Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

TFS YAJA NA MALENGO YA KUCHANGIA ZAIDI SERIKALI

$
0
0
Tanga: Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), imejiwekea malengo zaidi ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 122 katika mwaka huu mpya wa fedha 2018/19 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali katika usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na nyuki ili waweze kuchangia mfuko mkuu wa fedha za serikali.

Akifunga mafunzo ya siku nne ya kuhusu taratibu za kukusanya maduhuli ya serikali iliyofanyika katika ukumbi wa VETA mjini hapa, Mtendaji Mkuu wa TFS Professa Dos Santos Silayo, amesema lengo hilo litatilia mkazo uibuaji vyanzo vipya vya mapato.

“Nawashukuru watumishi wote wa TFS kila mmoja kwa nafasi yake, uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Mhe Waziri Dkt. Hamisi Kigwangala, Bodi ya Ushauri iliyomaliza muda wake chini ya mama Ester Mkwizu na wajumbe wote kwa uchapakazi na uongozi thabiti uliowezesha TFS kukusanya na hatimaye kuwasilisha sehemu ya mapato yake kwa serikali. 

“Kwa kweli ni fahari kwetu kama taasisi kuweza kuwasilisha bilioni 22.41 katika mfuko huo wa serikali kiasi kwamba tumeshika nafasi ya tano katika utoaji wa gawiwo hilo,” amesema Profesa Silayo.

Akizungumzia mikakati ya TFS katika mwaka huu wa fedha, Profesa Silayo amewataka watendaji wake kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato visivyokuwa na madhara katika shughuli za uhifadhi ili kuondoa dhana iliyojengeka kwamba vya taasisi hiyo kazi yao ni kuuza mbao na mkaa.Kusoma zaidi BOFYA HAPA>>>>>>>>>
Baadhi ya wahasibu wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea
Baadhi ya wahasibu wakifuatilia mkutano uliokuwa unaendelea
Picha ya Pamoja Mtendaji Mkuu wa TFS akiwa na wahasibu wa TFS Tanzania nzima mara baada ya kufunga mafunzo yao katika Ukumbi wa Veta jijini Tanga Ijumaa jioni.

Rais Magufuli amemteua pia Bibi Gift Isaya Msuya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora,Mh.Gift Isaya Msuya



JAJI MKUU AWATAKA MAHAKIMU KUTOCHELEWESHA MASHAURI

$
0
0
Na Magreth Kinabo 

Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe .Profesa Ibrahim Juma amewataka mahakimu wapya wasiwe chanzo cha ucheleweshaji wa mashauri.

Aidha kuacha kulalamika bali pale linapotokea matatizo, bali wawe chachu ya kuyatafutia ufumbuzi katika utendaji wao wa kazi wa kutoa huduma za haki kwa wananchi.Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mkuu huyo wakati akiwaapisha Mahakimu wapya kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

“ Kiapo mlichoapa ni uzito muda wote mtakaofanya kazi ya kuwatumikia wananchi, wananchi wanataka kutatuliwa kwa malalamiko yao kwa haraka,” Aliongeza kwamba mfumo wa sasa sio wa kukaa na kulalamika, kama kuna tatizo litafutiwe ufumbuzi na kuepuka kuwa chanzo cha ulalamishi.

Alisema mahakimu hao wanapaswa kuwa weledi wanapotoa huduma za utoaji haki ili waweze kutoa hukumu zinazoeleweka kwa kujibu wa sheria na kanuni. Hivyo wanapaswa kushirikiana na wadau wengine wa mahakama ili kuahakikisha hukumu zinatoka kwa haraka.Alisisitiza mahakimu hao kwamba kufanya kazi kwa kuepuka rushwa na kwa nidhamu.

Jaji Mkuu huyo alifafanua kuwa changamoto za majengo chakavu na umbali , visikwamishe utendaji kazi wao, hivyo mahakama iko katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano ambao unalenga kutoa huduma za haki kwa wote na wakati, ikiwemo kuboresha miundombinu.

