Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

LIVE: SWALA YA EID EL HAJI NA BARAZA LA EID KITAIFA VINGUNGUTI JIJINI DAR


Article 10

NSSF INAWATAKIA IDD EL-ADH'HAA NJEMA

WANANCHI WILAYA YA NYASA WASIFU UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI

0
0
*Wasema wanamatumaini makubwa dhidi yake,DC azungumzia ujenzi barabara Mbiga hadi Nyasa


Na David John,Nyasa

WANANCHI wa Wilaya mpya ya Nyasa wamesema hawaamini kama barabara kutoka Mbinga hadi Nyasa inajengwa tena kwa kiwango cha lami.

Wamedai kwamba barabara hiyo ilipimwa tangu mwaka ya 1974 lakini hadi sasa hakuna kilichokuwa kimefanyika.Wakizungumza jana wilayani hapa wamesema wanapongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli na kwamba mara zote imekuwa serikali ya vitendo ikisema inatenda.

Hivyo wanaona kama ndoto barabara hiyo inajengwa tena kwa kiwango cha lami.Wananchi hao wameeleza hayo baada ya mwandishi wa habari hizi kufika katika wilaya hiyo kwa lengo la kuona namna viongozi wamejipanga kwa ajili ya maendeleo, ambapo walisema hawaamini kwani wanaona kama ndoto.

Mwananchi Stephano Nchimbi alisema marais wengi wamepita lakini leo Rais John Magufuli anafanya kazi na wanamuomba Mungu aendelee kumbariki."Eti nasisi leo tunakwenda kuiona lami baada ya miaka lukuki,ndugu mwandishi mimi nakumbuka barabara ilipimwa tangu miaka ya 1974 tena mimi nikiwa bado kijana mdogo lakini Magufuli anafanya kwa vitendo leo Mungu ambariki,"alisema Nchimbi huku wezake wakimshangilia.

Pia Nchimbi ameomba Serikali ya wilaya hiyo kuwapa maelekezo Wakandarasi wanaojenga barabara hiyo kutoa kipaumbele kwa vijana wa kinyasa kupata ajira tofauti na ilivyo sasa ambapo walidai vijana wengi wanaofanya kazi wanatoka mbali."Kumekuwepo na ubaguzi kidogo katika kupata kazi hususani sisi vijana wakinyasa hivyo tunaomba wakandalasi kama anavyosisitiza Rais wetu Magufuli kutoa kipaumbele kwa wenyeji,"amesema Pius Mbawala
DC Nyasa  Mh.Esabela Chilumba .

WATANZANIA WASHAURIWA KUTHAMINI, KUHESHIMU TAARIFA ZA HALI YA HEWA

0
0
*Serikali yazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa huduma za hali ya hewa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SERIKALI imesema ipo haja kwa Watanzania wote nchini kuhakikisha wanajenga tabia ya kuheshimu na kuthamini taarifa za kitaaluma ambazo zinazotolewa nchini zikiwamo zinazohusu taarifa ya hali ya hewa.

Pia imesema taifa lolote linapanga mipango ya maendeleo ni lazima kuwepo na mfumo madhubuti wa kupata taarifa za hali ya hewa hasa kwa kuzingatia uwepo wa changamoto ya mbadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliyekuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa nchini wenye lengo la kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinafika kwa wakati na kufanyiwa kazi kikamilifu.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na wageni waalikwa kutoka taasisi na Wizara mbalimbali za Serikali ambapo pia Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani naye ameshuhudia tukio hilo baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Rwanda.

Akizungumzia mfumo huoMavunde amesema umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwenye mchakato wa maendeleo ya watu na uchumi wa viwanda.Na hivyo kupata taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kwani hata unapopanga mipango ya maendeleo ni vema kujua na taarifa za hali ya hewa.
Katibu Mkuu Shirika la Hali ya Hewa Duniani Prof.Petteri Taalas ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnes Kijazi na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari.

SUA WAKABIDHIWA MAJENGO KWA AJILI YA KUANZA KAMPASI MPYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA MSIMU MPYA WA MASOMO 2018/2019

0
0
WANANCHI wa Kijiji cha Daraja mbili katika kata ya Namwinyu wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameahidi kutoa ardhi bure kwa ajili ya
matumizi ya Chuo cha kilimo (SUA) ikiwa ni kivutio kwa chuo hicho kuharakisha ukamilishaji wa shughuli zake.

