Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 244 | 245 | (Page 246) | 247 | 248 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu  akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo baada ya uzinduzi  wa kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kitengo hicho kipo katika  Jengo la Coco Plaza karibu ya ufukwe wa Coco Beach jijini humo.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya  (kulia) akisalimiana na Meneja wa Tawi la NBC Sea Cliff, Mariam Kombo  katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya  (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Idara Huduma za Kibenki kwa Wateja  Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya NBC, Andre Potgieter katika hafla  iliyoandaliwa na benki hiyo baada ya uzinduzi wa kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu na wa pili kulia ni mteja wa benki hiyo, Paul Chizi.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa  cha NBC, Andrew Massawe akizungumza katika hafla hiyo. Pamoja naye ni  baadhi ya maofisa katika kitengo hicho cha wateja binafsi wakubwa.
  Mmoja wa wateja wa NBC, Paul Chizi akiipongeza Benki ya NBC kwa jitihada za kuanzisha kitengo maalumu cha kuhudumia wateja wakubwa (Private Banking).
  Wasanii wa kikundi cha sarakasi cha Mama Afrika wakitoa burudani  katika hafla hiyo.

  0 0

  Timu ya KMKM ya Kisiwani Pemba ikifurahia ushindi wake wa Ngao ya Jamii,mara baara ya kuifunga timu ya Chuoni mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini ya mchezo kwa kufunguma bao 1-1.Mchezo huo ulipigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu ya Grand Malt,Zanzibar.
  Mgeni Rasmi katika Mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar na kuwaniwa kwa Ngao ya Jamii,Waziri wa Serikali ya Mapinduzi asiekuwa na Wizara Maalum,Mh. Haji Faki Shaali (wa pili kushoto) akikabidhi Ngao ya Jamii kwa Nahodha wa timu ya KMKM,Ame Hamis Kibobeo mara baada ya kutwaa Ngao hiyo kwa kufunga timu ya Chuoni kwa mikwaju ya penati 5-4,katika mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.
  Kikosi cha Timu ya Chuoni FC
  Kikosi cha Timu ya KMKM.
  Beki wa Timu ya Chuoni akijaribu kutaka kuondosha hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake.
  Mshambuliaji wa Timu ya KMKM,Juma Mbwana (8) akijaribu kutaka kumtoka Beki wa Timu ya Chuoni,Mwinyi Haji wakati wa Mchezo wao wa kuwania Ngao ya Jamii,uliochezwa jana Usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.hadi mwisho wa mchezo timu ya KMKM ilishinda kwa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati.

  0 0


  Hii imekaaje wadau. Ni maeneo ya Posta Mpya hio... 
  Ah, lakini iko siku tutafika tu
  Mdau WM

  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete with the Federal President of Austria H.E. Heinz Fischer (left) and the President of the European Commission H.E. Jose Manuel Barroso walk towards the congress centre of the European Forum Alpbach 2013 for the closing session of the annual event in Alpbach, Austria, over the weekend.
  President Jakaya Mrisho Kikwete with the Federal President of Austria H.E. Heinz Fischer, the President of the European Commission H.E. Jose Manuel Barroso walk pose for a group photo with students who have benefited from the European Forum Scholarship Programe at the congress centre of the European Forum Alpbach 2013 shortly before the closing session of the annual event in Alpbach, Austria, over the weekend.
  President Jakaya Mrisho Kikwete, the Federal President of Austria H.E. Heinz Fischer and the President of the European Commission H.E. Jose Manuel Barroso chat with students who have benefited from the European Forum Scholarship Programe at the congress centre of the European Forum Alpbach 2013 shortly before the closing session of the annual event in Alpbach, Austria, over the weekend.
  President Jakaya Mrisho Kikwete addresses participants at the congress centre of the European Forum Alpbach 2013 during the closing session of the annual event in Alpbach, Austria, over the weekend.

  MORE PHOTOS,CLICK HERE

  0 0

  Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa kwa kwa kutoa huduma na bidhaa za uhakika hususani huduma ya intanet.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na TTCL kwa ajili ya wateja wake wa mkoa wa Mwanza.