Aliwataka mahakimu hao kuielewa taasisi inayofanyakazi na mpango mkakati huo.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA NYUMBA 14 ZA WATUMISHI HALMASHAURI YA BUSEKELO ZILIZOJENGWA NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa nyumba 14 za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Busekelo zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Felix Manyama Maagi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu kinachoelezea utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika jimbo la Busekelo alichokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Mhe. Atupele Mwakibete wakati wa ufunguzi wa nyumba 14 za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Busekelo zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mzee Mark Mwandosya,alipowasili kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa nyumba 14 za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Busekelo zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Felix Manyama Maagi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Rais Dkt Magufuli afanya uteuzi na kuwahamisha vituo vya kazi viongozi wa Mikoa, Wizara na Wilaya

DIABETES AWARENESS & HEALTH TALK SEMINAR TODAY

WAKE WA VIONGOZI WAKIONGOZWA NA MKE WA WAZIRI MKUU MHE. MAMA MARY MAJALIWA WATEMBELEA KAMBI MAALUM YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO

$
0
0

Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) aliyefanyiwa upasuaji wa kuziba matundu ya moyo katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi wa kikundi cha Millennium Group walitembelea kambi hiyo leo na kuchangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wawili.
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akimsikiliza Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani akimuelezea aina za upasuaji wa moyo kwa watoto zinazofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza.
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwakabidhi hundi ya shilingi milioni nne wazazi wa watoto Anjela Francis (4) na Sabina Mnyango (4) fedha ambazo zimetolewa na kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto hao ambao wanatibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza.
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wake wa viongozi, wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wazazi wa watoto ambao kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kimewachangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza.
Wake wa viongozi wa kikundi cha New Millenium Group wakiongozwa na Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutemblelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope ya nchini Uingereza.

VOA Swahili: Zulia Jekundu


Bendi za Muziki wa dansi kutikisa katika maonyesho ya Kimataifa nchini Ujerumani. Tanzania ndiyo nchi lengwa katika maonyesho hayo mwaka 2018

$
0
0
Wakati siku zinakaribia na matayarisho yamekamilika kwa kuanza maonyesho ya kimataifa ya Intern.Afrika Festival Tubingen 2018 yanayo ambatana na maonyesho ya biashara ya (GaiExpo) German-Afrika International Expo,kuanzia tarehe 9 Agosti 2018 mpaka 12 Agosti 2018 katika mji wa Tubingen,nchini ujerumani ambapo nchi lengwa katika maonyesho hayo mwaka 2018 ni TANZANIA. 
Baadhi ya wasanii na bendi mbali mbali wameshathibitisha kushiriki katika maonyesho hayo kati ya bendi za muziki wa dansi maarufu kama "Bongo Dansi" zilizokuwa tayari huko ulaya ni bendi maarufu za Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni au "Viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens "  yenye makao yake ujerumani.
Pia kuna Saidi Kanda  na Mvula-Mandondo Band inayoongozwa na mwanamuziki Saidi kanda yenye makao yake kule Uingereza nao wameshakuwapo tayari tayari kwa kutumbuiza katika maonyesho hayo makubwa. 
Watayarishaji wa maonyesho hayo GaiExpo wamesema wanatarajia kupokea wageni wengi kutoka nchini Tanzania wakiwemo wafanyibiashara,wajasilimali,wasanii n.k,mialiko imeshatumwa kwa wageni wote na pia kopi za mialiko hiyo zimeshatumwa kwa ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania kilichobakia ni jukumu la ubalozi wa ujerumani uwape idhini na viza za kusafiria washiriki wa maonyesho hayo makubwa ambayo kwa mara ya kwanza Tanzania ni nche lengwa katika tamasha kubwa barani ulaya. 



RAIS DKT MAGUFULI ATOA POLE KWA MWANAHABARI ERIC SHIGONGO KWA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima za mwisho wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela walipofika kuwafariji msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa mwanafamilia Bi Leah James wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Mama Veneranda Shigongo, mke wa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 kutoa pole.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

AWESO AWAONYA WAHANDISI WA MAJI NCHINI

$
0
0
Kauli ya Naibu Waziri huyo aliitoa juzi wakati wa ziara yake ya kutembelea Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto alipokuwa akikagua miradi ya maji huku akilazimika tena kumsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Samadu Makau kutokana na kushindwa kusimamia vema mradi wa Maji Mgwashi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5 na kupelekea wananchi kukosa maji. 

