Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

MWANZA:MMOJA AFARIKI DUNIA KUMI WAJERUHIWA KATIKA AJALI

$
0
0

MAGARI MAWILI YANAYOBEBA WANAFUNZI YAMEGONGANA NA KUSABABISHA KIFO KWA MTU MMOJA NA KUJERUHI WATU KUMI WILAYANI ILEMELA.


KWAMBA TAREHE 23.08.2018 

MAJIRA YA SAA 05:50HRS ALFAJIRI KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SIMIYU ENEO LA NANENANE WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.506 BYE AINA YA MITSUBISHI ROSA, MALI YA SHULE YA KIVULINI PRIMARY SCHOOL, LIKIENDESHWA NA DAEREVA AITWAYE KURWA CHARLES WAYALA MIAKA 27, MKAZI WA KISESA, LILIGONGANA NA GARI NAMBA T.745 ANF AINA YA NISSANI CIVILIAN, MALI YA NYAMUGE PRIMARY SCHOOL, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ALBERT MUSA  JORAM, MIAKA 58, MKAZI WA NYAMUGE NA KUSABABISHA KIFO KWA DEREVA WA GARI LA NYAMUGE PRIMARY SCHOOL  ALBERT MUSA  JORAM KISHA KUJERUHI WANAFUNZI NANE, DEREVA WA GARI LA KIVULINI  PAMOJA NA KONDAKTA WA GARI LA NYAMUGE.


WANAFUNZI WATATU MAJERUHI PAMOJA NA DEREVA WA GARI LA KIVULINI PRIMARY SCHOOL WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, VILEVILE KONDAKTA WA GARI LA NYAMUGE PRIMARY SCHOOL BWANA ISAYA JOSEPH, MIAKA 21, AMELAZWA HOSPITALI YA SEKOU TOURE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, HALI ZAO WOTE ZINAENDELEA VIZURI.  AIDHA WANAFUNZI WATANO TAYARI WAMEPATA MATIBABU KATIKA ZAHANATI YA BUZURUGA HALI ZAO NI NZURI NA TAYARI WAMERUHUSIWA.


AIDHA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA CHANZO CHA AJALI NI UZEMBE WA DERE WA GARI LA KIVULINI AMBAYE ALIHAMA UPANDE WAKE KISHA KWENDA KULIGONGA  GARI LA SHULE YA MSINGI NYAMUGE. POLISI BADO WANAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA AJALI HIYO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA NA KUBAINI UPO UZEMBE BASI DEREVA WA GARI LA KIVULINI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE. 

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI  WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA. 

SAMBAMBA NA HILO PIA ANAWATAKA WANANCHI WAPAZE SAUTI DHIDI YA MADEREVA WAZEMBE ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUSHUGHULIKIWA KWA MUJIBU WA SHERIA.

IMETOLEWA NA:

DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

Kabeho asisitiza wazazi kuwaandikisha watoto shule

$
0
0

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Charles Kabeho akizungumza na wananchi wakiwemo wanafunzi alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Kishapu.

Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Kishapu

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho amewasisitiza wazazi kuwaandikisha watoto wao shule ili wapate elimu itakayowasaidia katika mazingira yanayowazunguka.


Kabeho alitoa kauli hiyo Agosti 20 wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2018 wilayani Kishapu wakati ukipitia miradi mbalimbali ya maendeleo.


Alisema wazazi wana wajibu wa kuwasomesha watoto wao na si kuwapa majukumu ambayo yanawanyima wasaa wa kwenda shule na kupata elimu.


“Ndugu zangu wazazi hivi sasa tunatambua Serikali yetu ya Awamu ya Tano inaendelea na Mpango wa elimu bure, imefuta ada na michango iliyokuwa mzigo kwa wazazi hivyo mtumie fursa hiyo kuwasomesha watoto wenu,” alisistiza.


Kiongozi huyo aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wananchi imewekeza katika ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo madarasa, mabweni, nyumba za walimu, mabwalo na vyoo ili elimu itolewe katika mazingira mazuri.


