Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

Maafisa Habari Watekeleze Wajibu Wa Kutoa Habari kwa Umma

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewataka Maafisa Habari Nchini kufanya kazi zao kwa kufuata sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambayo inawapa fursa Waandishi wa Habari kupata,kuhariri na kurusha habari kwa wananchi ili waweze kuelewa maendeleo ya nchi yao.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti Jijini Dar Es Salaam Ijumaa Agosti 24, 2018 alipotembelea Kampuni ya Magazeti ya New Habari na Shirika la Habari linalounganisha Redio zenye Maudhui ya kijamii la TADIO ambao walimweleza Msemaji Mkuu wa Serikali kuhusiana na changamoto za kupata habari wanazofanyiwa na baadhi ya Maafisa Habari wa Taasisi mbalimbali za Serikali Nchini.

“Ni kweli wapo baadhi ya Maafisa Habari ambao wanakwamisha juhudi za waandishi kupata Habari,Idara ya Habari MAELEZO tumeliona hilo na tulishaanza mkakati wa kuhakikisha kila taasisi inatoa habari ili wananchi waelewe maendeleo ya maeneo yao na taasisi hizo, tumekaa na Maafisa Habari mara kadhaa na tumewapa mafunzo na sasa changamoto hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa” alisema Dkt Abbasi.

Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba 5 Mwaka 2016 na Kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Novemba 16 mwaka huo huo wa 2016, pamoja na mambo mengine, inalenga kulinda maslahi ya waandishi wa habari,kulinda kazi zao pamoja na kuboresha Taaluma hiyo ili iweze kuheshimika kama taaluma ilivyo kwa zingine.

Aidha Dkt. Abbasi amezungumzia mkakati wa kuanzishwa kwa mfuko wa taaluma ya habari ili kuwawezesha waandishi kumudu kufanya kazi za utafiti wa habari na vipindi mbalimbali vya kijamii badala ya kutegemea ruzuku za mashirika ambazo pia huja kwa masharti ambayo mengi yanaweza kuwaingiza hatiani.

Aidha Dkt. Abbasi pia amewakumbusha Waandishi wa Habari nchini kujiunga na vyuo mbalimbali ili kujiendeleza kitaaluma na hatimaye waweze kuendana na kanuni ya kuwa na diploma itakayoanza kutumika mwishoni mwa mwaka 2021.

“Kanuni ya kumtaka mwanahabari awe na diploma kwenda juu katika fani ya habari itaanza kutumika mwaka 2021, tumetoa muda wa kutosha kabisa kwa waandishi kujiendeleza,kama hukufanya hivyo sheria haitakuruhusu kupata ithibati ya kuendelea na majukumu ya kazi za Habari,” alisisitiza Dkt. Abbasi.

TRA YATOA ELIMU KWA WAFANYABASHARA WA SOKO LA SIDO MBEYA

Uchukuzi SC yaahidi kuendeleza ubabe SHIMIWI

$
0
0
TIMU ya michezo ya Sekta ya Uchukuzi (USC), imeahidi kuendeleza ubabe kwa kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ya Watumishi wa Umma ikiwemo michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI); Mei Mosi na mabonanza mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho leo katika bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo ya SHIMIWI inayotarajia kufanyika Mkoani Dodoma kuanzia Septemba 25 mpaka Oktoba 3.
Mhandisi Dkt. Chamuriho amesema ana matumaini makubwa na timu ya Uchukuzi kwakuwa imekua ikileta ushindani na ushindi katika mashindano mbalimbali ambayo imekuwa ikishiriki.
"Nina imani kubwa sana na timu hii ya Uchukuzi kwa kuwa mmekuwa mkileta ushindi kila mnaposhiriki, nimefurahi pia kusikia kwamba mmeshida vikombe vinane vya ushindi wa kwanza, vikombe viwili vya ushindi wa pili na vikombe vitatu vya ushindi wa tatu na hivyo kuwa washindi wa jumla kwa kujikusanyia vikombe 13", alisema Dkt Chamuriho.
Hatahivyo, Dkt Chamuriho ameihimiza timu hiyo kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii, ili kupata mafanikio makubwa Zaidi katika michezo mbalimbali.
"Siku zote kuwa namba moja sio kazi ila kazi ni kubaki namba moja, hivyo nawahimiza muendelee kufanya mazoezi ili mzidi kuleta ushindi zaidi katika mashindano mnayoshiriki", alisema Dkt Chamuriho.
Pia, Dkt Chamuriho ameahidi kushughulikia changamoto zote ambazo zimekuwa zikijitokeza mara timu hiyo inapotaka kushiriki katika mashindano mbalimbali, ikiwemo changamoto za vifaa na malipo ya fedha za kujikimu kwa wachezaji wanapoenda kushiriki katika mashindano hayo.

