Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

INTRODUCING "NIKUPE" BY MYCOELY


MICHUZI TV: MASHINDANO YA MBIO ZA MAGARI KUANZA RASMI WIKI IJAYO MKOANI PWANI

UJENZI WA RELI YA KISASA SGR, MATALUMA YA ZEGE YAANZA KUTENGENEZWA, UJENZI SASA NI 20%

Mkuu wa mkoa wa Pwani azindua utoaji wa huduma ya Paspoti za kieletroniki katika mkoa wa Pwani

$
0
0
 Picha kuonesha meza kuu ya mgeni rasmi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
 Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa kibaha, Injinia Evarist Ndikilo akikabidhi paspoti kwa baadhi ya wananchi waliofanya maombi yao ya paspoti mkoani 
wa Pwani.
Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa kibaha, Injinia Evarist Ndikilo akiwasalimia viongozi wa kamati ya ulinza na usalama wa Mkoa mara tu baada ya kufika kwenye tukio.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Changamkieni hii fursa iliyotolewa na Ubalozi wa India- RC Mwanza

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka wafanyabiashara kutumia vyema fursa za kibiashara zilizofunguliwa na Ubalozi wa India hapa nchini kwa kutanua wigo wa biashara zao.


Mhe. Mongella ametoa rai hiyo wakati akifungua mkutano baina ya Balozi wa India nchini Tanzania na wafanyabiashara mkoani Mwanza kupitia taasisi ya wafanyabiashara wa kilimo na viwanda TCCIA uliofanyika jana katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.


Alisema Tanzania na India ni nchi ambazo zina uhusiano wa miaka mingi tangu enzi za Uhuru hivyo wawekezaji na wafanyabiashara mkoani Mwanza watumie fursa iliyotolewa na India ya kuwaunganisha na wafanyabiashara wa Tanzania na nchi hiyo hatua itakayoleta chachu ya mafanikio katika kuelekea Tanzania ya Viwanda.


Awali Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya alisema nchi hiyo ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa nchini Tanzania ikiwa na uwezo wa hali ya juu katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali hususani zana kilimo, viwanda, vyombo vya usafiri, afya pamoja na elimu hivyo mkutano huo umelenga kuongeza ushirikiano zaidi wa kibiashara baina ya India na Tanzania.


Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari alieleza fursa mbalimbali zilizopo mkoani Mwanza ikiwemo uwekezaji wa viwanda vya nguo, bidhaa za ngozi, ujenzi wa makazi ya kisasa pamoja na ufugaji wa samaki na hivyo kuhimiza India kutumia vyema fursa hizo kuwekeza mkoani Mwanza huku watanzania nao wakitumia fursa ya ushirikiano uliopo na India kwenda kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo teknolojia kwa ajili ya maendeleo ya taifa.



Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akifungua mkutano baina ya balozi wa India nchini Tanzania na wafanyabiashara mkoani Mwanza uliolenga kuangazia fursa za kibiashara kati ya Mwanza na India.
Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya akielezea fursa za kibiashara zilizopo India na namna India inashirikiana na Tanzania kibiashara
Katibu wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Hassan Karambi akizungumza jambo kwenye mkutano huo.

MKURUGENZI AWATUPIA LAWAMA WAZAZI RORYA, KUMALIZA KESI ZA MIMBA KIENYEJI.

$
0
0

Na Frankius Cleophace Rorya.

Mkurugenzi wa Halmashgauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Charles Chacha ametupia lawana wazazi na walezi wilayani humo kwa kumaliza suala la kesi zinazohusu mimba kienyeji huku wakishawishi watoto wao kusema uongo jambo ambalo linakwamisha ushaidi ili kuwatia hatiani watuhumiwa kwa lengo la kumaliza changamoto hiyo.

