Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: TANZANIA RED CROSS YAJIZATITI KUKABILIANA NA MAJANGA


MICHUZI TV: RC CHALAMILA AONGEA NA WAJASIRIAMALI MKOANI MBEYA

MICHUZI TV: WAZIRI LUGOLA ASHTUKIZA KITUO CHA POLISI MABATINI DAR ES SALAAM

KASI YA UJENZI WA JENGO LA TRA PWANI HAIRIDHISHI -RC NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI .

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la mamlaka ya mapato Tanzania, (TRA) mkoani humo ,ujenzi ambao unasuasua kwa miaka miwili sasa na kubaki gofu.
Aidha amesema jengo hilo hadi lilipofikia halilingani na thamani ya sh.bilioni 1.653.267 .510 ambayo ni awamu ya kwanza iliyofikia asilimia 61 hadi sasa. 

Kufuatia hali hiyo ,Ndikilo amemuelekeza meneja wa mamlaka hiyo mkoa ,kumfikishia salamu kamishna wa mamlaka ya mapato makao makuu kufuatilia mradi wa ujenzi huo . 

Mkuu huyo wa mkoa alieleza masikitiko hayo ,wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa viwanja ya taasisi binafsi na serikali katika halmashauri ya Mji wa Kibaha,ikiwemo Uhamiaji,TRA na CRDB. Alisema ,lengo la kupewa viwanja hivyo ni kujenga maeneo hayo na sio kukumbatia viwanja bila sababu za msingi.

“Serikali ya mkoa na waziri mkuu Kassim Majaliwa ilishatoa agizo tangu mwaka juzi kuwa maeneo hayo yote yahakikishwe yanajengwa na kama haiwezekani wanyanganywe wahusika na kupewa wengine wenye uwezo” alisisitiza Ndikilo. Ndikilo alishangazwa na kupewa taarifa pia kuwa ujenzi huo bado unahitaji zaidi ya milioni 200 wakati hatua ya kwanza haiendani na maelekezo ya serikali na mkoa. “Gharama imesemwa itakuwa bilioni 2.693.402.120 ,ambapo mkandarasi Humphrey Construction Ltd, bado anahitaji fedha zaidi ambayo itafikia bilioni 2.8 jambo ambalo haliniingii akilini'” .

“Kwanza mmeshaezeka mabati Leo hii mnaniambia mtaendelea na hatua nyingine ya ujenzi kwa ghorofa tatu ambapo mtaondoa mabati ambayo yameshagharamiwa halafu muongeze majengo tena , haiwezekani nitaagiza vyombo vyangu vya ulinzi na usalama vichunguze zaidi, ” alifafanua Ndikilo .


Jengo la mamlaka ya mapato mkoani Pwani ambalo linasuasua katika ujenzi wake ambao ulitakiwa kukamilika tangu june 2016 .(picha na Mwamvua Mwinyi).
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo alipotembelea jengo la idara ya uhamiaji mkoani Pwani ambalo limekamilika kwa gharama ya bilioni 1.6(picha na Mwamvua Mwinyi) .
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo(kulia) alipotembelea ujenzi wa jengo la CRDB mkoani Pwani ambalo limekamilika kwa gharama ya milioni 900 , mbele kulia meneja CRDB Pwani Rosemary Nchimbi. (picha na Mwamvua Mwinyi

NEWZ ALERT:SHULE YA ST MARRY'S YATEKETEA KWA MOTO USIKU HUU MKOANI TABORA

$
0
0
Moto mkubwa umezuka katika majengo ya Shule ya Sekondari St Marry's zamani Mihayo Sekondari iliyopo mkoani Tabora na kuteketeza baadhi ya mali.

Kikosi cha zima moto tayari kimefika eneo la tukio ili kuudhibiti moto huo, ambao kwa kiasi kikubwa umeenea katika baadhi ya majengo ya shule hiyo.

Taarifa zaidi tutaendelea kuwajuza.

