Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

Hospitali za Wilaya 67 Kujengwa Mwaka Huu wa Fedha

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.

SERIKALI ya Awamu ya Tano Kujenga Hospitali za Wilaya 67 katika mwaka huu wa  fedha ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha sekta ya Afya nchini.


Akizungumza Katika Kipindi cha TUNATEKELEZA Kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO, Waziri wa Nchi Ofisi  ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Serikali itatumia shilingi bilioni 105 kutekeleza mradi huo.


 “Tangu tupate uhuru tulikuwa na hospitali za wilaya 77 lakini sasa Serikali ya Awamu ya Tano inaenda kuweka historia kwa mageuzi makubwa yanayofanyika katika sekta hii ya afya na tumejipanga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma bora za afya,” alisisitiza Mhe. Jafo.


Akifafanua Mhe. Jafo amesema kuwa Serikali  imeweka  historia, kwa kuwa tangu Taifa lipate uhuru kulikuwa na vituo vya afya vinavyofanya upasuaji 115 nchi nzima lakini katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imejenga vituo vya afya vyenye uwezo wa kufanya upasuaji 208 vinavyoenda sambamba na ujenzi wa hospitali za wilaya zinazoanza kujengwa  mwaka huu.


Aidha amesema, Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imeshapatiwa fedha ili iweze kusambaza vifaa tiba katika vituo vya afya vilivyojengwa ili viweze kuanza kufanya kazi.Katika mwaka wa fedha 2017/2018 Mamlaka za Serikali za Mitaa zimapata mafanikio makubwa katika kuimarisha sekta za elimu,  afya na ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, vyumba vya  madarasa na miundo mbinu mingine inayochochea  maendeleo ya wananchi.

Pia ameziagiza Halmashuri zote nchini kusimamia ukusanyaji wa mapato, lengo likiwa ni kuweka mfumo mzuri wa ufuatiliaji ili kuboresha makusanyo na  kusimamia matumizi ya fedha hizo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.“Nawataka wakurugenzi wote wawe wakali katika ukusanyaji mapato na tutatoa onyo maalum kwa halmashauri zote ambazo hazifanyi vizuri katika ukusanyaji mapato,” alisema Mhe. Jafo.

Kipindi cha TUNATEKELEZA kinaratibiwa na Idara ya HABARI MAELEZO na kurushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na awamu hii inawashirikisha Mawaziri wote ambapo wanapata fursa ya kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Sera na program mbalimbali  zinazotekelezwa na Serikali.
 Sehemu ya Vifaa vya Kisasa vya Upasuaji kama vinavyoonekana katika moja ya vituo vya afya vilivyojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Wataalamu wa afya wakikagua sehemu ya vifaa tiba vipya  katika moja ya Kituo cha afya kilichojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

(Picha zote na OR- TAMISEMI).

KATIBU MKUU SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI ATEMBELEA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

$
0
0
SHIRIKA la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa yanayohusiana na ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na namna mifumo hii inavyoathiri mazingira yetu. 

Shirika hufanya kazi zake kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama (National Meteorolgical and Hydrological Services - NMHSs) ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni mwakilishi rasmi wa shirika hili hapa nchini. 

Katibu Mkuu wa WMO amefanya ziara katika ofisi za TMA ili kujionea shughuli za hali ya hewa na namna ambavyo WMO inaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali yahusuyo hali ya hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa vya hali ya hewa. Aidha aliipongeza TMA katika juhudi zake za utekelezaji wa programu za WMO na kuzisaidia nchi zingine za Afrika. 

Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni taasisi ya mfano Afrika katika utoaji wa huduma bora za hali ya hewa 
IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO 

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA .

   Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akishuhudia na kushiriki mkutano wa kuandaa utabiri wa siku unaofuatilia hali mbaya ya hewa kwa nchi za Afrika mashariki zilizoko katika Bonde la Ziwa Victoria.
 Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas katika picha ya pamoja na menejimenti ya TMA.
 Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akichangia jambo baada ya kupata maelezo ya mfumo wa kisasa utoaji taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wakati alipotemebelea ofisi za hali ya hewa zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere. hewa.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA MOU-KAMPALA- UGANDA

$
0
0

TANZANIA na Uganda zilitia saini Mikataba mbalimbali ya ushirikiano ikiwa pamoja na Mkataba wa Uendelezaji wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda na mwingine ni Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Kupeleka Umeme katika Vijiji vya Mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Uwekaji saini huo ulifanyika katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala Uganda kwa siku tatu kuanzia tarehe 21 Agosti 2018.