Akijibu hoja ya diwani viti maalum kata ya Robour Diana Charles kuhusu suala la waischana kupata mimba na kukatisha masomo yao, Mkurugenzi amesema kuwa kesi zipo lakini chagamoto kubwa ni wazazi na walezi kumaliza kesi zao na watumiwa kienyeji jambo ambalo linapoteza ushaidi ili polisi waweze kuendelea na kesi hiyo kwa lengo la kuwatia hatiani watuhumiwa hao.

“Binti akiletwa polisi kuhojiwa anaambiwa na mzazi kuwa aseme alikutana na mwanaume sokoni akampa mimba kweli kwa kawaida mtu ukutane nae siku ya soko apo apo uwe na mahusiano akupatie ujauzito siyo kweli hivyo sasa wazazi na madiwani tushilikiane vyema kutokomeza suala hilo pia wazazi waondokane na suala la kumaliza kesi wenyewe jambo hilo linapoteza ushaidi na watoto wetu wanazii kuangamia ” alisema Charles.

Akichangia hoja diwani wa viti maalum kata ya Rabour Diana Charles amesema kuwa Mikakati ambayo iliwekwa kipindi cha Nyuma takwimu za watoto kupata mimba zilishuka lakini kwa awamu hii ya robo ya tatu takwimu zimepanda tena ambapo watoto 18 wa shule za msingi na sekondari wilayani humo wamesitisha masomo kwa kupatiwa Ujauzito hivyo amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuendeleza mikakati ya awali ili kupunguza takwimu hizo.

Naye diwani wa kata ya Nyamagaro Ezra Masana amependekeza kuwa maofisa elimu sekondari na msingi ngazi ya kata wachukue jukumu la kufuatilia masuala ya mimbo kwa watoto wa shule na siyo jukumu hilo kuwaachia maofisa watendaji wa kata.“Ili jukumu la kufuatilia watuhumiwa wanaowapa watoto wetu mimba sasa maofisa elimu msingi na sekondari waweke mkazo na siyo kuwaachia jukumu hili watendaji wa kata kila mara wako mahakamani na kushindwa kufanya shughuli za utendaji” alisema Masana.

Akichangia katika Sekta ya Elimu Diwani wa kata ya Koryo Peter Sarungi anabainisha kuwa suala la wanafunzi wa Shule za Msingi kutokujua kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) bado ni changamoto katika baadhi ya shule za msingi wilayani humo hivyo Madiwani wamesisitizwa kuleta taarifa hizo kwenye baraza la madiwani ili ziwezekufanyiwa kazi.

“Kuna baadhi ya kata wamelta taarifa hizo zimo kwenye vitabu lakini wengine hawajaleta na mimi nilifanya ziara na kamati ya Elimu Afya na Maji lakini kuna baadhi ya shule wanafuzi zaidi ya Miambili darasa la kwanza mpaka la tatu hawajui KKK” alisema Peter.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Charles Chacha akisistiza suala watoto kupatiwa ujauzito amabapo anazidi kulaumu wazazi na walezi wilayani humo kumaliza kesi kienyeji na kusababisha kupotea kwa ushaidi ili kuwatia hatiani watuhumiwa.

Tanzania yajitwalia medali za dhahabu Tamasha la Michezo Afrika Mashariki

$
0
0
Timu za mpira wa miguu za Wanawake ya Tanzania (waliovalia jezi nyeupe) na Burundi wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mechi ya marudiano iliyofanyika katika uwanja wa Gitega, Burundi. Katika mpambano huo wa Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea nchini humo Tanzania imeibuka na ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Burundi katika

Aidha, Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki katika kipengele cha mpira wa miguu limekamilisha ratiba kwa mpambano kati ya Tanzania na Burundi, ambapo Tanzania imejishindia medali ya dhahabu kufuatia ushidi ilioupata. Burundi imejitwalia medali ya fedha kwa kushika nafasi ya pili katika mchezo huo.

