Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro aahidi na kuomba ushirikiano wa watumishi wote

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha 
 Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amewaahidi  watumishi wa halmashauri ya Meru kuwapa ushirikiano wa kuweza kutimiza majukumu yao ikiwa ni njia mojawapo ya kutoa  huduma bora kwa wananchi . 
 Hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi, watumishi wa halmashauri hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ambapo aliwahaidi kuwapa ushirikiano watumishi wote katika swala zima la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

"Napenda kuwatoa hofu watumishi wote kwa ujio wangu kwani nitawapa ushirikiano na kuwawezesha kutimiza majukumu yenu ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma bora ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi pamoja na rasilimali za Tanzania ili kuwanufaisha wananchi wote hasa wanyonge na watoto wa maskini, nukuu nimekuja hapa kutimiza torati na si kuivunja" alisema Mhe. Muro. 

Alisisitiza kuwa ushirikiano huo utaanza kwa kuwapa fursa watumishi hao kwa kueleza changamoto zao na kupokea mawazo,maoni na mikakati itakayoleta maendeleo kwenye halmashauri hiyo na Wilaya ya Arumeru. Alibainisha kuwa anatarajia kufanya kikao kingine Jumatatu Agosti 6 2018.

 Awali aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta akimkabidhi ofisi hiyo alisema kuwa watumishi wa Meru ni wazuri na wachapakazi na amemkabidhi pamoja na ofisi wakiwa weupe na wenye afya tele pia wanyeyekevu.
Mhe. Kimanta aliwawataka watumishi hao kumpa ushirikiano mkubwa mkuu huo mpya wa wilaya kama walivyompa yeye ili kuweza kuwaletea maendeleo wananchi wa meru na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Arumeru akiongea kabla ya kukabidhi ofisi kwa DC mpya Mhe. Jerry Muro.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru wakiwa kwenye kikao hico
Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akiongea kwenye kikao hicho

TULIA TRUST YAWAPA FURSA VIJANA YA KUSOMA NJE YA NCHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Taasisi ya Tulia Trust inayojihusisha na masuala ya Afya na Elimu nchini imeweza kuwasaidia watoto mbalimbali wanaoishi katika mazingira magumu na wengine kutoa fursa kwa vijana watano (5) kwenda kuendelea na elimu yao ya Sekondari Nchini Nigeria.

Tulia Trust ni shirika lisilo la kiserikali Trust lilianzishwa mwaka 2015 na Mheshimiwa. Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Tulia Trust Dotto Bernad Bwakeya ' Lameck Ditto" amesema kuwa katika kuchangia na kusaidia sekta ya Elimu Tulia Trust imetoa nafasi ya pekee kwa vijana watano (5) ambao watakwenda kuendelea na masomo ya sekondari Nchini Nigeria katika Taasisi ya Rochas Foundation College of Africa.

Ditto amesema Kupitia ziara mbalimbali za Dkt. Tulia katika Shule za Sekondari mkoani Mbeya alifanikiwa kukutana na kuunganishwa na vijana hao ambao wengi wao wanatoka katika hali duni kiuchumi, yatima na wengi wao wanalelewa na mzazi mmoja au ndugu. 

Amesema jitihada zilizofanywa na Tulia Trust ni kuhakikisha vijana hawa ambao kielimu wamekua wakifanya vizuri achilia mbali changamoto walizonazo kiuchumi na waliweza kufaulu vizuri mitihani ya darasa la saba ni kuwapatia msaada wa kielimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
 Balozi wa taasisi ya Tulia Trust, Dotto Bernad 'Ditto' akDitto'mza  na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar as Salaam, juu ya Taasisi ya Tulia Trust inavyolenga katika kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kutoa fursa kwa vijana watano  kwenda kusoma elimu ya  sekondari nchi ya Nigeria.(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Mlezi wa mtoto Anna Bernad, Mzee Lupyuto Mwamakula akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar as Salaam,ambapo ameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa kumpeleka kijana wake  kusoma nchi Nigeria.

