Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110111 articles
Browse latest View live

MPINA APIGA MARUFUKU UKAMATAJI HOLALA WA MIFUGO

$
0
0
NA JOHN MAPEPELE, MOROGORO 

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku tabia ya ukamataji mifugo kiholela inayofanywa na baadhi ya watumishi wa umma na kusababisha mifugo mingi kufia mikononi mwa Serikali kwa kukosa huduma muhimu ikiwemo maji, malisho na matibabu na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla. 

Mpina amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali kuendesha operesheni za kukamata mifugo na kuifungia bila kuipatia huduma muhimu ikiwemo maji, malisho na matibabu na matokeo yake mifugo mingi hufa na kusisitiza kuwa operesheni hizo zinapofanyika ni lazima zihusishe pia maofisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuwa na uelewa wa pamoja wa jambo hilo. 

Aidha Mpina alisema utaratibu unaofanyika hivi sasa wa kukamata hovyo mifugo ni ukiukwaji wa sheria namba 17 ya Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003 na, Sheria ya Ustawi wa Wanyama Namba 19 ya Mwaka 2008 ambazo zinataka mifugo inapokamatwa kuzingatia masuala ya magonjwa na ustawi wa mifugo katika kipindi chote inapokuwa imeshikiliwa. 

Akifunga maonesho ya 25 ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro katika viwanja vya Mwalimu JK Nyerere mjini Morogoro kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Waziri Mpina pia alielezea kutoridhishwa na utoaji wa mikopo wa Benki ya Kilimo (TADB) ambapo kwa taarifa iliyotolewa sekta ya uvuvi hakuna mkopo wowote uliotolewa katika mwaka wa fedha uliopita huku upande wa sekta ya mifugo wakiambulia wajasiamali wanne tu . 


KAULI YA MBWANA SAMATA BAADA YA POLISI KUMSHAMBULIA MWANDISHI WA HABARI DAR

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKATI Watanzania mbalimbali wakitoa matamko ya kulaani kitendo cha Mwandishi wa habari wa Wapo Redio Silas Mbise kushambuliwa na Polisi katika mechi kati ya Simba na Asante Kotoko Siku ya Simba Day mchezaji wa kimataifa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’Mbwana Samata amesema kitendo hicho si cha kiungwana.

Samata ametoa kauli hiyo kutokana na kusambaa kwa video inayoonesha namna ambavyo mwandishi huyo akishambuliwa licha ya kujisamilisha.
Hivyo kutokana na video hiyo Samata kupita ukurasa wake wa Tweet ameelezea kusikitishwa na shambulio hilo.

Samata amesema hivi “Sio kitendo cha kiungwana askari kupiga mwandishi katika eneo la michezo , mpira ni mchezo unaoleta amani sio kuvunja amani.”.Wakati Samata akitoa kauli hiyo tayari leo mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linalaani vikali tukio hilo linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandishi huyo.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema tukio hilo limetokea Agosti 8 mwaka huu siku ya mechi kati ya Simba na Asante Kotoko ya nchini Ghana.Aidha amesema Polisi Kanda Maalum imeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha ya video hiyo inayosambaa na kuonesha askari polisi na mwandishi huyo wa habari ili kubaini ukweli.

Mambosasa amesema hiyo inakwenda sambasamba na kumtaka mtendewa wa kosa hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe na kwamba mtu yoyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.

NANGANGA-RUANGWA KUJENGWA KWA LAMI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni tano katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa yenye urefu wa kilomita 57 kwa kiwango cha lami.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 10, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Likunja wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.Waziri Mkuu amesemaSerikali imeendelea kuboresha huduma za jamii nchini kwa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo ya Nanganga-Ruangwa-Nachingwea hadi Masasi unatarajiwa kuanza hivi karibu, hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.Akizungumza kuhusu nyumba zilizowekewa alama ya X, Waziri Mkuu aliwataka wahusika wazibomoe wenyewe ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa walivamia eneo na watakaosubiri hadi Serikali iwabomelee watalazimika kuilipia gharama, hivyo ni vema wakatii.