Katika mchezo wa awali Tanzania iliibuka na ushindi wa goli 8-1 dhidi ya Burundi.
Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania ikishangilia ushindi wa medali za dhahabu kufuatia ushindi wa goli 5-0 ilioupata dhidi ya Burudi katika Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki 
Sehemu ya mashabiki wakishangilia mchezo uliokuwa ukiendelea kati ya Tanzania na Burundi 
Mmoja wa wachezaji wa timu ya Tanzania akipongezwa na Bw. Addo Komba Afisa kutoka Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo mara baada ya kuvishwa medali ya dhahabu .


TCRA INAKULETEA ELIMU YA MAADILI NA KIZAZI KIPYA KUHUSU MATUMIZI YA MITANDAO

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA LIWALE

$
0
0

Idara ya Habari-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale Mkoa wa Lindi, kufutia kujiuzulu kwa alieyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Ndugu. Zuberi Mohamed Kuchauka.

Kujiuzulu kwa Mbunge huyo ambaye alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kunamfanya apoteze sifa ya kuwa mbunge na hivyo kulifanya jimbo hilo kuwa wazi.

Akitangaza uchaguzi huo Jijini Dar es Salaam leo (Agosti 25, 2018), Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema tangazo la uchaguzi linakuja baada ya Tume kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ameitaarifu Tume kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Liwale Mkoa wa Lindi, kuanzia tarehe 13 Agosti, 2018, kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndugu Zuberi Mohamed kujiuzulu uanachama wa Chama cha Wananchi – CUF, na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge,” amesema.

Jaji Kaijage aliongeza kuwa “…kwa mujibu wa vifungu vya 37 (1) (b),(5) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume inatoa taarifa kwa Umma kuwa Jimbo la Liwale lipo wazi..”

Akizungumza juu ya ratiba ya uchaguzi huo mdogo, Mwenyekiti huyo wa Tume alisema, kutoa fomu za uteuzi itakuwa kati ya tarehe 07 hadi 13 Septemba mwaka huu, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 13 Septemba mwaka huu, kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 14 Septemba na kumalizika tarehe 12 Oktoba mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa tarehe 13 Oktoba mwaka huu. 

“Tume inavikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, miongozo, na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi huo mdogo,” Jaji Kaijage amesema.

WILAYA YA NZEGA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
Changamoto kubwa inayoikabili Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ni uharibifu mkubwa wa mazingira utokanao na uvunaji holela wa rasilimali za misitu na shughuli za kilimo. 

Hayo yamesemwa hii leo na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bw. Godfrey Ngukuwa wakati akiwasilisha taarifa ya Wilaya yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika Kijiji cha Ngukumo na Mwambaha, Wilayani Nzega.

“Wilaya yetu imekuwa na ongezeko kubwa la wavamizi kutoka Mikoa jirani wanaojihusisha na shughuli za ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na kilimo kisichoendelevu, kwa kiasi kikubwa wanachangia uharibufu wa Mazingira, kwa kuwa hivi sasa Nzega imekuwa soko la Mkaa kwa Shinyanga na Mwanza” alisisitiza Bw. Ngukuwa

Akielezea jitihada zilizofanywa na Ofisi yake Bw. Ngukuwa amesema kuwa doria za mara kwa mara zianaendelea Kijiji hapo kwa kushirikiana na wananchi wenyewe kubaini wavamizi hao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ngukumo, Kata ya Nkiniziwa Wilayani Nzega, Mkoani Tabora kuhusu changamoto kubwa inayokabili Kijiji hicho ya ukataji ovyo wa rasilimali za misitu. Waziri Makamba ametoa wito wa wananchi hao kuweka ulinzi madhubuti. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mazingira ya Kijiji cha Ngukumo na kuwakumbusha wajibu wao katika kusimamia mazingira. Waziri Makamba amewataka kutumia kutumia Sheria ndogo ndogo za Kijiji kunusuru mazingira yao 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akipanda mti kuunga mkono jitihada za upandaji miti kwa wakazi wa Kijiji cha Nkiniziwa. Mti huo pia ameukabidhi kwa mtoto Masoud Maganga ili aweze kuutunza kama kielelezo cha kutunza mazingira. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwambaha, Wilayani Nzega wakijibu maswali mbalimbali ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kutembelea Shule hiyo kupanda miti na kuimarisha Club ya Mazingira Shuleni hapo kwa kuiwezesha kuanzisha kitalu cha miche ipatayo Elfu tano. 

