Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA MPYA YA KLINIKI YA MOYO INAYOTEMBEA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuzindua huduma mpya ya kliniki ya moyo inayotembea (Cardiac Mobile Clinic) kwa kufuata wagonjwa popote pale walipo na kuwahudumia. Huduma hii maalum inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Ruvuma tarehe 23/7/2018.

Kuanzishwa kwa huduma hii kutasaidia wananchi wengi hasa wa mikoani ambako ni mbali na Taasisi yetu ilipo kufikiwa kwa urahisi zaidi na kupata huduma za matibabu ya moyo ya kibingwa.

Baada ya kufanyika kwa uzinduzi huo tutaendelea kutoa huduma kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 23-28/7/2018. Huduma hii ya kliniki inayotembea itakuwa endelevu katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Siku za karibuni tutatoa ratiba kamili kadri ya maombi yatakavyotufikia kutoka Tawala za Mikoa.

Huduma tutakazozitoa ni kutoa matibabu baada ya kufanya vipimo kwa kutumia mitambo mahususi tuliyokuwa nayo. Ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora, kutoa Rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa watakaokutwa na matatizo ya Moyo kuja kwenye Taasisi yetu kwa uchunguzi wa tiba zaidi.

Dhumuni la Taasisi ni kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma bora na kuwa na elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo. Wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma pamoja na mikoa ya jirani tunawakaribisha mfike katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (Songea) ili muweze kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Makatibu Wakuu kuonesha uwezo wao wa kusakata kabumbu

$
0
0
Na Lorietha Laurence -WHUSM,Dodoma.

Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wataonesha uwezo wao wa kusakata kabumbu siku ya Jumamosi ya tarehe 21 Julai 2018 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya Bonanza la michezo liloandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo.

Hayo yamesemwa leo Jijini hapa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Yusuph Singo ambapo ameeleza kuwa lengo la bonanza hilo ni kuhamasisha michezo kwa jaili ya afya pamoja na kuwakaribisha watumishi wa umma waliohamia Makao Makuu ya nchi . 

“Katika bonanza hili mtashuhudia mechi kali itakayowahusisha Makatibu Wakuu wa Wizara zote za Serikali pamoja na Watumishi wa Umma wakichuana vikali” amesema Bw. Singo.Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa mbali na fainali hizo kutakuwa na michezo ya ufunguzi ambayo ni mazoezi ya kutembea (jogging) ambayo yataanzia viwanja vya Jamhuri , kupitia Nyerere Square kuelekea mzunguko wa CDA (Round About)na kuhitimishwa katika viwanja vya Jamhuri.

Anazidi kufafanua kuwa baada ya mazoezi ya kutembea yatafuata mazoezi ya viungo (Aerobic) na baadaye mechi za ufunguzi ambazo ni mpira wa pete kati ya Watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Habari, na baadaye kufuatiwa na Makatibu Wakuu dhidi ya Watumishi wote.

Mechi nyingine ni mpira wa miguu kati ya Wizara ya Habari dhidi ya Ofisi ya Rais Utumishi, Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Viwanda na Biashara , Kampuni ya Tigo na Kikundi cha Muungano na mwisho ni kati ya Makatibu Wakuu na Watumishi.Bw Singo ameeleza kuwa mbali na kuhamasisha michezo pia Bonanza hilo linaunga mkono kauli mbiu ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi kwa afya. 

Wananchi wa Dodoma wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia Bonanza hilo lililosheheni michezo mbalimbali itakayochezwa katika Bonanza hilo ikiwa ni kuamsha ari ya michezo kwa watumishi na wakazi wa Jiji la Dodoma.

MJUE NA KUMSIKILIZA KING CHAVALA

HOSPITALI YA AMANA DAR YAKABIDHIWA VITANDA 10

$
0
0
HOSPITALI ya Amana jijini Dar es Salaam , imekabidhiwa vitanda 10 vya kujifungulia wanawake vyenye thamani ya Sh. milioni 14 kama msaada uliotolewa na ubalozi wa China.

