Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE AMRI ATHUMAN ‘KING MAJUTO’ LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Hamza Amri Athuman mtoto wa marehemu Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally akisoma dua kumuombea Marehemu Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Mara baada ya dua hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliongoza mamia ya wananchi kutoa heshima za mwisho katika msiba huo,anaefuta kushoto kwa Rais ni Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete. 
PICHA NA IKULU


BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 09.08.2018

NGUZO ZA DARAJA LA RELI YA SGR STESHENI YA DAR ES SALAAM HADI ILALA

WITO...WITO...WITO... KWA WANA MACHAME GIRLS SECONDARY SCHOOL WOTE

$
0
0
Tunawatangazia watu wote waliosoma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Machame kuundwa kwa “Machame Girls Alumni”. 

Lengo kuu ni kuienzi elimu bora tuliyoipata, kwa kushirikishana  masuala ya maendeleo, yanayoihusu shule hiyo na jamii kwa ujumla.

Kwa wote wanaopenda kujiunga nasi, tafadhali piga au tuma ujumbe wa simu au whatsapp kwa namba 0784485678 au 0784368484/0768368484 kabla ya tarehe 30 August, 2018.

 JIVUNIE SHULE YAKO, JENGA TAIFA LETU
KAMATI YA MAANDALIZI

MIKOA YA GEITA, NJOMBE, RUKWA NA SIMIYU KUPATA VYUO VYA VETA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (Kushoto)alitazama mwonekano katika picha wa Chuo cha Mkoa huo pindi kitakapomaliza.
Mwenyekiti wa Bodi wa Bodi ya VETA Ndg. Peter Maduki akikabidhi mchoro wa chuo cha VETA Geita kwa mkandarasi wa kampuni ya Skywards Construction aliyepewa kazi ya ujenzi wa chuo hicho
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Ndg.Peter Maduki wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Geita.Wengine ni Wakurugenzi wa VETA na wakandarasi wa mradi huo.
Uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Chato, Uongozi wa VETA,Wakandarasi na baadhi ya wananchi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa chuo cha Wilaya hiyo kwa Mkandarasi.

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeanza utekelezaji wa  ujenzi wa Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Mikoa ya Geita, Njombe, Rukwa na Simiyu ikiwa ni sehemu ya kutoa huduma ya ufundi na ujuzi ili kukidhi mahitaji ya mikoa hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi maeneo ya ujenzi wa vyuo vya mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato, Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Peter Maduki  alisema  ujenzi wa vyuo hivyo kwa mikoa hiyo una lengo la kutekeleza mkakati wa Mamlaka wa  kuongeza udahili hadi kufikia idadi ya wanafunzi 700,000 ifikapo mwaka 2020.

Alisema kuwa jitihada hizo zinaenda sanjari na utekelezaji wa nia njema ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kuwa vijana wanapata ujuzi stahiki utakaowawezesha kuajiriwa au kujiajiri ili kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi na kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Akikabidhi rasmi nyaraka za ujenzi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Mkoa wa Geita chenye ukubwa wa hekta 27 kwa Mkandarasi anayejenga chuo hicho Kampuni ya Kitanzania Skywards Construction
 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Maduki alisema kuwa gharama ya ujenzi wa chuo hicho ni kiasi cha Sh bilioni 9.9 fedha za mkopo kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

EXIM BANK TANZANIA WAKABIDHI JEZI MASHINDANO YA MAJESHI YA POLISI EAPCCO

$
0
0
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa akipokea jezi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Stanley Kafu (kushoto) zilizodhaminiwa na benki hiyo kwaajili ya Mashindano ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (EAPCCO) yaliyotarajiwa kuanza jana kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Mashindano hayo yanayoshirikisha nchi 14 yatahusisha michezo ya Mpira wa Miguu, Netiboli, Mpira wa wavu, Kulenga shabaha, Kareti, Judo na Taekondo na yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii. 
MAJESHI-- Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa akiwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu (kushoto) wakionesha moja kati ya jezi zilizodhaminiwa na benki hiyo kwaajili ya Mashindano ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (EAPCCO) yaliyotarajiwa kuanza jana kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Mashindano hayo yanayoshirikisha nchi 14 yatahusisha michezo ya Mpira wa Miguu, Netiboli, Mpira wa wavu, Kulenga shabaha, Kareti, Judo na Taekondo na yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii. Wengine ni Abdul Nkondo (kulia), Meneja msaidizi wa idara ya masoko na mawasiliano wa Benki ya Exim Bank Tanzania and PC Daniel Mashaka (kushoto).