Wakati Huo huo,Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo asilimia 95 ya vijiji vyote vya wilaya ya Ruangwa vinapata huduma hiyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wananchi wa kata hiyo kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.“Tumeendelea kuboresha huduma za jamii katika vijiji vyote vikiwemo na vya wilaya hii. mkakati wetu ni kuhakikisha wananchi wote mnapata maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yenu na tayari asilimia 95 ya vijiji vinapata maji,” amesema.

Kuhusu changamoto ya zahanati ya kijiji cha Likunja kutokuwa na nyumba ya mganga, Waziri Mkuu amewashauri wananchi hao wafyatue matofali na kisha waanze ujenzi wa boma na Halmashauri itawasidia kuwapa vifaa vya viwandani kama saruji, mabati na misumari.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAAA, AGOSTI 10, 2018.

Balozi wa Saudi Arabia akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
Mhe. Balozi Dkt.Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akisalimiana na Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania (kulia) walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam. Mazungumzo baina ya Viongozi wa Wizara na Balozi Mohamed yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Mataifa haya mawili (Tanzania na Saudi Arabia).

Aidha viongozi hao wamekubaliana kukamilisha maandalizi ya kongamano la biashara litakalo husisha wafanyabiashara na wadau wengine kutoka Saudi Arabia na Tanzania. Balozi Mohamed amebainisha kuwa ujumbe kutoka Saudi Arabia utakuwa na wafanyabiashara zaidi ya 40 wakiongozwa na Waziri wa Biashara wa Saudi Arabia.

Aidha Balozi Mohamed ameonesha nia yakuanzisha majadiliano kati ya Tanzania na Saudi Arabia ya kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Saudi Arabia kwa lengo la kukuza biashara baina ya nchi hizi mbili. 
Mhe. Balozi Dkt.Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Bw. Suleiman Saleh Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati (wa kwanza kulia) na Bw. Hangi Mgaka Afisa Mambo ya Nje (wa kwanza kushoto) 
Bw. Suleiman Saleh Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, akisalimiana na Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam 
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam 
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Ben Mansour Al Malek Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania (wa pili kulia) .

WANANCHI WA MONDULI WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
Wananchi wa Mto wa mbu na Makuyuni wilayani Monduli Mkoani Arusha wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kwa uboreshaji wa huduma za afya wilayani humo. Wananchi hao wametoa pongezi hizo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Waziri Jafo anakagua miradi ya maendeleo na kufanya ufuatiliaji wa maagizo yake aliyo yatoa miezi ya nyuma katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo kwasasa ametokea mikoa ya Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, na kigoma. Hatua ya ziara hiyo ilitokana hivi karibuni serikali imepeleka fedha katika kituo cha afya Mtowambu kiasi cha shilingi milioni 400 na baadae imepeleka fedha zingine shilingi milioni 400 katika kituo cha afya Makuyuni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. 

Katika ziara ya Waziri hiyo wilayani Monduli, Wananchi hao wameishukuru serikali na kwamba hatua hiyo itaboresha na kuwezesha huduma bora kutolewa kwenye vituo hivyo. Wamesema ukosefu wa vituo hivyo uliwafanya kukosa huduma za upasuaji. Kwa upande wake, Waziri Jafo amemshukuru aliyekuwa mbunge wa Monduli Julius Kalanga kwa kufikisha kero za wananchi wa Monduli katika Ofisi yake na serikali ikapeleka fedha hizo ili kuwasaidia wananchi hao ambao walikuwa wakitaabika miaka yote bila ya kuwa na vituo vya afya vinavyoweza kufanya huduma ya upasuaji. Jafo amewapongeza sana wananchi hao kwa kuungana na serikali na kufanikisha uboreshaji wa kituo cha afya mtowambu pamoja na juhudi za ujenzi zinazo endelea katika kituo cha afya Makuyuni. 

