Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live

NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA DAR KUTATUA CHANGAMOTO ZA USARISHAJI MIZIGO

$
0
0
 Washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya semina iliyohusu kubadilishana uzoefu wa usafirishaji wa mizigo barani Afrika.
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Usaje Asubisye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya semina ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu usafirishaji wa mizigo kati ya nchi moja na nyingine barani Afrika.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
NCHI wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wamekutana Dar es Salaam kujadili na kubadilishana uzoefu wa kutatua changamoto hasa wanazokutana nazo katika usafirishaji mizigo kati ya nchi moja na nyingine.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Usaje Asubisye wakati anafungua semina kwa washiriki wa nchi hizo.

Amefafanua msingi wa kukutana kwao ni kujadili kwa kina kutatua changamoto zilizopo na lengo lao ni kuhakikisha nchi za Afrika zinashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi.

Ametaja baadhi ya nchi ambazo zimeshiriki semina hiyo ni Rwanda,Afrika Kusini ,Kameruni,Every Coast na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Amesema kuwa pamoja na mambo mengine watajadili namna ya kuboresha utoaji huduma ya kusafirisha mizigo na kwa Tanzania nayo itatoa uzoefu wake na namna ambavyo wamefanikiwa kuondoa changamoto.

“Afrika tunataka liwe bara ambalo litakuwa na uchumi imara na hivyo kwetu sisi kupitia semina hiii tutaangalia nini kifanyike ili tupige hatua,”ameongeza.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA KISIWA CHA GANA UKEREWE

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Gana wilaya ya  Ukerewe mkoa wa Mwanza ambapo aliwasisitiza polisi pamoja na mgambo wanapoenda kwenye operesheni ya kupambana na  uvuvi haramu wawewanaenda na maafisa uvuvi kwa kuwa wao wanajua zana haramu pamoja samaki wasioruhusiwa kisheria.
(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Naibi Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea katika kisiwa cha Gana Wilaya ya Ukerewe  kwaajili ya kuhamasisha ufungaji wa samaki kwa vizimba katika Vctoria.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wapili (kushoto) akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Lucas Magembe (kushoto) wakiwasili katika kisiwa cha Gana.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

MKANDARASI WA UJENZI WA FLY OVER YA TAZARA AWEKA REKODI YA AINA YAKE

$
0
0
*Atumia saa milioni 2.4 ya kazi bila kupata ajali.
*Mwakilishi JICA ataja vipaumbele miradi ya maendeleo


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWAKILISHI Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan(JICA) nchini Tanzania Toshio Nagase amesema Mkandarasi wa kijapani amefanikiwa kuweka rekodi ya usalama wakati wa ujenzi Fly over ya Tazara ambapo kwa zaidi ya saa milioni 2.4 ya kazi yamepita bila ajali.


Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea namna JICA wamekuwa wakishiriki katika kutoa misaada ya mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya miradi ya kimaendeleo.


Amefafanua JICA imekuwa inatekeleza miradi mbalimbali hapa nchini tangu mwaka 1963 na kwamba Watanzania 18,000 wamepata mafunzo Japan, wataalam 2,000 wa Japan wamekuja nchini.Pia watalaam wa kujitolea kutoka nchi hiyo 1600 wameletwa Tanzania kwa nyakati tofauti.


Hivyo wakati anazungumzia ujenzi wa Fly over hiyo amesema mkandarasi Japan ameweka rekodi kwani hadi sasa hakuna aliyepata ajali.


“Barabara ya juu ya kwanza yenye urefu wa mita 425 ambayo itakamilika Septemba mwaka huu.Msongamano wa magari kwenye makutano ya barabara yenye magari mengi hapa nchini utapungua kwa kiasi kikubwa.
 Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan(JICA) Ofisi ya Tanzania Toshio Nagase akizungumza leo jijini Dar es Salaam ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) Ilala, Dastani Ndamugoba  katikati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar ees Salaam leo kuhusu mradi wa umeme uliopo Muhimbili. Kulia ni Meneja wa Tanesco Ilala Mhandisi Sotco Nombo.
 Jinsi barabara ya flyover ilivyo.
Baadhi ya wajumbe kutoka JICA wakifurahia kukamilika kwa ujenzi wa Fly over ya Tazara jijini Dar es Salaam.


WACHEZAJI SITA WA SIMBA WAONDOLEWA TIMU YA TAIFA

$
0
0
Kikosi cha Taifa Stars.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Emmanuel Amunike amewaondoa kikosini wachezaji Sita(6) wa klabu ya Simba na mchezaji mmoja(1) wa klabu ya Yanga kwa kushindwa kuripoti kambini. 