WAZIRI MWIJAGE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MWANAHABARI SHADRACK SAGATI LEO MNAZI MMOJA JIJINI DAR

$
0
0
 Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles akitoa heshima za mwisho mbele ya sanduku lililobeba mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi kitengo cha Mawasiliano katika Wizara hiyo,Marehemu Shadrack Sagati wakati wa shughuli za kutoa heshima za mwizo,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja,Ilala jijini Dar.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitoa heshima za mwisho mbele ya sanduku lililobeba mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi kitengo cha Mawasiliano katika Wizara hiyo,Marehemu Shadrack Sagati wakati wa shughuli za kutoa heshima za mwizo,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja,Ilala jijini Dar
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu akitoa heshima za mwisho mbele ya sanduku lililobeba mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi kitengo cha Mawasiliano katika Wizara hiyo,Marehemu Shadrack Sagati wakati wa shughuli za kutoa heshima za mwizo,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja,Ilala jijini Dar
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akitoa heshima za mwisho mbele ya sanduku lililobeba mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi kitengo cha Mawasiliano katika Wizara hiyo,Marehemu Shadrack Sagati wakati wa shughuli za kutoa heshima za mwizo,zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja,Ilala jijini Dar

WASTARA AMSHUKURU RAIS DK. MAGUFULI

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Msanii wa Filamu nchini Bi.Wastara Juma (kulia) alipofika ofisini kwake leo jijini Dodoma kwa ajili ya kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Serikali kwa ujumla kwa michango waliyotoa kufanikisha matibabu yake yaliyofanyika nchini India katika hospitali ya Saifee.

Msanii wa Filamu nchini Bi.Wastara Juma (kulia) akitoa shukrani zake Kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe za kumshuruku Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa msaada aliyoutoa kwake kufanikisha matibabu yake ya mguu yaliyofanyika nchini India katika hospitali ya Saifee Februari mwaka huu ambapo alieleza kwa sasa afya yake imeimarika.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akiwa katika picha ya pamoja msanii wa filamu nchini Bi.Wastara Juma (katikati) alipofika ofisini leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Serikali kwa kumsaidia kufanikisha matibabu yake ya mguu yaliyofanyika nchini India, Februari mwaka huu katika hospitali ya Saifee kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bw.Francis Songoro.

BENKI YA TANZANIA YACHUKUA UDHAMINI WA BENKI M

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

JWTZ yatangaza nafasi za madaktari wa Binadamu

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa linauhitaji mkubwa madaktari katika taaluma mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza nafasi za ajira katika jeshi hilo, Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la JWTZ Kanali Ramadhan Dogoli amesema kuwa watanzania wenye sifa kuomba nafasi katika jeshi hilo .

Amesema nafasi za madaktari wa binadamu zinatolewa ili kuongeza idadi ya watalaam wa Tiba watakaotoa huduma za afya katika hospitali za jeshi, Vituo vya Afya na Zahanati kulingana na mahitaji ya sasa na siku zijazo.

Nafasi zinazohitajika ni Doctor of Medicine, Doctor of Dental Surgery, Bachelor of Pharmacy, BSC Health System Management, Bachelor in Labaratory Science, Bachelor of Science in Nursing, Bachelor of Science in Physiotherapy pamoja na bachelor of Science in Prosthetics and Orthotics.

Kanali Dogoli amesema kuwa sifa kati ya umri wa miaka 18-28, muombaji awe hajawahi kupatikana na hatia za kijinai mahakamani na kufungwa jela, kuhitimu pamoja na mafunzo ya vitendo na kutunikiwa vyeti na kusajiliwa na Bodi.

Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na jeshi hilo wafike katika kambi ya Jenarali Abdallah Twalipo Mgulani Agasti 28 kuanzia 1:00.
Waombaji watajigharamia Chakula, Usafiri

IGP AFANYA ZIARA CHUO CHA POLISI - DAR ES SALAAM POLICE ACADEMY (DPA)

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wakufunzi na Askari Wanafunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Chuoni hapo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Naibu Kamishna wa Polisi DCP Anthony Rutta
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana  na Wanafunzi wanaosomea ngazi ya Uofisa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Chuoni hapo
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana  na Wanafunzi wanaosomea ngazi ya Uofisa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) (Picha na Jeshi la Polisi).

Umeme wa Stiegler’s Gorge waiva

$
0
0
*Mawaziri, makatibu wakuu washuhudia kazi nzito 

NDOTO ya Rais Dk. John Magufuli ya kuifanya Tanzania inakuwa na uchumi wa kati na wa viwanda huenda ikatimia baada ya timu ya mawaziri na makatibu wakuu wa wizara 14 ambazo zinatekeleza mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge kuona kazi ya ujenzi wa umeme huo inavyokwenda kwa kasi.