Aidha Waziri Jafo amewajulisha wananchi hao kwamba serikali itapeleka vifaa tiba vyote katika kituo cha afya Mtowambu ambacho tayari kimekamilika ili wananchi hao wapate kuonja matunda mazuri ya utekelezaji wa Ilani ya CCM. Katika ziara hiyo Jafo amewataka viongozi walio chini ya Ofisi yake kuanzia mikoani hadi wilayani wahakikishe wanajituma muda wote katika maeneo yao kwa lengo la kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa amembeba mtoto aliyeletwa Kliniki katika kituo cha afya Mto wa mbu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akisalimiana na wananchi wa mto wa mbu wilayani Monduli.
Wananchi wa mto wa mbu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
Viongozi wakiwa eneo la Makuyuni wakikagua ujenzi wa miundombinu ya kituo cha Afya Makuyuni.

JESHI LA POLISI LALAANI VIKALI TUKIO LA KUPIGWA MWANAHABARI WA KITUO CHA WAPO RADIO, SILAS MBISE

WAZIRI WA MADINI ANGELA KAIRUKI AWAPA ONYO WATOROSHAJI WA MADINI YA RUBY MUNDARARA LONGIDO

$
0
0
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya Vito ya Ruby katika Kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha kujitafakari upya na kuwa wakweli katika biashara hiyo ya madini.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kujionea shughuli za uchimbaji wa madini hayo ya vito pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili Waziri Kairuki alifanya pia mkutano mkubwa wa hadhara kijijini hapo. Akizungumza na wananchi hao wa Mundarara Waziri Kairuki aliwataka wananchi hao kushirikiana na Serikali katika kuwafichua watu wasiowaaminifu kwa rasilimali za taifa.

“Nyinyi wananchi na wafanyabiashara hapa mnawajua wanaotorosha madini kwenda nchi jirani, niwaombe muwafichue kwani madini hayo ni fedha mnazozihamishia nchi nyingine ambazo zingewaletea maendeleo nyinyi. “Tafadhaili sana kwa wafanyabiashara naowamba muache kuanzia sasa kwani mtajikuta mkiwa katika wakati mgumu wa kupteza mitaji yenu na hata kupoata hasara kubwa pindi mtakapokamatwa,” alisema Waziri Angela. “Kiama kikubwa kinakuja kwa watoroshaji wote wa madini sasa nimekuja hapa kuwaambia ole wao wanaowasaidia na wanaoshirikiana nao haoa mpo karibu na mpaka nawaomba mjiepushe na biashara hiyo haramu,” alisema. 

Kupitia ziara hiyo Waziri Kairuki alitumia fursa hiyo kuwataka wawekezaji kumaliza migogoro ya mitobozano inayowakabili ambapo pia alifanya ziara katika Mpaka wa Namanga kwa lengo la kujionea changamoto zinaawakabili wafanyakazi wa wizara hiyo. 
 
Waziri wa Madini Angela Kairuki akiangalia kwa makini mgodi wa madini ya Ruby wa Mundarara unaomilikiwa na mwekezaji Rahimu Mollel ambapo alifanya ziara hiyo kujionea shughuli za uchimbaji na kufahamu changamoto zinazowakabili.
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akiongoza msafara wa Waziri wa Madini Angela Kairuki aliyefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutembelea mgodi huo.
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akimuonyesha Waziri wa Madini kipande cha Ruby mara baada ya kuvunja jiwe gumu.
Waziri wa Madini Angela Kairuki akisoma Leseni ya uchimbaji ya kampuni ya Sendeu inayomilikiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani Longido Michael Laizer
Waziri wa Madini Angela Kairuki akihutubia wananchi na wachimbaji wadogo wa madini ya vito ya Ruby katika eneo la Kijiji cha Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha.
 

UJUMBE WA UAE WATEMBELEA MIRADI MBALI MBALI YA MAENDELEO MIKOA YA PEMBA

$
0
0
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Abdalla Mzeee ya Mkoani Mkoa wa Kusine Pemba Dk.Haji Mwita (kushoto) akifuatana na  Ujumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulipofika kutembelea Hospitali hiyo leo kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu
Mkurugenzi Idara ya Tiba  DK.Mohamed Dahoma alipokuwa akitoa maelezo kwa ujumbe wa timu ya wataalamu kutoka katika  Serikali ya Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) wakati ulipofika kutembelea katika Hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Nchi za UAE Mwanzoni kwa mwaka huu

