Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 245 | 246 | (Page 247) | 248 | 249 | .... | 3284 | newer

  0 0
 • 09/02/13--08:06: Article 2


 • 0 0

  Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Diana Melrose akitoa hotuba fupi kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani uliofanyika leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Mfuko wa Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani(WHO).
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akiwasilisha Mada kuhusu uimarishwaji wa Miundombinu ya Usalama Barabarani katika Mkutano wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani. Kamishna Jenerali wa Magereza alikuwa ni Miongoni mwa Wadau walioalikwa kushiriki katika Mkutano huo wa masuala ya Usalama Barabarani kutokana na Jeshi la Magereza kuwa lipo mbioni kufungua Kiwanda cha kutengeneza Kofia ngumu katika Gereza Kuu Ukonga.
  Baadhi ya Washiriki mbalimbali na Wadau wa Masuala ya Usalama Barabarani wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano wa siku moja wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani uliofanyika leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Diana Melrose(wa pili kushoto) akisikiliza mada fupi iliyowasilishwa na Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani Tanzania, DCP. Mohammed Mpinga katika Mkutano wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani uliofanyika leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
  Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Usalama Barabarani wa Kamisheni ya Usalama Duniani, Saul Billingsley(wa kwanza kulia),Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani Tanzania, DCP. Mohammed Mpinga(wa pili kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Masuala ya Usalama Barabaran, Kelvin Watkins leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Masanja Mkandamizaji afunguka alipolonga na Vijimambo kuhusu kudaiwa kuhusika na madawa ya kulevya na kuhusu kushikiliwa kwa Passport yake na Serikali, MSIKILIZE

  Hii ndio Nyumba ya Ghorofa ya Masanja Mkandamizaji inayomhusisha na madawa ya kulevya

  0 0

  IMG_5252
  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akifungua warsha siku tano kwa Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika inayosisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwenye shughuli na majukumu ya Umoja wa Mataifa katika za Kusini mwa Afrika yenye ujumbe wa Delivering As One (DAO) kutoa matokeo ya pamoja katika kuratibisha na kuboresha majukumu ya Umoja wa Mataifa katika nchini hizo.
  Akifungua warsha hiyo Dk. Kacou amesisitiza umuhimu wa mkutano kuwapa jukwaa wafanyakazi wote wa Ofisi za waratibu wakazi jinsi ya kujielimisha na kupata habari ya mabadiliko ya Dunia na majukumu ya Kikanda yanayoendana na maboresho ya kuratibu shughuli za Umoja wa Mataifa wenye lengo la kuleta matokeo ya pamoja.
  Alisema warsha hiyo itawajengea uwezo kwa washiriki umuhimu wa kujenga mazoea ya kujielimisha kimkakati na stadi za kazi zenye kuleta ufanisi katika kusaidia kuleta mabadiliko ya kazi za Umoja wa Mataifa katika nchi za Kusini mwa Afrika.
  Dk. Kacou ameongeza katika kuleta matokeo ya pamoja Waratibu wakazi wanajukumu la kuhakikisha Haki za Binadamu na Mashirika yanayotetea Haki za Binadamu yanapewa wigo mpana katika kushiriki kwenye mchakato wa Demokrasia na Haki za Binadamu.
  Amefafanua kuwa Mkutano huu unafanyika Tanzania kwa sababu ni nchi iliyoonyesha mafanikio katika nyanja hizi za Kiuchumi, Kisiasa, Demokrasia na Haki za Binadamu.
  Warsha hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Kikanda cha Maendeleo Umoja wa Mataifa (UNDG) Mashariki na Kusini mwa Afrika ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya kuchukua na kupeleka mbele mabadiliko ya kimkakati yanayoleta matokeo ya pamoja.
  IMG_5294
  Kamishina Msaidizi wa Bajeti Wizara ya Fedha Bw. Jerome Buretta akizungumza kwenye majadiliano ya warsha hiyo kwamba Serikali ya Tanzania iliamua kuingia katika mpango huu wa matokeo ya pamoja(DAO) na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ili kuleta ufanisi katika nyanja mbalimbali ambazo zinafadhiliwa na Umoja wa Mataifa hapa nchini.
  Bw. Buretta amesema katika mpango huo inaiwezesha Serikali kukaa pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kupanga Bajeti na matumizi ya fedha zitolewazo na nchi wahisani ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya kwenye jamii.
  IMG_5266
  Baadhi ya Maofisa kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku tano iliyoanza leo jijini Dar.
  IMG_5304
  Kwa upande wake Kansela wa Mambo ya Siasa Ubalozi wa Norway nchini Bi Elisabeth Schwabe Hansen amesema kwamba nchi yake ya Norway ni mdau wa muda mrefu wa maendeleo nchini Tanzania katika kuhakikisha maboresho na mipango ya Umoja wa Mataifa yanapitia katika mkondo sahihi kuhakikisha miradi ya maendeleo na ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Tanzania unaleta matokeo ya pamoja.
  Bi. Hansen ameongeza kuwa katika mipango hiyo ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ni kuhakikisha inajenga uwezo wa rasilimali watu na kuratibu programu za Umoja wa Mataifa ambazo zinaendana na dira ya maendeleo ya Taifa.
  IMG_5333
  Mmoja wa Afisa kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akibadilishana uzoefu juu ya Programu hii ya matokeo ya pamoja kwa baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
  IMG_5338
  Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
  IMG_5216IMG_5213IMG_5313
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria ufunguzi wa warsha ya Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa Mashariki na Kusini mwa Afrika inayoendelea jijini Dar katika Hoteli ya Kunduchi Beach Resort.
  IMG_5380
  Mwezeshaji wa warsha hiyo Bi. Jacqueline Olweya kutoka UNDG (kushoto) akimsindikiza Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou (katikati) kwenda kupata picha ya pamoja na washiriki. Kushoto ni Mkuu wa uendeshaji na ushauri wa Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanazania Bw.George Otoo.
  IMG_5389
  Washiriki wa warsha ya siku tano ya Waratibu Wakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka nchi 21 kutoka Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi wa warsha hiyo leo.