Ahadi hiyo ilitolewa na wananchi hao katika hafla fupi ya makabidhiano ya majengo yaliyo kuwa kambi ya wakandarasi wa shauri wa kampuni iliyojenga barabara kwa Kiwango cha lami Kilimesera-Matemanga.

Wananchi hao wamefikia uamuzi huo kwa tamko hilo kwa pamoja katika mkutano huo wakiwa wanajibu kauli mbali mbali za viongozi.Ambapo walisema kuwa mbali na mkutano mkuu wa kijiji hicho wapo tayari kutoa zaidi ya hekari 500 kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho na kwamba wapo tayari kuongeza endapo kutakuwa na mahitaji zaidi.

Kauli hiyo ambayo pia ilisisitizwa na Diwani wa Kata hiyo Thabiti Said walisema kuwa ujio wa chuo hicho katika eneo la kijiji chao kutasaidia kupanua kujengeka kwa Kijiji, kuharakisha maendeleo pamoja na kuwasaidia kuelimisha ndugu, jamaa na watoto wao hali itakayo wafanya kuanza kulima kilimo cha kisasa.

Awali Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Raphael Chibunda amewaeleza wananchi hao kuwa katika utekelezaji huo, Chuo hicho ambacho endapo watakipokea kwa kupeleka wanafunzi wengi kila mwaka kitakua haraka na kuwa chuo kinacho jitegemea katika kipindi kifupi kijacho.

Prof. Chibunda amebainisha kuwa katika utelekezaji huo chuo kimejipanga kuanza Oktoba mwaka huu kwa kutoa mafunzo katika nyanja za utalii, teknolojia na kutunza kumbukumbu."Ila baadae kitajitanua na kuongeza kilimo utaalamu wa vipando, Ugani, lishe,Tiba za wanyama, uzalishaji

wa Lishe ya Wanyama, Ufugaji wa samaki, sayansi ya utunzaji wa mazingira, misitu na wanyama pori, kilimo biashara pamoja na mafunzo ya maendeleo ya vijiji," amesema.

Amesema katika kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinaanza haraka na kuleta tija kwa wananchi wa maeneo hayo Chuo hicho kimepanga kupeleka trekta moja kati ya marekta 10 waliyokabidhiwa na Rais Dk.John Magufuli hivi karibuni na kuanzisha mashamba darasa ambayo yatasaidia wananchi wengi kwenda kujifunza kwa vitendo.

Kwa upande was Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkwanda Sudi amesema kuwa katika utekelezaji huo kwa kuanzia wananchi hao wamekubaliana kutoa hekta tisa na majengo 11 ambayo yalitumika na wakandarasi washauri wakati wa ujenzi wa barabara ya lami.

Mbunge wa jimbo la Tunduru kusini Daimu Mpakate amesema kuwa ujio wa Chuo hicho ni ukombozi wa wananchi waishio mikoa ya pembezoni ikiwemo Wilaya ya Tunduru pamoja na wilaya zilizopo katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amewataka wananchi kujipanga kwa kupeleka watoto wao Shule na kuhakikisha wanafaulu vizuri ili chuo hicho kiweza kuwanufaisha wakazi wa Tunduru, Namtumbo na watanzania wote kwa ujumla.

Amesema kwa vile Chuo kipo Tunduru itapendeza endapo kutakuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaotoka ndani ya wilaya ya Tunduru na wengine maeneo ya jirani kama Namtumbo, Nanyumbu, Masasi na Tanzania kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera pichani kulia akipiga makofi kuashiria furaha ya makabidhiano ya majengo hayo ya chuo ndani ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera  (kushoto) akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA ,Profesa Raphael Chibunda .
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera pichani kati akisoma moja ya taarifa kabla ya makabidhiano ya majengo hayo ya chuo cha SUA ndani ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma

SUPER STAR AKILI THE BRAIN AIBUKA UPYA BAADA YA KIMYA KIREFU

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFANYA ZIARA TUNDURU,AHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA MFUKO WA BIMA YA TAIFA

0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Josephat Kandege amefanya ziara  wilayani  Tunduru mkoani Ruvuma.

Katika ziara hiyo, aliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera ambae aliambatana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama. Akiwa katika ziara hiyo Kadege alikagua vituo viwili vya Afya cha Matemanga na Mkasale.