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba Dk.Omar Issa(kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa ujumbe wa timu ya wataalamu kutoka katika  Serikali ya Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) wakati ulipofika kutembelea sehemu mbali mbali katika Hospitali ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Nchi za UAE Mwanzoni kwa mwaka huu
 Afisa Mdhamini katika Wizara ya Kazi,uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Pemba Nd,Khadija Khamis Rajab (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa Mshauri wa Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE)  Bibi Najla Al- Kaabi (katikati)akifuatana na ujumbe wa wataalamu kutoka Serikali ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) uliotembelea kaaika Ushirika wa Wajasiriamali wa Kikundi cha Upendo Group Wete Pemba 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd.Shomari Omar Shomari (wa pili kulia)pamoja na Viongozi wengine wakimsikiliza Nd.Ali Humaid Alderei(kushoto) kutoka Mfuko wa Maendeleo wa (Abudhabi Fund) katika Ujumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ulipofika kutembelea mradi wa Barabara ya Mkoani-Chakechake  Pemba leo kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyoifanya (UAE) mwanzoni mwa mwaka huu
Picha na Ikulu.


Serikali yakabidhi Pikipiki 27 kwa Maofisa Elimu Kata Halmashaauri ya Wilaya Mufindi.

$
0
0

Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekabidhi  Pikipiki ishirini na saba (27) aina ya Honda kwa Maofisa elimu kata  kutoka kata zote ishirini na saba (27)  za Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mkoani Iringa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri David William, amesema Pikipiki hizo zimefika kwa wakati muafaka ili kurahisisha jukumu la ufuatiliaji na usimamizi wa elimu katika Halmashauri.
“Mmepata usafiri huu ambao utachangia kutatua changamoto za kufanya kazi zenu hivyo, hatutaki kuona utoro unaendelea, hatutaki kuona mimba zinandelea hasa katika shule za sekondari, sasa hatuna sababu ni lazima tuhakikishe elimu inakua bora zaidi na ufaulu wetu kitaifa kama Halmashauri unapanda” alisema Mhe William.
Aidha, Mhe. William, ametoa wito kwa Maofisa elimu kata kuhakikisha wanazitunza Pikipiki hizo na kusisitiza kwamba usafiri huo sio kwa ajili ya kufanyia biashara ya bodaboda bali zifanye kazi iliyokusudiwa.
Pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Maafisa Elimu Kata Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William (kushoto)  akizindua pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Maafisa Elimu Kata. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina na anyefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Issaya Mbenje.  

JESHI LA POLISI LALAANI TUKIO LA KUPIGWA MWANAHABARI WA KITUO CHA WAPO RADIO, SILAS MBISE

KING MAJUTO ALIPOONGEA NA DANGA CHEE YA MICHUZI TV BAADA YA KURUDI HIJJA SEPTEMBA 2015

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

TRENI ZA PUGU, TRC RELI TV: UBUNGO NA ZILE ZA MIKOANI KUISHIA KAMATA, KUPISHA UJENZI WA KITUO CHA KISASA STESHENI

VOA Swahili: Duniani Leo Agosti 10, 2018

Jumia kunogesha sikukuu ya Eid kwa kutoa mbuzi bure kwa wateja

$
0
0
Dar es Salaam - Agosti 10, 2018. Waumini wa dini ya Kiislamu nchini na duniani kote wanatarajia kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha siku ya Jumanne ya tarehe 21 mwezi wa Agosti. Hata hivyo, hii ni tarehe inayokadiriwa kwa sababu siku rasmi inaweza kubadilika kutegemeana na kuonekana kwa mwezi wa Dhul Hijjah.

Eid Al Adha ni sikukuu ambayo husherehekewa na miongoni mwa Waislamu duniani kote katika kukumbuka sadaka aliyoitoa Nabii Ibrahim (AS) kutokana na imani aliyokuwa nayo kwa mwenyezi Mungu (SWT). Nabii Ibrahim alionyesha utayari wake wa kumtoa sadaka mwanaye wa pekee, Ismail, lakini baadaye Mungu alimtoa mwanakondoo ili awe mbadala wa sadaka. Mwenyezi Mungu alipendezwa sana na usikivu wa Ibrahim kwake na kuwataka Waislamu kukifanya kitendo hiki na imani iliyoonyeshwa kuwa sehemu ya maisha yao.

