Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

DIRA YA DUNIA JUMATANO 22/08/2018


Wananchi kijiji cha Magubike wilayani Kilosa mkoa wa morogoro wakipatiwa Hati Miliki za Kimila

0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Mhe. Adam Mgoyi  amewataka wananchi kutumia fursa zinazotokana na urasimishaji ardhi uliowezesha kutolewa kwa hati zaidi ya 300 za kimila za kumiliki ardhi kwa wakazi wa Kata ya Magubike Wilayani humo jana.
Akizungumza na mamia ya wananchi  wa Kijiji hicho waliojitokeza katika hafla ya kutolewa kwa hati hizo amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano  ni kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi wake kupitia mpango wa matumizi bora ya adhi uliotekelezwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara  za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) na Halmashuri ya Wilaya hiyo.
“Tumieni hati hizi kutatua changamoto za kiuchumi kwani zinawawezesha kupata mitaji kutoka  katika taasisi za fedha zilizopo ambazo zimeonesha nia yakuwawezesha wananchi na nyingine zimeanza kutoa mikopo kwa wananchi wetu wenye hati za kimila” Alisisitiza Mgoyi.
Akifafanua amesema kuwa hati  hizo zitasaidia kuondoa migogoro ya ardhi, kuongeza thamani ya ardhi na kuwapa wananchi uwezo wa kujiendeleza kiuchumi ambapo tangu MKURABITA ianze zoezi la urasimishaji ardhi Wilayani humo wananchi wengi wamenufaika na mikopo iliyowawezesha kuwa na kilimo chenya tija.
Aliongeza kuwa Vijiji 37 vimenufaika na mpango wa matumizi bora ya ardhi katika Wilaya ya Kilosa ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“ Halmashuri ya Wilaya inao wajibu wa kutenga sehemu ya mapato yake ya ndani kuwawezesha wananchi katika upimaji wa ardhi na kuleta mpango bora wa matumizi ya Ardhi” Alisisitiza Mgoyi.
Pia kwa kuzingatia umuhimu wa kurasimisha ardhi Mgoya alibainisha kuwa mpango huo  unasaidia kubainisha maeneo ya ufugaji na yale ya kilimo katika Wilaya hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akisisitiza kuhusu wananchi kutumia hati  za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo ikiwemo kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha wakati wa hafla ya kuwakabidhi wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa hati hizo zilizotolewa baada ya maeneo yao kurasimishwa kwa kupimwa
 Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akisisitiza umuhimu wa hati za kimila za kumiliki ardhi katika kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi wakati wa hafla ya kutolewa kwa hati hizo kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani kilosa ambapo Mpango huo kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya hiyo wamefanikisha upimaji wa ardhi katika Vijiji 37.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akimkabidhi mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Magubike hati kimila ya kumiliki ardhi.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\2b.JPG

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Magubike wakipatiwa Hati Miliki za Kimila na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi. Pichani ni Bw. Jackson Mgoma, akiwa katika furaha baada ya kuipata Hati hiyo.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