Amesema  lengo la ziara hiyo ilikuwa kuona utekelezaji wa mradi unavyoendelea, upanuzi wa majengo ya upasuaji, nyumba ya mganga, maabara, wodi ya mama na mtoto, nyumba ya kuhifadhia maiti, jengo la mionzi na kichomea taka.

Akikagua ukarabati huo Kandege ametoa maagizo yakiwamo ya Serikali izungumze na wananchi wanaoishi jirani na  kituo cha Afya Matemanga ili kupisha upanuzi wa eneo la kituo cha Afya hadi kufikia ekari 8 kwa sasa ni ekari 4.

Pili, usimamizi uendelee kwa miradi ya afya inayoendelea hadi sasa Serikali imetoa Sh.milioni 500 katika kituo cha Afya Matemanga na Sh.milioni 400 katika kituo cha Afya Mkasale.Pia ameagiza wananchi wajitokeze kwa wingi kujiunga na huduma ya Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa sasa waliojiunga Tunduru ni asilimia 43.5 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.

Amefafanua  huduma hiyi inapatikana kwa Sh.30,000 kwa mwaka  na inajumuisha Mama Baba na watoto wa nne.Pia kujenga majengo ya mionzi kwa kila kituo cha afya ili kurahisha upatikanaji wa huduma ya Mama mjamzito na matatizo mengine yanayofanana na hayo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkasale Mkuu wa wilaya ya Tunduru Homera awewahakikishia wananchi Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John  Magufuli itaendelea kuleta fedha za maendeleo kwa wakati.

"Na kwa sasa fedha za ujenzi wa vitanda kwa ajili ya bweni la wasichana wa shule ya sekondari namasakata imetengwa zaidi ya Sh. milioni sita na umeme wa jua utafungwa hivi karibuni na sh. million 19 zitapelekwa shule ya sekondari Muhuwesi kujenga madarasa mawili inayotarajia kuanza kidato cha kwanza mapema 2019 Januari.Hapa kazi tu," amesema.
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akimkaribisha Naibu Waziri Ofis ya Rais Tamisemi,Mh. Josephati kandenge kazungumza na Wananchi wa kijiji cha Kasale kata ya Namasakata wilayani Tunduru,baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya Mkasale kinachojengwa na serikali ya awamu ya tano ya CCM kwa shilingini Millioni 400.
Naibu waziri Tamisemi Mh  Josephat Kandege (wa tatu kulia) akiwa ameambatana Mkuu wa Wiaya ya Tunduru Mh.Juma Homera na viongozi wengine mbalimbali wakati wa ukaguzi wa kituo cha afya Mkasale ,Matemanga wilayani Tunduru na 
Taarifa ya Ukaguzi wa nyumba ya mganga,maabara,mochwari,jengo la upasuaji la akina mama,wodi ya akina mama,kichoma taka, nk
Naibu Waziri Tamisemi Mhe Josephat kandege akitoa maelekezo kwa DC Homera

MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI ASIMULIA KIFO CHA DADA YAKE

NEEC, Ubalozi wa Uholanzi wazindua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana

0
0
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi, Beng’i Issa wa pili kulia akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini, wa pili kushoto ni Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul,kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza hilo, Suleiman Malela na kushoto ni Ofisa wa Ubalozi huo, Bw. Ulrich Juhudi. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi, Beng’i Issa wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul wapili kulia wakati wa uzinduzi wa program ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini na wengine ni wakurugenzi na maofisa kutoka taasisi hizo. (Picha na Mpiga picha Wetu, Dar es Salaam).

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
BARAZA la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi nchini wamezindua program ya mafunzo ya ujasiriamali na malezi ya biashara kwa vijana waliohitimu elimu ya juu katika juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira na kuchochea uchumi wa viwanda.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi, Beng’I Issa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yanawalenga  vijana 50 wenye umri wa miaka 18 hadi 35 waliohitimu elimu ya juu nchini kuanzia sasa hadi miaka mitano iliyopita ambao wana nia ya kuanzisha, kupanua na kuboresha biashara zao.