Hivyo basi, kila mwaka ifikapo siku ya 10 ya mwezi wa Dhul Hijjah, Waislamu wote duniani husherehekea sikukuu ya Eid Al Adha. Katika siku hii, Waislamu huchinja mwanakondoo, mbuzi, kondoo, ng’ombe au ngamia kuheshimu kitendo kilichofanywa na Ibrahim. Sherehe hii hutawaliwa na matendo ya ukarimu na shukrani.
Katika kunogesha shamrashamra za sikukuu hii ya Eid, Jumia Tanzania, kampuni inayojishughulisha na utoaji wa huduma za manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandaoni, imeamua kujumuika na wateja wake kwa kutoa mbuzi bure ili kufanikisha azma zao.

Mbuzi hao watatolewa kwa namna ya kipekee kabisa ambapo wateja watahitajika kutembelea tovuti ya Jumia ili kujishindia. Mbuzi watafichwa kwenye bidhaa tofauti zinazopatikana mtandaoni na mteja atakayefanikiwa kumtafuta mpaka akampata atakuwa ndiye mshindi halali. Washindi wote watapigiwa simu mara baada ya kushinda na kukabidhiwa hadharani.

Zoezi hilo litafanyika kwa kipindi cha wiki yote ijayo kuanzia Agosti 16 mpaka 20 ili kutoa fursa ya kuwakabidhi mbuzi wao na kuendelea na maandalizi ya sherehe za sikukuu ya Eid. Kwa kila siku ya shindano mteja mmoja ataweza kujishindia mbuzi mmoja aliyefichwa kwenye miongoni mwa bidhaa zilizomo kwenye mtandao wa Jumia. Vivyo hivyo kwa siku zitakazofuatia mpaka mwisho wa kampeni.
“Eid Al Adha au Eid ya kuchinja kama inavyofahamika na wengi pia ni sikukuu muhimu kwa ndugu zetu Waislamu. Tunafahamu kuwa sio watu wote wanao uwezo wa kununua mnyama wa kuchinja siku hiyo hivyo tumeona ni vema kutoa fursa kulifanikisha hilo,” alisema na kuhitimisha Afisa Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Hadijah Natalia Tuwano, “nawasihi wateja wetu kujaribu bahati yao kwa kucheza ili kushinda mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid. Fursa hii ni kwa wateja wote bila ya upendeleo wowote. Tunawatakia kila la kheri wote watakaoshiriki katika zoezi hili na ikiwezekana kuwaalika na wenzao, tunaamini litakuwa na manufaa kwao, familia, ndugu na jamaa zao.”

Sikukuu ya Eid Al Adha inalenga kumfanya Muislamu kutenda mema zaidi na kujipima na matendo yake. Haitakiwi kutoa sadaka pekee; bali inamaanisha kujifunza masomo yaliyojificha ndani yake ambayo ni kuwa huru dhidi ya matamanio ya kwa mbinafsi, na kumuinua Muislamu dhidi ya chochote kinachokwamisha uwezo wake wa kutekeleza majukumu yake kama Muislamu.

UCHAFU NI ADUI WA AFYA YAKO,YATUNZE MAZINGIRA YAKO YAKUTUNZE.

$
0
0
 Mfanyabiashara wa Matunda akiendelea na biashara yake huku pembeni kukiwa na mtaro wa maji machafu katika eneo la Mbagala jijini Dar as Salaam,jambo ambalo ni hatari kwa afya ya walaji.Wananchi wanaaswa kutunza mazingira yao na kuwa safi kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uchafu.
 Maandalizi ya biashara ndogondogo yakiendelea katika eneo la Mbagala jijini Dar as Salaam.
Maandalizi ya biashara ndogondogo yakiendelea katika eneo la Mbagala jijini Dar as Salaam. (Picha zote  na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAZINDUA USAFI KWA FUKWE ZA BAHARI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Wizara ya Maliasili na Utalii Nchini imezindua  rasmi kampeni ya kufanya usafi katika maeneo ya fukwe kwa ajili ya kuvutia utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na  Bodi ya Utalii nchini (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo pamoja na kufanya usafi kwenye Fukwe ya Hotel ya Ramada Resort, Mkurugenzi Msaidizi Leseni na Udhibiti Idara ya Utalii Rosada Msoma amesema kuwa utaratibu huu uliowekwa na Bodi ya Utalii Nchini ya kufanya usafi kutasaidia kuboresha na kuvutia watalii wengi zaidi.