  0 0

  Mr. Robert Kahendaguza, the Acting Director of the Department of Regional Cooperation in the Ministry of Foreign Affairs welcomes Hon. Minister Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation to deliver the final report of the SADC Observer Mission to the Zimbabwe Elections (SEOM), earlier today in Harare.
   Hon. Minister Membe explains about the Zimbabwean elections as they were free, peaceful and credible as he delivers the final report of the SADC Electoral Observer Mission in Zimbabwe earlier today at the Rainbow Towers Hotel and Conference Centre in Harare. 
  Listening on are Cabinet Ministers and Members of Diplomatic Corps that include Hon. Simbarashe Mumbengegwi (4th left), Foreign Minister of Zimbabwe.   
  Also in the audience is Ambassador Adadi Rajab (right) of the United Republic of Tanzania in Zimbabwe.

  Ambassador George Mwanjabala (first left), former Ambassador of Tanzania to Zambia. Sitting behind is Mr. Isaac E. Mwakiluma(right), Minister Plenipotentiary at the Tanzania Embassy in Zimbabwe.

   Retired Ambassador David Kapya (2nd right) and Dr. Harold Utouh (3rd right). 

  Minister Membe addresses the audience during the press conference. 

  Commenting on is one of the members of the Zimbabwean Electoral Commission.

  Hon. Simbarashe Mumbengegwi, Foreign Minister of Zimbabwe shares few laughters with Zimbabwean Electoral Commission Chairperson Justice Rita Makarau (right) and Deputy ZEC Chair Joyce Kazembe (center).

