Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200

$
0
0
WAFANYABIASHARA wa Soko la Mabibo, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati na kuzuia mpango wa manispaa kuwaondoa wafanyabiashara hao na kuwahamishia Soko la Simu 2,000.

Akizungumza na waandishi wa habari Mmoja wa Wafanyabiashara George Mligo alisema, viongozi wa Manispaa ya Ubungo wamewataka wahame katika soko hilo ambalo linauza mazao na matunda mbalimbali.Mligo alisema wanamuomba Rais Magufuli aingilie kati sakata hilo ili kupata ufumbuzi. Mligo alisema, awali waliambiwa watapelekwa soko la Makuburi lakini baadae walipewa taarifa kuwa eneo hilo lipo karibu na mto hivyo wanapaswa kuhamishiwa Soko la Simu 2,000 ambalo ni dogo.

Alisema katika soko la Mabibo kuna zaidi ya wafanyabiashara 4,000 ambao wanauza viazi, ndizi, nyanya, vitunguu, matunda na mbogamboga.“Kilio kikubwa tulichonacho wafanyabiashara wa soko la Mabibo, Serikali imeshindwa kututafutia soko lenye hadhi ya Kimataifa kama walivyoahidi na kinyume chake wanataka kutupeleka soko la Simu 2000 ambalo haliwezi kupokea zaidi ya watu 1,500 huku sisi hapa tupo zaidi ya 4,000,” alisema.

Mligo alisema, mchango wa soko hilo kwa mwezi ni zaidi ya Sh. Milioni 120 hivyo kitendo cha manispaa kuwaondoa katika eneo hilo kitapoteza fedha nyingi.Akizungumzia kadhia hiyo Mfanyabiashara Swadaka Magesa alisema, hawapo tayari kuhama katika soko hilo kwani hoja za Serikali hazina mashiko kwa sasa hasa kwa kukosa eneo ambalo linaweza kuwatosha.Magesa alisema iwapo watapatiwa eneo lenye sifa ya kupokea wafanyabiashara zaidi ya 4,000 na magari 130 kwa wakati mmoja watahama kwani wanaamini watafanya biashara kwa uhuru.“Kusema kweli Simu 2,000 sio sehemu sahihi ya sisi kuhamia kwani hata vitengo viwili haviwezi kuingia kwani eneo ni dogo hadi tunawaita tumeandika barua hadi kwa Rais Magufuli kumuomba aje kuona hali hii ili atusaidie,” alisema.

Akizungumzia sakata hilo Meya wa Manispaa hiyo Boniface Jacob, alisema, sio kwamba wanawahamisha ila ni mwenye eneo ambaye ni Kiwanda cha Urafiki kuhitaji eneo lake.“Sio kwamba tunawahamisha, Urafiki wanataka eneo lao ambalo wanalimiliki kisheria sasa sisi tufanyeje.“Eneo ambalo tunaweza kuwahamishia ni Simu 2,000 kwani manispaa haina maeneo, lakini naomba umtafute Mkurugenzi ataeleza kila kitu,” alisema.Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo simu yake iliita bila kupokelewa na baadae alituma ujumbe kuwa hawezi kuzungumza.
Mmoja wa Wafanyabiashara wa Soko la Mabibo George Mligo akieleza kwa hisia juu ya kuchukizwa na zoezi la wao kutolewa katika soko hilo 


SAFARI YA KWANZA YA NDEGE YA BOEING 787-8 DREAMLINER MIKOA YA KILIMANJARO NA MWANZA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano, Dkt. Leonard Chamuriho akishuka katika ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoanza rasmi shughuli zake rasmi leo Jumapili Julai 29, 2018 kwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro. Anayemlaki ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira na baadhi ya Watendaji wengine wa Sekretarieti ya Mkoa huo.

 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akisalimiana na mmoja wa Marubani wa ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner wakati ndege hiyo ilipokuwa ikianza rasmi kazi zake leo jumapili Julai 29, 2018. Ndege hiyoitaanza kufanya  safari zake katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe akizungumza na Watendaji, Watumishi na Wananchi mbalimbali waliohuduhuria katika hafla ya kuanza kazi kwa ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoanza kazi zake leo Jumapili Julai 29, 2018. Kushoto ni Mkoa wa Mwanza John Mongella, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo.

 . Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho akisalamiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira muda mfupi baada ya kushuka katika ndege ya Serikali ya Boeing 787-8 Dremaliner iliyoanza safari zake leo Jumapili Julai 29, 2018. Ndege hiyo itaanza kufanya safari zake katika Mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro. 


Mhudumu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), akitoa maelekezo kwa abiria waliopanda ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dremaliner muda mfupi kabla ya kuondoka Jijini Dar es Salaam kuanza safari zake nchini kwa kuanzia na Mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Mwanza na Dar es Salaam.

(PICHA NA MAELEZO)   


DK.SHEIN AAGANA NA BALOZI WA KUWAIT ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa 
Kuwait katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jasem Ibrahuim Al-Najem alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Kuwait katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jasem Ibrahuim Al-Najem alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini,[Picha na Ikulu.] 29/07/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Balozi wa Kuwait katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jasem Ibrahuim Al-Najem alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais, baada ya mazungumzo yao ambae amemaliza muda wake wa kazi Nchini

GEREZA LA KWITANGA KUWA KITUO KIKUU CHA MICHIKICHI-MAJALIWA

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeliteua Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa zao la michikichi nchini.