  Amesema TTCL ndio mhimili mkuu wa mawasiliano hapa nchini na ni ukweli ulio wazi kuwa Watanzania wengi wanaiona TTCL kuwa tegemeo lao la kwanza katika Mawasiliano hapa nchini

  Aidha amesema “pamoja na huduma bora za mawasiliano mnazotoa, bado mna changamoto ya kuboresha zaidi mtandao wenu kwani kuna baadhi ya maeneo ambayo hayana mtandao wa TTCL hivyo kuwanyima fursa wananchi wazalendo kutumia huduma hii ambayo pia ni ya kizalendo ili kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Tunatambua juhudi mnazofanya katika kuwafikia wateja zaidi maeneo ua vijijini, tafadhalini ongezeni kasi katika jambo hili.”

  Akijibu baadhi ya maoni kutoka wateja, Afisa mkuu wa masoko na mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Bw. Peter Ngota amesema pamoja na mafanikio mengi tuliyoyapata TTCL, bado tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na Wizi au hujuma katika njia zetu za mawasiliano yaani nyaya na mikonga ya simu katika maeneo mbali mbali mkoani hapa na kusababisha wateja wetu kukosa mawasiliano na kupata usumbufu usio wa lazima.

  Mbaya zaidi kuna baadhi ya maeneo hapa Mwanza wamefikia hatua kutumia nyaya za TTCL kujiunganishia umeme kwa njia zisizo halali, jambo ambalo ni hatari kwa uhai wao na watu wanaowazunguka pia wanaisababishia kampuni na taifa hasara kubwa kupitia hujuma hii.

  Kukatika mara kwa mara kwa Mkongo wa taifa kunakosababishwa na shuguli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara n.k. ; tunawaomba wananchi wa Mwanza kuachana na vitendo vya hujuma na kuwa waangalifu wakati wa shughuli zao za kijamii na maendeleo ili kuepuka uharibifu kwenye njia za mawasiliano.

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amesema, akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa mwanza, atahakikisha miundombinu ya TTCL inalindwa kwa kuwaagiza vyombo vya usalama kuhakikisha mtandao huu hauhujumiwi ili kuleta maendeleo kwa wateja na wa TTCL na wananchi kwa ujumla.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo akiongea na wateja wa TTCL.
  Afisa mkuu wa masoko na mauzo wa TTCL Bw. Peter Ngota akiongea na wateja wa TTCL katika hafla hiyo.
  wafanyakazi wa TTCL katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo.
  Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na ujumbe alioongozana nao.
  mgeni rasmi akiongea na mameneja wa TTCL kutoka mikoa mbalimbali kwa kutumia "Bongo phone" katika huduma ijulikanayo kama "Conference call" ambayo iliwavutia wateja wengi waliohudhuria hafla hiyo. anayefuata baada ya mkuu wa mkoa (kulia) ni Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Mhe. Halifa Hassan Hida.

  0 0

   The Chairperson East African Cement Association Pascal Lesoinne stresses a point during a Seminar to discuss the Contribution of the Construction sector to the country’s Economic Development that brought together various stakeholders in Dar es Salaam at the weekend. 
   The Chairperson East African Cement Association Pascal Lesoinne stresses a point during a Seminar to discuss the Contribution of the Construction sector to the country’s Economic Development that brought together various stakeholders in Dar es Salaam at the weekend. 
   The Chairperson East African Cement Association Pascal Lesoinne stresses a point during a Seminar to discuss the Contribution of the Construction sector to the country’s Economic Development that brought together various stakeholders in Dar es Salaam at the weekend. 
  The Chairperson East African Cement Association Pascal Lesoinne stresses a point during a Seminar to discuss the Contribution of the Construction sector to the country’s Economic Development that brought together various stakeholders in Dar es Salaam at the weekend. 
  =======   ========  ============
  Government pledges to improve investment environment

  By Staff Reporter.

  THE Government has pledged to support various investment initiatives in the country as part of its plan to attract more investment opportunities in the country. Speaking during a seminar to discuss the role of the Cement Industry in Tanzania’s economic Development held in Dar es Salaam at the weekend, the Deputy Principal Secretary at the Ministry of Finance prof. Adolf mkenda said creating good investment climate would help the country increase it’s Gross Domestic Product (GDP.

  “The Ministry of Finance understands the challenges facing the cement industry that includes poor infrastructure networks, stiff competition and cement imports. “We will continue working with other government ministries and agencies to ensure that the cement sector continues playing a pivotal role in the country’s economic development process,” he said.

  He said the cement sector for the last five years has been growing at an average of 9 percent with its contribution to the country’s Gross Development Process (GDP) increasing from 7.7 percent in 2008 to 8.1 percent in 2012.

