Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Tume ya Madini kupanga bei elekezi ya Madini nchini


KAMPUNI YA MONSANTO YAZINDUA MBEGU MPYA YA MAHINDI

$
0
0
Na Pamela Mollel,Arusha.

Kampuni ya Uzalishaji wa Mbegu ya Monsanto imezindua mbegu mpya aina ya DK 777 ,ambayo ina uwezo mkubwa wa kustahimili ugonjwa wa Mnyauko wa Mahindi uliowasumbua wakulima wengi hususan katika kanda ya Kaskazini na kusababisha wakulima kukosa mazao .

Mtafiti wa Mbegu hizo kutoka kampuni ya Monsanto ,Honest Temu amesema kuwa ugonjwa wa Mnyauko umeawaathiri wakulima wengi suala lililowasukuma kufanya utafiti ambao ulikamilika hivi karibuni na mbegu hizo zilisajiliwa na serikali kwa ajili ya kutumika na wakulima .

Meneja Kiongozi wa Kampuni hiyo Frank Wenga amesema kuwa mbegu hizo zitakua mkombozi kwa wakulima na kuleta mavuno ya kutosha kwa ajili ya chakula na ziada kwa ajili ya biashara ili kukuza pato la mkulima na kuinua uchumi wa taifa kupitia kilimo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mbegu nchini Bob Shuma akizindua mbegu hizo amesema kuwa sekta ya mbegu ni sekta muhimu katika kukuza kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa hivyo wadau wa mbegu hawana budi kufanya tafiti zitakazosaidia kukuza kilimo na kuinua ustawi wa mkulima kupitia uzalishaji wa mbegu bora.

Kwa upande wake Mkulima Nko amesema kuwa mbegu hizo zitawasadia wakulima kupata uhakika wa kupata mazao ya kutosha kutosheleza mahitaji ya nyumbani na mahitaji ya soko hivyo kusaidia upatikanaji wa chakula na kukuza pato la mkulima.
Meneja Kiongozi wa Kampuni ya Monsanto Frank Wenga Akizungumza katika uzinduzi wa mbegu mpya aina ya DK 777 ,ulifanyika katika viwanja vya Kituo cha utafiti wa kilimo Selian jana Mkoani Arusha.Picha na Pamela Mollel Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mbegu nchini Bob Shuma akizungumza katika uzinduzi wa mbegu mpya aina ya DK 777 jana Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa kilimo
Viongozi wa kampuni ya Monsanto na wadau wa kilimo wakiwa katika shamba darasa.

WATEULIWA WAPYA KUAPISHWA KESHO JUMATANO IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu, Dar es Salaam.
Wakuu wa Mikoa wanne, Makatibu Wakuu wawili, Naibu Makatibu Wakuu wawili na Makatibu Tawala wa Mikoa 13 walioteliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano     wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Jumamosi tarehe 28 Julai, 2018 wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 01 Agosti, 2018 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara mnapaswa kuhudhuria tukio hili.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

30 Julai, 2018

MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA SASA KUPATA HESHIMA NCHINI

WANAHABARI NGULI WALIOPATA KUWA WAHARIRI WAKUU WA DAILY NEWS, SUNDAY NEWS NA HABARI LEO

$
0
0
Wanahabari hawa walipata kuwa wahariri wakuu (Managing Editors) wa magazeti ya serikali ya Daily News, Sunday News na Habari leo katika nyakati mbalimbali. Kutoka kushoto ni Isaack Mruma, Dkt. Jim Yonazi na Mkumbwa Ally. Mruma alimuachia kijiti Mkumbwa ambaye naye alimuachia Gabriel Nderumaki kabla ya Dkt Yonazi kuchukua hatamu. Ila nafasi hiyo ipo wazi kwa sasa baada ya majuzi Rais Dkt. Magufuli kumteua Dkt Yonazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano).

