Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

MKUU WA WILAYA YA MONDULI AKAGUA MADHARA YA MOTO ULIOTEKETEZA BIASHARA KADHAA KIJIJI CHA IRERENDENI

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta ametembelea waathirika wa janga la moto huko katika kijiji cha Irerendeni kata ya Engaruka akiwa amefuatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Julias Kalanga 
Kwenye ziara hiyo viongozi hao walijionea adha iliyokumba wafanyabishara hao kwa kuunguliwa na vibanda vyao vya maduka  kwa moto ulioanza tarehe 17.07.2018 saa saba usiku na kudumu kwa saa tano na kuleta athari kubwa na kifo kwa mfanyabiashara mmoja aliyejulikana ka kwa jina la Siriel massawe ambaye umauti ulimkuta baada kuzidiwa na moto mkubwa ndani. 
Jumla ya maduka saba yaliteketea kwa moto na Mkuu wa wilaya aliwapa pole sana waathirika na kuwataka kuwa watulivu wakati vyombo vya ulinzi vikifanya uchunguzi.  
Pia kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imeahidi kutoa mkono wa pole Tsh.200.000/= kwa kila mfanyabiashara na kuwalipia madeni ya Mikopo yao waliokopa kwenye taasisi za kifedha baada uhakiki mikopo yao.  
  Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta (mwenye fimbo) akikagua madhara ya moto uliotokea katika kijiji cha Irerendeni kata ya Engaruka akiwa amefuatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Julias Kalanga 
 Sehemu ya eneo likionesha madhara ya moto uliotokea katika kijiji cha Irerendeni kata ya Engaruka akiwa amefuatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Julias Kalanga 
 Madhara ya moto huo
Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta akitoa maelekezo na kuwapa pole kwa waathirika wa  madhara ya moto uliotokea katika kijiji cha Irerendeni kata ya Engaruka akiwa amefuatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Julias Kalanga 

UJENZI WA RELI YA KISASA WAFIKIA ASILIMIA 16 ,VIONGOZI WA TRC WAITEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YOTE

Balozi Dkt. Abdallah Saleh Possi akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Romania Bw. Klaus Werner Lohannis

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Saleh Possi akiwasilisha hati za utambulisho  kwa Rais wa Romania, Bw. Klaus Werner Lohannis Jumatano Julai 18, 2018 mjini Bucharest, Romania. Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin, Ujerumani,  pia unahudumia maeneo mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo nchi ya Romania.

 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Saleh Possi akipeana mikono na  Rais wa Romania Bw. Klaus Werner Lohannis baada ya wasilisha hati zake za utambulisho  Jumatano Julai 18, 2018 mjini Bucharest, Romania. 
  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Saleh Possi akipozi na  Rais wa Romania Bw. Klaus Werner Lohannis baada ya wasilisha hati zake za utambulisho  Jumatano Julai 18, 2018 mjini Bucharest, Romania. 
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Saleh Possi akiagana na  Rais wa Romania Bw. Klaus Werner Lohannis baada ya wasilisha hati zake za utambulisho  Jumatano Julai 18, 2018 mjini Bucharest, Romania. 

Kuwait yakabidhi misaada yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa wahanga wa mafuriko Wilaya ya Same Kilimanjaro

$
0
0
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al- Najem (kanzu nyeupe) amemkabidhi Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki misaada ya kibinadamu na vyakula tani saba vyenye thamani ya dola za marekani 8500 sawa na shilingi milioni 20 takriban kwa kaya 980 za wananchi 7,000 waliokumbwa na mafuriko katika kijiji cha Ruvu Jiungeni Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. 

Hafla ya kukabidhi misaada hiyo iliyotolewa na Serikali ya Kuwait kwa kupitia Ubalozi wake ulipo nchini ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemery Sinyamule, Kaimu Mkuu wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki, Suleiman Saleh, maafisa mbalimbali wa Serikali na wananchi wa Kilimanjaro.

Akikabidhi chakula hicho ukiwemo, mchele, mahindi, maharage, sukari na mafuta ya kupikia ,  Balozi Al-Najem ameahidi kutoa misaada zaidi kwa wahanga wa mafuriko hayo yakiwemo mahema.

Naye Waziri wa  Madini, Angela Kairuki amezitaka kamati za ugawaji za ngazi zote kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na kuahidi kuendelea kutafuta wahisani zaidi kwa kuwa wahanga hao bado mahitaji yao ni makubwa.
 Sehemu ya misaada uliyotolewa na Serikali ya Kuwait kwa kupitia Ubalozi wake ulipo nchini ikiwa tayari kugawiwa kwa walengwa, baada ya kupokelewa na Waziri wa  Madini, Angela Kairuki katika kijiji cha Ruvu Jiungeni Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

WADAU SAME WAHIMIZWA KUMALIZIA MICHANGO YAO ILI KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA

$
0
0
WADAU mbalimbali wilayani Same wamekumbushwa kukamilisha ahadi zao ili kufanikisha ujenzi wa madarasa 50 yaliyokusudiwa ili ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu yawe yamekamilika. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule wakati akizungumzia michango ya ujenzi wa madarasa hayo ambapo kata 10 ambazo zimekamilisha michango zimekabidhiwa fedha za kukamilisha majengo. 