Miradi mingine iliyojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda kuja Tanzania (EACOP), Mradi wa Utafutaji wa Mafuta katika Kitalu cha Eyasi Wembere, Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Murongo Kikagati (14MW) na Mradi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Nsongezi (MW 35).


Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulifanya tathmini ya utekelezaji wa masuala yaliyokubalika wakati wa mkutano wa kwanza wa JPC uliofanyika Arusha mwezi Aprili 2017 na kuweka mikakati ya utekelezaji kwa masuala ambayo hayajakamilika.


Aidha, ulijadili mikakati ya kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa nchi hizo mbili.

Katika Mkutano huo ujumbe wa Wizara ya Nishati uliongozwa na Naibu Waziri,  Subira Mgalu, pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizarani, TANESCO na Shirika la Maendeleo ya Petroli ( TPDC)
Naibu Waziri wa Nishati, Subira  Mgalu akishuhudia utiaji saini wa Mikataba ya Makubaliano (MoU) inayohusu utekelezaji wa Miradi ya Umeme na Gesi asilia, kati ya Tanzania na Uganda. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.
Watendaji mbalimbali wa Serikali za Uganda na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Mkutano wa Pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala Uganda kwa siku tatu kuanzia tarehe 21 Agosti 2018.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar awatahadharisha Wananchi juu ya matumizi ya umeme

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud wakifika katika eneo la tukio kuifariji na kuipa pole Familia ya Watoto Tisa ya Marehemu Maalim Rajab Mzee kufuatia Nyumba yao kuungua Moto.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameinasihi Jamii Nchini kuwa na tahadhari kubwa wakati wa matumizi ya vifaa vya umeme ili kuwepuka madhara yanayoweza kuleta maafa makubwa hapo baadae. 

Alisema Huduma ya umeme ni nzuri na muhimu katika matumizi ya mwanadamu kwenyea harakati zake na kimaisha za kila siku lakini inaweza kuwa janga iwapo mwanaadamu huyo ataamua kutumia huduma hivyo ovyo. Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo muda mfupi tu alipopata taarifa ya kutokea kwa Janga la Moto katika Nyumba ya Familia ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni iliyopo Rahaleo mbele ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Muembe Shauri. 

Hata hivyo hakuna mtu aliyepata matatizo kutokana na mripuko wa moto huo uliosababishwa na kuungua kwa Hita iliyokuwemo kwenye Nyumba hiyo ambayo wakati inawaka alikuwemo Kijana Mmoja wa familia ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni. 

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda maisha na mali za Rais imeazimia kujenga Vituo vya Huduma za Zimamoto kila Wilaya kwa lengo la kuwa tayari wakati yanapojitokeza matukio ya majanga. “ Umeme tunaupenda sana katika matumizi yetu ya kawaida ya kila siku lakini pia unahatari iwapo hatutakuwa makini katika matumizi yake ya ovyo”. Alisisitiza Balozi Seif. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikipongeza Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kwa umakini wake uliopelekea kuuzima moto huo kwa dakika chake na kuepusha maafa ya kuendelea kuathiri nyumba zilizo jirani na eneo hilo.

Mabaki ya Nyumba ya Marehemu Maalim Rajab Mzee iliyopo Mtaa wa Rahaleo ambayo iliungua moto mapema asubuhi uliosababishwa na Hiter ya Umeme.
Wa kwanza na wa Pili kutoka Kulia ni miongoni mwa Watoto Tisa wa Familia ya Marehemu Maalim Jaba Mgeni wa Nyumba iliyoungoa Moto mapema asubuhi katika Mtaa wa Rahaleo wakimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mkasa uliowapata wa kuunguliwa Nyumba yao.
Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kutoa pole na kuisisitiza Jamii kuwa na tahadhari ya matumizi salama ya huduma za Umeme ili kuepuka maafa.

UTARATIBU MPYA WA KUSAJILI KAMPUNI

$
0
0
Na Bashir Yakub.
TOKEA April mwaka huu 2018 utaratibu wa kusajili kampuni umebadilika. Ni tofauti kabisa na ambavyo tulizoea.Hata hivyo, yapo mambo ambayo yamebaki vile vile kama awali, kadhalika yapo mengi pia yaliyobadilika.
Tutapitia utaratibu wa awali kidogo na huu mpya.