CHALINZE KUTENGA BAJETI KILA MWAKA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MAABARA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo wakati alipotembelea maktaba ya shule ya sekondari Mboga ,aliyesimama ni mkuu wa shule ya sekondari ,George Mwakihaba.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (mwenye shati jeupe) akiangalia namna mwanafunzi wa shule ya sekondari Mboga akifanya mafunzo ya somo la sayansi kwa vitendo wakati alipotembelea maabara ya shule ya sekondari Mboga.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo wakati alipotembelea maktaba na maabara ya shule ya sekondari Mboga .(picha na Mwamvua Mwinyi).

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

SHULE 13 za sekondari, halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani ,zinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya maabara za masomo ya sayansi, ikiwa ni sawa na upungufu wa vyumba 39.

Afisa elimu sekondari Chalinze, Timothy Bernard aliyasema hayo ,wakati mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alipotembelea maabara zilizokamilika shule ya sekondari Mboga, ikiwa ni sehemu yake ya kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo jimboni humo. Alisema ,halmashauri hiyo ina jumla ya shule 17 za serikali ambapo shule nne zimeshakamilisha vyumba 12 vya maabara zinazotakiwa.

"lengo letu ni kuhakikisha tunatenga bajeti kila mwaka ili kujenga maabara hizo, awamu kwa awamu hadi hapo tutakapomaliza tatizo hilo ,na hatimae watoto wetu waendelee kunufaika na masomo ya sayansi kwa vitendo" alisema Bernard.

Mkuu wa shule ya sekondari Mboga, George Mwakihaba ,alimshukuru mbunge huyo ,wadau ,bank ya dunia, ,halmashauri na nguvu za wananchi kwa kujitoa kwao kukamilisha maabara zote shuleni hapo. Alisema miaka ya nyuma walikuwa na maabara moja pekee ,iliyotumika kwa masomo yote matatu ya sayansi, hali iliyokuwa ikisababisha wanafunzi kutofanya vizuri kwenye masomo ya mafunzo kwa vitendo.

Mwakihaba alielezea ,licha ya changamoto ya ukosefu wa maabara kubaki historia wanakabiliwa na ukosefu stuli na vifaa vya kuhifadhia kama makabati.

Nae Ridhiwani alisema kuwa ,viongozi wanapaswa kujenga tabia ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyokamilika na ambayo bado kukamilika ili kujiridhisha namna ya ujenzi unaofanyika. Alisema, maabara ya sekondari Mboga ina upungufu wa baadhi ya vifaa suala ambalo amelibeba na ataangalia namna ya kulisaidia .

Akizungumzia ziara yake kwenye miradi ya maendeleo ,Ridhiwani alieleza ,ametembelea kituo cha afya Msoga ,maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa unaojengwa Msoga, sekondari ya Mboga na kiwanda cha Sayona .

WANAKIJIJI WAKIRI MBELE YA NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. HASUNGA KUVAMIA HIFADHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo kata ya jangwani mara baada ya kupewa zawadi ya gunia la mahindi na samaki wakati alipotembelea kwa ajili ya kuzungumza wananchi waliohamia ndani ya hifadhi ya Lipalamba iliyopo wilayani Nyasa moani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.

NA LUSUNGU HELELA- RUVUMA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Wakazi wa Kijiji cha Ndondo kata ya Jangwani wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamekiri mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga kuwa wamevamia na wanaishi ndani ya eneo la hifadhi ya pori la akiba la Lipalamba lakini kwa kuwa hilo eneo wameshalizoea wanaiomba serikali kubadilishana nao na eneo jingine la kijiji lenye ukubwa sawa na eneo hilo walioingia ndani ya hifadhi hiyo.

Wananchi hao wametoa maombi hayo jana kwenye kwenye mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri huyo alioambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyasa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kwenye ziara ya siku tatu ambayo Naibu Waziri huyo aliifanya ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji wenzake, Pancrease Ndunguru alisema kuwa mpaka unaotenganisha kati ya kijiji na pori hilo ni mto unaojulikana kwa jina Tanginyama lakini wao wamejikuta wamevamia eneo hilo kwa kuanzisha makazi hivyo wanaomba hiyo sehemu waendelee kuishi lakini wakubali kubadilishana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndondo waliovamia Pori Akiba la Lipalamba iliyopo wilayani Nyasa moani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.