Mradi huo wa umeme ambao ni mkubwa kwa historia ya Tanzania unatarajiwa kuzaliwa umeme wa megawati 2,115 ambazo zinatarajiwa kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Akitoa maelezo kwa kamati hiyo ya mawaziri na makatibu wakuu pamoja na watalaamu katika eneo la mradi huo, Meneja mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco- ETDCO, Mhandisi Elangwa Mgheni Abubakar, alisema kwa sasa kazi ya ujenzi inayoendelea na usimika waya maalumu zenye madini ya kopa kutoka katika kituo cha Matambwe hadi kwenye eneo la mradi.

Pamoja na hali hiyo alisema kutokana na ukubwa wa mradi huo wa kihistoria nguzo zitakazotumika kwa mara ya kwanza ni za zege zaidi ya 700. “Mradi mzima utakuwa na nguzo za zege 700 zenye urefu wa milimita 17. Na huu ni mradi wa kwanza kutumia nguzo za aina hii.

“Tunaendelea na ujenzi huu huku tukiwa tumezingatia masharti ya kitaalamu ikiwamo kukata miti bila kuathiri mazingira kutoka usawa wa ndege. Kwa sasa kazi inayoendelea mafundi wanalaza kebo ambayo itazunguka na kupita chini ya reli na daraja. Awamu ya pili itakuwa kama ya ujenzi pia tutaweka kebo. “Hii line itabeba 33 KV na ya pili nayo itakuwa na ukubwa kama huo ambayo ndani yake kuna waya wa kopa pamoja na nyaya zake ambazo ni nzito,” alisema Mhandisi Elangwa
Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Tanesco (ETDCO), Mhandisi Elangwa Mgheni Abubakar, akitoa maelezo kwa mawaziri na makatibu wakuu waliotembelea mradi wa ujenzi wa umeme wa Stiegler’s Gorge, ambao unatarajiwa kuzaliwa megawati 2,115 katika eneo la mradi Selou Mto Rufiji.
Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi ya Utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa umeme wa Stiegler’s Gorge, Justus Mtorela, alitoa maelezo kwa mawaziri na makatibu wakuu namna bwawa la umeme likavyojengwa kando ya Mto Rufiji
Mafundi wa Kampuni Tanzu ya Tanesco (ETDCO), wakiendelea na kazi ya usambazaji kebo chini ya ardhi kuelekea kwenye eneo la mitambo ya umeme wa Stiegler’s Gorge.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akifafanua jambo kwa mawaziri wenzake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akihoji kuhusu mradi huo kwa Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi ya Utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa umeme wa Stiegler’s Gorge, Justus Mtorela. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani.

IFM yamtunuku kitita cha fedha mwanafunzi bora wa mwaka 2017

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimempa zawadi ya fedha taslimu sh.milioni 2.2 muhitimu bora katika katika chuo hicho kwa mwaka 2017 Novath Mushi .

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo Mkuu wa Chuo cha IFM, Profesa Tadeo Satta amesema kuwa utoaji wa zawadi hiyo ni utaratibu wa vyuo vyote duniani ikiwa ni kuwatia moyo wanafunzi wengine kuweza kujituma katika ufaulu wa mitihani yao.

Profesa Satta amesema kuwa katika fedha hizo Chuo Kimetoa sh.milioni moja, Baraza la Chuo sh.milioni moja pamoja na mmoja walimu katoa sh.200,000.

Amesema kuwa mwanafunzi kufanya vizuri katika mitihani kunatokana na kujituma pamoja na nidhamu ambapo hata wanafunzi wengine wakifuata misingi hiyo wanaweza kufanya vizuri zaidi.

Nae Mhitimu wa Chuo cha IFM Novath Mushi amesema kuwa kwa zawadi aliopewa imetokana na juhudi za kujituma na kuwa nidhamu kwa kile anachokisomea.Mushi amesema kuwa alichagua kusomea uhasibu kutokana mporoko wa uchumi uliotokea 2007 na kuona anawajibu wa kuweza kutoa mchango huo kama unatokea wa uchumi .

Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji zawadi kwa mwanafunzi bora mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akimkabidhi Cheti mwanafunzi bora mwaka 2017 Novatt Mushi katika hafla iliyofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akiwa katika picha ya pamoj na baadhi ya wakuu watendaji wa chuo hicho katika  utaoaji wa zawadi kwa mwanafunzi boara Novath Mushi katika hafla iliyofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akimkabidhi zawadi fedha tasilimu sh.milioni 2.2 mwanafunzi bora mwaka 2017 Novatt Mushi katika hafla iliyofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam .

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AKAGUA SHAMBA LA MAHINDI GEREZA KUU, ARUSHA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia zao la mahindi katika shamba la mradi wa Kilimo Gereza Kuu Arusha leo Agosti 3, 2018 alipotembelea gereza hilo katika ziara yake ya kikazi. Shamba hilo linaukubwa wa hekari 150 na limelimwa katika msimu wa Kilimo mwaka 2017/2018. Matarajio ya mavuno ni zaidi ya gunia 2,500 yenye ujazo wa kilo 90(kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto) akikagua shamba la mradi wa Kilimo Gereza Kuu Arusha leo Agosti 3, 2018 kama inavyoonekana katika picha.
Bwana Shamba wa Gereza Kuu Arusha, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Ayub Mahai(wa pili toka kulia) akitoa maelezo ya kitaalam mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini kuhusiana na uzalishaji wa zao hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NSSF YAPELEKA ELIMU KWA WAKULIMA SIMIYU

$
0
0

Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Omary Mgumba akisikiliza maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa NSSF kwenye maonyesho ya Nanenae Simiyu.


NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), inashiriki katika maonyesho ya Nanenae yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo, alisema kuwa kauli mbiu ya maonyesho ya Nanenane mwaka 2018 ni 'Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda.

Katika maonyesho ya Nanenane Mkoani Simiyu, NSSF inatoa huduma mbalimbali zikiwemo elimu kwa umma juu ya Wakulima Scheme. Lengo la Wakulima Scheme ni kutoa mafao yote yanayotolewa na NSSF kwa wanachama walio katika sekta ya kilimo.

Kwa kujiunga na NSSF wakulima na familia zao wanaweza pata matibabu ya bure, pia NSSF inawawezesha kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kununulia pembejeo, kusomesha watoto wao na kufanya shughuli zingine za kimaendelo.

Huduma zingine zinazotolewa katika banda la NSSF ni pamoja na elimu ya mafao na umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa watu walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kuadikisha wanachama wapya, kutoa taarifa za michango ya wanachama na maelezo juu ya miradi ya nyumba zinazouzwa na Shirika, viwanja na majengo ya kupangisha.

NSSF inawakaribisha wakazi wote wa Simiyu na maeneo ya jirani wafike katika banda la NSSF lililopo pembeni ya mabanda ya Benki ya NMB na NBC ili waweze kupata huduma za NSSF kwa ajili ya kuboresha maisha ya sasa na baadae.
Afisa wa NSSF Hamisi Duma akitoa maelezo kwa wakina mama waliotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.

Afisa wa NSSF Hamisi Duma akitoa maelezo kwa wakina mama waliotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenae Mkoani Simiyu.

UNZIP TANZANIA: We are Back!!!

kibali cha DPP chasubiriwa Kesi ya kina Aveva

$
0
0
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kugushi na utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wameshafanyia marekebisho hati ya mashtaka ya kesi hiyo na kwa sasa wanasubiria kibali cha DPP ili iweze kuendelea.

Wakili wa Serikali Shadrack Kimaro, ameeleza hayo leo, Agosti 3.2018 Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja  kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (PH).

Wakili Kimalo ameeleza kuwa, tayari wameshatimiza amri ya mahakama ya kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaondoa watuhumiwa wawili waliotakiwa kuondolewa ili kesi ya msingi iweze kuendelea.

Aliongeza kuwa, kwa kuwa hati hiyo mpya ya mashtaka inatakiwa kupata kibali cha DPP ili Mahakama ya Kisutu iweze kuendelea wameirudisha kwake kwa ajili ya kupata kibali hicho na kuongeza kuwa kwa sasa DPP hayupo hivyo wanaiomba mahakama itoe ahirisho fupi kwa ajili ya kusubiria kibali hicho.

Naye Wakili wa Utetezi Nehemiah Nkoko amedai kuwa ni kweli amefuatilia na kubaini kuwa PH ipo tayari lakini kinasubiriwa kibali hicho ili washtakiwa hao wasomewe mashtaka mapya.