  Minister Membe exchanges views with one of the members of Diplomatic Corps in Zimbabwe.
  Hon. Membe shares a moment with one of the ZEC members and one of the members of the Diplomatic Corps. 
   Foreign Ministers from Tanzania and Zimbabwe took time to exchange views after the delivery of the Final REport on Zimbabwe's Elections.
  For more photos CLICK HERE

  By Tagie Daisy Mwakawago
  Harare, Zimbabwe
  “We want to reiterate again that the harmonized elections of the 31st of July were free and expressed the will of the people,” said Tanzania Foreign Minister Bernard K. Membe earlier today while delivering the SADC final report on the Zimbabwe’s Elections.

  He further explained that President Robert Mugabe won the elections with flying colors, despite the media polarization and the delay of voters roll. 

  Minister Membe was speaking at a press conference that was also attended by cabinet ministers, representatives of political parties and members of the diplomatic corps who had gathered at the Rainbow Towers Hotel and Conference Centre in Harare to witness the delivery of the SADC Election Observer Mission to Zimbabwe final report of which he was a Leader.

  This SADC final report comes after the preliminary report issued on the 2nd of August 2013, which was issued by Minister Membe on behalf of the then Chairperson of the SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation, President Jakaya Mrisho Kikwete.

  “As you may recall, the main message in the preliminary report was that the elections in Zimbabwe were free and peaceful,” explained Hon. Membe. Previously, the SADC observer mission for the 31 July elections judged the vote as free and peaceful, but had not yet commented on its fairness and credibility aspect until today.

  The Minister arrived yesterday night in Harare International Airport, and was received by Zimbabwean Foreign Minister Simbarashe Mumbengegwi and other Senior Government Officials.  The chief goal of the trip was to submit the Southern Africa Development Community (SADC) Electoral Observer Mission final report, based upon the presidential elections that took place on July 31st, 2013.  Tanzania was a former Chair of the SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation under the Chairmanship of His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Repulic of Tanzania. 

  “We were required as chair of the monitoring team of the SADC Election Observer Mission to deliver a report outlining the outcome of the process and also commending the nature of the elections,” said Hon. Membe.   The report will be delivered today at 10 a.m. local time in Harare.

  President Robert Mugabe had landslide won the elections with 61 percent of the presidential votes and 76 percent of the parliamentary seats, leaving behind MDC-T Leader Mr. Morgan Tsvangirai with 33 percent.  The win extends President Mugabe yet another five years in addition to the already 33-year rule.

  Zimbabwean opposition leader Morgan Tsvangira’s MDC party had recently withdrawn a legal challenge to the elections, claiming the courts would not be fair.

  Answering reporters questions regarding the fairness of the elections, Minister Membe said that the SEOM has put forth a wide range of recommendations that include the need for the state media to provide equal opportunity to all competing parties in future elections.  “There must be a fair and balanced reporting,” highlighted the Minister.

  On the issue of pirate tv and radio stations, Minister Membe strongly condemned the interference of the political process by broadcasters outside Zimbabwe.

  Previously, the African Union Election Mission Head Olusegun Obasanjo, former Nigerian President called the Zimbabwe election as free and peaceful.   

  Meanwhile, the Southern African Heads of State and Government recently endorsed the Zimbabwe elections during the 33rd Summit in Lilongwe, Malawi and called for the lifting of the sanctions against Zimbabwe. 

  SADC had deployed 573 observers to monitor the Zimbabwe elections, whereby it endorsed the elections as free and peaceful and that it had wholly reflected the will of the people of Zimbabwe.

  0 0

  Mjumbe Maalum  wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika  Kanda ya Maziwa Makuu,  Bi. Mary  Robinson
  Na Mwandishi Maalum

  Kufuatia  kurejea tena kwa  mapigano makali yaliyotokea wiki iliyopita kati ya majeshi  ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  ( FARD) yakisaidiwa na  Jeshi la MONUSCO  na kundi la   waasi  la M23. Umoja wa Mataifa sasa  unajaribu kutafuta suluhu ya kidiplomasia inayolenga katika kujaribu  kuweka sawa hali ya mambo.

