Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUGOLA AKUTANA NA BAADHI YA WANANCHI NA KUSIKILIZA KERO ZAO

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam, jana kuwasilisha malalamiko mbalimbali ili wapate ufumbuzi wa kero zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam, jana kuwasilisha malalamiko mbalimbali ili wapate ufumbuzi wa kero zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza mmoja wa wananchi, Sheikh Issa, aliyefika ofisini kwa waziri, jijini Dar es Salaam, kuelezea malalamiko yake juu ya ndugu yake kuuawa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza mmoja wa wananchi, Martha Mtungi (wakwanza kulia), aliyefika ofisini kwa waziri, jijini Dar es Salaam, kuelezea malalamiko yake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 

Kamati ya Bajeti Yaipongeza NBS kwa Ufanisi wa Kazi Zake

MKUU WA WILAYA YA HAI,OLE SABAYA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa Askari wa Jeshi la Akiba ,mafunzo yanayofanyika Masama ,Machame wilayani Hai.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wameketi tayari kumsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa askari wa jeshi la akiba.
Baadhi ya Wakufunzi na viongozi katika usimamizi wa mafunzo hayo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya aksalimiana na washiriki wa mafunzo hayo mara baada ya kufungua rasmi.
Washiriki wa Mafunzo wakianza rasmi mazoezi kwa vitendo ya kuwaandaa kuwa wakakamavu.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


UONGOZI WA MAHAKAMA DODOMA WAFANYA JITIHADA KUPATA MAHAKAMA ZA WILAYA KATIKA WILAYA ZISIZO NA MAHAKAMA

$
0
0



Na Stanslaus Makendi, Mahakama Kuu Dodoma.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imeanza mpango wa uanzishaji wa huduma za Kimahakama katika Wilaya zisizo na huduma hizo kwa sasa.Viongozi wa Mahakama katika Kanda hii wameanza kufuatilia na kukutana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na Chamwino ili kupata maeneo ambayo yatatumika na Mahakama za Wilaya katika kipindi ambacho mpango wa kujenga Mahakama za Wilaya katika maeneo hayo unafanyiwa kazi.

Utekelezaji huu unafuatia agizo la Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania juu ya kufanya jitihada ya kuwa na Mahakama hizo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.Katika mazungumzo waliyofanya katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ilibainika kuwa huduma ya Kimahakama inahitajika sana kwa sasa katika eneo hilo kutokana na umbali mrefu uliopo kufikia eneo ambalo huduma za Mahakama ya Wilaya inapatikana kwa sasa (Kondoa).

Baada ya mazungumzo hayo viongozi wote wa pande mbili walitembelea na kuona eneo ambalo Ofisi ya Mkurugenzi imetenga kwa ajili ya matumizi ya Mahakama na Taasisi nyingine muhimu ambazo hazipo kwa sasa katika Wilaya hiyo.

Sambamba na hilo, viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino nao walionesha uhitaji mkubwa wa uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya katika eneo hilo na wameahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha huduma hiyo inaanzishwa mapema katika Wilaya hiyo. 
 Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Bi. Maria Francis Itala ( wa pili kushoto) akiwa katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Zahara Muhidin Michuzi kufuatilia upatikanaji wa majengo kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya ya Chemba.
2 (33)
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na Hakimu Mkazi Mfawidhi (M) wakitoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kwenda kuona eneo lililopendekezwa kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya pamoja na kuoneshwa kiwanja cha Mahakama katika Wilaya hiyo.
4 (18)
Muonekano wa nje wa jengo lililopendekezwa kwa ajili ya Mahakama ya Wilaya ya Chemba.
6 (7)
Muonekano wa jengo linalotumika kwa sasa na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa ambayo inatoa huduma za kimahakama kwa Wilaya ya Kondoa na Chemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

WATUHUMIWA 11 WAPANDISHWA KIZIMBANI KISUTU KWA KESI TATU IKIWEMO YA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Watu 11 wakiwamo raia wawili wa Guinea wamepandishwa katika Kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na vipande 660 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.5.