Hivyo ameuagiza uongozi wa gereza hilo waongeze nguvu katika uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha michikichi na kupanda miche mipya ya michikichi na kukata ya zamani.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati alipotembelea gereza hilo akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma.

Amesema Serikali imedhamiria kwa dhati kufufua kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma, hivyo kila mwananchi lazima awe na shamba la michikichi.Katia hatua nyingine, Waziri Mkuu ameuagiza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma Bw. Sabas Matolo kuhakikisha Gereza la Kwitanga linawezeshwa kwa kuwa na zana bora na za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na vifaa vya kuvunia ili waweze kuongeza uzalishaji wa mafuta.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Matolo awahamishe askari ambao ni wataalamu wa kilimo wenye ujuzi wa zao la michikichi kutoka kwenye Magereza mengine mkoani Kigoma na kuwahamishia katika gereza la Kwitanga ili kuimarisha uzalishaji.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mazao ya michikichi yaliyokuwa yakikamuliwa kuwa mafuta ya kula wakati alipotembelea Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma kujionea kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta ya mawese katika gereza hilo Julai 29, 2018. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojiwa na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kitalu cha kuzalisha miche ya Michikichi cha Asasi ya Seed Change katika kijiji cha Simbo kwenye jimbo la Kigoma Vijijini Julai 29, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo, Alex Chetkovic.
Wananchi wa Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama kijijini hapa kuwasalimia Julai 29, 2018. Alikuwa njiani kwenda Uvinza kuendelea na ziara ya mkoa wa Kigoma. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza alipokuwa safarini kwenda Uvinza akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Julai 29, 2018.

Serikali kuendelea kujenga miundo mbinu ya barabara kuwawezesha wakulima kuyafikia masoko.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kujenga miundo mbinu ya barabara hasa za ndani kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kuyafikia masoko.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. “Serikali imetoa shilingi bilioni 6 kujenga barabara ya Rujewa – Ubaruku inajengwa kwa kiwango cha lami”

Makamu wa Rais ameipongeza kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd kwa kujenga kituo cha afya kitakacho hudumia watu zaidi ya elfu kumi na kulaza wagonjwa 42 kwa wakati mmoja. Aidha Makamu wa Rais amesema migogoro yote itafanyiwa kazi kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mmoja.

Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mhe. Haroon Pirmohamed ameahidi kuwalipia deni la shilingi milioni 800 wakulima wanaodaiwa deni waliokupa kununulia power tila .Mbunge huyo wa Mbarali amesema kuwa Serikali ya awamu imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Akizungumza na Wananchi wa Kapanga katika mkutano huo, Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameahidi kutoa mifuko 200 kutoka kwenye Taasisi yake ya Tulia Trust kusaidia ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika kituo cha Kapanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele unaozalishwa na kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd , kulia ni Mkuu wa kampuni hiyo nchini Bw. Nillard Chawdry akimpa maelezo Makamu wa Rais namna wanavyotumia teknolojia ya kisasa katika kukoboa na kufungasha mpunga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akihutubia wananchi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Kapunga,pichani kushoto ni Mkuu wa kampuni ya Kapunga Rice Project Ltd Bw. Nillard Chawdry.Kituo hicho kimejengwa na Kapunga Rice Project Ltd kitakacho hudumia watu zaidi ya elfu 10 na kulaza wagonjwa 42 kwa wakati mmoja. Kituo cha Afya Kapunga ambapo Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi .Sehemu ya Wakazi wa kijiji cha Kapunga waliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WASAMBAZAJI WA PEMBEJEO 'PETROBENA' WAANZA KUTEKELEZA KWA VITENDO AGIZO LA JPM

$
0
0
Kampuni ya usambazaji ya Pembejeo ya PETROBENA EAST AFRICA LTD imeanza kuunga mkono kwa vitendo Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungwano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha wanafikisha pembejeo za kilimo kwa wakati kwa wakulima nchini.

Akiongea leo mkoani Morogoro katika mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kwa maafisa kilimo na wasambazaji wa pembejeo,Mkurugenzi wa Kampuni ya PETROBENA Peter Kumalilwa amesema wameamua kuweka Ghala kubwa mkoani Morogoro ili kuhakikisha wakulima wa mkoa huo na mikoa jirani wanapata pembejeo kwa haraka kupitia wauzaji wadogo na wakubwa.

Kumalilwa amesema PETROBENA ikiwa wakala mkuu wa kampuni ya Mbolea ya YARA watahakikisha mbolea inapatikana katika katika kipindi chote na siyo kama ilivyo sasa katika maeneo mengi ambapo mbolea inaanza kupelekwa wakati wa msimu hali inayosababisha kuchelewa kutokana na ubovu wa miundo mbinu pamoja na umbali wa walipo wahitaji.

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Morogoro wanatarajia kuwa na wauzaji wa pembejeo wapatao 700 katika wilaya zote sita ambao watapewa mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo itakayowasaidia kuwapa elimu wakulima wa mazao mbali mbali mkoani humo wakiwemo wa Miwa,Mpunga,Mahindi,Mboga mboga na mazao mengine.

