Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE ATETA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma alipomtembelea Ofisini kwake leo Julai 19, 2018 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha rasmi tangu aapishwe kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, Julai 14, 2018.

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (kulia) akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga alipotembelea Ofisi ya Jaji Mkuu wa Tanzania jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike wakiteta mambo mbalimbali juu ya ushirikiano wa vyombo hivyo muhimu katika kusimamia sheria na haki. Kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma(kushoto) ni  Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma baada ya mazungumzo ambapo Kamishna Jenerali wa Magereza ameahidi kutoa ushirikiano kwa Vyombo vyote vya Haki jinai ili kutimiza majukumu yake ipasvyo(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza).

MSIKIE STEVE NYERERE ALIYOMJIBU MUNA LOVE

BILIONI MBILI KUWEZESHA WAHITIMU WA FANI ZA KILIMO SUA KUANZISHA MIRADI YA KILIMO BIASHARA

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Taasisi binafsi ya kusaidia Sekta ya kilimo nchini (PASS) imetenga kiasi cha shilingi Bilioni mbili kwa ajili ya kuwawezesha Wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kuweza kuanzisha miradi ya Kilimo Biashara .

Upatikanaji wa fedha hizo umelenga uanzishwaji wa miradi 100 ya majaribio katika Chuo hicho kupitia mpango wa Maalumu utoaji wa Mazoezi na Majaribio kupitia Vituo Maalum (Incubators)  vyenye lengo la kutoa uzoefu kwa Wajasiliamali Vijana .

Hatua hiyo imebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay baada ya kuingia makubaliano  na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya  kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo.

“Baada ya kuona uwepo wa changamoto ya Wahitimu katika masuala ya kilimo pamoja na fani nyinginezo wakishindwa kushiriki katika shughuli za kilimo-biashara baada ya kukosa mitaji PASS kupitia Idara yake ya Agribusiness Innovation Center (AIC)  imeona ije na mpango huu”

Amesema mpango huo  utawawezesha Wajasiliamali vijana kupata mitaji pamoja na nyenzo mbalimbali katika maeneo maalumu kwa lengo la kuwaandaa kuwa Wajasilimali watakao weza kumiliki Miradi ya Kilimo-Biashara.
Bwana Bohay amesema kipaumbele kitatolewa kwa Wajasiliamali Vijana watakaojihusisha na uzalishaji wa mbogamboga kwenye mahema (greenhouse), ufugaji wa samaki, Kuku, mbuzi, usindikaji na viwanda vidogo vya kuzalisha bidhaa zinazotokana na kilimo kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay akiongea katika hafla ya makubaliano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo iliyofanyika chuoni hapo mjini Morogoro. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda akitoa shukrani zake za pekee kwa Taasisi binafsi ya kusaidia Sekta ya kilimo nchini (PASS) jinsi walivyojitoa kuwasaidia wajasiliamali kujikwamua katika kilimo kibiashara ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa elimu.
Wageni pamoja na wakuu wa idara mbali mbali katika chuo kikuu cha SUA mjini Morogoro wakimsikiliza kwa makini makamu wa chuo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PASS Bwana Nicomed Bohay (katikati waliokaa) na Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda (kwanza kushoto) wakiasaini mkataba wa makubaliano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ya kuwaandaa kwa vitendo Wajasiliamali vijana wahitimu wa fani mbalimbali hususani katika sekta ya Kilimo. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa PASS na Chuo Kikuu cha SUA.
Wakibadilishana mkataba wa makuabaliano.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

WAZIRI KIGWANGALLA AWAPA NOTISI YA SIKU 45 WALIOVAMIA PORI LA AKIBA KIJERESHI KUHAMA

$
0
0

Na Hamza Temba-Simiyu
*Atoa miezi mitatu kwa Muwekezaji kurudisha Serikalini 
hati miliki ya kipande cha ardhi kilichopo ndani ya Pori hilo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewapa siku 45 wananchi wanaoishi kinyume cha Sheria ndani ya kinga (buffer zone) za Pori la Akiba Kijereshi kuondoka kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu. 