Mapema leo asubuhi washtakiwa hao waliachiwa na kufunguliwa mashtaka mapya baada ya masaa matatu yale yale.

Awali walikuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo hayo ya uhujumu uchumi ambapo waliachiwa huru na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde lakini baada ya kuachiwa walikamatwa na ndani ya Masaa matatu walipandishwa tena kizimbani na kusomewa mashtaka mapya.

Wakiwasomewa mashtaka mapya mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizire, Wakili wa Serikali, Salim Msemo amewataja washtakiwa hao kuwa ni Ally Shariff na Fatoumata Saumaolo raia wa Guinea, Victor Mawalla, Calist Mawalla, Solomoni Kuhembe, Haruna Abdallah’ Kasa’, Abas Hassan ‘Jabu’,Ismail Kasa, Khalfan Kahengela, Musa Ligagabile na Kassim Said@ Bedui

Imedaiwa kuwa washtakiwa kwa pamoja kati ya Aprili 6 na Juni 23, 2016 jijini Dar es Salaam, waliratibu na kusafirisha vipande 660 vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 2,105, 181 ambazo sawa na biklioni 4.5 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na sheria ya wanyama pori.

Imedaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao walijihusisha na nyara za Serikali kinyume na sheria ya wanyamapori ambapo wanadaiwa walisafirisha vipande hivyo.Pia washtakiwa watano kati ya hao, Ally, Victor, Calist,Haruna na Abbaswanadaiwa kuwa walikutwa na vipande vya meno ya tembo kinyume na sheria za wanyamapori.

Hata hivyo, Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea.

Hata hivyo washtakiwa hao walilalamika mahakamani hapo kuwa hiyo siyo kesi mpya ilifutwa Masaa matatu kabla hawajafunguliwa kesi hiyo mpya hivyo waliomba kutendewa haki kwa sababu wanaumia gerezani na upande wa mashtaka unaumiza familia zao.Hivyo waliomba hiyo kesi iende mahakama Kuu kwa sababu hapo hawawezi kupata haki.

Wapo ndani tangu mwaka 2016 wakitaka kuomba dhamana mahakama Kuu Upande wa Mashtaka unawaeleza kesi imeiva, wahisi wanataka kuwauwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 3,2018.
  Watuhumiwa 11 wa kesi ya Uhujumu Uchumi

MBUNGE JIMBO LA CHUMBUNI AZUNGUMZIA TAMASHA LA YATIMA LITAKALOFANYIKA OKTOBA, 2018

$
0
0


Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Fondeshen ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la Mayatima ambalo hufanyika kila ifikapo Mwezi kumi(10)Mfunguo Tatu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villas mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Fondeshen ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Tamasha la Mayatima ambalo hufanyika kila ifikapo Mwezi kumi(10)Mfunguo Tatu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villas mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Fondeshen ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza kuhusiana na Tamasha la Mayatima ambalo hufanyika kila ifikapo Mwezi kumi(10)Mfunguo Tatu katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villas mjini Zanziba

Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Muhimbili yafikia 19

$
0
0
Dar es salaam 21-08-2018 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma ya kupandikiza figo ambapo hadi hivi sasa tayari wagonjwa 19 wamenufaika na huduma hiyo tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini Novemba mwaka 2017.

Utoaji wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambayo ili elekeza kuweka mipango thabiti ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo yalikuwa hayatolewi hapa nchini ama kutokana na wataalam wa kutoa huduma hizo au vifaa vya uchunguzi.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Prof. Lawrence Museru kuhusu upandikizaji figo.

“Tunapenda kuwafahamisha kuwa wagonjwa wote tuliowapandikiza figo pamoja na ndugu zao waliojitolea figo wanaendelea vizuri na shughuli zao kama kawaida. Hii inaonesha ni kwa kiwango gani huduma hii imefanikiwa tangu ilipoanzishwa Novemba mwaka jana ”. amesema Dkt Swai.