Naye Afisa Biashara wa kampuni ya YARA nyanda za juu kusini John Meshak amesema wameamua kuzindua ghala la mbolea Morogoro kwa kuwa kuna wakulima wengi wanaolima mazao mengi ila hawapati nafasi ya kupata mbolea bora na kwa wakati hali inayopunguza kasi ya uzalishaji wa mazao yao.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA LIMITED Peter Kumalilwa mipango ya kampuni hiyo katika kumkwamua mkulima wa Tanzania.
Mtaalamu wa kilimo kutoka kampuni ya YARA Maulid Mkima akitoa darasa la kwa maafisa kilimo na maafisa wa pembejeo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi mpya ya PETROBENA mkoani Morogoro.Picha zote na William Bundala.
Maafisa Kilimo na Wauzaji wa Pembejeo kutoka wilaya za mkoa wa Morogoro wakiwa makini katika mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo na umuhimu wa kutumia mbolea.

HIVI NDIVYO MAMBI YALIVYOKUWA BAGAMOYO MARATHON 2018

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala (wa pili kulia) akiwa ameambatana pamoja na wakimbiaji wengine wakati wakihitimisha mbio za 21 KM katika Bagamoyo Historical Marathon, iliyofanyima mapema leo, Bagamoyo Mkoani Pwani. Dk. Kigwangala ndiye alikuwa Mgeni rasmi katika mashindano hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala akipongeza na baadhi ya washiriki wenzake baada ya kumaliza mbio za 21 KM katika Bagamoyo Historical Marathon, iliyofanyima mapema leo, Bagamoyo Mkoani Pwani.
 Baadhi ya Washiriki wa mbio za Kilometa 21 katika Bagamoyo Historical Marathon wakianza kuondoka katika uwanja wa Shule ya Bagamoyo.
 Mdau Godwin Semunyu wa Benki ya CRDB akiwa na mmoja wa washiriki wenzake katika Bagamoyo Historical Marathon, iliyofanyima mapema leo, Bagamoyo Mkoani Pwani.

Kanisa la Waadiventista Wasabato laishukuru TaSUBa

$
0
0
Na Sophia Mtakasimba(TaSUBa)
KANISA la waadiventista Wasabato Tanzania limeishukuru Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kutoka nafasi kwa wanamuziki wa kanisa hilo kujifunza Muziki katika taasisi hiyo,kupitia program maalumu ya Kozi fupi ya Muziki ya mwezi mmoja  iliyoanza tarehe 1 Julai na kuhitimishwa leo.



Akizungumza katika ufungaji wa program hiyo uliofanyika leo  katika ukumbi wa TaSUBa Bagamoyo, Mhazini wa kanisa la wasabato kutoka Jimbo  la Kusini mwa Tanzania ,Mchungaji January Athanas Sigome amesema kuwa kanisa linaishukuru Sana TaSUBa kwa kutoa nafasi kwa  Waimbaji ,Viongozi na watunzi wa nyimbo kutoka makanisa ya Waadventista wasabato,kujifunza Muziki na anaamini wahitimu wataenda kuwa chachu ya mabadiliko katika makanisa yao.


 Aliongeza kuwa kanisa liliamua kushirikiana na TaSUBa kuendesha program hiyo ili kuwafanya watenda kazi wake wajifunze muziki na kuweza kurejesha heshima ya ibada kwa Mungu kama ilivyo katika maandiko matakatifu ,maana katika nyakati za sasa kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa juu ya namna bora ya kurejesha ibada ya sifa kwa Mungu.



Aidha Bw.Sigome alisema kuwa kanisa limeichagua taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)kwa kuwa ndio sehemu pekee yenye wakufunzi wenye weledi wa kutosha pamoja na vifaa vya kufundishia vya kutosha.


Nae Leonard Busee ambaye ni mhitimu wa program hiyo amesema kuwa wakiwa TaSUBa wamejifunza mambo mengi ambayo awali walikuwa hawayajui ikiwemo upigaji wa vyombo vya muziki,Falsafa ya muziki ,kusoma muziki pamoja na ufundi wa sauti


Nae mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema kuwa ,kozi hiyo maalumu ni miongoni mwa program  mbalimbali ya kimafunzo ambayo TaSUBa inatoa kwa makundi maalumu kulingana na mahitaji yao.Pia kozi za muda mrefu za Stashahada na Astashahada  katika  fani za mbalimbali zinaendelea kutolewa na sasa milango ipo wazi kwa wanaohitaji kutuma maombi ya kujiunga na chuo.
Mhitimu mwenye umri mdogo kuliko wote , msichana Naomi Yonazi akipotea cheti cha ushiriki wa program maalumu ya muziki.
 Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye (wa pili kushoto), pamoja na Mhazini wa kanisa la waadventista wasabato Jimbo la  kusini mwa Tanzania Mchuganji January Atanas Sigome (anayefuata baada ya Dkt.Makoye ), wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa program maalumu ya mafunzo ya muziki .