"Nimezisikia changamoto zote mlizozisema zote tutazifanyia kazi, lakini ni muhimu pia kuzingatia mnapokua mnapanga bajeti zenu, ili kusudi muda wote mnapohitaji kushiriki mashindano ya michezo gharama zote zinakuwa tayari zimeainishwa katika bajeti", alisema Dkt Chamuriho.

Aidha amewaasa watumishi kuzingatia weledi mara zote hasa wakati wachezaji wanaokwenda kushiriki michezo mbalimbali wanapochaguliwa na kuepusha maneno kwamba wengine wameachwa ingawa wanaviwango bora.
Awali Katibu Mkuu wa USC, Bw. Mbura Tenga amesema mazoezi rasmi ya kujiandaa na michezo ya SHIMIWI yataanza Agosti 28 kwenye viwanja vya michezo vya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo wachezaji watachaguliwa kupitia makocha kulingana na kuwa na viwango vya juu.
Hatahivyo Bw. Tenga amesema timu hiyo inakabiliwa na changamoto ya vifaa, posho na ruhusa za wachezaji kutoka kwenye taasisi zilizozopo chini ya Uchukuzi, na kusababisha kupeleka wachezaji wachache tofauti na matarajio ya klabu.
Naye Mkurugezi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Bw. Paul Rwegasha ambaye alimwakilisha  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela amesema kwamba Mamlaka itaendelea kutoa kipaumbele katika ushiriki wake katika michezo ili kuweza kufanikisha ushindi wa pamoja katika timu.

"Napenda kukushukuru sana Katibu Mkuu kwa kuwa pamoja nasi siku hii ya leo, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini itaendelea kushiriki katika mashindano yote, ili kuonesha ushirikiano na ushikamano na kuleta ushindi wa pamoja katika sekta ya Uchukuzi", alisema Bw. Rwegasha.

Pia Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA),  Bw. Hamza Johari amesema kwamba Mamlaka hiyo itaendelea kupeleka wanamichezo zaidi, ili kuleta tija sehemu ya kazi, ambapo mtumishi mwenye afya njema huzalisha zaidi
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza Johari (wa pili kulia) akiwa na Katibu  Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho (wa tatu kushoto) akiwa katika bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo ya Wizara, Idara na Taasisis za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Wa pili kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Uchukuzi, Bw. Alphonce Mwingira.
 Timu ya wanawake ya kuvuta Kamba ya Uchukuzi wakivutana na wenzao ambao hawapo pichani katika bonanza la uzinduzi wa michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
 Timu ya wanaume ya kuvuta Kamba ya Uchukuzi wakivutana na wenzao ambao hawapo pichani katika bonanza la uzinduzi wa michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) lililofanyika leo kwenye Viwanja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Hamza Johari (mbele namba 11) akiwafanyisha mazoezi watumishi kutoka taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Sekta ya Uchukuzi, katika bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya TCAA.  Wa kwanza kulia mbele ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela katika michezo ya bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), lililofanyika leo kwenye viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Dkt Leonard Chamuriho (aliyesimama) akizungumza na wanamichezo wa Sekta ya Uchukuzi walioshiriki leo kwenye bonanza la uzinduzi wa mazoezi ya michezo Wizara, Idara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI) lililofanyika katika viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).


Afisa utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani rukwa afanya hip-hop kuonesha njia