Ametoa agizo hilo jana alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi na kutatua changamoto zake.

Baada ya kushuhudia makazi na shughuli nyingine za kibinadam ndani ya pori hilo, Dk. Kigwangalla aliamua kutoa agizo hilo na kusema kuwa sheria za uhifadhi wa wanyamapori haziruhusu vitendo hivyo ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa kisheria pamoja na kingo zake (buffer zone) ambazo ni mita 500 kutoka kwenye mpaka halisi wa eneo la hifadhi.

"Mpaka itakapofika tarehe 31 mwezi ujao (Septemba) wananchi wote hawa wawe wameshaondoka eneo hili kwa hiari yao wenyewe, muwatangazie na mpime eneo hili vizuri muweke alama ili wajue ni wapi wanatakiwa kuondoka.

"Na ikifika tarehe 1 Septemba kama kuna watakaokuwa wamekaidi agizo hili, basi mfanye oparesheni maalum muwaondoe na msafishe kila kitu, ni lazima ifike mahali kila mmoja aheshimu sheria za nchi" alisema Dk. Kigwangalla kuuagiza uongozi wa pori hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Kijereshi na Meneja wa pori hilo, Dianna Chambi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu. Alitoa siku 45 kwa wananchi wote waliovamia kingo/bafa za hifadhi hiyo kuondoka kwa hiari yao. Kulia ni Mkuu wa Kanda wa Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Serengeti, Johnson Msella.

 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Meneja wa Pori la Akiba Kijereshi, Dianna Chambi (wa pili) kuhusu wananchi waliovamia hifadhi hiyo alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu.  
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua koki ya maji katika eneo la hoteli ya kitalii ya Kijereshi Tented Camp iliyopo ndani ya Pori la Akiba Kijereshi alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ametoa miezi mitatu kwa mmiliki wa hoteli hiyo kurudisha hati miliki ya kiwanja chenye hekta 464 kilichopo ndani ya pori hilo kwa kamishna wa ardhi kwakuwa ni batili na aendelee kutoa huduma kwa kuzingatia sheria na taraibu za uwekezaji. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la kingo/bafa la Pori la Akiba Maswa ambalo limevamiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli kilimo alipolitembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Mbunge wa Itilima, Njaru Silanga na Meneja wa Pori hilo, Lusajo Masin.


SIMBA SC YAPELEKA MAJESHI UTURUKI, CV YA KOCHA WAO MPYA USIPIMEE....

WAANDISHI WA HABARI ZA MAHAKAMA WAPEWA MAFUNZO KWA VITENDO MKOANI MOROGORO

$
0
0
Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Morogoro
Waandishi wa habari za Mahakama kutoka vyombo mbalimbali wamepatiwa mafunzo kwa vitendo katika Mahakama za Mkoa wa Morogoro ili kuona namna Mahakama hizo zinavyotekeleza majukumu yake ya kila siku.
Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wadau wa mahakama wakiwemo waandishi wa habari wanakuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa weledi.
Akitoa maelekezo namna mahakama zinavyofanya kazi, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele amesema kuwa , katika mahakama zipo kesi zinazosikilizwa katika Mahakama za wazi na nyingine husikilizwa Mahakama za ndani( Chamber).
” Kesi zote zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia mfano ubakaji, kesi za mambo ya ndoa au kesi yoyote ambayo itamhusisha mtoto kesi zao husikilizwa katika mahakama za ndani (Chamber)” ameongeza Mhe. Hakimu Nyembele.
Aidha, Mhe. Hakimu Nyembele amesema kuwa kwa mkoa wa Morogoro wamekuwa wakipokea kesi nyingi zinazohusiana na masuala ya unyang’anyi, madawa ya kulevya na ujangili unaosababishwa na mkoa huo kuzungukwa na mapori.
Akizungumza kuhusu suala la rushwa kwa makarani wa mahakama, Mhe. Nyembele ametoa rai kwa watumishi wote wa mahakama kuepuka kupokea rushwa na kuwa waaminifu katika utendaji wao.
Vilevile amesema kuwa katika kudhibiti suala la rushwa katika mahakama nchini, mahakama imetoa elimu kwa umma pamoja na matangazo ya huduma mbalimbali za kimahakama zinazotolewa bure mfano nakala za hukumu.
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe. Agnes Ringo amesema kuwa kwa sasa kuna utaratibu mpya wa namna kesi za watoto zinavyoendeshwa bila kutoa utambulisho rasmi wa mtoto husika.
Nae Mtendaji Mkoa wa Mahakama Nestory Mjunangoma amesema kuwa katika mkakati wa kuboresha huduma za mahakama, Mahakama mkoa wa Morogoro inatarajia kuanza ujenzi wa ghorofa nne katika mwaka huu wa fedha zitakazokuwa na huduma zote za kimahakama kuanzia Mahakama ya Mwazo hadi Mahakama Kuu.
Aidha, Mjunangoma ameongeza kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Mafunzo hayo ni moja ya mradi wa maboresho ya huduma za mahakama inayotekeleza programu mbalimbali chini ya mpango mkakati wa mahakama wa miaka mitano 2015/2016-2019/202 iliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
 Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotembelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwenye moja ya ziara za kimafunzo wakiwa katika semina ya Waandishi wa habari za mahakama mkoani Morogoro Alhamisi Julai 19, 2018.