SERIKALI IMETENGA BILIONI 30 KUJENGA HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA

$
0
0

Na.WAMJW-Dodoma

Serikali imetenga shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya hospitali zaRufaa za Mikoa kila mkoa ili kuweza kuwawezesha wananchi kupata huduma za rufaa za kibingwa karibu na wanapoishi na hivyo kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiwasilisha taarifa za uendeshaji wa hospitali za rufaa za Mkoa kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Jijini Dodoma.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha hospitali za Rufaa za Mikoa ya Geita, Katavi, Simiyu, Njombe na Songwe ambapo zipo katika hatua za ujenzi wa hospitali hizo hivyo itafanya idadi ya hospitali hizo kuwa 28 pindi zitakapokamilika.

“Serikali ilifanya mabadiliko ya kuzihamishia hospitali za Rufaa za Mikoa Wizarani ili kuboresha huduma za kibingwa ikiwemo kutoa fursa nzuri ya udhibiti ,usimamizi na mgawanyo wenye tija zaidi wa rasilimali chache zilizopo”alisema Dkt.Ndugulile.

Alisema kuwa baada ya Wizara kukabidhiwa hospitali hizo ilifanya tathimini ya awali ya hali halisi na kubaini changamoto mbalimbali zilizoathiri utoaji wa huduma za afya katika maeneo yote ambayo ni nguzo ya msingi katika kuwezesha upatikanaji wa huduma bora. “Hospitali za Rufaa za Mikoa zinapaswa kutoa huduma za kibingwa ambazo hazitolewi katika hospitali ngazi ya Halmashauri,Huduma za kibingwa ambazo ni lazima kupatikana katika hospitali za Rufaa”.Alisema Naibu Waziri Dkt. Ndugulile

Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya uendeshaji wa hospitali za rufaa za mikoa mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma. 
Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwasilisha ripoti ya uendeshaji wa Hospitali za rufaa za mikoa mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma. 
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Mhe. Peter Selukamba akitoa neno wakati wa kuwasilisha kwa taarifa za uendeshaji wa hospitali za rufaa za mikoa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto jijini Dodoma. 
Wajumbe wakifuatilia mjadala uliokua unaendelea katika kikao cha mawasilisho ya taarifa za uendeshaji wa Hospitali za rufaa za mikoa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto katika kamati ya kudumu ya Huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma 

RAIS DKT SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA BoT

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens D.M Luoga alipofika Ikululu Mjini Zanzibar leo akifuatana na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 28 Aug 2018.

Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akifuatana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof Florens D.M Luoga baada ya mazungumzo alipofika Ikululu Mjini Zanzibar leo akifuatana na ujumbe wake,[Picha na Ikulu.] 28 Aug 2018.

Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akizungumza na Ujumbe wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ulipofika Ikululu Mjini Zanzibar leo ukiongozwa na Gavana Prof Florens D.M Luoga (wa pili kuli),[Picha na Ikulu.] 28 Aug 2018.

Waziri Mwakyembe atembelea Global Group

$
0
0

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho (kulia) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati Waziri alipotembelea ofisi za Global Group mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mhariri wa gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kushoto) akimuonesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati Waziri alipotembelea ofisi za gazeti hilo Global Publishers mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza na wafanyakazi Global Group wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) alipotembelea ofisi za Global Group mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Global Group wakati Waziri alipotembelea ofisi za Global Tv mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (mwenye shati la zambarau) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global Group wakati Waziri alipotembelea ofisi hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI KIJAZI AMJULIA HALI DKT.KIGWANGALLA MOI

$
0
0

Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Mhandisi John Kijazi leo tarehe 28/08/2018 amemtembelea na kumjulia hali Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara.

Balozi Kijazi amempa pole Mh Dkt. Kigwangalla na kumtakia heri na apone haraka ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kila siku kwani Taifa linauhitaji mchango wake. “Pole sana. Mungu atajalia utapona na utarejea nyumbani mapema, na kwa kuwa wewe ni daktari ukiona hali si nzuri utawafahamisha wenzio mapema ili mjadiliane namna ya kuikabili hali itakayojitokeza” Alisema Balozi Kijazi wakati wa kumjulia pole Hospitalini hapo.

