Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

WATOROSHAJI TANZANITE KIAMA KINAKUJA- WAZIRI KAIRUKI

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Simanjiro

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema Serikali itaaendelea kusimamia ulinzi na kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite na watakaokwenda kinyume na matakwa ya Sheria, kiama chao kinakuja.
Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 1 Agosti wakati wa ziara yake mkoani Manyara wakati alipotembelea migodi mbalimbali ya madini ya tanzanite ndani ya ukuta wa Mirerani.

Alisema ziara hiyo ililenga kuangalia suala zima la ulinzi katika ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, shughuli za uchimbaji madini mengine zinavyofanyika na kuangalia namna uzalishaji wa madini ya tanzanite unavyoendelea katika migodi husika. Kairuki aliongeza kuwa, ziara hiyo ililenga kuangalia namna Sheria ya Madini inavyotekelezwa, masuala ya Mikataba ya watumishi katika migodi na namna migodi husika inavyolipa kodi mbalimbali za Serikali yakiwemo masuala ya usalama sehemu za kazi na wafanyakazi kwa ujumla.

“Utoroshaji madini hausaidii, fedha ni za haraka lakini zinawaadhibu watanzania walio wengi kwa kuwa, fedha hizo hizo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo. Hivyo, kila mtanzania awe mlizi wa mwenzake,” alisema Kairuki.

Awali, akizungumza katika eneo Lemshuku kunakofanyika shughuli za uchimbaji wa madini ya Green Garnet, waziri Kairuki alisema kuwa, serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika kuchangia pato la taifa kupitia shughuli za uchimbaji, hivyo akawaasa wachimbaji nchini kufuata Sheria, kanuni na taratibu ili kufanya shughuli halali ikiwemo kulipa kodi stahiki.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia moja ya seal inayotumika kufunga madini ya tanzanite baada ya kuzalishwa na kufanyiwa tathmini kwa lengo la kuhakikisha serikali inapata mapato yake stahiki.
Waziri wa Madini Angellaha Kairuki akipima ubora wa madini ya Tanzanite katika kifaa maalum baada ya kuzalishwa kutoka katika mgodi wa moja ya wachimbaji madini ya tanzanite.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia madini ya Green Garnet alipotembelea moja ya migodi inayochimba madini hayo katika eneo la Lemshuku Wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara wakati wa zira yake.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akieleza jambo wakati akipata ufafanuzi kutoka kwa mchimbaji (aliye ndani ya shimo) wakati alipotembelea moja ya migodi ya madini ya Green Garnet katika eneo la Lemshuku wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.
Sehemu ya wachimbaji katika eneo la Lemshuku Wilayani Simanjiro kunakofanyika shughuli za uchimbaji madini ya Green Garnet wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki hayupo pichani wakati wa ziara yake katika eneo hilo.



Maamuzi ya taasisi lazima yashirikishe baraza la wafanyakazi –Profesa Msanjila

$
0
0
Na Chalila Kibuda.

Maamuzi yanapotakiwa kufanyika ni lazima uwepo ushirikishaji ili kuweza kuendesha taasisi na kupata mafanikio ya kimaendeleo na taifa kuona tija ya tasisi husika.

Hayo aliyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila wakati akifungua Baraza la Pili la Shirika la Taifa la Madini (Stamico) amesema sheria ya mashauriano katika utumishi wa umma, serikali imebainisha nia yake thabiti ya kutaka kuona wafanyakazi wakishirikishwa katika kusimamia na kuendesha taasisi wanazozimamia.

Amesema kuwa baraza ni chombo muhimu katika taasisi hivyo lazima kitumike katika kujadili mambo mbalimbali yanayoyohusu masilahi na ustawi wa watumishi , mipango na malengo ya kazi ya kuishauri menejimenti ya Stamico.Profesa Msanjila amesema viongozi waliochaguliwa katika baraza la wafanyakazi wa stamico kunadhihirisha imani ya wafanyakazi kuwa kile wanachokitaka kitafanyika kutokana na maamuzi ya ushirikishwaji.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Stamico Mhandisi Kanali Sylvester Ghuliku amesema baraza lilopita lilikuwa na changamoto nyingi ambazo zilikuwa zinatokana na shirika lenyewe kwa kutokuwa na fedha za kuitisha mkutano wa baraza na fedha ambazo zilikuwa zinapatikana katika shirika kidogo na hata kuendesha ofisi hazikutosha.Amesema kuwa baraza litafanyaka kazi katika misingi iliyowekwa katika uanzishaji katika kufikia lengo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akizungumza na baraza jipya la wafanyakazi la pili la Stamico lilofanyika Ofisi za Stamico jijini Dar es Salaam.
Watoa maada kutoka ofisi ya Kamishina wa madini, , Idara ya kazi na wawakilishi kutoa Chama cha wafanyakazi wa Migodi, Nishati , Ujenzi na Kazi Nyinginezo (Tamico)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila wa sita kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la pili jipya la Wafanyakazi wa Stamico, kulia kwa katibu Mkuu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Stamico Mhandisi Kanali Sylvester Ghuliku wane kutoka kushoto mstari wa mbele ni Katibu Mpya wa Baraza hilo Juma Mbawambo

