Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

ZITTO KABWE APEWA SIKU MBILI AWE AMEJISALIMISHA KWA JESHI LA POLISI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kupitia Chama cha ACT Wazalendo ametakiwa kujisalimisha katika kituo chochote cha Jeshi la Polisi nchini.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ambapo amesema asipojisalimisha atasakwa kokote aliko.

Lugola amesema sababu za kumtaka Zitto kujisalimisha inatokana na kutoa kauli za uchochezi na kutoa lugha chafu dhidi ya viongozi wa nchini.

Amefafanua Zitto alitoa kauli hizo akiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Kilwa Abdallah Bunga maarufu kwa jina la Bwege.“Zitto ajisalimishe kituo cha Polisi Mkoa wa Lindi au kituo chochote cha Polisi nchini.Ametoa kauli hizo chafu kwenye jimbo ambalo kimsingi halimhusu.Hivyo amesema Lugola.

Pia ametoa agizo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro kuhakikisha anamchukulia hatua Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kilwa kwa kushindwa kumchukulia hatua Zitto akiwa katika wilaya hiyo.Wakati huo huo Lugola amewaonya wabunge wenye tabia ya kutoa lugha chafu na za uchochezi kwani hataacha hali hiyo ikaendelea na yoyote atakayethubutu atamchukulia hatua.

Amesema ni marufuku kwa mbunge yoyote kutoa lugha chafu, hata katika chaguzi ndogo zinazoendelea , uchaguzi wa mwakani na hata uchaguzi mkuu ujao.”Ni marufuku kwa mbunge yoyote kutoa lugha za uchechezi na katazo hili ni la mile na mile,”

SERIKALI KUKUZA UTALII KUPITIA MCHEZO WA GOLF – DK. KIGWANGALLA

$
0
0
Na Hamza Temba-WMU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itatumia fursa ya ujio wa Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus kutoka nchini Marekeni kubuni viwanja vya mchezo huo karibu na maeneo ya vivutio vya utalii nchini ili kuvutia watalii wengi wa kimataifa na hivyo kukuza pato la sekta hiyo.

Dk. Kigwangalla amesema hayo jana mara baada ya kumuaga mchezaji huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam alipokuwa akirudi nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku kumi yeye na familia yake katika vivutio mbali mbali vya utalii hapa nchini.“Tutatumia utaalamu na uzoefu wake kwenye mchezo wa Golf kwa kumtaka aje na kampuni yake atusaidie kutengeneza plan (mpango) ya kujenga viwanja vya golf.

“Amedesign viwanja zaidi ya 300 kwenye nchi zaidi ya 50 duniani na nchi hizo zimefaidika, amesema katika project zake zaidi ya asilimia 90 zinafanya vizuri pamoja na kwamba ni uwekezaji wa gharama kubwa bado imelipa kwa kiasi kikubwa na hakuna hata kiwanja kimoja kimepata hasara na vimekuwa vinasaidia kukuza utalii katika nchi hizo.

“Lengo letu ni kutengeneza ukanda maalum wa viwanja vya golf ambao utakuwa na viwango vya kimataifa na utavutia wacheza Golf kutoka nchi mbalimbali duniani, kwahiyo hii ni aina nyingine ya utalii wa watu wenye uwezo ambao wataleta pesa nyingi kwa wakati mmoja.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni zawadi ya kinyago cha Makonde walipoagana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuondoka kurudia kwao baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni na familia yake na uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Jaji Mst. Thomas Mihayo muda mfupi kabla ya ugeni huo kuondoka na kurudi kwao.

MKUU WA WILAYA KAKONKO AWATAKA VIJANA WASIKUBALI KUTUMIKA KUVURUGA AMANI

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewataka Vijana wilayani Kakonko wasitumiwe na watu wenye nia mbaya katika Kipindi hiki cha kampeni na wakati wa uchaguzi kuvuruga amani iliyopo.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza na vijana wa Bodaboda katika Kata ya Kasanda wilayani humo ambapo aliwataka vijana hao kufanya shughuli za maendeleo zitakazo waondoa katika umasikini na kuachana na watu wachache wenye lengo la kuvunja amani katika Wilaya hiyo kwa kuchochea vurugu.