Aidha, Balozi Kijazi amemueleza Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface kwamba kwa sasa wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na MOI na Muhimbili kwa ujumla na hii ni faraja kubwa kwa Serikali na hivyo kuelekeza ari hiyo iendelezwe. “Pamoja na Jitihada kubwa za Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli za kuboresha huduma za Afya hapa nchini, nanyi pia kwa upande wenu mnajitahidi sana na wananchi wanaridhishwa na huduma mnazotoa. Nafahamu kuna changamoto chache lakini bado mmeendelea kufanya kazi nzuri” Alisema Balozi Kijazi.

Kwa upande wake, Dkt Hamis Kigwangalla amemshukuru Balozi Kijazi kwa kumtembelea na kumjulia hali na amemueleza kwamba afya yake imeendelea kuimarika na anaamini katika kipindi kifupi kijacho madaktari watakapojiridhisha wanaweza kumpa ruhusa ya kutoka hospitalini.

“Ninaendelea vizuri, afya yangu inaimarika siku hadi siku, na pia naendelea na mazoezi na kila siku najiona imara zaidi na hii ni ishara tosha kwamba ninaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani” Alisema Dkt. Kigwangalla. Dkt. Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.

Katibu Mkuu Kiongozi nchini, Balozi Mhandisi John Kijazi akitoa maelekezo kwa jopo la Madaktari Bingwa na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Taasisi ya Mifupa ya MOI ambao wanamtibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (Aliyeketi) alipomtembelea mapema leo Agosti 28,2018, Wodi ya Kitengo cha Mifupa MOI. 
Katibu Mkuu Kiongozi nchini, Balozi Mhandisi John Kijazi akishuhudia picha  ya X ray inayoonesha eneo la mkono wa kushoto wa Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla anayepatiwa tiba MOI namna unavyoendelea. Aliyeshika Xray ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface, wengine ni Mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Laurence Museru na Mkurugenzi wa Tiba MOI Dkt. Samuel Swai. Mapema leo Agosti 28,2018, Wakati alipomtembelea Wodi ya Kitengo cha Mifupa MOI. 

Songwe,Kigoma, Mwanza yajipanga kudhibiti Ebola

$
0
0
UONGOZI wa Viwanja vya Ndege vya Songwe na Kigoma, umejiandaa kwa kushirikiana na maafisa afya, kuhakikisha hakuna mgonjwa mwenye dalili za Ebola anaingia nchini, akitokea maeneo ya Tunduma na nchini Burundi.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Pius Kazeze alimwambia Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi.Bahati Mollel kwa njia ya simu kuwa, tayari Maafisa wa Afya wameshafunga mashine maalum (thermo scanners) inayotambua joto la mwili la abiria ambaye anasafiri kwa kupitia kiwanja hicho, na likizidi 38 anatakiwa kutoa taarifa za afya yake.

Bw. Kazeze amesema Kiwanja cha Songwe ni tofauti kidogo na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo zaidi wanakagua abiria wanaoondoka kwa kuwa wengi wanatoka mpakani maeneo ya Tunduma na kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Tayari maafisa Afya wamefunga mashine ya ukaguzi wa afya eneo la nje la kuondokea abiria kwani kwetu huku tunapata abiria wengi wanaotoka nchi jirani wanaopitia mpakani Tunduma, hivyo wengi wao wanatoka nchi zinazopakana na Kongo, ambayo inasadikika ugonjwa wa Ebola umeibuka kwa kasi kubwa,” alisema Bw. Kazeze.