‘’Hili eneo sisi tushalizoea tunaiomba serikali ikubali ombi letu la kuweza kubadilishana na eneo lingine nje ya ukubwa sawa na eneo hili Alisema Pancreance Ndunguru. Naye, Diwani wa eneo hilo Ditram Nchimbi alimsihi Naibu Waziri alifanyie kazi ombi hilo la wanakijii kwa vile wameonesha uungwana kwa kutambua kuwa wamevamia baadhi ya eneo katika hifadhi ya Lipalamba lakini kitendo cha kukiri kosa ni uungwana wa hali ya juu hivyo walifanyie kazi ombi lao.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

LUGUMI BAADA YA KUKUTANA NA WAZIRI KANGI LUGOLA

$
0
0
 Mmiliki wa makampuni ya Lugumi, Said Lugumi (kulia) akitoka katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es salaam muda huu, baada ya mazungumzo na Waziri Kangi Lugola.


MICHUZI TV BREAKING: MFANYABIASHARA SAIDI LUGUMI ARIPOTI MAKAO MAKUU YA POLISI, APELEKWA KWA WAZIRI LUGOLA

$
0
0
Mfanyabiashara Saidi Lugumi akiongozwa na Ofisa wa Polisi kuelekea ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola baada ya kutoka Makao Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.(Picha na Jeshi la Polisi)

MAHAKAMA YAMPA ONYO MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE

$
0
0
Na Ripote wa Globu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa onyo  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), Freeman Mbowe kwa kutohudhuria mahakamani mara mbili  katika kesi ya uchochezi inayomkabili yeye na wenzake nane. Ameambiwa iwapo atarudia tena kutofika mahakamani kwa sababu ambazo hazina msingi basi dhamana yake itafutwa.

Onyo hilo limetolewa leo Julai 31 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).

"Mwambieni asiendelee tena na huo mchezo aheshimu masharti ya dhamana na akirudia tena mahakama itamchukulia hatua ikiwamo kumfutia dhamana yake na kutaifisha fungu la dhamana ambalo ameliweka".

Aidha Hakimu Mashauri ameondoa kumbukumbu barua zilizowasilishwa na wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu ambazo ni nakala ya kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa katika maombi ya marejeo namba 126,2018 ya Mahakama Kuu na mwenendo wa maombi hayo.  

Amesema, ataweka kumbukumbu hiyo pale wahusika watakapoyafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria. Kesi hiyo imepangwa Agosti 2,2018 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa (PH).

Mapema wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu alieleza mahakamani kuwa Mbowe hayupo lakini mdhamini wake yupo. Mdhamini wa Mbowe, ameileza mahakama kuwa amefanya mawasiliano na mshtakiwa (Mbowe) na amemueleza kuwa amekwama kwenye foleni.

Baada ya kutolewa kwa Maelezo hayo, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiomba mahakama kumuingiza Mbowe kwenye kumbukumbu zake kuwa hiyo ni Mara ya pili mfululizo mshtakiwa ahudhurii kesi mahamani bila ya kutoa sababu za msingi.

"Julai 25, mwaka huu Mbowe hakufika mahakamani na mdhamini alieleza kuwa ameharibikiwa na gari akitokea Arusha, Leo amekwama katika foleni.
Naomba mahakama itoe onyo kwa washtakiwa kuheshimu masharti ya dhamana na kufika mahakamani kwa wakati." Amedai Nchimbi.

Wakili Mwasipu amedai mahakamani hapo kuwa, pamoja na kesi hiyo kupangwa kwa PH leo lakini mawakili wanaoiendesha kesi hiyo, Peter Kibatala yupo Mahakama Kuu na Jeremiah Mtobesya yupo Mwanza wameomba kesi iahirishwe hadi Agosti 2,2018 Saa 5 asubuhi watakuwepo.

Pia amewasirisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa mahakamani hapo na barua ya kuomba mwenendo wa maombi ya marejeo Mahakama Kuu.

Hata hivyo, wakili Nchimbi aliiomba mahakama kwa sasa isipokee maombi ya taarifa hiyo hadi pale yatakapofikishwa kwa kufuata utaratibu na msingi wa sheria.

