (CUF) ,Karimu Kasimu katibu tawi chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere (Chadema) ,Selemani Mwinyimkuu mwenyekiti tawi (Cuf),David Mramba Act,Latifa Sangalala mwanachama Chadema Mkoani B na Jumanne Urembo Diwani kivuli ACT kata ya Sofu.

Awali Ramadhani Lutambi alisema ,chama kinachofaa kuongoza nchi daima ni CCM kwani vyama vingine havina uwezo,na havijali  viongozi wa ngazi za chini .

Alifafanua ,ameamua kuondoka Chadema ili kutekeleza yale yanayofanywa na Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wanyonge.

Lutambi alikiri kuondoka Chadema kwa hiari yake, kwa akili zake timamu na kudai anajivua vyeo vyote alivyonavyo kuanzia sasa.
 Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja, Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema amekimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) mkoani Pwani Ramadhani Maneno akizungumza baada ya kuwapokea madiwani watano kutoka upinzani na viongozi na wanachama wengine wa vyama hivyo wapatao sita.

Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja, Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema akiwapungia mkono baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM katika ofisi za CCM mkoani Pwani baada ya kuacha chama hicho na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VIONGOZI WAPYA WA TSA WATALETA MAENDELEO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limesema kuwa uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) ulienda vizuri ingawa kulikuwa na changamoto zilizojitokeza hapo awali.

Uchaguzi huo uliofanyika mapema wiki hii, uliweza kuwapata viongozi wapya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka minne ambao wameapa tayari kwa ajili ya kuanza kutumikia nafasi zao kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo.

Akizungumzia uchaguzi huo Ofisa habari wa BMT Najaha Baklari amesema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani kubwa sana ingawa awali kulitokea changamoto mbalimbali na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Juma Ikangaa aliweza kutoa rai kwa wagombea wote walioshinda nafasi zao wakazitumikie kwa ueweledi mkubwa ili kuleta manufaa kwa chama hicho, pia hata wale ambao hawakupata nafasi wae dele kuunga mkono.

Amesema kuwa  uchaguzi ulikuwa na ushindani mkubwa sana hususani katika nafasi za  Makamu Mwenyekiti  na Katibu Mkuu ambapo zilikuwa na wagombea zaidi ya mmoja na nafasi nyingine kuwa na mgombea mmoja mmoja lakini hakukuwa na wakati mgumu sana katika nafasi ya mwenyekiti, Mweka Hazina na Mkugenzi wa Elimu na Maendeleo ambazo  zilikuwa na mgombea mmoja mmoja.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images