MABINTI 40 TARIME WAPATIWA ELIMU YA UJASIRIAMALI KUJIKWAMUA KIMAISHA.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Mabinti 40 ambao wako nje ya mfumo rasmi wa shule kutoka kata tano wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya ujasiramali kwa lengo la kuongeza mbinu, sifa na dhana bora katika kufanya shughuli zao za baishara ili kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kuondokana na utegemezi.

Mabinti hao baadhi yao hawakubahatika kwenda shule na wengine wao wamekatisha masomo kwa kupatiwa ujauzito wakiwa shuleni ,wengine kuolewa katika umri mdogo kutokana na mila na desturi ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike, huku wengine wakiwa kwenye ndoa japo wameolewa katika umri mdogo, na baadhi wameshindwa kumudu ndoa hizo na kuachika hapa kilio chao kikubwa ni kuomba Serikali kwa kushirikiana na shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime kuwapatia Mitaji pamoja na Malighafi baada ya kupatiwa ujuzi.

Magreth Kichele kutoka kata ya Komaswa ameiomba serikali kwa kushirikiana na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto kuwapatia malighafi pamoja na vifaa ili waweze kujitegemea na kuendeleza biashara zao huku wakionyesha tofauti baada ya kupatiwa elimu hiyo ya siku tatu na kuhaidi kwenda kufanyia kazi elimu hiyo waliyopewa.

“Sisi tunaishi vijijini tunamaisha magumu sasa kama tumepatiwa elimu changamoto kubwa ni mitaji wengine wanavyereani hawana pesa za kununu malighafi hivyo sasa shirikal na serikali wakishirikiana wakatusaidia tutashukuru sana” alisema Magreth.

Kambibi Kamugisha kutoka shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akitoa ufafanuzi jinsi mafunzo hayo yalivyotolewa kupitia Shirikal hilo kwa kushirikiana na Shirika la Plan Internation Tanzania chini ya Ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Sweden (Sida) pamoja na Shirika la Umoja wa Ulaya.
Washiriki wa Mafunzo hayo ambao ni mabinti 40 kutoka kata tano Halmashauri ya Tarime Vijijini wakiendelea kupatiwa elimu ya ujasiraimali.

Picha ya pamojana washiriki wa mafunzo hayo baada ya kupatiwa elimu ya ujasiriamali.Kambibi Kamugisha kutoka shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akitoa ufafanuzi wa jambo katika Mafunzo hayo ya siku tatu katika ukumbi wa MCN Mjini Tarime Mkoani Mara.

DC ODUNGA AWATAKA WANANCHI KIJIJI CHA ITOLWA WAACHE KUNG'ANG'ANIA KWAMBA WAPO KITETO, WAO NI WA CHEMBA TU

$
0
0

Na Shani Amanzi,Chemba

MKUU wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga amewataka wananchi wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolwa waache mara moja mgogoro wa kung’ang’ania kuwa wapo eneo la Wilaya ya Kiteto.

Badala yake amewataka wajue kabisa bado wapo wilayani Chemba kwani Serikali inafata ramani ambayo inatambulika.

Odunga amesema wanatambua kabisa kitongoji cha Lalalami kipo mpakani kati ya Wilaya ya Chemba na wilaya ya Kiteto ambapo mgogoro ulianza kuanzia mwaka 2012 na mwaka 2016 kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia vifungu vyake vya sheria ya ardhi waliamua Kitongoji cha Lalalami kuwa wilayani Chemba."Lakini bado wananchi wakakataa maamuzi hayo na ukweli ndiyo huo. Leo hii ni mara ya tatu mwaka 2018 Serikali imeamua kukaa chini na wananchi tena kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa ,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chemba na Kiteto .