Kanali Ndagala amesema vijana wengi wamekuwa wakitumika sana katika kipindi cha uchaguzi kufanya maandamano na vurugu mbalimbali wakitumiwa na baadhi ya wanasiasa wasio waaminifu, ambapo aliwaasa vijana hao kuwa wazalendo na kusikiliza wagombea wote ili waweze kuchagua mgombea atakaye wasaidia kuleta maendeleo.Mkuu huyo amesema Serikali haita mvumilia yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani katika Wilaya hiyo na atakayebainika anatumika vibaya hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Amesema lengo la Serikali ni kuona uchaguzi huo unaisha salama na kampeni zinazofanyika ni za kistaarabu kwa kuwa amani na utulivu ndio nguzo bora ya kuwafanya wananchi wafanye shughuli zao."Mpaka sasa hatujapata taarifa ya kuwepo na vurugu katika maeneo ambayo kampeni zinaendelea niwaombe vijana msikubali kutumika kuleta vurugu wakati huu fanyeni kazi ili muweze kujikwamua kiuchumi nguvu mnazo lazima mzitumie katika kuleta maendeleo," amesema Kanali Ndagala.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo amewataka vijana hao katika msimu mpya wa kilimo kila kijana kuwa na shamba ekari moja ya pamba ili kuweza kuinua uchumi wao kwa kuwa zao hilo ni moja kati ya mazao ya biashara katika Wilaya.Hata hivyo baadhi ya Vijana hao waliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo na kuomba serikali kuendelea kudumisha amani na usalama katika Wilaya hiyo.Thadeo Bitungwa ni moja kati ya vijana wajasiliamali amesema kwa sasa amani imeimalika tofauti na kipindi cha nyuma ambapo vijana wengi walikuwa wanatekwa na Kunyang'anywa bodaboda zao, kwa sasa vitendo hivyo havipo.Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Vijana wa Boda boda katika kata ya Kasanda mapema leo Wilayani Kakonko, kuhusu kukataa kutumiwa na watu wenye nia mbaya katika Kipindi hiki cha kampeni na wakati wa uchaguzi kuvuruga amani Wilayani humo.DC Ndagala amewataka vijana hao kujishughulisha na shughuli za maendeleo zitakazo waondoa katika umasikini na kuachana na watu wachache wenye lengo la kuvunja amani katika Wilaya hiyo kwa kuchochea vurugu.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA MAGEREZA YA MKOA WA KILIMANJARO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche mara baada ya kuwasili Gereza la Wilaya Same kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia leo Julai 31, 2018, Mkoani Kilimanjaro kabla ya kuendelea na ukaguzi katika magereza ya mwanga na Gereza Rombo. Lengo la ziara hiyo ni kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiongea na Maafisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Same alipotembelea gereza hilo katika ziara yake ya kikazi leo Julai 31, 2018(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche.
Maafisa na askari wa Gereza Same wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza(hayupo pichani) alipotembelea gerezani hapo katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (wa kwanza kushoto) akikagua nyumba ya askari inayojengwa kwa njia ya kujitolea katika Gereza la Wilaya ya Same. Nyumba hiyo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi familia nne za askari hivyo kutatua uhaba wa nyumba katika gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza la Wilaya ya Same alipotembelea gereza hilo kwa lengo la kukagua utendaji kazi pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo Mkoani Kilimanjaro leo Julai 31, 2018(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

BIASHARA MATANGAZO

KUTOKA KIBANDA CHA MSWANO LEO

$
0
0
 Muuzaji wa Utumbo wa Ng'ombe (jina lake halikupatikana kwa haraka) akimpimia mteja wake Utumbo kama alivyokutwa na kamera yetu mapema leo, eneo la Tandale kwa Mtogole jijini Dar es salaam.
 Utumbo ukiwekwa kwenye mizani ili kupata kipimo sawia.