 Waandishi wa Habari waliotembelea Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro wakimsikiliza Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Mhe. Elizabeth Nyembele (hayupo pichani) alipokuwa akiwapa ufafanuzi juu ya matumizi ya Mahakama ya wazi ‘open court’ .
 Mwandishi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Bw. Alpha Wawa akiuliza jambo kwa Mhe. Nyembele.
 Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Bw. Nestory Mujunangoma akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari waliotembelea katika Mahakama hiyo.
 Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele akiendelea kutoa somo kwa waandishi wa habari waliopo katika semina ya uandishi  wa habari za mahakama mkoani Morogoro, lengo la ziara hiyo ni kujifunza kwa vitendo jinsi Mahakama inavyofanya kazi. 
Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Wilaya Morogoro, Mhe. Agnes Ringo (aliyesimama kulia) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari waliotembelea Mahakama hiyo Julai 19, 2018.
Picha na Mary Gwera, Mahakama-Morogoro

NEWS ALERT: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea (kusini) Lee Nak-yon Kutua nchini kesho Jumamosi kwa ziara ya kikazi

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea,

Mhe. Lee Nak-yon (pichani) atafanya ziara ya kikazi nchini kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kuanzia tarehe 21 hadi 23 Julai 2018. Ziara hiyo itakuwa ya kwanza kufanywa na kiongozi wa ngazi ya juu kutoka Jamhuri ya Korea tangu nchi zetu mbili zianzishe mahusiano ya kidiplomasia mwaka 1992.  

Madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kufungua zaidi fursa za ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi katika ngazi na sekta mbalimbali. Mhe. Waziri Mkuu Lee atafuatana na ujumbe mzito wa maafisa wa Serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa. Ujumbe wa wafanyabiashara utakaoongozana na Mhe. Lee unatarajiwa kukutana na wenzao wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Wafanyabiashara uliopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 23 Julai 2018. Mkutano wa kwanza ambao ulikuwa na mafanikio makubwa ulifanyika Seoul mwezi Februari 2018.
Mhe. Lee Nak-yon atawasili nchini saa kumi na mbili na nusu jioni (12:30) ya tarehe 21 Julai 2018 na atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku inayofuata, Waziri Mkuu Lee na mwenyeji wake Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), watafanya mazungumzo rasmi jijini Dar es Salaam na baadaye watashuhudia uwekaji saini wa mkataba wa kuondoa hitaji la visa kwa wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za utumishi (diplomatic and official/service passport). Aidha, Mhe. Lee atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa ajili ya kusalimiana.
Jamhuri ya Korea ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania ambapo kupitia  Shirika la Kimataifa la Maendeleo (KOICA) na Mfuko wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (EDCF) yamekuwa yakitoa misaada na mikopo mingi ya masharti nafuu kwa Tanzania ikiwemo misaada ya fedha katika bajeti, ujenzi wa miundombinu ya jamii, mafunzo ya muda mfupi na mrefu, wataalamu mbalimbali wa kujitolea, vifaa na mashine kwa ajili ya sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.
Baadhi ya miradi ambayo imegharamiwa na Serikali ya Korea ni pamoja na Mradi wa kuboresha Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Chanika, Mradi wa Mfumo wa Usajili wa Meli na Mabaharia kwa Njia ya Mtandao Zanzibar, Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Taifa ya Taaluma na Tiba (MUHAS) kampasi ya Mloganzila na ujenzi wa daraja katika mto Malagarasi.
Vile vile, Korea ni mshirika mkubwa katika kusaidia maendeleo ya Bara la Afrika ambapo hivi karibuni katika mkutano wa Sita wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na Africa (KOAFEC VI) uliofanyika mwezi Mei 2018, Busan, Korea ambapo Serikali ya Korea ilitangaza msaada wa Dola za Marekani bilioni 5 kwa ajili ya Bara la Afrika kwa kipindi cha mwaka 2018/2020. Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika na msaada huo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam

19 Julai 2018

TANZIA: MAMA SALMA KIKWETE AFIWA NA BABA YAKE MZAZI, MAZISHI KUFANYIKA LEO IJUMAA SAA TISA KATIKA MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



KUMRADHI...
MABADILIKO KIDOGO YA RATIBA YA MUDA WA MAZISHI

Kwa niaba ya Familia ya Mama Salma Rashid-Kikwete na Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, nasikitika  kutoa taarifa kuwa leo Alhamisi Julai 19, 2018 Mama Salma Rashid Kikwete amefiwa na Baba yake Mzazi,  Mzee Rashid Mkwachu, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Shughuli za Msiba  zitakuwa yumbani kwa Mama na Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Msasani jijini Dar es salaam. 

Mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu  leo Ijumaa Julai 20, 2018 Saa tisa kabla ya Swala ya Alasiri (kunradhi, sio saa 10 kama ilivyotangazwa awali). Kisomo na dua vitafanyika hapo Msasani  kabla ya Swala ya Ijumaa.

Kwa niaba ya Familia 
Ridhiwani Kikwete



MBEBA MIZIGO ABEID AMRI ANYAKUA KOMBE LA‘SUPA MZUKA CUP’ LA MILIONI 300

$
0
0

TatuMzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini Tanzania leo umemkabidhi Mshindi wa kampeini ya ‘SupaMzuka Cup’ aliyeshinda katika fainali tarehe 15 Julai 2018 kitita cha milioni 300 za kitanzania.

Abeid Amri, 28 anayeishi Mbagala Wilaya ya Temeke Dar es Salaam ndiye ameibuka mshindi wa Jackpot kubwa kuwahi kutokea nchini Tanzania. Amri hakushinda peke yake bali alichagua timu yake ya watu 10 ili kukamilisha timu yake ya watu 11 ambapo kila mmoja amepata milioni 1.

“Tumepata faraja kubwa kushuhudia Mtanzania mwenzetu akipata ushindi mkubwa kiasi hiki. Umetuandikia historia leo kwa sababu haijawahi kutokea nchini Tanzania mtu kushinda million 300. ” Alisema Bwana Sebastian Maganga, Mkurugenzi wa mawasiliano wa TatuMzuka

Kwa Msimu huu wa SupaMzuka Jackpot watu wamecheza na kushinda na marafiki, na Bwana Amri pia alichagua timu yake ambao ni; 1 Mwanaidi Omary, 2.Subira Issa 3. Jasmin Issa 4. Shufwaa Issa 5. Farhat Issa 6. Omary Issa, 7. Amin Issa 8. Mwanaasha Omary, 9. Agness Samwel, 10. Magdalena.