ALI KIBA ASHEREHEKEA EID AL HAJJ NA MASHABIKI JIJINI TORONTO, CANADA

LUGOLA ATAKA POLISI CHATO KUTOKUNYANYASA WANANCHI, AHOJI UWEPO WA PIKPIKI NYINGI KITUONI HAPO

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitaka ufafanuzi kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, mkoani Geita, Alex Mukama (kulia),  kuhusu uwepo wa pikipiki kituoni hapo wakati alishatoa agizo pikipiki ambazo hazina kesi mahakamani ziondolewe vituo vya polisi nchini. Kushoto ni Mkuu wa Kituo  cha Polisi Chato, Haruni Kasubo. Waziri Lugola alifika kituoni hapo mara baada ya kutoka kuhani msiba wa dada wa Rais Dkt. John Magufuli, wilayani humo leo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimpa maelekezo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, mkoani Geita,  Alex Mukama (kushoto), kuhusu polisi wilayani humo wafanye kazi kwa weledi bila kunyanyasa wananchi. Waziri Lugola alifika Kituo cha Polisi Chato wilayani humo kusalimia pamoja na kupata taarifa ya utendaji kazi wa polisi, alipokua anatoka kuhani msiba wa dada wa Rais Dkt. John Magufuli, mjini Chato, leo. Kulia ni Mkuu wa Kituo hicho, Haruni Kasubo, na wapili kushoto, Diwani wa Kata ya Muungano, wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akionyeshwa eneo la Kituo cha Polisi Chato na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, mkoani Geita, Alex Mukama (kushoto).  Waziri Lugola alifika Kituo cha Polisi Chato wilayani humo kusalimia pamoja na kupata taarifa ya utendaji kazi wa polisi, alipokua anatoka kuhani msiba wa dada wa Rais Dkt. John Magufuli, mjini Chato, leo. Katikati ni Mkuu wa Kituo hicho, Haruni Kasubo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BABATI NYOTA SEARCH YASHIKA KASI, KATI YA WASHIRIKI 40 WAMEBAKI 11

0
0
John Walter, Babati
Mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba Mjini Babati mkoani Manyara, maarfu kama Babati Nyota Search,  yanazidi kushika kasi na kuwaibua vijana wengi wenye uwezo mkubwa katika muziki wa kizazi kipya.
Kutoka washiriki  40 mpaka sasa wamebaki washiriki 11 huku mshiriki wa jinsia ya kike akiwa ni mmoja pekee Apple D. Kila wiki anatoka mshiriki mmoja hadi wafike watatu ambao watachuana ili kupatikana mmoja atakaenyakua kitita cha shilingi laki tano pamoja kurekodiwa wimbo mmoja na video.
Akizungumza Chief Jaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Smile Fm Radio ya  Babati  Juma Msuya  amesema mashindano hayo ni fursa tosha kwa washiriki  kutambua  uwezo walionao  katika tasnia ya muziki.
Amesema mpaka sasa amegundua viapaji zaidi ya 20 vya muziki hivyo ni wakati wa wakazi wa Babati kujitokeza na kuwasaidia vijana hao ili kuinua vipaji walivyonavyo.
Msanii Wiliam Stebin Loya [Mono Music] alieimba wimbo wa Jux Looking For you aliomshiriksha Joe Makini ulikuwa kivutio kikubwa kwa mamia ya mashabiki waliokuwa wakishangilia alipokuwa akiimba kwa ufundi wa hali ya juu.
Mashindano hayo yanafanyika kila Jumapili saa tatu usiku na kurushwa live kupitia Babati Cable Tv na Smile Fm Radio.

INTRODUCING "MASHALLAH" BY AKIL THE BRAIN

AZAM TV HIGHLIGHTS: SIMBA SC 1-0 TANZANIA PRISONS (TPL 22/08/2018)

AZAM TV HIGHLIGHTS: COASTAL UNION 1-1 LIPULI FC (TPL 22/08/2018)


SWALA EID EL HAJI NA BARAZA LA EID KITAIFA VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM 2018

MICHUZI TV: HARMONIZE AFANYA KWELI BAADA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA, SHILOLE NDANI YA MJENGO MPYA.

WASANII TUNAWAJIBU KUSIFIA UTENDAJI KAZI WA SERIKALI YA RAIS MAGUFULI - PETER MSECHU

DC NYASA AWAKUMBUSHA WALIOPEWA BAHASHA MAALUM KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI KUENDELEA KUCHANGIA

0
0
*Pia agusia tamasha litakalofanyika Septemba 8 Ubungo Plaza Dar 

Na Ripota Wetu,Nyasa

SEPTEMBA   8 mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kutafanyika tamasha kubwa la harambee ya kuchangia elimu kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi hasa  wakike kwa ajili ya Wilaya ya Nyasa.

Tamasha hilo ambalo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo lengo likiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi huo wa mabweni.Akizungumza leo wilayani nyasa Mkuu wa wilaya hiyo Esabela Chilumba amesema anawakumbusha wadau wote wa elimu kuendelea kuchangia.