“Ni mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanaotaka kujiunga wanahitajika kuandaa michanganuo ya mawazo ya biashara katika maeneo ya utalii, kilimo, nishati mbadala na mazingira,”,  fomu za kujiunga zinapatikana katika tovuti ya baraza ya www.uwezeshaji.go.tz au zinapatikana katika ofisi za baraza hilo aliongeza kusema, Bi. Issa.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya wiki moja ambapo vijana hao watapata fursa ya kujifunza mambo ya ujasiriamali na kuingia kwenye biashara pamoja na mambo mengine watapata nafasi ya kuandika michanganuo yao itakayo shindanishwa ambapo washindi watatu watapatiwa zawadi.

“Vijana watakao chaguliwa katika program hiyo watapewa mafunzo ya siku nne juu ya mipango ya biashara kabla ya kuendelea na mchujo wa kutafuta washindi watatu ambao watapewa mbegu mtaji,” mshindi wa kwanza atapata milioni 10, wa pili milioni saba na mshindi wa tatu atapata milioni tano na washiriki wengine watanufaika na ushauri wa kitaalamu, alisema, Bi. Issa.

Bi Issa alifafanua kwamba mafunzo hayo yanalenga maeneo manne ambayo ni utalii, Kilimo, Nishati mbadala na mazingira ambayo ni maeneo yenye kuleta matokeo chanya kwa haraka katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na kupambana na tatizo la ajira nchini.

Alisisitiza kwamba mafunzo hayo yanawalenga wahitimu hao wa fani mbalimbali ambao wakiingia kwenye biashara watafanya vizuri na kuanzisha makampuni yatakayopata maendeleo makubwa na kuweza kujiajiri na kuajiri wenzao.

Bi Issa alisema kwamba hii ni programu ya majaribio kwa kushirikiana na Serikali ya ya Uholanzi kupitia program hiyo na na baada ya mafanikio itapanuliwa zaidi. 

“Pamoja na program hii kuwa ya majaribio, sisi kama baraza tumekuwa tukiendesha mafunzo kama haya tangu 2013 kwa kushirikiana na taasisi zingine” kwa sasa ni mwendelezo wa program hiyo.

Kwa upande wake, Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu kama moja ya njia madhubuti ya kuhamasisha ujasiriamali katika kupambana na tatizo la ajira hapa Tanzania.

“ Serikali ya Uholanzi inayo furaha kushirikiana na baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kuhamasisha ujasiriamali kwa sababu kuna wigo mpana na fursa za biashara na kujiajiri,” alisema

Balozi huyo aliongeza kwamba kila mwaka kuna idadi kubwa ya vijana ambao wanaingia kwenye soko la ajira lakini hawana ujuzi na uzoefu wa kutosha kuweza kumudu changamoto hizo za mahitaji ya soko hilo, kwahiyo mafunzo hayo ni muhimu kwao kuweza kuajiri kupitia ujasiriamali.

Alieleza kwamba hapa nchini kuna wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali ambayo yanahitaji vijana wenye ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira na biashara za uwekezaji.

Balozi Verheul alisema kwamba serikali ya Uholanzi inaona program hiyo inamaana kubwa na matarajio yake ni kwamba makampuni mengi kutoka Uholanzi wataweza kusaidia programu hiyo.

WAZIRI MKUU ATUMIA USAFIRI WA BOENG 787-8 DREAM LINER YA. ATCL KUTOKA MWANZA HADI DAR

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisafiri kwa Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner wakitoka Mwanza kwenda Dar es salaam kupitia KIA, Agosti 22, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Phillip Mangula (watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla kuondoka kuelekea Dar es salaam kwa ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner Agosti 22, 2018.
Ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ikiwa Juu Ziwa Viktoria Mwanza ikijiandaa kutua katika uwanja wa Mwanza leo 22/Agosti /2018 .Picha na Chriss Mfinanga wa Ofisi ya Waziri Mkuu

JESHI LA POLISI PWANI LIMEKAMATA PULI NA MBEGU ZA BANGI HUKO KISARAWE-RPC SHANNA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KISARAWE .


JESHI la polisi mkoani Pwani, linamsaka dereva aliyefahamika kwa jina la Moshi Ramadhan Malinganya mkazi wa Kisarawe kwa tuhuma za kusafirisha bangi puli 193,katika gari alilokuwa akiliendesha .