“Mimi sijala vizuri, wala kulala tangu siku hiyo jumapili. Kila saa nawaza kama ni ndoto alafu nitaamka, lakini sasa naamini kabisa kwamba ni kweli nimeshinda” aliezea Amri. “Nina furaha sana na pia kushinda na marafiki, najiskia kama wengi tumeshinda!” alisisitiza Amri.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa TatuMzuka Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),wakati wa akimtambulisha Mshindi wa kampeini ya ‘SupaMzuka Cup’ aliyeshinda katika fainali tarehe 15 Julai 2018 kitita cha milioni 300 za kitanzania,Abeid Amri mkazi kutoka Mbagala

Abeid Amri, 28 anayeishi Mbagala Wilaya ya Temeke Dar es Salaam ndiye ameibuka mshindi wa Jackpot kubwa kuwahi kutokea nchini Tanzania. Amri hakushinda peke yake bali alichagua timu yake ya watu 10 ili kukamilisha timu yake ya watu 11 ambapo kila mmoja amepata milioni 1. Mwakilishi kutoka kampuni ya michezo ya kubahatisha Abdallah Hemed
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo 
Mkurugenzi wa mawasiliano wa TatuMzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa kampeini ya ‘SupaMzuka Cup’ aliyeshinda katika fainali tarehe 15 Julai 2018 kitita cha milioni 300 za kitanzania,Abeid Amri mkazi kutoka Mbagala

WAZIRI MHAGAMA AITAKA NSSF KUIFIKIA SEKTA ISIYO RASMI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwa na mkakati utakaoliwezesha Shirika hilo kuifikia sekta isiyo rasmi ili kuwezesha shirika hilo kupanua wigo wa hifadhi ya Jamii na kukusanya michango itakayowezesha shirika kulipa mafao kwa wakati na kufanya shughuli za uwekezaji nchini.

Akizungumza na wajumbe wa Bodi na menejimenti ya NSSF jana tarehe 18 Julai 2018, jijini Dar es Salaam, Mhe. Mhagama alifafanua kuwa sekta isiyo rasmi ni moja ya sekta ambayo haijafikiwa na hifadhi ya jamii kwa kiwango cha kuridhisha, hivyo NSSF haina budi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inafikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Mfuko huu pamoja na mambo mengine umepewa jukumu la kusimamia sekta isiyo rasmi na katika sekta ambazo hazijafikiwa na hifadhi ya jamii kwa mujibu wa ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na sekta isiyo rasmi, hakikisheni mnaifikia sekta hiyo, hamuwezi kufanya uwekezaji katika miradi bila kuwa na wanachama wanaochangia mfuko ” Amesema Mhagama.

Katika mkutano huo, Mhe. Mhagama alimtambulisha Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii, Bw. William Erio, na kumtaka Mkurugenzi huyo kusimamia kwa weledi shuhghuli za uwekezaji zinazofanywa na NSSF nakuhakikisha mradi wa Mkulazi unafikia malengo na unazalisha sukari kama ilivyokusudiwa.Mhe. Mhagama amemtaka Mkurugenzi huyo kufikia maamuzi ya mwisho kuhusu mradi wa Dege na kufanya mapitio ya miradi yote na kuona hali halisi ilivyo na kufanya maamuzi stahiki na kuleta tija kwa wanachama na taifa.

‘’Mkurugenzi uendelea kulinda fedha za wanachama na kulipa mafao kwa wakati. lakini Bodi pamoja na menejimenti ya NSSF, mpeni ushirikiano Mkurugenzi huyu na fanyeni kazi kwa uadilifu na uzalendo ili kuweza kuhakikisha kuwa mfuko huu unakuwa na tija kwa wanachama na kujenga uchumi wa nchi” Amesema Mhagama.

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilianzishwa chini ya sheria Na. 28 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sura Na. 50 na Sheria ya pensheni kwa watumishi wa umma Na. 2 ya mwaka 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu akifafanua jambo wakati wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ( wa kwanza) akifuatilia kikao, wakati wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifuatilia kikao wakati walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, jijini Dar es Salaam.

KASI YANGU WIZARANI HAITAPUNGUA BALI ITAONGEZEKA ZAIDI- LUGOLA

$
0
0
 *Pia agusia aina ya suti anazovaa ambazo zimeibua mjadala

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema kuwa kasi aliyoanza ndio ambayo itaendelea zaidi ya hapo na kusisitiza kasi yake ni kama gari imeanza na zero na sasa inazidi kwenda mbele.