   Mapingano  hayo ambayo  siyo tu  yanasadikiwa kuliondoa kundi la M23   katika ngome yake ya vilima vya  Kibati  Magharibi ya Kivu.   Yamelaaniwa vikali na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu  Ban ki  Moon hasa baada ya kundi hilo la M23 kusababisha  kifo cha  mwanajeshi Mtanzania na kujeruhi wengine kumi wakiwamo wanajeshi  kutoka Afrika ya Kusini.

   Mchakato huo wa   kisiasa  unafanywa  na Mjumbe Maalum  wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika  Kanda ya Maziwa Makuu,  Bi. Mary  Robinson, ambaye amewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya  jumapili na kutoa  rambirambi zake kwa wahanga wa  mapigano hayo.

  Taarifa kutoka  ofisi ya  Mjumbe huyo Maalum, inataarifu kwamba, Katika  mchakato huo wa kutafuta suluhu ya  kidiplomasia ,  Mary  Robinson ataongoza ujumbe  maalum utakaowahusisha  Mwakilishi wa  Umoja wa Afrika,  Bw. Boubacar Diaraa,  Bw. Russ Feigold, ambaye ni Mjumbe  Maalum wa Serikali ya  Marekani katika Eneo la  Maziwa Makuu, Bw. Martin Kobler Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu  katika DRC na  Mkuu wa MONUSCO, wakati Jumuiya ya Ulaya itawakilishwa na  Mratibu Mwandamizi katika Maziwa Makuu,  Bw. Koen Vervaeke.

  Kabla ya kuungana na ujumbe huo, Bi. Mary Robison atafanya mazungumzo  ya ndani na washirika wa Umoja wa Mataifa katika DRC na kisha atakwenda Goma  kama hatua ya kuonyesha mshikamano wake na  wananchi wa eneo hilo na  Jeshi la Kulinda  Amani  la Umoja wa Mataifa  ( MONUSCO).

  Kwa mujibu wa Ofisi ya   Bi Mary Robison    ziara ya Mjumbe huyo na ujumbe wake,   pamoja na kutembelea DRC pia watakwenda  Uganda na Rwanda   kati ya  Septemba 4-7, ambapo  pamoja na mambo mengine  watakutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa na Mashirika ya Kiraia  pamoja  na kuhudhuriwa  kikao cha  dharura  cha Mkutano wa Kimataifa wa   Kanda ya Maziwa Makuu  ( IGCLR).

  Taarifa hiyo inabainisha kwamba akiwa katika nchi hizo, Bi. Mary Robinson atasisitiza haja na umuhimu wa pande zinazohusika kusitisha vitendo vya  uhasama na kuelekeza nguvu  zao katika majadiliano ya kisasa  pamoja na mchakato wa Kampala  ( Kampala Process).

  Aidha  inaelezwa  kwamba wakati Bi. Robison na ujumbe wake watakapohudhuria mkutano wa  IGCLR   utakaofanyika  Septemba   5 jijini Kampala,  watahimiza uharaka wa utekelezaji wa  Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama na maendeleo katika DRC na Eneo la Maziwa Makuu,  mpango ambao ulisainiwa mapema mwaka huu  na  nchi 11 na wadhamini  wanne wa kimataifa .

  Ziara hiyo  ya Bi. Mary Robison na ujumbe wake inafuatia  kurejea upya kwa mapigano makali katika eneo la  Mashariki ya DRC   mapigano ambayo yameifanya  hali  ya mambo katika eneo la Maziwa  Mkuu kuwa tete, huku  kukiwa na ongezeko kubwa la wakimbizi, hali inayochagiza uharaka wa  kutafuta suluhu ya kisiasa ili kurejesha hali ya  utengamano katika  DRC na eneo la Maziwa Makuu.  0 0
 • 09/02/13--21:41: kijiwe cha ughaibuni

 • 0 0


   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akifungua warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) jijini Dar es salaam.
   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo jijini Dar es salaam.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Usawa na Uwezeshaji wa Wanawake jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwemo waheshimiwa Majaji wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa warsha hiyo ya siku 1.
   ke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) , mama Salma Kikwete (kulia) akiagana na viongozi wa Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania mara baada ya kufungua wa warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.
  Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