Alibainisha kuwa tangu mwaka 2015 hadi 2018 idadi ya wanafunzi walioanza chekechea imeongezeka kutoka 917,000 hadi milioni 1.1 huku darasa la kwanza wakifikia milioni 1.6 kutoka milioni 1.3 na darasa la kwanza ni asilimia 85.77


Alibainisha kuwa Serikali inafanya uwekezaji wa elimu imeajiri walimu wa sayansi lakini pia inatambua umuhimu wa sayansi imewekeza katika vifaa vya maabara katika shule za sekondari 1625 nchini hatua inayosaidia wanafunzi kusoma kwa vitendo.

WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA

$
0
0
 KAIMU Mganga  Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga  Mkoa  wa Pwani Ndaki Barnabas amethibitisha  kuwapokea  majeruhi watatu  ambao walijeruhuwa katika kata ya Bupu Wilayani Mkuranga na kundi la wafugaji  wanao sadikika kuwa ni kutoka jamii ya wamang'ati waliowavamia  jana jioni wakitokea katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani.

Dokta Ndaki amesema amewataja majeruhi hao kuwa ni  Leonard Kondo,  Mustafa Seif  na  Abdallah Rashid  waliopokewa hospitalini hapo na kupatiwa matibabu  majira ya saa nne usiku jana.

Dokta Ndaki anasema kuwa walipofikishwa hospitalini hapo hali za majeruhi hao zilikua mbaya na kuvuja damu lakini sasa wanaendelea vizuri baada ya kushonwa na kupata tiba ya awali huku akisema kuwa  Daktari wa zamu amepita na kutoa ruhusa kwa majeruhi wawili huku majeruhi mmoja  watampa rufaa ili aende kupata vipimo vya   XRay na kipimo cha Ultra Sound sababu ameumia kwenye maeneo ya ndani ya mwili ikiwemo  mbavuni na ana maumivu makali.
 Wakizungumza na globu ya jamii mchana huu wakiwa wodini wagonjwa hao wameelezea namna walivyovamiwa na kupigwa vibaya na wafugaji hao.


Akizungu huku akiwa kitandani  majeruhi Abdallah rashid  ambaye ni mkazi wa Mbagala amesema akuwa  yeye alikwenda Kisarawe kuwasalimia wakwe zake na kadhia hiyo ilimkuta wakati alipokwenda dukani kununua vocha ndipo ghafla  wakatokea  wamang'ati huku wakimuuliza kama ameonga ng'ombe aliyekatwa mguu akajibu hajaona ghafla wakamvamia na kuanza kumpiga  kwa kutumia gongo kichwani.

"Nikawaona wenyeji wanakimbia  na mimi nikaona hapo sasa kuna hatari nikakimbia nankwenda kujificha kwenye nyumba nikapata akili ya kumpigia Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lkn akasema yeye hivi sasa ameshahamishwa hivyo akaniambia nimpigie RPC mpya wa sasa nikafanya hivyo Kamanda wa sasa alipokea simu na kuniambia ndani ya nusu saa askari watakuwa wamefika kutuokoa kweli walifika ndani ya muda na wakatuchukua kutupeleka hosputali" anasema  majeruhi huyo.


Tukio limethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Philiberto Sanga huku akiahidi kuwa kesho ataambatana na Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Mkuranga  kwenda katika eneo la tukio.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Madiwani na wananchi waanzishe daftari la kuwaandika wageni wanaoingia nankutoka katika maeneo yao ili kudhibiti vitendo viovu.

WAZIRI LUGOLA AWAONGOZA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YAKE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA

$
0
0

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu) akizijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama baada ya Wizara yake kukutana na Kamati hiyo Jijini Dodoma leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu), akisoma Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu hali ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kipindi cha Agosti 2018 mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha Kamati hiyo ambapo wamekutana na  Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kupokea Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu hali ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kipindi cha Agosti 2018 na Taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Jeshi la Zimamoto, katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiingia katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge, jijini Dodoma leo, kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Nyuma ya Waziri, ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SHIWATA kumkumbuka Mwenyekiti wao Jumamosi

$
0
0
Mwenyekiti wa (SHIWATA) marehemu Cassim Taalib kusoto enzi za uhai wake.