  “The cement industry has also grown simultaneously from a total production of 2,409,000 tons in 2011 to 3,425,991 tons in 2012. If all the cement produced in the country is sold within in the country without exporting , total cement production can meet up to 75 percent of the country’s total demand.

  The Deputy Director Marine Transport Services in the Ministry of Transport Deogratius Mukasa during the event said his ministry has put in place a mechanism to enhance security at all the country’s various entry points and ports entry points. He however called upon various stakeholders to join the war on fighting importation of substandard and illegal goods if the problem is to be solved.

  “We will continue to work hand in hand with other line ministries but all stakeholders including public should effectively play their part if we are to win the war,” he added.

  The TPCC Managing Director Pascal ring the event called upon the Government to put in place additional anti-dumping and countervailing duties that will help check influx of sub-standard imported goods entering the Tanzanian market including cement.

  “Importers have with the cooperation of unscrupulous Government officers used loopholes in the Port and Customs systems to avoid paying statutory taxes and duties, by under-declaration of import prices and  quantities. “Instead of 25 % duties and 18 % VAT, they end-up paying 5 to 10 % duties and 3 to 5 % VAT,” he said.

  He added that if action is not taken fast, it would lead to a complete collapse of blue-chip companies in Tanzania and the associated loss to the local economy with huge negative consequences on employment and image of Tanzania as an investment destination.

  0 0


  0 0

  It is one year exactly since you were called to glory from this world. Your untimely departure clouded our hearts with untold sadness and grief. Your death reminded us of a phrase from the Canticle of Prophet   Isaiah  that says ”My dwelling is plucked up and removed from me like a shepherd’s tent; Like a weaver I have rolled up my life ; he cuts me off from the loom.”

  As we pray for you on this day you are fondly remembered by your beloved Wife Proscovia Atugonza, you Son David and your daughter Doreen. Together with them your brothers and sisters Evans Maro, Aggy Maro,Freddy Maro,Hilder Maro, Robert Maro and Edith Maro and so many of your friends and relatives.

  “Show Raymond your merciful  love, Lord, give him eternal rest.
  Amen”.

  0 0

   Wakizundua rasmi bia ya Tusker Lite kanda ya ziwa katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijiniMwanza, kutoka kulia ni Meneja mipango na masuala ya habari wa Kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombella, Meneja wa vinywaji vya Tusker Sialuoise Shayo, Meneja mipango na Ugavi wa SBL kanda ya ziwa Dilip Chudasama na Meneja mauzo wa kanda Octavian Migire(wa kwanza kushoto). 
   Burudani murua kabisa ilitolewa na bendi.
   Baadhi ya viongozi wa idara ya masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiwaonesha wageni waalikwa(hawapo kwenye picha) chupa ya bia ya Tusker Lite  katika hafla ya uziduzi wa bia hiyo kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza, kutoka kulia ni Meneja mipango na masuala ya habari wa Kampuni ya bia yaSerengeti Bi Nandi Mwiyombella, Meneja wa vinywaji vya Tusker, Bi Sialuoise Shayo, Meneja mipango na Ugavi wa SBL kanda ya ziwa na Meneja mauzo wa kanda Octavian Migire(wa kwanza kushoto).
   Timu nzima ya mauzo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kanda ya ziwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa  bia ya Tusker Lite kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza.

  0 0

  Airtel Tanzania inatangaza uteuzi wa Bw. Frank Filman kuwa mkurugenzi wa kitengo cha teknolojia ya IT aliyechukua nafasi hiyo rasmi kuanzia sasa

  Filman ambaye ni mtanzania alianza kazi Airtel akiwa kama munagalizi wa system (system Admistrator) na baadaye alipanda cheo na kuwa Meneja wa Mradi wa Technolojia ya IT. Kutoka mwaka 2007 mpaka 2009, alikuwa Meneja wa kitengo hicho nchini Ghana ambapo alisimamia na kutoa mchango mkubwa uzinduzi wa mtandao wa Airtel nchini Ghana.

  Mwishoni mwa mwaka 2009 Filman alirejea Tanzania akiwa kama Meneja wa Huduma za kimtandao (Network service Manager ) za Airtel Tanzania.

  Baadaye alijiunga na kitengo cha mauzo na kama meneja wa Techonologia na biashara na huko aliweza kuchangia ongezeko la mapato kwa kiasi kikubwa hadi kufikia 100% kwa mienzi 12 tu.

  Katika miaka yake 12 na Airtel, Filman amefanya kazi miaka miwili Airtel Ghana na zaidi ya miaka tisa akiwa na Airtel Tanzania.