UTARATIBU WA AWALI.
a ). Ulikuwa unatakiwa kuandika barua kuuliza jina unalotaka kutumia kama jina la kampuni iwapo lipo au hapana. Kama lipo ungetakiwa kuleta jingine, na kama halipo ulikuwa unapewa ruhusa ya kulitumia katika usajili.

b ).Ulikuwa unatakiwa kuandaa waraka na katiba ya kampuni(article and
memorandum of association). Zilikuwa zinatakiwa kwa uchache angalau nakala nne.

C ) Ulikuwa unatakiwa kupakua fomu namba 14(a) na 14( b ) kutoka kwenye
mtandao wa BRELA, au kuzifuata fomu hizo hapohapo BRELA ambapo ungetakiwa kuzijaza kisha kuzisaini.

d ) Kisha ulikuwa unatakiwa kubeba hizo nakala za waraka na katiba ya kampuni, pamoja na hizo fomu zilizojazwa na kuzipeleka BRELA mnazi mmoja jengo la ushirika kwa ajili ya usajili.

e ) Huko BRELA, baada ya kuzipitia na kuona hazihitaji masahihisho sasa
ungepewa ruhusa ya kulipia ambapo malipo yalikuwa yakifanyika kupitia benki ya CRDB.

f ) Baada ya hapo ungetakiwa kusubiri kipindi cha wiki moja au wiki na
sikukadhaa, au wiki mbili ili uweze kupatiwa cheti rasmi cha usajili wa
kampuni(certificate of incorporation).
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

KORTINI KWA TUHUMA ZA KUONGOZA MBINU ZA KIHALIFU,KUSAIDIA KUSAFIRISHA BINADAMU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

WATU nane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kuongoza mbinu za kiuhalifu na kusaidia kusafirisha binadamu.

Hata hivyo, ni watuhumiwa wanne tu waliofanikiwa kusomewa mashtaka yao kwa kuwa watuhumiwa wengine wanne hawakuwa wakijua lugha ya Kiswahili wala Kingereza.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Faraji Nguka  amewataja washtakiwa wanne waliosomewa mashtaka yao kuwa ni, Abdallah Kassim Bashrahil, Idd Hussein Said, Muhidin Said Machelenga, Swed Twaibu Swed.

Mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde imedaiwa kuwa, katika siku na mahali tofauti tofauti, ndani ya Jiji la Dar es Salaam, na nchi ya Comorro washtakiwa hao waliongoza genge la uhalifu na kuweza kutekeleza tukio la kusafirisha binadamu kutoka Comorro kwenda Saudi Arabia kupitia Tanzania. 

Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, siku na mahali hapo hapo, washtakiwa hao, walisaidia kuwasafirisha Halima Mmadi, Tereha Mlahaili, Ali Miraaji na raia 162 huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Imedaiwa  walifanya hivyo kwa kuwapatia hati za kusafiria za Tanzania huku wakijua kuwa watu hao ni raia wa Commoro. 
Pia washtakiwa wanadaiwa kufanya hivyo ili kuwarahisishia kupata kibali cha makazi kutoka Idara ya Uhamiaji ya Tanzania kwa lengo la kuwasafirisha watu hao kwenda nchini Saudi Arabia.

Hata hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chohote mahakamani hapo kwani Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi mahakama kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 27 mwaka 2018 kwa ajili ya washtakiwa wengine wanne kusomewa mashtaka yao mkalimani atakapopatikana.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika.

 Watuhumiwa wanaotarajiwa kusomewa mashtaka yao Jumatatu ni Said Ally, Ahamada Mchangama, Hamada Ali Ben Ali na Suulaimana Abdallah.

USHAURI WA JULIUS MTATIRO IWAPO ATAONANA NA RAIS DK. MAGUFULI HUU HAPA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Julius Mtatiro amesema iwapo atapata nafasi ya kuonana na Mwenyekiti wa Chama hicho kuna jambo la msingi ambalo anataka kumshauri kwa maslahi ya Watanzania walio wengi.

Mtatiro ambaye kabla ya kujiunga na CCM alikuwa Chama cha Wananchi(CUF) ambapo akiwa huko alishika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za juu na sasa anasema baada ya kujiunga CCM anaoana ni kama ameutua mzigo mzito uliokuwa kichwani.

Akizungumza na Michuzi Blog katika mahojiano maalum yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Mtatiro amezungumzia mambo mbalimbali na kubwa ni kwamba viongozi wa ngazi zote za juu ndani ya CCM wamempokea na kumpa baraka na siku yoyote atachukua kadi.

