Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

AZAM TV: WAKUU WA WILAYA WAPYA ZA LONGIDO NA ARUMERU WALIPOKULA KIAPO


RC MAKONDA ATAKA MALI ZA UMMA ZILIZOTAIFISHWA NA WAJANJA KUREJESHWA MARA MOJA

$
0
0



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Kuunda Timu ya kufanya ukaguzi wa Mali zote za serikali zilizotaifishwa na wajanja ikiwemo maeneo ya wazi, Nyumba za umma na kubainisha mikataba yote mibovu inayoinyonya serikali. 

RC Makonda ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya kuwakaribisha wakuu wapya wa wilaya za Kinondoni na Kigamboni, Katibu Tawala Mkoa na kuwaaga wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ambapo amemuagiza katibu tawala kuhakikisha anakamilisha ripoti kabla ya September 03 mwaka huu. 
Aidha RC Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo suala la ukusanyaji wa mapato na kuangalia chanzo kilichopelekea Mkoa huo kutofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza.
Pamoja na hayo RC Makonda amemtaka katibu tawala kupanga safu mpya ya utendaji kazi ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi ambapo ametaka kuanza na idara ya ardhi, Biashara, Usafi, Mapato na michez* ambazo bado hazijamridhisha kiutendaji kazi.
Hata hivyo RC Makonda amewasihi viongozi walioteuliwa kuchapa kazi ili kuenda sambamba na kasi ya Rais Dkt.John Magufuli aliewaamini na kuwateua.

RC ALLY HAPI AMSHUKURU RAIS MAGUFULI, AWAAGA WANAKINONDONI

WAKAZI WA VIJIJI VYA MTONGWE NA MITEMA MTWARA WALILIA DARAJA

$
0
0
Wakazi wa vijiji vya Mtongwele na Mitema katika Halmashauri ya wilaya ya Newala Mkoani Mtwara wameiomba serikali kufanya jitihada kujenga daraja katika mto huo ili kuweza kuunganisha mawasiliano ya barabara na kuondokana na adha wanayoipata kwa sasa. Wanasema unalazimika kukunja nguo pindi wanapohitaji kuvuka mto huo kuelekea upande wa pili ambapo maji huwafikia hadi kiunoni huku wakihofia  maisha yao.

JOKATE MWEGELO NA ZAINABU KAWAWA WAAPISHWA PWANI NA KUKUTANA NA MAAGIZO 16 KUTOKA KWA RC NDIKILO

$
0
0


Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amewaapisha wakuu wa wilaya wapya wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na Zainab Kawawa wilaya ya Bagamoyo na kutoa maagizo 16 kwa wakuu wa wilaya zote ili kutekeleza majukumu yao. Agizo kubwa ni kuhakikisha kila mkuu wa wilaya anasimamia mapato na kufikia asilimia zaidi ya 25 ifikapo septemba mwaka huu.
Pamoja na hilo ,Ndikilo  amewataka wamiliki wa makampuni kuhakikisha wanakata namba za utambulisho wa biashara TIN ndani ya mkoa badala ya kukatiwa Dar es Salaam kama baadhi yao yanavyofanya na kusababisha kuunyima mkoa mapato. Hafla ya kuwaapisha wakuu hao wa wilaya ilifanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa vilivyopo wilayani Kibaha.
Ndikilo alisema wakuu wa wilaya wanapaswa kufanyia kazi suala la makusanyo na kutoa rai kushirikiana na halmashauri kufikia si chini ya asilimia 25. Alitoa rai kwa wakuu hao wa wilaya, kudhibiti na kusimamia vyanzo vya mapato ya ndani ikiwemo mchanga na kokoto ili kujua vinaingiza mapato kwa kiasi gani.
"Kuhusu taarifa ya mkaguzi mkuu wa serikali CAG halmashauri zote za mkoa zimepata hati safi lakini msibweteke simamieni sekta zote ili tuendelee kupata hati hizo.
Alimtaka Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,kudhibiti magendo kwenye bandari bubu ambapo kwa Bagamoyo ziko 19 ambazo zinainyima serikali mapato na bidhaa hizo zinaweka rehani maisha ya wananchi kwani hazikaguliwi. Aidha alitaka Jokate na Zainab kwenda kuuliza kwenye maeneo yao kama kuna kamati za amani na endapo hakuna waunde kamati hizo.
“Hakikisheni mnadhibiti migogoro ya ardhi, wakulima na wafugaji kwani kwa mkoa wa Pwani damu iliwahi kumwagika kwenye wilaya za Bagamoyo, Kisarawe, Rufiji na Chalinze "
Ndikilo aliomba nguvu iongezwe ili kuepuka adha hiyo kwa wakati mwingine.