Wachezaji walioitwa kwenye timu ya Taifa walitakiwa kuripoti Jumatatu jioni Agosti 27,2018 isipokuwa wachezaji wa Yanga wanaokabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na wale wanaocheza soka nje ya Tanzania.

Wachezaji walioondolewa kikosini ni Erasto Nyoni,Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Ramadhan Kichuya, John Bocco,Hassan Dilunga wote Simba na Feisal Salum wa Yanga.

Feisal ameondolewa kwa kushindwa kuripoti kambini kwa kuwa hakuongozana na klabu yake ya Yanga kwenda nchini Rwanda kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho kutokana na kutokuwa na leseni ya kucheza mashindano hayo hivyo alitakiwa kuripoti kambini kama alivyotakiwa. 

Wachezaji walioitwa kuziba nafasi hizo ni 
Salum Kimenya(Tz Prisons)Paul Ngalema,(Lipuli),Frank Domayo(Azam FC),Salum Kihimbwa(Mtibwa),Kelvin Sabato(Mtibwa)David Mwantika(Azam FC) na Ally Abdulkarim(Lipuli)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

Mzee Mwinyi amuombea dua na kumjulia hali Dkt. Kigwangalla MOI

$
0
0

RAIS Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi leo Agosti 29,2018 amemtembea na kumuombea dua maalum Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara.

Mzee Mwinyi aliambatana na Mkewe Bi. Siti Mwinyi ambapo wamemjulia hali pamoja na kufanya dua hiyo ili aweze kupona haraka kurejea kwenye majukumu yake ya kitaifa.“Nimefika leo kukujulia hali na upokee dua hii upone haraka. Sisi tunaendelea kukuombea muda wote kwa muumba” alieleza Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Dkt. Hamis Kigwangalla amemshukuru Mzee Mwinyi na Mama Mwinyi kufika kumjulia hali ambapo awali alimuelezea kuwa anaendelea vizuri na muda wowote ataruhusiwa.“Nashukuru kufika kwenu na sasa naendelea na mzoezi vizuri huku kubwa nikisubiria ruhusa ya Madaktari wanaoendelea kunipatia matibabu” alieleza Dkt. Kigwangalla.

Katika hatua nyingine kwa sasa Dkt. Kigwangalla afya yake imeendelea kuimarika zaidi ambapo jana jioni ya Agosti 28, ameweza kutembea umbali wa zaidi ya Kilometa Nane ambapo hii ni hatua nzuri kwani kila siku amekuwa akiongeza umbali wa kutembea kwa lengo la kufanya mazoezi ya viungo vyake.

Dkt Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiteta jambo alipomtembelea kumjulia hali Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono. Kushoto ni Mke wa Mzee Mwinyi, Bi. Siti Mwinyi.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeketi (katikati) akiongoza dua maalum kumuombea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla (kulia)ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono. Aliyekaa kushoto ni Mke wa Mzee Mwinyi, Bi. Siti Mwinyi.

FLYOVER YA TAZARA YAKAMILIKA KWA ASILIMIA 98-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemaujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara umekamilika kwa asilimia 98 na itafunguliwa Oktoba mwaka huu na Rais Dkt. John Magufuli.


Mradi wa barabara ya juu (Mfugale flyover) chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani, unalengo la kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere.Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29 ,2018) baada ya kukagua ujenzi wa mradi huowa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar Es Salaam. 

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa kazi ya umaliziaji wa mradi huo inayoendelea kwenye hilo.“Mradi utapunguza muda wa usafiri katika barabara ya Nyerere hususani kwa wananchi wanaotoka katikati ya jiji kwenda uwanja wa ndege na wanaotoka Buguruni, Temeke.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi Mkoa wa Dar Es Salaam watafute eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kuondoka kandokando ya barabara hizo za juu zinazojengwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe kuhusu barabara ya juu ya TAZARA wakati alipokagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara ya juu ya eneo la TAZARA wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale kuhusu ujenzi wa barabara ya juu ya eneo la TAZARA wakati alipokagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaaam, Paul Makonda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua hatua za mwisho za ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la TAZARA jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam Agosti 29, 2018. Watatu kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Wataalam wa afya kutoka Japan watembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