Alipoulizwa iwapo atapata nafasi ya kuonana na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli Mtatiro amejibu iwapo atakutana naye atamshauri umuhimu wa kuongeza juhudi katika kupambana na umaskini nchini.Amesema anapongeza juhudi zinazoendelea katika kuondoa umaskini lakini ukweli ni kwamba umaskini bado mkubwa na anaamini Rais akifanikiwa katika hilo atakuwa ameondoa changamoto inayowakabili Watanzania wengi.

Amesema sababu za yeye kuamua kuingia katika siasa ni kutokana na hali ya umasikini uliopo kwenye familia anayotoka na jamii inayomzunguka.Hivyo anasema aliamini akiwa katika siasa atashiriki kuhamasisha na kuweka mipango ya maendeleo na ndio maana siku zote amekuwa akishauri namna bora ya kuondoa umaskini nchini.

"Jambo kubwa ambalo nitamueleza Mwenyekiti wangu wa CCM ni kumshauri aongeze kasi katika kuondoa hali ya umaskini kwani watanzania wengi wamezungukwa na umaskini." Ndio maana pamoja na sababu nyingi ambazo nimetoa wakati naondoka CUF moja ilikuwa ni kujiunga na CCM ili kama kijana na Mtanzania mzalendo nishiriki katika kuzungumzia na kuhamasisha maendeleo badala ya kukaa upande wa kupinga kila kinachofanyika,"amesema Mtatiro.

Alipoulizwa anajisikiaje anavyoshambuliwa na kutukanwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii,Mtatiro amejibu anaona na kusikia namna anavyotukanwa lakini haimuumizi kwani anaamini amefanya uamuzi sahihi.Amefafanua kabla kuondoka CUF amefanya utafiti wa kutosha kwa kuangalia aina ya siasa za upinzani, siasa za nchi na CCM na kuona sehemu sahihi ni huko alikokwenda sasa kwani yupo salama.

DKT. KIGWANGALLA AENDELEA NA MAZOEZI MOI, ATEMBEA UMBALI WA KM4

$
0
0
NA ANDREW CHALE, DAR
HALI ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla anayepatiwa matibabu na Madaktari Bingwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa Mgongo Muhimbili (MOI), imeendelea kuimarika siku hadi siku ambapo kwa sasa ameweza kufanya mazoezi ya kutembea umbali wa Kilometa 4, kwa kutumia muda wa saa moja na dakika 23.

Dkt. Kigwangalla ameweza kufanya zoezi hilo jana jioni kutembea umbali huo wa Kilometa 4 na kisha kupanda jengo la MOI kwa kutumia ngazi kutoka chini mpaka gorofa ya Sita.

“Kwa sasa naendelea vizuri. Tofauti na awali nilipokuwa natembea umbali mdogo kutoka Wodi ya Mwaisela nilipokuwa nimelazwa na kutembea mpaka getini la kuingilia Hospitali hii ya Muhimbili. Kwa sasa natembea umbali mrefu zaidi, nilianza na Kilometa moja, nikaongeza kilometa moja na nusu na baadae mbili… Lakini nikaona leo niongeze zaidi na kuweza kumaliza Kilometa hizi nne.

Mazoezi haya ya kutembea yananisaidia kuimarisha zaidi mapafu. Ila kwa sasa bado nashughulikia mkono pekee” Alieleza Dkt. Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla uanza kufanya mazoezi hayo kila siku kuanzia majira ya jioni kwa lengo la kiafya pamoja na tiba kwa hali yake hiyoambayo kwa sasa akiendelea na matibabu.

Kwa upande wa Madaktari wa MOI wamebainisha kuwa licha ya kuendelea vizuri, bado wanafuatilia kwa ukaribu hali ya afya yake hadi watakapojiridhisha ndipo watamruhusu kurejea nyumbani kuendelea na majukumu yake.