Kuhusu kuona kuwa anavaa vazi la aina moja(Suti)kila siku amesema anazo nyingi lakini ameamua zote zinafanane , hivyo hata anapobadilisha hakuna anayejua.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo wakati anazungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu ambayo ilitaka kufahamu mambo mawili kutoka kwake likiwemo la mavazi anayovaa ambayo yamekuwa gumzo pamoja na kasi aliyoanza nayo.

Lugola ameteuliwa na Rais Dk.John Magufuli kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Dk.Mwigulu Nchemba.

Hata hivyo baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo Lugola ameonekana kuwa na kasi kubwa katika kutekeleza majukumu yake.

Kuhusu mavazi Lugola amesema kuwa anazo nguo nyingi tu lakini amemua ziwe katika muonekano huo ambao sasa wengi wanauona na ataendelea kuonekana hivyo hivyo.

Wakati alipoulizwa hukusu kasi yake amesema "Kasi yangu ni kama vile unavyoona spidi ya gari ambayo inaanza na Zero lakini kadri unavyokanyaga mafuta ndivyo inavyoongezeka.

"Hivyo kasi ambayo nimeanza nayo ni kama Zero kwenye gari na itaongezeka zaidi ya hapo.Wanaodhani natania au nafanya mzaha wafahamu tu si tanii na wala sifanyi mchezo bali ninatekeleza majukumu yangu kwa kasi,"amesema Lugola.

Waziri Ndalichako akabidhi magari 47 kwa wathibiti ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya

$
0
0
 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kukabidhi magari 47 kwa ajili ya wathibiti wa  ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika hafla iliyofanyika hapa Mjini Dodoma.
 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia  Profesa Joyce Ndalichakoakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa magari hayo kwawathibiti  wa ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika hafla iliyofanyika hapa Mjini Dodoma.
 Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika gari mara baada ya kuzindua
Sehemu ya magari ya wathibiti wa  ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Profesa Joyce Ndalichako amekabidhi magari kwa ajili ya kuimarisha Uthibiti wa ubora elimu.
Jumla ya magari hayo ni 47, ambapo  magari 45 ni kwa ajili ya wathibiti ubora wa  Shule  wa Kanda na Wilaya na magari  mawili  kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo mjini Dodoma Profesa Ndalichako amesema  wathibiti ubora  wa shule kutumia  magari hayo   kwa malengo yaliyokusudiwa na hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaotumia magari hayo kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
Amesema kwa mujibu wa Dira yetu ya Maendeleo, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 Tanzania inalenga kujenga uchumi wa Viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Profesa Ndalichako amesema kufikia malengo ya uchumi wa kati  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndiyo yenye dhamana ya kusimamia utoaji elimu, ujuzi, maarifa na stadi zitakazowawezesha vijana wetu kutoa mchango unaotakiwa katika ujenzi wa uchumi wetu.
Aidha Wizara itasimamia vyema elimu na mafunzo yatolewayo ili kuhakikisha yanakuwa bora na yanatoa mchango wenye tija katika ujenzi wa uchumi wetu.  
“Ninathubutu kusema kuwa Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inasimamia kwa dhati kabisa jukumu hili la utoaji wa elimu bora kwa kununuaa pikipiki 2,894 ambazo zimesambazwa kwenye Halmashauri 156 katika mikoa 25 kwa ajili ya kusaidia  Waratibu Elimu Kata katika kutekeleza majukumu yao ili kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa shuleni katika maeneo yao.

UTENGENEZAJI WA CHOKAA KIGAMBONI, DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwananchi akiwa katika harakati za kutengeneza chokaa eneo la ufukwe wa Kigamboni jijini Dar es salaam. Rangi hiyo ya asili imekuwa ikitengenezwa nz kutumiwa kwa karne na karne

Mkeka wa Arusha-Dodoma unanoga!