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA UINGEREZA (DFID) MHE. PENNY MORDAUNT IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha albamu ya picha Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt inayoonesha Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyobomolewa kabisa na Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera lililotokea Septemba 10, 2016  ambayo imejengwa upya na serikali ya Uingereza kupitia mpango wake wa maendelo ya elimu kupitia UKAid/DFID. Picha hizo zinaonesha shule hiyo baada ya tetemeko, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi siku ya mwaka mpya wa 2017 na inavyoonekana sasa baada ya kujengwa upya. Mhe. Mordaunt, ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi, alimtembelea  Rais Dkt. Magufuli akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago cha "Umoja"  Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke aliyeongozana na , Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana pia na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy aliyeongozana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke,  walipomtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari kuishukur serikali ya Uingereza  kwa misaada yake mbalimbali ikiwemo Shilingi Bilioni 307 kwa kuunga mkono juhudi zake za kuopambana na rushwa pamoja na kuboresha sekta za afya na elimubaada ya kukutana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (Department of International Development - DFID - ) Mhe. Penny Mordaunt aliyemtembelea akiwa ameongozana na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke, na Mkuu wa ofisi ya DIFD nchini Mama Beth Arthy Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2018.

Picha na IKULU

SIERRA LEONE YAFURAHISWA NA HATUA KUBWA YA MAENDELEO YANAYOFANYWA NA NSSF NCHINI

$
0
0
Nchi ya SIERRA LEONE imefurahishwa na hatua kubwa ya maendeleo yanayofanywa na mfuko wa Taifa wa Hifadhi wa Jamii NSSF nchini na kwamba italazimika kuiga baadhi ya masuala ikiwemo kuanzisha kitengo kipya cha viatarishi katika mfuko wao ili kuongeza ufanisi na kuzuia kutokea kwa majanga yanayoweza kujitokeza.
Hayo yamesema na  Naibu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Bima SIERRA LEONE ,Mohammed Gondoe alipotembelea katika makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, William Erio ambapo amesema kuna mambo mazuri yamefanywa na NSSF hivyo hawana budi kujifunza.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa NSSF William Erio amesema Tanzania na SIERRA LEONE zitaendelea kushirikiana na kuwa na mahusiano mazuri katika kuhakikisha wanabuni mipango ya kusaidia ukuaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii ya Taifa. 
Mifuko ya Hifadhi ya jamii ya TANZANIA na SIERA LEONE imekuwa ikishirikiana kwa muda mrefu jambo ambalo limesaidia kuongeza ufanisi na weledi katika utendaji kazi wake kwa wafanyakazi wa mifuko hiyo.
Gondoe na wajumbe wenzake kutoka nchini SIERA LEONE wapo nchini kujifunza masuala mbali mbali ya hapa nchini ikiwemo mfumo wa utoaji mikopo ya elimu ya juu uliopo chini ya wizara ya elimu,sayansi na teknolojia. 

Imetolewa na Idara cha Uhusiano na Masoko.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii-NSSF
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ,William Erio(kulia) akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Naibu MKurugenzi wa mfuko wa Hifadhi  ya Jamii na Bima  wa Sierra Leone,Mohammed Gondoe aliyemtembelea  leo katika makao makuu ya ofisi ya NSSF iliyopo jijini Dar es salaam