HOSPITAL YA MSOGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA

$
0
0
Mwakilishi kutoka Tanzania Health Promotion Support (THPS) ,Sisty Moshi akimkabidhi mbunge wa Chalinze ,Ridhiwani Kikwete msaada wa vifaa mbalimbali vilivyogharimu milioni 48.412 katika hospital ya wilaya ya Msoga.
Mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze ,Rahim Hangai akimkabidhi taarifa ya hospital ya wilaya ya Msoga, mwakilishi kutoka THPS, Sisty Moshi wakati wa makabidhiano ya vifaa katika hospital hiyo .

NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE

WADAU wa afya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ,wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vilivyogharimu milioni 48.412 katika hospital ya wilaya ya Msoga,Chalinze Mkoani Pwani. Kati ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mabenchi za wagonjwa 30, meza za ofisi kumi ,viti vya ofisini 12 ,makabati ya kuhifadhia nyaraka matatu na stool kwa ajili ya maabara 13.#

Akikabidhi vifaa hivyo kwa mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ,mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze na uongozi wa hospital hiyo, mwakilishi kutoka THPS ,Sisty Moshi alisema ,wamewezesha vifaa hivyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta hiyo. Alieleza ,kuanzia 2016/2018 wameshatoa vifaa tiba na samani zenye thamani zaidi ya milioni 761.508  mkoani Pwani, kati ya hivyo vifaa vilivyogharimu milioni 236.647.568 vilipelekwa Chalinze.

"Katika mradi huu wa kusaidia kuzuia maambukizi mapya ya VVU ,kutoa huduma,tiba na msaada wa kisaikolojia kwa ufadhili wa serikali ya Marekani , sisi tunafanya kazi katika mikoa ya Kigoma,Pwani na visiwa vya Zanzibar"

"Ufadhili huu unatokana na makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Marekani kufuatana na malengo ya kitaifa " alifafanua Moshi.

Awali akitoa taarifa ya hospital ya wilaya ya Msoga ,mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze ,Rahim Hangai ,alisema tarehe 12/10/2017 waziri wa afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia ,wazee na watoto aliridhia na kutoa kibali cha kituo cha afya Msoga kuwa hospital ya wilaya. Alisema lakini bado inakabiliwa na ukosefu wa jengo la utawala,ukosefu wa gari kwa ajili ya shughuli za kiutawala,upungufu wa watumishi na chumba cha kuhifadhia maiti.

Changamoto nyingine ni ukosefu wa jengo la maabara ,jengo la tiba na mafunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC),jengo la mionzi ,ukosefu wa mashine ya X-ray ya ziada na chumba cha daktari na wodi ya wagonjwa wa akili. Hangai, alisema vituo vya afya na hospital hiyo ,vimekuwa vikipokea majeruhi wengi wa ajali za barabarani kwa takwimu za julai 2016-juni 2017 vimepokea majeruhi 799 na wagonjwa waliokuwa na dharula 5,477 na wajawazito 4,678 .

Akikabidhiwa vifaa hivyo ,Ridhiwani aliwashukuru wadau hao na kuomba wadau wengine wasiwachoke kuendelea kuisaidia changamoto ambazo zinazoikabili hospital ya Msoga. Ridhiwani alielezea kuwa ,halmashauri ya Chalinze inapitiwa na barabara kuu tatu ikiwemo Dar-es-salaam -Chalinze-Arusha,Chalinze -Msata-Arusha na Bagamoyo-Msata-Arusha. Alibainisha, vituo vya afya vilivyopo katika halmashauri hiyo vimekuwa vikipokea majeruhi wengi wa ajali za barabarani na magonjwa mengine.

GAVANA WA BoT ATANGAZA BANK M SASA IKO CHINI YA USIMAMIZI WAO

$
0
0
*Ni baada ya mtaji wake kutetereka, yapewa siku 90 kujitathimini

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BOT) imeamua kuchukua usimamizi wa Bank M kuanzia leo na uamuzi huo unachukuliwa baada ya kubainika benki hiyo ina upungufu mkubwa wa ukwasi.

Akizungumza leo Dar es Salaam Gavana BoT Profesa  Florens Luoga amesema kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha Sheria namba 56 (1)(g)(III)cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 ameamua kuchukua uamuzi huo kwa Benk M na sasa itakuwa chini ya usimamizi wa BoT.

"Upungufu huu wa ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa Bank M kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake,"amesema Profesa Luwoga.