Hatahivyo, amesema mbali na mashine hiyo kubwa iliyowekwa sehemu maalum, pia wanamashine mbili ndogo zinazotumiwa kwa kushikwa mkononi na maafisa Afya, lakini wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Watumishi wa afya, ambao tayari wameshaomba kuongezewa mmoja ili kufanikisha kazi hiyo kuwa rahisi.
Mmoja wa abiria akikaguliwa na mashine ya mkono, iliyoshikwa na Afisa Afya wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Peter Maseke, ikiwa ni moja ya njia za kudhibiti wagonjwa wa Ebola wasiingie nchini. Ugonjwa huo umetangazwa hivi karibuni kusambaa nchini Kongo.
Afisa Afya wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Peter Maseke (katikati) akikagua hati za kusafiria za mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Dar es Salaam, ambapo (kulia) ni mashine maalum inayotambua abiria wenye homa kali, ambayo ni moja ya dalili za ugonjwa wa Ebola.
Abiria wakiwa katika eneo la nje la kuondoka kwenye Kiwanja cha Ndege cha Songwe


RAIS SHEIN AZINDUA PROGRUM YA PAMOJA ZANZIBAR

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (,kushoto) na Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez wakifungua pazia kuashiria Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar uliofanyika leo Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar ambapo mpango huo utafanikisha maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar,[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar akiwepo na Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto),[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar (wa tatu kushoto)Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez,[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.
Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi zana za Kazi Bibi.Mwanaisha Makame (Topu) (wa pili kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar uliofanyika leo Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar (katikati) Mwakilishi Mkaazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) Bw.Alvaro Rodriguez,[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018. 
 
Wananchi na Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa PROGRAMU ya Pamoja Zanzibar iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Idrisa Abduwakil Mnazi Mmoja mjini Zanzibar,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mswenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]28 Aug 2018.

WALENGWA WA TASAF MKOANI KILIMANJARO WAIANGUKIA SERIKALI.

$
0
0



Na Estom Sanga-Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro kukutana na wananchi wanaonufaika na huduma za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF kupitia Mpango wake wa Kunusuru Kaya Maskini- PSSN.

Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Mkuchika amejionea namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, walivyoboresha maisha yao kwa kutumia huduma za TASAF kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini zinazoambatana na ruzuku ya fedha, elimu ya ujasiliamali na utekelezaji wa masharti ya Elimu na Afya huku mkazo ukiwekwa katika kuwajengea mazingira ya kukuza kipato cha Walengwa hao.

Akizungumza na Walengwa katika wilaya za Same, Mwanga,Siha na Hai kwa nyakati tofauti ,Mhe. Mkuchika amesema shughuli za TASAF ni mwendelezo wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 ambayo imeielekeza serikali kutumia mbinu mbalimbali za kutatua kero ya umaskini miongoni mwa wananchi kwa lengo la kuboresha maisha yao.

Amesema kutokana na dhamira thabiti ya serikali katika mapambano dhidi ya Umaskini , wananchi kwa ujumla wao hususani wale waliojumuishwa kwenye Mpango wa TASAF wanapaswa kujituma zaidi katika kuanzisha na kutekeleza miradi ya uzalishaji mali ili waweze kujiongezea kipato na hatimaye kuondokana na adha ya umaskini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (aliyevaa kofia) akikagua nyumba inayojengwa na mmoja wa Walengwa wa TASAF (wa kwanza kulia ) katika kijiji cha Kileo,wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Mhe. George Mkuchika Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (aliyevaa koti nyeusi ) akihesabu fedha kabla ya kumkabidhi mmoja wa Walengwa wa TASAF mkoani Kilimanjaro baadhi ya kuridhishwa na jitihada za mlengwa huyo katika kupambana na umaskini kwa kutumia ruzuku ya TASAF.
Waziri Mkuchika akiangalia moja ya mazizi ya mbuzi za Walengwa wa TASAF katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ikiwa ni mojawapo ya njia za kujiongezea kipato kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mhe. Kippi Warioba(wa pli kulia )akieleza jambo baada ya Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mhe. George Mkuchika kutembelea mojawapo ya makazi ya Mlengwa wa TASAF (mwenye kilemba) wilayani Siha.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Redcross Tanzania yadhamiria kutoa elimu ya huduma ya Kwanza.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

REDCROSS Tanzania imedhamiria kuleta mapinduzi kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja anawajibika kutoa msaada wa majanga yanayojitokeza ili kusaidia waathirika wa majanga hayo wasipoteze maisha kwa kukosa huduma ya kwanza.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Redcross Julius Kejo wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana kazi zinazofanywa na Redcross Tanzania na namna kuhakikisha jamii inawajibika kusaidia kuwa mstari wa mbele katika majanga mbalimbali yanayotokea na kuachana na tabia ya kukimbilia kuona bila ya msaada wa huduma ya kwanza.