Uzinduzi umefanyika katika Shule ya Msingi Moipo iliyopo katika Kata ya Mabilioni.Hivyo moja ya mambo ambayo wadau wamekumbushwa ni kukamilisha ahadi ili kazi hiyo ikamilike.Uzinduzi wa ujenzi umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Wikaya ya Same, Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani na wataalamu. 

" Ukamilishaji wa madarasa haya utawezesha watoto 2250 kupata madarasa ya uhakika ya kusoea,"amesema Mkuu wa Wilaya hiyo wakati anawashukuru wananchi waliochangia.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashaurinameahidi kusimamia vizuri michango hiyo na kuagiza kuwe kunatolewa taarifa ya matumizi kwa wananchi. 

Wakati huo huo wananchi wahimizwa kuhakikisha watoto wanaenda shuleni ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake ya kutaka watoto wote wapate elimu bure, wale watoro wazazi wao kushughulikiwa. 

" Elimu bora ni wajibu wa kila mwanajamii".
 Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule akipokea Mbuzi kwa mmoja wa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi  wa madarasa 50 yaliyokusudiwa  kukamilia ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu.
 Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule akipokea vifaa vya ujenzi  ikiwemo mifuko ua Saruji na Mabati kutoka Wananchi ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi  wa madarasa 50 yaliyokusudiwa  kukamilia ifikapo Novemba, 2018 mwaka huu. 
 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wamekaa nje ya jengo la shule ambalo linatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Kamati ya Bunge yazindua minara ya Tigo wilayani Gairo

$
0
0
Mwenyekiti wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Dk Joseph Kilongola akitoa risala zake wakati wa hafla ya uzinduzi wa minara ya simu itakayowezesha upatikanaji wa mawasilino kwa mara ya kwanza katika kata za Kumbulu, Balama na Nongwe, WIlaya ya Gairo Mkoani Morogoro. Minara hiyo ilijengwa kwa ushirikiano baina ya Tigo na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuzinduliwa jana na wahemshimiwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano ya Bunge. 
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge - Miundombinu, Mhe mbunge Rashid Mohammed Chwachwa (Masasi- aliyejifunga shuka) wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Naibu Waziri wa Miundombinu - Mhe Eng Atashasta Ndikiye (katikati aliyevaa kofia) wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakiigiza adha walizokuwa wanazipata kupata mawasiliano ya uhakika ya simu wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo. Mnara huo pamoja na mingine katika kata za Balama na Nongwe ilijengwa kwa ushirikiano baina ya Tigo na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuzinduliwa na wahemshimiwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano ya Bunge.

MAFUNZO YA MAAFISA UANDIKISHAJI WA CHF ILIYOBORESHWA YAFANYIKA WILAYANI CHEMBA

$
0
0
Na Shani Amanzi


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amewataka waandikishaji waliopata Mafunzo ya maboresho ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) wakawatumikie vyema Wananchi kwani lengo kubwa la Serikali ni kuona jamii inapata huduma bora ya Afya. 

Dkt. Semistatus Mashimba aliyazungumza hayo alipokuwa anafungua mafunzo ya siku mbili ya Maafisa uandikishaji wa CHF wa vijiji vyote vya wilaya ya Chemba kwa kushirikiana wadau wa mradi wa HPSS-Tuimarishe afya kuanzia Tarehe 16 mpaka 17 Julai 2018 katika ukumbi wa Godown mjini Chemba. 

“Nawaomba muwe mabolozi wazuri kwa wilaya ya Chemba kwa kupunguza malalamiko na kutoa elimu ya kutosha juu ya mabadiliko ya bei ya uandikishaji wa kitambulisho cha bima ya Afya ya CHF Iliyoboreshwa kutoka tsh 13,000/= kwenda tsh 30,000/=, na lengo kubwa la serikali ni kuwasaidia wananchi hasa walio kwenye hali ya chini kupata huduma za afya katika vituo mbalimbali vya afya vilivyoko nchini” aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Semistatus Mashimba. 

Naye Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) wilaya ya Chemba Ndg. Haruna Haji amesema katika zoezi la uandikishaji Wilaya ya Chemba, atahakikisha kwanza anatoa elimu ya kutosha kwa Maafisa Uandikishaji wa Mfuko wa CHF katika kila kijiji ili kuondokana na vikwazo kwa wanachama wa CHF na pia atahakikisha elimu hii muhimu ya bima ya afya inawafikia wananchi wote wilayani hapo. 

Ndg.Haji amesema “katika uhifadhi wa nyaraka kuna utunzaji mkubwa na kuendelea kuwahamasisha kukusanya fedha kamili kabla ya kutoa kitambulisho pia tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi maboresho yanayoendelea ya CHF ikiwemo bei mpya ya kitambulisho cha CHF. 