$
0
0
Wataalam wa afya kutoka nchini Japan leo wametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa Hospitali hiyo. 
Katika mazungumzo yao watalaam hao wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu wa utoaji huduma za afya na kujadiliana namna ambavyo wanaweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma . 
Mkurugenzi wa huduma za tiba Dkt. Hedwiga Swai amesema MNH ina mipango mbalimbali ya kuboresha huduma zake za ubingwa wa juu ikiwemo upandikizaji figo na kusisitiza kuwa huduma hiyo ni endelevu na imekuwa na mafanikio makubwa tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini Novemba mwaka jana . 
“Lengo letu ni kuhakikisha huduma za kibingwa zinakuwa endelevu lakini pia kama hospitali mipango yetu ni kuanzisha huduma zingine mpya ambazo hapo awali hazikuwepo”amesema Dkt. Swai.
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za tiba shirikishi Dkt. Praxeda Ogweyo amesema pamoja na mafanikio ambayo Muhimbili imepata lakini pia kuna changamoto ya upungufu wa watalaam katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma
 Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na wataalam wa afya kutoka Japan wakijadiliana juu ya utoaji wa huduma bora za afya .

 Mmoja wa wataalam kutoka  Japan Yoshio Mikamo akielezea ambavyo huduma za afya zinatolewa nchini humo.
 Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya Hospitali ya Taifa Muhimbili wakisikiliza  maelezo yanayotolewa na mtaalam huyo.

 Mkuu wa Idara ya Famasia MNH Deus Buma akiwaelezea wataalam hao kuhusiana na huduma za utoaji dawa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mara baada ya kutembelea moja ya  maduka ya dawa ya hospitali hiyo.

Meneja wa jengo la wagonjwa wa nje Sista June Samwel akifafanua  
huduma zinazotolewa katika jengo hilo

INTRODUCING "RINGA" BY DRAMA CHATTA FEAT BELLE 9 RINGA


Twanga Pepeta kusheherekea miaka 20 Septemba 29

$
0
0
Bendi kongwe nchini, The African Stars maarufu kama Twanga Pepeta imeandaa onesho maalum la kutimiza miaka 20 tokea kuanzishwa kwake Septemba 29. Bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1998, itafanya onyesho lake kwenye ukumbi wa Club Legends uliopo Namanga na maandalizi yake yameanza.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa sambamba na onyesho hilo, shughuli mbalimbali zitafanywa na wanamuziki wa bendi hiyo ikiwa pamoja na kutembelea ofisi za vyombo vya habari mbalimbali, kusaidia watoto yatima na wagonjwa.Baraka alisema kuwa kudumu kwa miaka 20 katika muziki wa dansi si kazi ndogo kwani kuna bendi nyingi zilizoanzishwa baada ya bendi yao kuanzishwa zimeshindwa kuendelea na shughuli za muziki. Bendi hiyo ilifanikiwa kuzindua albamu 14.

Alisema kuwa bendi yao imepitia changamoto nyingi kwa kipindi chote hicho ikiwa pamoja na kupanda na kushuka, lakini uongozi wa kampuni inayomiliki bendi hiyo, African Stars Entertainment Tanzania (Aset) ilisimama kidete kuhakikisha wanadumu katika soko la muziki tofauti na bendi nyingine.
“Miaka 20 si midogo kudumu katika shughuli za muziki, kwa kweli tumepitia changamoto nyingi sana, wanamuziki kuhama, soko la muziki wa dansi kushuka kutokana na mabadiliko ya sekta hiyo ikiwa pamoja na kuibuka kwa muziki wa kizazi kipya (bongo fleva), taarab na Singeli. Mashabiki walibadili muelekeo, lakini sasa mambo yamerejea,” alisema Baraka.

Alisema kuwa kwa miaka hiyo 20, wameweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwa pamoja na kuanzisha bendi nyingine kama African Revolution enzi ya Chumvi Chumvi mpaka Tam Tam na baadaye kubadilishwa jina na kuwa Vibration Sound.
“Pia tuliweza kuanzisha studio (Aset Production), gazeti (Zeze), kituo cha kuibua vipaji (Aset Academia) na kuibua wanamuziki nyota kama Totoo Kalala ambaye kwa sasa anatamba na bendi ua Bogos ya Musica na wanamuziki wengine wengi sana,” alisema.Alifafanua kuwa pia waliwekeza katika sekta ya filamu na kufanya kazi na waigizaji mbalimbali nchini ikiwa pamoja na marehemu, Steven Kanumba na wengineo huku wakisaidia wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya kupata maonyesho ya nje kama Uingereza na nchi nyinginezo.