 Wahitimu wa Programu maalumu ya mafunzo ya muziki  wakiimba katika hafla ya ufungaji wa mafunzo.
Wakufunzi wa TaSUBa walioendesha  program  maalumu ya mafunzo ya muziki wakiwa katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Heri Kaare,Rhoda Mitanda,Peter Zengo,Melkiades Banyanka na John Sagati.

LTSP YAPONGEZWA KWA KUTATUA KERO ZA ARDHI MOROGORO

$
0
0
Mradi wa kuwezesha umilikishaji wa ardhi LTSP, umepongezwa kwa kufanikiwa kutatua kero ya migogoro sugu thelathini na tano ya ardhi iliyodumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi na tano  na kusababisha vifo, majeruhi na upotevu wa mali.

Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Charles Kabeho wakati wa zoezi la ugawaji wa hati 3,063 za kimila kwa  wanavijiji wa vijiji vya Igima na Mpofu vilivyoko kata ya Mbingu,wilaya ya Kilombero mkoani morogoro.

“Napenda kuishukuru serikali kupitia mradi wa upimaji na urasimishaji ardhi(LTSP) chini ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutatua migogoro hiyo kwa kupima ardhi,kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi na utoaji wa hati za kimila,”alisema.

Aliongeza tangu mradi huo wa majaribio ufike kwenye wilaya tatu za Malinyi,Ulanga and Kilombero,migogoro hiyo imekomeshwa kwa kufanya uratibu mzuri wa masuala ya ardhi.
                                                                  
Kwa mujibu wa kiongozi huyo,hati hizo za kimila zitawasaidia wanavijiji hao kupata mikopo na kuhuisha thamani ya ardhi zao tofauti ilivyo awapo awali.
 Mratibu wa mradi wa Mradi wa LTSP Godfrey Machabe akisoma taarifa ya mradi kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Charles Mabeho (Hayupo pichani) baada ya Mwenge kuwasili katika kijiji cha Igima Kata ya Mbingu Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Mabeho akimkabidhi Hati ya Kimila mkazi wa kijiji cha Igima katika hafla fupi iliyofanyika mara baada ya Mwenge kuwasili kijijini hapo. 
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Mabeho akipata maelezo kutoka kwa kiongozi wa kazi za uwandani wa mradi wa LTSP Swagile Msananga baada ya Mabeho kufika katika banda la LTSP 
Charles Mabeho akiwa na viongozi wa wilaya ya Kilombero, Mratibu wa mradi wa LTSP na wananchi waliojitokeza kuupokea Mwenge wakicheza muziki uliokuwa ukiimbwa na Mrisho Mpoto (hayupo Pichani).


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VUNJO WAZINDUA TAASISI YAO ,ITASHUGHULIKA NA MIUNDOMBINU YA BARABARA,ELIMU,AFYA NA MAJI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini , Baba Askofu Dkt Martin Shao amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo itayoshughulika na kutatua kero katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ,Elimu ,Afya na Maji.

Kwa kuanza taasisi hiyo imepanga kuanza matengenezo ya barabara katika vijiji vyote Vilivyoko katika Jimbo la Vunjo ,barabara ambazo zinakadiliwa kuwa na urefu wa Km 272.8 ambazo zitagharimu kiasi cha Sh Bil 7 na Mil 290.Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo uliofanyika katika kata ya Mshiri ,Marangu wilaya ya Moshi ,Katibu wa Bodi ya taasisi hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia amesema Vunjo litakuwa jimbo la kwanza kufanya tukio hilo.

“Mzigo huu tulionao utakuwa mwepesi tukiw ana raha kwenye nafsi zetu ,na tunataka tuongoze kama wana vunjo hili liwe jimbo la kwanza Tanzania kwa watu wake kuwa na raha bila ya kuwa na bughdha za aina yoyote”alisema Mbatia.Alisema tukio la kuleta viongozi wa Dini pamoja ,viongozi wa vyama vya siasa pamoja na ananchi pamoja kufanya na kukubaliana kwa maendeleo yao na kwamba litakuwa ni jimbo la mfano kwa majimbo mengine kwa kuanzisha utaratibu huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo,Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Dkt Martin Shao alisema taasisi hiyo bado ni changa lakini hata hivyo tayari imeweza kuanza kazi kwa upande wa miundombinu ya barabara.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akikata utepe katika mtambo unaotumika kukarabati barabara ikiwa ni ishara ya kuanza kazi kwa Taasisi ya Maendeleo katika jimbo la Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza barabara katika jimbo la Vunjo.
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini ,Baba Askofu Dkt Martin Shao akibariki moja ya Mitambo itakayotumika katika kufanya matengenezo ya barabara katika jimbo la Vunjo.
Mtambo wa kukwangua barabara ukianza kazi muda mfupi baada ya kuzinduliw kwa Taasisi ya Maendeleo ya Vunjo ambayo moja ya kazi zake ni kutengeneza miundo mbinu ya barabara.

Yvonne Chakachaka kufanya kazi na msanii mwingine kutoka Tanzania.

$
0
0
Collabo mpya ya Yvonne Chakachaka na msanii wa Tanzania.

Miezi kadhaa iliyopita King wa Bongo Flava Ali Kiba alitangaza rasmi ujio wa ngoma yake na mwanamuziki mkongwe, maarufu na wa zamani kutoka Afrika ya Kusini Yvonne Chakachaka. 