Vilevile Afisa wa Mradi wa HPSS- Tuimarishe afya wilaya ya Chemba bi. Salome Chilongani ametoa shukurani zake kwa mkuu wa wilaya pamoja mkurugenzi wa halmashauri ya Chemba kwa kuonesha ushirikiano wao mkubwa kwenye mafunzo hayo. 

Bi. Salome amesema “Kwanza nianze kwa kutoa pongezi na shukurani kwa viongozi wetu wa wilaya ya Chemba, yaani mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wa halmashauri, kwa kuonesha ushirikiano mkubwa sana kwenye mafunzo haya, kwakweli wameshiriki kikamilifu sana na wameweza kuwaelewesha Maafisa Uandikishaji hawa umuhimu wa elimu waliyoipata na kutoa msisitizo kuilinda dhamana waliyoibeba. 

Mimi kama mdau nimefarijika kuona jinsi viongozi hawa walivyotupokea na kujali shughuli zinazotekelezwa na mradi wa HPSS, nina matumaini mwaka mmoja baada ya mafunzo haya tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa na tutakuwa na wanachama wengi sana wa CHF katika wilaya yetu ya Chemba” 

 Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Semistatus Mashimba akizindua Mafunzo ya CHF iliyoboreshwa

Baadhi ya Wadau mbalimbali waliohudhuria mafunzo hayo.

TEMBO, NDEGE, CHATU NA UBUYU WAVUTIA MAELFU YA WATALII KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

$
0
0
Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii, Tarangire
Maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire iliyo umbali wa kilometa 118  kutoka jiji la arusha katika barababra ya lami ya Arusha-Dodoma, na Kusini Mashariki mwa Ziwa Manyara. 
Jina la hifadhi hii yenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,850 lina asili ya 
 Mto Tarangire unaotiririsha maji mwaka mzima kuelekea upande wa Kaskazini mwa hifadhi hii ndio umeipa hifadhii hii jina hilo, sababu ya uwepo wake katika kipindi chote cha mwaka ni msaada mkubwa kwa maisha ya wanyamapori ndani na nje ya hifadhii hii. 
Hifadhi hii ni maarufu kwa makundi makubwa ya tembo wakubwa na wenye pembe ndefu kuliko hifadhi nyingine nchini Tanzania. 
Pia inaongoza duniani kwa kuwa na tembo wengi kwenye eneo la kilometa za mraba, ambapo unaweza kuona kundi la tembo zaidi ya mia tano kwa mara moja. Hifadhi hii pia ina mandhari nzuri ya kuvutia inayotokana na maumbile ya mibuyu inayosadikiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka elfu nane. 
Wanyama wa aina nyingi wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na punda milia, nyumbu, swala, simba, nyati, kongoni, chui, duma na wengine wengi pamoja na aina 550 za ndege . Hifadhi hii ni maarufu katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania ambapo wengi, kutoka ndani na nje ya nchi kwani hupenda kutembelea hifadhi hii. 
Umaarufu mwingine wa hifadhi hii ni pamoja ya aina ya chatu walio na uwezo wa kukwea miti. Kutokana na umaarufu huu idadi ya wageni wanaotembelea hifadhi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. 
 Unaweza kutembelea hifadhi hii wakati wote wa mwaka na kuwaona wanyama wote bila matatizo kutokana na mazingira mazuri ya hifadhi yanayosaidiwa na Mto Tarangire unaokatiza katikati ya hifadhi. 
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ina zaidi ya jamii 550 za ndege ambao ndio wamejulikana, na kati ya ndege hao baadhi yao wapo katika tishio la kutoweka. Tafiti zinaonyesha kwamba kipindi cha mvua ndio kipindi kizuri sana kwa aina nyingi za ndege kwenye eneo hili kuzaliana kwa wingi. Mabwawa na mito iliyopo katika hifadhi hii yanakuwa ndio sehemu nzuri zaidi ya kuona ndege wengi sana. Vile vile uoto wa asili katika hifadhi hii ndio unaopelekea wingi wa ndege katika eneo hili.
Tayari idadi ya watalii imeongezeka maradufu baada ya uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kutangaza kikamilifu vivutio adimu, vilivyoko katika hifadhi hiyo. 
 Watalii wanaoongoza kila mwaka kutembelea hifadhi hiyo ni watalii wa nje, wakati watalii wa ndani ni wachache, hali inayotokana na ukweli kwamba Watanzania wengi kutojua kikamilifu vivutio vya hifadhi zao, hivyo hawajui wanachokikosa.
Takwimu za kuongezeka kwa idadi ya watalii Tarangire  zimo katika taarifa maalumu ya hali ya utalii katika Hifadhi ya Tarangire, iliyotolewa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire, Stephano Qolli. 
 Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watalii wa ndani waliotembelea hifadhi hiyo mwaka 2008/2009 ilifikia 72,757 huku wale wa ndani ni 31,953, ambapo jumla ni watalii 104,710. 
 Mwaka 2009/2010 watalii wa nje walikuwa ni 69,690 wakati watalii wa ndani walikuwa 33,136 na kufanya jumla ya watalii kuwa 102,826.
Taarifa inasema mwaka 2011/2012 watalii kutoka nje walikuwa ni 107,591 huku watalii wa ndani 47,795 hivyo kufikisha watalii 150,386. 
 Mwaka jana jumla ya watalii 112,163 kutoka nje ya nchi, walitembelea hifadhi hiyo huku wale wa ndani 65,038, hivyo kufikisha watalii 177,201.