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa dua kesho Jumamosi ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wao marehemu Cassim Taalib aliyefariki Juni mwaka huu.

Kaimu Mwenyekiti wa SHIWATA, Deo Kway alisema dua hiyo itakayoongozwa na shekhe wa wilaya ya Ilala wasanii mbalimbali na viongozi wa chama na serikali wamealikwa.

SHIWATA imekuwa ikisoma dua kila mwaka unakumbuka baba wa taifa,Julius Nyerere na kila inapotokea vifo vya wanachama wake ikiwemo vifo vya wasanii wa bendi ya taarabu ya Five Stars na mwigizaji wa filamu Steven Kanumba.

Marehemu Taalib atakumbukwa na Wanashiwata kwa mikakati yake ya kuwaunganisha wasanii na kuwatafutia maisha bora ya kuanzisha kijiji cha wasanii cha Mwanzega wilayani Mkuranga na kununua shamba kwa ajili ya wasanii.

Pia alikuwa msimamizi wa wanamichezo na kuendesha matamasha mbalimbali ya wasanii na kuinua vipaji vya wasanii wanaotamba katika fani mbalimbali za maigizo,sarakasi na ngoma za asili.

MKUU WA MKOA WA MWANZA ASHIRIKI MAZISHI YA BI ANNA MANASSE

$
0
0




MKUU wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella leo Agosti 23, 2018 ameungana waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi ya Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni bibi wa Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.

Mazishi ya Bi. Manasse ambaye alifariki dunia juzi Agosti 21, 2018 akiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu, yamefanyika katika makaburi ya nyumbani yaliyopo Kahangala wilayani Magu.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa serikali mkoani Mwanza, Mhe. Mongella amewaombea uvumilivu ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwahimiza kumuombea kwa Mola ili apumzike kwa Amani. 
 Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella aliye kaa katikati waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni bibi wa Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.
 Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam akiwa kwenye makaburi kwaajili ya kumzika bibi yake.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella  akiweka shahada kwenye kaburi la Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni bibi wa Mhe.Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.

UPELELEZI WA KESI YA MAUAJI YA MWANAJESHI BADO HAUJAKAMILIKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi dhidi ya kesi ya mauji inayomkabili Mwanajeshi MT 109795 Private Ramadhan Mlaku (28) anayedaiwa kuumua askari mwenzie, MT 79512 SGT Saimon Munyama bado haujakamilika na inasubiliwa ripoti ya mtaalamu wa milipuko ili kukamilisha.

Hayo yameelezwa leo Agosti, 23.2018 na wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba shauri hilo lilipoitishwa  mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Mwita amedai kuwa bado wanasubiri ripoti ya mtaalamu wa milipuko ili kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo na kuongeza kwamba mawasiliano kidogo yamesumbua kuhusu baadhi ya vielelezo baina ya Jeshi la JWTZ na Polisi, 

Baada ya taarifa hiyo, Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuharakisha mchakato huo ili hatma ya kesi ijulikane na ameiahirisha kesi hiyo hadi September 6,2018 kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa huyo ambaye ni Mwanajeshi wa Kambi ya Jeshi Makongo anadaiwa kutenda kosa la mauaji October, 30, 2017 akiwa Makao Mkuu ya JWTZ Upanga Ilala Dar es Salaam ambapo alimuua askari mwenzie MT 79512 SGT Munyama.

ZANTEL YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WAZEE ZANZIBAR

$
0
0
 Baadhi ya wazee waliohudhuria katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.
Mmoja wa wazee akipokea msaada wa chakula kutoka kwa mkuu wa Zantel Zanzibar,Mohammed Khamis Mussa (Baucha)
Baadhi ya wazee waliopokea msaada katika picha ya pamoja na Mkuu wa Zantel Zanzibar na viongozi wa serikali na Chama Cha Wazee wa Zanzibar 
Na Mwandshi Wetu.