Dkt. Kigwangalla aliletwa MOI tangu Agosti 12, mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa mkono wake ambao ulivunjika kutokana na ajali aliyoipata Agosti 4, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Manyara.
Waziri wa Maliasiali na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifanya mazoezi ya kutembea katika viunga vya Upanga Mashariki Jijini Dar es Salaam jana usiku ambapo alitembea umbali wa Kilometa nne. Wengine ni wasaidizi wake (Kulia) ni Katibu wa Waziri Ephraim Mwangomo na kushoto Ramadhan Magumba.
Waziri wa Maliasiali na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipanda ngazi jingo jipya la MOI lenye gorofa 6, jana usiku akirejea kwenye Wodi yake anapopatiwa matibabu. Wengine ni Wasaidizi wake (kushoto) ni Katibu wa Waziri Ephraim Mwangomo.
PICHA NA ANDREW CHALE

MCHENGA BBALL STARS KUTETEA UBINGWA WAKE JUMAMOSI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MABINGWA watetezi wa michuano ya Kikapu ya Sprite Bball Kings Mchenga Bball Stars wameendelea kujiweka vizuri kwenye mbio za kutetea ubingwa wao walioutwaa mwaka 2017 baada ya kushinda game 2 kwa pointi 85 dhidi ya 65 za Flying Dribblers.

Matokeo hayo sasa yamewafanya Mchenga Bball Stars kushinda game mbili mfululizo kwenye 'best of five' ya fainali ya Sprite Bball Kings baada ya Mabingwa watetezi wa michuano ya Kikapu ya Sprite Bball Kings Mchenga Bball Stars wameendelea kujiweka vizuri kwenye mbio za kutetea ubingwa wao walioutwaa mwaka 2017 baada ya kushinda game 2 kwa pointi 85 dhidi ya 65 za Flying Dribblers.


Katika mchezo uliochezwa jana uliopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay mchezaji Baraka Sadick wa Mchenga ameendelea kuwa moto wa kuotea mbali baada ya kuongoza kwa pointi katika game 1 na leo kufanya hivyo tena akifunga pointi 28 kati ya 85 za Mchenga Bball Stars. 

Pia amechukua rebound 9 na kutoa Assist 5. Kwa upande wa Flying Dribblers mchezaji Steve Mtemihonda, amefunga pointi 19 na kuchukua rebound 6 pamoja na kutoa Assist 2.  

Game 3 ya 'best of five' itapigwa Jumamosi Agosti 25, kwenye uwanja wa ndani wa taifa, ambapo kama Mchenga watashinda watatetea ubingwa wao rasmi lakini kama Flying Dribblers watasawazisha basi itasubiriwa game 4.

Michuano ya Sprite BBall Kings inayodhaminiwa na kinywaji cha Sprite na Kituo cha East Africa Radio na Tv yameweza kusaidia kuinua vipaji kwa vijana na kurejesha heshima ya mchezo wa mpira wa kikapu na mshindi wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Shilingi Milioni Kumi na kikombe, mshindi wa pili atapata milioni 3 huku mchezaji bora wa mashindano (MVP) atapata milioni 2.

MADIWANI TABORA WAPEWA SIKU 14 KURUDISHA VIWANJA WALIVYOJILIMBIKIZIA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT-
RS TABORA.
SERIKALI ya Wilaya ya Tabora imetoa siku 14 kwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ambao wamejilimbikizia viwanja vingi bila kuviendeleza kuvirudisha mara moja.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati akijitambulisha kwao.

Alisema uchunguzi alioufanya amegundua kuwa baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo wamekuwa na tabia kusimamia mambo yasiyo halali kama vile udalali wa viwanja, kulazimisha mikataba ya utekelezaji wa miradi wapewe wao au marafiki zao.

Kitwala alisema vitendo vya namna hiyo havisaidii kuiendeleza Halmashauri hiyo na wananchi wake badala yake vinawaumizi wanyonge ambao kodi zao zinatumiwa na baadhi ya watu kwa maslahi binafsi.

Aliongeza kuwa Madiwani na Watendaji wenye tabia za kuendekeza ubinafsi hawafai kuendelea na nafasi zao badala yake wanatakiwa kupitisha ili watu wenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi ndio wasimamie majukumu yao.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema Manispaa ya Tabora ina uwezo wa kuwa na fedha nyingi kama Madiwani na Watendaji wakisimamia vizuri mianya ya ukwepaji kodi.

Wakati huo huo Kitwala alisema kuanzia hivi sasa ataanza kukagua miradi yote inajengwa na inayoendelea kujengwa ili kuona kama inavyo viwango vinavyostahili.

Alisema akikuta mradi katika eneo husika hauna kiwango atalazimika kumchukulia hatua mhusika ikiwemo kuwafikisha Mahakamani.