Rosada ambaye ameshiriki kusafisha ufukwe wa Ramada Resort, amesema ana imani kampeni hiyo itakuwa endelevu kwani ni miongoni mwa mipango ya Serikali kuvutia utalii wa fukwe."Tutakapokuwa tunafanya usafi kwenye fukwe zetu,  zikiwa safi kiukweli zitavutia utalii na watalii wengi watakuja kutoka sehemu mbalimbali kwa wanaopenda matembezi lakini pia kwa wazawa ni fursa ya kufanya biashara,” amesema Rosada.

Rosada amesema kuwa, wao kama Wizara ya Maliasili zoezi la usafi walilizindua Mwezi April mwaka huu wakiwa na lengo la kuboresha maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kuvutia watalii nchini.Mkurugenzi wa masoko wa TTB, Ernest Mwamaja amesema fukwe nyingi hazipo katika hali ya usafi na uchafu wake kwa asilimia kubwa ni makopo ya plastiki yanayoletwa na maji yanayotiririka kutoka kwa wananchi sehemu mbalimbali wanaotupa kwenye vyanzo vya maji kama vile mito.
Mkurugenzi Msaidizi wa Leseni na Udhibiti Idara ya Utalii Rosada Msoma akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kufanya usafi katika fukwe za Bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.
 Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) Godfrey Meena akiwa sambamba na Kamishna msaidizi wa Polisi Makao Makuu Ferdinand Mtui wakishiriki usafi kafika fukwe za bahari kwa ajili ya kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli ya Ramada Resort Bharath Swarup akiwa anashiriki usafi  katika uzinduzi wa kampeni ya kufanya usafi katika fukwe za bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania ( TTB) na Hoteli ya Ramada Resort.


Wananchi na wafanyakazi mbalimbali wa Bodi ya Utalii na Hoteli ya Ramada Resort wakiendelea na usafi wakati wa uzinduzi wa kampenk ya kufanya usafi katika fukwe za Bahari kwa ajili ya kuvutia Utalii wa fukwe kwa  wazawa na wageni.

Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii (TTB) Ernest Mwamwaja  (katikatk) akiwa anafanya usafi wakati wa kampeni ya uzinduzi ya kufanya usafu katika fukwe za bahari  kwa ajili ya kuvutia utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni iliyoanzishwa na Bodi ya Utalii Nchini Tanzania (TTB) na Hoteli ya Ramada Resort. Picha ya chini akiwa anazungumza na wanahabari baada ya kumaliza usafi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
http://michuzijr.blogspot.com/2018/08/wizara-ya-maliasili-na-utalii-yazindua.html

TIRA:WANANCHI KATENI BIMA YA KILIMO

$
0
0
Na. Vero Ignatus Arusha.


Wito umetolewa kwa wananchi kukata Bima ya kilimo ili iwasaidie wakati wa majanga.

Meneja Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Kanda ya kaskazini Eliezer Rweikiza amesema kuwa mamlaka hiyo inatimiza azma ya serikali ya kuhakikisha kilimo kinasimama, kinachangia pato la Taifa, kunakua pamoja na kuwasaidia wananchi

Amesema Serikali inafanya jitihada nyingi kuhakikisha kilimo kinapata bima, hivyo kupitia ofisi ya Kamishna mkuu wa bima nchini hatua nyingi zimefanyika ikiwemo sera ya bima ya taifa inayozungumzia maswala ya kilimo kwa ujumla, sheria zilizotungwa kuielezea huduma hiyo.