“Bendi yenyewe ilifanya maonyesho nje ya nchi mbalimbali za Scandinavia kama Norway, Sweden, Denmark na Finland, pia bendi ilifanya maonyesho kadhaa nchini Uingereza na kushiriki katika tamasha la mfalme wa Oman,” alisema.
Mkurugenzi wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Asha Baraka (wanne kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana sherehe maalum ya miaka 20 ya bendi hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Club Legends, Namanga, jijini Dar es salaam Septemba 26, 2018. 

DKT SHEIN AIAGIZA BOT KUENDELEA KUSIMAMIA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kusimamia maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kuhakikisha hayajihusishi na utakasishaji fedha haramu.
Alitoa agizo hilo wakati alipofanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu, Prof. Florens Luoga na Manaibu Gavana, Bw. Julian Banzi Raphael, Dkt. Bernard Kibesse na Dkt. Yamungu Kayandabila Ikulu, Zanzibar tarehe 28 Agosti, 2018 walipokwenda kujitambulisha.
Dkt. Shein alisema kwa siku za karibuni, maduka hayo yamekuwa yakituhumiwa kujihusisha na utakasishaji wa fedha haramu, na amenesha kukerwa na matumizi makubwa ya fedha za kigeni (dollarization) hapa nchini na kuagiza suala hilo lishughulikiwe haraka.
“Haiwezekani tunapoenda Uingereza tulipe paundi na nchini mwetu pia watutake kulipa kwa paundi ya Mwingereza,” alisema Rais.
Rais huyo aliwasifu Gavana na wasaidizi wake kwa kusimamia ipasavyo masuala ya uchumi, hali inayochangia uchumi kukua vizuri.
“Si kazi rahisi kusimamia masuala haya ya uchumi kwani wenzetu wa nchi zilizoendelea wameanza siku nyingi sana, hatuwezi kujilinganisha nao,” Rais alisema.
Mapema katika maelezo yake, Gavana Luoga alieleza kwamba lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujitambulisha kwa Mhe. Rais na kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Benki Kuu na sekta ya fedha kwa ujumla.
Prof Luoga alimfahamisha Mhe. Rais kuwa Benki Kuu inaendelea kuwa  imara katika kutekeleza majukumu yake ya msingi na kwamba viashiria vyote vinaonyesha kuwa Taasisi iko vizuri.
Mathalani, kuhusu jukumu la msingi la Benki Kuu ambalo ni kuhakikisha kuna utulivu wa bei, kiashiria chake ni mfumuko wa bei, eneo ambalo hali nzuri, kwani lengo ni kuwa na mfumuko wa bei usiozidi asilimia 5. Akizungumzia sekta ya mabenki, Prof Luoga alisema; “pamoja na changamoto zake, hususan, uwepo wa mikopo chechefu, bado sekta hii ni thabiti na inasimamiwa vizuri. Benki Kuu imeshachukua hatua kadhaa za kudhibiti hali hii na inafuatilia kwa karibu kuhakikisha kuwa tunaondokana na tatizo hili la mikopo chechefu.”
Akizungumzia akiba ya taifa ya fedha za kigeni, Gavana alisema hali ni ya kuridhisha, kwani tuna akiba ya kutosha uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje za kukidhi kipindi cha miezi mitano.
“Aidha, mahusiano yetu na serikali ni mazuri sana kwa sababu tunaamini sera za kibajeti na sera za fedha ni vyema zisemezane”, aliongeza Gavana. Prof Luoga alimhakikishia Mhe. Rais kuwa yeye na viongozi wenzake wataendelea kuisimamia Benki Kuu kwa uadilifu na kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.
Akimjibu Prof Luoga, Mhe. Rais wa Zanzibar alianza kwa kuwashukuru viongozi hao kwa kumtembelea kwa ajili ya kufahamiana, na pia kubadilishana mawazo. Pia, alimshukuru Prof Luoga kwa kukubali uteuzi wa nafasi ya Gavana kwani angeweza kukataa.
Dkt. Shein alisema anafarijika sana kuona kuwa Benki Kuu ya Tanzania iko imara  na inazidi kutekeleza majukumu yake vizuri. “Nikiangalia tu nyuso zenu nawaona kabisa kuwa ninyi ni watu makini mtakaoisimamia vema sekta ya fedha, hivyo imani yangu kwenu ni kubwa sana,”alisema Mhe. Rais.Pamoja na viongozi hao wakuu wa Benki Kuu, ujumbe wa BoT uliwashirikisha Kaimu Mkurugenzi wa Tawi la BoT Zanzibar, Ndugu Suleiman Masudi, Msaidizi wa Gavana Dkt Nguling’wa Balele na Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bibi Zalia Mbeo.