$
0
0
Afisa utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa Charles Kiheka a.k.a K Chars ametoa kibao chake cha muziki wa hip-hop ili kuonyesha jamii uwezo alionao katika fani hiyo.na kuwaonyesha njia vijana wanaochipukia katika sanaa. 
 Afisa huyo amesema kuwa kutoa kwake wimbo huo ni kudhihirisha wazi kuwa maafisa utamaduni Tanzania nzima ambao wameaminiwa na serikali huwa hawabahatishi katika kutekeleza majukumu Yao yanayohusiana na kazi za Sanaa. 
 "Kazi yangu kama afisa utamaduni no kuhakikisha kuwa nashauri na kuwaonyesha njia vijana wenye vipaji vya sanaa ili iwe ajira kwao, Ofisi kwangu wanakuja wasanii wadogo wengi kunitaka ushauri tu, naweza pia kuifanya kazi hiyo na kuihamasisha jamii kupenda utamaduni na kazi za sanaa" alisema Kiheka. 
 Afisa utamaduni huyo alisisitiza kuwa mikoa iliyopo pembezoni ina vijana wengi wenye vipaji ila hawajapata fursa sahihi ya kuonyesha uwezo wao na kudhani kuwa mikoa hiyo haina vipaji vya kuleta ushindani katika sanaa, hivyo kupitia kazi yake hiyo na nyingine zijazo anaamini kuwa wasanii wa manispaa ya sumbawanga Mkoani Rukwa nao wataanza kusikika na kuutangaza mkoa. "Kwa miaka mingi Sumbawanga watu wamekuwa wakiitafsiri tofauti jambo hili limekuwa likiniumiza Sana kama afisa utamaduni na kuona hakuna namna bali kuanza kubadili fikra za watu kuhusu Sumbawanga, na huu ni mwanzo tu, mengine mazuri yanakuja",alisema. 
 Katika kuhakikisha wilaya ya sumbawanga inatambulika kisanaa afisa utamaduni huyo ameanza kuwaunganisha wasanii wanaofanya Sanaa za kufanana kama vile kuwa na shirikisho la wasanii wa maigizo, vikundi vya utamaduni, waimbaji, na madensa. Ambapo mwaka 2017 alianza na mashindano ya SUMBAWANGA DANCE SAKATA na mshindi wa Kwanza hadi wa tatu walizawadiwa fedha taslim na vyeti kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa hiyo.

WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Felix Lyaviva amewashauri wanafunzi waliopo shuleni kujiandaa kujiajiri na siyo kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo yao.
Lyaviva ametoa rai hiyo leo alipokuwa akifunga mafunzo ya ukakamavu ya wanafunzi wa Kidato cha Tano 2018 wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya jijini Dar es Salaam.
Akiwahutubia wanafunzi hao mbele ya wazazi, walimu, maafisa wa jeshi wakiwemo wastaafu na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, Lyaviva alisema; "Nawapongeza sana kwa mafunzo ya ukakamavu mliyopewa, mmeonesha ni jinsi gani mlivyoiva lakini niwaombe muwe na ndoto za kujiajiri siyo kuajiriwa mara mtakapotoka hapa."
Mkuu huyo wa wilaya, amewaasa wanafunzi kutojihusisha na vitendo vya mapenzi, uvutaji wa madawa ya kulevya na sigara ambavyo vinaathari kubwa katika maisha.
"Nyie wanafunzi wa kike, nawaasa msikubali kurubuniwa na wenzetu wa kiume kwani athari zake ni kupewa mimba ambazo zitawaharibia maisha yenu huku wao wakiendelea na masomo," alisema Lyaviva.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
 Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakifuatilia gwaride hilo.
 Kikosi cha nne kikitoa heshima kwa mgeni rasmi kilipokuwa kikitembea kwa mwendo wa haraka.
 Gwaride la ukakamavu likipita mbele ya mgeni rasmi.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akimkabidhi zawadi Julieth Peter aliyekuwa kamanda wa kikosi namba tatu kwa kuongoza vizuri kikosi chake. 



MTEKETA: NIMEFIKA DARAJA LA MAGUFULI KABLA SIJAFA

$
0
0
Ni la Mto Kilombero ,atoa shukran zake za dhati kwa Rais kwa niaba ya wananchi 

Na Ripota Wetu, Kilombero

MBUNGE wa zamani wa Kilombero, Abdul Mteketa (CCM), ametimiza azma yake ya kutembelea daraja jipya la Magufuli lililopo Wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Akizungumza leo baada ya kutembelea daraja hilo, alisema yeye alikuwa ni moja ya viongozi waliopigania ujenzi wa daraja hilo ukamilike haraka wakati Rais Dk. John Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya awamu ya tatu.

“Kama unavyojua katika maisha yangu ya kuumwa pengine nisingeliona hili daraja. Lakini leo nimefika na kuona kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli.