Amefafanua kutokana na uamuzi huo ,Benki Kuu imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa Bank M kuanzia leo(Agosti 2) mwaka huu na kutokana na uamuzi huo BoT imemteua Meneja Msimamizi atakayesimamia shughuli za benki hiyo kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi.

Ameongeza Watanzania wafahamu kuwa katika kipindi kisichozidi siku 90 kuanzia leo , shughuli zote za utoaji wa huduma za kibenki za Bank M zitasimamiwa ili kuipa nafasi BoT kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

P ia kuwa BoT itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

BoT YARIDHIA UUNGANISHWAJI WA BENKI YA TWB NA TPB BANK Plc

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeridhia ombi la uunganishwaji wa benki za Benki ya Wanawake Tanzania(TWB) pamoja na TPB Bank Plc.

Kutokana na hatua hiyo sasa kutakuwa na benki moja kuanzia Agosti 3 mwaka huu itakayoendelea kuitwa benki ya TPB Bank Plc ambayo itaendelea kuwa na mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florenc Luoga amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na ombi la wanahisa la kutaka kuunganishwa kwa benki hizo. Amesema hivyo kuanzia sasa wateja, wafanyakazi , mali a madeni yote ya TWB yataunganishwa na yale ya benki ya TPB huku akifafanua muunganiko wa benki hizo unaifanya benki ya mpya ya TPB Bank Plc kuwa imara zaidi na itakuwa ina mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa chini ya kifungu cha 17 cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha.

"Benki Kuu inawaomba wateja wa benki ya TWB kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mpito cha uunganishwaji wa benki hizi na watendelea kupata huduma za kibenki kwa utaratibu utakaotolewa na menejimenti ya uongozi wa benki ya TPB,"amesema Profesa Luoga. Wakati huo huo amesema Benki za TOBACO na KCBL kwa sasa zimeweza kuongeza mtaji na kukidhi kiwango kinachohitajika kisheria na hivyo zinaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Amesema BoT inawagakikisha wananchi kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha. Awali Gavana Luoga amefafanua Januari 4 mwaka huu BoT iliongeza muda wa miezi sita kwa benki tatu ambazo ni Tandahimba Community Bank Limited (TOBACO), Tanzania Women's Bank Plc(TWB) na Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL).

Ambapo mpaka Juni 30 mwaka huu ili kufikisha kiwango cha mtaji kinachohitajika na sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2007 na kanuni zake za kiwango cha chini cha mtaji cha Sh.bilioni mbili kwa benki za wananchi. Aidha benki hizo ziliongezewa muda wa mwezi mmoja hadi Julai 31 mwaka 2018 ili kukamilisha taratibu za kuongeza mtaji.

Kutokana na kutolewa kwa muda huo ndipo wanahisa wa TWB na TPB walipoamua kuunganisha benki hizo na BoT imeridhia.

BINTI THERESIA,MKAZI WA MBURU ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU

$
0
0
"Huyu binti anaitwa Theresia yupo hapa Mbulu, aliugua ghafla na kupooza upande wa kulia toka 2011,alikuwa hawezi kuongea kabisa kwa zaidi ya mwaka mmoja,baada ya matibabu kwa mwaka mmoja alianza kuongea kidogo na kukaa,

Lakini kutokana na hali kuwa ngumu ya kumuhudumia ,wazazi wake walishindwa kuendelea na matibabu,na kwa zaidi ya miaka sita amekuwa akilala ndani tu muda wote,na hawezi kufanya chochote japo kuwa kwa sasa anaweza kuongea kidogo saana na kwa mbali ananyanyua mkono wake,tumemtembelea na kumpatia kiti cha kumuwezesha hata kutoka nje. 

Tunatamani binti huyu aweze kuanza kupatiwa matibabu tena na mazoezi! Watanzania wenzangu tumsaidie, Tutawajulisha pindi tutakapojua taratibu zote za matibabu na gharama kisha tutatoa mawasiliano ya wazazi wake! Ana umri wa miaka 27 na kabla alikuwa ni mfanyakazi katika mamlaka ya maji safi Mbulu". 

Mungu Ibariki Tanzania

Taarifa hii ni kwa Hisani ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga

 Pichani ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akimsaidia  binti  Theresia mkazi wa Mbulu, kumtoa nje kwa njia ya baiskeli ya walemavu (Wheel Chair) ,Theresa aliugua ghafla na kupooza upande wa kulia tangu mwaka 2011,kufuatia hali hiyo bint huyo anahitaji msaada wa Matibabu

MPIGANAJI SHADRACK SAGATI SASA KUAGWA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM KUANZIA SAA SABA MCHANA

$
0
0
Mwili wa Marehemu Msemaji wa Wizara ya Viwanda, Shadrack Sagati sasa utaagwa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam leo kuanzia saa 7 mchana hadi saa 11 jioni. 