Washtakiwa waliokuwepo mahakamani ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Former African Heads of State, Government and Business Leaders to discuss Financing for Sustainable Development

$
0
0
The fifth African Leadership Forum (ALF), hosted by the former President of the United Republic of Tanzania, H.E. Benjamin William Mkapa and organised by UONGOZI Institute will take place in Kigali, Rwanda from Thursday 02nd August, 2018 to Friday 03rd August, 2018.

This year’s Forum, under the theme, “Financing Africa’s Transformation for Sustainable Development” seeks to provide a platform to deliberate on the prospect of increased, improved, and effective financing for Africa’s transformation.
“The meeting will provide an opportunity to learn from the successes and set-backs in national, regional and continental attempts to address specific financing challenges, and to put forward recommendations for unlocking increased financing for Africa’s development,” said Prof. Joseph Semboja, CEO of UONGOZI Institute.

The Keynote Address will be delivered by H.E. Paul Kagame, President of the Republic of Rwanda. Participants of the Forum will include H.E. Joaquim Chissano, former President of the Republic of Mozambique; H.E. Olusegun Obasanjo, former President of the Federal Republic of Nigeria; H.E. Moncef Marzouki, former President of the Republic of Tunisia; H.E. Hassan Sheikh Mohamud, former President of the Republic of Somalia; and over 100 other distinguished leaders from the public sector, private sector, academia and civil society. 

Speakers at the event will include Dr. Vera Songwe, Executive Secretary of UNECA, Dr. Donald Kaberuka, former President of the African Development Bank, Prof. Njuguna Ndung’u, former Governor of the Central Bank of Kenya and Dr. Mukhisa Kituyi, Secretary General of the United Nations Conference on Trade and Development and Amb. Dr. Yonov Frederick Agah, Deputy Director General, World Trade Organization.

The African Leadership Forum was conceived of as a space for Africa’s eminent elders to interact with current and future leaders around the strategic challenges facing the Continent. The annual meeting brings together former Heads of State as well as leaders from government, civil society, the private sector and academia from across Africa.

MCHENGA, FLYING DRIBBLERS WASHINDA NUSU FAINALI YA KWANZA YA SPRITE BBALL KINGS

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NUSU Fainali ya kwanza ya Michuano ya Sprite BBall Kings imefanyika wikiendi hii kwa michezo miwili kupigwa katika Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Mchezo wa kwanza ulianza kwa kuwakutanisha Flying Dribblers dhidi ya The Team Kiza ulikuwa na ushindani mkubwa sana kwa timu zote mbili kutafiuta ushindi wa kwanza na ulimalizika kwa timu ya Flying Dribblers kuibuka na ushindi wa vikapu 84 kwa vikapu 75 vya The Team Kiza.

Portland waliwakaribisha Mabingwa watetezi Mchenga BBall Stars katika mchezo wa pili, mechi hiyo iliyokuwa na presha kwa pande zote mbili kuanzia nje ya uwanja huku manahodha wakitambia uliweza kuleta burudani ya aina yake.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa mpaka inafikia dakika ya mwisho ya mechi hiyo Mabingwa watetezi Mchenga BBall Stars waliweza kuondoka kidedea kwa vikapu 70 dhidi ya 54 vya Portland.

Nusu fainali ya pili inatarajiwa kuwa wikiendi ijayo ambapo zitawakutanisha tena The Team Kiza akiwa mwenyeji kwa kumkaribisha Flying Dribblers kwa mchezo wa kwanza na Mchenga BBall Stars akiwa mwenyeji dhidi ya Portland.

Katika mchezo huo wa pili, timu itakayoshinda mfululizo itafanikiwa kuingia moja kwa moja katika hatua  ya fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 na mshindi wa michuano hiyo atajiondokea na kitita cha Milioni 10, mshindi wa pili akipata Milioni 3 huku mchezaji bora wa michuano (MVP) akibeba Milioni 2.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Sprite pamoja na kituo cha  runinga cha EATV na EA Radio ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Flying Dribblers dhidi ya The Team Kiza uliomalizika kwa Flying Dribblers kuibuka kidedea kwa vikapu 84 kwa 75.