"Wataalam wa Halmashauri za Wilaya zote na kufanya maamuzi ya pamoja ya kuzuia kabisa mgogoro huo wa mara kwa mara wa wananchi kukataa kuwa eneo la Serikali ya Wilaya ya Chemba na atayekwenda kinyume hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa sababu serikali haiwezi kupoteza muda na fedha kusuluhisha mgogoro ambao ukweli unajulikana,” amesisitiza Odunga.

Aidha Odunga amesema “tunajua sababu kubwa ni shughuli za kiuchumi ambapo jamii iliopo inafanya shughuli za ufugaji na mnataka kujumuika na jamii yenzenu ya Kiteto ya Ufugaji lakini wilaya ya Chemba wengi wao ni wakulima." Lakini mkumbuke jamii zote hizi mbili za wakulima na wafugaji zipo wilayani Chemba na huwa wanafata kanuni na taratibu za ufugaji na kilimo ili kuzuia migogoro ya ardhi,wakulima na wafugaji ambapo ni janga la nchi nzima,"amesema.

Odunga alifanya ziara ya siku moja kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Magesa ambayo ilikuwa Agosti 21 mwaka huu ambapo walikuwa wanasuluhisha mgogoro kati ya wilaya na wilaya kati ya Chemba na Kiteto.
MKUU wa Wilaya ya Chemba Saimon Odunga akizungumza na Wanachi wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolwa,kuhusua kuacha mara moja mgogoro wa kung’ang’ania kuwa wapo eneo la Wilaya ya Kiteto,na badala yake amewataka wajue kabisa bado wapo wilayani Chemba kwani Serikali inafata ramani ambayo inatambulika.Katika mkutano huo DC wa Chemba aliambatana na DC wa Kiteto pamoja na maofisa mbalimbali wa wakiwemo wa Ulinzi na usalama,kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa.



Baadhi ya wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kitongoji cha Lalalami katika Kijiji cha Itolw,wilayani Chemba

JK KUMUWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KUAPISHWA RAIS WA ZIMBABWE

WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI SHULE YA SEKONDARI TOLEDO TANGA ATOA NENO KWA WAZAZI NCHINI

$
0
0
WAZAZI kote nchini wametakiwa kuacha kulalamikia wadau wa elimu na badala yake wameshauriwa kushirikiana na walimu kukagua madaftari ya watoto wao kwa lengo la kuongeza ufaulu ili kupunguza mimba za utotoni zinazosababisha ndoto zao kushindwa kufikiwa. 

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati halfa ya kukabidhiano ya madawati na viti vyake 40 aliyoyatoa kwenye shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga. 

Ummy ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama cha Mapinduzi {CCM) mkoa wa Tanga alisema kimsingi wazazi wanapaswa kutambua kufanya hivyo kutawasaidia kuwawezesha vijana wao kuongeza ufaulu na hivyo kufanikiwa kuepukana na vishawishi ambavyo wanakabiliana navyo wakati wakiwa shuleni. 

“Ndugu zangu wazazi na walezi lazima tutambue jukumu letu la kufuatilia maendeleo ya watoto wetu kwani hii ndio njia pekee inayoweza kuwasaidia kwa kushirikiana na walimu wao kwa lengo la kuwezesha kufikia ndoto zao”Alisema. Naye ka upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwataka wanafunzi kutumia fursa hiyo kuongeza jitihada kwenye kusoma ili azma ya serikali ya kuongeza ufaulu kwa shule zake iweze kufikiwa. 

“Ndugu zangu wanafunzi mmepata madawati haya yatumieni vizuri kwenye matumizi yaliyokusudiwa kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo yenu kwa kuongeza ufaulu “Alisema. Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo na kuongeza kuwa bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo vya wasichana . 