Hii ilikuwa ni hatua muhimu sana ya kimuziki kwa nguli huyo wa muziki kutoka Tanzania katika juhudi za kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya mipaka, lakini pia kuuthibitisha umma juu ya uwezo wake kimuziki. 

Lakini inaonekana kwamba Yvonne Chakachaka aliyetamba na nyimbo kama "Mama Afrika", "Thank you Mr. Dj" na "Umqombothi" miaka ya 80, amevutiwa sana na muziki wa Bongo na hivyo kuwa tayari kufanya kazi na wasanii wengine kutoka hapa nchini. 

Hii inathibitika baada ya hivi karibuni, kupitia account yake ya instagram kuonesha kuwa yuko studio na moja ya wasanii wa Tanzania, Otuck William, wakirekodi wimbo. Legend huyo wa muziki wa Africa AKA "The Princess of Africa" aliandika, "Spending some time with my son @otuck_william in Kigali, doing some work for the youth. Day well spent, thank you @mrmingz". 

Yvonne Chakachaka alikua jijini Kigali, nchini Rwanda kwa ajili ya onesho na kukutana na Otuck, ambaye pia alikua huko kwenye shughuli zake za kikazi na kimuziki, hivyo tutegemee kikubwa kutoka kwa hivi vichwa viwili. Otuck ni msanii mkongwe wa RnB nchini anayetambulika sana na ngoma zake kama Deja Vu, Roho Juu alitomshirikisha Heri Muziki na So Cold aliyoitoa hivi karibuni.

Kanisa la Waadiventista Wasabato laishukuru TaSUBa

$
0
0

Na Sophia Mtakasimba(TaSUBa)

Kanisa la waadiventista Wasabato Tanzania limeishukuru Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kutoka nafasi kwa wanamuziki wa kanisa hilo kujifunza Muziki katika taasisi hiyo,kupitia program maalumu ya Kozi fupi ya Muziki ya mwezi mmoja iliyoanza tarehe 1 Julai na kuhitimishwa leo.

Akizungumza katika ufungaji wa program hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa TaSUBa Bagamoyo, Mhazini wa kanisa la wasabato kutoka Jimbo la Kusini mwa Tanzania ,Mchungaji January Athanas Sigome amesema kuwa kanisa linaishukuru Sana TaSUBa kwa kutoa nafasi kwa Waimbaji ,Viongozi na watunzi wa nyimbo kutoka makanisa ya Waadventista wasabato,kujifunza Muziki na anaamini wahitimu wataenda kuwa chachu ya mabadiliko katika makanisa yao.

Aliongeza kuwa kanisa liliamua kushirikiana na TaSUBa kuendesha program hiyo ili kuwafanya watenda kazi wake wajifunze muziki na kuweza kurejesha heshima ya ibada kwa Mungu kama ilivyo katika maandiko matakatifu ,maana katika nyakati za sasa kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa juu ya namna bora ya kurejesha ibada ya sifa kwa Mungu.

Aidha Bw.Sigome alisema kuwa kanisa limeichagua taasisi ya sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)kwa kuwa ndio sehemu pekee yenye wakufunzi wenye weledi wa kutosha pamoja na vifaa vya kufundishia vya kutosha.

Nae Leonard Busee ambaye ni mhitimu wa program hiyo amesema kuwa wakiwa TaSUBa wamejifunza mambo mengi ambayo awali walikuwa hawayajui ikiwemo upigaji wa vyombo vya muziki,Falsafa ya muziki ,kusoma muziki pamoja na ufundi wa sauti

Nae mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye amesema kuwa ,kozi hiyo maalumu ni miongoni mwa program mbalimbali ya kimafunzo ambayo TaSUBa inatoa kwa makundi maalumu kulingana na mahitaji yao.Pia kozi za muda mrefu za Stashahada na Astashahada katika fani za mbalimbali zinaendelea kutolewa na sasa milango ipo wazi kwa wanaohitaji kutuma maombi ya kujiunga na chuo.
Mhitimu mwenye umri mdogo kuliko wote , msichana Naomi Yonazi akipotea cheti cha ushiriki wa program maalumu ya muziki.
Mtendaji mkuu wa TaSUBa Dkt.Herbert Makoye (wa pili kushoto), pamoja na Mhazini wa kanisa la waadventista wasabato Jimbo la kusini mwa Tanzania Mchuganji January Atanas Sigome (anayefuata baada ya Dkt.Makoye ), wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa program maalumu ya mafunzo ya muziki .
Wahitimu wa Programu maalumu ya mafunzo ya muziki wakiimba katika hafla ya ufungaji wa mafunzo.
Wakufunzi wa TaSUBa walioendesha program maalumu ya mafunzo ya muziki wakiwa katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Heri Kaare,Rhoda Mitanda,Peter Zengo,Melkiades Banyanka na John Sagati .