MWISHO WA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA MAOMBI YA MKOPO ELIMU YA JUU NI LEO USIKU!

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuwa mfumo wa kupokea maombi ya mkopo kwa njia ya mtandao (https://olas.heslb.go.tz) utafungwa usiku wa leo, Jumanne, Julai 31, 2018.

Hata hivyo, waombaji ambao tayari wamejisajili katika mfumo na wapo katika hatua mbalimbali za maombi, wataruhusiwa kukamilisha maombi yao na kutuma nakala ngumu (hardcopies) za maombi ya mkopo kwa ‘EMS’ kupitia Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Tarehe ya mwisho ya kutuma fomu kwa ‘EMS’ ni Jumatano, Agosti 15, 2018 ili kutoa nafasi kwa HESLB kuchambua, kuhakiki, kupanga na kutoa orodha ya waombaji wenye sifa watakaopata mikopo kabla ya vyuo kufunguliwa.

Hadi kufikia leo, waombaji mikopo zaidi ya 76,000 wamewasilisha maombi yenye viambatisho vinavyotakiwa kwa njia ya mtandao. Maombi yote yatachambuliwa kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyotangazwa.

Uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo
Kuhusu kuwasilisha nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji wa mikopo na vile vya vifo vya wazazi waliofariki dunia, HESLB inafanya kazi kwa karibu na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambao wanakamilisha uhakiki wa vyeti vyote walivyopokea.

HESLB itapokea orodha kamili yenye majina ya waombaji wote wa mikopo waliowasilisha vyeti RITA kwa ajili ya uhakiki ili kuoanisha na taarifa zilizowasilishwa na waombaji kwa njia ya mtandao na nakala ngumu.

Hivyo basi, waombaji wote wa mikopo ambao hadi sasa hawajapokea taarifa za uhakiki kutoka RITA, wapandishe (upload) nakala laini walizonazo katika mfumo wa maombi (https://olas.heslb.go.tz) na kutuma nakala ngumu kwa njia ya ‘EMS’ kama ilivyoelekezwa.

Hitimisho
Pamoja na ufafanuzi huu, tunapenda kuwakumbusha waombaji wa mikopo wanaokamilisha maombi yao kuzingatia maelekezo yaliyomo katika ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa mwaka 2018/2019’. Mwongozo huu unapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz). Iwapo wana maswali, wawasiliane nasi kupitia:

Simu:0736665533 au 022 5507910
Barua pepe: 

Taarifa hii pia inapatikana kwenye tovuti ya HESLB 
 Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM

Serikali yaahidi kuufikisha mchezo golf nchi nzima

$
0
0
 Mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa huku serikali ikiahidi kushirikiana na wadau wa mchezo huo kuhakikisha unachezwa maeneo yote nchini ili utumike kutangaza sekta ya utalii zaidi. 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi mkoani Iringa, Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda alisema mashindano hayo yameonesha wazi kuwa endapo mchezo huo utasambaa zaidi katika maeneo yote hapa nchini yatavutia zaidi washiriki kutoka mataifa mbalimbali ambao pia watakuja kama watalii.

“Ni kupitia mashindano haya ndio nimeweza kugundua nguvu ya mchezo wa golf katika kutangaza utalii kwa sababu umeweza kuwavutia washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ni bahati mbaya tu kwamba kwasasa mchezo huu unachezwa kwenye mikoa michache sana hapa nchini tena ukitafsiriwa kuhusisha tabaka flani jambo ambalo si kweli,’’ alisema.

Aliongeza kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kwamba mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge yanakuwa ya kimataifa ili yavutie zaidi washiriki kutoka mataifa ya nje.

Mashindano hayo ya siku tatu yaliandaliwa na serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na yalihusisha washiriki zaidi ya 80 wakiwemo wachezaji wa kulipwa yaani ‘Professionals’ na washiriki wa kawaida yaani ‘Amateurs’ ambapo mchezaji Aidani Nziku kutoka klabu ya Golf ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam akiibuka mshindi wa jumla.

Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda (alieva jaketi la kaki) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 , mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi mkoani Iringa. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela 
Naibu Waziri wa Tamisemi, Bw Joseph Kakunda akionyesha ufundi wake kwenye mchezo huo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Bw Richard Kasesela nae akionyesha utaalamu wake kwenye mchezo huo.
Kapteni wa klabu ya Golf ya Mufindi Bw Glyn akionyesha umahili wake kwenye mchezo huo mbele ya wageni waalikwa.



JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA BENKI YA CRDB KUENDELEA KUBORESHA MAHUSIANO

$
0
0
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (wa kwanza kushoto) akizungumza na Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa wa Jeshi hilo, mikakati ya kudumisha uhusiano baina ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Benki ya CRDB, wakati wa kikao na Uongozi wa Benki ya CRDB, walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam.
 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Peter Mabusi, akifafanua jambo kwa Uongozi wa Benki ya CRDB, wakati wa kikao walipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (Wa kwanza kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei na (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage (watano kulia),  akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (mwenyesuti nyeusi), Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliombatana na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo na Viongozi Waandamizi wa Benki ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
habari na Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Former African Heads of State, Government and Business Leaders to discuss Financing for Sustainable Development in Kigali, Rwanda

$
0
0

The 5th African Leadership Forum (ALF), hosted by the former President of the United Republic of Tanzania, H.E. Benjamin William Mkapa and organised by UONGOZI Institute will take place in Kigali, Rwanda from Thursday 02nd August, 2018 to Friday 03rdAugust, 2018.

This year’s Forum, under the theme, “Financing Africa’s Transformation for Sustainable Development” seeks to provide a platform to deliberate on the prospect of increased, improved, and effective financing for Africa’s transformation.
“The meeting will provide an opportunity to learn from the successes and set-backs in national, regional and continental attempts to address specific financing challenges, and to put forward recommendations for unlocking increased financing for Africa’s development,” said Prof. Joseph Semboja, CEO of UONGOZI Institute.
The Keynote Address will be delivered by H.E. Paul Kagame, President of the Republic of Rwanda. Participants of the Forum will include H.E. Joaquim Chissano, former President of the Republic of Mozambique; H.E. Olusegun Obasanjo, former President of the Federal Republic of Nigeria; H.E. Armando Guebuza, former President of the Republic of Mozambique; H.E. Moncef Marzouki, former President of the Republic of Tunisia; H.E. Hassan Sheikh Mohamud, former President of the Republic of Somalia; and over 100 other distinguished leaders from the public sector, private sector, academia and civil society.
Speakers at the event will include Dr. Vera Songwe, Executive Secretary of UNECA, Dr. Donald Kaberuka, former President of the African Development Bank, Prof. Njuguna Ndung’u, former Governor of the Central Bank of Kenya and Dr. Mukhisa Kituyi, Secretary General of the United Nations Conference on Trade and Development and Amb. Dr. Yonov Frederick Agah, Deputy Director General, World Trade Organization.

The African Leadership Forum was conceived of as a space for Africa’s eminent elders to interact with current and future leaders around the strategic challenges facing the Continent. The annual meeting brings together former Heads of State as well as leaders from government, civil society, the private sector and academia from across Africa.

SEKTA BINAFSI,POLISI,IDARA YA MAHAKAMA ZADAIWA KUONGOZA KULALAMIKIWA KWA VITENDO VYA RUSHWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Ilala imesema taasisi za idara ya sekta binafsi, polisi na idara ya mahakama ndizo zinazoongoza kulalamikiwa zaidi kwa vitendo vya rushwa.

Amezitaja pia Tamisemi, Idara ya Afya, Wizara ya Ardhi, idara ya elimu na kampuni za bima.

Zainabu Bakari ambaye ni mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala,amesema hayo Leo Julai 31 ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya utendaji wao wa kazi kwa mwaka 2017/2018.