MAOFISA MAGEREZA 20 KWENDA NCHINI SHELISHELI KUTEKELEZA JUKUMU LA UREKEBISHAJI WA WAHALIFU

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiagana na Mkaguzi wa Magereza Godfrey Mpagike(kulia) ambaye ni miongoni mwa maofisa na askari 20 wa Jeshi la Magereza ambao wanatarajia kuondoka Agosti 16, 2018 kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu  kwa mkataba wa miaka miwili.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuagananao leo Agosti 10, 2018 jijini Dar es Salaam. Maafisa hao wanatarajia kuondoka kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza(walioketi) na askari wa Jeshi hilo vyeo mbalimbali(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya kuagananao leo Agosti 10, 2018 jijini Dar es Salaam. Jumla ya maafisa na askari 20 wa Jeshi la Magereza wanatarajia kuondoka kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili
Maafisa wa Jeshi la Magereza ambao wanatarajia kuondoka kuelekea nchini Shelisheli kutekeleza jukumu la Urekebishaji wa wahalifu kwa mkataba wa miaka miwili wakijadiliana jambo mara baada ya kuagana rasmi na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.

MICHEZO YA SHIRIKISHO LA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI YASHIKA KASI VIWANJA VYA UDSM.

$
0
0
 Mchezaji taekwondo wa Polisi Tanzania mkaguzi wa Polisi (INSP) Danny  ameshika 
   nafasi ya kwanza kwa mchezo wa uzito wa juu katika michezo ya karate ya TaeKwondo kwenye michezo ya EAPCCO inayoendelea viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam
 Naibu kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Khamisi akikabidhi kobe kwa mshindi wa mchezo wa Taekwondo kutoka Polisi Kenya katika michezo ya EAPCCO GAMES yanayoendelea viwanja vya chuo kikuu cha Dar es SALAAM.
Wachezaji wa mchezo wa Taekwondo kutoka Polisi Rwanda wakishagilia ushindi wa kwanza wa ujumla baada ya kupata vikombe viwili katika mchezo huo. Picha zote na Jeshi la Polisi

UKAGUZI WA CAG KATIKA MASHIRIKA YA TBC NA TANESCO 2016/217

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) halijawahi kupata gawio kutokana na umiliki wa hisa 35 mtaji wa Star Media LTD tangu mwaka 2013 kwa sababu ya star Media kuripoti hasara ya sh.bilioni 61.

Akizungumza katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi na Kukusanya maoni kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 iliyofanyika Katika Ukumbi wa PPF Tower Mkaguzi wa Mashirika ya Umma Pascal Mahwago amesema kuwa star media iliripoti uchakavu wa vitu na kufanya TBC kukosa gawio licha ya kuwa na hisa.

Amesema kuwa ushauri wa CAG ulitaka kuhakikisha shughuli zote za kifedha zinafuatiliwa kwa ukaribu katika kuweza kupata gawio kutokana na uwekezaji wa hisa hizo.Kahwago amesema katika ukaguzi mwingine ni Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) lilikabidhi mali zisizohamishika kwa kampuni ya kufua umeme ya Songas mwaka 2004 zilizokuwa ndani ya Ubungo Complex kwa kupewa hisa 10,000 bila ya kukokotoa thamani halisi ya Mali walizokabidhi. 

Amesema Tanesco ilishauriwa kufanya tathimini na kupitia mkataba wa kuhamisha mali uliosainiwa ili kuangalia kama zilizohamishwa zinaendana na thamani ya hisa walizopewa.Aidha amesema kampuni ya Songs iliwekeza Euro 285.7 sawa na asilimia 73 katika mradi wa Songas hata hivyo hauonyeshi sehemu yeyote ya umiliki kwa serikali kwenye mradi huo licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali.

Kahwago amesema mapendekezo ya CAG ni serikali kupitia upya mpangilio wa mradi na kutathimini kama mkataba uliofanyika kwa kuangalia usawa wa pande zote mbili.
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Wendy Massoy akizungumza katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Nje wa Wizara Grace Trofumo akitoa mada kuhusiana na ukaguzi mbambali unaofanywa na CAG katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Mashirika ya Umma Pascal Kahwago akizungumza kuhusiana na mada ya ukaguzi katika mashirika ya umma.
Mkaguzi wa Serikali za Mitaa Ally Said akitoa mada ya ukaguzi wa Serikali za Mitaa katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi na Kukusanya maoni kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 iliyofanyika Katika Ukumbi wa PPF Tower.
baadhi ya wadau katika warsha ya Toleo Maalum kwa Wananchi na Kukusanya maoni kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2016/2017 iliyofanyika Katika Ukumbi wa PPF Tower
Picha ya pamoja ya wadau na mgeni rasmi Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Wendy Massoy.