Ubao ulio katika njia panda karibu na Minjingu katika barabara ya Arusha-Dodoma ikikualika kutembelea Tarangire

Familia  nzima ya watalii ikipumzika na kupata mlo wa mchana eneo lijulikanalo kama Matete Picnic area katikati ya Tarangire
Watalii wakiangalia tembo wakinywa maji ya Mto Tarangire
Watalii wakiangalia wanyama eneo la Matete Picnic area.


JAJI MKUU AWAASA MAWAKILI WAPYA KUWEKA NGUVU NYINGI VIJIJINI

MAAFISA UHAMIAJI WAANZA KUNOLEWA KATIKA MAFUNZO YA WADAU KATIKA MNYORORO WA UTALII

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
CHUO KIKUU cha utalii kinachotoa huduma ya utalii, ukarimu na utafiti kimeandaa kozi fupi kwa wadau muhimu katika mnyororo wa utalii wakianza na maafisa uhamiaji ili kuweza kushirikiana katika kukuza sekta ya utalii ambapo Chuo hicho kilicho chini ya Wizara ya Utalii na Maliasili, sekta ya utalii ni moja kati ya sekta ambayo huiingizia kipato serikali.

Akizungumza na vyombo vya habari Ofisa Mtendaji Mkuu Chuo Kikuu cha Utali Shogo Sedoyeka ameeleza kuwa dhima ya kuandaa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na watalii milioni 2 ifikapo 2020.

Ameeleza kuwa nguvu za ziada zinahitajika ili kuweza kuyafikia malengo kwa kuwa sekta hiyo  mtambuka inashirikiana na sekta nyingi kama afya na miundombinu huduma ambazo watalii huhitaji wakiwa nchini.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wadau muhimu kama vile maafisa uhamiaji, polisi na usafirishaji na wadau wengine ili kuweza kufikia malengo na wameanza na maafisa uhamiaji.

Kuhusu mafunzo hayo Shogo ameeleza kuwa yatahusu mada mbalimbali kama vile: huduma kwa wateja, mapokezi, mbinu za kushughulikia malalamiko ya wateja, muda katika utoaji wa huduma, mawasiliano na wateja na jinsi ya kuhudumia wateja wenye mahitaji maalumu.

Amewataka maafisa wahamiaji kuzingatia mafunzo hayo ambayo mbali na kuongeza kipato kwa taifa wataitangaza nchi na  kupata watalii wengi zaidi kutokana na huduma bora zitakazotolewa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka(kulia) akifungua mafunzo ya  kuwajengea uwezo kwa maafisa uhamiaji ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na watalii milioni 2 ifikapo 2020 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam. 

 Baadhi ya maafisa uhamiaji wakisikiliza hotuba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka alipokuwa anafungua mafunzo kwa maafisa hao kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam leo.
Mkufunzi Jesca William akitoa mafunzo kwa maafisa uhamiaji kuhusu umuhimu wa wageni pamoja na sifa za mtoa huduma wakati wa mafuzo yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam.
Mafunzo yakiendelea

WAZIRI MKUU ATETA NA BALOZI MBELWA KAIRUKI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki na amempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya tangu aende huko.

Amekutana na Balozi Kairuki leo Alhamisi, Julai 19, 2018 katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, na amemtaka Balozi huyo ahakikishe anaboresha mahusiano kati ya Tanzania na China.

“Ni lazima nikupongeze kwa namna unavyoendelea kufanya kazi na unavyojitahidi kudumisha mahusiano na China. Tunashukuru kwamba wageni wanaokuja hapa nchini kutoka China wanatoa taarifa nzuri na jinsi unavyosaidia kuitangaza nchi yetu huko nje.”

“Umefanya kazi nzuri ya kuwaelekeza wawekezaji wa huko kwamba wakati tunaunda Serikali na kutengeneza mfumo wa utawala, tuliamua kujenga kwanza mifumo imara na kutambua fursa zetu tulizonazo ili baadaye Watanzania waweze kunufaika na hizo fursa.”

Amesema kupitia utaratibu huo, Serikali ilitaka Watanzania wamiliki ardhi ndipo mgeni apate, na kama kuna uzalishaji wowote unafanyika basi Mtanzania awe wa kwanza kunufaika, Serikali inufaike na mwekezaji naye anufaike.