Alisisitiza utunzaji wa hifadhi ya misitu na kuilinda ili isivamiwe na kukabili uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kukata mkaa,kuni na mbao.
Katika hilo ,alimuasa Jokate na Zainabu kwenda kusimamia hifadhi ya misitu mikubwa ya Kazimzumbwi -Kisarawe na Uzigua na Ruvu Kusini na Kaskazini-Bagamoyo.
“Nasisitiza maelewano baina ya viongozi wa ngazi mbalimbali kwani baadhi yao hawaelewani hili ni tatizo ambalo halipaswi kuendelea kwani wanaoumia ni wananchi ambao wanapaswa kuongozwa,” alisema Ndikilo.
Kuhusu sekta ya maji ,alimuagiza mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate kumsimamia mkandarasi wa maji kutoka Mloganzila kwenda Kisarawe ili akamilishe kazi kwa wakati .
Ndikilo alisema tatizo la maji ni kubwa wilayani humo hivyo ahakikishe anakuwa mstari wa mbele kushirikiana na mkoa kuusukuma mradi huo ukamilike ili kumtua ndoo mama kichwani.
Kwa upande wao, Jokate Mwegelo na Zainab Kawawa walisema wamepokea maagizo yote na watayafanyia kazi. Jokate alieleza ,hatomuangusha mh.Rais,na wananchi wa Kisarawe na kudai hajaenda kutengua tolati bali amekwenda kuitimirisha,na kuwaomba wote wakutane kazini.





Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo alipokuwa akiapishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,katika viwanja vya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa alipokuwa akiapishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,katika viwanja vya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa. (picha na Mwamvua Mwinyi).

Balozi Seif Ali Iddi akutana na Timu ya Madakatari wa Brazil

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo haja ya kuendelezwa kwa kamisheni ya pamoja kati ya Tanzania na Brazil itakayoratibu mashirikiano ya Kidiplomasia katika Nyanja za Kiuchumi, Historia na Maendeleo ikilenga kuimarisha ustawi wa wananchi wa pande hizo mbili.
Alisema Tanzania na Brazil zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu katika masuala ya Utamaduni na Biashara unaopaswa kuendelezwa  kwa kuzingatia  kwamba ni Mataifa yanayofafana Kimaendeleo katika harakazi zao za kujiimarisha Kiuchumi.
Akizungumza na timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC  Ofisini kwake Vuga, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Kamisheni ya pamoja kati ya pande hizo mbili ipo lakini kinachohitajika kwa sasa ni ufuatiliaji wa malengo iliyoazimiwa kuyatekeleza.
Balozi Seif alisema Zanzibar kwa upande wake inaweza kufaidika  na mpango huo kwa kujikita zaidi katika kufungua milango ya ushirikiano na Nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kwenye Sekta za Biashara, Taaluma katika masuala ya kukabiliana na Maafa pamoja na huduma za Afya.
Aliueleza ujumbe huo wa timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC likiongozwa na Bw. Fabio Webber Tagliari  kwamba  Zanzibar hivi sasa inaendelea kuimarisha Sekta ya Afya kwa kuvijengea uwezo zaidi vitengo vinavyosimamia huduma za  Afya ya Mama na Mtoto.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC  Ofisini kwake Vuga.
 Kiongozi wa timu ya Wataalamu wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil-ABC Bw. Fabio Webber Tagliari kulia akiagana na Balozi Seif  mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Vuga Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akibadilishana mawazo na Balozi Mteule wa Brazil anayetarajiwa kufanya kazi zake  Zanzibar mara baada ya kukamilisha  kwa taratibu za Kidiplomasia.
Afisa wa Mahusiano ya Kimataifa wa ABD Bibi Layana Coasle Alves Kulia akibadilishana mawazo na Balozi Seif  mara baara ya kumaliza mazungumzo yao Ofisini  kwake Vuga.