H:\picha\Zanzibar\Picture 1.jpg

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akisalimiana na  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga alipotembelea Ikulu ya Zanzibar pamoja na Manaibu gavana jana.


H:\picha\Zanzibar\Picture 2.jpg

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akifafanua jambo kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga alipotembelea Ikulu ya Zanzibar jana.


H:\picha\Zanzibar\Picture 3.jpg

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akifafanua jambo kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga alipotembelea Ikulu ya Zanzibar pamoja na Manaibu gavana jana. Kutokea kushoto ni Dkt. Yamungu M. Kayandabila Naibu Gavana, Uchumi na Sera (EFP), Dkt. Bernard Y. Kibesse Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (FSD), Bw. Julian Banzi Raphael Naibu Gavana, Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC).


H:\picha\Zanzibar\Picture 4.jpg

Rais wa ZanzibarMhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Dkt. Yamungu M. Kayandabila Naibu Gavana, Uchumi na Sera (EFP) kwenye ziara ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga jana katika Ikulu ya Zanzibar.


H:\picha\Zanzibar\Picture 5.jpg

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Dkt. Bernard Y. Kibesse Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (FSD) kwenye ziara ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga jana katika Ikulu ya Zanzibar.


H:\picha\Zanzibar\Picture 6.jpg

Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Bw. Julian Banzi Raphael Naibu Gavana, Utawala na Udhibiti wa Ndani (AIC) kwenye ziara ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga jana katika Ikulu ya Zanzibar.

TCRA YASHIRIKI VYEMA WIKI YA ZIMAMOTO DODOMA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia) na Kamishna Jerenali wa Zimamoto, Thobias Andengenye wakisikiliza maelezo kutoka kwa ofisa Mwamdamizi wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mabel Masasi juu ya huduma za anuani za makazi zinavyoweza kusaidia utoaji haraka wa huduma za zima moto na uokoaji nchuni. Waziri Lugola alikuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya Zimamoto Nchini, iliyozinduliwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni miongoni mwa taasisi za serikali zilizoshiriki katika maonesho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji kitaifa ambayo inafanyika jijini Dodoma kwa mara ya kwanza nchini.

Lengo kuu la maadhimisho hayo ni kutoa elimu juu ya namna bora ya kuepuka majanga ya moto na kuwawezesha wananchi kuzifahamu vyema shughuli nyiongi zinazofanywa na jeshi hilo ambazo si tu kuzima moto kama inavyofahamika na wananchi wengi lakini ni pamoja na kusaidia katika majanga mbalimbali na ajali.

TCRA kama mdau mkubwa wa zimamoto mbali na kusaidia katika mawasiliano baina ya wananchi na Jeshi la Zimamoto kuwa rahisi na ya bure kwa mujibu wa sheria lakini pia kupitia mradi wao wa anuani za makazi unasaidia Jeshi hilo na wananchi kuweza kufikiwa kirahisi.

Ofisa Mwandamizi Mkuu wa Mawasiliano, Mabekl Masasi alimwambia Waziri Kangi lugola kuwa kupitia anuania za makazi zimeweza kurahisisha jeshi hilo kufika katika maeneo mengi kirahisi kwa kutaja jina la mtaa na namba ya nyumba la eneo husika. 
 Waziri wa Mambi ya Ndani, Kangi Lugola akiuliza jambo katika banda hilo la TCRA 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia) na Kamishna Jerenali wa Zimamoto, Thobias Ndengenye wakisikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) juu ya huduma za anuani za makazi zinavyoweza kusaidia utoaji haraka wa huduma za zima moto na uokoaji nchuni. Waziri Lugola alikuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya Siku ya Zimamoto Nchini, Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma jana.
Wananchi na maofisa mbalimbali wa Jeshi la Zimamoto wakiwa katika Banda la TCRA kupata vipeperushi na maelezo mbalimbali ya kazi za taasisi hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>

HOW TO CUSTOM: AF1 SICCKM8 Detailed Artwork Custom Time lapse | Power Rangers Megazord x Gundum

AFISA MIRADI UMOJA WA ULAYA AFANYA ZIARA SHINYANGA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WATOTO

$
0
0
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union - EU) John Villier amefanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni mkoani Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto la Save The Children.

Ziara hiyo imeanza Jumatano Agosti 29,2018 kwa Afisa Miradi huyo kukutana na wadau wanaoshiriki katika kutekeleza mradi huo wakiwemo viongozi wa serikali ya mkoa wa Shinyanga, Shirika la Save The Children na Shirika la Agape Aids Control Programme (AACP) ambao kwa pamoja wanaendelea kushirikiana katika kufanikisha mradi huo.