  Akizungumzia juu ya uteuzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema "Uteuzi wa Filman kuwa Mkurugenzi wa kitengo cha Teknolojia ya IT ni ushahidi wa dhamira ya Airtel Tanzania kuendeleza, kulea na kukuza vipaji vya wafanyakazi wake ndani ya nchi. Sisi tunayo furaha kubwa kuona Watanzania wanachukua majukumu makubwa katika moja ya makampuni yanayokuwa kwa kasi na nyeti kama hii.Teknolojia ya IT ni msingi muhimu wa mafanikio katika mawasiliano ya simu kwa sababu huduma zetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha yaani Airtel Money na internet zinategemea teknolojia hiyo."

  Aliendelea kwa kusema Kampuni imemteua Bw. Filman ikiwa na uhakika kwamba ataifanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kabisa.

  "Tunaamini Bw. Filman atafanya vyema kazi yake kutokana na uzoefu alionao lakini vilevile Airtel itaendeleza dhamira yake kuwaendeleza na kuwawezesha wafanyakazi wengine kushika nyazifa kama hizi nchini na kwenye nchi nyingine za Afrika na Asia ambapo Airtel inafanya biashara. pia Airtel tutaendelea kuwapa mafunzo wafanyakazi wetu ambayo yatawafanya wawe kwenye viwango vya kimataifa" Alisema Bw. Golaso.

  Akizungumzia uteuzi wake Filman alisema, "Nimekuwa nikitamani kupata nafasi hii na nilijua siku moja naweza nikaipata na ninayofuraha kupata wadhifa huu Airtel Tanzania . kwa miaka mingi nimepitia mafunzo mbalimbali, na nina uzoefu nilioupata nchini Ghana pamoja na nchi nyingine Airtel inayofanya biashara. Hivyo niko tayari na nimejiandaa vyema kukabiliana na changamoto zote katika utendaji wa kazi hii na kuhakikisha natoa huduma zenye ubora kwa watanzania."

  Airtel tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kitamaduni , kasi ya kazi na kibiashara. Airtel imewekeza katika kukuza uwezo wa wafanyakazi na kutoa nafasi ya kukuza fani ndani ya kampuni. Mafunzo ya ujuzi daima imekuwa ni mikakati yetu inayoendana sambamba na ujuzi unaohitajika kimataifa alisema bw Sunil Colaso mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania

  Airtel imeweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake ili kuhakikisha wafanyakazi wa Airtel wanatoa huduma bora za kitaalamu kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kumekuwa na fursa ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wafanyakazi wa Airtel Tanzania katika vitengo vya masoko, Mauzo, IT, pamoja na kuwa na mfumo wa kuwapeleka baadhi ya wafanyakazi wake nchi tofauti kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa kufanya kazi kwa mienzi 6 hadi 18 katika Airtel Afrika na India.

  Airtel pia imekuwa ikiendesha mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wa mauzo, masoko na huduma kwa Wateja kupitia Chuo Kikuu cha Centum . Ambapo wafanyakazi wamekuwa wakipewa ujuzi na maarifa muhimu yanayowasaidia kutoa huduma bora kwa wateja ambazo zinaleta maendeleo makubwa na kuonesha utofauti katika soko la ushindani la mawasiliano ya simu.

  0 0

  Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akimsikiliza Bi. Dina Lemmens akimweleza matarajio yake ya kutembelea vivutio mbalimbali Tanzania. Bi. Dina akiongozana na Kikundi cha Watalii saba watatembelea Tanzania na wakirudi Watashirikiana na Ubalozi kuitangaza Tanzania Ubelgiji. Bi. Dina akifuatana na Bi. Doreen Mwansi walimtebelea Balozi Kamala ofisini kwake, Brussels - Ubelgiji leo.

  0 0

  WANAFUNZI waliojitokeza katika Maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), hususani katika Fao la Urithi.

  Fao hilo lililowafurahisha mno wanafunzi hao, linawawezesha watoto wenye umri chini ya miaka 18 hadi 21 kunufaika, huku likiwawezesha kupata asilimia 60 ya mgao wa mwanzo endapo mtegemezi anapofariki.


  Akizungumzia sababu zinazowafanya wanafunzi kuifurahia huduma ya Fao la Urithi, Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga alisema kuwa fao hilo limekuwa mkombozi kwa wanafunzi kwa kuwawezesha katika elimu pindi mtegemezi anapofariki, hivyo kuwanufaisha watoto walio mashuleni. 