Msimu mpya wa Premier League na DStv

$
0
0
Baada ya Msimu wa Kombe la Dunia kuisha tunarudi kwenye ratiba yetu rasmi ya Soka la Kibabe la Ligi ya EPL. Wanaotufungulia dimba Ijumaa hii ni mechi kati ya Manchester United dhidi ya Leicester City. Wazee wa kazi wanasema biashara asubuhi, je wabingwa hawa wataanzaje msimu huu?

MAJIBU tutayapata Ijumaa hii ndani ya Supersport 3 Saa 3:50 usiku LIVE kwenye DStv pekee ikiwa kwenye Lugha yetu tamu adhimu ya Kiswahili.

Bila kusahau, wateja wa DStv wanaweza pakua “Download Application” ya DstvNow itakayowawezesha watanzania wengi kufurahia msimu huu wa soka kwani unachotakiwa tu ni kuwa na akaunti yako ya DStv na unaweza kutazama katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida ukiwa mahali popote wakati wowote!

Huu Moto hauzimi na kama sio DStv, Basi Potezea!

JUMAA AKABIDHI GARI YA WAGONJWA KWALA ILI KUPUNGUZA ADHA YA USAFIRI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha Vijijini

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amekabidhi gari la wagonjwa (ambulance ),iliyogharimu mil.75 ,katika kituo cha afya cha Kwala .

Gari hiyo itaendelea kusaidia kupunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa hasa mahututi na warufaa.Akikabidhi gari hilo ,kwa mganga mfawidhi wa kituo hicho ,diwani wa kata ya Kwala, mbele ya wananchi ,Jumaa alisema ataendelea kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao .

"Serikali yetu inafanya makubwa katika kupunguza changamoto mbalimbali kwenye sekta ya afya na nyingine kama elimu ,miundombinu na nishati ya umeme""Kwa kutambua hayo ,July 2017 nilikabidhi magari mawili ya wagonjwa yaliyotokana na mfuko wangu na jingine moja ni msaada kutoka kwa Rais John Magufuli ikiwa ni kati ya magari ya wagonjwa 67 yaliyogawanywa katika maeneo mbalimbali nchini" alisema Jumaa.

Hata hivyo Jumaa ,alisema ameamua kujikita kutatua kero mbalimbali ili kwenda pamoja na kauli mbiu yake ya SISI KWANZA SERIKALI BAADAE .Mbunge huyo ,aliomba magari hayo yatunzwe na kutumike kwa matumizi lengwa.Nae mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,ambae pia ni diwani wa Kwala , Mansoor Kisebengo ,alisema hairuhusiwi wananchi kugharamia mafuta kwenye magari hayo .

Alielezea, halmashauri hiyo imekuwa inachangia gharama za mahitaji ya mafuta ili kuondoa bugudha kwa wananchi .Kwa upande wake mganga mfawidhi kituo cha afya Kwala ,dk.Mustapha Jaffar alimshukuru mbunge huyo kwa msaada alioutoa .Alisema hajafanya makosa kupeleka gari eneo la Kwala ,kwani litakuwa msaada mkubwa kwa wajawazito na wagonjwa wa rufaa.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa akikabidhi funguo ya gari la wagonjwa ambalo limegharimu mil.75 ,kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Mansoor Kisebengo ambae pia ni diwani wa kata ya Kwala.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Mansoor Kisebengo ambae pia ni diwani wa kata ya Kwala, akizungumza na wananchi wa Kwala ,kabla ya mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa kukabidhi gari la wagonjwa ambalo limegharimu mil.75 ,kwenye Kituo cha afya cha Kwala.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa akizungumza na wananchi wa Kwala kabla ya kukabidhi gari la wagonjwa ambalo limegharimu mil.75 ,katika kituo cha afya cha Kwala.

Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

$
0
0
Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (The 38th Ordinary of the SADC Summit of Heads of State and Government) utafanyika tarehe 17-18 Agosti, 2018.