Amesema, katika kipindi hicho chote walichokitaja, Takukuru imeweza kupokea taarifa za rushwa 352 kwa njia mbali mbali zikiwamo njia za simu, barua na watu kufika ofisini.Amesema kutokana na taarifa hizo, majalada 25 yamefunguliwa na yana RB huku majalada 15 yakiwa tayari yamekamikika na majalada saba yamepokelewa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kuombewa kibali cha mashtaka.

Ameongeza kuwa, ni majalada manne tu ndio yamepata kibali cha DPP, na kesi mpya 12 zimeishafunguliwa mahakamani huku kesi walizoshinda zikiwa saba na kesi walizoshindwa ni tano.Zainabu ameeleza kuwa, Takukuru wanafanya udhibiti wa rushwa kwa kufanya uchambuzi wa mifumo na ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo ili kubaini mianya ya rushwa iliyopo katika taasisi na idara mbali mbali na katika matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.

Aidha ameshauri wakandarasi walipwe kwa wakati ili kumaliza tatizo la rushwa na kusema katika kipindi hiki wamefuatilia matumizi ya fedha ya maendeleo kwa uratibu wa Public Expenditure Trucking Survey(PETS) kwa idara za ujenzi na maji na kubaini kuwepo kwa ucheleweshaji wa maalipo ya wakandarasi.

Amewaasa Mwananchi pale wanapoona kuna dalili ama ushawishi wa rushwa mahali popote wasisite kutoa taarifa takukuru kwa kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo.

UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUUNGANISHA GESI ASILIA KWA MATUMIZI YA MAJUMBANI WASHIKA KASI

$
0
0
Ni miezi mitatu sasa tangu Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipozindua rasmi mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi asilia linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam na bomba la kipenyo kidogo linalotoka Ubungo kuelekea Mikocheni. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba alifafanua kwamba utekelezaji wa mradi huo unalenga kuongeza matumizi ya gesi asilia kwa jiji la Dar es Salaam kwa kuwaunganisha wateja zaidi wa matumizi ya majumbani na viwandani. 

Mradi huu unahusisha ujenzi wa msingi kwa ajili ya kusimika mtambo wa kupunguza mgandamizo, uunganishaji wa vipande vya mabomba, kuthibitisha njia ya bomba, uchimbaji na ulazaji wa bomba litakalochukua gesi kutoka bomba kubwa, uwekaji wa viainisho vya bomba linapopita na ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu kuvuka mto Ubungo. 

Akizungumza juu ya hatua za utekelezaji, Meneja Mradi Ndg. Denice Byarushengo alisema “mradi umepiga hatua kubwa na muhimu ambapo hadi sasa ujenzi wa msingi kwa ajili ya kusimika mtambo wa kupunguza mgandamizo umekamilika kwa asilimia 97%, uthibitisho wa njia ya bomba na zoezi la kuchimba mitaro kwa ajili ya mabomba umekalimilika kwa asilimia 76.8%, uunganishaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 88.6%, ulazaji na ufukiaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 56.9%, viainisho sita (6) vya bomba linapopita vimeshawekwa na ujenzi wa dara la waenda kwa miguu umekamilika kwa asilimia 90%”.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mha. Kapuulya Musomba (mwenye overall ya bluu) akijadiliana jambo na Ndg. Ildefons Mnimbo ambaye ni mtaalamu kutoka kampuni ya Plasco anaesimamia zoezi la kuunganisha mabomba, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara na lile la kutoka Ubungo kuelekea Mikocheni. 
Sehemu ya eneo la barabara ya Ubungo Maziwa inayochimbwa kitaalamu bila kuvunja barabara ili kuruhusu bomba la gesi kuvuka barabara hiyo. 
Bomba lenye kipenyo cha 315mm likiwa limelazwa katika mtaro tayari kufukiwa, hii ni sehemu ya bomba linalochukua gesi asilia kutoka kwenye bomba kuu linalotoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kuunganisha na bomba linalotoka Ubungo kuelekea Mikocheni. 

WAAJILI WATAKIWA KUTENGA CHUMBA MAALUM CHA KUNYONYESHEA.