Aidha ameunga mkono ombi la kuahirisha kesi hiyo lililotolewa na upande wa mashtaka kutokana na kukosekana kwa kibali hicho.

Hakimu Simba amemtaka upande wa mashtaka kufuatilia kibali hicho kwa DPP kipatikane haraka kwani kesi hiyo imekwisha kaa muda mrefu.

Kesi hiyo sasa itatajwa Agosti 10.2018

Aveva anashtakiwa pamoja na Makamu wake Godfrey Nyange Kaburu. 

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi,  kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.  

KATIBU MKUU HAZINA, DOTO JAMES AWANYOOSHEA KIDOLE TRA

$
0
0
Benny Mwaipaja, MOFP, Dar es Salaam

KATIBU MKUU wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amewaonya watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA wanaojihusisha na vitendo vya ukosefu wa maadili vinavyochangia kuikosesha serikali mapato yake yatokanayo na kodi, vikiwemo vitendo vya rushwa, kwamba watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.

Bw. James, ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha kikao maalum kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango, Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Menejimenti pamoja na Mameneja wa Mikoa yote ya Tanzania Bara wa Mamlaka hiyo.

Amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo ikiwemo vitisho kwa wafanyabiashara wakati wa kukusanya kodi havikubaliki na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kukabiliana navyo kwa nguvu zote.Tayari wafanyakazi kadhaa wa Mamlaka hiyo wamefukuzwa kazi huku wengine wakihamishwa vituo vyao vya kazi kutokana na mwenendo wao usioridhisha na kulalamikiwa kutofuata maadili yao ya kazi wakati wanatekeleza majukumu yao.

Katibu Mkuu huyo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kuhakikisha kuwa inafikia malengo ya kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 18 katika mwaka huu wa Fedha wa 2018/2019, ikiwa ni sehemu ya Bajeti ya shilingi trilioni 32.47, iliyopitishwa na Bunge ili kutekeleza majukumu mbalimbali ya Serikali ikiwemo miradi ya maendeleo.

Kwa Upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Bw. Adolf Ndunguru, amesema kuwa Mamlaka yake imefanyakazi kubwa ya kuongeza makusanyo ya kodi kutoka wastani wa shilingi bilioni 800 hadi kufikia shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi.

Bw. Ndunguru amebainisha kuwa mafanikio mengine ni pamoja na kuongeza idadi ya walipakodi ikiwemo kuwasajili na kuwarasimisha wafanyabiashara ndogondogo walioko katika sekta isiyo rasmi ili waweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.

Ametaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Mamlaka yake kuwa ni upungufu wa wafanyakazi, vitendeakazi yakiwemo magari, matumizi madogo ya mashine za EFD na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo kukwepa kodi, jambo ambalo amesema wameanza kulikabili na hatua zake zimeanza kuzaa matunda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini-TRA, kuweka mikakati ya namna Mamlaka hiyo inavyoweza kufanikisha ukusanyaji wa shilingi trilioni 18 ambazo Serikali imeipangia kukusanya katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi, (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Uhusiano wa Sekta Binafsi na Serikali (PPP), Dkt. John Mboya, wakifuatilia mkutano kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Francis Mwakapalila (kushoto) na Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama ya Kitaifa, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, wakiwa katika Mkutano maalum kati ya Manejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA-kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, uliofanyika Jijini Dar es Salaam uliojadili fursa na changamoto za kufikia malengo waliyopangiwa TRA ya ukusanyaji kodi, Shilingi trilioni 18, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Kaimu Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Mgonya Benedicto (kulia), akiwa katika Mkutano maalum kati ya Manejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA-kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, uliofanyika Jijini Dar es Salaam, uliojadili fursa na changamoto za kufikia malengo waliyopangiwa TRA ya ukusanyaji kodi, Shilingi trilioni 18, katika Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, mkoa wa Kilimanjaro, Bw. MMsafiri Mbibo, akichangia hoja wakati wa kikao maalum kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kuweka mikakati ya namna Mamlaka hiyo inavyoweza kufanikisha ukusanyaji wa shilingi trilioni 18 ambazo Serikali imeipangia kukusanya katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

WANAWAKE KUNUFAIKA NA HUDUMA YA HEDHI SALAMA KIMTANDAO

$
0
0
     Na Khadija Seif,Globu ya jamii

Washiriki wanaowania taji la Ulimbwende kwa mkoa wa Dar es salaam, wametakiwa kuzungumza na wanawake hasa wasichana wadogo na kusambaza elimu kuhusu hedhi salama ili kupunguza na kutokomeza mimba za utotoni na zisizotarajiwa pamoja na matatzo ya afya ya uzazi kwa ujumla
Hayo yamebainishwa leo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries Flora Njelekel,alipokuwa akizungumza na warembo mbalimbali kuhusu Afya ya uzazi pamoja na hedhi salama.
Njelekela Alisema kuwa kwani wasichana wengi wamekua wakipitia changamoto ya kupata maumivu makali pindi wanapoingia kwenye hedhi zao.