Pamoja na hilo ,kwenye buti ya gari hilo kumekutwa na ndoo ndogo mbili za lita kumi zenye bangi na kiroba kidogo chenye mbegu za bangi kilo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kisarawe, kamanda wa polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna ambae anasubiri makabidhiano kuhamia Mwanza kikazi,alisema mtuhumiwa ametoroka baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka wakati akiwakimbia polisi.

Alieleza , tukio hilo lilitokea agosti 21 majira ya usiku eneo la shule ya sekondari Minaki akiwa anaendesha gari namba T 801 AAF aina ya Toyota Mark II.
kamanda wa polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna akionesha namba za Gari kwa Wanahabari (hawapo pichani)

“Tulipata taarifa toka kwa wasamaria wema juu ya gari hilo kusafirisha bangi kutoka kijiji cha Gwata kwenda Mombasa Jijini Dar es Salaam tuliweka mtego eneo la mnara wa TBC lakini tulipomsimamisha hakusimama”, alisema Shanna.Shanna alisema ,polisi walimkimbiza lakini walikuta gari hilo limepinduka huku dereva huyo akiwa amelitelekeza .” Vitu vingine vilivyokutwa katika gari hilo ni namba za magari mbili ikiwemo namba T 321 AJH na TZH 7255 jambo linaloashiria kuwa mtuhumiwa alikuwa akibadilisha namba hizo wakati wa matukio ya biashara haramu ya dawa za kulevya,”alisema Shanna.

Hata hivyo, alielezea wanamshikilia mmiliki wa gari hiyo (Majaliwa Salehe) kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusu gari lake kukutwa na madawa hayo.Kwa mujibu wa kamanda huyo ,wataiomba mahakama kutaifisha gari hilo kwa mujibu wa sheria ili kuwakomesha watu wanaojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya

MRADI WA UMWAGILIAJI MWASUBUYA KUWA MRADI WA MFANO

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuutumia Mradi wa Umwagiliaji wa Mwasubuya kubadilisha maisha ya wananchi wilayani Bariadi, kupitia kilimo cha kisasa kinachotumia zana za kisasa na kuufanya kuwa mradi wa mfano ambao watu wataenda kujifunza.

Mtaka ameyasema hayo katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 yaliyofanyika Kitaifa mkoani Simiyu na kuwashukuru viongozi wa Chama na Serikali, Watendaji, Watumishi, wafanyabiashara na wadau wengine waliofanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.

Amesema mradi huo wenye ekari 514 zitakazolimwa kupitia Kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia maji ya Bwawa la Mwasubuya lililoigharimu Serikali shilingi bilioni 1.24, utahusisha kilimo cha kisasa chenye kutumia zana za kisasa katika hatua zote kuanzia kuandaa shamba, kupanda, palizi na kuvuna badala ya kuhusisha zana za kilimo za mikono.

“ Nimewaambia watu wa Bariadi tunahitaji Kijiji kimoja ambacho tutabadilisha maisha ya wananchi na watu wataenda kujifunza na kuangalia transformation(mabadiliko) ya kile kijiji, lakini pia tunahitaji lile shamba lote la ekari 514 lilimwe pasipo kutumia mikono ya wanadamu kuanzia hatua za kuandaa shamba, kupanda, palizi hadi kuvuna” alisema

Ameongeza kuwa dhamira ya Mkoa ni kuona wananchi wanalima kisasa kwa kutumia zana bora za kilimo ambazo baada ya mazungumzo na Kampuni ya Agricom Africa imekubali kuikopesha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi zana zote muhimu ili kuwawezesha wakulima katika mradi wa Mwasubuya kuongeza tija katika uzalishaji.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza katika Kikao cha Tathmini Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha maonesho hayo, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi.



TANZANIA NA UGANDA ZA AZIMIA KUKUZA BIASHARA KATI YAO

0
0



Tanzania na Uganda za azimia kukuza biashara kati yao


Tanzania na Uganda zimeazimia kuondoa vikwazo vya kibiashara ili kukuza kiwango cha biashara kati yao ambacho kwa takwimu zilizopo sasa zinaonesha kipo chini mno.


Hayo yalibainishwa katika mkutano wa Jukwaa la biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika leo kando ya Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) unaofanyika kwa silku tatu jijini Kampala tokea tarehe 21 Agosti 2018.