  0 0

    
  Mike Mhagama "enzi" zake akiwa studio za Radio One Stereo/ Picha kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Mike Mhagama Michael Pesambili Mhagama ni mmoja wa watangazaji wa awali waliojikita katika harakati za kuutambua, kuuboresha na kuupa hadhi muziki ambao sasa unatambulika kama BONGO FLAVA. 
   Pia ndiye aliyeanzisha JINA hilo la Bongo Flava. Jumamosi ya Aug 31, 2013, alifanya mahojiano na JAMII PRODUCTION na kueleza mengi kuhusu Muziki huu wa Bongo Flava Ameeleza harakati zao kuuweka kwenye ramani ya muziki nchini, matatizo yanayoukabili, mafanikio na hata ambapo angependa kuuuona ukifika na kuwafikisha wahusika wake. 
   Unajua jina BONGO FLAVA lilipotoka na lilivyotokea? Alikabiliana vipi na UTATA WA MUASISI WA JINA BONGO FLAVA? Lakini je, ni yeye muasisi wa harakati za kuwa na muziki huu radioni? Anauonaje muziki huu? Unakua ama? Wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki huu nchini ni upi? Karibu uungane nasi NB: Tunaomba radhi kwa ubora wa sauti katika sehemu za mahojiano haya

  0 0


   Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART), ya Strabag, wakiwa nje ya lango kuu la kuingilia makao makuu ya kampuni hiyo, Ubungo, Dar es Salaam asubuhi hii baada ya uongozi wa kampuni hiyo kuwafungia nje, kutokana na mgomo wa kudai maslahi zaidi kufanyika jana.
  Chanzo BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  Washiriki  wa  tamasha  la  11  la mtandao  wa  jinsia  Tanzania (TGNP) wakishiriki maandamano  ya amani ya  maadhimisho ya miaka 20 ya  mapambano ya   ukombozi  wa  wanawake kimapinduzi makao makuu ya taasisi hiyo Mabibo, jijini Dar es salaam.  Kwa picha zaidi na Francis Godwin BOFYA HAPA
   Waadamanaji  hao  wakiwa na mabango  yenye  ujumbe  mbali mbali leo

  0 0

  Mkurugenzi wa kampuni ya Free Mind Events yenye makazi yake jijini Dar es Salaam, AbdulMalik Fundikira akiwa na Mzee Maiko, mmoja kati ya walezi wa kituo cha New Hope, kilichopo Mjimwema, Kata ya Ungindoni, eneo la Kigamboni jijijni Dar es salaam ambapo jana kampuni yake ilifungua mwezi Septemba kwa kula chakula cha mchana na watoto hao
   Chakula kilipikwa na kampuni hiyo inayotoa pia huduma ya Catering, hapa Malik akionesha chakula na kukionja kuhakikisha kwamba ni salama kwa kuliwa
   Hapa ni maandalizi yakiendelea, Abdul Malik, na Anna Mwakatundu ambao ni wakurugenzi wa kampuni ya Free Mind Events wakiwa washughulikaji wakuu
   Msosi fresh, pamoja na watoto
   Baadhi ya watoto wa kituo cha New Hope wakiendelea na msosi

  0 0

  Timu ya Travelport ikiongozwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Travelport, Eliasaph Mathew (wa kwanza kulia msitari wa mbele).
  Timu ya Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Sauda Rajab (katikati).
   Timu ya Travel Agent nayo ilishikiriki kikamilifu.
  Timu ya Simbanet nayo haikuwa nyuma.
  Ilikuwa ni mchaka mchaka kwa timu ya Simbanet (aliyevaa jezi nyeupe) akimpelekesha mchezaji wa timu ya Precision Air.
   Kampuni ya Travelport mwishoni mwa wiki iliandaa bonanza la kuzimisha miaka 15 tokea kuanzishwa kwake lililofanyikia katika viwanja vya Don Bosco Osterbay jijini Dar. Katika bonaza hilo kulikuwemo na michezo mbali mbali ambao iliweza kuwashirikisha makampuni mbali mbali ambao ni wadau wao wakiwemo, wadau mbali mbali wakiwemo Precision Air, Simbanet, Travel Agent.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Precision Air, Sauda Rajab akitoa zawadi ya kikombe kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Travelport, Eliasaph Mathew ambaye alikuwa ni kapteni wa timu hiyo. Timu ya Travelport alishinda timu zote na kujinyakulia ubingwa huo.