DK.SHEIN AONDOKA NCHINI LEO KUELEKEA INDONESIA KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Viongozi mbali mbali katika Uwanja wa Ndge wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokuwa akiondoka Nchini leo kuelekea Indonesia katika ziara ya Kikazi akifauatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Watendaji wengine wa Serikali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud (kushoto) katika Uwanja wa Ndge wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokuwa akiondoka Nchini leo kuelekea Indonesia katika ziara ya Kikazi akifauatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kulia) pamoja na Watendaji wengine wa Serikali,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Balozi Seif Ali Iddi (kulia) katika Uwanja wa Ndge wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokuwa akiondoka Nchini leo kuelekea Indonesia katika ziara ya Kikazi akifauatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani) pamoja na Watendaji wengine wa Serikali.
Picha na Ikulu.

MABONDIA NCHINI KUPEWA ZAWADI SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU.

$
0
0
Na Agnes Francis,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Golden boy promotion wakishirikiana na wadau mbali mbali wa mchezo wa ngumi za kulipwa,  wamewakutanisha mabondia wa hapa nchini kujadili maendeleo ya tasnia hiyo.

Ambapo wanafanya maandalizi ya kukutana na Serikali ili kuwatambulisha mabondia hao na Taifa liweze kuwatambua kuwa ni kitu gani huwa wanakwenda kufanya katika mapambano yao pamoja na kuwapa zawadi kama motisha kwao.

Promota wa ngumi za kulipwa hapa nchini Shomary Kimbau akizungunza na vyombo vya habari katika hotel ya The Cage sports kurasini Jijini Dar es Salaam,amesema kuwa sasa ni wakati wa mambondia hao kujulikana na Watanzania kwa kazi wanayoifanya ndani na hata nje ya nchi.

Kimbau amesema kwa mwaka huu kuna vijana watano wameshinda mikanda nje na kurudi nayo nyumbani ,lakini hawakuweza kutambulika katika jamii kwa kulitangaza Taifa letu na kufanya vizuri."Kuna bondia mmoja anaitwa Maono Ally ameshinda mkanda mkubwa wa WBC huko nchini Afrika kusini kwa nokauti raundi ya 2,tangu karudi hakuna mtu aliempa zawadi au kwa kumpongeza kwa sababu pia hajulikani"amesema kimbau

Promota huyo amesema kwa kutambua hilo wataungana na wadau mbali mbali hapa nchini septemba Mosi mwaka huu kuwapa zawadi mabondia wote waliowahi shinda mikanda ndani na nje ya nchi.Ambapo siku hiyo wanatarajia mgeni rasmi kuwa Waziri wa habari utamaduni na michezo Harrison Mwakyembe,hafla hiyo itaambatana na burudani ya mipambano minne ya ndondi.

Bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa Rashid Matumla amewashukuru wadau hao kwa kuanzisha programu hiyo ambayo ni ya mara ya kwanza,vile vile ametoa wito kwa serikali indelee kuunga mkono na wadhamini wajitokeze kama ilivyo michezo mingine. 

Bingwa wa ngumi za kulipwa hapa nchini Ibrahim Clasic amesisitizia kuwa programu hiyo ilioanzishwa iwe endelevu kwa kuwa italeta mapinduzi ya mchezo huo na vijana watajitokeza kwa wingi.
Promota wa ngumi za kulipwa Tanzania Shomary Kimbau  akizungumza katika hotel ya The Cage sports mivinjeni Jijini Dae es Salaam leo,kuhusu programu ya kuwatambulisha mabondia walioshinda mikanda mbali mbali ndani na nje ya nchi pamoja na kupewa zawadi Septemba Mosi mwaka huu,Bondia wa zamani Rashid Matumla katikati,Bingwa wa ngumi za kulipwa Tanzania Ibrahim Classic kulia.

UCHAGUZI WA KIHISTORIA WAFANYIKA LEO ZIMBABWE, MUGABE ASHUHUDIA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

UCHAGUZI wa kihistoria bila kuwepo kwa jina la aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kama mgombea umefanyika leo nchini Zimbabwe.

Imeelezwa kuwa zaidi ya watu milioni 5 wamejiandikisha na kujitokeza kupiga kura wakiwa na shauku ya kuona mabadiliko baada ya utawala mrefu wa Robert Mugabe(94).

Wagombea wanaochuana vikali ni Rais Emmerson Mnangagwa (75) kutoka ZANU-PF aliyekaimu nafasi mara baada ya Mugabe kujiuzulu na mwanasheria Nelson Chamisa (40) kutoka MDC.

Robert Mugabe amenukuliwa akisema kuwa uchaguzi huu utaiondoa serikali isiyo ya kikatiba madarakani, kauli hii imetafsiriwa kuwa Mugabe anaunga mkono upinzani licha ya Chamisa kukanusha hivyo.Chamisa amejihakikishia ushindi mara baada ya kupiga kura.

Mwaka 1987 Mugabe alichukua kiti cha urais na kuhudumu kwa miaka 37 hadi November 2018 ambapo jeshi la nchi lilipompindua na makamu wake kukaimu nafasi hiyo na hii ni baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu huyo kazi kwa kuamini utawala wa Mnangagwa ni haramu na fedheha kwa nchi yao.
Rais Mstaafu wa Zimbabwe Robert Mugabe

TFF wasaini Mkataba na KCB kudhamini ligi kuu msimu huu

$
0
0
Na khadija seif ,Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 420 na Benki ya KCB kwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu Benki ya KCB nchini Cosmas Kimario ameeleza madhumuni ya Benki hiyo ni kushirikiana na TFF kwa ajili ya kukuza sekta ya Michezo, ambapo hapo awali walishirikiana kwenye msimu uliopita 2017/2018 kwa kuwa moja wa wadhamini wa ligi kuu nchini.