Mgeni Rasmi katika mkutano huo ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushirikia ya Uganda, Balozi Julius Onen alieleza kuwa Tanzania na Uganda zina nafasi kubwa ya kukuza biashara endapo njia za usafiri zitaboreshwa, vikwazo visivyo vya kibiashara vitaondolewa pamoja na kuwa na mikakati ya pamoja ya kuweka viwango vya ubora vinavyotambulika katika nchi zote na kanda nzima kwa ujumla.


Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wawakilishi mbalimbali wa Tanzania akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko alisema kuwa Mamlaka ya Bandari imeboresha kwa kiasi kikubwa huduma zake ikiwemo kuanza upya kwa njia ya Dar Es Salaam- Mwanza hadi bandari ya Bell nchini Uganda. Alisema kufunguliwa kwa njia hiyo kumepunguza idadi ya siku za kusafirisha mizigo kutoka Dar Es Salaam hadi Uganda ambapo kwa sasa mizigo inasafirshwa kwa siku nne  na kwa kiwango kikubwa na gharama nafuu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushirika wa Uganda, Balozi Julius Onen akisoma hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika Kampala siku ya Jumatano tarehe 22 Agosti 2018. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akichangia mada katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mamlaka ya Bandari imeboresha kwa kiasi kikubwa huduma zake 
Mkurugenzi wa Shirika la kukuza Biashara katika nchi za Afrika Mashariki kwa upande wa Uganda (Trademark East Africa), Bibi Dawali Ssali akieleza mikakati ya inayofanywa na shirika hilo katika kuboresha mazingira ya biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. mikakati hiyo ni pamoja na kushirikiana na nchi za EAC kujenga vituo vya kutoa huduma kwa pamoja mipakani. 
Wajumbe wa Uganda na Tanzania wakijadili mikakati ya kukuza na kuimarisha biashara kati ya nchi zao.

Wananchi Waridhia Bwawa La Urughu kutangazwa kama Eneo Lindwa-kimazingira

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Iramba kwa kutembelea bwawa la Urughu na kuwataka wakazi wa eneo hilo kusimamia rasilimali hiyo kwa mustakabali wa maisha yao ili kuendeleza fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na masuala ya uvuvi na kilimo.

Mhe. Makamba amesema ili bwawa hilo liweze kutangazwa kama eneo lindwa ki-mazingira ni lazima wananchi wawe na utashi, utayari na uwezo wa kutunza bwawa hilo kwa kufuata masharti yatakayotolewa katika tangazo la Serikali ikiwa ni miongoni mwa maeneo 77 yaliyopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.

Waziri Makamba amesema uhifadhi wa bwawa hilo utaendana na makatazo kwa baadhi ya shughuli za kibinadamu ili kulinusuru ikiwa ni pamoja na kuzuia shughuli za uvuvi na kilimo kisicho endelevu katika Vyanzo vya maji. Aidha, Waziri Makamba ameutaka Uongozi wa Wilaya ya Singida kupitisha azimio lao la kuhifadhi bwawa la Urughu na Msitu wa Ushora katika Baraza la Madiwani.

Waziri Makamba ameahidi bila kuchelewa kutangazwa Bwawa la Urughu kuwa eneo nyeti kimazingira na kusaidia kuondoa kadhia ya kujaa kwa mchanga katika bwawa hilo. “Ili sisi tuendelee na mchakato huo tuleteeni sifa za maeneo husika kama vile, milima, mabwawa na mashamba yenye umuhimu mkubwa na historia inayojenga hoja ya umuhimu wa ulinzi katika eneo hilo, pia lipatikane azimio la Baraza la Madiwani kuwa ni eneo nyeti na kuwasilisha ombi ili Waziri aweze kuchukua nafasi yake kisheria” Makamba alibainisha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula mara baada ya kuwasili Wilayani hapo kwa ziara ya kikazi. Waziri Makamba ametembelea bwawa la Urughu na Ziwa Kitangiri ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa kuwa maeneo lindwa kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wakazi waishio pembezoni mwa ziwa Kitangiri Wilayani Igunga. Waziri Makamba amewaasa wakazi hao kuwa chachu katika kuhifadhi mazingira ya ziwa hilo kwa manufaa ya sasa na baadae.
Wakazi wa mwalo wa Shauri-Tanga katika Ziwa Kitangiri Wilayani Iramba, wakizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba juu ya namna wanavyotumia ziwa hilo kwa shughuli za uvuvi.