Katika kusheherekea siku kuu ya Eid, kampuni ya mawasiliano ya Zantel, imetoa msaada wa chakula chenye thamani ya shilingi milioni nane katika kituo cha kutunza wazee cha ‘Amani Sebuleni kwa Wazee’ kilichopo Zanzibar.Msaada huo ni mwendelezo wa sera ya kampuni ya Zantel ya kusaidia shughuli za kijamii.

Msaada huo umetolewa katika kipindi hiki cha msimu wa sikuu ya Eid, kinadhihirisha kuwa Zantel inajali makundi mbalimbali yenye mahitaji kwenye jamii inakofanyia biashara zake. Msaada uliotolewa kwa wazee ni mchele, mafuta ya kupikia,sukari na unga,mbali na msaada huo wafanyakazi wa Zantel walijitoa kusafisha maeneo yanayozunguka kituo hicho cha kutunza wazee.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo.Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) alisema “Wakati huu tunaposheherekea sikukuu ya Eid Al Hajj, tunapenda jamii yetu kujisikia kuwa Zantel inawajali watu wote,bila kusahau makundi yenye mahitaji kama wazee, ndio maana tumeamua kutoa msaada wetu katika kituo cha kutunza wazee na kujitoa muda wetu kusafisha maeneo mbalimbali ya kituo hiki”.

Mussa aliongeza kusema kuwa Zantel imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya kusaidia jamii kama vile ya wakulima na wanafunzi lakini katika msimu wa sikukuu hii ya Eid Al Hajj, imetoa msaada kwa wazee ili nao waisherekee kwa furaha.”Mbali na kutoa msaada wa chakula kwa wazee wa Pemba na Unguja wafanyakazi wameshiriki kufanya usafi maeneo ya kituo cha Sebuleni kuonyesha kuwa wanawajali wazee hao na afya zao kwa kuhakikisha wanaishi katika mazingira safi” alisisitiza.

Yanga sc,Mtibwa Sugar vuta ni kuvute katika dimba la Taifa

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii.

IKIWA imebaki masaa machache tu kikosi cha Yanga kushuka dimbani  katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu 2018-19.         

Mabingwa hao wa kihistoria mara 27 watamenyana na wakatamiwa wa mkoa wa Morogoro  mtibwa sugar, ambapo msimu huu ligi inatarajia kuwa na ushindani kutokana na maandalizi yaliyofanywa kwa kila kikosi,  vilevile pia ongezeko la timu kutokea 16 hadi 20 litaleta msisimko.
   
Yanga iliyoweka kambi ya wiki mbili Mkoani Morogoro imerejea upya kwa nguvu zaidi baada ya kuichapa USM Alger mabao 2-1 katika mchezo wa wa Kombe la shirikisho,ambapo magoli ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke pamoja na Heritier Makambo mchezaji nyota raia wa Kongo.    

Msimu uliopita kikosi cha Yanga kilikuwa na wakati mgumu kwa wachezaji wake waandamizi  kuwa  majeruhi wa  mara kwa mara kwa wacheza  mpaka kupelekea timu  kushiriki mashindano mengi ikiwa na kikosi finyu.

"Sipendi  kuliona hilo litokee tena msimu huu, nitaakikisha angalau asilimia 80%  ya wachezaji wanakuwa na utimamu wa kimwili na naamini kutwaa ubingwa  msimu huu  kwa kuwa kikosi changu kipo vizuri na kipana"amesema kocha mkuu Zahera raia wa Kongo. 

Wachezaji wa yanga  watakaokuwa sehemu ya mchezo huo dhidi mtibwa ni 1 Claus Kindoki,2Juma Abdu,3Gadiel Michael,4Vicent Andrew,5Kelvin Yondan,6Papy  Kabamba,7Mrisho Ngasa,8 Feisal Aballa (Fei toto),9Heritier Makambo,10 Ibrahim Ajibu, pamoja na Deus Kaseke anaevalia  jezi namba 11.

Mchezo huo unatarajia kuchezwa leo majira ya Saa 12jioni katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha VIP A 10000,VIP B 3000,na kwa viti vingine vilivyobaki ni 1500.

AZAM YAPANGA KUANZA NA USHINDI DHIDI YA MBEYA CITY

$
0
0
KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Hans Van Der Pluijm, ameelezea mikakati yake kuelekea mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Mbeya City.