Kimario amesema udhamini huo unalenga zaidi kuendeleza soka hilo nchini pamoja na kuwapatia ajira vijana na kuipeperusha bendera ya nchi ya Tanzania.

Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) Wallace Karia ametoa shukrani za dhati kwa benki ya KCB kwa udhamini huo, kwani watanufaika na kusaidia kunyanyua michezo katika msimu wa 2018/19. Hata hivyo  Karia amesema Benki ya KCB imekuwa ikishirikiana na TFF kwenye michezo na hata msimu uliopita walishirikiana nao kudhamini michezo nchini na hii ikiwa ni mara ya pili.

Kaimu mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Fatma Chiro ameeleza Benki hiyo imetoa ajira kwa watu wengi na rasmi,hivyo inaunga mkono kauli ya serikali katika kutoa ajira kwa vijana na wameamua kuanza na sekta ya michezo.

Amefafanua zaidi kuwa benki hiyo haitaishia hapo kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu (TFF) katika kudhamini michezo hususani mpira wa miguu na kutazama uwezekano wa kusaidia timu ya mpira wa miguu ya wanawake Kilimanjaro Queens ambao wameshinda mechi waliocheza hivi karibuni dhidi ya Ethiopia na kurudi na kombe nchini Tanzania.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420 kutoka kwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chilo baada ya kusaini  mkataba wa udhamini kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Bw. Boniface Wambura.

KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINA MANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA-MBUNGE JOSHUA NASSAR

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar amesema ushiriki wa Viongozi vijana wa Kiafrika Katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama ,Obama Foundation ni chachu kwa viongozi walioko madarakani kuendelea kuwamini kwa kuwapa nafasi za ju za uongozi .

Nassar ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita siku chache tangu ashiriki Kongamano lililoandaliwa na taasisi ya Obama Foundation na kuwashikisha vijana 200 kutoka mataifa 44 barani Afrika wanaofanya kazi serikalini ,asasi za kiraia na sekta binafsi ambao walikutana kwa muda wa siku tan katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Amesema katika Kongamano hilo kama vijana wamejifunza mambo mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yatachangia kujitokeza kwa vijana wengi zaidi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi watakaosaidia kuleta mabadiloko chanya katika bara la Africa.

Katika kongamano hilo lililoenda sambamba na sherehe za kilele cha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela,vijana nane kutoka Tanzania walichaguliwa kuiwakilisha nchi ya Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar akizungumzajambo na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama walipokutana nchini Afrika Kusini akiwa ni miongoni mwa Viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Afrika waliochaguliwa kushiriki Programu ya OBAMA AFRICA LEADERS PRORAM.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar kwa pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama wakiwajibika kwa kufanya kazi za mikono katika kuboresha miundombinu ya shule ya Far North School iliyopo pembezoni mwa jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Mbali na kushiriki kazi za mikono Rais Mstaafu wa Marekani,Barack Obama pia alipata nafasi ya kutoa mada katika kongamano lililowashirika viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Africa.
Wengine waliowasilisha mada katika Kongamano hilo ni pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Koffi Annan ,Rais wa Kwanza Mwananmke Barani Afrika na Rais Mstaafu wa Liberia ,Ellen Johnson Sirleaf 

MASAUNI: SERIKALI HAITOMVUMILIA ASKARI ATAKAEBAINIKA KULA RUSHWA NA KUBAMBIKIA KESI WANANCHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na watumishi raia, askari na maafisa (hawapo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao wakati wa ziara ya kikazi, mkoani Shinyanga, leo.Ambapo amewataka askari kutojihusisha na matendo ya rushwa pamoja na kubambikia rushwa wananchi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sajenti wa Jeshi la Magereza, Athumani Massawo, akizungumza wakati wa kikao cha ndani cha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao wakati wa ziara ya kikazi, mkoani Shinyanga, leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyaga,Mrakibu Mwandamizi Venance Mwamakula akizungumza wakati wa kikao cha ndani cha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao, mkoani Shinyanga, leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Askari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hawapo pichani), wakati wa kikao cha ndani na watumishi hao wakati wa ziara ya kikazi, mkoani Shinyanga, leo.Ambapo amewataka askari kutojihusisha na matendo ya rushwa pamoja na kubambikia rushwa wananchi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

OPARESHENI MAALUMU YANASA WAHAMIAJI WASIO RASMI 1054 WILAYANI BUHIGWE/KASULU MKOANI KIGOMA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

JUMLA ya wahamiaji Wasio rasmi 1054 Wamekamatwa katika Wilaya ya Buhigwe na Kasulu mkoani kigoma, Kwa kipindi cha Mwaka mmoja katika oparesheni zilizofanywa na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya hizo.