Kitwala alisema Serikali haiwezi kuvumilia fedha za wanyonge zinatumika vibaya kwa ajili ya maslahi binafsi.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI LEO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke kabla ya kuanza kufanya mazungumzo ya kikazi katika ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam leo Agosti 24/2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke nakufanya naye mazungumzo ya kikazi katika ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam   leo    Agosti 24/2017

WARAMI WAMVAA MBOWE WAMTAKA ASIIPANGIE KAZI MAHAKAMA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuishukia mahakama kuwa haimtendei haki, Watetezi wa Rasilimali za taifa Wasio na Mipaka (WARAMI) wameibuka na kupinga vikali kitendo hicho kwa kusema Mahakama aingiliwi wala aipangiwi hivyo ni vyema wakaicha ifanyekazi kwa weledi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi wa Tafiti wa Warami, Philipo Mwakibinga, alisema kitendo kilichofanywa na Mbowe cha kulalamika kwa vyombo vya habari kuhusu kesi ambayo bado ipo mahakamani, ni fedheha na kuidhalilisha Mahakama.

Amesema Mbowe kupitia tamko lake alidai kuwa kuna viashiria ambavyo vinaonyesha kuwa mahakama inaingiliwa na dola huku akijua kwamba si kweli na kwamba mahakama ni mhimili unaotenda kazi zake kwa uhuru.

“Si mara ya kwanza kwa Mbowe kuingilia uhuru wa mahakama hasa pale anapoona kuwa kusa analoshtakiwa nalo linaweza kumtia hatiani kwa mujibu wa sheria,” alisema Mwakibinga na kuongeza Mbowe anafanya hivyo kwa nia ya kupata huruma ya watanzania.

“Jana (juzi) kupitia tamko lake alisema kuwa dola inaingilia mahakama ili kuishinikiza yeye ashindwe. Utagundua kwamba huku ni kuvunja sheria na taratibu ambazo tumejiwekea. Tunafahamu kwamba suala lililopo mahakamani halipaswi kuzungumzwa katika public (hadharani) likiwa bado linaendelea mahakamani,” amesema Mwakibinga.
Mkurugenzi wa Tafiti wa Warami, Philipo Mwakibinga.



WAZIRI AZINDUA RIPOTI YA TAKWIMU YA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINADAMU LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ), Mohamed Aboud Mohamed (aliyeshika mkasi), akizindua Ripoti ya Takwimu ya Biashara Haramu ya Usafirishaji wa  Binadamu kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakati wa kuhitimisha warsha iliyozikutanisha nchi 16, uliokuwa na lengo la Kupambana na  Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo, uliofanyika leo  jijini  Dar es Salaam. Kulia ni  Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana  na  Biashara  Haramu  ya  Binadamu, Amatus Magere. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ), Mohamed Aboud Mohamed akizungumza wakati wa Uzinduzi wa  Ripoti ya Takwimu ya Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa  Binadamu  kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa  Afrika (SADC), wakati  wa  kuhitimisha warsha iliyozikutanisha nchi 16, uliokuwa  na  lengo la  Kupambana na  Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa  Binadamu, Tanzania  ikiwa mwenyeji  wa  mkutano huo, uliofanyika leo  jijini  Dar es Salaam. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ), Mohamed Aboud Mohamed,akisalimiana na wawakilishi wa nchi mbalimbali baada ya  kuzindua  Ripoti ya Takwimu ya Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa  Binadamu kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakati wa kuhitimisha Warsha iliyozikutanisha nchi 16, uliokuwa na lengo la Kupambana na  Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu,Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo,uliofanyika  jijini Dar es Salaam.

Waziri  wa  Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ), Mohamed Aboud Mohamed (katikati mstari wa mbele), akiwa  katika  picha  ya  pamoja  na  Washiriki kutoka  nchi 16 baada ya kuzindua  Ripoti ya Takwimu  ya  Biashara  Haramu ya Usafirishaji  wa  Binadamu kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakati wa kuhitimisha  Warsha iliyozikutanisha  nchi  hizo, uliokuwa na lengo la Kupambana na  Biashara Haramu  ya  Usafirishaji  wa  Binadamu, Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo, uliofanyika leo  jijini Dar es Salaam. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi.

TABORA: WATU WATATU WAKAMATWA NA POLISI KWA MATUKIO MATATU TOFAUTI

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora limewakata watu watatu kwa matukio tofauti akiwemo dereva aliyekuwa akiendesha Treni ya abiria huku akiwa amelewa na wengine wawili walikutwa wakisafirisha madawa ya kulevya aina ya Bhangi.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo imemtaja Dereva aliyekamatwa akiendesha treni ya abiria akiwa amelewa kuwa ni Elirehema Macha mkazi wa Dodoma.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Emanuel Nley alisema kuwa dereva huyo alikamatwa wiki iliyopita baada ya kuendesha treni ya abiria namba B 12 iliyokuwa ikitoka Dar es salaam kuelekea Kigoma akiwa amelewa na kutosimama kusimama katika kituo cha Malongwe.