NEWS ALERT: MKUU MPYA WA WILAYA YA HAI LENGAI OLE SABAYA AAPISHWA KILIMANJARO LEO

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini
MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira leo amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya katika hafla fupi ya kuapishwa kwa mteule huyo wa Rais Magufuli katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,Wakurugenzi,Makatibu tawala wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na ndugu na marafiki wa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Hai.
Mkuu mpya wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya akila kiapo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira (hayupo pichani) ,Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya akitia saini katika karatasi ya Kiapo mara baada ya kuapa kushika nafasi ya Ukuu wa wilaya ya Hai.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira (kushoto) akitia saini katika karatasi ya kiapo,mbele yake ni Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai Mhe. Lengai Ole Sabaya akishuhudia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya katiba ya Jamhuri ya Muungano muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu Mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya Ilani ya Chama cha Mapinduzi muda mfupi baada ya kuapishwa.

BREAKING NEWSSSS: Mfuko Mpya wa Hifadhi ya Jamii PSSSF Kuanza Kazi kesho Agosti Mosi Mwaka Huu

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-Maelezo, Dodoma
Serikali imetangaza rasmi kuanza kutumika kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma (PSSSF) kuanzia Agosti 1, mwaka huu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametangazaa leo jijini Dodoma.
Mhe. Mhagama amesema kuwa Serikali imekamikisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa Sheria ya PSSSF na imeridhika kwamba Mfuko huo unaweza kuanza kutekeleza majukumu yake, na kwamba kutokana na hatua hiyo wafanyakazi wote watakaoajiriwa katika sekta ya umma watasajiliwa katika Mfuko wa PSSSF na wale watakaoajiriwa katika sekta binafsi watasajiliwa katika Mfuko wa NSSF.
"Napenda kutangaza rasmi kwamba, kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha 1(1) cha Sheria ya PSSSF nimeteua tarehe 1 Agosti, 2018 kuwa ndiyo tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya PSSSF", alisisitiza mhe. Mhagama
Waziri Mhagama kaongeza kuwa Wanachama wote ikiwa ni pamoja na wastaafu na warithi waliopo katika mifuko inayounganishwa watahamishiwa katika mfuko wa PSSSF na haki na stahili zao zitaendelea kutolewa na mfuko huo bila kuathiriwa kwa namna yeyote ile.
Akizungumzia rasilimali, vitega uchumi, madeni, mifuko ya hiari na mikataba iliyokuwa chini ya mifuko inayounganishwa  Waziri Mhagama amesema itahamishiwa katika Mfuko mpya wa PSSSF. Pia Waziri Mhagama amewatoa hofu ya kupoteza ajira watumishi wote wa mifuko iliyounganishwa  kwa kuwa watahamishiwa katika mfuko mpya ambako uongozi wa mfuko huo utawapangia majukumu yao kwa kuzingatia muundo wa taasisi.
Amesema ili kuondoa sintofahamu Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi ya Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) imeandaa mkakati maalumu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu sheria na kanuni za PSSSF ili kuhakikisha kwamba wanachama na wadau wote wa sekta ya hifadhi ya jamii wanakuwa na uelewa sahihi wa sheria hizo na mabadiliko yaliyofanyika.
Mbali na hayo, Waziri Jenista ameteua wajumbe wa Bodi ya Mfuko huo ambao ni Bi. Leah Ulaya, Bw. Rashidi Mtima, Dkt. Aggrey Mlimuka, Bi. Stella Katende, Bw. Thomas Manjati, Bw. Henry Katabwa, Bi. Suzan Kabogo pamoja na Bw. Jacob Mwinula.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitangaza rasmi leo Jijini Dodoma tarehe ya kuanza  kufanya kazi kwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) ambapo mfuko huo unaanza kazi Agosti Mosi mwaka huu.Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera na Uratibu Prof. Faustine Kamuzora.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera  Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF)  unaanza kutekleza majukumu yake bila kuathiri huduma kwa wanachama wa mifuko iliyounganishwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma  (PSSSF) Bw. Eliud Sanga (katikati) akisisitiza kuhusu hatua watakazochukua kuhakikisha kuwa mfuko huo mpya unatatua changamoto zilizokuwepo awali katika mifuko iliyounganishwa kuunda mfuko huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera  Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza tarehe ya kuanza rasmi kufanya kazi kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa  Watumishi wa Umma(PSSSF) leo Jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa SSRA Dkt. Irene Isaka. Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO

TANZIA: MWANAHABARI SHADRACK SAGATI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI MKOANI GEITA

DC MJEMA AFUNGUA BARAZA LA UVCCM ILALA, APONGEZWA KUSHIRIKISHA VIJANA MBIO ZA MWENGE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefungua baraza la umoja wa vijana (UVCCM) katika kata zote za Ilala na kujadili masuala ya kimaendeleo ya jimuiya na chama.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mjema ameeleza kuwa baraza hilo litaleta maendeleo kama ilivyokuwa kwa wanawake wa Wilaya hiyo hasa ya kimaendeleo.

Aidha amewahaidi vijana hao mabadiliko na kuwataka wakae mkao wa kula kwani Agosti mwaka huu vijana wote wa Ilala maisha yao yatabadilika katika shughuli za kijasiriamali ambazo kama Serikali imejizatiti kuwahudumia.

Pia amewashauri vijana hao kuwa na nidhamu ili kwenda mbele zaidi na wafuate kanuni, taratibu na sheria sambamba na mshikamano na upendo.

Mjema amewashukuru vijana hao kwa ushirikiano wanaoonesha katika shughuli za kijamii.

Naye Mbunge wa Ilala na mwenyekiti wa kamati za Bunge Idd Azan Zungu amewashauri vijana katika kuwekeza na kufanya kazi kwa bidii na watumie asilimia 40 ya fedha iliyotengwa kwa vijana kuleta maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Pia mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani Ramadhan Mlawa amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa kushirikisha vijana katika shughuli za kijamii hasa katika kukimbiza mwenge wa uhuru  mwaka huu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau na vijana kutoka kata za kitunda, Chanika na Mchafukoge.

GULAMALI AHIDI KUTOA WASOMI MANONGA, ATOA FURSA KWA WANAFUNZI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali imeendelea kutoa hamasa kwa Wanafunzi wa Sekondari kwa kuwalipia Ada Wanafunzi wanaofaulu na kuendelea na Masomo ya Kidato cha Tano na Sita.

Akizungumza na Michuzi Blogu kuhusiana na namna anavyotoa hamasa hasa katika suala la elimu Jimboni humo Gulamali ameeleza kuwa licha ya kujenga na Kuboresha Shule za Kidato cha Tano na Sita Amekuwa na Utaratibu wa kuwalipia Ada kwa Wanafunzi wanaofanya vizuri katika Mitihani yao ya Kidato cha Nne kwa kupata Daraja la Kwanza na la Pili.

Ameeleza kuwa ni Mwaka wa 3 sasa anawalipia Wanafunzi wote wanaofaulu kidato cha Nne kwenda Cha Tano na Mwaka huu zaidi ya Wanafunzi 140 wamenufaika na kusomeshwa na ofisi ya Mbunge, utaratibu huo umekuwa unatoa hamasa zaidi kwa Wanafunzi walioko Mashuleni  kwa kuweka juhudi zao katika masomo ili nao waweze kunufaika.

Akieleza malengo ya fursa hiyo Gulamali amesema kuwa suala la Elimu katika Jimbo la Manonga ni la muhimu na amedhamiria kuzalisha wasomi wengi zaidi kutoka Jimboni humo na ametoa wito kwa wanafunzi kutumia fursa zinazotolewa na Serikali ili kuweza kufikia malengo.Utaratibu huu umekuwa Kivutio hamasa kwa Wanafunzi kusoma zaidi na kupata nafasi hizo za Mbunge, lakini pia umewasaidia Wazazi ambao  hushindwa kumudu Gharama za Watoto wao wanapochaguliwa  kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano hali inaowalazimu watoto hao kukatisha Masomo yao.

Miezi kadhaa iliyopita Gulamali alifungua shule ya Sekondari Ziba kwa ajili ya kidato cha Tano na Sita na bado Ujenzi wa Shule nyingine nyingi unaendelea na hii ni katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Serikali kwa kuendelea na Ujenzi wa Shule za  Sekondari kwa Kidato cha Tano na Sita kwa kila Tarafa.