Akifafanua amesem zoezi hilo la upandikizaji figo limeshirikisha wataalamu wazalendo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya BLK, Taasisi ya Saifee iliyopo Mumbai India pamoja na Hospitali ya kimataifa ya Sakra ya nchini India.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai( katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo, kuhusu maendeleo ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushoto ni Daktari bingwa upasuaji wa mfumo wa mkojo Njiku Kim , kulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya figo Onesmo Kisanga. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Njiku Kim akiandaa figo kabla ya kupandikizwa kwa mgonjwa. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo wa Muhimbili, Victor Sensa akishirikiana na Dkt. Kim kuaandaa figo kwa ajili ya kupandikizwa kwa mgonjwa mwingine. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt . Isaack Mlatie akitoa figo kwa ajili ya kupandikiza kwa mgonjwa mwenye tatizo la figo. Katikati ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, Muhimbili, Dkt. Gabriel Mtaturu akishiriki katika upasuaji huo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Sakra nchini India, Dkt. Girish Nelivigi akishirikiana na madaktari wa Muhimbili kufanya upasuaji huo.
Wataalamu wakiendelea na upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). 
Wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo kutoka nchini India.

Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda wafunguliwa jijini Kampala

$
0
0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Balozi Patrick Mugoya akisoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Uganda unaofanyika jijini Kampala kuanzia tarehe 21 hadi 23 Agosti 2018. Balozi Mugoya katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Uganda kuboresha miundombinu na kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kupunguza gharama za kufanya biashara kati ya Tanzania na Uganda

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi ambaye pia ni kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya maafisa waandamizi akisoma hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa JPC. Bw. Mbilinyi alisema kuwa Mkutano huo pamoja na mambo mengine utathimni utekelezaji wa masuala yaliyokubalika wakati wa mkutano wa kwanza wa JPC uliofanyika Arusha mwezi Aprili 2017 na kuweka mikakati ya utekelezaji kwa masuala ambayo hayajakamilika.
Balozi Mugoya na Bw. Mbilinyi wakiwa katika meza kuu kabla hawajasoma hotuba za ufunguzi.

Kutoka kushoto ni Bw. Mbilinyi, Bw. Innocent Luoga, Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Bi. Tuma Abdallah Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) wakiwa katika meza kuu.

Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia hotuba za ufunguzi wa Mkutano wa JPC. Kutoka kushoto ni Bi. Mwadawa Ali kutoka kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Bw. Paul Makelele kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Karim Msemo wa Wizara ya Mifugo.



WAJUMBE KAMATI ZA BUNGE WAJENGEWA UELEWA KUHUSU DHANA YA MISWADA ITAKAYOJADILIWA BUNGENI KATIKA MKUTANO WA BUNGE LA KUMI NA MBILI.

$
0
0

Katibu kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Ndg. Chacha Nyakega akizungumza na Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba (Kushoto) akimsikiliza Katibu kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Ndg. Chacha Nyakega (kulia) ambae ni mtoa maada akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo (hawapo kwenye picha) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi wa kamati za Bunge Ndg. Athuman Hussein (wa pili kulia) wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambae pia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian kapufi (katikati)akisisitiza jambo wakati wa semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe na Mbunge wa Mgogoni Mhe. Dkt. Ally Suleiman na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Silafu Maufi
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Ndogo, Mhe. Taska Mbogo (Kushoto)akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo ambao pia Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa majadiliano katika semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Ndogo ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika majadiliano baada ya semina ya kuwajengea uelewa Wabunge kuhusu dhana ya miswada itakayojadiliwa Bungeni katika Mkutano wa Bunge la Kumi na mbili (12) unaotegemewa kuanza tarehe 4 Septemba, 2018 Jijini Dodoma

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA CHATO MAZISHI YA DADA YAKE MAREHEMU MONICA MAGUFULI YALIYOFANYIKA LEO

$
0
0
Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aitwaye Monica Joseph Magufuli aliyefariki dunia Jumapili tarehe 19 Agosti, 1955 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza amezikwa leo katika makaburi ya familia yaliyopo katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita. 