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imewaagiza waajili wote wa Serikali na Sekta binafsi kutenga chumba maalum kwa ajili ya waajiliwa wao wanaonyonyesha.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.“Ninazitaka Halmashauri zote nchini kupitia maafisa kazi kuhakikisha wanawake waajiriwa waliojifungua wanapata haki yao ya likizo ya uzazi na muda wa kunyonyesha kwa ukamilifu” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amewataka Wanaume wanaopewa likizo za uzazi kuzitumia ipasavyo kwa kumsaidia mama kazi ili aweze kumnyonyesha mtoto mchanga aliyejifungua badala ya ktumia likizo hizyo kwenda kukaa baa.Waziri Ummy alisema kuwa vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya vinatekeleza vidokezo kumi vya kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama na hivyo kuwa rafiki wa Mtoto.

“Wazazi tunatakiwa kufuata taratibu za kunyonyesha ikiwemo kuanza kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja ya kwanza ya mama kujifungua, kunyonyesha mtoto mara kwa mara kadiri anavyohitaji, kuendelea kunyonyesha maziwa ya mama pekee bila kumpatia mtoto kitu kingine chochote hata maji katika miezi sita ya mwanzo na kuendelea kunyonyesha hadi anapofikisha umri wa miaka miwili au zaidi” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa takwimu za utafiti wa hali ya kidemografia na afya uliofanyika mwaka 2015 zinaonesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 0 hadi miezi 6 wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee.
“kila Mwajiri anatakiwa kumruhusu mfanyakazi mwanamke aliyejifungua kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi kwa jumla ya mpaka masaa 2 kwa siku kwa kipindi kisichopungua miezi 6 tangu kumaliza likizo yake ya uzazi” alisisitiza Waziri Ummy.

Kila ifikapo tarehe 1 – 7 Agosti ya kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama na maadhimisho yam waka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA NI MSINGI WA MAISHA.”


Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani kuhusu umuhimu wa kunyonyesha watoto wachanga wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pilia kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya afya mara baada ya tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya wakimsikiliza Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati akitoa Tamko kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

WAZIRI LUGOLA AMPA MIEZI MINNE LUGUMI

$
0
0
*Ni wa kufunga mashine Polisi, akishindwa Mahakama ya Mafisadi inamsubiri*

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametoa muda wa miezi minne kwa mmiliki wa Kampuni ya Lugumi ,Said Lugumi kuhakikisha anafunga mashine za utambuzi wa alama za vidole iwapo atashindwa ndani ya muda huo atampeleka Mahakama ya Mafisadi.

Lugola ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waaandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na Lugumi ambaye alijisalimisha ofisini kwake baada ya kuagiza aripoti Julai 31 mwaka huu.

Lugola ameeleza kuwa Lugumi aliwasili wizarani hapo kama walivyopanga na kuzungumza kuhusu mkataba aliongia na Serikali wa ufungaji wa mashine hizo na katika mazungumzo hayo amempa muda huo na amekubali.“Lugumi tumekubaliana ndani ya miezi 4 atakuwa amekamilisha kufunga mashine hizo na akishindwa katika kipindi hiki hicho ajue Mahakama ya Mafisadi inamsubiri.

“Mnafahamu Rais ameanzisha mahakama kwa ajili ya mafisadi na tangu kuanzishwa kwake bado ina uhaba wa wateja.Hivyo Lugumi akishindwa ajue atakuwa mteja wa Mahakama hiyo ambayo bado inahitaji watu,”amesema Lugola.Alipolizwa kwanini amezungumza na Lugumi na kisha kumruhusu aondoke badala ya kumuweka mahabusu,Lugola amejibu si kola jambo lazima mtu awekwe mahabusu.

Amesema kuwa katika mkataba huo Serikali ilishatoa fedha zake na hivyo kinachohitajika ni kufungwa kwa hizo mashine au fedha na Lugumi amekubali kufunga mashine na ndio maana amempa huo muda.

Kuhusu mkataba baina ya Lugumi na Serikali Lugola amesema kwanza mkataba huo unashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) na Wizara ya mambo ya ndani wanamshughulikia Lugumi kwa kutapeli jeshi la polisi kwa kutomaliza kazi aliyopewa ikiwa amelipwa.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images