Mkutano huu utatanguliwa na mikutano ifuatayo;

(i) Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao utapitia na kujadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. Mkutano huu utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe wake ambao ni Angola (Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama), Zambia (Makamu Mwenyekiti wa Organ) na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mwenyekiti wa Organ aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi).

(ii) Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 14 Agosti 2018 pamoja; na 

(iii) Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 11Agosti 2018.

Prof Adolf Mkenda, Katibu Mkuu, Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anaongoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Makatibu Wakuu akisaidiana na Eng. Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ( Ujenzi), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango. Mhe Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ataongoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Mawaziri.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC), Dkt. Stergomena L. Tax (kushoto) akishuhudia makabidhiano ya uongozi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Makatibu Wakuu wa SADC baina ya mwenyekiti anayemaliza muda wake, Bw. K E Mahoai Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti mpya, Balozi Selma Ashipala-Musavya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Namibia.Makabidhiano hayo yamefanyika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC uliofanyika katika Hoteli ya Safari Mjini Windhoek, Namibia tarehe 09 Agosti 2018. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu(kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa Kikanda (kulia), Balozi Innocent Shiyo wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika. 
Mwenyekiti wa Makatibu Wakuu wa SADC,Balozi Selma Ashipala-Musavyi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano huo ambapo aliwashukuru wajumbe kwa kuwa na imani naye na kumpa jukumu hilo na pia alisisitiza katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha anashirikiana na wanachama kusimamia suala la ulinzi na usalama linapatikana ndani ya jumuiya ili kuruhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Bw. K E Mahoai akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano mara baada ya kukabidhi nafasi ya uenyekiti ambapo aliwashukuru wajumbe kwa ushirikiano alioupata wakati wa uongozi huo kwa taifa lake. 
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC. 


Benki ya TPB Plc yawakaribisha wateja waliokuwa benki ya wanawake Tanzania (TWB).

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi, akiwakaribisha katika benki hiyo, wateja waliokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) Pia amefafanua mambo mbalimbali kuhusu kuwahudumia wateja wao bila ukiritimba wowote watashirikiana pamoja. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

 Baadhi ya wafanyakazi waliokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) wakimsikiliza kwa makini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi,hayupo pichani, wakati wa kuwakaribisha katika Benki ya TPB 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc Sabasaba Moshingi,kushoto akisalimiana na wateja waliokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB)na kuwakaribisha rasmi.Hafla hio ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.


3,955 WAENDELEA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI - TASAF SHINYANGA

$
0
0
Jumla ya walengwa 3,955 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF wanaendelea kunufaika na mpango huo katika Manispaa ya Shinyanga.

Hayo yamebainishwa jana Agosti 9,2018 na Mratibu wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza na waandishi wa habari.

Kiwone alisema Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika manispaa ya Shinyanga ulianza kutekelezwa mwaka 2015 ukiwa na walengwa 4,244 ambao hata hivyo walipungua kutokana na wengine kufariki na wengine tuliwaondoa kwa kukosa sifa za kuwa kwenye mpango lakini mpaka sasa tuna walengwa 3,955,

"Tangu mwaka 2015 mpaka sasa tumepokea fedha za serikali jumla ya shilingi bilioni 3,fedha ambazo tumewapa walengwa ni shilingi bilioni 2.7 na tayari zimewafikia walengwa ambapo fedha hizi zinawasaidia kwa sababu wanapewa fedha kisha kufundishwa namna ya kutumia fedha hizo",alifafanua.
Mratibu wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza na waandishi wa habari.- Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

UPANDE WA MASHTAKA WAPEWA SIKU SABA KUKAMILISHA MCHAKATO KUBADILI HATI YA MASHTAKA KESI YA AKINA AVEVA, NYANGE

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa mashtaka kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo ili kesi dhidi ya washtakiwa Evans Aveva na Godfrey Nyange iweze kuendelea.

Amri hiyo, imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya Wakili wa Takukuru, Leonard Swai kueleza mahakamani hapo kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa Aveva na Nyange wapo mahakamani.