Naibu Waziri ambaye alianza ziara yake mkoani Tanga kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe,Lushoto na Halamshauri zote ndani ya wilaya hizo ambapo alibaini kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali katika miradi ya maji tokea mwaka 2012 kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi makini wa watendaji wa serikali. 

Alisema ubadhirifu na upotevu wa fedha za Serikali inatokana na wahandisi wa maji wa mikoa na wilaya waliopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo na kushauri kushindwa kuwajibika ipasavyo hivyo kupelekea kuingiza hasara na kupelekea wananchi kukosa maji hivyo Wizara kuanza kutilia mashaka taaluma zao. 

Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani serikali inapeleka fedha nyingi kwenye miradi ili kuweza kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi huku wahandisi hao wa maji wakishindwa kusimamia kwa waledi miradi hiyo huku Serikali ikiwalipa fedha za mishahara kwa ajili ya kuisadia majukumu hayo. 

“Haiwezekani Serikali inatumia fedha nyingi sana kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa lengo la kuondokana na adha hiyo huku wahandisi waliopo kwa niaba ya Serikali wakishindwa kuisimamia badala yake unapewa taarifa ya ubabaishaji kila maeneo ya miradi unapotembelea”Alisema. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akionyeshwa na wananchi wa Kijiji cha Manolo Kata ya Manolo wilayani Lushoto maji wanayotumia kutoikana na kukabiliana na uhaba wa maji wakati wa ziara yake juzi iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji na kuzungumza na wananchi
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mgwashi Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua vyanzo vya maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
 aibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji kwenye kijiji cha Mgwashi wilayani Lushoto wakati wa ziara yake

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI KANISA LA MTAKATIFU PETRO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe wakishiriki katika ibada ya Jumapili katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe akipokea Sakramenti Takatifu wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018,PICHA NA IKULU

Serikali yaahidi kuyaboresha zaidi mashindano ya Golf Utalii Karibu Kusini

$
0
0
WAKATI mashindano ya golf ya Utalii Karibu Kusini Mufindi Golf Challenge 2018 yakihitimishwa leo kwenye Viwanja vya Golf vya Unilever wilayani Mufindi, Mkoani Iringa serikali imeahidi kuendelea kuyaboresha mashindano hayo ili yatumike kwa ufanisi zaidi kutangaza vivutio vya Utalii katika kanda za Nyanda za Juu Kusini.

Akizungumza kwenye viwanja hivyo, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii Wizara ya Mali Asili na Utalii, Bw Deogratius Mdamu alisema uamuzi wa Serikali kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa kutumia mashindano hayo kutangaza Utalii wa Nyanda za Juu Kusini umeonesha mafanikio licha ya kuwa mashindano hayo yanafanyika mara ya kwanza baada ya kupita miongo kadhaa.

“Lengo hasa nikuona ndani ya muda mfupi ujao mashindano haya yanakuwa makubwa si tu hapa nchini bali pia nje ya nchi ili tuweze kuvutia washiriki wengi hasa kutoka nje ya nchi tukiamini ujio wao hapa Mufindi utakuwa na tija si kimichezo bali pia kiutalii na kiuchumi,’’ alisema Mdamu.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mashindano hayo wamesema uwepo wa mashindano hayo utatumika kikamilifu kutangaza fursa na vivutio vya Utalii vinavyopatikana katika ukanda huo. Bw Yeckonia Chaula ambaye ni mchezaji mwandamizi wa golf kutoka klabu ya Golf ya Mufindi alisema:

“Naipongeza sana serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kuamua kutumia mchezo huu kutangaza vivutio vya Utalii katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na kwa kweli dalili za mafanikio zimeanza kuonekana mapema kwa sababu licha ya mashindano haya kufanyika mara ya kwanza baada ya miaka mingi sana lakini yamevutia washiriki kutoka klabu zote za mchezo huu hapa nchini ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Arusha na Mufindi,’’ Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii Wizara ya Mali Asili na Utalii, Bw Deogratius Mdamu (katikati) akikagua Uwanja wa Golf wa Unilever uliopo wilayani Mufindi mkoani Iringa ambapo mashindano hayo yanaendelea. Wengine ni pamoja na Afisa Utalii Mkoa wa Iringa Bi Hawa Mwachaga (kushoto) pamoja na Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw Clement Mshana.
Washiriki kutoka vilabu mbalimbali vya gofu nchini wakiendelea kushindana kwenye mashindano hayo.