Mabadiliko hayo yanafuatia kubadilika kwa njia zilizotumika kuusafirishia mwili huo kutokea mkoani Geita hadi Jijini Dar es Salaam,hivyo kusababisha kusogeza mbele kwa ratiba hiyo.

Kwa maana hiyo mabasi ya kuwachukua waombolezaji nyumbani kwa marehemu Kitunda Polisi, sasa yataondoka saa sita mchana, badala ya saa mbili asubuhi kama ilivyotangazwa hapo awali.

Hata hivyo kamati ya maandalizi pamoja na wahusika wote mnaombwa kuanza kuwasili uwanjani Mnazi mmoja saa 5 asubuhi.

Imetolewa na:
Kamati ya Maandalizi
Msiba wa Shadrack Sagati

DKT. MWANJELWA ATAO WITO KWA WAKULIMA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO, KULIMA KILIMO CHENYE TIJA

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mwanjelwa ametoa wito kwa wakulima kote nchini kulima kilimo chenye tija kwa kutumia zana bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji na kupata mavuno mengi na bora.

Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo Agosti Mosi, mara baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya Kilimo katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Bariadi, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu.

Dkt. Mwanjelwa amesema Serikali kupitia Mfuko wa pembejeo unatoa mkopo wa pembejeo kwa riba ndogo sana, hivyo akatoa wito kwa wakulima wote nchini kwenda katika Halmashuri zao na kupata utaratibu wa kuomba mikopo hiyo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kununua zana bora za kilimo.

“ Nitoe wito kwa wakulima wote nchini wajitahidi sana kwenda kwenye  kulima kilimo cha kisasa kilimo chenye tija, sisi kama Serikali tuna mfuko wetu wa pembejeo unaotoa mikopo kwa riba ndogo sana, hivyo wakulima wanaweza kuomba mikopo hiyo na kwenda kununua pembejeo bora za Kilimo” alisema Dkt. Mwanjelwa.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwanjelwa amewataka maafisa ugani kuwafuata wakulima shambani badala ya kukaa ofisini, ili kuwapa elimu ya kilimo bora na kuwawezesha wakulima  kufikia lengo la kulima kilimo chenye tija.
Naibu Waziri wa Kilimo,  Mary Mwanjelwa  akikagua mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya  mji wa Bariadi leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa  akikagua mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya  mji wa Bariadi leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalam wa kutoka Jeshi la Magereza akitoa maelezo kwa Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa wakati walipotembelea mabanda ya maonesho ya mifugo ya Jeshi hilo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi,  katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalam wa Ufugaji wa Samaki kutoka JKT, Luteni Joseph  Lyakurwa(kulia) akitoa maelezo kwa   Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu kushoto)  na Omary Mgumba (kushoto) wakati walipotembelea mashamba darasa ya JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi,  katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa Jeshi la Magereza akitoa maelezo ya namna ya kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya mimea kwa   Manaibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa (wa tatu kulia)  na Omary Mgumba (wa pili kulia) wakati walipotembelea mabanda ya maonesho ya Jeshi hilo katika  Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji Bariadi,  katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa akipewa maelezo kuhusu zana na mashine za kisasa  na wataalam wa JKT katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi leo Agosti Mosi, 2018, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018, Mkoani Simiyu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MASAUNI ZIARANI WILAYANI BUNDA KUKAGUA NA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA ASKARI POLISI

$
0
0
Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari polisi kote nchini, ikiwa ni kukabiliana na changamoto ya makaazi ya askari na uchakavu wa vituo vya polisi ili kuwawezesha askari hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea kijiji cha Makongoro wilaya ya Bunda mkoani Mara kuona changamoto wanazokutana nazo askari polisi katika kutekeleza majukumu yao ya ulinzi na usalama.

Alisema wizara iko katika mpango maalumu wa kuboresha makazi ya askari polisi nchini huku akitoa wito na nafasi kwa wadau wa maendeleo pia kujitokeza na kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli kuboresha makazi ya askari polisi

“Katika kukabiliana na changamoto ya askari nchi nzima tayari tushaanza kujenga makazi ya askari wetu tukianza na nyumba za polisi Kusini Pemba na tutaendelea na ujenzi huo wa nyumba 400 katika mikoa mingine nchini na kutokana na hali niliyoiona hapa Bunda basi tutatoa kipaumbele hapa”Alisema Naibu Waziri Masauni

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika ujenzi wa makazi ya askari polisi wilayani humo huku Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mussa Masilu aliongeza kuwa nyumba hizo ni chakavu na zinashusha hadhi ya Askari Polisi