Aliongeza kuwa kitendo cha dereva kutosimamisha treni kwenye kituo hicho kulileta taharuki kwa abiria waliokuwa wakitelemka na wale waliokuwa wakitaka kupanda ndipo taarifa ikatolewa polisi ambao waliweza kumkamata.


Katika tukio jingine Kamanda Nley alisema Polisi imekamata na madawa ya kulevya Amos Maziku ambaye ni Ajenti wa mabasi na Hassan Selemani dereva ambao walikutwa kwenye Kituo cha mabasi Sagara cha mjini Nzega wakiwa na Bhangi kilogram 51.45 wakiisafirisha.

Kamanda Nley alisema kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha bhangi hiyo kwenye basi la Shabco lenye namba za usahili T 501 BRZ lililokuwa likielekea jijini Mwanza huku wameweka ndani ya Ndoo kubwa ya maji na wamefunga ndani ya mifuko ya Sandarusi wakiwa wamechanganya na sufuria na sahani ili wasijulikane.


Aidha Kamanda huyo alisema katika misako inayoendelea wamefanikiwa kukamata Silaha mbili zilizotengeneza kienyeji

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Emanuel Nley akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya kukamatwa kwa watu mbalimbali kwa ajili ya matukio mbalimbali ya kihalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Emanuel Nley akiwaonyesha leo waandishi wa habari bhangi iliyokamatwa juzi Wilayani Nzega katika Stendi ya Mabasi ya Sagara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Emanuel Nley akiwaonyesha leo waandishi wa habari bastola iliyokamatwa juzi Wilayani Igunga hivi karibuni katika misakao ya kusaka wahalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Emanuel Nley akiwaonyesha leo waandishi wa habari Silaha aina ya Gobole iliyokutwa Porini baada ya Mhusika kujinyonga kwa kuogopa kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumua mke wake kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.

Matumizi bora ya Mtandao-Maadili na Kizazi Kipya-MAKIKI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James M. Kilaba akisisitiza kutumia vizuri Mfumo wa Mawasiliano kwa ajili ya Maendeleo yetu na kwa Faida ya Umoja na Mshikamano wa Taifa Letu.

DKT. HASSAN ABBASI AWATAKA WANAHABARI KUITANGAZA VYEMA TANZANIA NCHINI CHINA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James M. Kilaba alonga

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James M. Kilaba asisitiza tutumie Vizuri Mfumo wa Mawasiliano kwa ajili ya Maendeleo yetu na kwa Faida ya Umoja na Mshikamano wa Taifa Letu.

Wafanyakazi 54 wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Watunukiwa vyeti vya ufanyakazi bora

$
0
0
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamesisitizwa kufanya kazi kwa bidii , na kuzingatia nidhamu katika utendaji wao ili kutoa huduma bora na yenye viwango vya juu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru alipokuwa akizungumza katika hafla fupi ya kuwatunuku Vyeti  wafanyakazi bora 54 wa Hospitali hiyo kwa mwaka 2018.
Akizungumza katika hafla hiyo  iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwatunuku vyeti wafanyakazi hao, amesema serikali inathamini mchango wa kila mmoja katika kuhudumia Umma hivyo wafanyakzi wote hawana budi kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa bidii bila kusukumwa.
‘’Nawapongeza kwakutoa huduma bora katika hospitali yetu naomba muendelee kuwa mabalozi wazuri , kwani mmekuwa mfano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yenu ikiwa ni pamoja na utunzaji wa vifaa na kutoa lugha nzuri wakati wa kuwahudumiwa wateja’’. Amesema Prof. Museru.
Awali akikaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala Bwn. Makwaia Makani amesema wafanyakazi bora 54 hao wamewakilisha Idara mbalimbali, majengo  na vitengo vya hospitali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) Prof. Lawrence Museru (Katikati) akizungumza na baadhi ya watumishi wa MNH katika hafla fupi ya kuwatunuku vyeti wafanyakazi bora  wa hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala Bwn. Makwaia Makani, kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi Bwan. Mziwanda Salum na anayefuatia ni Afisa Utumishi Bwn. Michael Ngowi.
 Prof: Museru akimkabidhi cheti cha ufanyakazi bora Theophil Joseph

 Mmoja wa wafanyakazi bora Muuguzi Msaidizi Bi. Mkatareto Akyoo  akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Prof. Museru.
 Mfanyakazi bora kwa mwaka 2018 Philip Simya akikabidhiwa cheti mapema leo .
Wafanyakazi bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Prof; Lawrence Museru.