Washiriki kutoka vilabu mbalimbali vya gofu nchini wakiendelea kushindana kwenye mashindano hayo.
Waandaaji wa mashindano hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

MWILI WA MAMA YAKE SHIGONGO WAAGWA DAR, KUZIKWA JUMATANO JIJINI MWANZA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu wa jamii

MWILI wa Mama mzazi wa Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Mtunzi na mjasiriamali Eric Shigongo umeagwa leo katika kanisa katoliki la Mtakatifu Martha Mikocheni B jijini Dar es salaam na jioni ya leo utapelekwa katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea Jijini Mwanza katika kijiji cha Bupandwahela kwa maziko.

Imeelezwa kwamba mwili wa Bi. Asteria utapokelewa Nyakato Mwanza siku ya Jumatatu asubuhi na kuagwa majira ya saa kumi jioni na siku ya jumanne safari ya kuelekea Bupandwamhela kwa maziko itaanza.

Bi. Asteria atapumzishwa katika makao yake ya milele siku ya jumatano, Agosti 1 mwaka huu.

Marehemu alizaliwa Septemba 16, 1931 akiwa mtoto wa 3 kati ya watoto 3 kwa mama Asteria ambaye alifariki mara baada ya kujifungua mtoto wake wa mwisho ambaye ni mama wa Eric Shigongo na nduguze, marehemu alikuwa mjasiriamali na alibahatika kupata watoto 11 na walio hai ni 9 pekee, na ameacha wajukuu 42 na vitukuu 23.

Bi Asteria alianza kuugua muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali kama vile TMJ, Agha khan na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambako mauti yalimfika Julai  27 mwaka huu.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake Lihimidiwe. Amina.
 Eric Shigongo akisoma wasifu wa marehemu mama yake Wakati wa kuaga 
 Pichani wa Nne kushoto,Ndugu Eric shigongo akiwa na baadhi ya Ndugu jamaa na marafiki wakati wa kuaga mwili ya Mama yake mzazi nyumbani kwake Mikocheni B,Kinondoni jijini Dar

SERIKALI KUTAIFISHA MALI ZA KAMPUNI YA TANZAM 2000 ZILIZOPO NDANI YA PORI LA AKIBA MOYOWOSI/KIGOSI BAADA YA ILANI YA SIKU 7 - DK. KIGWANGALLA

$
0
0
Na Hamza Temba-Geita

Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi imetakiwa kuondoa vifaa na mitambo yake katika eneo la hilo ndani ya siku saba kwa amri ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kutoa ilani ya siku saba kwa kampuni hiyo iondoe vifaa na mitambo yake katika eneo hilo na endapo muda huo utapita bila kufanya hivyo mali hizo zitataifishwa na kuwa mali ya Serikali kwa kuwa wao ni wavamizi kwa mujibu wa sheria.

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo alihitimisha ziara yake ya siku 25 aliyoipa jina la Pori Kwa Pori kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi nchini na kutatua changomoto zake.

Alisema uwepo wa vifaa na mitambo ya muwekezaji huyo ndani ya hifadhi hiyo imekuwa kishawishi kikubwa kwa wachimbaji wadogo wa madini kuvamia maeneo hayo wakiamini kuwa eneo hilo lina dhahabu na kwamba bado linaruhusiwa kwa shughuli za uchimbaji.

Awali Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika alisema kampuni hiyo ilipewa kibali na Wizara ya Malisili na Utalii kwa ajili ya kufanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo hilo kwa mwaka 2005 hadi 2010 na kuongezewa muda hadi 2012.Alisema wakati kibali hicho kinatolewa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ambayo inazuia tafiti kama hizo na shughuli nyingine za kibinaadamu kwenye maeneo ya hifadhi ilikua bado haijatoka.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akimuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Mabula Misungwi (Kulia) kutoa ilani ya siku 7 kwa kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 ili itoe mali zake zote katika eneo la Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita na endapo muda huo utapita zitaifishwe kuwa mali na Serikali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa na mitambo ya kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni hiyo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali, Nyuma yake ni Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akioneshwa vielelezo (mchanga wa madini ya dhahabu na baiskeli) walivyokamatwa navyo wachimbaji wadogo wa madini katika eneo Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi na Meneja wa Sekta ya Kigosi Kaskazini, Salum Kulunge alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya siku 7 kwa kampuni ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu ndani ya pori hilo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali.