Alisema kutokana na uhaba huo umesababisha wasichana na wavulana kushiriki katika huduma hiyo.
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) kulia akimkabidhi madawati 40 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Toledo ya Jijini Tanga Daudi Nchia ikiwa ni mkakati wake wa kukabiliana na uhaba uliopo
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) kushoto akiwa amekaa kwenye moja ya madawati 40 aliyokabidhi kwa shule ya Sekondari Toledo Jijini Tanga 
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) katika akiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Toledo Daudi Nchia mara baada ya kuwakabidhi madawati 40
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga{CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Toledo mara baada ya kuwakabidhi madawati 40


Introducing "Kiddo" (Official Audio) by Jovi ft Deddy

INTRODUCING "K. MUNDENDE" by KARDINAL J.OTENGA

MAAFISA UHAMIAJI WAFANYA USAFI KATIKA MAKAZI YA WAZEE NUNGE WILAYA YA KIGAMBONI,WATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI

$
0
0


MAAFISA uhamiaji wamefanya usafi katika makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni kwaajili ya kuwafariji.

Zawadi walizowadawadia ni pamoja na Mchele,maharage, sukari, unga, mafuta, sabuni na sementi.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza walipowatembelea wazee hao leo amesema kuwa sementi waliyopewa ni kwaajili ya kutengenezea uzio wa eneo la kulima mboga mboga kwaajili ya wakazi wa makazi hayo.

Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando amewasihi watunze mazingira yao pamoja na mazingira ya vyoo pia amewaomba wataalamu wa saikolojia waweze kuwapa wakazi wa makazi ya Nunge ili kuwaweka katika usawa wa kimawazo kwani wengi wao hawana ndugu.

Kwa upande wa mwakilishi wa wakazi wa makazi ya Nunge yaliyopo wilya ya Kingamboni, Salumu Ubwabwa amewashukuru Maafisa uhamiaji kwa kuwafariji pamoja na kwapa msaada wa vitu mbalimbali.

Ubwabwa amesema kuwa changamoto zinazowakabiri ni pamoja na kukosa uzio wa eneo lao,umeme na maji kwa baadhi ya makazi pamoja na geti la kuingilia katika makazi hayo.

Pia amewaomba watu mbalimbali wanaoweza kuwasaidia waweze kuwasaidi kwani wao niwazee na hawawezi kujitafutia wenyewe chakula.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kulia akifanya usafi leo Augusti 25,2018 katika Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam mara baada ya maafisa uhamiaji kutembelea katika makazi yao.
   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kulia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando kushoto wakifyeka majani pamoja na miti ambayo ipo katika eneo la makazi ya  wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018 walipotembelea leo kwaajili ya kufanya usafi pamoja na kuwafariji watu hao waliopo katika kituo hicho.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akimsaidia bibi kushuka chika wakati walipotembelea kituo cha Nunge wilaya ya Kigamboni leo.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kulia akisafisha nyumba ya bibi Mgogo iliyopo katika makazi ya wazee, watu wenye ulemavu na wasiojiweza Nunge Wilaya ya Kigamboni leo Augusti 25,2018.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando wakiwa jikoni kujionea mlo kamili wanaopewa watu wanaoishi katika Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018.
Mzee Salumu Ubwabwa akiwashukuru maafisa uhamiaji waliofika kuwafariji, kuwafanyia usafi pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali katika makazi ya wazee, watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge kilichopo wilya ya Kingamboni jijini Dar es Salaam.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

MWENYEKITI UVCCM, KHERI JAMES AWATAKA VIJANA WASOMI KUTUMIA ELIMU YAO KATIKA KUINUFAISHA JAMII

$
0
0

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Kheir James amewataka vijana wasomi nchini kuhakikisha tija ya elimu waliyonayo inanufaisha jamii iliyowazunguka kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Rai hiyo aliitoa wakati akiwahutubia vijana waliofaulu mtihani wa kidatu cha sita kwa daraja la kwanza, la pili na tatu (Division I,II na III) mwaka 2018 Zanzibar huko katika ukumbi wa Z-ocean iliyopo Bububu Wilaya ya Magharibi ‘’A’’ Zanzibar.