“Tunakushukuru kwamba umesaidia kuwaambia wachina watulie wakati Serikali ikirekebisha mifumo yake. Na wao wameyaona mabadiliko hayo, kwani tumesimamia vita dhidi ya rushwa, na wao walikuwa ni waathirika wakubwa, lakini pia tumeongeza uwajibikaji. Watu wetu sasa wanawajibika kwenye viwanda na makampuni yao na Watanzania kwa ujumla, wametambua umuhimu wa kufanya kazi ili waweze kuishi,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali hivi sasa iko kwenye programu ya kutangaza utalii uliopo nchini hasa kwa kuamua kuagiza ndege kubwa zitakazobeba watalii na kuwaleta moja kwa moja hapa nchini.

“Sasa hivi tumepata wageni maarufu kutoka nje ya nchi akiwemo Rais mstaafu wa Marekani, Mheshimiwa Barack Obama na wachezaji maarufu duniani, kwa hiyo tunaendelea na mikakati yetu ya kutangaza utalii huko nje.”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam Julai 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam Julai 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TCRA YAWAWEKA KIKAANGONI HAMISA MOBETO, IRENE UWOYA

$
0
0

*Ni baada ya kuonesha picha zao za hovyo katika Instagramu zao

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WASANII Irene Uwoya na Hamisa Mobeto wamejikuta wakiwekwa kikaangoni na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) baada ya kuweka picha ambazo hazina maadili kwenye Instagramu zao.
Kwa mujibu wa TRCA ni kwamba Uwoya na Hamisa kila mmoja kwa wakati wake waliweka picha ambazo hazistahili na hivyo wameitwa kwa ajili ya kujieleza.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA Valerie Msoka amesema waigizaji hao wamekiuka kanuni ya maudhui inayomtaka msanii kuhakikisha maudhui anayoweka mtandaoni yanakuwa salama na hayamuumizi mtu.

Amesema Hamisa aliweka picha hizo Juni 23 na Uwoya aliweka picha Julai 17 mwaka huu na kwamba baada ya wasaini kuweka picha hizo kamati yao iliwaita ili wajieleze kwani wasichukuliwe hatua.
Ameongeza baada ya kuwasiliza wote wawili wamekiri kosa na kuomba radhi  huku wakiahidi kutorudia tena kufanya kosa la aina hiyo.
"Baada ya kuwasikiliza kamati ilitoa onyo kwa waigizaji hao kwani wakirudia hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kuwataka kuomba radhi katika kurasa zao za instagramu kwa lengo la kuwaelimisha mashabiki wao,"amesema.

UWOYA AISHAURI SERIKALI

Kutokana na onyo la TCRA, Uwoya ametoa ushauri kwa TCRA kutenga siku maalumu kwa ajili ya kutoa semina kwa wasanii wote nchini kwani si wote wenye kuelewa kuhusu kanuni za maudhui mtandaoni.

ALICHOSEMA HAMISA

Kwa upande wake Hamisa yeye amesema hatarudia tena kufanya kosa la aina hiyo huku akitoa ahadi ya kuwa balozi kwa wengine katika kuhakikisha wanaitumia vizuri mitandao ya kijamii na si vinginevyo.

GCLA Kutoa Mafunzo Endelevu ya Kemikali UDOM

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho -  MAELEZO
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imejipanga kuanza kutoa mafunzo endelevu ya matumizi ya kemikali katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kuongeza uelewa wa matumizi bora ya kemikali hizo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu juu ya matumizi ya kemikali kwa jumla ya wanafunzi 40 wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaosoma masomo ya Uhandisi wa Uchenjuaji Madini.

Dkt. Fidelice amesema kuwa moja ya kazi za Mamlaka hiyo ni kutoa elimu kwa wadau wa kemikali ili kuwawezesha kufahamu matumizi bora ya kemikali yakiwemo ya uzalishaji, usafirishaji, uuzaji pamoja na uhifadhi wa kemikali.