RC MNYETI AWASHUKIA WAPINZANI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amemshukia vikali mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema) kutodandia maendeleo yanayofanywa na Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara na kuwadanganya wananchi kuwa yamesababishwa na Chadema.

Mnyeti aliyasema hayo jana mjini Babati kwenye mkutano wa hadhara baada ya Gekul kujinasibu kuwa maendeleo yanayoonekana Babati yanafanywa na Chadema.Mkuu huyo wa mkoa aliwaeleza wananchi kuwa fedha za bajeti ya mkoa wa Manyara alienda mwenyewe bungeni jijini Dodoma kuzitetea lakini Gekul na wapinzani walipinga ila wabunge wa CCM walitetea.

"Acheni kudandia maendeleo ya watu, diwani au mbunge atapata wapi fedha za kukamilisha miradi ya maendeleo kwenye halmashauri ambayo haina vyanzo vya mapato vya uhakika kama serikali kuu isipotoa fedha zake na kukamilisha hayo," alisema Mnyeti.Alimtaka mbunge huyo kuungana na wapenda maendeleo wa kweli na kuachana na siasa za kudanganya wananchi ili hali bungeni wanapinga maendeleo kwa kukataa bajeti.

Alisema baada ya serikali kujenga kilomita 4.5 za barabara za lami ndani ya mji wa Babati hivi sasa kutaongezwa kilomita nyingine 10 za lami ili kufanikisha miundominu bora ya eneo hilo ambalo ni makao makuu ya mkoa huo."Hizo barabara zilizotengenezwa mjini Babati na zinazoendelea kujengwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli alizoahidi wakati wa kampeni na siyo vinginevyo wapinzani msidandie maendeleo," alisema Mnyeti.

Alisema kila kiongozi anapaswa kubeba mzigo wake mwenyewe kwa kufanya mikutano mwenyewe na siyo kusubiri kudandia ziara ya mkuu wa mkoa na kuongopea wananchi waliojitokeza kwa wingi.Awali, Gekul ambaye alikuwa kwenye msafara wa Mnyeti alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi alisema Chadema imefanikisha maendeleo mengi Babati tangu wachaguliwe mwaka 2015.

"Tangu wananchi walipotuchagua na kutupa nafasi ya kuongoza halmashauri ya mji wa Babati tumefanikisha miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji na barabara na tutaendelea kuwatumikia," alisema Gekul.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mati Super Brands Ltd, David Mulokozi (kushoto) wakati akikagua vinjwaji vinavyotengenezwa na kampuni hiyo, katikati ni mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji huo Mohamed Kibiki.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti (watatu kulia) akiongoza ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo mjini Babati, kulia ni mbunge wa viti maalum wa mkoa huo Ester Mahawe.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti, akizungumza na wananchi wa mjini Babati ambapo alisikiliza kero zao na kuwapa majawabu, kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Mohamed Kibiki na mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul.

Muleba yaunganishwa rasmi umeme gridi ya Taifa

$
0
0
WAZIRI wa Nishati, Medard Kalemani, amezindua umeme wa gridi ya Taifa Wilaya ya Muleba, ambapo alisema kuwa hatua hiyo sasa inakwenda kuifanya wilaya hiyo kuwa na umeme wa uhakika. 

Akizungumza leo kwenye uzinduzi wa umeme huyo wa gridi ya Taifa ulifanyika katika Kijiji cha Nyamagojo Wilayani Muleba, Dk. Kalemani, amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania hasa wa maeneo ya vijijini wanapata umeme kwenye nyumba zao. 

Amesema katika utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa KV 33 wa umeme wa gridi ya Taifa kutoka Wilayani Chato, Rais Dk. John Magufuli, aliridhia na kutoa Sh milioni 778 ili kuweza kukamilisha kazi hiyo. 