Alisema endapo vijana hao watashindwa kuzitumia vizuri elimu zao kwa kuzinufaisha jamii zilizowazunguka basi elimu hizo zitakuwa hazina maana kwao wao na taifa kwa ujumla.

Alisema serikali zote mbili ambazo ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinaendelea kuthamini vijana kwa kuwawezesha kupitia nyanja mbali mbali hasa za kitaaluma.

Aliwataka vijana hao ambao watajiunga na elimu ya juu katika vyuo mbali mbali nchini kuwa wanatakiwa kusoma masomo ambayo wana uwezo nayo ili waweze kufaulu vizuri katika masomo ya elimu ya juu na wawe wataalamu wenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheir James akiwahubia wanafunzi wa kidato cha sita Zanzibar wa mwaka 2018 waliofaulu kwa kiwango daraja la kwanza, pili na tatu katika hafla ya kuwapongeza iliyoandaliwa na CCM Zanzibar ambayo imefanyika hoteli ya Z-ocean iliyopo Bububu Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. 
NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita Zanzibar waliofaulu masomo yao kwa kliwango cha daraja la kwanza, pili na tatu mwaka 2018, iliandaliwa na CCM. 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar ambaye pia ni mlezi wa UVCCM Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapongeza wanafunzi wa kidatu cha sita mwaka 2018 Zanzibar. 
BAADHI ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2018 waliofaulu wakifuatilia na kusikiliza nasaha mbali mbali kutoka kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali walioudhuria katika hafla hiyo. 


WADAIWA WA MASURUFU YA SAFARI KATIKA MANISPAA YA KUKATWA KATIKA MISHAHARA YAO YA SEPTEMBA

$
0
0

NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA

BARAZA la Madiwani limeuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuanza kuwakata fedha katika mishahara yao watumishi wote wanaodaiwa masurufu ya safari ambao wameshindwa kufanya marejesho kwa muda mrefu na hivyo kusababisha kupata hati yenye mashaka.

Kauli hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Tabora ambao ulikuwa ikipitia taarifa mbalimbali ikiwemo ya Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu. Diwani wa Kata ya Ndevelwa Selemani Maganga alisema haiwezekani Halmashauri hiyo iendelee kupata hoja inayotokana na watumishi kushindwa kufanya marejesho ya fedha walizopewa kwa ajili ya safari ya kikazi.

Alitaka watumishi wote wanaodaiwa waanze kukatwa katika mshahara wao wa Mwezi ujao(Septemba) ili fedha hizo zirejeshwe katika Halmashauri hiyo kwa ajili ya shughuli nyingine. Naye Diwani wa Kata ya Kanyenye na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tabora .Ghulam Dewji alisema urejeshaji wa masurufu ya safari kwa watumishi wa Manispaa ya Tabora hauridhishi na kutaka hatua kali dhidi yao zichukuliwe.

Alisema miongoni mwa hoja zilizosababishia kupata hati yenye mashaka iliyotokana na ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni masurufu yanafikia shilingi milioni 84 ambazo watumishi hawajafanya marejesho. Dewji alisema kati ya fedha hizo ni milioni 11 ndio zimefanyiwa marejesho kwa mujibu wa Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu wa Manispaa ya Tabora , bado milioni 73 hazijafanyiwa marejesho.


Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Nduguru akitoa ufafanuni kwa Madiwani leo juu hatua ambazo wameanza kuzichukua katika kuhakikisha wanafuta hoja ya masurufu yenye thamani ya milioni 84 ambayo hajafanyiwa marejesho na watumishi wa Halmashauri hiyo. 

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images