Akiwa katika ziara yake, John Villier pia amekutana na wanafunzi wa shule ya Msingi Mwamashele iliyopo kata ya Mwamashele kupitia “Tuseme Club” pamoja na kikundi cha watu wazima katika kijiji cha Itilima kata ya Itilima halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambao hukutana na kujadili namna ya kukabiliana na mila na desturi kandamizi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Villier alieleza kufurahishwa na jinsi mradi huo wa kutokomeza mila na desturi kandamizi unavyotekelezwa kwani umesaidia kupunguza mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akifanya mazungumzo na viongozi wa Shirika la Save The Children katika ofisi za Shirika hilo Mjini Shinyanga leo Jumatano Agosti 29,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akizungumza na viongozi wa Shirika la Save The Children na kuhoji masuala mbalimbali kuhusu Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni unaotekelezwa na Shirika la Save The Children kwa kushirikiana na Shirika la Agape Aids Control Programme (AACP) la Mjini Shinyanga wilaya ya Kishapu na Kahama mkoani Shinyanga.
Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akielezea namna jamii inavyoshirikishwa katika mradi huo ili kuufanya uonekane ni wa jamii na siyo wa shirika.
Katikati ni Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akielezea namna wanavyoshirikiana na shirika la AGAPE katika kutekeleza mradi wa Mila na Desturi Kandamizi katika mkoa wa Shinyanga. 

TAMASHA LA KWANZA LA MICHEZO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LAFIKIA TAMATI

$
0
0
Bw. Addo Komba Afisa kutoka Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo, akikabidhiwa kombe kufuatia ushindi timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania kwenye Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki lililofanyika Bujumbura, Burundi.

Tamasha la Kwanza la Michezo la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililokuwa likifanyika jijini Bujumbura limefikia tamati leo tarehe 29 Septemba, 2018. Hafla ya kufunga tamasha hilo ilihudhuriwa na Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchini Burundi.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Liberatus Mfumukeko alisema maadhimisho ya tamasha hilo yameleta tija kubwa katika kuleta na kuimarisha umoja na shirikiano, kuibua na kuendeleza vipaji mbalimbali vya wananchi wa Afrika Mashariki.

Mhe. Sindimwo Gaston Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, kwa upande wake amesema ni fahari kubwa kwa Burundi kuandaa tamasha hilo lililofanyika kwa kipindi cha wiki mbili. Aliongeza kusema washiriki wa wamichezo hiyo watakuwa mabalozi wa kuelezea sifa nzuri za amani na utulivu ulipo nchini Burundi tofauti na inavyosemwa na baadhi ya watu.

Katika tamasha hilo Tanzania imeshinda kombe moja la mpira wa miguu wa wanawake ,medali ya fedha katika riadha, mpira wa pete na karatee.

Tamasha hili lilifanyika kuanzia tarehe 16 hadi 29 Agosti 2018, katika Jiji la Bujumbura na Gitega nchini Burundi. 
Kikundi cha ngoma ya asili ya nchini Burundi kikisherehesha kwenye hafla ya kufunga Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki. 
Bw. Liberatus Mfumukeko Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (kulia) akikabidhi kombe kwa mkuu wa msafara wa Uganda. 
Bw. Liberatus Mfumukeko Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki akizungumza katika sherehe za kufunga Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki 
Wachezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa miguu Tanzania wakionyesha furaha yao ya kupata kombe baada ya kuibuka washindi katika mchezo huo kwenye Tamasha la Michezo la Afika Mashariki 

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO AGOSTI 29, 2018


WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto ,Dar es Salaam 

Hivi karibuni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ilitoa msamaha maalum wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 50 ya hapo awali. 

Msamaha huu umetokana na malalamiko ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwa Mhe. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli ya kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 19 Machi, 2018. 

Kufuatia malalamiko hayo, Rais aliwaambia wafanyabiashara hao kuzungumza na Wizara ya Fedha na Mipango ili waweze kupunguziwa riba na adhabu za madeni yao ya kodi. 

"Suala la kodi ni very sensitive (nyeti sana) hata Rais unaweza kushtakiwa kwa kukwepa kodi, mimi niwaombe wale mnaodaiwa kwa miaka ya nyuma nendeni mka-negotiate (mkajadiliane) na Wizara ya Fedha, ninajua kuna kipengele ambacho kinaweza kuwapunguzia", alisema Rais Magufuli. 