Kutokana na hali hiyo Waziri Dk. Kalemani, amesema kuwa mkakati wa Serikali kuunganisha Mkoa wa Kagera kwenye umeme wa gridi ya Taifa ambao ni wa uhakika katika kufanikisha uchumi wa viwanda kwa kjuwa na nishati ya uhakika na yenye usalama. 

“Kuzinduliwa kwa umeme huu wa gridi ya Taifa sasa kuzifanya Wilaya za Muleba, Biharamulo na Ngara sasa kuwa na umeme wa uhakika wa hapa nchini kwetu. Tena umeme huu ni salama zaidi maana awali tulikuwa tunategemea umeme kutoka kwa wenzetu nchi ya Uganda jambo ambalo hata wakizima kule hatuna la namna ya kuuliza. 

“Na ninafuraha kubwa kuwaambia kwamba mkataba wa kazi hii ya ulikuwa ni wa miezi miwili ambapo Juni 2, mwaka huu ulisaini na kuwekeana malengo kwamba hadi kufikia Agosti 2, mwaka huu kazi hii iwe imekamilika. Lakini leo (jana) ninafuraha kuona kazi hii imekamilika wiki moja kabla ya muda wa mkataba,” amesema Dk. Kalemani 
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akishangilia baada ya kuzindua umeme wa gridi ya Taifa katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera leo.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa umeme wa gridi ya Taifa Wilayani Muleba Mkoani Kagera leo.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyamagojo Wilayani Muleba Mkoani Kagera leo, wakati wa uzinduzi wa umeme wa gridi ya Taifa wa KV 33 ambapo sasa Wilaya ya Muleba, Biharamulo na Ngara zitakuwa zinatumia umeme huo.
Waziri wa Niashati, Dk. Kalemani, akiwashukuru mafundi waliofanikisha ujenzi znjia za umeme wa gridi ya Taifa baada ya kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

MKURUGENZI WA UCHAGUZI, DKT. ATHUMANI KIHAMIA AKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI MANISPAA YA MOSHI, ARUSHA NA LONGIDO.

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akizungumza jambo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (kulia) mara baada ya kuwasili katika Manispaa hiyo kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 1 . Kushoto ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi (kulia) akimweleza jambo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasili katika Manispaa ya Moshi kufuatilia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 1 Agosti 12 mwaka huu . Kushoto ni Afisa kutoka NEC, Bw. Athuman Masesa. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (kulia) akipokea taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 za jimbo la Longido kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Longido Bw. Jummaa Mohamed Mhina. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (katikati) akipokea taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 4 za jimbo la Arusha kutoka kwa Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Namyaki Wilfred Laitetei.PICHA ZOTE / NEC

NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA

$
0
0
Kwanza napenda kutumia fursa hii kuwapongeza vijana walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali, tambueni Rais amewaamini na amewapa nafasi hizo ili mkawe chachu ya maendeleo katika maeneo yenu ya kazi ili kutekeleza ilani ya CCM na kutatua kero za wananchi hasa wanyonge.

Najua tangu taarifa ya uteuzi ilipotolewa mmepokea salamu nyingi za pongezi, nawasihi 'msilewe' kwani Rais Magufuli amekuwa akisema katika teuzi zake pongezi ni chache ila pole ndiyo nyingi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, mefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa wizara, mikoa na wilaya mbalimbali. Ni uteuzi makini kwani Rais amezingatia sifa na mahitaji ya kiutendaji katika kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Tangu uteuzi huu ufanyike kumekua na maneno mengi mitandaoni ya kubeza na kejeli kwa baadhi ya wateule hawa wa Rais na huo ndiyo msingi wa andiko langu.

Wapo waliotumia maneno makali katika mitandao mbalimbali ya kijamii wakidai Rais Magufuli amewateua wapinzani waliokuwa wakimpinga wakati wa uchaguzi wa 2015 na kuwaacha vijana wa CCM waliohangaika usiku na mchana kuhakikisha kura zake zinatosha na CCM inashinda.Ukichunguza, ni watu hawahawa walipinga ununuzi wa ndege, wakawa wa kwanza kuipanda, wanapinga ujenzi wa reli ya kisasa, huku mataifa makubwa yakiona umuhimu wake, kiasi cha kumuahidi Rais wetu kumsaidia.