"Nimekutana na walimbwende na kuwapa machache kuhusu huduma ya hedhi salama itakayowafikia wahitaji kwa njia ya mtandao, ambayo itawasaidia wanawake kujua mzunguko wao wa hedhi na afya kuhusu hedhi salama,kuepuka mimba zisizotarajiwa na pia itawapa fursa kuongea na mdaktari kuhusu afya ya uzazi",alisema Njelekela.
Alisema kuwa huduma hiyo itawasaidia wanawake kufanya vipimo vya hedhi pamoja vipimo vingine vya saratani ya matiti .
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries, Flora Njelekela akifafanua kuhusu namna ya kujifunza mambo mbalimbali ya afya kwa njia ya mtandao.Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries,Flora Njelekela akifafanua jambo mbele ua Warembo mbalimbali leo jijini Dar as Salaam kuhusu afaya ya uzazi pamoja na hedhi salama,pichani kulia ni Mkurugenzi Msaidizi,Carolyne Njung’e.Mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi ya Anuflo Industries, Flora Njelekela akiwa katika picha na warembo leo jijini Dar as Salaam.picha ya pamoja

UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi.

MRADI wa Kiwanda cha kutengeneza Viatu cha Karanga Leather Industries Co.Ltd upo katika hatua ya mwisho kukamilika baada ya kufanyika maboresho katika ufungaji wa mitambo mipya ya kukata na kushona ngozi pamoja na mfumo wa umeme katika kiwanda hicho.

Kampuni inayosimamia Kiwanda cha kutengeneza Viatu cha Karanga -Moshi, ilianzishwa Mei 30 mwaka jana kwa ubia kati ya uliokuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii PPF na Jeshi la Magereza ,ambapo awali kilikuwa kikizalisha jozi 150 kwa siku.

Baada ya Maboresho kukamilika kiwanda hicho sasa kitaweza kuzalisha Jozi 400 kwa siku na kutokana na sasa kuweza kuweka soli za viatu,kushona ngozi na kazi nyingine.Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini ,Phaustine Kasike pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Onesmo Buswelu wametembelea Kiwanda hicho kujionea maboresho hayo ambayo yanakadiliwa kufikia kiasi cha Sh Bil 2.7 katika uwekezaji wa Mitambo na kuoneshwa kuridhishwa.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea Kiwanda hicho,kamishna Jenerali Kasike amesema ujenzi wa miradi hiyo miwili pamoja na utekelezaji wa agizo la Rais kuwa na Tanzania ya Viwanda ,lakini pia itaongeza ajira na kuwawezesha wafungwa kuwa na ujuzi ambao watautumia kuajiri na kujiajiri baada ya kutukimikia kifngo.
Kamishana Jenerali wa Magereza,Phaustine Kasike pamoja na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Onesmo Buswelu (mwenye suti katikati) wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kiwanda cha Viatu-Karanga,Ezron Nganoga.
Kamisha Jenerali wa Magereza akitizama bidhaa za viatu ambazo zilinazalishwa katika kiwanda cha Viatu cha Karanga kinachomilikiwa kwa ubia kati ya uliokuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF) na Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza ,akiizama bidhaa mbalimbali za Viatu zinazozalishwa na kiwanda hicho.