Amesema siku zinazidi kusogea hivyo wote waliopewa bahasha maalum za kuchangia anawakumbusha kuendelea kuchangia kwa njia mbalimbali ambazo zimewekwa wazi kwa ajili ya kukusanya fedha hizo." Binafsi niwaombe wadau mbalimbali waendelee kutoa michango yao lengo nikufanikisha harambee hiii ambayo lengo hasa nikukusanya Sh. bilioni moja ambazo zitatumika kujenga mabweni hayo,"amesema Esabela

Ameongeza  kupitia kamati na akaunti mbalimbali zilizowekwa wazi wadau waendelee kuchangia kwani watoto wakike wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mimba za utoto." Ndugu mwandishi kama nilivyosema awali kutokana na watoto wengi kuishi mazingira ya mbali na shule inapelekea waliowengi kukatisha masomo kwasababu ya kupata mimba za utoto,"amesema

Amesema mbali na mimba wengine wanashindwa kumaliza shule kwa sababu ya utoro unaotokana na kuishi mbali naazingira ya shule hivyo nivema wakajitokeza kwa wingi kuchangia.Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa wilaya ambayo ipo pembezoni mwa Ziwa Nyasa ambapo shughuli zake kubwa ni uvuvi na kilimo hivyo  kujengwa kwa mabweni kutasaidia wanafunzi wa  kike kukaa shule na mwisho wa siku kufanya vizuri katika masomo yao.

Pia Chilumba amewataka wananchi wa wilaya hiyo ya Nyasa kuendelea kushikamana na kudumisha usalama ukizingatia ni wilaya ambauyo ipo mpakani  na pia waendelea kuchapa kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao huku wakiunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.

MAFANIKIO MAKUBWA YAMEPATIKANA KUPITIA JPC, BALOZI MWINYI

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda kwa ngazi ya Makatibu Wakuu. Katika hotuba hiyo, Balozi Mwinyi alieleza kuwa tokea JPC kati ya Tanzania na Uganda ilipoanzishwa mafanikio makubwa yamepatikana. Mafanikio hayo ni pamoja na kusainiwa kwa mikataba ya makubaliano mbalimbali ikiwemo mkataba wa kushirikiana katika ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kikagati/Murongo na makataba wa kushirikiana katika usafiri wa anga ambapo Tanzania inakusudia kuanza safari za moja kwa moja kutoka Dar Es Salaam kwenda Kampala hivi karibuni. 
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini hotuba ya Balozi Mwinyi 
Ujumbe wa Uganda ukifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zinasomwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Uganda. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akiongea na mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Balozi Patrick Mugoya kabla ya viongozi hao hawajafungua rasmi mkutano wa JPC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda nchini Uingereza, Mhe. Leonard Mugerwa nje ya ukumbi wa mikutano. 

MBUNGE NA MUAKILISHI JIMBO LA CHUMBUNI WALA CHAKULA CHA MCHANA PAMOJA NA WATOTO YATIMA ZANZIBAR

0
0

Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Foundeshen akiwa pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akishiriki pamoja na Wananchi wa Jimbo hilo kusoma dua ya kuwaombea wazee waliotangulia mbele ya haki katika Chakula cha mchana kilichotayarishwa na Taasisi hiyo kwa Watoto yatima na wenyemazingira magumu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Foundeshen akiwa pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akijumuika na Watoto Mayatima na wenye mazingira magumu katika Chakula cha mchana kilichotayarishwa na Taasisi hiyo kwa Watoto yatima na wenyemazingira magumu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa Zanzibar.
Muakulishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Mussa akijumuika na Watoto Mayatima na wenye mazingira magumu katika Chakula cha mchana kilichotayarishwa na Taasisi Pondeza Foundeshen katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

SPIKA AHUDHURIA SEMINA YA UZAZI NA MALEZI BORA JIJINI DODOMA

0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akimsikiliza kwa makini mwezeshaji katika semina ya uzazi na malezi bora iliyoandaliwa na Chama cha UMATI kwaajili ya wabunge iliyofanyika  jana jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifungua semina ya uzazi na malezi bora iliyoandaliwa na Chama cha UMATI kwaajili ya wabunge iliyofanyika jana jijini Dodoma.
Wabunge wakimsikiliza kwa makini Spika katika semina ya uzazi na malezi bora iliyoandaliwa na Chama cha UMATI kwaajili ya wabunge iliyofanyika jana  jijini Dodoma.
Waheshimiwa wabunge wakipata picha ya pamoja na Spika Mhe Job Ndugai ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika semina iliyoandaliwa na UMATI 