Akimkaribisha Waziri Mkuu katika Wilaya ya Buhigwe Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema wameendelea kuimalisha ulinzi na usalama katika Wilaya hizo kuhakikisha Wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani na utulivu na kuendelea kupambana na vitendo vya uhalifu na uingizwaji wa silaha kiholela .

Alisema kutokana na Muingiliano uliopo baina ya Wilaya hizo na Nchi jirani ya Burundi, kumekuwa na Wahamiaji haramu wengi wanaoingia Nchini bila vibali na wengine wamekuwa wakishirikiana na Watanzania kufanya vitendo vya utekaji kwa kutumia silaha ambapo Wamejitahidi kuzuia vitendo hivyo kwa kuwakamata wote wanaoingia bila Vibari Nchini .

"Kwa sasa hali ya ulinzi na usalama Imeendelea kuimarika na Wananchi wameendelea kuiunga mkono serikali kwa kutoa taarifa endapo wanamuhofia mtu anapoingia katika maeneo yao na tumefanikiwa katika hili na kwasasa hakuna malalamiko yoyote ya uvunjifu wa amani kutoka Kwa Wananchi", alisema Brigedia Jenerali Gaguti. 

Nae Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa aliwataka Polisi kwa kushirikiana na Maafisa uhamiaji kudhibiti njia ambazo sio rasmi katika Wilaya ya Buhigwe kwaajili ya kuzuia silaha zinazoingizwa Nchini kiholela na watu wanaingia bila vibali.Alisema Serikali inampango wa kuifanya mji wa Manyovu kuwa mji wa biashara hovyo jeshi la polisi wanatakiwa kuwa macho kwaddhibiti vizuizi hivyo ilikuhakikisha wote wanaoingia Nchini wanakuwa na vibali na kudhibiti silaha zilizopo katika Nchi jirani kuingia Nchini.

" Tunajua Wilaya hii inachangamoto ya muingiliano Mkubwa na ndugu zetu wa Nchi jirani, Leo hii Tanzania tunarekodi mbaya ya kumiliki silaha kinyume na taratibu zote hizi zinatoka Nchi za jirani na kufanya uharifu wa kutumia silaha", alieleza Waziri Mkuu."Lazima jeshi la polisi Muandae mipaka iliyo rasmi ilikudhibiti haya uwezo huo mnao hatutaki kuona uhalifu unaendelea kuingia Nchini jeshi la polisi kazi yenu ni kulinda amani na jukumu hili ninlakwenu", alisema.

Alisema Serikali ya Tanzania inamahusiano mazuri na Nchi jirani hivyo mahusiano hayo yaendelee lazima utaratibu uwekwe na usalama uimalishwe.

WANAFUNZI 200 SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI KUONESHA KAZI ZAO ZA TEKNOLOJIA YA UGUNDUZI NA SAYANSI

$
0
0
JUMLA ya Wanafunzi 200 kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini wanatarajiwa kuonesha kazi zao za teknolojia ya ugunduzi na sayansi kukabiliana na changamoto za maendeleo nchini.

Kazi hizo ziko katika nyanja za sayansi kama kemia,fizikia ,hesabu, baiolojia, mazingira, sayansi ya jamii na teknolojia.Maonesho ya kazi hizo za wanafunzi yameandaluwa na Taasisi inasaidia wanasayansi Chipukizi ya YST ikiwahusisha pia walimu 100 wakiambatana na wanafunzi hao ili kuonesha kazi hizo walizoziandaa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumzia maonesho hayo yatakayofanyika Agosti 1 na 2 jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi Mwenza was YST ,Dr Gosbert Kamugisha alisema katika mashindano ya kazi hizo, wataonesha kazi za kigunduzi na wale watakaoshinda watapata udhamini wa kusoma masomo ya sayansi katika vyuo vya elimu ya juu.

Alisema lengo la maonesho hayo yaliyoanza kuoneshwa nchini tangu mwaka 2012 ,yatasaidia kuinua ari ya wanafunzi kusoma masomo ya sayansi jambo litakalosaidia kupata wataalam wengi katika eneo sayansi na kufanya kazi katika viwanda.

" wanasayansi hao ambao ni chipukizi watakaonesha ugunduzi mzuri wataawadiwa pesa taslimu,medali na vifaa vya maabara," alisema na kuongeza kuwa wanne watapewa ufadhili kusomeshwa elimu ya chuo kikuu ambao huyolewa na shirika la Karimjee,Jivanjee Foundation ili kuendelea kjimarisha vipaji vyao vya ugunduzi wa kisayansi.

Amesema maonesho hayo kuhamasisha wanafunzi was sekondari kupenda sayansi na ugunduzi na kujenga utamafuni was kisayansinkwa vijana was kitanzania,in fursa nzuri kwa wanafunzi was sekkndari kuonesha njia madhubuti za kukabiliana na chanhamoto za kijamii na kiuchumi.
 Mwanzilishi Mwenza wa YST,Dk Gosbert  Kamugisha (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu wanafunzi 200 kutoka shule za sekondari nchini  wanaotarajiwa kuonesha kazi zao za teknolojia Agosti 1,2 mwaka huu  katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.
Mwanzilishi Mwenza wa shirika la YST,Joseph Clowry (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya maonesho yatayofanyika Agosti 1,2  mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar as Salaam.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images