“Watu wa Kilombero, Ulanga na Malinyi tunamshukuru kwa dhati kiongozi wetu mpendwa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kulijenga taifa letu na kuleta maendeleo kwa kasi.“…tayari umekamilisha ujenzi wa daraja na ameshaweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Kidatu hadi Ifaraka- Ulanga, sasa ametufuta machozi watu wa Kilombero-Ulanga na kwa dhati ninampongeza Rais Magufuli,” alisema Mteketa

Akizungumza hali yake ya kiafya, alisema anamshukuru Rais Magufuli kwani kwa sasa hali yake imeimarika baada ya kupata msaada wa matibabu.
“Awali nilikuwa natembetea kwenye wheel chair lakini kwa sasa ninaweza alau kusimama kwa msaada wa magongo. Sina la kusema zaidi ya kusema asante Rais Magufuli nasi Watanzania tunakuombea kwa Mungu akupe afya njema ili uweze kuongoza taifa letu kwa upendo kama unavyofanya sasa,” alisema.

TANZANITE KUWA NA HATI YA UTAMBULISHO KIMATAIFA

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Dodoma
Serikali imesema inafanya utaratibu wa kuwa na Hati ya Utambulisho wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite, ambayo yanapatikana katika nchi ya Tanzania pekee katika vilima vya Mirerani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Agosti na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa Semina ya mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo imefanyika Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma.
Waziri Kairuki amesema kuwa, serikali inataka kuona kuwa dunia inafahamu kuwa, madini hayo yanapatikana Tanzania pekee na kuhakikisha kwamba yanajulikana zaidi.
Semina ya wabunge imefanyika kufuatia maelekezo ya Kamati hiyo ambayo ilitaka kufahamu kuhusu mwenendo mzima wa Madini ya tanzanite, biashara na udhibiti wa madini hayo baada ya kujengwa kwa Ukuta wa Mirerani unaozunguka migodi ya madini ya tanzanite, Muundo wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini na majukumu yao.
Waziri Kairuki amesema kuwa, Wizara imepata fursa ya kuwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwemo mikakati ya serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini hayo na mipango madhubuti ambayo serikali inakusudia kuifanya ili kuhakikisha kwamba rasilimali madini inalinufaisha taifa na hatimaye sekta ya madini iweze kufikia asilimia 10 ya machango wake katika pato la taifa ifikapo mwaka 2025.









Afisa Madini Mkazi wa Mirerani, Mhandisi David Ntalimwa, akieleza jambo wakati akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Nishati na Madini. 
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushauri na Uchambuzi wa Kazi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, akiwasilisha mada kuhusu Muundo na Majukumu ya Wizara ya Madini na Tume ya Madini. 
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizotolewa kwa kamati ya Bunge. 
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizotolewa kwa kamati ya Bunge. 

MAHOJIANO YA KUSISIMUA - MTANZANIA DAUDI MAYOCHA anayeishi MAREKANI na safari yake huko, alivyoingia na Dola 30


RAIS DKT MAGUFULI AKAGUA BUSTANI ZA MBOGA MBOGA ZILIZOKUWA ZIKILIMWA NA MAREHEMU DADA YAKE.

$
0
0


Picha mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua bustani za mbogamboga mbalimbali zilizokuwa zikilimwa na Marehemu Dada yake Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua bustani za mbogamboga mbalimbali zilizokuwa zikilimwa na Marehemu Dada yake Monica Magufuli katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.

MBUNGE MAVUNDE AITAKA JAMII KUSHIRIKIANA NA SERIKALI NA VIONGOZI WAO KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde amewataka wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kushirikiana na serikali na Viongozi wao katika kujiletea maendeleo na kutoa wito kwa jamii kujitoa kwa dhati kuchangia maendeleo kama wanavyofanya kwenye shughuli mbalimbali za kijamii hasa katika sherehe mbalimbali zikiwemo harusi.

Mavunde ameyasema hayo jana wakati akiongoza mamia ya wananchi wa kata ya kikuyu kusini katika ujenzi wa vyumba vya madarasa leo Jijini Dodoma ambapo Mbunge huyo amechangia matofali 1000 na mifuko ya Saruji 130,Computer 1,Jezi na mipira pamoja kuweka magoli ya Chuma katika uwanja wa michezo uliopo katika Shule ya Msingi Kikuyu B.

Akimuunga mkono Mh Mavunde,Mbunge wa Jimbo la Bahi Mh Omary Badwell amewapongeza wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini kwa muitikio wao mkubwa kwenye shughuli za maendeleo na kuahidi kushirikia na Mh Mavunde kutatua changamoto za shule hiyo kwa kuchangia **mifuko 20 **ya Saruji iliyopo eneo ambalo na yeye ni mkazi wake na watoto wake pia wanasoma katika shule husika.