Dk. Magufuli alitumia baraza hilo pia kuwasisiza wafanyabiashara kulipa kodi ambapo alisema "Tunahitaji kodi kwa ajili ya survival (kudumu) ya nchi hii, mtu ajue kwamba kulipa kodi ni wajibu wake na kukwepa kodi is a big crime (kosa kubwa). Hivyo ninawaomba wafanyabiashara msikwepe kulipa kodi, mjitahidi kulipa kwa maana kodi hizi ndio zinatusaidia kuijenga nchi yetu". 

Baada ya mkutano huo wa baraza la biashara, Bunge la Tanzania katika kikao chake cha bajeti cha Mwaka wa Fedha 2018/19 cha mwezi Juni, 2018 lilipitisha marekebisho ya Kifungu cha 70 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Fedha ya kutunga kanuni maalum za kutoa msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi ya nyuma. 

Kupitia marekebisho hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, alimpa Mamlaka Kamishna Mkuu wa TRA kutoa msamaha maalum wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 50 ya awali. 

Ni kufuatia mamlaka hayo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere alitangaza msamaha huo maalum mnamo tarehe 11 Julai, 2018 kwa lengo la kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kuwapa fursa ya kulipa kodi ya msingi (principal tax) mara moja au kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza msamaha maalum wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 jijini Dar es Salaam Julai, 2018. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo Richard Kayombo. 

Global Winners Announced for ‘SDGs and Her” Competition for Women Micro-Entrepreneurs Helping to Achieve the SDGs

$
0
0

Today the global SDGs and Her Competition announced its inaugural 2018 winner chosen from over 1,200 entries. The contest -- co-sponsored by the World Bank Group, the Wharton School Zicklin Center, UNDP, and UN Women -- showcases women micro-entrepreneurs helping to achieve the Sustainable Development Goals (SDGs) through their business operations.

The winning entry is Tanzania-based WomenChoice Industries owned by Lucy Odiwa. Her micro-enterprise seeks to empower women and girls in Tanzania by promoting safer menstrual health hygiene management (MHM), sharing information, products, and related services. The lack of MHM products often affects the ability of low-income women and girls to attend school and to work, Odiwa says. WomenChoice Industries produces reusable sanitary pads, post-partum maternity pads, child and adult diapers, and promotes MHM in schools to promote quality education for all, helping Tanzania to achieve SDG target 3.7 (Women’s health), and SDG target 4.1 (Girls’ access to education).

The second-place winner is Mukuru Clean Stoves of Kenya, owned by Charlot Magayi, which recycles waste metal to produce improved, reliable, and affordable cook stoves to reduce indoor air pollution, which is a major health challenge in the developing world.  Her business addresses SDG8 (Decent Work), SDG1 (End Poverty), and SDG3 (Good Health).
Odiwa and Magayi will be flown to New York City this September to attend the UN General Assembly and to discuss their work and impact, and may also receive leadership training and mentoring from partner organizations. Over 1,200 entries from 88 countries were submitted, and while nearly half of the entries were from Sub-Saharan Africa, submissions were received from every region of the world, including Latin America and the Caribbean, South Asia, the Middle East and North Arica, Europe and Central Asia, and East Asia and the Pacific. The SDGs and Her competition seeks to increase knowledge about the SDGs and their potential impacts on women, as well as to collaborate with private sector partners, and share best practices and innovative ideas.

SDGs and Her is open to women who own and/or lead microenterprises, have nine or fewer employees, and which have loan eligibility under USD $10,000 or annual sales under $100,000.  Applicants completed a short online template, describing their work and linking their initiative/product to one or more SDGs. Entries will be accepted for the 2019 competition between September 24 and December 31, 2018. Winners will be announced in early 2019.

The winners were chosen based on their impact on the SDGs, vision and purpose, and clarity of the entries. The final judging panel included: Administrator of the United Nations Development Programme, Achim Steiner; United Nations Under-Secretary-General and Executive Director of UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka; World Bank Group Senior Vice President, Mahmoud Mohieldin; Lecturer and Senior Fellow, Zicklin Center for Business Ethics Research at Wharton School, Djordjija Petkoski; Senior Director for Gender at the World Bank Group, Caren Grown; and Head, Gender Secretariat, International Finance Corporation, Henriette Kolb.

In 2015, all 193 United Nations member countries signed on to 17 Sustainable Development Goals (SDGs) to "create the future we want in 2030." To learn more about the SDGs, the SDGS and Her Competition, or to enter, click here or visit worldbank.org/sdgs.

PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI

$
0
0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wataalmu wa somo la Hisabati katika kongamano la tano la Hesabu lililofanyika nchini kwa kuandaliwa na Chuo Kikuu cha Agha Khan.
 