Mholanzi huyo wakati amesema kuwa jambo la muhimu ni kikosi chake kuanza vema msimu wa ligi kesho Alhamisi kwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu hiyo yenye maskani yake jijini Mbeya, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex saa 2.00 usiku.

“Maandalizi yetu kuelekea ligi yamefanyika vizuri matarajio yetu ni makubwa nadhani sio kwetu tu ni kwa kila mtu hadi hivi sasa tuna majeruhi wawili ambao hawawezi kuwepo kwenye mechi ya kwanza watakaokuwepo kwenye mechi zinazofuata lakini nafikiri tunatimu nzuri.

“Ninachojua kuhusu Mbeya City, siku zote wamekuwa wapinzani wagumu, sio tu wanapokutana na Azam FC au Simba au Yanga daima wamekuwa wakionyesha zaidi kuliko wanavyoonyesha mechi nyingine lakini najua kitu cha kufanya na ndio maana nipo hapa, tunatarajia mchezo mgumu,” alisema Pluijm.   

Azam FC itaingia kwenye msimu mpya wa ligi ikiwa na morali kubwa baada ya kutwaa ubingwa wa pili mfululizo wa michuano ya Kombe la Kagame, ikiifunga Simba mabao 2-1, yaliyofungwa na mshambuliaji Shaaban Idd, aliyehamia CD Tenerife ya Hispania na nahodha Agrey Moris, aliyefunga la ushindi akizima bao lililosawazishwa na Meddie Kagere.

Kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea, Ashanti Gold za Ghana, Singida United na Yanga, alisema ugumu wa mchezo huo sio kitu kwani kila mechi si sawa akidai anaamini wataibuka na ushindi baada ya dakika 90.

“Cha muhimu ni timu yetu kucheza kwa mpangilio na kutofanya makosa na kutumia nafasi tunazopata na mwisho wa siku baada ya dakika 90 naamini tutaibuka na ushindi,” alisema.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana ndani ya Azam Complex, Azam FC iliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Mbaraka Yusuph.

MBWANA SAMATTA APIGA HAT TRICK USIKU KUAMKIA LEO: Racing Genk vs Brondby 5-2 Highlights 24-Aug-2018

AZAM TV: HIGHLIGHTS: YANGA SC 2-1 MTIBWA SUGAR (TPL 23/08/2018)

MAHAKAMA KISUTU YAPOKEA NYARAKA ZA KANUNI ZA FEDHA TFF

$
0
0
*Ni kwa ajili ya kilelezo katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF,wenzake.

Na mwandishi wetu, Glogu ya Jamii
MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea nyaraka ya kanuni za Fedha za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kama kielelezo cha ushahidi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake wanne.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametolewa uamuzi huo, leo baada ya kupitia hoja za pingamizi za kielelezo hicho, zilizowasilishwa ba Wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza na zile za upande wa Jamuhuri.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri amesema si sahihi kusema nyaraka ya kanuni za fedha za TFF iliyowasilishwa mahakamani hapo imetengenezwa, 
 kwani hiyo ni nyaraka ya umma,  na chini ya sheria ya ushahidi haihitaji uthibitisho wa kisheria.

Hivyi amesema inakubalika na imepokelewa kama kielelezo cha ushahidi.

Uamuzi huo, umetolewa baada ya Katibu Mkuu wa (TFF), Kidao Wilfred wakati akiongozwa na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai kutoa ushahidi katika kesi hiyo, kudai kuwa TFF katika kukopa fedha inaongozwa na Kanuni za Fedha za TFF na katiba ya shirikisho hilo ya mwaka 2013 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2015.

Baada ya kueleza hayo, shahidi huyo aliomba mahakama ipokee katiba ya TFF na kanuni za fedha za shirikisho hilo kama kielelezo cha ushahidi kwenye kesi hiyo.

Wakili wa utetezi, Richard Rweyongeza na Abraham Senguji walipinga kupokelewa kwa nyaraka hiyo ya kanuni za fedha za TFF kwa madai ya kwamba nyaraka hiyo ni nakala na siyo halisi na kwamba imekuwa kama ya kutengeneza.