              


BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 03/08/2018

LAMUNA MOO AACHIA NGARINGARI NA ATAMBA KUWAKILISHA VYEMA MKOA WA MOROGORO


RC WA IRINGA ALLY HAPI AMSHUKURU RAIS MAGUFULI, AWAAGA WANA-KINONDONI

MPIGIE KURA MDAU SUNDAY SHOMARI WA VOICE OF AMERICA ATUSHINDIE TUZO

$
0
0
Shime shime wananchi na tumpigie kura mtangazaji mahiri wa Kitanzania anayefanyia kazi Voice of America (VOA) Swahili jijini Washington DC nchini Marekani Sunday Shomari ashinde tuzo ya kimataifa ya Best Talk Show. Baada ya KUBOFYA HAPA angalia majina upande wa kulia, la chini mstari wa kwanza kulia utaliona jina la Sunday Shomari. Weka alama kwenye kitone cha duara pembeni yake kisha bofya VOTE. Ni rahisi sana. 

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA EXIMBANK YA INDONESIA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) na Ujumbe wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Benki ya Kibiashara ya Exim Bank ya Nchini Indonesia (kulia pichani) katika ukumbi wa Hoteli ya Borobudur iliyopo katika Mjini Jakarta jana, wakiwa katika ziara ya Kikazi nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) alipokuwa akiuliza Suala akiwa na Ujumbe wakati wa mazungumzo na Uongozi wa Benki ya Kibiashara ya Exim Bank ya Nchini Indonesia (hawapo pichani) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Borobudur iliyopo katika Mjini Jakarta jana, katika ziara ya Kikazi nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla,wengine (kushoto) Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe.Amina Salum Ali,Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais na Mwenyejkiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Isaa Haji Ussi Gavu (kulia) na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Malaysia pia akiiwakilisha Indinesia Mhe.Balozi Ramadhan Kitwana Dau,
Mkurugenzi Mtendaji wa Eximbank ya Indonesia Nd,Dwi Wahyudi (katikatri) alipokuwa akijibu masuala yaliyoulizwa wakati wa kikao cha pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (hawapo pichani) jana katika Hoteli ya Borobudur iliyopo katika Mji wa Jakarta katika ziara ya Kikazi nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla,wengine (kulia) Mkuu wa masuala ya Fedha Nd,Ridha Farid Lesmana,na Mkuu wa masuala ya Uchambuzi katika sehemu za fedha Tito Andrean Elvano (kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Kibiashara ya Exim Bank ya Nchini Indonesia baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Borobudur iliyopo katika Mjini Jakarta jana, katika ziara ya Kikazi nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Eximbank ya Indonesia Nd,Dwi Wahyudi (kulia) baada ya kumalizika mazungumzo ya pamoja yanayohusu kuimarishwa kwa uchumi katika Ukumbi wa Hoteli ya Borobudur iliyopo katika Mji wa Jakarta akiwa katika ziara ya Kikazi nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla,wengine (kushoto) Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe.Amina Salum Ali na Kaimu Mkurugenzi Mambo ya Nje Ofisi ya Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza,[Picha na Ikulu

Introducing "NIMESAMEHE" by Peter Msechu

NAFASI ART SPACE CELEBRATE ITS 10TH ANNIVERSARY THIS SEPTEMBER WITH A MONTH OF PUBLIC ART EVENTS, WORKSHOPS AND OUTREACH PROGRAMS

$
0
0

“Life is short, but art endures.”

In 2008 a small group of Tanzanian artists got together and dreamt up a platform for contemporary art in Tanzania. With support from The Danish Embassy, a space was located, six studios where constructed and Nafasi Art Space was born. Since then Nafasi has built from the ground-up a thriving artistic ecosystem of 37 studios, exhibition and performance spaces, artworks, meeting and learning opportunities, and has become Tanzania’s leading contemporary art center –inspiring and supporting artists in Tanzania while giving audiences and art lovers a place to experience and appreciate arts and culture, in Dar es Salaam.