Vitanda hivyo vilikabidhiwa jana kwa Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk.  Meshack Shimwera na Waziri wa Madini, Angella Kairuki baada ya kuomba msaada katika Ubalozi huo na kukabidhiwa vitanda 36.

Akizungumza wakati akikabidhi viwanda hivyo, Waziri Kairuki amesema vitanda vitano walikabidhi hospitali ya vijibweni, Temeke vitanda sita na Amana vitanda 10.Amesema pia wataendelea kuvigawa katika Kituo cha Afya Sinza na Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala lengo likiwa ni  kupunguza idadi ya wanawake wanaojifungulia chini au kwenye vitanda vya kawaida.

“Msaada huu ni katika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini. "Leo nakabidhi vitanda 10 na nitajitahidi kuleta vitanda vingine ili kumaliza kabisa tatizo hili katika Mkoa wa Dar es Salaam  na kuhakikisha kila mwanamke anajifungua sehemu salama, " amesema Kairuki.

Naye Mganga Mkuu, Dk. Shimwera amesema vitanda hivyo vitafungwa kwenye wodi mpya ya kujifungulia wanawake na mahitaji yao yalikuwa ni vitanda 17.“Tunamshukuru Waziri Kairuki na ubalozi wa China, vitanda hivi tutavifunga kwenye wodi mpya hivyo vitasaidia akina mama wanaokuja kujifungua katika hospitali hii," amesema.

Pia amesena wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa magari ya kubebea wagonjwa baada ya waliyokuwa nayo saba kuyagawa kwenye vituo vya afya.Amesema kwa kuanzia wanahitaji magari matano ya kubebea wagonjwa pamoja na mashine ya CT-Scan na vifaa tiba kwenye chumba cha upasuaji na cha wagonjwa mahututi.


“Kutokana na kukosekana kwa mashine ya CT-Scan tunalazimika kupeleka wagonjwa 3,000 katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila lakini kama tungekuwa nazo tungeweza kuwatibu wenyewe," amesema Dk. Shimwera.
Waziri wa Madini,Angella Kairuki akimkabidhi Mganga mkuu wa hospital Amana,Dkt Meshack Shimwela vitanda 10 jijini Dar as Salaam. Picha na Emmanuel Massaka wa MMG.
Waziri wa Madini,Angella Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM)

NAIBU WAZIRI ATEMBELEA VIWANDA VYA NGOZI KILIMANJARO

$
0
0
Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdalla Hamisi Ullega amefanya ziara mkoani Kilimanjiro kwa kutembele jumla ya viwanda vya ngozi vitatu na wadau wengine wa sekta ya mifugo.

Katika ziara hiyo Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Himo Tanners & Planters LTD Waiso amemweleza Naibu Waziri kuwa changamoto iliyopo kwa sasa katika kiwanda hicho ni pamoja na tozo nyingi zisizo na tija ambazo zinatozwa kuanzia Serikali ya kijiji mpaka Serikali Kuu. 

"Tozo zimekuwa nyingi mno katika Viwanda,ambapo inafikia wakati kiwanda kinashindwa kujiendesha kwa Ufanisi kwa sababu ya Muda na gharama za kufuatilia tozo hizo katika mamlaka husika,"amesema Waiso.

Aidha Waiso ametaja baadhi ya tozo hizo kuwa ni pamoja na Service Levy,Export Permit,Business Licence,Water use fee,Water right fee na Chemical Permit fee. 