 Baada ya uamuzi huo kutolewa, Wakili Swai aalidai hawana shahidi kwani Shahidi Kidao ambaye alitarajiwa kuendelee kutoa ushahidi amepata udhuru kwa sababu wamepata ugeni kutoka CECAFA,  hivyo anahusika sehemu kubwa katika ugeni huo.

Kesi hiyo imeiahirishwa hadi Septemba 4 mwaka 2018 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Mbali na Malinzi washtakiwa wengine  katika kesi ni  Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine, Mhasibu wa TFF,  Nsiande Mwanga, Meneja wa  Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao Kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka 30 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na Sh. 43,100,000.

Waziri, Dr Harrison Mwakyembe (MB) Afafanua, FTA

LYANGA-TUNAWASAKA WAFUGAJI AINA YA KIBARABAIG WALIOWAJERUHI WATU SITA MKURANGA

$
0
0
  NA MWAMVUA MWINYI, MKURANGA
KAMANDA wa kanda ya kipolisi Rufiji,mkoani Pwani, Onesmo Lyanga ,amesema wanawatafuta wafugaji aina ya Kibarabaig, ambao walitoroka na mifugo yao, mara baada ya kuwajeruhiwa watu sita ,kijiji cha Kondo Mwilanzi, kata ya Bupu wilayani ,Mkuranga, mkoani Pwani. 

Aidha alieleza, thamani na ukubwa wa mashamba yaliyoharibiwa na ng'ombe aliyejeruhiwa, wanasubiri taarifa kutoka kwa wataalamu wa kilimo na mifugo.

Lyanga aliwaasa wafugaji ,kuacha tabia ya kutumia sheria mkononi kwa kutumia silaha mbalimbali ikiwemo za jadi ,ili kuepusha madhara makubwa baadae.

"Niyatake makundi ya wakulima na wafugaji kuheshimiana ,kila upande uthamini shughuli ya mwenzake ,na kuacha kushambuliana bila sababu zisizo na tija " alisisitiza Lyanga.
Lyanga alizitaka ,jamii hizo kuishi kwa amani pasipo kutishia amani.

Aliwataja ,walioshambiliwa ni pamoja na Abdallah Kiwembe (34),Shaban Mohammed (49),Nasra Ramadhani,(19),Mustapha Seif (38),Leonard Adolf na Imran Yasne (23)mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo cha SUA kozi ya maabara na Nasra Ramadhani.

Lyanga alitaja chanzo cha ugomvi kuwa ni ng'ombe wa wafugaji kuingia kwenye mashamba ya wakulima watatu ,ndipo walipomkata ng'ombe mmoja mguu na ugomvi ukaanzia hapo.

Baada ya hapo wafugaji walianza kuwashambulia wakulima kisha walitoroka na mifugo yao.

Kufuatia tukio hilo , mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga aliwataka wananchi kuwa watulivu kwani tayari vyombo vya ulinzi vimedhibiti hali ya vurugu na hali ipo shwari.

"Wafugaji hao ambao waliondolewa wilayani Kisarawe walifika kijijini hapo na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kusababisha kutokea kwa vurugu" alisema Sanga.

Nae diwani wa kata ya Bupu Abass Msangule alisema , majeruhi hao walipelekwa hospitali ya wilaya ambapo hali zao zinaendelea vizuri na kuviomba vyombo vinavyohusika na ulinzi kuimarisha ulinzi ili kuwadhibiti wafugaji hao.

Msangule alisema kuwa wafugaji hao walikwenda Kijijini hapo wakiwa na nia mbaya hali ambayo imewafanya wananchi wakose amani tangu kuingia kwa wafugaji hao ambao wana makundi ya ngombe.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa wilaya ya Mkuranga Ndaki Barnabas Mkuranga alielezea, alipokea majeruhi hao,majira ya saa nne usiku wakiwa wamejeruhiwa wawili waliumia kichwani na mwingine kifuani na mguu wa kushoto.
Alisema, hali zilikuwa si nzuri kwani walikuwa wakitoka damu na waliwashona wakawa wanaendelea vizuri ambapo wawili wameruhusiwa mmoja atafanyiwa vipimo zaidi ambaye aliyeumia kifuani ili afanyiwe Xray na ultra sound.