Amesema bado kuna tatizo kubwa kwa jamii kutowajibika pale yanapotokea majanga ikiwamo ya ajali na mengineyo kwa kushindwa kuwasaidia kwa haraka watu wanaopata athari katika majanga hayo badala yake kubaki washudiaji tu na kupiga picha.

“Ajali ikitokea, badala ya watu kutoa msaada wa huduma ya kwanza kuokoa maisha yao, watu wanawazunguka kuwashangaa, na wengine wanatumia muda huo kuchukua picha kutuma kwenye mitandao na kuacha wenzao wakihangaika au baadhi ya wengine wanapoteza maisha wakati huo huo kwa kukosa huduma ya kwanza wakati pengine wangewasaidi kuokoa maisha yao ,” amesema Kejo

Amesema umefika wakati watanzania kubadilika kujitoa katika kupata elimu ya huduma ya kwanza ambayo itatumika katika kuokoa maisha ya watu katika majanaga mabalimbali kwani kusaidia mtu katika majanga ni haki kwa yule yaliyompata.
 Katibu Mkuu wa Recross Tanzania Julius Kejo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na kazi ya Redcross katika utoaji wa huduma wakati wa Majanga yanapotokea, mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.


Mwakilishi wa Ubelgiji Red cross Tanzania An Vanderheyden akizungumza uzoefu wa Redcross katika kujitoa katika uchangiaji.

Dkt.KIJAJI AFUNGUA MKUTANO 41 WA BIMA KUTOKA NCHI 39 MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA (OESAI)

$
0
0
Na.Vero Ignatus.Arusha

Mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) umefunguliwa  rasmi mkoani Arusha.

Mkutano huo umefunguliwa na Naibu waziri wa fedha Dkt. Ashatu Kijaji ambapo ameyataka makampuni ya Bima kutoa huduma za Bima kwa wakulima ili kufikia uchumi wa kati. 

Dk, Kijaji amesema asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima ambao bado hawana elimu kuhusu bima ikiwemo kupata mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua changamoto za kilimo na kufikia katika uchumi wa kati. 

Ameyataka makampuni ya bima nchini kuangalia kundi hilo la wakulima ili nao waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa na ni fursa kwa makampuni ya bima nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa bima. 

Amesema watanzania wanaotumia bima hapa nchini ni chini ya asilimia moja idadi ambayo hairidhishi kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu za Taifa. Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware amesema mkutano huo wa 41 unatoa fursa kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini kujifunza jinsi kampuni za nje za bima zinavyofanya kazi kwa ufanisi. 
Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji akizungumza katika mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) .Picha na Vero Ignatus. 
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha. 
Wapili kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji, aliyepo kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware, akifuatiwa na Rukia Adam Mjumbe kutoka (TIRA) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka baadhi ya matataifa 39 Duniani. Picha na Vero Ignatus. 



MAVUNDE AJITOLEA KUMSOMESHA NA KUMLEA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA MIGUU

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amejitolea kumsomesha na kumlea mtoto Christopher Edward kutokea kijiji cha Mtita, Wilaya ya Bahi jijini Dodoma ambaye amekatwa miguu yote miwili katika Hospital ya kibingwa ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kufuatia kupatwa na ugonjwa wa kupooza miguu.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana katika Hospital hiyo ya kibingwa wakati akikabidhi kiti cha matairi (wheelchair) kwa mtoto Christopher kilichotolewa na Hospital ya Benjamin Mkapa ikiwa ni njia ya kumrahisishia usafiri kumtoa sehemu moja kumpeleka sehemu nyingine katika kutimiza majukumu yake ya kila siku ikiwemo elimu.