"Mafunzo ya masuala ya kemikali ni ya muhimu hasa ukizingatia nchi yetu inaelekea katika uchumi wa viwanda ambapo matumizi ya kemikali yataongezeka hivyo tunajipanga kuweka mikakati bora ambayo itatuwezesha kutoa mafunzo ya kemikali chuoni hapa kwa wanafunzi wanaosoma kozi zinazohusisha matumizi ya kemikali", alisema Dkt. Mafumiko.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama) akitoa hotuba wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wahitimu wa masomo ya Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Madini na Uchakataji Madini (B.Sc. Metallurgy and Minerals Processing Engineering) wa Chuo cha Sayansi ya Ardhi (CoES), Chuo Kikuu cha Dodoma, yaliyofanyika mkoani Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Ardhi (CoES), Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa William Mwegoha (aliyesimama), akizungumza kabla ya Mgeni Rasmi wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kuhusu Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wahitimu wa masomo ya Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Madini na Uchakataji Madini (B.Sc. Metallurgy and Minerals Processing Engineering) yaliyofanyika Dodoma na kuandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kati, Mkoani Dodoma.
 Washiriki wa mafunzo ya Matumizi Salama ya Kemikali yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kati, wakifuatilia hotuba ya kufunga mafunzo hayo iliyokuwa inatolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (hayupo pichani).
Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kati, Bw. Musa Kuzumila, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wahitimu wa masomo ya Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Madini na Uchakataji Madini wa Chuo kikuu cha Dodoma.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali.
 Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Ardhi (UDOM), Prof. William Mwegoha, watumishi wa Chuo, watumishi wa Maabara ya Kanda ya Kati na wahitimu walioshiriki mafunzo ya Usimamizi Salama wa Kemikali mara baada ya kufunga mafunzo hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Balozi Seif Ali Idd akutana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Naibu Waziri wake Dr. Suzan Alphonce Kolimba Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dr. Suzan Alphonce Kolimba, Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Ramadhan Muombwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Suzan Alphonce Kolimba kushoto akibadilishana mawazo ya kiutendaji na Balozi Seif walipokutana Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha  Mawaziri wa Wizara zinazofanana wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wale wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kukutana wakati unaporuhusu katika azma ya kubadilishana uzoefu kiutendaji ili kuboresha jukumu la kuwahudumia vyema Wananchi.

Alisema hatua hiyo muhimu ambayo ilikuwa ikifanyika katika kipindi tofauti itaendelea kujenga mapenzi zaidi, Umoja na Mshikamano  baina ya Watumishi wa Serikali zote mbili zilizopewa jukumu la kuwatumikia Watanzania wote.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Naibu Waziri wake Dr. Suzan Alphonce Kolimba ulipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kwa mazungumzo ya kubadilishana uzoefu.

Alisema Mikutano vikao vya mara kwa mara vya mazungumzo vitakavyowajumuisha  Mawaziri wa Wizara zinazofanana za pande hizo mbili hasa pale zinapojichomoza hitilafu ndogo ndogo katika pande mbili za Muungano husaidia kupunguza kero za Muungano.

“ Vikao vya mara kwa mara vya Mawaziri wa Wizara zinazofanana wale wa SMZ na SMT vina uwezo wa kupunguza au kuondoa kabisa vile vikao vya Watendaji Wakuu wanaokutana kujadili Kero zilizopo katika Muungano”. Alisema  Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe huo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwamba Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara  Kihistoria ni wamoja kwa Karne kadhaa zilizopita kutokana na maingiliano yao ya Mila, Kibiashara, Silka na Utamaduni.

Balozi Seif alieleza kwamba udugu huo ndio uliopelekea Waasisi wa pande hizo mbili kufikia makubaliano yaliyowezesha kurasimishwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania mnamo Tarehe 26 Aprili Mwaka 1964.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Uongozi  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Dr. Suzan Alphonce Kolimba alisema kazi inayokabili Viongozi hasa Mawaziri Wapya ni kuendelea kupata mawazo na fikra za watangulizi wao ili jukumu walilokabidhiwa na Taifa walitekeleze kwa ufanisi uliotukuka.

Dr. Suzan alisema licha ya Taaluma waliyokuwa nayo Viongozi wachanga lakini bado busara na hekima za wale wazoefu zinapaswa kujumishwa pamoja katika utendaji wao kwa lengo la kuwatumikia vyema Wananchi walio wengi Mjini na Vijijini Tanzania Bara na Zanzibar kwa ujumla.

Viongozi hao wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wapo Zanzibar kwa shughuli za Kikazi likiwemo suala la kuratibu masuala ya Kimataifa  yanayojumuisha Serikali zote mbili ile ya SMT na SMZ.

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUFUKIA VIFUSI BARABARA YA HALTON

$
0
0
 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akishiriki kusambaza kifusi kilichowekwa kwa ajili ya kufukia kifusi kwenye eneo la Halton ambalo mtaro ulikatika na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi hasa nyakati wa mvua.
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku katika akiwa na Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama CUF Taifa Masoud Omari kushoto wakifukia vifusi kwenye barabara ya Halton ili kuweza kuondoa kero ya wananchi kutokana na kuwepo kwa mtaro uliokatika.

DCB YATANGAZA KUPATA FAIDA YA SH. BILIONI MOJA

$
0
0
Said Mwishehe,Globu ya jamii
BENKI ya Biashara Dar es Salaam(DCB) imetangaza kupata faida ya Sh.bilioni moja katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2018 ambacho kimeishia Juni.

Akizumgumza leo Dar es Salaam Mkurugenzi wa Fedha wa DCB Zacharia Kapama amesema faida hiyo ni ongezeko la asilimia 106 kutoka faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2017.

"Ongezeko hilo la faida pia lilipatikana kutokana na kuimarika kwa mapato yatokanayo na riba pamoja na yale yasiyotokana na riba.