Misa Takatifu ya Mazishi ya Monica Joseph Magufuli ameongozwa na Askofu Jimbo Katoliki la Rulenge Mhashamu Severine Niwemugizi aliyeambatana na Maaskofu wengine saba, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. 

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mhe. Raila Amolo Odinga, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mawaziri, Wabunge, Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wengine mbalimbali wa Mikoa, Wilaya, Taasisi, Idara na Kampuni. 

Akisoma Wasifu wa Marehemu kwa niaba ya Familia, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Bw. Gerson Msigwa amesema marehemu Monica Joseph Magufuli alizaliwa tarehe 25 Novemba, 2018 na ni mtoto wa kwanza wa Mzee Joseph Marco Magufuli (ambaye ametangulia mbele za haki) na Mama Suzana Ngolo Magufuli ambaye yupo hai. 

Msigwa amesema Monica ameacha Mme, watoto 9 na Wajukuu 25. 



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza lenye mwili wa  Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
3 (1)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia  Mama yake mzazi Suzana Magufuli wakati wakuweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo ndani ya kaburi la Marehemu Dada yake Monica Magufuli nyumbani kwao katika kijiji cha Mlimani Chato mkoani Geita.
6 (2)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kanisani katika Misa takatifu ya kumuombea Marehemu Dada yake Monica Magufuli. Wengine katika picha ni Mama yake Suzana Magufuli, Stanslaus Lori Madulu(Mme wa marehemu) , Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

WAKAZI WA KILAMBO MKOANI MTWARA WAOMBA KIWANDA CHA KUSINDIKA MAZAO YA KILIMO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Mtwara

WAKAZI wa Kijiji cha Kilambo, Wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara, wameiomba Serikali iwasaidie kuwatafutia mwekezaji atakayejenga kiwanda cha kusindika matunda na mazao ya kilimo katika kijiji chao kutokana na kijiji hicho kuwa na matunda na mazao mbalimbali yanayokosa soko na kuwasababishia umasikini.

Wakazi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo Bw. Mohamed Mkama, wametoa ombi hilo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, aliyefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Forodha cha Kilambo, kilichoko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara, kwamba kijiji chao kina fursa nyingi za kilimo zinazohitaji viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yao na kutoa ajira kwa vijana.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo Bw. Mohamed Mkama, alisema kuwa Kijiji chao kinapakana na nchi ya Msumbiji ambako kuna mwingiliano mkubwa wa watu katika masuala ya biashara na uhusiano wa kijamii ikiwemo pande
mbili za nchi kuoleana hivyo kuwafanya wananchi wa Msumbiji waishio mpakani kutegemea bidhaa kwa wingi kutoka katika kijiji chao.

"Watu kutoka Msumbiji wananunua sana chakula na bidhaa nyingine kutoka kwetu lakini tunawauzia bidhaa bila kuongeza thamani hivyo uwepo wa kiwanda utakuza uchumi wa kijiji chetu na tunakuomba Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, utusaidie kupata kiwanda ili nasi tuweze kunufaika" alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Kijiji

Mkazi mwingine wa Kijiji hicho Bw. Selemani Kumamba, alimweleza Waziri wa Fedha na Mipango kwamba Kijiji chao ni maarufu kwa kilimo cha matunda hivyo wanapendekeza kujengwa kwa kiwanda cha kusindika matunda ili juisi itakayozalishwa katika kijiji chao iwe na soko.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), akitoka kukagua Kituo cha Forodha na Ushuru cha Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji (Kilambo), alipofanya ziara na kuzungumza na wafanyakazi wa Kituo hicho, mkoani Mtwara.
 Meneja wa Kituo cha Forodha na Ushuru cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara Bw. Emmanuel William (wa tatu kulia), akitoa maelezo ya eneo jipya la ujenzi wa Ofisi za Kituo hicho katika Kijiji cha Kilambo, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. 
 Diwani wa Kata ya Tangazo Bw.(kushoto), akijadili jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipokutana na wakazi wa Kijiji cha Kilambo, akiwa katika ziara yake ya kukagua Kituo cha Forodha na Ushuru-Kilambo, kilichoko mpakani kwa Tanzania na Msumbiji.
 Wazee wa Kijiji cha Kilambo wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa utendaji wake mzuri wa kazi, alipofanya ziara ya kutembelea Kituo cha Forodha katika Mpaka wa Tanzania na Msumbiji- Kilambo Mkoani Mtwara.
 Mzee Seleman Kumamba (kushoto) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), ambapo alimuomba Waziri huyo kuangalia uwezekano wa kuweka kiwanda katika eneo hilo  kikiwemo cha kusindika matunda kwa kuwa watanufaika kutokana na soko la mazao yao lililopo nchi jirani ya Msumbiji.