Kutokana na changamoto hizo zinazomkabili mtoto Christopher, Naibu Waziri Mavunde akishirikiana na Mbunge wa Bahi Mh Omary Badwell wameahidi kumsaidia miguu ya bandia miwili na pia kumsomesha katika shule ya Fountain Gate Medium School iliyopo Miyuji Jijini Dodoma ili kumsaidia mtoto kutimiza ndoto zake za kielimu na maisha kwa ujumla.

Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dr Alphonce Chandika alisema Hospital imeona imsaidie mtoto Christopher kiti hicho cha kutembelea ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuwajali na kuwasaidia watanzania wenye vipato vya chini.

"Kweli tumeokoa maisha ya Christopher tena bila kumtoza gharama, lakini tusingeishia hapo kwasababu tayari ni mhitaji, hivyo tumempatia kiti hiki na sasa tunawaomba watanzania wamsaidie miguu bandia, suala elimu na mahitaji mengine muhimu ili ajimudu katika maisha yake" alisema Dkt Chandika.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusu kujitolea kumsomesha na kumlea mtoto Christopher Edward kutokea kijiji cha Mtita, Wilaya ya Bahi jijini Dodoma ambaye amekatwa miguu yote miwili katika Hospital ya kibingwa ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma kufuatia kupatwa na ugonjwa wa kupooza miguu.
Naibu Waziri Mavunde akikabidhi kiti cha matairi (wheelchair) kwa mtoto Christopher kilichotolewa na Hospital ya Benjamin Mkapa ikiwa ni njia ya kumrahisishia usafiri kumtoa sehemu moja kumpeleka sehemu nyingine katika kutimiza majukumu yake ya kila siku ikiwemo elimu. 
Picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano.

WILAYA YA MANYONI MKOANI SINGIDA YATENGA ZAIDI YA EKARI 5000 KUPANDA MIKOROSHO MIPYA

$
0
0
WILAYA ya Manyoni mkoani Singida imetenga zaidi ya ekari 5000 kwenye Kijiji cha Masigati kwa ajili ya kupanda mikorosho mipya baada ya wananchi kuhamasisha kupanda zao hilo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya korosho nchini ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini ambao yalifanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho.

Viongozi wa bodi hiyo ambao walifika kwenye shamba la mfano lililopo katika Kijiji cha Masigati kwenye Halmashauri ya Manyoni ambalo lilianza mwaka jana ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba na Afisa Uhusiano Bryson Mshana wakiwa kwenye uhamasishaji wa kilimo hicho kwenye maeneo mapya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya hizo ekari zilizopandwa ni 1250 kwa msimu uliopita wa kilimo na msimu umekaribia mwezi Desemba mwaka huu wataanza tena kuendelea na upandaji wa mikorosho mipya.

“Pamoja na kwamba tumetenga ekari 5,000 kwa ajili ya kulima kilimo cha Korosho lakini mipango yetu ni kufikia ekari 10,000 alisema pamoja na hayo tutaendelea kufanya uhamasishaji kwa wananchi kuweza kuchangamkia fursa ya zao hili na kupanda mikorosho kwa wingi “Alisema.
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini yaliyofanyiwa utafiti  na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho ukafanyika akielezia mikakati ya wilaya yake kupanda zaidi ya ekari 5000 za mikoroshoMkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana wakati wa ziara ya viongozi wa bodi kuhamasiha kilimo cha zao la Korosho kwenye maeneo mapyaAfisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo ,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo na viongozi wa bodi ya Korosho mara baada ya kumalizia mazungumzo nayo kushoto ni Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana na kulia ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba 

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU.

$
0
0

NEC – Dodoma.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini, Monduli na kwenye Kata 23 za Tanzania Bara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni wakati wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi huo mdogo jijini Dodoma.Jaji Kaijage amewataka Wasimamizi hao kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili wapunguze na kuondoa malalamiko yanayojitokeza wakati wa uchaguzi.