"Na limechagizwa na mkazo wa benki katika amana za gharama nafuu, usimamizi wa mizania wenye ufanisi, ufunguaji wa tawi la Dodoma na vituo vya huduma, ukuaji wa mfumo wa kibenki wa kidijitali na wa mawakala pamoja na ongezeko la wateja na miamala,"amesema.

Kapama amesema pia mafaniko hayo yametokana na ukuaji wa mikopo ambapo benki hiyo imefanikiwa kuongeza kiwango cha mikopo kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mikopo iliyokuwepo katika Desemba mwaka 2017.

Pia amesema ufanisi wa benki hiyo umeongezeka hasa katika usimamizi wa matumizi ya riba na yasiyo ya riba, ufanisi wa mizania na uboreshaji wa huduma za utoaji wa mikopo.

Amefafanua katika utoaji huduma, benki ya biashara ya DCB imefanikiwa kuongeza idadi ya wateja kufikia 191,133 katika nusu ya pili ya mwaka iliyoishia Juni mwaka 2018 kutoka 188,305 Desemba mwaka 2017.

"Ongezeko hili la wateja 2,828, limechangia kuimarisha mapato ya benki kupitia kuongezeka kwa miamala, amana za kudumu na utoaji mikopo.
Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati benki hiyo ikitangaza faida ya Sh.bilioni 1.0 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2018. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Rahma Gemina na kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa ndani Deogratias Thadei.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Uingereza kuwekeza Mkoani Morogoro

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe anamsikiliza Mgeni wake baada ya kumkabidhi kitabu kinachoonyesha maeneo ya Uwekezaji Mkoani Morogoro (Morogoro Region Investment Guide).

Na. Andrew Chimesela - Morogoro

Serikali ya Uingereza imeonesha nia ya kushawishi wawekezaji nchini mwake kuja kuwekeza hapa nchini hususan katika Mkoa wa Morogoro katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Kilimo, viwanda na Madini. Hayo yamefahamika jana Julai 18 mwaka huu wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro baina ya Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke na Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa huo.

Awali viongozi hao wawili walianza mazungumzo yao kuhusu miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Uingereza hapa nchini hususan iliyopo Mkoani Morogoro ikiwemo miradi ya Elimu - Educationa Programme for Results (EP forR), ambapo Mhe. Cooke alisema nchi yake imeongeza ufadhili wake kutoka 34% mwaka 2012 hadi 70/% mwaka 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke kitabu cha Uwekezaji.

Kwa upande wa Afya Balozi huyo alisema katika Mkoa wa Morogoro, Uingereza imefadhili Vituo vya Afya katika eneo linalolenga Mpango wa Uzazi kwa akina mama kupitia Mradi wa Population Service International (PSI) ambapo hadi sasa jummla ya akinamama 9,400 Mkoani humo wamefaidika na huduma hiyo.

Aidha, Viongozi hao wawili walizungumzia ufadhili unaotolewa na Uingereza katika nyanja za Maji na Usafi wa Mazingira ikiwemo Kampeni inayoendelea sasa Mkoani Morogoro ya usichukuliepoanyumbanichoo, Mkoa huo ukiwa ni Mkoa wa Majaribio katika Kampeni hiyo.

Pamoja na miradi mingine mingi waliyoizungumzia , Viongozi hao pia waligusia miradi ya Sekta ya Kilimo na Miundombinu. Kwa upande wa Sekta ya Miundombinu upo mradi wa IRAT yaani Improving Rural Access in Tanzania ambapo Uingereza imefadhili matengenezo ya makaravati ya barabara ya Chagongwe - Kumbulu iliyopo Wialaya ya Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe anamsindikiza mgeni wake, Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke baada ya kukamilisha mazungumzo yao.

Baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu miradi inayofadhiliwa na nchi ya Uingereza, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe alimshukuru Balozi wa Uingereza kwa Ufadhili wa miradi yote hiyo ukiwemo mradi mkubwa wa Upimaji na umilikishaji wa Ardhi unaotekelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi kupitia Land Tenure Support Programme.

Dkt. Kebwe ametumia fursa hiyo kumweleza Balozi Sarah Cooke uwepo wa maeneo mazuri ya uwekezaji katika Mkoa wa Morogoro na akawasilisha ombi kwa balozi huyo kushawishi wawekezaji walioko nchini mwake kuja kuwekeza Mkoani Morogoro katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Kilimo, viwanda na uchimbaji wa madini ya dhahabu na Graphite.

Balozi Sarah Cooke alionekana kushawishika na ombi la mwenyeji wake na kuahidi kulifanyia kazi haraka huku akiahidi kutafuta muda wa kufanya ziara katika Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kutembelea miradi wanayoifadhili lakini pia kutembelea maeneo ya uwekezaji kama alivyokuwa ameombwa na mwenyeji wake.