Tanzania yatia fora Tamasha la michezo Afrika Mashariki jijini Bujumbura

$
0
0
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania (waliovalia jezi nyeupe) ikichuana na timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Burundi katika uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi. Katika pambano hili timu ya Taifa ya Tanzania iliibuka na ushindi mnono wa magoli 8-1 dhidi ya timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Burundi. 

Kufuatia ushindi huu timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania inatarajia kukutana na Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Kenya katika mchezo utakaofanyika siku ya Alhamis terehe 23 Agosti 2018 kwenye uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi.

Aidha, timu ya mpira wa pete ya Taifa ya Tanzania pia iliibuka na ushindi mnono wa magoli 79-14 dhidi ya timu ya mpira wa pete ya Burundi. Kufuatia shindi huo timu ya Taifa ya mpira wa pete inatarajia kukutana na timu ya mpira wa pete ya Uganda hapo kesho tarehe 22 Agosti, 2018 katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha ENS jijini Bujumbura

Vilevile timu ya mchezo wa Karate ya Taifa nayo imeanza kushiriki mchezo huo katika hatua mbalimbali, ambapo hadi sasa mwenyeji wa tamasha hilo Burundi ndiye anayeongoza kushida kwenye vipengele vingi vya mchezo huo.

Tanzania katika Tamasha hili inashiriki katika michezo minne tofauti ambayo ni Riadha (mashindano bado hayajaanza), mpira wa miguu (kwa timu ya wanawake pekee), karate na mpira wa pete.Tamasha la kwanza la Michezo la Afrika Mashariki lilianza kufanyika tarehe 15 Agosti na litafikia tamati Agosti 30, 2018 nchini Burundi. 
Moja wa msambuliaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania akiwachambua mabeki wa timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Burundi. Katika mchezo huo Tanzania iliibuka na ushindi wa magoli 8 - 1 
Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania ikishangilia ushindi pamoja mashabiki waliojitokeza kushuhudia shindano hilo 
Mmoja wa washiriki wa mchezo wa karate akionesha umahiri wake katika mchezo huo kwenye Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea jijini Bujumbura, Burundi 

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Menejimenti na Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa msiba wa dada yake Bi. Monica Joseph  Magufuli uliotokea tarehe 19 Agosti, 2018 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa.
Jjina la Bwana lihimidiwe - AMINA.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 21/08/2018

GOOD NEWS....VIJANA WAZAWA 49 WAANZA KUPIKWA KUJIANDAA NA SGR NA MIRADI MINGINE YA TRC


HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

Huduma za Benki ya Azania Kivutio Kwa Wadau wa Mkutano Mkuu wa Nne wa ZSSF Viwanja Vya Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar

$
0
0
Senior Manager Retail Banking Azania Bank Mr. Jackson Lohay akizungumza na kutowa maelezo ya huduma zinazopatikana kupitia Benki ya Azania kwa Wananchi na Wateja wao wakati wa hafla ya Uzinduzi wa ZSSF Mobile App na kuadhimisha Miaka 20 pamoja na Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Jamii Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. Azania Benk ni wadau wa Mfuko wa Jamii Zanzibar ambapo hutuoa huduma mbalimbali kwa Wanachama wa ZSSF.
Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakifuatilia maelezo ya Mwakilishi wa Benki ya Azania wakati akitowa maelezo na fursa zinazopatikana kupitia Benki hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau wa Mfuko huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 
Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakifuatilia mkutano huo wa Nne wa Wadau wa ZSSF uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakifuatilia Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadfau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakati Mwakilishi wa Benki ya Azania akitowa maelezo na fursa zinazotolewa na benki hiyo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Hospitali ya Taifa Muhimbili yafikia 19