WAZIRI ISACK KAMWELWE AKAGUA KIWANJA CHA NDEGE CHA MOSHI

$
0
0
Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) mkoa wa Kilimanjaro Bw. Julius Mlungwana (kulia), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto), hati ya kiwanja cha Ndege cha Moshi wakati alipokuwa akikagua kiwanja hicho, mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) mkoa wa Kilimanjaro Bw. Julius Mlungwana (kulia), wakati akikagua Kiwanja cha Ndege cha Moshi, mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua barabara ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua barabara ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya kuruka na kutua ndege na jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Moshi. Kiwanja hicho kimetengewa kiasi cha Shilingi bilioni moja kwa ajili ya matengenezo ya awali.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA KUWAIT-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya Kuwait katika sekta mbalimbali ikiwemo ya usafiri wa anga.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 3, 2018) wakati alipokutana na Balozi wa Kuwait nchini, Balozi Jasem Al Najemkatikamakazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Balozi Al Najem ambaye anamaliza muda wake, amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga na kwamba leo anatarajia kuondoka nchini na kurejea Kuwait.Waziri Mkuu amemshukuru balozi huyo kwa ushirikiano alioutoa Tanzania katika kipindi chote cha uwakilishi wake na kwamba nchi hizo zinatarajia kuanza ushirikiano katika usafiri wa anga.

Amesema Kuwait ni moja kati ya nchi rafiki, ambayo imeshirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa shughuli za maendeleo kupitia Balozi Najem, hivyo wataendelea kumkumbuka.“Balozi Najem amejitoa sana katika kuwasaidia Watanzania hususan kwenye miradi ya huduma za jamii kwa kupeleka maji mashuleni, vituo vya afya, zahanati na hospitalini,”.

“Pia Ubalozi wa Kuwait umesaidia kuleta vifaa tiba katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na madaktari katika baadhi ya hospitali nchini. Ushirikiano huu umeleta tija sana,” amesema.Waziri Mkuu amesema mbali na miradi hiyo ya huduma za jamii, pia balozi huyo ameshiriki kuendeleza Sekta ya utalii nchini kwa kuleta watalii wengi kutoka nchini Kuwait kuja Tanzania.

Waziri Mkuu meongeza kuwa Balozi Al Najem ameshiriki kikamilifu katika kuratibu shugughuli zote za maendeleo kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuunganisha sekta binafsi.Kadhalika, Waziri Mkuu amemuhakikisha balozi huyo kwamba Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Kuwait na kwamba ipo tayari kumpokea mwakilishi mwingine.

Kwa upande wake, Balozi Al Najem ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyompa katika kipindi chote alichokuwa akiiwakisha Serikali ya Kuwait nchini.Amesema tangu alipowasili nchini amekuwa akipewa ushirikiano mkubwa na viongozi wote wa Serikali jambo lililomrahisishia utekelezaji wa majukumu yake nchini.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mazungumzo na Balazi wa Kuweit Mh Jasem Ibrahim AI Najem ,ambaye amemaliza muda wake .Balozi Jasem. amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga leo Julai 3/2018 Jijini Dar es salaam

WAZIRI MHAGAMA AMKARIBISHA RASMI KATIBU MKUU MPYA OFISI YA WAZIRI MKUU

$
0
0
Na Jonas Kamaleki-MAELEZO, Dodoma

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Andrew Massawe kusimamia ipasavyo mifuko mipya ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha michango ya watumishi inakusanywa.

Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kumpokea Katibu Mkuu huyo aliyeteuliwa hivi karibuni.“Katibu Mkuu nakuagiza uhakikishe michango inakusanywa na malipo yanalipwa kwa wakati ili kuondoa changamoto kwa wanufaika ikiwemo wastaafu”, alisema Mhagama.

Waziri Mhagama amemtaka Katibu Mkuu kusimamia vizuri uwekezaji uliofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii kabla ya kuunganishwa. Ametaja uwekezaji huo kuwa ni kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Magereza cha Karanga, Moshi, kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari cha Mkulazi.

Aidha, Waziri Mhagama amesema kiwanda cha sukari kitaongeza ajira hasa kwa vijana na kuongeza fedha za kigeni kwani uagizaji wa sukari toka nje utapungua.Kiwanda hicho kinatarajia kuzalisha tani 250 kwa mwaka, ambazo zikiunganishwa na uzalishaji wa viwanda vingine vya sukari nchini zitaondoa uhaba wa bidhaa hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu wa ofisi hiyo baada ya kumkaribisha rasmi ofisini hapo Agosti 3, 2018. (Katikati) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vina na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka ofisi hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha Katibu Mkuu Mpya wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe alipowasili ofisini hapo Agosti 3, 2018 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa ofisi hiyo mara baada ya kukaribishwa rasmi ofisini hapo Agosti 3, 2018 Jijini Dodoma.

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images