Hadi sasa serikali imeshaanza taratibu za awali ikiwemo tathmini ya ujenzi wa nyumba hizo mia nne za askari polisi nchini ambapo mikoa mbalimbali itanufaika na ujenzi huo utakaotekelezwa kwa awamu tofauti ukienda sambamba na ujenzi na ukarabati wa vituo vya polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua moja ya makazi ya askari polisi katika kijiji cha Makongoro B, kilichopo wilayani Bunda wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kushughulikia changamoto za makazi ya askari polisi ambapo jumla ya nyumba mia nne za askari polisi zinatarajiwa kujengwa nchi nzima.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisoma maelezo ya mmoja ya mtuhumiwa aliyemkuta katika chumba cha mahabusu katika Kituo cha Polisi Bunda wakati wa ziara ya kikazi ya kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka ya mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili na wengine ni viongozi waandamizi wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Bunda.
Afisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mara, Mrakibu Mwandamizi ,Jeremiah Shila akitoa maelezo ya mwenendo wa mashtaka ya watuhumiwa walioko katika Kituo cha Polisi Bunda kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili(watatu kulia), wakati wa ziara ya naibu waziri kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka ya mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto), akifuatilia wakati mpelelezi akifunua jalada la mmoja wa mahabusu aliyemkuta katika chumba cha mahabusu katika Kituo cha Polisi Bunda wakati wa ziara ya kikazi ya kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka ya mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili na wengine ni viongozi waandamizi wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Bunda.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NAONA FAHARI UWEKEZAJI WA MWANGA GEMS - KAIRUKI

$
0
0
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) akitembelea maeneo mbalimbali katika kiwanda cha Kuchakata Madini ya Graphite cha GodMwanga Gems Ltd. Wa kwanza kulia ni Mmiliki wa kiwanda hicho Godlisten Mwanga na wa kwanza kuli kwa waziri ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Tumaini Magesa.
Mmiliki wa kampuni ya God Mwanga Gems Ltd.Godlisten (kulia) Mwanga akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki madini ya Grahite ambayo tayari yamechakatwa.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) akipita katika maeneo mbalimbali ya kiwanda cha God Mwanga Gems Ltd kuona namna shughuli mbalimbali za uchakataji wa madini ya Kinywe zinavyofanyika.

Na Asteria Muhozya, Simanjiro

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema anaona fahari kutokana na uwekezaji wa Kiwanda cha Kuchakata madini ya Kinywe (Graphite) uliofanywa na Kampuni ya wazawa ya GOD Mwanga Gems Ltd iliyopo Kata ya Endiamtu, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara. Waziri Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 2 Agosti, alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujionea shughuli zinazofanywa na kiwandani hapo.

Amesema Serikali imekuwa ikihamasisha waombaji wa leseni za madini kuwekeza katika maeneo mbalimbali hivyo, jambo lililofanywa na kiwanda hicho ikiwemo malengo ya kiwanda husika kufungua viwanda vingine katika mikoa ya Tanga na Manyara ni jambo la kujivunia na fahari kwa Tanzania.

“Nimefurahishwa sana namna kampuni hii inavyofanya kazi. Serikali kupitia wizara yangu imekuwa ikihamasisha uwekezaji. Tuko tayari kuwasimamia na kuwasaidia katika hili. Tunataka kutengeneza ajira zaidi, kukuza uchumi kupitia madini lakini pia serikali kupata kodi,” amesisitiza Kairuki. Akijibu ombi la kampuni hiyo kupata kibali cha kuuza madini hayo nje, Waziri Kairuki ameahidi kampuni hiyo kuwa mara baada ya taratibu za utoaji vibali kukamilika Wizara kupitia Tume ya Madini itatoa kibali kwa kampuni husika iendelee na taratibu zake za kuuzwa nje ya nchi madini hayo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUKAMATA SILAHA ZILIZOKUWA ZINATUMIWA NA WAHALIFU.

$
0
0
Mkuu Wa Operesheni Maalum za Jeshi La Polisi, Naibu Kamishna (DCP) Liberates Sabas, akikagua na kuangalia silaha zilizokamatwa na askari Polisi katika operesheni maalum ya kutokomeza uhalifu nchini inayoendelea mkoani Mtwara. (Picha na Jeshi la Polisi)