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma ya kupandikiza figo ambapo hadi hivi sasa tayari wagonjwa 19 wamenufaika na huduma hiyo tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini  Novemba mwaka 2017.
Utoaji wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambayo ili elekeza kuweka mipango thabiti ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo yalikuwa hayatolewi hapa nchini ama kutokana na wataalam wa kutoa huduma hizo au vifaa vya uchunguzi.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Prof. Lawrence Museru kuhusu  upandikizaji figo.
“Tunapenda kuwafahamisha kuwa wagonjwa wote tuliowapandikiza figo pamoja na ndugu zao waliojitolea figo wanaendelea vizuri na shughuli zao kama kawaida. Hii inaonesha ni kwa kiwango gani huduma hii imefanikiwa tangu ilipoanzishwa Novemba mwaka jana ”. amesema Dkt Swai.
Akifafanua amesem zoezi hilo la upandikizaji  figo limeshirikisha wataalamu wazalendo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya BLK, Taasisi ya Saifee iliyopo Mumbai India pamoja na Hospitali ya kimataifa ya Sakra ya nchini India.
“Tunapenda kuwataarifu kuwa katika kutoa huduma hii, tayari wataalamu wetu wa ndani hususani Madaktari bingwa wa upasuaji wamepata ujuzi wa kufanya upandikizaji wenyewe kwa kiwango cha asilimia 75 huku asilimia 25 wakielekezwa na wataalamu kutoka nje. Hii ni hatua kubwa sana katika kuongeza ujuzi wa kutoa huduma hiyo. Maeneo mengine tayari wamefikia asilimia 100 hususani wauguzi wa vyumba vya upasuaji, Madaktari bingwa wa tiba ya magonjwa ya figo (Nephrologists), wataalam wa vipimo vya maabara na Radiolojia.
Kwa mujibu wa Dkt. Swai MNH  itaendelea kufanya upasuaji kwa wagonjwa watano kila mwezi ikiwa ni mpango  wa muda mfupi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia sasa ambapo mpango wa muda mrefu  ni kufanya upasuaji kwa mgonjwa mmoja kila siku sawa na wagonjwa 20 kwa mwezi ambapo watakuwa wagonjwa 200 hadi 240 kwa mwaka.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya figo Hospitali ya Taifa Muhimbili Onesmo Kisanga amesema utafiti uliofanyika Kaskazini mwa Tanzania unaonesha kwamba asilimia 6.8 wana matatizo ya ugonjwa wa figo. Hivyo amewashauri Watanzania kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka na kuepuka matumizi mabaya ya dawa bila ushauri wa Daktari ili kuepuka magonjwa hayo.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt . Isaack Mlatie akitoa figo kwa ajili ya kupandikiza kwa mgonjwa mwenye tatizo la figo. Katikati ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo, Muhimbili, Dkt. Gabriel Mtaturu akishiriki katika upasuaji huo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji  wa Mfumo wa Mkojo kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Sakra nchini India, Dkt. Girish Nelivigi akishirikiana na madaktari wa Muhimbili kufanya upasuaji huo.

 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Njiku Kim akiandaa figo kabla ya kupandikizwa kwa mgonjwa. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo wa Muhimbili, Victor Sensa akishirikiana na Dkt. Kim kuaandaa figo kwa ajili ya kupandikizwa kwa mgonjwa mwingine.
 Wataalamu wakiendelea na upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa upasuaji wa mfumo wa mkojo kutoka nchini India.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai( katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo, kuhusu maendeleo ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushoto ni Daktari bingwa upasuaji wa mfumo wa mkojo Njiku Kim , kulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya figo Onesmo Kisanga.

MAGAZETI LEO AGOSTI 22, 2018

EID MUBARAK

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images