MICHUZI TV: WANAWAKE KUNUFAIKA NA HEDHI APP

Abiria mwenye umri wa miaka 100 afanyiwa 'suprise birthday' na ATCL ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner

$
0
0
Wafanyakazi wa Shirika la ndege ATCL  jana Ijumaa wamemfanyia 'Suprise Birthday Party' mmoja wa abiria wao Mzee Kimweri Kivo mwenye umri wa miaka 100 kwa kumwandalia sherehe ndani ya ndege ya Beoing 787-8 Dreamliner  baada ya kutua katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitokea Dar es Salaam. 

Mzee Kivo ambaye hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kupanda ndege tangu azaliwe, aliishukuru ATCL kwa ukarimu wao na pia  amempongeza Rais John Magufuli kwa ununuzi wa ndege hiyo na nyingine ambapo umemwezesha naye kutimiza ndoto ya kuipanda na pia kwa kuiwezesha ATCL kuwa na ndege za kisasa zenye huduma za kimataifa.
Wafanyakazi wa Shirika la ndege ATCL  wakiandaa keki maalum kwa mmoja wa abiria wao Mzee Kimweri Kivo katika kusherehekea birthday yake ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner

Mzee Kimweri Kivo akijiandaa kukata keki katika kusherehekea birthday yake ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner
Mzee Kimweri Kivo akisherehekea  birthday yake ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner
Mzee Kimweri Kivo akijichana ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner

UNAKARIBISHWA KATIKA MISA YA KISWAHILI JIJINI NEW YORK SIKU YA JUMAPILI AGOSTI 12, 2018

$
0
0
Image result for misa ya kiswahili new york

Wakristu wapendwa,
Tumsifu Yesu Kristu.

Tunapenda kuwatangazia ya kuwa,
Tutakuwa na misa yetu ya kiswahili itayofanyika Jumapili tarehe 12 Mwezi Agusti 2018, kuanzia saa nane mchana. ( Sunday, 12 August 2018 at 2 pm). Tunawakaribisha watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada yetu ya Kiswahili.
Karibuni tumshukuru Mungu.

Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia, 120 East 106 Street, New York, NY 10029. Between Lexington and Park Avenue. 

Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St. Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.

Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi.

Mbarikiwe na
Karibuni...sana..
Kutoka kwa Padre Mushi

BREAKING: Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangwallah apata ajali

$
0
0
 Taarifa zilizopatikana muda huu zinasema Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangwallah  amepata ajali asubuhi hii akitokea Arusha katika eneo la msitu kabla ya kijiji cha Magugu maarufu kama Mguu wa Mjerumani ama Mdori.
Kwa mujibu wa mbunge wa Mbulu vijijini Mhe. Flatei Massay mtu moja ambaye ni mwandishi wa habari amepoteza maisha.  
Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni Twiga aliyekuwa anakatisha barabara mbele yao na katika kumkwepa gari likapinduka.
Taarifa zinapasha kuwa Dkt.  Kigwangwala amepata majeraha ya mkono na kifua na kukimbizwa katika kituo cha afya cha Magugu kupatiwa matibabu na kwa mujibu wa mleta habari, hali sio nzuri sana.
Hivi sasa inasubiriwa helikopta ije kumchukua kumpeleka hospitali kubwa. 
Tunafuatilia kwa karibu tutatoa taarifa zaidi baadaye.

mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati azikwa leo nyumbani kwao Mwiruruma, Bunda, mkoani mara

$
0
0
Ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara, mchana wa leo. 
Marehemu Sagati alifariki dunia pamoja na watu wengine wawili katika  ajali wilayani Geita. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema ajali hiyo ilitokea  Jumatatu Septemba 30, 2018 wakati dereva wa gari lenye namba   STK 9565 aina ya Toyota Land Cruiser V8, alipomkwepa mpita njia, Happiness James (7), aliyekatiza barabarani ghafla  wilayani Chato, Mkoa wa Geita. 
Alisema kutokana na ajali hiyo, watumishi wa wizara hiyo akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Ludovick Nuhiye, Mchumi Nickson Matembo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Yusuph Mbwalwa na dereva, Lucas  wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita wakipatiwa matibabu.
Kamanda Mwabulambo  alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Minkoto, Kijiji cha Kalembela wilayani Chato mkoani Geita. “Gari hilo lilikuwa likitokea Mkoa wa Kagera kwenda Mwanza na  binti huyo   alinusurika kugongwa baada ya dereva kufanya jitihada za kumkwepa.
“Dereva alilazimika kupeleka gari upande wa kulia ambako pia alikutana na kumgonga na mpitanjia,   Semeni Kibiriti,  ambaye alifariki dunia hapo  hapo.
 Waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
 Kiongozi wa dini akiongoza ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
 Ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikiendelea nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
 Wanahabari Mgaya Kingoba na Abdulwakil Saiboko wakisaidiana na waombelezaji wengine kuweka sawa jeneza wakati wa ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
 Sehemu ya waombolezaji katika ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
Viongozi wa dini wakiongoza ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara.