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Walimu wa Somo la Hisabati nchini wanaongezeka hili kuweza kukidhi mahitaji ya walimu hao katika shule za Msingi na Sekondari.

Profesa Ndalichako amesema hayo alipokuwa akifungua Kongamano la tano la Wakufunzi wa Hisabati kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Agha Khan hapa nchini.

“Mkutano huu umekutanisha wataalamu kutoka Afrika na Nje ya Afrika kwa lengo la kuongeza jitihada za kuimarisha mbinu za ufundishaji wa Hisabati , hivyo tunataka kuongeza walimu wa hesabu hapa nchini lakini tumekuwa na upungufu wa vijana wanaomaliza elimu yao ya sekondari ambao ni wataalamu wa Hisabati hivyo nyie muende kuhamasisha vijana wakapende hesabu hili tuweze kupata mzunguko mzuri wa wataalamu wa hesabu kila mwaka”amesema Ndalichako.

Amesema hali ya uchache wa utayari wa vijana wanaojitokeza kuja kusoma hesabu imekuwa chanzo cha upungufu wa walimu wa somo hilo nchini hivyo Serikali ipo katika mpango kabambe wa kuhamasisha watoto wakasoma hesabu na kufanya vizuri katika masomo yao wakiwa darasani.

Waziri Ndalichako amesema kuwa ukiboresha ufundishaji wa somo la hesabu utasaidia kuboresha masomo mengine kwani masomo mengi yanategmea utalaamu wa hesabu kufanikisha ufaulu.

Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kupokea maoni ni namna gani itaweza kuboresha mfumo wa utoaji wa elimu hasa kwa somo la hesabu hili kuweza kuongeza ufaulu katika shule za serikali.

Ametaja kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli imeweza kuleta mfumo wa elimu bure kwa kutoa elimu ya kiwango cha hali ya juu na sio bora elimu hivyo walimu ni vyema wakathamini mchango unaotolewa na serikali ya awamu ya tano kwa wanafunzi kwa kumuunga mkono Rais wetu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akisalimiana na baadhi ya magwiji wa Hesabau waliofika katika mkutano huo.
Sehemu ya Washiriki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Chuo Kikuu cha Agha Khan wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano hilo

RAIS DKT MAGUFULIA KUFANYA ZIARA MIKOA MITATU

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, atafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kati ya tarehe 3 na 10  Septemba, 2018.


HAKI MADINI WAJENGEA UWEZO JAMII WA ARDHI NA MADINI

$
0
0
SHIRIKA la Haki Madini la jijini Arusha, limewajengea uwezo viongozi wa serikalini, wa kimila na baadhi ya wananchi wa mikoa ya kanda ya kaskazini, juu ya utambuzi wa uthamini wa fidia ya ardhi na madini. 

Mwanasheria wa shirika la Haki Madini, Erick Luwogo akizungumza mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro,  alisema kupitia mafunzo waliyotoa, elimu ya fidia ya ardhi na madini itaifikia jamii ipasavyo. 

Luwogo alisema wanataka kuona changamoto ya ucheleweshaji wa fidia, isiyo sahihi na kukatazwa kufanya maendelezo zinapatiwa ufumbuzi kwa haraka. 

"Tumekutanisha wadau wengi wakiwemo wanasheria, wenyeviti wa vijiji, watendaji wa vijiji, viongozi wa kimila, jamii na lengo hasa ni kupata majawabu ili serikali inapotoa fidia iwe inafanya kwa wakati," alisema. 

Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Anthony Mavili alisema miradi mingi mikubwa ya eneo hilo imefanyika lakini wananchi ambao waliathirika kwa namna moja au nyingine hawakufidiwa. 
 Baadhi ya viongozi wa serikali, wanasheria na wananchi walioshiriki kwenye warsha ya sheria ya fidia ya ardhi na madini iliyoandaliwa na shirika la Haki Madini, mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. 
 Baadhi ya walioshiriki warsha hiyo mwanasheria wa TLS Linda Shamba (kushoto) na mhandisi wa madini Ernest Sanka.
 Mmoja kati ya wawezeshaji wa warsha hiyo, mthamini mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha, Rosemary Kirenga (kushoto) na mwanasheria wa shirika la Haki Madini, Erick Luwogo wakizungumza na washiriki wa warsha hiyo. 
Mkazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Anthony Mavili akizungumza juu ya fidia kwenye warsha ya sheria ya fidia ya ardhi na madini iliyoandaliwa na shirika la Haki Madini mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro. 
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live




Latest Images