MAHAKAMA MORO YAZUIA WATUHUMIWA WANAOACHIWA KUKAMATWA NDANI YA VIUNGA VYA MAHAKAMA HIYO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Morogoro, imezuia watuhumiwa wanaoachiwa kwa kifungu ambacho kinaruhusu wao kukamata, kukamatiwa ndani ya viunga vya mahakama hiyo.

Hayo yameelezwa leo mkoani hapa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro Elizabethi Nyembele wakati wa ziara ya waandishi wa habari za mahakamani walipofika katika Mahakama hiyo.

Waandishi hao wapo katika mafunzo ya siku tano yambayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.Mafunzo hayo yameahirikisha waandishi 30 wa vyombo mbalimbali nchini.

Amesema, wamezungumza na Polisi wasiwakamate watuhumiwa pindi wanapokuwa wameachiwa ndani ya viwanja vya Mahakama kwani ni fedhea.

" Tumezungumza na Polisi wasifanye hivyo, kwa sababu mara nyingine mshtakiwa anakamamatwa hata mbele ya hakimu bila kujali wapo katika eneo gani,

" Mtuhumiwa anakufuata anakwambia mheshimiwa naomba nilinde wanataka kunikamata kitendo ambacho si kizuri na hakileti picha," amesema Hakimu Nyembele

Ameongeza kuwa, hakimu anapoifuta kesi huku akijua inahitilafu kisheria anamueleza mtuhumiwa kuwa anaweza kufunguliwa kesi nyingine.Wengine ni waelewa unamuachia pale pale anaingia mikono ni mwa polisi bila kukimbia
Hakimu Mkazi  Mwandamizi  Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Elizabeth Nyembele akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotembelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kwenye moja ya ziara za kimafunzo kwa Waandishi wa habari za mahakama mkoani Morogoro
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  Elizabeth Nyembele akizungumza na wananchi waliokuwa wakisubiri kuanza kwa mashauri yao kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro katika ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari  mkoani Morogoro.  (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MOROGORO)
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro  Elizabeth Nyembele akionyesha waandishi wa habari nembo ya iliyopo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza maelezo ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Mhe. Elizabeth Nyembele hayupo kwenye picha.
Mtendaji wa Mahakama mkoa wa Morogoro Nestory Mjunangoma akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Morogoro.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATU 18 MBARONI KWA TUHUMA MBALIMBALI MKOANI TABORA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

POLISI Mkoa wa Tabora linawashikiria watu 18 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuwachoma moto na wengine kushiriki katika mauaji. Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Emmanuel Jackson. Alisema watuhumiwa 16 wanashikiriwa kwa tuhuma cha kujaribu kuwaua wanawake wanne kwa kuwachoma moto.

Kamanda huyo alisema wananchi kwa kushirikiana na Polisi wa wilaya ya Kaliua waliweza kuwaokoa wanawake hao wanne waliokuwa wamekamatwa na walinzi wa jadi zaidi ya miambili.

Kamanda Jackson alisema kuwa julai 16 mwaka huu saa nne usiku huko msitu wa Hifadhi ya Isawima kata ya Igwisi wilaya ya Kaliua kiongozi wa Sungusungu aitwaye Ingese Irea akiwaongoza wenzake 200 na kuwakamata akinamama wanne.

Alisema kuwa watu hao waliwakamata akinamama hao waliotambuliwa kwa majina ya Velediana Paulo (70), Modesta Magazi (45), Joyce Elias Magazi (33) na Nyamizi Dotto (40) walitaka kuwaua wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.

Kamanda huyo aliongeza kuwa watuhumiwa hao na wenzao ambao bado wanasakwa baada ya kuwakata wakina mama hao walikusanya kuni nyingi na kisha kuwasha moto kwa dhumuni la kuwachoma.

Jackson alisema kuwa wakati watuhumiwa wakiendelea na za kufanikisha unyama huo taarifa toka kwa wananchi wema zilifika Polisi ambao bila kukawia walifika eneo la tukio na kuwaokoa na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao.

Matukio ya aina hii ambayo yameegemea kwenye imani za kishirikina yanaendelea kushamiri katika vijiji mbali mbali vya mkoa wa Tabora hasa ambako wanaishi jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma na kuupa mkoa sifa mbaya.

Mwishoni mwa mwaka uliopita watu wengine 55 wakazi wa kata ya Loya wilaya ya Uyui mkoani hapa akiwemo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho walikamatwa baada ya jaribio lao la kutaka kuwaua wakina mama wanne kwa kuwachoma moto kwa imani hizo hizo kushirikana.

Wakati huo huo jeshi la Polisi linamshikiria Maganga Machibya (22) anayetuhumiwa kumuua Edina Mayunga mkazi wa kijiji cha Ifumba Wilaya ya Nzega kwa kumkata shingo kutokana na imani za kishirikina.

Katika tukio jingine la mauaji Abdalah Salehe mkazi wa Ipuli Manispaa ya Tabora anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mkewe Regina Athuman kwakumpiga na kisha kumnyonga

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 19.07.2018

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images