UWANJA WA NDEGE WA TERMINAL III KUANZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKANI

$
0
0
Na Ripota wetu, Globu ya Jamii
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe leo amefanya ziara ya mafunzo na ukaguzi wa Jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha  kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara hiyo Waziri Kamwelwe amesema amefurahishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kwamba anaamini akifika kwa awamu ya pili mambo yatakua mazuri zaidi. Amesema kuwa kufikia mwakani mwezi mei abiria wataanza kutumia uwanja wa Terminal 3.

"Nimefurahishwa sana na hatua ambayo ujenzi umefikia, kiwanja hiki kimejengwa kwa ubora wa kimataifa na miundombinu pamoja na vifaa vitatakavyo tumika katika jengo hili vitakua ni vya kisasa zaidi ambavyo viwanja vyote vya kimataifa hutumia", alisema Waziri Kamwelwe.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha JNIA Mhandisi Paul Rwegasha ameeleza kuwa kukamilika kwa jengo la tatu la abiria kunakuja na faida nyingi za kiuchumi kwa Taifa na mwananchi mmoja mmoja.

"Ukamilishwaji wa jengo hili la tatu la abiria katika Kiwanja Cha Kimataifa cha Julius Nyerere kutafungua milango mingi ya kiuchumi, serikali itaweza kupata mapato kupitia kodi za huduma mbalimbali zitakazo tolewa katika jengo hili, wananchi watapata ajira, wawekezaji wataongezeka na watalii pia", alisema Bwana Rwegasha.

Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha JNIA ameweka wazi kwamba, tayari mchakato wa kumpata mzabuni kwa ajili ya maandalizi ya kuhamia katika jengo la tatu la abiria na wazabuni kwa ajili ya upangaji wa maeneo ya huduma zitakazo patikana ndani ya jengo unaendelea.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe akizungumza na viongozi wanaosimamia mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati wa ziara yake aliyoifanya uwanjani hapo leo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA), Paul Rwegasha akizungumza kuhusu usimamzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Wolfgang Marschick akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria wakati wa ziara ya kwanza ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe akizungumza wakati alipokuwa anatembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kujionea ujenzi unavyoendelea.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe(wa pili kushoto) wakazi wa ziara ya kutembelea  mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la III  la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKAZI WA KANDA YA ZIWA SASA KUJISHINDIA MAMILIONI NA PEPSI.

$
0
0


Kampuni ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi aina ya Pepsi, Mirinda, 7up, Mountain Dew na Evervess, Mkoani Mwanza wanayo furaha kuwaletea Shindano kabambe litakalojulikana kwa jina la“Jishindie Mamilioni ” Shindano hili litahusu soda aina ya Pepsi, Mirinda Orange, Mirinda Fruity, Mirinda Lemon, 7Up za ujazo wa mililita 350, na Mountain Dew (300ml).