Aidha Diwani wa kata ya Kikuyu Kusini Mh Kutika amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kusaidia kutatua kero hiyo ya ukosefu wa vyumba vya madarasa na hivyo ujenzi huo utasaidia kuboresha miundombinu ya shule hiyo na hivyo kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde akiongoza mamia ya wananchi wa kata ya kikuyu kusini katika ujenzi wa vyumba vya madarasa Jijini Dodoma, ambapo Mbunge huyo amechangia matofali 1000 na mifuko ya Saruji 130,Computer 1,Jezi na mipira pamoja kuweka magoli ya Chuma katika uwanja wa michezo uliopo katika Shule ya Msingi Kikuyu B.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa Jijini Dodoma, ambapo Mbunge huyo amechangia matofali 1000 na mifuko ya Saruji 130,Computer 1,Jezi na mipira pamoja kuweka magoli ya Chuma katika uwanja wa michezo uliopo katika Shule ya Msingi Kikuyu B.

RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE KUMUWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA ZIMBABEWE MJINI HARARE

$
0
0
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi hii kuelekea Harare nchini Zimbabwe ambapo anakwenda Kumuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwenye  Sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe.Emmerson Mnangagwa zinazofanyika leo tarehe 26 Agosti, 2018 katika uwanja wa michezo waTaifa Mjini Harare.
Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam,  Mhe.Rais Mstaafu  Kikwete ambaye amefuatana na  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg. Philip Mangula na Mwenyekiti wa Chama cha UDP Ndg. John Cheyo , amesema Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu  wa kindugu kwani katika kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya wananchi wake  waliwahi kuishi nchini Tanzania, husasani wanachama wa Chama cha ZANU PF, na kupata mafunzo hapa nchini.
‘’Baadhi ya wanajeshi wetu wameshiriki pamoja na wanajeshi wa Zimbabwe katika harakati za ukombozi wa Zimbabwe na ndio maana kwenye Jeshi letu kuna medani ya Zimbabwe’’ amesema Rais Mstaafu Kikwete.
Rais Mnangagwa anaapishwa leo kuongoza taifa la Zimbabwe baada ya kushinda katika uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 30 Julai, 2018
Imetolewa na: Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Agosti, 2018

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda ndege ya Rais tayari kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo Mhe.  Emmerson Dambudzo Mnangagwa zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg. Philip Mangula akiwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP) Ndg. John  Momose Cheyo wakiwa ndani ya ndege ya Rais kabla ya kuondoka kuelekea mjini Harare, Zimbabwe, kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo Mhe.  Emmerson Dambudzo Mnangagwa  zinazofanyika leo Jumapili Agosti 26, 2018. Katika safari hiyo viongozi hao wanafuatana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) ambaye atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Picha na IKULU

TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto-Kigoma

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa elimu juu ya namna ya kuomba msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali mkoani Kigoma, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Rose Mahendeka amewaambia wafanyabiashara hao kuwa lengo la kutoa msamaha huo ni kuwapunguzia mzigo ili waweze kulipa kodi ya msingi isiyokuwa na riba wala adhabu ambapo mwisho wa kulipa kodi hiyo ni tarehe 30 Juni, 2019.

“Serikali imeamua kutoa msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 ili kuwasaidia wafanyabiashara kulipa kodi ya msingi tu ambayo mfanyabiashara anaweza kuilipa mara moja au kwa awamu ndani ya Mwaka wa Fedha 2018/19,” alisema Mahendeka.

Mahendeka ameeleza kuwa, msamaha huu ni wa miezi 6 na ulianza mwezi Julai na utamalizika Desemba, 2018 na kuongeza kuwa huu ni muda muafaka wa wafanyabiashara hao kutuma maombi ya msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

“Natumia fursa hii kuwasihi wafanyabiashara kutuma maombi TRA ya msamaha huu kabla ya mwezi Novemba, 2018 na msisite kuwasiliana na ofisi yetu ya hapa mkoani pindi mtakapohitaji ufafanuzi zaidi,” aliongeza Mahendeka.Aidha, Mahendeka alisisitiza kuwa TRA itatoa majibu ya maombi ya msamaha huo kwa maandishi ndani ya siku thelathini (30) tangu siku ya kupokea maombi.
Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka akitoa elimu juu ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Chama Siriwa akiwasilisha mada kuhusu msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi wakati wa semina elekezi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

Baadhi ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali waliohudhuria semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo.

Baadhi ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali waliohudhuria semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi iliyofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu msamaha huo. 