Bwawa la Urughu lilipo Wilayani Singida liko hatarini kutoweka kutokana na matumizi yasiyoendelevu ya shughuli za kibinadamu yanayopelekea kujaa mchanga na kupungua kwa kina cha maji. Waziri Makamba ameazimia kutangaza bwawa hilo kama eneo lindwa kimazingira ili kuweka ulinzi na matumizi endelevu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA VYEMA MIRADI YA MAENDELEO

0
0
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kutekeleza miradi ya maendeleo yenye ubora na kwa gharama nafuu.

Pia ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa fedha kwa ajili ya uimarishaji wa vituo mbalimbali vya afya pamoja na sekta ya elimu.Kabeho ametoa pongezi hizo jana kwa nyakati tofauti wakati akikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya mendeleo wilayani humo ambako Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa.

Sanjari na hilo Kiongozi huyo alipongeza wilaya hiyo kwa kuishirikisha jamii katika kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya jambo ambalo linachangia uboreshaji wa sekta hizo.“Kishapu mna kitu cha pekee tofauti na huko kwengine nilikopita, hapa ninyi katika miradi yenu mlipopewa fedha ndani ya gharama mmebakiza chenji na mnaongeza miradi mingine kwa fedha hizo hizo hivyo mnafanya kitu cha kuigwa,” alisema.

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge aliongeza kuwa kwa kuishirikisha jamii katika utekelezaji wa miradi hali inayoifanya nayo ifanye uwekezaji wa maendeleo katika senkta mbalimbali.Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwa maendeleo ya Taifa letu” ulikabibidhiwa mkoani Shinyanga wilayani Kishapu ukitokea wilayani Maswa mkoani Shinyanga umepitia miradi ya sh.bilioni 2.2.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho akizindua mradi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya msingi Wishiteleja wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Charles Kabeho akiwa ndani ya chumba cha darasa cha Shule ya sekondari Maganzo ambao ni mradi wenye thamani ya sh. miloni 141 uliogharamiwa na fedha kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Charles Kabeho akikagua moja ya vyumba vya madarasa Shule ya msingi Wishiteleja wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali wilayani Kishapu ambako ulikagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani sh. bilioni 2.2.

DKT. PHILIP MPANGO: KITUO CHA UTAFITI NALIENDELE MKOANI MTWARA KUPEWA FEDHA ZA KUTOSHA

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Mtwara

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameuahidi uongozi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele kwamba Serikali itakiwezesha Kituo hicho na vituo vingine vya utafiti nchini ili viendeleze kazi ya utafiti wa mazao ya kilimo ambacho kinategemewa na watanzania wengi katika kujikwamua kiuchumi.

Dkt. Mpango ametoa ahadi hiyo alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara, ambacho uongozi wake ulielezea wasiwasi wake wa kupata rasilimali fedha za kuendeleza utafiti wa mazao likiwemo zao la korosho pamoja na watumishi baada ya kuondolewa kwa fedha za ushuru wa korosho inayouzwa nje, zilizokuwa zikitumika kuendeleza utafiti huo.

Alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa shughuli za utafiti katika kuendeleza uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla na kwamba atajitahidi kama Waziri wa Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Waziri mwenzake anayeshughulikia kilimo ili taasisi hiyo isikwame kufanya shughuli zake.

"Niwahakikishie kabisa kwamba Serikali haitakubali utafiti wa mazao yote unaofanyika hapa likiwemo zao la korosho udhurike, litakuwa ni janga kubwa, kwahiyo upatikanaji wa fedha za Kituo hiki litakuwa ni moja ya vipaumbele vyangu" alisisitiza Dkt. Mpango

Alisema kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa na kwamba hakutakuwa na mapinduzi ya viwanda bila kilimo kwa sababu viwanda vinavyojengwa vinatarajiwa kuongeza thamani ya mazo ya kilimo pamoja na mazao ya mifugo na uvuvi.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipata maelezo kuhusiana na zao la Korosho,alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara
Mmoja wa Wataalamu pichani juu na chini kutoka kituo cha Utafiti Naliendele akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipotembelea Kituo cha Utafiti Naliendele, mkoani Mtwara

Ongala Music Festival kulindima kesho Agosti 23-25,Kigamboni

0
0
Na Andrew Chale, Dar

Tamasha kubwa na la aina yake la muziki wa Kiafrika maalum kumuenzi gwiji wa muziki Hayati Dk. Remmy Ongala lililopewa jina la ONGALA MUSIC FESTIVAL, linatarajiwa kulindima kwa mara ya kwanza kuanzia hapo kesho katika fukwe mwanana za Malaika Beach Club, Kigamboni, Agosti 23-25.