Nae mmoja wa majeruhi wa tukio hilo Abdallah Rashid ambaye ni mkazi wa Mbagala alieleza, yeye alikwenda Mkuranga kuwasalimia wakwe zake na kadhia hiyo ilimkuta wakati alipokwenda dukani kununua vocha .

"Ghafla wakatokea wafugaji hao huku wakimuuliza kama ameonga ng'ombe aliyekatwa mguu akajibu hajaona ghafla wakamvamia na kuanza kumpiga kwa kutumia gongo kichwani.

MBEYA:JESHI LA POLISI MBEYA LAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA UHUJUMU UCHUMI NANE

$
0
0

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 21/08/2018 limewafikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Mbeya watuhumiwa nane [08] kutokana na kosa la uhujumu uchumi kesi namba ECO/13/2018.
Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani ni pamoja:-

1.      BOSCO TAYARI [55]

2.      DAMAS RICHARD [25]

3.      HADI MWINUKA [38]

4.      NICOLAUS AMAN [20]

5.      ELIA JACKSON [50]

6.      MAJUTO MUSA [22]

7.      ANDREW JACKSON [19]

8.      ELDA ZABRON [19]

Wote wakazi wa Kijiji cha Ngole.


Watuhumiwa hao wamerudishwa Gerezani hadi tarehe 05/09/2018 pale kesi hiyo itakapotajwa tena kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi hapa Jijini Mbeya.
Watuhumiwa hao mnamo tarehe 14/08/2018 kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Ngole, Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa makusudi na bila halali waliharibu mabomba na vyanzo vya maji kwa kutumia silaha za jadi na kusababisha hasara ya takribani Shilingi za Kitanzania Milioni 14 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni michango ya baadhi ya wanakijiji na wafadhili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICK O. MATEI anatoa msisitizo kwa watanzania na wana Mbeya wote kuhakikisha wanalinda rasilimali zetu ikiwemo miundombinu ya afya, elimu, barabara, maji na nishati ili kufikia malengo tarajiwa ya uchumi wa viwanda. Pia Kamanda MATEI anatoa rai kwa yeyote atakayeharibu miundombinu hiyo, tutamkamata na kumfungulia shitaka la kuhujumu uchumi [Sabotage] na kuhakikisha wanafikishwa Mahakamani.


Imesainiwa na:

[ULRICH O. MATEI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SHUKURANI KWA VIONGOZI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWA KUMFARIJI WAKATI WA MSIBA WA DADA YAKE