WADAU WAOMBWA KUISAIDIA TABLE TENNIS

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu ya taifa ya tennis ya walemavu (Table Tennis) imeshindwa kusafirisha wachezaji wake kuelekea nchini Malaysia kutokana na uhaba wa fedha pamoja na vifaa ikiwemo viti (wheel chairs)

Kocha wa timu hiyo Riziki Salum amesema changamoto kubwa katika chama chao kumekuwa ni uhaba wa fedha unaopelekea kushindwa kuwasafirisha wachezaji wake kuelekea katika mashindano mbalimbali.

Riziki amesema, katika safari ya Malaysia wamempeleka mchezaji mmoja tu kwa ajili ya mashindano yaliyopo huko, wakati wanatakiwa wapeleke wachezaji japo wanne ili waweze .Amesema, kuna safari zingine ikiwemo ya Afrika Kusini ya Septemba 28 itahitajika kwenda kwa wachezaji wannne na gharama ni dola 400 kwa kila mmoja itakayotumika kwa ajili ya nauli ya kwenda na kurudi pamoja na malazi.

Ameongezea kuwa ndani ya mwaka huu kuna mashindano pia nchini Sweden, Ghana na Nigeria na gharama ya kusafirisha timu nzima inafikia dola 7000 ila watashindwa kuwasafirisha kutokana na ukata wa fedha.

Riziki amewaomba wadau wa table tennis kujitokeza kwa ajili ya kuisaidia timu yao kifedha ambapo kwa sasa wapo katika maandalizi kwenye kipindi hiki ili waweze kusafirisha timu nzima kuelekea Afrika kusini, Sweden, Ghana na Nigeria.
Timu ya Taifa ya tennis ya walemavu (Table Tennis)

NAIBU WAZIRI HASUNGA AWAITA WAWEKEZAJI KWENYE HIFADHI TANO ZILIZOPANDISHWA HADHI

$
0
0
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA 

Baada ya kuyapandisha hadhi mapori matano ya akiba, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kuwekeza katika Mapori hayo.

Aidha, Amesema Serikali imefuta kodi ya kuingiza magari ya watalii nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi kuingia katika biashara hiyo ikiwa lengo ni kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya Utalii. Ametaja aina ya uwekezaji unaohitajika kuwa ni ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya nyota moja hadi zenye nyota tano, nyumba za kulala wageni, uanzishwaji wa makampuni ya utalii pamoja na kutoa huduma za vyakula kwa ajili ya watalii.

Ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Karagwe mkoani Kagera kabla ya kutembelea ziwa Ngoma ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyopo katika Pori la Akiba la Kimisi ambalo ni miongoni mwa mapori yaliyo katika mchakato wa kuwa hifadhi za taifa.

Naibu waziri huyo anatembelea mapori ya mkoa wa Kagera kufuatilia hatua iliyofikiwa na Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA)katika kuyaendeleza. Amesema Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika ni hazina na fursa kwa mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kufunguka kiutalii kwa wananchi wa maeneo hayo na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa ramani inayoonesha Ziwa Ngozi ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika Pori la Akiba la Kimisi na aliyekuwa Meneja wa Pori hilo Bigilamungu Kagoma wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngala pamoja na baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( katikati) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wakati alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa, Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Godfrey Luheluka 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akisaini kitabu cha  wageni mara alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU) 

ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuhudia wananichi wa mkoa wa Mwanza    wakiteketeza zana haramu  wakizozisalimisha  katika ziara yeke ya  kuhamasisha  ufungaji samaki kwa vizimba katima Ziwa Victoria.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafanyabiashara na wavuvi  katika soko la  samaki la kimataifa Kirumba jiji Mwanza ambapo amewaomba kulipa kodi ili kuongeza patato la taifa.
 Maibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza wakikagua  miundombinu ya soko la samaki kimataifa la Kirumba.

Sehemu ya wavuvi pamoja na wafanya biashara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.

Na Leandra Gabriel, Glob ya jamii.
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza Maafisa uvuvi  kuweka hadharani tozo za samaki pamoja na mazao ya uvuvi kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo.

Ulega amesema hayo leo katika soko la samaki la kimataifa la  Kirumba jijini Mwanza wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya mifugo na uvuvi.

Ulega ameeleza kuwa viongozi husika lazima wajue na kutambua majukumu yao bila kusubiri Waziri kuja kukagua maendeleo ya masoko. Na amewataka na maafisa na wafanyabiashara kukaa na kupanga mikakati ya kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha ameagiza kuwa masoko yote ya  samaki yaweke wazi tozo ambazo mfanyabiashara anatakiwa kulipa pindi wanunuapo bidhaa.