Balozi Seif Ali Iddi atembelea nyumba iliyoteketezwa na moto mtaa wa Rahaleo, Unguja

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameinasihi Jamii Nchini kuwa na tahadhari kubwa wakati wa matumizi ya vifaa vya umeme ili kuwepuka madhara yanayoweza kuleta maafa makubwa hapo baadae.
Alisema Huduma ya umeme ni nzuri na muhimu katika matumizi ya mwanadamu kwenyea harakati zake na kimaisha za kila siku lakini inaweza kuwa janga iwapo mwanaadamu huyo ataamua kutumia huduma hivyo ovyo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo muda mfupi tu alipopata taarifa ya kutokea kwa Janga la Moto katika Nyumba ya Familia ya  Marehemu Maalim Rajab Mgeni iliyopo Rahaleo mbele ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Muembe Shauri.
Hata hivyo hakuna mtu aliyepata matatizo kutokana na mripuko wa moto huo uliosababishwa na kuungua kwa Hita iliyokuwemo kwenye Nyumba hiyo ambayo wakati inawaka alikuwemo Kijana Mmoja wa familia ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda maisha na mali za Rais imeazimia kujenga Vituo vya Huduma za Zimamoto kila Wilaya kwa lengo la kuwa tayari wakati yanapojitokeza matukio ya majanga.
“ Umeme tunaupenda  sana katika matumizi yetu ya kawaida ya kila siku lakini pia unahatari iwapo hatutakuwa makini katika matumizi yake ya ovyo”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikipongeza Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kwa umakini wake uliopelekea kuuzima moto huo kwa dakika chake na kuepusha maafa ya kuendelea kuathiri nyumba zilizo jirani na eneo hilo.
Balozi Seif pia akalipongeza Shirika la Utangazaji Zanzibar {ZBC – REDIO} kwa kuwapasha Wasikilizaji Wananchi katika mfumo wake wa matangazo wa moja kwa moja wa haraka { Breakingnews} ambao ulisaidia baadhi ya Wananchi wa karibu na maeneo hayo kufika mara moja kusaidia kuiokoa Nyumba hiyo.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alisema licha ya uharaka na utayari wa Wananchi na vyombo vya Dola katika kuokoa maafa lakini bado lipo changamoto kubwa la baadhi ya Wananchi kujenga makaazi yao bila ya kuzingatia mipango miji.
Balozi Seif  alieleza kwamba ujenzi wa nyumba  katika baadhi ya maeneo bila ya kufuata  utaratibu wa ujenzi hupelekea Kikosi cha Zima moto na Uokozi kupata usumbufu wakati wa majanga kutokana na Magari yao kusindwa kupenya katika baada ya Mitaa.
Nyumba hivyo ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni iliyorithiwa na Watoto Tisa hapo Rahaleo iliyoungua majira ya saa Moja na Robo asubuhi imeteketea kwa moto na hakuna kitu kilichopatikana ndani sambamba na kutofahamika hasara yake hadi hivi sasa.
 Mabaki ya Nyumba ya Marehemu Maalim Rajab Mzee iliyopo Mtaa wa Rahaleo ambayo iliungua moto mapema asubuhi uliosababishwa na Hiter ya Umeme.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud wakifika katika eneo la tukio kuifariji na kuipa pole Familia ya Watoto Tisa ya Marehemu Maalim Rajab Mzee kufuatia Nyumba yao kuungua Moto.
 Wa kwanza na wa Pili kutoka Kulia ni miongoni mwa Watoto  Tisa wa Familia ya Marehemu Maalim Jaba Mgeni wa Nyumba iliyoungua Moto mapema leo asubuhi katika Mtaa wa  Rahaleo  wakimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  mkasa uliowapata wa kuunguliwa Nyumba yao.
 Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kutoa pole na kuisisitiza Jamii kuwa na tahadhari ya matumizi salama ya huduma za Umeme ili kuepuka maafa. Picha na – OMPR – ZNZ.

INTRODUCING "PUSH PUSH" BY HENNESSEYY

Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images