Akizungumza Mratibu wa tamasha hilo Bi. Aziza Ongola anaesimamia mfuko wa Ongala (Ongala Foundation), amesema tayari maandalizi yote yameenda vizuri na watu wakae mkao wa kulishuhudia tamsha hilo ambalo ni la urithi wa muziki kutoka kwa gwigi Dk. Remmy.

Aziza amesema kuwa, Wasanii mbalimbali kutoka Nchi tofauti za Afrika na bendi zao watatoa burudani kwa muda wa siku tatu yaani kuanzia Agosti 23-25,2018 katika fukwe hizo za Malaika, Kigamboni.

“Tutamuenzi Baba kupitia nyimbo zake nyingi ambazo zimekuwa na umaarufu ndani na nje ya Afrika. Hivyo tamasha ili ni kuamsha hali ya Muziki aliouacha na pia kuendelea kumkumbuka kupitia mashairi yake” alieleza Aziza.Aziza ameongeza kuwa, tamasha hilo pia litasaidia kuimarisha kumbukumbu na kazi za gwiji huyo aliyefariki Desemba 2010, Nchini.

Kwenye tamasha hilo vikundi 22 kutoka nchi mbalimbali za Afrika vitatumbuiza kwa siku hizo tatu.Miongoni mwa wasanii hao ni msafiri Zawose, Ally Swahi, Siti and the Bend, Hokororo, King kiki na Sikinde. Pia atakuwepo Ashimba, Carola Ongala Music Festival kulindima kesho Agosti 23-25,Kigamboni

Tamasha kubwa na la aina yake la muziki wa Kiafrika ambalo ni maalum kumuenzi gwiji wa muziki Hayati Dk. Remmy Ongola lililopewa jina la ONGALA MUSIC FESTIVAL, linatarajia kulindima kwa mara ya kwanza kuanzia hapo kesho katika fukwe mwanana za Malaika Beach Club, Kigamboni.

Akizungumza Mratibu wa tamasha hilo Bi. Aziza Ongola anaesimamia mfuko wa Ongala (Ongala Foundation), amesema tayari maandalizi yote yameenda vizuri na watu wakae mkao wa kulishuhudia tamsha hilo ambalo ni la urithi wa muziki kutoka kwa gwigi Dk. Remmy.

DKT SHEIN AONGOZA SWALA YA EID EL HAJJ (MAKUNDUCHI) KUSINI UNGUJA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali na Mashekhe wa Mkoa wa Kusini Unguja katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,ambapo Swala hiyo imeongozwa na Sheikh Suleiman Haji Ibrahim
Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,ambapo Sheikh Suleiman Haji Ibrahim(hayupo pichani) aliongoza Swala hiyo,iliyohudhuriwa na Viongozi wa Kitaifa akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya akinamama waliojumuika katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja
Sheikh Abdalla Issa Makame (kulia) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja akisoma Khutba mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine pamoja na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo baada ya Swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika uwanja wa Jamhuri Makunduchi

BARAZA LA EID EL HAJJ KIZIMKAZI MKOA WA KUSINI UNGUJA

0
0
 Askari wa Kikosi cha Polisi FFU wakitoa salamu ya Hesma kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa  akipokea salamu hiyo ya heshma  katika  Sherehe  za Baraza la Eid el Hajj zilizofanyika leo  katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa  akipokea salamu ya heshma kwa gwaride maalum la kikosi cha Polisi FFU wakati wa Sherehe  za Baraza la Eid el Hajj zilizofanyika leo  katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa  akisalimiana na Wananchi na kuwatakia kheri na salama katika Sikukuu ya Eid el Hajj baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa  akisalimiana na Wananchi na kuwatakia kheri na salama katika Sikukuu ya Eid el Hajj baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa  akisalimiana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Wananchi na kuwatakia kheri na salama katika Sikukuu ya Eid el Hajj baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja.
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images