Pia Naibu Waziri amewataka Maafisa kutembelea masoko kila wiki ili kujua maendeleo ya masoko, Kuhusu udhibiti wa uvuvi haramu Ulega amewapongeza wavuvi kwa kutii sheria bila shuruti kwani hakuna nyavu haramu iliyokamatwa katika ukanda wa ziwa Viktoria na Kayenze.

 Pia amewashauri wafanyabiashara kujua tozo wanazotakiwa kutoa kabla ya kununua mizigo kwani itawasaidia sana katika ufanyaji wao wa biashara kwa kutambua kiasi wanachotakiwa kulipa kama tozo kuliko kutoa tozo bila kujua nj kiasi gani wanatakiwa kulipa.

Kwa upande wao wavuvi pamoja na wafanyabiasha ra wameishukuru serikali kwani kwa sasa samaki wanapatika tofauti na mwaka jana na wamewataka maafisa kushirikiana nao ili kuweza kufikia malengo ya juu zaidi.

TAZAMA LIVE MATANGAZO YA KUAPISHWA KWA RAIS WA ZIMBABWE MJINI HARARE HIVI SASA

TEMESA KUSIMIKA TAA ZA BARABARANI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kulia na kaimu Meneja wa Kikosi cha Umeme kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Pongeza Semakuwa wakitia saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio hilo lilifanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, huo ni mradi wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kulia akifurahia jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu kushoto mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, mradi huo ni wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kushoto akijadiliana na uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, mradi huo ni wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja Kikosi cha Umeme TEMESA Mhandisi Pongeza Semakuwa, Mtendaji Mkuu Dkt. Mussa Mgwatu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Shomari Shomari na mwanasheria wa TEMESA Bi. Joyce Senkondo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt Mussa Mgwatu, Mhandisi Pongeza Semakuwa, Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara hiyo Ndg. Hatibu M. Hatibu na kushoto ni Mwanasheria Bi. Joyce Senkondo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Shomari Shomari. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA ZANZIBAR)

Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF William Erio ametembelea daraja la Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara ya lami yenye urefu wa Kilomita mbili inayo unganisha daraja la Nyerere na barabara ya Feri - Kibada iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akikagua barabara hiyo mwishoni mwa wiki, William Erio amemtaka Mkandarasi CRJE kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa haraka na kuhakikisha gharama ya ujenzi hazizidi kiasi cha gharama kilicho kubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi kati ya NSSF na Mkandarasi huyo.

Kwa upande wa Mkandarasi amepokea maelezo ya Mkurugenzi Mkuu na kuahidi kutekeleza ujenzi huo. Pamoja na kuahidi utekelezaji, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda kutokakana na changamoto za kupatikana kwa malighafi ya udongo hasa ile ya G15.

Gharama ya mradi huu ni Tsh 21.3 billioni ambao unahusisha ujenzi wa barabara yenye njia sita, tatu kila upande zenye urefu wa kilomita mbili kutoka mwisho wa daraja hadi kwenye makutano ya barabara ya Fery - Kibada.

Pia, ujenzi unajumuisha mzunguko wenye mita za mraba 5,762, mifereji ya maji taka na yale ya mvua, kingo za katikati ya barabara "new jersey barriers", kalavati nne za umbo la boksi na moja ya ya umbo la bomba.
Sehemu ya kipande cha barabara unganishi kutoka mwisho wa daraja upande wa Kigamboni kuelekea barabara ya Fery - Kibada.Kaimu Meneja wa Miradi NSSF Abdon Mhando (wa pili kushoto), akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio (wa kwanza kushoto), wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF Bw. Gabriel Silayo.

HAKUNA SEKTA YOYOTE ISIYOHITAJI HIFADHI YA MAZINGIRA – MAKAMBA

$
0
0
Siku ya Sita ya ziara ya Waziri Makamba imemfikisha Mkoani Geita, Wilayani Chato katika Kijiji cha Nyamirembe ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Makamba ametembelea Kisiwa cha Magafu na kuahidi kutuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya tathmini ya namna ya kulinda kisiwa hicho kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, ikiwa ni eneo tengefu kwa mazalia ya samaki. 

Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Geita Waziri Makamba amesema kuwa jitihada za Serikali ni pamoja na kuhakikisha ulinzi madhubuti kwa kisiwa hicho ili kiwe kielelezo cha mandhari tulivu kwa mazalia ya samaki na bioanuai.