Urasimishaji Biashara Waingiza Mapato Zaidi ya Milioni 600 Manispaa ya Morogoro

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Kebwe Steven Kebwe akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay alipofika ofisi kwa Mkuu wa Mkoa huyo hivi karibuni mjini Morogoro. Kutoka kulia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John Chiligati, Mtendaji Mkuu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Bw. Emmanuel Mayeji.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Cliford Tandari akiteta jambo na wajumbe Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) pamoja na watendaji wa mpango huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Daniel Ole Njolay (katikati) walipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro hivi karibuni. Kutoka kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Emmanuel Mayeji, Mtendaji Mkuu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe, Mwenyekiti mstaafu wa kamati hiyo Kapteni John Chiligati na mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Bw. Ibrahim Janabi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogorgo, Bi. Ruth John akielezea jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) pamoja na watendaji wa mpango huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Daniel Ole Njolay (katikati) walipotembelea ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Morogoro hivi karibuni.
Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bibi. Anna Mwasha aakifafanua jambo mbele ya Afisa Biashara wa Manispaa ya Morogoro ambaye pia ni Mratibu wa MKURABITA katika Manispaa hiyo, Bw. Herman Festus wakati wa ziara ya kutembelea Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara  katika Manispaa ya Morogoro hivi karibuni.Kituo hicho kinatoa huduma za urasimishaji wa biashara ambapo mpaka sasa kimefanikiwa kurasimisha biashara 5000 na kufanyikisha ukusanyaji wa mapato ya takribani shilingi milioni 500. Kulia kwake ni Meneja wa Urasimishaji wa Biashara Heavy Kombe na mmoja wa watoa huduma wa Kituo hicho Bi. Mary Lyimo.
Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA),Bibi. Seraphia Mgembe akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Wanawake Wazalishaji wa Chakula Tanzania (WFPT), Bibi. Emmy Kiula hivi karibuni mjini Morogoro. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay.
Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA),Bibi. Seraphia Mgembe akikagua kifungashio cha mvinyo walipotembelea Kampuni ya ADUKE Food Processing wakati wa wa ziara ya kutembelea wanufaika wa mafunzo ya MKURABITA mkoani Morogorogo hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay, kushoto ni Afisa Biashara Manispaa ya Morogoro, Herman Festus na wapili kushoto ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Bibi. Angelista Kihaga.
Mwenyekit wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akiongoza kikao cha majumuisho baada ya kuhitimisha ziara ya siku 12 kukagua maendeleo ya utekelezaji ya shughuli za Urasimishaji Ardhi na Biashara katika maeneo ya Urambo, Bariadi, Ikungi, Chamwino na Manispaa ya Morogoro kikoao kilichofanyika mjini Morogoro mapema hivi karibuni. Picha na Frank Shija- MAELEZO

WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA IDARA NA VITENGO VILIVYOPO OFISI YA WAZIRI MKUU

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametembelea Idara na Vitengo vilivyopo Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ili kujionea hali halisi ya utendaji kazi wa watumishi wa ofisi hiyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa afisa  wa hifadhi ya jamii wa Ofisi hiyo Bw. Saimon Mwanjala wakati alipotembelea Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuona utendaji wao leo jijini Dodoma. (Kushoto) Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Peter Kalonga.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Gabriel Saelie leo Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kutembelea Idara na Vitengo vya Ofisi hiyo kujionea jinsi wanavyotekeleza majukumu yao.
 Mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Leinila Mtilanjala akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama leo mjini Dodoma wakati alipotembelea Vitengo na Idara zilizopo chini ya Ofisi hiyo.
 Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu wakimsikiliza. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea Idara na Vitengo vya Ofisi hiyo kujionea jinsi wanavyotekeleza majukumu yao.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Peter Kalonga akimwelezea jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake ya kutembelea Idara na Vitengo vilivyopo chini ya Ofisi hiyo. (Kulia) Mtakwimu Mwandamizi Idara ya Ajira Bw. Godwin Mpelumbe.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UGENI KUTOKA BUNGE LA KENYA, MKUU WA WILAYA YA BAHI MTEULE LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Moses Cheboi (wa pili kushoto) pale ugeni kutoka Bunge la Kenya ulipomtembelea leo tarehe 02 Agosti, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Wabunge Mhe. Wafula Wamunyinyi na Mhe. Farhiya Haji (kushoto).
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Kenya ulipomtembelea leo tarehe 02 Agosti, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Ugeni huo ulioongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Moses Cheboi (kulia kwake).
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Bunge la Kenya ulipomtembelea leo tarehe 02 Agosti 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Moses Cheboi, Mhe. Farhiya Haji (kushoto) na Mhe. Wafula Wamunyinyi


 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mteule, Mhe. Mwanahamisi Mukunda alipomtembelea leo tarehe 02 Agosti, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mteule, Mhe. Mwanahamisi Mukunda alipomtembelea leo tarehe 02 Agosti, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kwa ajili ya kumpongeza na mazungumzo mafupi