Amedai mara ya mwisho Mahakama ilitoa agizo la kuwaondoa Poppe na Lauwo katika hati ya mashtaka ili kesi iendelee kwa Aveva na Nyange.
Amedai utaratibu umefanyika na jalada limepelekwa kwa DPP na amejitahidi kulifuatilia hadi leo asubuhi na ametoka kwa DPP lakini hajaweza kulishughulikia, yupo nje ya Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo ameomba Mahakama wapewe wiki mbili kwa ajili ya kuhakikisha DPP analifanyia kazi hata kama atakuwa Dodoma watamfuata huko huko.Baada ya Hakimu Swai kueleza hayo, Aveva aliomba wapewe muda wa siku saba kwa sababu siku 14 ni nyingi na kuongeza kuwa upande wa mashtaka wanavyochelewesha jambo hilo wanawaumiza.

Pia Nyange ameongeza kuwa jambo hilo la kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa hao ni la muda wa zaidi ya miezi miwili wakati wanajua wapo mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kuendelea kukaa huko ni tatizo.Amesisitiza kuwa kuendelea kuwapatia upande wa mashtaka wiki mbili ni kama kuendelea kuwaficha Keko bila sababu za msingi.

Baada ya malalamiko hayo ya washtakiwa Hakimu Simba alimuuliza Wakili Swai unaona malalamiko ya washtakiwa hayana msingi. Swai akamjibu Hakimu Simba kuwa malalamiko yao yanamsingi mheshimiwa.Hakimu Simba unasemaje na afya ya mshtakiwa wa kwanza Aveva inaonekana ana kliniki kila wiki hivyo anawapa siku saba wakamilishe taratibu. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 17 mwaka 2018

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.

NZEGA MJI YAHAMISHA STENDI YA ZAMANI KUONDOKA MSONGAMANO KATIKATI YA MJI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT,TABORA

HALMASHAURI ya Mji Nzega imefanikiwa kuhamisha mabasi yote ya abiria ambayo yalikuwa yakitumia Stendi ya zamani katika upakiaji na ushushaji wa abiria kutoka mjini kwenda katika eneo la Sagara ambalo lina ukubwa wa ekari 10 kwa ajili kuondoa msongamano katikati ya Mji huo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Halmashauri hiyo kufanikiwa kuweka miundo mbinu yenye thamani ya milioni 277.7 ambayo imesaidia katika hatua za awali za ufunguzi wa Stendi hiyo mpya ambayo itatoa huduma kwa magari ya abiria yanayopitia Mkoani Tabora na yake kutoka Mkoani humo.

Kauli hiyo ilitolewa jana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa Stendi hiyo iliyopo kando kando ya barabara kuu ya kwenda Shinyanga na Singida na maeneo mengine .

Alisema kwa kuwa Nzega iko kwenye ni njia panda eneo la Stendi ya mabasi ya zamani lilikuwa dogo na kulifanya kushinwa kuhimili wingi wa mabasi yaliyokuwa yakitoka nje ya Nchi na yale ya mikoa mbalimbali ambayo yalikuwa yakipitia Nzega na kusababisha msongamano na karaha kwa wasafiri na watumiaji wengine wa barabara.

Magesa alisema baada ya kuona hawawezi kukamilisha kazi zote kwa wakati mmoja waliamua kutumia fedha hizo kidogo kuanza na hatua za awali za kujenga jengo la kupumzikia abiria, Kituo Kiodogo cha Polisi, vibanda sita(6) vya kukatia tiketi, vyoo na ofisi, vibanda vya askari , Mamlaka ya Usafirishaji Tanzania(SUMATRA) na kulipa fidia wananchi waliokuwa katika eneo ilipojengwa Stendi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kazi nyingine ilikuwa ni kujenga uzio wa nyaya kuzunguka eneo la stendi,vibanda vya askari wa usalama barabarani, wakusanyaji mapato ya Halmashauri, kuweka taa za mwanga wa jua katika Ofisi na kwa ajili ya kuimarisha usalama nyakati za usiku .
 Baadhi ya Wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea na shughuli zao jana  baada ya uzinduzi wa Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara kwenye Halmashauri ya Mji Nzega.
 Magari ya abiria kutoka sehemu mbalimbali yakipita katika Geti la Ukaguzi na malipo ya ushuru katika Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara kwenye Halmashauri ya Mji Nzega baada ya kuzinduliwa jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa (mbele waliosimama), Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula(wa pili waliosimama) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (wa tatu waliosimama) na abira wengine wakiwa katika gari la abiria ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara katika Halmashauri ya Mji Nzega jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mbele) akiwaongoza viongozi mbalimbali kutembelea Kibanda cha Ukaguzi wa Magari na kile cha Malipo ya Ushuru wakati wa uzinduzi wa Kituo Kipya cha Mabasi cha Sagara katika Halmashauri ya Mji Nzega jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa (katikati walio mbele) akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey (kulia walio mbele)mara baada ya uzinduzi jana wa Kituo Kipya ch Mabasi ya Abiria cha Sagara cha Halmashauri hiyo. Kushoto mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula.