$
0
0
Mkeka wa Arusha-Dodoma ambao una urefu wa Kilometa 329 au maili 204 

WATUMISHI WA AFYA WASIOTAKA KWENDA MIKOANI NDANI YA SIKU 14 WANAJIFUTA KAZI WENYEWE

$
0
0
Watumishi wa kada mpya ya afya wasiotaka kwenda kufanya kazi mikoani ndani ya siku 14 ambazo wameitwa kwa ajira mpya kinyume nah apo watakuwa wamejifuta kazi wenyewe,  amesaema Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  alipotembeleaa Hospitali ya Rufaa mkoa Kigoma Maweni wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya utoaji huduma za afya mkoani humo .
“Watumishi walioitwa kazini kwenye ajira mpya ya kada za afyana Wizara ya afya na kupangiwa Hospitali ya za Rufaa za Mikoa wanatakiwa wawe wameripoti vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu kuitwa kazini asiyefanya hivyo atakuwa amejifuta kazi mwenyewe.
"Serikali kupitia wizara  hii imepanga kuweka utaratibu wa kuwafanya watumishi waliopo mikoani kupenda kufanya kazi kwenye vituo vyao vya kazi na wasitegee kupata uhamisho kwenda Dar es salaam", Waziri Ummy amesema, akiongeza  kuwa Serikali haitaki kumuona Mwanamke mjamzito yeyote anapoteza Maisha kwa sababu ya kutimiza wajibu wake wa kuzaa hivyo wanaimarisha miundombinu ikiwemo kujenga wodi za mama wajawazito na watoto pamoja na vyumba vya upasuaji wa dharura wa kutoa mtoto tumboni kuhakikisha mjamzito anajifungua salama.
Katika kuboresha Afya za wananchi wa Kigoma Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 ya kukarabati miundombinu ikiwemo Wodi ya wagonjwa mahututi,Jengo la wagonjwa wan je (OPD), Wodi ya wagonjwa wa dharura na chumba cha upasuaji katika Hospitali hiyo ya Maweni.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Paul Chawote amesema kuwa amepiga hatua katika kupunguza vifo vya wajawazito mpaka kufikia vifo 34 ukilinganisha na miaka ya nyuma kwani walikuwa wanafanya vibaya.
Aidha Dkt. Chawote amesema kuwa idadi ya wajawazito wanaojifungulia kwenye katika vituo vya afya ni asilimia 78 na wajawazito wanaohudhuria kliniki ni asilimia 98 na upatikanaji wa dawa katika mkoa huo ni asilimia 95.
Mbali na hayo dkt. Chawote amesema kuwa mbali na mafaniko hayo kwenye huduma za afya bado Mkoa Kigoma unasumbuliwa na maambukizi ya Malaria ingawa upatikanaji wa dawa ,unyunyiziaji wa dawa kwenye mazalia ya mbu pamoja na kugawa vyandarua vyenye dawa vinafanyika kwa kaiasi kikubwa.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mama mzazi Bi. Leticia Lukurugu (23) mkazi wa Kigoma mara baada ya kujifungua salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni , kulia ni daktarin Bingwa wa watoto katika hospitali hiyo Dkt. Yakayashi Macrice wakati wa ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni , kulia ni daktarin Bingwa wa watoto katika hospitali hiyo Dkt. Yakayashi Macrice wakati wa ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya mpango wa Serikali juu ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi waliofika kupata matibabu katika salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni wakati wa ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiona wagonjwa na kukagua miundombinu ya  wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni wakati wa ziara yake mkoani humo.


ZIARA YA MWALIMU NYERERE YA IKULU YA MAREKANI MAKA 1963

WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE.

$
0
0
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amempa mwezi mmoja mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kukamilisha kazi hiyo hadi tarehe 31 Agosti mwaka huu ili kurahisisha mawasilino kwa wananchi wanao tumia daraja hilo.

Waziri Mhagama ameyasema hayo hapo jana tarehe 19 Julai 2018, alipotembelea katika daraja la Nyerere ili kukagua ujenzi wa barabara hiyo na uendeshaji wa shughuli katika daraja la Nyerere ambapo amesema serikali kutokamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kunasababisha kero kwa wananchi wanaovuka kwa miguu na wanaovuka kwa kutumia vyombo vya usafiri kushindwa kupita kwa urahisi, hali inayochangia kupungua kwa mapato yanayokusanywa darajani hapo.(PAUSE-INSERT)

Kwa upande wao Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio na Mkandarasi wa barabara hiyo, Mhandisi Jamal Mruma wote kwa pamoja wamemuhakikishia Waziri Mhagama kutekeleza maagizo hayo kwa wakati ili kuondoa usumbufu uliopo kwa sasa katika daraja na kuweza kuongeza makusanyo ya mapatokatika daraja hilo.