(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

JAJI KIONGOZI APEWA UFAFANUZI JINSI MFUMO WA ‘VIDEO CONFERENCE’ UTAKAVYOFUNGWA NA UTAKAVYOFANYA KAZI MAHAKAMANI

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewasihi Watumishi wa Mahakama kuwa na utayari katika matumizi ya mifumo mbalimbali ya Teknolojia inayoanzishwa Mahakamani ili kuendelea kuboresha  huduma ya utoaji haki nchini.
Aliyasema hayo Agosti 02, alipokuwa akiwasilishiwa mada juu ya mfumo wa ‘Video Conferencing’ utakavyofungwa na utakavyofanya kazi katika Mahakama husika iliyowasilishwa na Mkandarasi atakayefanya kazi  ya ufungaji wa mfumo wa ‘Video Conferencing’, Kampuni ya ‘Invention Technologies.’
“Mahakama yenyewe inatakiwa kuwa tayari kutumia mifumo mbalimbali inayowekwa ili hata Wadau wengine kama Magereza, Polisi waweze kwenda sambasamba na Mahakama katika kuboresha huduma ya utoaji haki,” alisisitiza Mhe. Feleshi.
Aidha Wajumbe wengine waliohudhuria katika kikao hicho, ambao ni Majaji wawili wa Mahakama Kuu, Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Msajili Mahakama ya Rufani, Mkurugenzi wa TEHAMA-Mahakama, na Maafisa wengineo waliunga mkono juu ya Mahakama kuwa na mfumo huo na kumtaka Mkandarasi kutekeleza kazi hiyo kwa wakati kama alivyoahidi.
Kwa kuanzia mfumo wa ‘Video Conferencing’ utafungwa maeneo yafuatayo; Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto na Gereza la Keko.
Aidha; Mkandarasi anayefanya kazi hii ameahidi kukamilisha kazi hii mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2018. Kwa sasa mfumo wa ‘Video conferencing’ Mahakamani umefungwa katika Kituo cha Mafunzo-Kisutu pamoja na Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya.
Mfumo wa ‘Video conference’ Mahakamani utasaidia na utakuwa ni chachu kubwa ya kuharakisha uendeshaji wa mashauri, kupunguza gharama za mashahidi watokao mbalina Mahakama husika na vilevile utasaidia hata katika kuendesha mafunzo mbalimbali ya Watumishi wa Mahakama katika vituo vyao vya kazi.
Mahakama ya Tanzania kupitia Mradi wa Maboresho ya huduma za Mahakama chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia inaendelea na miradi mbalimbali ya maboresho yote yakiwa na lengo la kuwapa wananchi huduma bora ya upatikanaji wa haki zao.
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akiongoza majadiliano mara baada ya uwasilishwaji wa mada ya mfumo wa ‘Video Conferencing.’
 Wajumbe wakifuatilia mada katika kikao hicho.
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akiongea jambo katika kikao hicho.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi (mwenye suti nyeusi) akichangia jambo katika kikao hicho.
Mtaalamu kutoka ‘Invention Technologies’ akiwasilisha mada.

RAIS SHEIN AFANYA MAZUNGUMZO NA JUMUIYA YA WAFANYABISHARA NA VIWANDA NCHINI MALAYSIA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) wakati Rais alipofika katika Ofisi za Jumuiya hiyo kwa mazungumzo na Wanajumuiya hiyo Jakarta Indinesia kwa mualiko wa Makamu wa Rais wa Nchi hiyo katika ziara ya kikazi ya siku saba,(kulia) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Malaysia pia akiiwakilisha Indonesia Balozi Ramadhan Kitwana Dau.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) wakati Rais alipofika katika Ofisi za Jumuiya hiyo kwa mazungumzo na Wanajumuiya hiyo Jakarta Indinesia kwa mualiko wa Makamu wa Rais wa Nchi hiyo katika ziara ya kikazi ya siku saba.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo ya pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) wakati Rais alipofika katika Ofisi za Jumuiya hiyo kwa mazungumzo na Wanajumuiya hiyo Jakarta Indinesia kwa mualiko wa Makamu wa Rais wa Nchi hiyo katika ziara ya kikazi ya siku saba.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo ya pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) wakati Rais alipofika katika Ofisi za Jumuiya hiyo kwa mazungumzo na Wanajumuiya hiyo Jakarta Indinesia kwa mualiko wa Makamu wa Rais wa Nchi hiyo katika ziara ya kikazi ya siku saba.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)  alipokuwa akiiuliza suala kwa Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) (hawapo pichani) wakati wazungumzo yaliyofanyika jana katika  Ofisi za Jumuiya hiyo ziliopo Mjini  Jakarta Indinesia katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamu wa Rais wa Nchi hiyo katika ziara ya kikazi ya siku saba.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN)Bw.Rosan  P.Roeslan (kulia)  pamoja na Viongozi wengine wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Jumuiya hiyo jana katika ukumbi wa Ofisi hiyo uliopo Mjini Jakarta Indonesia  katika mkutano wa siku moja,katika  ziara ya muaaliko wa Makamo wa Rais Mohammed Jusuf Kalla.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Mwani ya ASOSIASI RUMPUT LAUT INDONESIA (ARLI) Bw.Safari Azis mara baada ya Mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda katika Ofisi za Jumuiya hiyo Jakarta Nchini Indonesia akiwa katika ziara ya Mualiko wa Makamo wa Rais wa nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla,(katikati) Bw.HermanMoeliana Mkurugenzi Mkuu waPT INTERA LESTARI POLIMER
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( kulia) alipokuwa akiangalia mifuko inayotengenezwa kwa kutumia Unga wa Muhogo mara baada ya mazungumzo na  Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) katika Ofisi za Jumuiya hiyo ziliopo Jakarta Indinesia akiwa katika ziara ya mualiko wa Indonesia Mohamed Jusuf Kalla,wengine(kushoto)  Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara  na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN).
 (Picha na Ikulu)