Amesema Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

“ Tunakutana hapa kwa muda wa siku tatu (3) ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi,” Amesema Jaji Kaijage.

Aidha, amewataka Wasimamizi hoa waepuke madhara yanayotokana na ukiukaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi na akisisitiza kwamba katika kipindi hiki chaguzi zinafanyika katika mazingira ambayo yana hamasa kubwa ya Kisiasa, kutoaminiana na wakati mwingine hutawaliwa na mihemko ambayo imekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

Jaji Kaijage amewaeleza Wasimamizi hao kwamba wameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo za usimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wajiamini na kujitambua.Amaetoa wito kwa Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi na kuhakikisha kwamba wanawatumia vizuri wasaidizi walio nao katika maeneo yao kwa matokeo bora.

Kuanzia Septemba 5 Visimbuzi Kuonesha Channeli za Ndani Bure

$
0
0


Na  MAELEZO

Serikali imesema kuanzia septemba 5, mwaka huu visimbuzi vitaanza kuonesha channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.

Akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusu yaliyozungumzwa katika kikao kati ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo baada ya visimbuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV kutoonesha channeli za ndani, kulingana na aina ya leseni zao.

“Ningependa watanzania wafahamu kwamba kuanzia septemba 5 mwaka huu, visimbuzi vya TIN, Starmedia, Continental na Digtek vitaonesha takribani channeli 34 za ndani bure, ili kutoa fursa ya kila mwananchi kuwa na haki ya kupata taarifa” alisema Dkt. Abbasi.Aidha, alielezea kuwa wadau hao na wamiliki wa televisheni wameonesha kuridhishwa na hatua hiyo ya kwa vile Serikali imetengeneza miundombinu itanayoruhusu channeli zao kuonekana nchi nzima.

Dkt. Abbasi, alisisitiza kuwa “nchi imeandaa mfumo, ambao unaweza kufanyakazi bila kutegemea kampuni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuonesha channeli za ndani au matangazo, kwa hivyo wadau au wamiliki wa vyombo vya habari wasihofu kuhusu hilo”

Kikao kati ya Waziri Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini, kimefanyika kwa lengo la kuwa na majadiliano ya pamoja baina serikali na wadau hao ili kupata muafaka kuhusu kutooneshwa kwa chaneli za ndani katika visimbuzi vilivyokiuka masharti ya leseni zao.

Aidha, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia James Kilaba, pamoja na wataalamu wake.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi.
TCRA Wadau 3
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba.
TCRA Wadau 1
Baadhi ya wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi.

DKT MPANGO AWAAGA WATUMISHI WATANO WIZARA YA FEDHA WANAOKWENDA KUSOMA UINGEREZA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango amewaaga watumishi watano wa wizara hiyo wanaosafiri kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya ufadhili wa Masomo, uliotolewa na DFID Kupitia mfuko wake wa UKAID.

Akizungumza na Michuzi Media Group katika Mkutano wa kuwaaga watumishi hao, Waziri Mpango aliwataka Vijana hao kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutokubali kuyumbishwa na jambo lolote la ujanja kutoka kwa watu wa Mataifa mengine.

“Hii nafasi niliomba mimi kwa ajili ya watumishi wa Wizara muende kujifunza na hili ni kundi la pili ,hivyo naomba mkafanye kile kilichowapeleka kwani watanzania  zaidi ya Milioni Hamsinii wanategemea kuja kunufaika na ujuzi mlioupata kutoka huku ili muweze kuja kuendesha taasisi hii,ambayo ndio Ubongo wa uchumi wa nchi yetu” alisema Dkt. Mpango.