SHILOLE, DOGO ASLAY WASAINI MKATABA WA TTCL NA NYUMBANI KUMENOGA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akisaini mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mkataba huo ambaao pia Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaaini na kampuni hiyo ili waasanii hao kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania. 
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana mkataba na msanii Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ (kushoto), mkataba huo ambaao pia Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley amesaaini na kampuni hiyo ili waasanii hao kushiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.
SHIRIKA  la Mawasiliano Tanzania, TTCL leo limetiliana saini na wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Zuena Mohamed maarufu kama Shilole ‘Shishi Baby’ na Asley Isihaka maarufu kama Dogo Asley  watakaoshiriki katika Kampeni kubwa ya Rudi Nyumbani Kumenoga itakayoshirikisha Mikoa yote ya Tanzania.
Akizungumza na Waandhishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino  Mhandisi Isaack Kamwelwe Agosti 31 mwaka huu Mkoani Katavi.
Amesema lengo la Kampeni hiyo ni kuwafikishia taarifa wananchi kuhusu TTCL mpya ambayo kwa sasa imefanya mabadiliko makubwa katika biashara ya Huduma za Mawasiliano hapa Nchini.
Asema Tamasha hilo ambalo halitakuwa na kiingilio litakuwa la aina yake ambapo wasanii wamejipanga kutoa burudani kabambe huku wananchi wakipata fursa ya kuelimishwa kuhusu Shirika la TTCL, Huduma zake na majukumu yake ya msingi pamoja na  kujipatia Sim Kadi na kujisajili bure na kuuziwa bidhaa mbalimbali za TTCL kwa bei nafuu.
“Hii ni kampeni ya Mkoa kwa mkoa, ambayo pia itatumika kutatua changamoto na kero mbalimbali walizonazo wateja wetu juu ya huduma na bidhaa zetu” alisema Kindamba
Kwa upande wake Zuena Mohamedi kw aniaba ya msanii mwenzake amesema amejipanga kutoa burudani kabambe itakayotoa hamasa kwa wananchi kupenda vya kwao na hivyo kurudi nyumbani kwa kutumia Mtandao wa TTCL.
“Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe wazalendo tutumie bidhaa za nyumbani, mfano mimi nina line ya TTCL ambayo intaneti yake ni ya kasi zaidi inaniwezesha kufanya kazi zangu kwa urahisi  ikiwa ni pamoja na kuendesha Akaunti zangu katika mitandao mbalimbali ya kijamii” alesema Shilole.
TTCL imedhamiria kuwa Shirika kinara katika utoaji wa huduma za Mawasiliano Nchini, nafasi iliyokuwa nayo hapo awali. Kupitia maboresho makubwa inayoyafanya, TTCL imeweza kutoa gawo la Tsh Bilioni 1.5 mwaka huu wa fedha na kuahidi kuongeza kiasi cha gawio katika miaka inayofuata sambamba na kuongeza uwekezaji katika teknolojia za kisasa, ubora wa huduma na ushiriki wa TTCL katika kutoa ajira kwa Watanzania na kusaidia shughuli za kijamii.

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA ATATUA MGOGORO MATUMIZI YA ARDHI

$
0
0
 Na Shani Amanzi,Chemba.
 
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Saimon Odunga amewataka Wananchi wa Kwamtoro waache tabia ya kuchukua maeneo kiholela badala yake wafate kanuni na taratibu za kuwa na ardhi kwani Serikali inapoteza muda mwingi na pesa katika kuwataftia wananchi maeneo mengine na kuwalipa fidia.

Mhe.Saimon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anafanya Mkutano wa Adhara ndani ya siku moja akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chemba,Wataalam wa Halmashauri ya Chemba pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kwamtoro kwa ajili ya kutatua mgogoro wa ardhi , tarehe 20/8/2018.

Mhe.Saimon Odunga amesema “Wananchi wamekuwa na tabia ya kuvamia maeneo na hata wakipewa maeneo mengine wanatabia ya kuyauza kitendo ambacho siyo kizuru na kusababisha serikali kupoteza muda kuendelea kufatilia nini kifanyike na wengine wanajua kabisa maeneo wanayoyachukua au kukaa ni ya matumizi ya umma kama shuleni,sokoni pamoja na stand ya mabusi”

Aidha amewataka wakazi wa Kwamtoro waliojenga nje ya utaratibu maeneo ya soko,standi na shule watoke haraka sana ndani ya siku 90 na Viongozi wa siasa pamoja na wa Serikali wasipende kutoka nje ya taratibu na kusababisha uchochezi bali fateni taratibu za ardhi kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli inafata kanuni,taratibu na sharia za nchi hasa kwenye ardhi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amesema Serikali haiwezi kuwaonea wananchi wake ni sawasawa na baba kumuonea mwanae ,badala yake wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu wanaowauzia maeneo sa nyingine kwani huwa wanawapotosha kwa kuwauzia maeneo ya umma kitendo ambacho kipo kinyume na taratibu .

Mashimba aliongeza kwa kusema “kwa wale wenye tabia ya kujiegesha maeneo ambayo siyo na kutegemea fidia tabia hiyo waiache mara moja kwani mambo ya kupeleka kesi mahakamani wakati wanajua wapo kinyume na taratibu wanasababisha Serikali kutumia gharama kubwa kuendesha kesi mahakamani na kupoteza muda” .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba

MKURABITA Yawezesha Wananchi Kupata Hati za Kimila Zaidi ya 300 Kilosa

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live


Latest Images