Hivyo mwanachi asiwe na wasiwasi kuhusiana na bima hii kwani uhusika wetu kwenye makampuni yanayotoa Bima iwe ni ya kilimo, Afya, mali au ya maisha lazima tusadajili sisi na kujua utendaji wao, huduma wanazozitoa niyo sababu tupo karibu yao"Alisema Rweikiza.

Amesema Bima hiyo ipo mahususi kwa watu wanaojihusisha na kilimo ambayo inakinga majanga yanayotokana na shughuli za kilimo.'' Majanga haya yanatofautiana kutoka eneo moja kwenda nyingine, majanga ya mvua nyingi, mabadiliko ya hali ya hewa, mafuriko, tetemeko la ardhi, na majanga yanayohusiana na wizi shambani hivi vyote ukiwa na bima hii unaweza ukapata fidia. "alisema.

Wakwanza kushoto (mwenye miwani) Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akiwa watumishi wengine kutoka Mamlaka hiyo wakitoa elimu kwa wageni waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane Jijini Arusha. 
Mmoja wawaliotembelea banda la TIRA akiuliza swali kwa watumishi wa Mamlaka ya Bima nchini katika maonyesho ya nanenane Jijini Arusha. 

RISALA YA MWENYEKITI WA NEC KUHUSU UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI MDOGO

ULEGA AZIDI KUWAKUNA WAPIGA KURA WAKE,ACHANGIA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI MKURANGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Glogu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amechagia kiasi cha shilingi milioni 4.7 katika kata ya Nyamato, mifuko 250 ya Saruji kwaajili ya ujenzi wa vituo vya afya, shule na nyumba za Wauguzi hii ni katika kuhakikisha huduma za elimu na afya zinaimarika na kuwa faafu kwa wananchi wote wa Mkuranga.

Wakati huo huo Ulega pia ametoa amechangia shilingi laki sita kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Kimanzichana na ameahidi kutoa kiasi cha milioni 2 kwaajili ya vikundi vya wanawake wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa utoaji wa mchango huo Ulega ameeleza kuwa ushirikiano wa wananchi unampa nguvu ya kufanya makubwa zaidi katika kuleta maendeleo na amewataka watendaji kufuata kasi iliyopo na kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa juhudi anazoonesha katika kuleta maendeleo nchini.

Pia Ulega amesema kuwa yupo pamoja na wananchi wa Mkuranga wakati wote na katika kufanya kila jambo litakaloleta maendeleo bila kujali itikadi wala chama.Katibu wa CCM Wilaya ya Mkuranga, Abihudi Shila ameeleza kuwa wanachama waendelee kufanya kazi na viongozi waliopo na amempongeza Rais kwa juhudi anazozifanya katika kuleta maendeleo hasa katika kukemea rushwa na ufisadi pia katika ujenzi wa miradi ya kimaendeleo nchini kama miradi ya umeme na miundombinu.

Aidha amemshukuru Rais kwa kumteua Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah Ulega katika kumsaidia kuongoza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kama naibu Waziri na wanashukuru kuona mbunge wao anafanya kazi kwa dhati katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Aidha Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamato Idd Kimbapule amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdalah Ulega kwa kutoa kipaumbele katika huduma muhimu kama afya, elimu na miundombinu na ameendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha shughuli za ujasiriamali kwa akina mama zinakuwa ili waweze kujipatia kipato.

Kimbapule amewashauri wananchi kuonesha ushirikiano kwa viongozi wa mfano wa Ulega ambaye amejitoa katika kuwahudumia wananchi ili kuweza kujenga maendeleo kwa kasi zaidi. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega akizungumza na wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi mifuko 250 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya shule pamoja na nyumba za waganga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega  (kulia) akikabidhi Shilingi  laki sita kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kimanzichana ambapo  pia aliahidi kuongeza milioni mbili kwa ajili ya vikundi vya wajasiliamali.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega akiwakabidhi kadi za (CCM) wanachama  waliorudi wakitokea chama cha CUF  Abed Majala, Modesta Antoni katika kijiji cha Kimanzichana Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Viewing all 110111 articles
Browse latest View live




Latest Images