Shindano hili litatangazwa Katika Radio, Magazeti, Mabango na Vipeperushi mbalimbali. Madhumuni ya kuwaletea shindano hili niKuboresha hali ya maisha ya wateja wetu wa kanda ya Ziwa kwa kuwapatia zawadi za fedha taslimu ili kuwawezesha kujikomboa kiuchumi.Shindano hili litaendeshwa Kwa muda wa wiki sita kuanzia tarehe 01/08/18 hadi 16/09/18 katika mikoa ifuatayo: Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Tabora, Geita, Kigoma na Kagera. 
Kutoka kushoto ni Phocas lusato Meneja Rasilimali watu SBC, akifuatia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Hussein Mkwawa ambaye ni Meneja mauzo Kanda ya Ziwa wakisikiliza vyema maswali ya waandishi wa habari (hawako pichani) katika utambulisho rasmi wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
Balozi wa PEPSI Albert G. Sengo (kulia) akitoa maelezo kwa wawezeshaji SBC, anayemsikiliza mbele yake ni Meneja Mauzo kanda ya Ziwa Hussein Mkwawa, Meneja Mafunzo na Uwezeshaji SBC Tanzania Limited Rashid Chenja na Meneja Rasilimali Watu Phocas Lusato katika utambulisho wa shindano la Jishindie Mamilioni, uliofanyika ukumbi wa mikutano SBC Nyakato jijini Mwanza.
Nikama wakisemezana "Hebu tuone umepata nini ndani ya kizibo chako...." Balozi wa PEPSI Albert G. Sengo (kushoto) Sara Onesmo kutoka Clouds Tv na Johari Shani wa Mwananchi Communication.
Shindano hili la“Jishindie Mamilioni” litakuana vizibo vya rangi ya Silva. Shindano hili litakua na zawadi nyingi za pesa taslimu kuanzia shilingi za Kitanzania 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5000/-, 1000/= na SODA YA BURE.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI LUGOLAAKUTANA NA WADAU WA USAFIRI NA USAFIRISHAJI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, na Ajira, Mhe Antony Mavunde, alipokua akiwafafanulia jambo wadau wa usafiri na usafirishaji kuhusu jinsi ya kupambana na ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwa Waziri Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akifafanua jambo kwa wadau wa Usafiri na Usafirishaji jinsi ya kupambana na ajali za mara kwa mara nchi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri Kangi Lugola wa wizara hiyo akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw Kailima Ramadhani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimsikiliza Omari Mponda, Kaimu Rais Chama cha Wasafirishaji Tanzania akichangia jambo jinsi wadau hao wanavvyoweza kushirikiana na wizara hiyo katika kupambana na ajali za barabarani .. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, na Ajira, Antony Mavunde. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.

KIGAMBONI WAPONGEZWA KWA KUJENGA OFISI YA KISASA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo amewapongeza wilaya na Manispaa ya Kigamboni kwa kuanza ujenzi wa Ofisi za Kisasa.

Waziri Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya za Manispaa ya Kigamboni. Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi unaoendelea wilayani humo unaojengwa na Wakala wa Majengo(TBA) chini ya mkandarasi Mshauri kutoa Chuo cha Ardhi.

Jafo amewataka wakandarasi kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda ili watumishi wa Manispaa ya Kigamboni wapate maeneo mazuri ya kufanyia kazi. Naye, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando amemuhakikishia Waziri Jafo kwamba viongozi wote wa Kigamboni wamejipanga vyema ili ujenzi huo ukamilike ndani ya muda uliopangwa. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kigamboni katika eneo la ujenzi wa majengo ya Ofisi ya Mkuu wa wilaya na Halmashauri ya Kigamboni.
Kazi ya ujenzi inavyoendelea kigamboni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akiendelea na zoezi la ukaguzi wa jengo la Manispaa ya Kigamboni.
Ukaguzi wa maendeleo ya jengo la Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kigamboni.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE

NHIF KUPIMA BURE MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA MAONESHO YA NANENANE MKAONI SIMIYU

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kupata huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyaombukiza katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwenye Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane yatakayofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi. 

Mhe. Mtaka ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) lililopo Uwanja wa Nananenane kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi. 

Amesema NHIF itatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti, kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza bure , hivyo hii ni fursa wananchi wa mkoa huo kwa kuwa itawapunguzia gharama waitumie vizuri. 

Wakati huo huoMtaka ametoa wito kwa wananchi mmoja mmoja na vikundi vikiwemo vyama vya ushirika zaidi ya 390 mkoani humo kujiunga nakuwa na kadi za Bima ya Afya, ili waweze kuwa na uhakika wa kupata huduma wakati wowote na kupunguza gharama za matibabu. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi. 
Meneja Masoko na Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Hilipoti Lello akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la maonesho la Mfuko huo, lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari jengo la maonesho la mkoa huo, lililojenhgwa katika Uwanja wa Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi leo, ambalo lipo katika hatua za ukamilishaji. 