VICHAKA VYA ITIGI ‘ITIGI THICKETS’ HATARINI KUTOWEKA

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba hii leo amehitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Singida na kuwasili katika Mkoa wa Tabora, ikiwa ni mwendelezo wa kukagua, kutathmini, kuzungumza na viongozi, na wananchi kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, sambamba na uanzishwaji na ufuatiliaji utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira ya mwaka 2004 katika ngazi za Serikali za Mitaa. 

Katika siku ya tatu ya ziara yake Mhe. Makamba ametembelea vichaka vya Itigi ‘Itigi thicket” na kupata fursa ya kuzungumza na viongozi wa wilaya ya Manyoni juu ya namna bora ya kuhifadhi eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 410,000 na kuahidi kutuma wataalamu kuandaa andiko la Mradi utakaonufaisha wakazi wa eneo hilo katika sekta uvunaji wa asali kwa njia ya kisasa zaidi.

“Ndani ya muda mfupi nitatuma wataalamu wangu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, waje wakae na wataalamu wenu na kuandaa Mradi utaonufaisha wakazi wa wanaozunguka eneo lote la msitu ili kutunza na kuhifadhi rasilimali za asili zilizopo katika eneo hili” Makamba alisisitiza.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Bi. Rahabu Jackson kuwasilisha kwake majina wa watalaamu wa Mazingira ambao wana sifa za kuwa Wakaguzi wa Mazingira ili waweze kuteuliwa kwa mujibu wa Sheria.
Mwananchi ambae jina lake halikupatikana mara moja amejikita katika suala la hifadhi ya vichaka vya Itigi, ambavyo humsaidia kuongeza kipato kwa kuvuna asali. 
Sehemu ya vichaka adimu duniani vinavyopatikana Itigi, “Itigi thickets” katika bara la Afrika vichaka kama hivyo vinapatikana Tanzania na Zambia pekee, viko hatarini kutoweka kutoweka kutokana na shughuli za kibinadamu. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimiana na Bw. Khatib Ally mmoja wa wananchi waliojitokeza kumpokea katika Kijiji cha Aghondi Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo ambalo lina vichaka vya aina yake na vyakipekee barani Afrika. Wananchi wa eneo hilo wamewasilisha ombi kwa Waziri Makamba la kuweka ulinzi wa kutosha na namna bora ya kuhifadhi eneo hilo. 

 

IBADA YA SHUKRANI YA MAMA YETU MPENDWA BI.JOYCE CLARA KIBAJA

0
0
Familia ya Marehemu Bw & Bibi Julius Vicent Kibaja wa Makongo Juu Dar es Salaam tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Ndugu, Jamaa na marafiki, Wauguzi na Madaktari kwa ushirikiano wenu mkubwa mlioutoa kwetu tangu kutokea kwa kifo cha MAMA YETU MPENDWA Bi. JOYCE CLARA KIBAJA tarehe 5-07-2018 katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) na mpaka tulipompumzisha kwenye nyumba yake ya milele katika Kijiji cha Kwemhosi- Kigunga-Muheza –Tanga .

Ibada ya shukrani itafanyika tarehe 25-08-2018 katika Kanisa la Mt. Jacob lililopo Kijiji cha Kwemhosi - Muheza ikitanguliwa na mkesha tar 24-08-2018.

Aidha, siku ya Ijumaa tarehe 31-08-2018 kutakuwa pia na ibada ya shukrani itakayofanyika katika kanisa la Anglikan la Mt. .Nikolaus - Ilala Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni, Wote mnakaribishwa. 