Mbali na gaizo hilo la kukamilishwa kwa barabara , pia
Waziri Mhagama amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kuhakikisha unawekwa mfumo bora wa utambuzi wa vyombo vya usafiri vinavyovuka darajani hapo ili kujua gharama halisi ya tozo ya vyombo vinavyovuka na kuepuka upotevu wa mapato kutokana na kutokuwa 
na mfumo wenye kutambua tozo halisi kwa vyombo hivyo.

Daraja la kigamboni tangu lianze kufanya kazi mwezi Mei mwaka 2016
hadi mwezi Juni 2018, mpaka sasa limeingiza mapato ya takiribani shilingili bilioni 17.1 mapato hayo yanayotokana na tozo kwa vyombo vya usafiri vinavyopita katika daraja hilo.

Imetolewa na Afisa Uhusiano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF
Angella Msangi.

TUNATEKELEZA: MAKUBWA YALIYOFANYIKA SERIKALI YA AWAMU YA TANO SEKTA YA ELIMU

NEWZ ALERT:MKURUGENZI WA BRELA ATENGULIWA,KUPANGIWA KAZI NYINGINE

PROF MBARAWA AWATAKA MAKAMPUNI YA UCHIMBAJI VISIMA KUOMBA VIBALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa ameyataka makampuni ya uchimbaji visima kuomba vibali ili waweze kuchimba visima hivyo pamoja na ulipaji wa kodi ya utumiaji wa maji.

Hayo yamesemwa na Waziri leo alipokagua visima vya kampuni ya Winners Traders iliyochimba visima katika Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.

Prof Mbarawa amesema kuwa jukumu la utoaji vibali la uchimbaji wa visima ni kutoka kwa Bonde la Wami Ruvu na ni lazima wakubaliwe kwa ajili ya kuendelea na shuguli zao za kuchimba wakiwa wamekamilika.

Amesema kuwa, makampuni mengi yamekuwa yanachimba visima bila kuwa na vibali na amewataka wamiliki wote kuanza kufuatilia vibali ili waweze kupewa haki ya uchimbaji ikiwemo na kulipa kodi ya kila mwaka kwa serikali.

"Awali katika Wilaya ya Temeke ukiwa unachimba kisima unatumia mita 40 unakuta maji ila sasa hivi unaweza kufika mita 90 ndio unakutana na maji hilo linatokana na uharibifu uliokuwa umefanywa na watu wasio waaminifu kuchimba pasipo kuwa na kibali kutoka kwa wahusika ambao ni Bonde la Wami Ruvu," amesema Prof Mbarawa.

Kwa upande Bonde la Wami Ruvu, Afisa Maji Wami Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa jukumu la utoaji vibali ni la kwao na utakapokuja kuomba lazima ulipie hicho kibali pamoja na ada ya kila mwaka, yapo makampuni waliyopewa na wengine hawajapewa tuliwakatalia ila wamekuwa wanaendelea kuchimba.

Ngonyani ametoa rai kuwa, wanawapa muda ili makampuni hayo yaende wenyewe kushughulikia vibali kwa wakati kabla hawajaanza kuwachukulia hatua kwani wamekuwa wanakwepa kulipa kodi kutokana na kuchimba visima kinyemela.

Prof Mbarawa amekuwa katika ziara maalumu ya kukagua miradi mbalimbali ya maji ikiwemo kwenye viwanda vinavyopata huduma za maji kutoka DAWASCO.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa anafuatilia namna Mtaalamu Usanifu Maabara wa Maji Ramadhan Zahoro wakati alipotembelea kisima kilichochimbwa katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiangalia moja ya Kisima kilichochimbwa katika Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kukagua kisima kilichopo Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa na Uhuru Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images