MAFUNZO YA UONGEZAJI THAMANI WA VIAZI LISHE YAFANA SUGECO MOROGORO

$
0
0
Washiriki wa Mafunzo ya Uongezaji Thamani Viazi Lishe kutoka mikoa mbalimbali nchini,wakionesha mikate na mandazi waliyotengeneza kwa kutumia urojo wa viazi hivyo pamoja na unga wa ngano wakati wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika Ushirika wa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (Sugeco). Washiriki hao walifundishwa mambo mbalimbali ikiwemo uandaaji wa shamba, kupanda, uangalizi, mavuno, biashara pamoja na faida ya viazi hivyo vyenye wingi wa vitamini A. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sugeco, Revocatus Kimario.

Kuanzia leo naahidi kuwaletea yaliyojiri wakati wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa na walimu makini na wenye weledi mkubwa kuhusu zao hilo.MWANDAAJI RICHARD MWAIKENDA
Washiriki wakipata maelezo kuhusu mfano wa kilimo cha umwagiliaji kinachotumi matone katika eneo la Segeco, Sua Morogoro.
Wakitembelea Dryer inayotumia Nishati ya jua
Richard Mwaikenda akiangalia aina ya mbegu ya viazi lishe ya mataya katika bustani iliyopo Sugeco. Kushoto ni Mtaalamu wa Viazi Lishe, Jolanta Joseph
Mwalimu wa mafunzo hayo, Jolanta akitoa maelezo ya kuzingaatia wakati wa kutengeneza juisi.

SERIKALI YAWALILIA WANAFUNZI WA KIMBIJI WALIOFARIKI WALIPOKUWA WAKIOGELEA

$
0
0
SERIKALI imesikitishwa na vifo vya wanafunzi wanne ambao ni wasichana wa kidato cha nne kutoka shule ya sekondari Kimbiji iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam waliofariki kwa ajali ya maji walipokuwa wakiogelea katika bahari ya Hindi.

Vifo vya wanafunzi hao vilitokana na sherehe iliyoratibiwa na shule husika ili kuwapongeza wanafunzi hao wa kidato cha nne baada ya kufanya vyema mitihani yao ya kujipimAkizungumza kwa majonzi shuleni hapo,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amesema serikali imepokea kwa masikitiko vifo hivyo na kutoa pole kwa wanafunzi, wazazi, na walimu wa shule hiyo kwa msiba huo mzito.

Waziri Jafo amewataka walimu wote nchini kujiepusha na ufanyaji wa sherehe za wanafunzi katika mazingira hatarishi. Aidha, Waziri Jafo aliwasilisha rambirambi kwa familia nne za wafiwa.Wanafunzi waliofariki dunia ni Secilia Ernest Paulo, Selestina Vitus Malipesa, Agnetha Philipo Mlaki na Queen Leonard Mandala.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa pole kwa shule ya sekondari ya Kimbiji katika maombolezo ya vifo vya wanafunzi wanne.tika huzuni kubwa ya kifo cha wenzao wanne
Wanafunzi wa sekondari ya Kimbiji wakiwa katika huzuni kubwa ya kifo cha wenzao wanne
Watumishi wa Kigamboni pamoja na wazazi walipoungana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo kwenye maombolezo ya vifo vya wanafunzi wanne.

KANGI LUGOLA, WAZIRI WA CANADA WAJADILI MASUALA YA WAKIMBIZI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsindikiza Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa nchini Canada, Ahmed Hussein, mara baada ya kumaliza kikao chao kilichojadilia masuala mbalimbali ya Wakimbizi pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Canada. Katika kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa nchini Canada, Ahmed Hussein (wapili kushoto) alipokua akimfafanulia jambo katika kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo, viongozi hao walijadili masuala ya mbalimbali ya Wakimbizi pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Canada. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Watatu kushoto ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles, na kushoto ni Kansela wa Masuala ya Uhamiaji wa Balozi huo hapa nchini, Erin Brouse. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa nchini Canada, Ahmed Hussein (wapili kushoto). Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam leo, viongozi hao walijadili masuala ya mbalimbali ya Wakimbizi pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Canada. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Watatu kushoto ni Balozi wa Canada nchini, Ian Myles. Na kushoto ni Kansela wa Masuala ya Uhamiaji wa Balozi huo hapa nchini, Erin Brouse. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images