Waziri Makamba amesema kuwa hakuna sekta yoyote muhimu kwa uchumi wa nchi isiyohitaji Hifadhi ya Mazingira hivyo Sheria ya Mazingira kifungu namba 51 inatoa mamlaka na nafasi ya kulinda maeneo nyeti na kuainisha kuwa kuna dhana potofu kuwa uhifadhi wa mazingira ni kinyume na maendeleo.

Dhana ya uhifadhi inaendana na utashi, uwezo, utayari na ushirikishwaji wa wananchi wenyewe. “Tunapoongelea uhifadhi tunaamanisha, kuweka utaratibu wa kutumia maeneo yaliyopendekezwa kuhifadhiwa kwa taratibu zitakazopendekezwa, mfano kama tunahifadhi kisiwa, tutaweka utaratibu maalumu wa uvuaji wa samaki katika eneo hilo” Makamba alisisitiza.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nyamirembe juu ya utayari wao wa kuhifadhi mazingira ya Kisiwa hicho ili kuwa miongoni mwa maeneo yanayopendekezwa kulindwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua maeneo ya Kisiwa cha Magafu, takribani mwendo wa dakika thelathini kutoka mwalo wa Nyamirembe. Waziri Makamba aheahidi kutuma wataalamu ili kujiridhisha zaidi kabla ya kutanga katika gazeti la Serikali. 


Waziri Mwakyembe Atoa Miezi 3 kwa Maafisa Utamaduni kukamilisha Ukusanyaji Maoni Ya Sera

$
0
0


Na Anitha Jonas – WHUSM- Marangu Kilimanjaro – Moshi

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya kuwahimiza wadau wa Sekta ya Utamaduni kuwasilisha maoni yao ndani ya miezi mitatu.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Saba wa Umoja wa Machifu nchini wenye lengo la kujadili namna ya kuhakikisha umoja huo unasajiliwa kisheria pamoja na kuzungumzia nini kifanyike kutokana na kuwepo na mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa kiasi kikubwa.

“Serikali iko katika mchakato wa kufanya maboresho ya Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ambayo imeonekana kuwa na mapungufu kulingana na hali ilivyosasa,hivyo basi nitoe rai kwenu Machifu kama wadau wakuu wa Sekta ya Utamaduni kutoa maoni yenu kwa haraka kwani yatasaidia kwa asilimia kubwa kuongeza ubora katika sera hii tunayoboresha na hivyo basi hakikisheni mnawasilisha maoni yenu kwa Maafisa Utamaduni ndani ya miezi hiyo,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle alieleza kuwa umoja huo ulianza tangu mwaka 2014 na mpaka sasa unajumla ya wanachama 105 na kupitia umoja huo umekuwa ukisisitiza wajumbe wake kusimamia utunzaji mazingira pamoja usimamazi wa maadili katika jamii kwani machifu ndiyo mhimili wa kulinda utamaduni wa taifa.

“Mbali na Machifu hawa kujitahidi kupigania usimamizi wa maadili katika jamii zao wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi kwani kwa baadhi ya maeneo wamekuwa wakitolewa maneno ya dharau na kejeli kwa kuwaelezwa kuwa utawala wao umepitwa na hauna maana kwa sasa ombi letu kwa serikali ni kuhakikisha kupitia maoni yetu tutakayowasilisha kwa ajili Sera hii ya Utamaduni inayofanyiwa marekebisho yatiliwe mkazo ili kuonyesha wa nguvu ya machifu kwa jamii,”alisema Marrialle.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(katikati) akitoa maagizo kwa Maafisa Utamaduni Mkoa na Wilaya nchini kukamilisha ukusanyaji wa maoni ya wadau wa Sekta ya Utamaduni kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,Kushoto ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi.Lilian Beleko kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle (kushoto) akitoa ahadi ya umoja huo kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya kuboresha Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe(hayupo pichani) katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,kulia kwake ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela. 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhi nakala 21 za Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwa Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela (kushoto) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania,uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kugawa kwa Machifu waliyoshiriki Mkutano huo ili waweze kutoa maoni yao kutokana na mapungufu ya sera hiyo inayofanyiwa marekebisho.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe aliyeketi (watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Machifu wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Umoja wa Machifu Tanzania uliyofanyika leo katika Kijiji cha Marangu Mkoani Kilimanjaro,wanne kulia ni Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela,na wanne kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Frank Marrialle. 


Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images