UJUMBE WA SIERRA LEONE WATEMBELEA WIZARA YA FEDHA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Ufundi toka nchini Sierra Leone Dk. Turad Senesie (kulia) akiuliza swali kwa Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (hayupo pichani) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Ofisi za hazina na ujumbe wake ili kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kushoto ni Wajumbe aliombatana nao toka nchini Sierra Leone.
 Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (kulia) akifafanua jambo kwa ujumbe toka nchini Sierra Leone (hawapo pichani) uliokuja nchini kwa lengo la kujifunza namna ya uendeshaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Katikati ni Afisa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Omega Ngole na kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Godfrey Chawe.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha toka nchini Sierra Leone, Mathew Dingie (katikati) akiuliza swali kwa Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (hayupo pichani) wakati walipotembelea Ofisi za hazina ili kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Kushoto ni Wajumbe aliombatana nao toka nchini Sierra Leone. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Ufundi toka nchini Sierra Leone Dk. Turad Senesie.
 Afisa Msimamizi Mwandamizi wa Fedha toka Wizara ya Fedha,Alexander John (kushoto) akifafanua jambo kwa ujumbe toka nchini Sierra Leone uliokuja nchini kwa lengo la kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (kulia) akifafanua jambo kwa ujumbe toka nchini Sierra Leone uliokuja nchini kwa lengo la kujifunza namna Wizara ya Fedha inavyoweza kutoa fedha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.Picha na MAELEZO

 Kamishna Msaidizi wa Sera toka Wizara ya Fedha, Sauda Msemo (mwenye kilemba) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe toka nchini Sierra Leone uliokuja nchini kwa ziara ya kikazi ya kujifunza namna ya uendeshaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

NAMUNGO FC KUPAMBANA NA SIMBA YA JIJINI DSM

$
0
0

*Ni katika uzinduzi wa uwanja wa Halmashauri ya Ruangwa

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ruangwa kesho (Jumamosi, Agosti, 11, 2018) inatarajia kuzindua uwanja wake wa michezo, ambapo timu ya wilaya hiyo Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza itapambana na bingwa wa ligi kuu 2018/2019 Simba SC ya jiji Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Namungo FC ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini, imeupa heshima mkoa wa Lindi kwa kuwa ndiyo pekee inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa uwanja huo leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mbali na timu ya Simba pia timu hiyo inatarajia kucheza na timu za Yanga , Azam za jijini Dar es Salaam na Dodoma FC ya jijini Dodoma.Uwanja wa mpira wa miguu wa wilaya Ruangwa unaoitwa Majaliwa Stadium umejengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndio utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo FC kuchezea mechi za nyumbani.

“Lazima tuisapoti timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”Kadhalika Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa timu ya Namungo FC kucheza na timu kama za Simba, Yanga, Azam na Dodoma FC kwa sababu zinasaidia katika kuimarisha viwango vya wachezaji na kuwaondolea uoga wa kupambana na timu nyingine.

Kiingilio katika mechi ya Namungo FC na Simba SC ni sh. 3000. Tayari timu ya Simba imeshawasili wilayani Ruangwa leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018), saa 11.01 jioni kwa ajili ya mechi yake na timu ya Namungo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 (Picha na  Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akionesha jezi ya Namungo FC, baada ya kupokea jezi hizo zilizotolewa na wafadhili wa timu hiyo, Haojue Company Limited Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 Kushoto ni Mkurugenzi wa Haojue Brand Martin Francis. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 (Picha na  Ofisi ya Naziri Mkuu).
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images