MBOLEA NANE NANE MBEYA

$
0
0
Kampuni ya GSM Tanzania kupitia kampuni yake Tanzu ya GS Agro inayoshughulika na Mambo ya kilimo imejikita katika kusambaza mbolea za aina zote pamoja na madawa ya kilimo pia. 
Wako Nane Nane mbeya karibuni au
 wasiliana nao kwa namba +255784000000

VYUO VYA POLISI VYAWEKA MIKAKATI KUBORESHA ELIMU.

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka Wakufunzi wa Vyuo vya Polisi vya Dar es Salaam na Zanzibar kuhakikisha wanawafundisha Askari Polisi Wanafunzi waliopo katika vyuo hivyo kwa kuzingatia mitaala iliyotolewa ili wanapotoka waweze kuwatumikia Wananchi na kupunguza uhalifu hapa nchini.
IGP Sirro ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake  katika vyuo hivyo ambapo alizungumza na Wakufunzi pamoja na Askari wanafunzi wanaosomea vyeo mbalimbali ambapo lengo la ziara hiyo ni kukagua muenendo wa mafunzo katika vyuo vya Polisi.
Amesema lengo la mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo yanapaswa kutolewa kwa weledi ili kila Askari anayehitimu aweze kupata maarifa ambayo yatawezesha kufanya kazi za Polisi vyema jambo ambalo litaendelea kupunguza uhalifu hapa nchini.
“Kila mkufunzi anapaswa ahakikishe lile somo analolifundisha wanafunzi wake wanalielewa ili kusudi kama ni Ofisa, Mkaguzi na Kiongozi mdogo ndani ya Jeshi la Polisi anafanya kazi kwa kufuata ile misingi iliyopo” Alisema Sirro.
Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Anthony Rutta amesema lengo la mafunzo katika Chuo hicho ni kuhakikisha kila Askari anayatambua majukumu yake ili kupunguza uhalifu hapa nchini na watahakikisha ukakamavu na nidhamu inazingatiwa ili kuwa na Jeshi lenye kufuata kanuni na taratibu zilizopo.
Naye Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Geofrey Kamwela amesema Chuo hicho kinakabiliwa na Changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa miundombinu yakiwemo majengo na bwalo la Chakula ambapo IGP Sirro aliahidi kutuma fedha za awali kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la kulia chakula chuoni hapo.
Kamwela alisema hivi sasa wanaendelea kutekeleza mradi wa kuweka mfumo wa Tehama ambao utawezesha wanafunzi kujisomea na kupata matokeo yao kwa njia ya mtandao jambo ambalo litawafanya kwenda kisasa katika utoaji wa elimu chuoni hapo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini yupo katika ziara ya kukagua mafunzo yanayoendelea katika vyuo vya Polisi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yanawajenga Maofisa na Askari kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kupunguza uhalifu hapa nchini.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana  na Maofisa wa Polisi Kamisheni ya Zanzibar wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Vyuo vya Polisi hapa nchini kwa lengo la kuboresha elimu inayotolewa na vyuo hivyo
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiimba wimbo pamoja na Askari wakati wa kikao chake na Askari wanafunzi katika Chuo cha Polisi Zanzibar wakati wa ziara yake. Kulia kwake ni Kamishna wa Polisi Zanzibar Mohamed Hassan Haji na kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha Kamisheni ya Polisi Zanzibar Faustine Shilogile
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Mafundi wa Nguo za Polisi waliopo katika Kiwanda cha Polisi cha kushona nguo Kamisheni ya Polisi Zanzibar wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Vyuo vya Polisi hapa nchini kwa lengo la kuboresha elimu inayotolewa na vyuo hivyo (Picha na Jeshi la Polisi).
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images