Ni hawa hawa walitangaza hatuwezi kujenga barabara za juu, lakini ndio watakuwa wakwanza kupita pale Tazara, wakienda kupanda Dreemliner pale Uwanja wa JK Nyerere.Watu hawa leo wameibuka kivingine wanajaribu kuuaminisha umma kwamba uteuzi uliofanywa na Rais unashaka ndani yake na hauna afya kwa wanaCCM. Hawa ni watu wa kupuuzwa. Nakupongeza Rais wangu Dk. John Magufuli kwa uamuzi wako wa kuwapotezea.

Eti wanadiriki kuwataja wateule hawa eti ni wapinzani kana kwamba hawakustahili kupewa nafasi hizo Patrobas Katambi, David Kafulila na Moses Machali. Katika hoja zao mitandaoni wengine wamediriki kusema uteuzi huu umeleta makundi mawili ndani ya chama kwamba eti umeibua vita kati ya CCM asilia wanaobaki watazamaji na CCM wahamiaji wanaopewa nafasi. Kauli kama hizi zinapaswa kupuuzwa kwani zinapandikiza chuki na kuchochea mpasuko ndani ya chama (CCM).

Kabla sijaendelea nitumie fursa hii kumkaribisha Patrobasi Katambi Dodoma, karibu mh DC tushirikiane kusukuma maendeleo katika jiji letu la Dodoma.Chama Cha Mapinduzi kimejengwa katika misingi ya umoja na ushirikiano unaohanikizwa na kaulimbiu ya Umoja Ni Ushindi. WanaCCM wamejengwa katika misingi hiyo na wanaamini hakuna kununa katika chama kwani kazi za kufanya zipo nyingi ndani na nje ya chama ni suala la muda tu! Hivyo hakuna sababu ya kununa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MGALU YAPELEKA NEEMA YA UMEME MTWARA

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Blogu ya jamii

NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameendelea na ziara yake Mkoani Mtwara kukagua miradi na kuangalia utekelezaji  wa huduma ya umeme kwa wananchi mkoani huo.

Katika ziara yake Mgalu ameeleza kuwa kwa mwaka huu wananchi wa kata ya Chipuputa wataunganishiwa huduma ya umeme kwa bei ya shilingi elfu  99 ,gharama ambayo Tanesco iliwatangazia Wananchi tangu hapo awali.

Aidha Waziri Mgalu ameagiza kuwa bei hiyo ya elfu 99 walizoahidiwa na shirika hilo kipindi cha nyuma, ndizo zitakazotumika kuwaunganishia huduma ya umeme kwa wananchi wa kata ya Chipuputa kijiji cha Kagera.

"Takribani bilioni 1 zimetumika kwenye mradi huo, hivyo wananchi watakaokosa nafasi mwaka huu,waondoe hofu kwani  kuna nafasi zitaongezwa ambazo zitawafikia wakazi wa Mtwara'',alisema Waziri Mgalu na kuongeza kuwa amemwagiza Meneja wa Tanesco kuandaa orodha ya wananchi waliojiandikisha kupata huduma hiyo ili wapatiwe  huduma ya kwa wakati kama ilivyopangwa.

Mgalu amesema kuwa kwa mwaka huu wananchi wa kata ya Chipuputa wajiandae kupokea umeme ,kwani ujio wa huduma hiyo itawasaidia katika shughuli za kukuza uchumi wao.Aidha wakazi wa Chipuputa wameshukuru kwa ujio wa Naibu Waziri na kueleza kuwa changamoto iliyodumu kwa muda mrefu sasa imetatuliwa.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kata ya Chipuputa kijiji cha Kagera mkoa wa Mtwara , ambapo alimuagiza Meneja wa Tanesco kuhakikisha wananchi wanaunganishwa umeme kwa bei ya zamani ya shilingi 99,000.

Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mtwara wakikagua maendeleo ya mradi wa mashine mbili mpya za kuzalisha umeme katika Halmashauri ya Mtwara.

Muonekano wa mashine mbili mpya za kuzalisha umeme zinazoendelea kufungwa katika Halmashauri ya Mtwara.

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akimsikiliza msimamzi wa mradi wa ujenzi wa mashine mbili mpya za kuzalisha umeme, Mhadisi Mkulugwa Chinumba namna mradi huo unavyofanya kazi. 
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images