  KUONA PICHA ZAIDI ZA BONANZA HILO BOFYA HAPA 

  0 0

  Na Veronica Kazimoto – MAELEZO,Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Penina Mlama (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari - MAELEZO leo, Uteuzi huo wa Profesa Mlama unaanzia mwaka 2013 na unatarajia kumalizika mwaka 2016.

  Prof. Mlama ni Profesa wa Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Aidha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla watu 12 kuwa wajumbe wa BASATA kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka huu.

  Walioteuliwa ni pamoja na wawakilishi wa Vyama na Asasi mbalimbali wa Baraza hilo ambao ni Dkt. Vincensia Shule, John Kitime , Angela Ngowi, Dkt. Herbert Makoye, Erick Shigongo na Alex Msama.

  Wawakilishi wengine ni pamoja na Juma Adam Bakari, Daniel Ndagala, Michael Kadinde na Joyce Fisoo. Wanaoingia kwa mujibu wa nyadhifa zao ni Prof. Hermas Mwansoko na Katibu Mtendaji wa BASATA.

  Katika hatua nyingine Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua Bwana Ghonche Materego kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

  Kabla ya uteuzi huo Materego alikuwa amemaliza muda wake kama Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa.

  Wajumbe wa Bodi hiyo walioteuliwa na Waziri Mukangara ni Dkt. Herbert Makoye, Prof. Emanuel Mbogo, Dkt. Lucy Mboma, Prof. Hermas Mwansoko pamoja na Katibu Mtendaji wa BASATA.

  Wakati huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla ya watu 21 kuwa wajumbe wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

  Wajumbe hao ni Dkt. Shani Omari, Prof. Yohana Msangila, Ester Riwa, Dkt. Issa Zidi, Khadija Juma na Dkt. Martha Qorro.

  Wengine ni Mmanga Mjawiri, Razia Yahaya, Richard Mbaruku, Selina Lyimo, Keneth Konga, Amour Khamis, John Kiango, na Shani Kitogo.

  Wajumbe wengine ni Ally Kasinge, Ahmed Mzee, Rose Lukindo, Shabani Kisu pamoja na Edwin Mgendera. Taarifa hiyo imefafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la BAKITA atachaguliwa na wajumbe watakapokutana kwenye kikao chao cha kwanza.

  0 0
 • 09/03/13--02:55: Article 12


 • 0 0

  Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu akifungua kikao cha Pamoja kati ya Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na ,Maafisa wa Mikopo kutoka vyuo vya Elimu ya Juu nchini, katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl-Ubungo, Dar Es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo Bw. Onesmus Laizer, akiwasilisha mada katika kikao hicho.
  Afisa Mikopo wa Taasisi ya Elimu Ya Watu wazima, Bw. Beny Mwenda akichangia katika kikao kazi kati ya Maofisa Mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
  Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bi.Sophia Nchimbi, akiuliza swali katika kikao hicho.
  Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), akichangia mada katika Kikao hicho.
  Picha ya Pamoja kati ya Maafisa Mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo, Aliyekaa katikati ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof .Sylvia Temu, na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Bw. George Nyatega.

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imefanya kikao kazi na maafisa Mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo- Dar Es Salaam na kuazimia kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuboresha shughuli za utoaji mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

  Kikao hicho kilikuwa kwa ajili ya kupitia yaliyojiri mwaka uliopita, kufanya maandalizi na kuwekana sawa kwa mwaka wa masomo 2013/14, ambao kwa vyuo vingi utaanza mwezi Oktoba, 2013.