  "Mwanachama endepo akifariki asilimia 60 ya mgao wa mwanzo unakwenda kwa watoto wasiozidi 4 wenye umri chini ya miaka 18 hadi 21 ambao wapo mashuleni  kwa ajili ya kujiendeleza kielimu, hii imewafanya wengi miongoni mwa wanafunzi kuvutiwa na huduma hiyo," alisema Kapinga.

   NSSF imeanzisha matibabu ya bure kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambapo imeingia mkataba na hospitali za vyuo kupitia Fao la SHIB, ambalo linamuwezesha mwanafunzi wa chuo kupata huduma za matibabu bure, endapo mwanafunzi atachangia sh. 20,000 kwa mwezi. 

  NSSF pia hutoa mikopo ya Elimu kupitia Saccos ambapo wanachama wanaweza kukopa kuanzia milioni 50 hadi bilioni 1.
  Wanafunzi wakipata maeleo mbalimbali kuhusiana na Fao la Urithi, ambalo linamuwezesha mtoto chini ya umri wa miaka 18 hadi 21 kupata asilimia 60 ya mgao wa mwanzo wa ambapo ,wanachama atafariki kwa ajili ya kumuwezesha katika elimu.
   Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dk.  Didas Masaburi, kuhusu Fao la Urithi ambalo linamuwezesha mwanafunzi kupata asilimia 60 ya mgao wa mwanzo endapo mtegemezi atafariki kwa ajili ya kumuwezesha katika masomo yake,  wakati wa Maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 yaliyofanyika kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Ofisa Matekelezo NSSF, Rose Kayombo. 
  Kutoka kulia ni Ofisa Matekelezo NSSF, Rose John Kayombo, Ofisa Idara ya Kompyuta, Grace Magigita na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na Madaktari wa Jamuhuri ya Uturuki mara baada ya kuwashukuru kufuatia kukamilisha mpango wao wa kutoa huduma mbali mbali za afya ukiwemo upasuaji hapa Zanzibar.
  Mdhamini wa Madaktari wa Uturuk waliokuwa wakitoa huduma za Afya hapa Zanzibar Profesa MuratTuncer wa Chuo Kikuu cha Hacettepe Nchini Uturuki akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada kukutano na madaktari hao katika ukumbi mdogo wa Jumba la Wananchi Forodhani Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Wasanii wa Muziki wanaounda kundi la Kigoma All Stars (Leka Dutigite) wakiwapagawisha Mashabiki wao waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma wakati wa Tamasha la Muendelezo la Kili Music Tour 2013 lililofanyika mwishoni mwa wiki. 
  Barnaba akifanya mambo yake.
  Mkali wa RnB,Muite Ben Pol akionyesha kujikubali kwake wakati wa Tamasha la Kili Music Tour 2013,lililofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
  Mkali wa Hip Hop kwa Mwaka 2012/13,Kala Jeremier akionyosha ukali wake kwa Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wakati wa Tamasha la Kili Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.
  Fid Q akiwapa kitu roho inapenda wakazi wa Kigoma.
  Ni Shangwe tupu kwa Wakazi wa Kigoma.


  0 0

  Tunayofuraha kukupa taarifa rasmi kuwa Tasnia ya Filamu Tanzania sasa imepata tamasha la kuonyesha sinema za kiswahili (Bongomovies). Tamasha litafanyika tarehe 24-26, Septemba 2013, Katika Viwanja Vya Posta-Kijitonyama. Pia Workshop, Exhibition na Film Forum vitafanyika. 

  Kiingilio ni Bure!!!! Samabaza Ujumbe kwa wapenzi wa filamu. kwa habari zaidi tembelea www.filamucentral.co.tz

  0 0


  Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (19) akipozi kwa p[icxha mara baada ya kuibuka mshindi wa taji hilo na kuwa mrembo wa kwanza kutinga nusu fainali za Miss Tanzania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29 katika shindano hilo dogo kuelekea fainali za Redd’s Miss Tanzania 2013. 

  ********   ********
  Mrembo wa Mkoa wa Dodoma,  na mwakilishi wa Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa, juzi amenyakua taji la Redds Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa  mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2013. 


  Happiness amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2013.

  Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki kutoka magazeti ya Serkali Daily News, Habarileo na Spotileo.

  Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha wa Jambo Leo Richard Mwaikenda na Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Aika Kimaro.

  Dalili za kuonesha kuwa Happiness amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na warembo ulilipuka kwa kwashangwe.

  Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda na Happiness Watimanywa aliyeibuka mshindi.

  Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Septemba 7 mwaka huu, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.

  Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.

  Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na mrembo Lucy Stephano kutoka Manyara na Kanda ya Kaskazini, kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa. 

  Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar es Salaam Septemba 21,2013.
  Mrembo Happiness Watimanywa akiwa amekubwa na butwaa baada ya kutajwa Mshindi wa Redd's Miss Photogenic 2013. 

  Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa (katikati) akipozi kwa picha na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya kumsaka mshindi wa taji la Miss Photogenic 2013. Kutoka kulia ni Anastazia Donald ,Latifa Mohamed, Clara Bayo na Jacline Luvanda.

  0 0
 • 09/02/13--06:39: KUMBUKUMBU
 • TUNAKUKUMBUKA MAMA YETU MPENZI MAMA JOYCELYNE MKAMSURI SAWAYA MAWALLA- MAREALLLE

  MAMA LEO TAREHE 2 SEPTEMBA 2013 UMETIMIZA MIAKA MITATU TANGUULIPOAGA DUNIA. HATUNA LA KUSEMA ILA MAMA TUNAKUKUMBUKA SANA KWA UPENDO NA UCHESHI WAKO NA PIA UKARIMU WAKO. SISI WANAO TUNAJIULIZA KWA NINI ILIKUKUWA MAPEMA HIVYO? LAKINI HATUNA LA KUSEMA KWANI KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA.

  UNAKUMBUKWA SANA NA WATOTO WAKO EMILY NA LEONARD. PIA MKWE WAKO CAROLYNE.

  WAJUKUU ZAKO VANESSA AMBAYE ULIKUWA UKIMUITA DOKTA, JOYCELYN AMBAYE UL IKUWA UKIMUITA INJINIA, NA EVA AMBAYE PIA ULIKUWA UKIMUITA DOKTA MUNGU AKIPENDA MAJINA HAYO ULIYOKUWA UKIWAITA WAJUKUU ZAKO NA IWE KWELI.

  PIA UNAKUMBUKWA SAAANA NA NDUGU ZAKO WA UKOO WA SAWAYA MAWALLA, WATOTO WA KAKA ZAKO NA DADA ZAKO NA MARAFIKI ZAKO WOTE NA MAJIRANI ZAKO WA DRIVE INN ESTATE PUMZIKA KWA AMANI MAMA!

  0 0

  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha mchezaji Henry Joseph wa Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

  Tayari Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Taifa Stars ambayo iko chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu, na leo jioni itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

  Programu ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho (Septemba 3 mwaka huu) itafanya mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Karume.

  Wakati huo huo, kesho (Septemba 3 mwaka huu) saa 6 kamili mchana Kocha Kim Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari.

  LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI CL
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Coton Sport ya Cameroon na Esperance ya Tunisia.

  Mechi hiyo ya kundi B itachezwa Septemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Omnisport Roumdeadjia mjini Garoua, Cameroon. Kamishna atakuwa Bema Doumbia wa Ivory Coast.

  Waamuzi wanatoka Madagascar wakiongozwa na Hamada Nampiandraza. Wasaidizi wake ni Jean Eric Pierre Andrivoavonjy, Ferdinand Velomanana Linoro na Bruno Marie Andrimiharisia.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akipokelewa na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali Mhe. Ludovick Uttoh, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC Mhe. Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa SADCOPAC Mhe. Sipho Makama kutoka Afrika Kusini alipokuwa akiwasili katika Ukumbi wa AICC Arusha kufungua Mkutano wa Mwaka wa SADCOPAC kwaniaba ya Rais Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC Mhe. Zitto Kabwe akitoa salam za ukaribisho kwa wajumbe wote wa SADCOPAC.
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa Mwaka wa SADCOPAC katika ukumbi wa AICC mjini Arusha.
  Wajumbe wa mkutano wa SADCOPAC katika mkutano huo leo.


  0 0

   A minister sharing some jokes before the official  opening of the Conference.
  Minister Getting Brieafings from ISACA President before officially opening the Conference.
   A Minister in a jovial modies with  the CEO of NRD East Africa (Left) Mr Sebastian Marondo and Tanzania ISACA President Mr Boniface Kanemba.
   Cross Section of Cyber Security Participants  following the opening Ceremony
   Group Photo

older | 1 | .... | 244 | 245 | (Page 246) | 247 | 248 | .... | 3272 | newer