“Bwana alinitokea zamani akisema, Naam nimekupenda kwa Upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu” YEREMIA 31:3 

“ JOYCE CLARA KIBAJA YOU ARE THE BEST DEVOTED MUM FOREVER IN OUR HEART” 

R.I.P 

Breaking News: Wakili wa Chadema ajiondoa ghafla

0
0
Wakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi Tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe amejitoa leo Agosti 23, 2018 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamuru washtakiwa wasomewe Maelezo ya awali, (PH).

Mtobesya amejitoa leo mahakamani  hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Willbard Mashauri baada ya kuamuru PH dhidi ya washtakiwa isomwe kufuatia maamuzi aliyotoa mapema leo dhidi ya maombi ya utetezi ya kutaka kesi hiyo Namba 112/2018  iahirishwe kusubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufani kuhusu kusimamishwa kwa kesi hiyo.


Hata  hivyo Hakimu Mashauri ameyatupilia mbali maombi hayo kwa sababu kifungu Namba 225 (1)(2) hakiipi mamlaka mahakama ya Kisutu kuahirisha kesi hiyo.


" Mheshimiwa Hakimu Mimi najitoa katika kesi hii kwani nahisi haki haitatendeka". Amesema Mtobesya na kusimama na kutoka nje.

Hii takribani mara ya tatu kwa maombi ya Chadema kutupiliwa mbali.

viongozi Tisa wa Chadema wakiwa mahakamani.

Halotel yaja na Ninogeshe na Halopesa

0
0
Wateja wa Halotel sasa kutuma pesa bure.

Kampuni ya mawasiliano ya Halotelimezindua kampeni kabambe ya “Ninogeshe na Halopesa” maalum kwa wateja wanaotumia huduma za Halopesa.

Kuanzia sasa, wateja wa Halopesa wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa muda wowote.Kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni muendelezo wa azma ya kuboresha huduma za fedha kwa njia ya mtandao kwa wananchi wenye vipato tofauti.

Licha ya kuondoa gharama za miamala kwa wateja wanaotuma fedha kutoka Halotel kwenda Halotel, wateja wetu watapata nafuu wanapotuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine.Kampeni hii ni maalum kwa wateja wote wa Halotel waliopo mjini na vijijini wanaotumia huduma zetu kwa miaka miwili sasa tangu tulipoingia sokoni ambao watanufaika zaidi kwa kuokoa fedha ambazo wangekatwa wanapotuma pesa. Fedha hizo sasa wataweza kuzitumia kukidhi mahitaji yao mengine.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Nguyen Van Son amesema kampeni hii ni hatua nyingine ya kuhakikisha wateja wanakuwa na wigo mkubwa kufurahia na kunufaika zaidi na huduma za Halopesa bila kuwa na wasiwasi wa makato kila wanapotuma pesa mahali popote na wakati wowote.

“Hii ni fursa nyingine kwetu kuongeza tabasamu na furaha kwa wateja wetu walioenea nchi nzima kwa kuwapa huduma za fedha iliyo madhubuti inayoendana na hali ya uchumi kuondokana na usumbufu ambao wangeupata kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha. Sasa wataokoa makato ya kufanya miamala,” alisema Son.Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba licha ya kuondoa gharama katika kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda Halopesa, wateja watapata muda wa maongezi bure kila wanapoweka pesa kwa wakala.

“Habari njema tuliyonayo kwa wateja wetu ni kuendelea kuwanufaisha kila wanapotumia huduma ya Halopesa ambapo kwa sasa kila mteja atakaye weka pesa kwa wakala kuanzia shilingi elfu moja (1,000/=) atapata muda wa maongezi wa bure. Si hivyo tu wateja wetu wataendelea kunufaika kwa namna mbalimbali kila wanapotumia huduma za Halopesa,” alihitimisha Son.

Sambamba na uzinduzi wa kampeni ya Ninogeshe na Halopesa, kampuni ya Halotel imeingia makubaliano na msanii chipukizi wa kike wa nyimbo za kizazi kipya (bongo fleva), Faustina Mfinanaga maarufu kama “Nandi” kuwa balozi wake ambaye atahusika katika kampeni za Halopesa.