  Awali akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu, aliipongeza Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kwa utendaji wake mzuri wa kazi licha ya changamoto nyingi wanazokumbana nazo.

  ` `Serikali inapongeza utendaji wenu mzuri wa kazi kwa mwaka wa masomo ulioisha kwani tumeshuhudia utulivu kwenye vyuo vyote na kwamba hakuna migomo iliyojitokeza. Aidha tunatambua changamoto ni nyingi lakini bado hamkukata tamaa katika kuleta ufanisi na kufikia malengo’’, alisema Prof. Temu.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. George Nyatega ameishukuru serikali kwa namna ambavyo imeendelea kuipa Bodi ushirikiano kwa kutoa fedha kwa wakati na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha utoaji wa mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya juu unafanyika kwa ufanisi..

  Maafisa Mikopo walielezea changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika utendaji kazi wao ikiwemo ya ugumu wa kuwasilisha taarifa kwa mfumo unaopendekezwa na Bodi.

  Katika kutatua tatizo hilo, Menejimenti ya Bodi imeandaa mfumo wa kompyuta utakaowezesha shughuli zote za uwasilishaji au upatikanaji wa taarifa za wanafunzi kupitia katika mtandao huo kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa pande zote zinazohusika na mikopo ya wanafunzi.

  0 0


  0 0

  The First Instance Division of the East African Court of Justice today, dismissed a Matter filed by Alcon International Limited (Kenya) against Standard Chartered Bank Uganda Limited for not paying them for the construction of a building known as Workers House in Kampala, Uganda.

  Alcon International Limited (K) came to court claiming an award of $8,858,469, with interest and costs, which was made in favor of Alcon International (Uganda) by an arbitrator and adopted by the High Court of Uganda. The award arose from a contract between the Government of Uganda and Alcon International Limited (K) who later sub-contracted Alcon International Limited (U) to finish the construction of the Workers House building, leading to a dispute about which Alcon Company should be paid for the work done.

  Court said that, it cannot give itself jurisdiction in a case outside its jurisdiction on the ground that it would be for the convenience of the Parties and witnesses. Also Court found that there was no merit in the reference before it hence dismissed it and ordered that each party to bear their costs.

  EACJ First Instance Division had previously dismissed the case by Kenyan construction company, Alcon International (K) Limited, on grounds that the matter was improperly before the Court. However the Appellate Division noted that the First Instance Division did not in its ruling consider whether it had jurisdiction to entertain the matter, which was a fundamental issue which the Court had to decide on.

  The Applicant brought the case to court under article 29 (2) and Article 54 (2) (b) of the protocol on the establishment of the East African Community Common Market of the on protection of Investors across the border, emphasizing that the alleged sister construction company Alcon International Uganda does not exist.

  Also the Registrar today ruled on a preliminary objection raised by Counsel for the Respondent in a case for costs in an Appeal filed by Alcon International Limited (K) against The Standard Chartered Bank and 2 others.

  The Appeal was allowed and they were awarded costs to be taxed by the Registrar. The Registrar ruled that the court was not functus officio (a general rule that, a final decision of a court cannot be reopened) and that he did not make a final decision in this matter when it came up for taxation. The Registrar ordered that the matter proceeds for taxation and that the parties will be notified of the date.

  0 0

  SERIKALI ya Ujerumani imetoa msaada wa Euro milioni nane (sawa na sh: bilioni 17.6) kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi unaojihusisha na Utafiti wa kutambua mikakati bunifu ya kuimalisha usalama wa chakula kwa kutumia teknolojia na upelekaji wa maarifa kwa wakulima vijijini ( TRANS – SEC) katika Mkoa wa Dodoma na Morogoro.

  Mradi wa utafiti huo wa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka huu na umelenga kuwajengea uwezo wakulima kwa kutumia utafiti shirikishi ambao utatoa fursa za utekelezaji wa malengo yatakayowanufaisha wakulima 4,000 kutoka vijiji viwili katika Wilaya ya Kilosa, Morogoro na vingine viwili vya Wilaya ya Chamwino , mkoani Dodoma.