KATIBU MKUU HAZINA AKUTANA NA MAMENEJA WA TRA NCHINI

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akihutubia Bodi ya Wakurugenzi, Viongozi na Mameneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara, kuhusu umuhimu wa kusimamia ipasavyo makusanyo ya kodi, katika kikao maalumu kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam

 Wajumbe wa Menejimenti wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiwa pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kujadili namna ya kuhakikisha kuwa zaidi ya shilingi trilioni 18 kati ya shilingi trilioni 32.47 zilizopitishwa na Bunge kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 zinazotakiwa kukusanywa na Mamlaka hiyo zinapatikana kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Meza Kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa tatu kulia), wakati wa kikao maalumu kati ya Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango na Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti ya TRA na Mameneja wa Mamlaka hiyo kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, waliokutana katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu, Jijini Dar es Salaam, kujadili pamoja na mambo mengine namna ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa na Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Adolf Ndunguru.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akisisitiza jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi, Viongozi na Mameneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara, kuhusu umuhimu wa kusimamia ipasavyo makusanyo ya kodi, katika kikao maalumu kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ATEMBELEA GEREZA LA KILIMO MANG'OLA, KARATU

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiwasili katika Gereza la Kilimo Mang’ola, Wilayani Karatu Agosti 2, 2018 tayari kwa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
 Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro(wa tatu toka kulia) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa pili kushoto) ramani ya eneo linapojengwa Gereza la jipya la Mahabusu Wilayani Karatu.

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua tanuru la tofali za kuchoma katika eneo la Gereza la Kilimo Mang’ola. Tofali hizo za kuchoma hutumika kujenga nyumba za watumishi katika gereza hilo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akizungumza na Askari wa Gereza Mang’ola(hawapo pichani) katika ziara yake ya kikazi.
 Askari wa vyeo mbalimbali wa Gereza Mang’ola wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
 Mkuu wa Gereza Mang’ola, Mrakibu wa Magereza, Masesa Magere(wa kwanza kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike maeneo mbalimbali ya gereza hilo leo Agosti 2, 2018
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega(kulia) akiwa ameongezana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa pili kushoto) katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Arusha. Kamishna Jenerali Kasike amefika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Arusha kabla ya kuanza ziara yake katika Gereza la Kilimo Mang’ola leo Agosti 2, 2018
(Picha zote na Kitengo cha Habari na
Mawasiliano Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza).

Introducing new hit "Simu Mbovu" by Phillz ft. ZAiiD

DK.SHEIN ATEMBELEA KIWANDA CHA SAMAKI NCHINI INDONESIA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji Risyanto Suanda wa  Kiwanda cha Uvuvi Perun Perikanan Nchini Indonesia akipotembelea Kiwanda hicho leo kuangalia maendeleo ya kazi zake katika kuzindika Samaki wa aina mbali mbali katika ziara ya Mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla,(kushoto) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Malaysia pia akiiwakilisha Indinesia Mhe.Balozi Ramadhan Kitwana Dau
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na viongozi na baadhi ya watendaji katika   Kiwanda cha Samaki cha  Perun Perikanan Nchini Indonesia wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda hicho pamoja na Ujumbe aliofutana nao katika ziara ya kikazi Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na Viongozi aliofuatana nao katika ziara ya kutembelea Kiwanda cha Samaki Perun Perikanan Nchini Indonesia pamoja na Mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji Risyanto Suanda (wa pili kulia) katika  ziara ya Mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla,(kushoto) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Malaysia pia akiiwakilisha Indinesia Mhe.Balozi Ramadhan Kitwana Dau,na Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe,Amina Salum Ali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Malaysia pia akiiwakilisha Indinesia Mhe.Balozi Ramadhan Kitwana Dau (katikati) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Risyanto Suanda (kushoto) wa Kiwanda cha Samaki kiliopo Perusahaan Umum kinachojulikana kama Perun Perikanan Nchini Indonesia wakiwepo na  Viongozi wengine aliofuatana nao katika ziara ya kutembelea Kiwanda cha Samaki hicho jana akiwa  katika  ziara ya Mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa na Viongozi katika Kiwanda hicho alipotembelea sehemu mbali mbali kuangalia kazi zinavyoendelea pamoja na  ujumbe wake alipotembelea kiwanda hicho jana katika ziara ya Mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla.


Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images