Hii ni hatua nyingine kwa msanii huyu kufanyakazi na Halotel na kuwakilisha huduma bora za mawasiliano inayotoa kwa mamilioni ya Watanzania nchi nzima.Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba na msanii huyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni imemchagua Nandi kwa sababu ana uwezo wa kuwa na mchango chanya utakaosaidia kukuza mauzo ya bidhaa na huduma, pamoja na kuimarisha jina la kampuni.

“Nandi ni msanii anayekonga nyoyo za mashabiki wake kupitia wimbo wake unaovuma kwa jina la ‘Ninogeshe’ na kumpa umaarufu unamfanya afahamike kwa watu wa rika zote. Unampa umaarufu ambao utasaidia kuiwakilisha vema kampuni ya Halotel,” alisema Semwenda.

Kwa upande wake, msanii wa bongofleva, Faustina Mfinanga (Nandi) amesema hiyo ni fursa kubwa na ya kipekee kwake kuwa miongoni mwa familia ya kampuni hiyo na kupewa jukumu la kuiwakilisha ipasavyo kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla kutokana na huduma bora za mawasiliano inazotoa.

Huduma ya Halopesa inatolewa na zaidi ya mawakala 55,000 wanawahudumia zaidi ya wateja milioni 1.5 walioenea nchi nzima.

Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Ya Halotel Nguyen Van Son, akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi wa Kampeni mpya iitwayo “NINOGESHE NA HALOPESA” itakayo wawezesha wateja wa mtandao wa Halotel Kutuma pesa bure kupitia Huduma ya Halopesa huku wakipata muda wa maongezi wa bure kila wanapoweka pesa kupitia kwa mawakala walioenea nchi nzima . Kulia ni Meneja Masoko wa Startimes David Malisa.

Msanii chipukizi wa kike wa nyimbo za kizazi kipya (bongo fleva), Faustina Mfinanaga maarufu kama “Nandi” akizungumza na waandishi wa Habari uzinduzi wa Kampeni mpya iitwayo “NINOGESHE NA HALOPESA” itakayo wawezesha wateja wa mtandao wa Halotel Kutuma pesa bure kupitia Huduma ya Halopesa huku wakipata muda wa maongezi wa bure kila wanapoweka pesa kupitia kwa mawakala walioenea nchi nzima. Nandi ndio Balozi wa Kampeni Hii ya Halopesa.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Ya Halotel Nguyen Van Son, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda, kaimu naibu Mkurugenzi kitengo cha Halopesa Hanh Nguyen na Msanii wa Kizazi Kipya Nandi wakigonga glasi za shampeni kuashiria uzinduzi wa Kampeni mpya iitwayo “NINOGESHE NA HALOPESA”.

POLISI KILIMANJARO YANASA GARI LA KIFAHARI LILILOIBIWA NCHINI KENYA

0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kukamata gari  aina ya V8 Nissan Patrol linalodaiwa kuwa la wizi na kuwekwa namba bandia za usajili T 194 DEO .

Kamanda Issah alisema Gari hilo linadaiwa kupotea Nairobi nchini Kenya huku likitajwa kuwa ni mali ya mfanyabiashara mkubwa wa nchini humo  kabla ya kukamatwa katika kizuizi cha asakri kilichopo jirani na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA ) eneo la kwa Wasomali.

"Tumekamata gari ambalo limeibiwa huko Kenya na tunawashikiliwa watu wawili ambao wanadaiwa kuhusika na wizi wa gari hilo ,tunategemea kulikabidhi kwa wahusika ,na hao watuhumiwa watapelekw Kenya kujibu mashtaka yao"alisema Issah.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Hamis Issa aikionesha kwa waandishi wa Habari Gari aina ya Nissan Patrol v8 linalodaiwa kuibiwa Nairobi nchini Kenya kabla ya kukamatwa likiwa njiani kuelekea jijini Arusha.
Muonekano wa Ndani wa gari hilo la kifahari ambalo hata hivyo lilikutwa kifaa cha kufuatilia mwenendo wa gari (Car Track) kikiwa kimeharibiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akizungka kutizma hilo gari nje ya kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi .

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images