  Mratibu wa Mradi huo wa Trans – Sec nchini Tanzania, Dk Khamaldin Mutabazi, alisema hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti wa Mazao kutoka Idara ya Utafiti na Maendeleo ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika, Dk Hussein Mansoor , kuzindua rasmi mradi huo, Septemba 2, mwaka huu katika Hoteli ya Morogoro.

  Uzinduzi huo pia uliwashirikisha baadhi ya watafiti mbalimbali kutoka Vyuo Vikuu vya nchini Ujerumani, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), pamoja na watendaji kutoka Mashirika ya Mitandao ya Wakulima nchini.

  Kwa mujibu wa Mratibu wa Mradi huo , vijiji viwili vilivyoainishwa kutoka kwenye Wilaya hizo, vitafanyiwa utafiti wa kina wa kimazingira ya kijamii na kiuchumi yanayozunguka mifumo ya chakula ili kuibua mbinu bora za usalama wa chakula ikiwa ni pamoja na kutambua kiwango cha wastani cha mvua kwa mwaka.

  Hata hivyo alisema , mbinu endelevu zitakazotumika zinasaidia kuleta mafanikio katika avijiji na mikoa husika na zitatumiwa kufikia walengwa wengi zaidi nchini na baada ya mradi kumalizika matokeo yataweza kutekelezwa katika ngazi tofauti za sera , ugani na utafiti.

  Kwa upande wake , Mwakilishi wa Ubalozi wa Serikali ya Ujerumani hapa nchini, ( Head of Cooperation), Claudia Imwolde-Kraemer, alisema Tanzania ni nchi yenye historia ya utajiri wa rasilimali mbalimbali, lakini bado inakabiliwa na changamoto juu ya usalama wa chakula kinachozalishwa.

  Hivyo alisema , Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Mendeleo ya kimataifa la nchi hiyo imeweka mkakati wa kusaidia kuzifanya rasilimali hizo zitumika kwa maendeleo ya wananchi wake.

  Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Ubalozi wa Serikali ya Ujerumani hapa nchini, Trans –SEC ,inafadhiliwa na Wizara mbalimbali za nchi ya Ujerumani ili kuwezesha watafifi kutoka Tanzania, Ujerumani, Kenya , USA na Brazil ili kufanya kazi kwa pamoja ya ufatifi wa miaka mitano .

  Lengo ni kuwezesha kuongeza na kuimalisha usalama wa chakula kwa wakulima wadogo ambao hawajitoshelezi kwa chakula wanachozalisha kwa msimu pamoja na kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi duaniani .

  Naye mgeni rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti wa Mazao kutoka Idara ya Utafiti na Maendeleo ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika, Dk Mansoor ,aliishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake hapa nchini kwa kuwezesha kuanzishwa kwa mradi huo muhimu wakati huu.

  Hata hivyo alisema , wakulima wanakabiriwa na changamoto nyingi zinazohitajiwa kupatiwa ufumbuzi hasa ya uboreshaji mifumo ya miundombinu ya barabara, hifadhi ya mazao na uvunaji wa maji ya mvua ili yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza mavuno.

  Mbali na hayo alisema A, mradi huo unakuwa ni chachu katika kuwezesha uboreshaji wa mazao ya chakula ili kukidhi haja ya kuwepo kwa usalama wa chakula nchini.
  Meneja wa ZALF , Stefan Sieber ( kulia) akimpongeza , Claudia Imwolde-Kraemer ambaye ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania na pia ni Head of Cooperation wa Ubalozi huo.
  Baadhi ya wageni waalikwa na watatiti wakisikiliza moja ya mada iliyotolewa baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa Trans - Sec
  Watafiti wakishiriki katika uzinduzi wa mradi wa Trans - Sec

older | 1 | .... | 245 | 246 | (Page 247) | 248 | 249 | .... | 3284 | newer