Dkt MPango alisisitiza kuwa yeye kama  Waziri anajivunia sana kuona Vijana wanapanua maarifa kwa kujiongezea elimu kutoka sehemu nyingine ,kwani kunasaidia kujiamini na kuzungumza kwa hoja za uhakika mbele ya umati wa watu.Alisema kuwa kama watalaamu wote hao kutoka wizara ya fedha watafanikiwa kufanya vizuri, watazidi kuiongezea sifa nchi yetu kuendelea kupata nafasi ya kupeleka vijana wengi kwenda kujifunza.

Ameweka wazi kuwa yeye atakuwa Waziri mwenye furaha sana kwa kuona kila idara katika Wizara yake ina vijana makini ambao ni weledi katika kazi zao.
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akizungumza na Vijana watano kutoka Wizara hiyo ambao wamepata ufadhili wa masomo nchini Uingereza 
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akisisitiza jambo kwa Vijana hao 
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akiagana na Vijana hao na kuwatakia Safari Njema
Wafanyakazi wa Wizara ya fedha , Sudah Joseph, Peter Kalugwisha,Morick Mwasagwa,Eliud Mkilamweni na Tunsume Mlawa wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango 
Waziri wa Fedha na Mipango , Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya Pamoja na Wanufaika wa Ufadhili wa Masomo wa DFID kupitia Mfuko wa UKAID

Muhimbili yapokea vifaa tiba

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea vifaa tiba 69 ambavyo vimefanyiwa matengenezo na kurejea katika viwango vyake vya matumizi.

Vifaa tiba hivyo (Screen) ambavyo vilikua chakavu vimetengenezwa upya na familia ya Bwn. Khakoo bila malipo yoyote, ambavyo hutumika kumsitiri mgonjwa akiwa kitandani huku akipatiwa huduma hospitalini na kwamba matengenezo yake yamegharimu shilingi milioni 2. 7.

Katika matengenezo hayo familia ya Khakoo imejitolea kulipa wafanyakazi , kununua vitambaa pamoja na mashono huku MNH ikiunga mkono jitihada hizo kwa kutoa mashine ya kuchomelea na vifaa vya kupakia rangi. Akipokea vifaa tiba hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameishukuru familia ya Bwn. Khakoo kwa msaada huo na kueleza vifaa hivyo ni muhimu kwa kutolea huduma hospitalini hivyo vitatumika kwa uangalifu.

‘‘Tunashukuru sana kwa msaada huu mkubwa kwakweli tumejifunza kwamba vifaa vilivyochakaa vinaweza kutengenezwa upya na vikakutumika tena, hili tumelichukua na tutalifanyia kazi kadiri  inavyowezekana’’.Amesema Prof. Museru. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa huduma za uuguzi, Sista Zuhura Mawona amesema kila wodi inahitaji screen 6 ambazo hutumika kumsitiri mgonjwa wakati akihudumiwa hivyo zitagawiwa kulingana na mahitaji.

Kwa upande wao familia ya Bwn. Khakoo imesema wameamua kutengeneza vifaa hivyo kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuboresha huduma za afya nchini na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo.

‘‘ Tuliviona vifaa hivi vikiwa chakavu tukaona kwamba kuna uwezekano wa kuvitengeneza na vikaendelea kutumika kwa wagonjwa , sisi ni watu binafsi tumeamua kama familia kujitolea na hivyo tumeokoa fedha nyingi takribani shilingi milioni 30. Amesema Bwn. Khakoo. Vifaa hivyo endapo vingenunuliwa vipya kimoja kingegharimu shilingi laki nne hadi laki tano. 



Familia ya Bwn. Khakoo ikimkabidhi vifaa tiba Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prf. Lawrence Museru mapema leo , kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma za uuguzi Sista Zuhura Mawona


Baadhi ya vifaa tiba (Screen) ambavyo hutumika kumsitiri mgonjwa wakati akipatiwa huduma.


Pichani ni vifaa tiba vilivyokuwa chakavu kabla ya kufanyiwa matengenezo na familia hiyo.
Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Bwn. Khakoo na baadhi ya wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Bwn. Khakoo akimuelezea Prof. Museru jinsi walivyofanyia matengenezo vifaa hivyo.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images