Pia Ulega alipata fursa ya kutembele kituo cha Utafiti wa Mifugo, West Kilimanjaro (TALIRI), kiwanda cha kusindika ngozi cha Moshi Leather industries limited,Shamba la mifugo Kafoi,Watengenezaji wa chakula cha Mifugo, Marenga Millers Company LTD na kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Shamba la Kuzalisha Kuku wazazi la The Irvines Group katika Halmashauri ya Siha.
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (wapili kulia) akiwa ameambatana na Mmiliki wa kiwanda cha ngozi Himo Tanners & Planters LTD , akipewa maelezo namna viatu vinavyotegenezwa kwa ngozi katika kiwanda hicho kilichopo mkoa wa Kilimanjaro.
Wanachi wa kijiji cha Lekirumuni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifungo Mhe.Abdallah Ulega katika mkutano uliofanyika kata ya Ndinyika wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega (kijani) akitembelea Shamba la mifugo la Serikali (NARCO)
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mmiliki wa kiwanda cha ngozi  Himo Tanners & Planters LTD   akikagua ngozi kiwandani katika kiwanda hicho kilichopo mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na  wananchi katika mkutano uliofanyika cha kijiji cha Lekirumuni kata ya Ndinyika  wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

TRA YAWATAKA WENYE VIWANDA KUTOA TAKWIMU SAHIHI ZA UZALISHAJI WAO

$
0
0
Na Rachel Mkundai, Manyara
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara wenye viwanda vya kutengeneza mali ghafi za kutengenezea pombe kali kutoa tawimu sahihi ya kiasi kinachozalishwa na mahali inapouzwa ili serikali iweze kukusanya kodi yake stahiki kupitia pombe kali.

Hayo yamesemwa na Kamishna waKodi za Ndani wa TRA Bw Elijah Mwandumbya mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza sukari cha Manyara Sugar Company Limited kilichopo mkoani Manyara na kuongeza kuwa takwimu hizo zitawezesha TRA kufuatilia kwa karibu na kupata takwimu sahihi za kikodi na kuongeza makusanyo ya mapato.

“Tunafahamu kwamba “Molasis”  au mali ghafi inayotokana na zao la miwa baada ya kutengeneza sukari ni bidhaa inayotumika kutengenezea pombe kali na hivyo takwimu zitatuwezesha kufuatilia wafanyabiashara wanaonunua bidhaa hiyo na kutengenezea pombe kali ili nasi tukadai kodi yetu na kodi hiyo ilete tija kwa taifa”, amesema Bw. Mwandumbya
 Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (wa pili kulia) akiwa ameongozana na uongozi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited kuelekea katika eneo la uzalishaji sukari wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
 Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (katikati) akitoa maagizo kwa uongozi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited kuhusu kutoa takwimu sahihi uzalishaji sukari wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
 Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited, Bw. Pratap Sisudya wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Manyara Sugar Company Limited, Bw. Pratap Sisudya (katikati) akimweleza Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (wa pili kulia) moja ya mtambo utumikao kuzalisha sukari wakati alipofanya ziara ya kikazi kusikiliza changamoto za Wafanyabiashara.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VIONGOZI MBALIMBALI WAMIMINIKA MSIBA WA BABA YAKE MZAZI SALMA KIKWETE JIJINI DAR.

$
0
0
Rais Mstaafu awamu ya nne,Mh Dkt Jakaya Kikwete akimpokea Rais Mstaafu awamu ya pili Mh.Alhaji Al-Hassan Mwinyi wakati wakiwasili Msasani kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar. 
Rais Mstaafu awamu ya nne,Mh Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa aliyeambatana na Mkewe Marry Majaliwa wakati wakiwasili Msasani kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar 
Rais Mstaafu awamu ya nne,Mh Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Mh Pinda,kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar 
Mawaziri Wakuu wa zamani Mh Edward Lowassa na Mizengo Pinda wakisalimiana msibani.
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mh Bernad Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu kiongozi Mstaafu,Ombeni Sefue kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar
Mama Maria Nyerere akiwa Wasaidizi wake wakiwasili kwenye kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar
Waziri Mkuu wa Zamani,Mh Edward Lowassa akizungumza jambo na Katibu Mkuu kiongozi Mstaafu,Ombeni Sefue kwenye msiba wa Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018,ambapo maziko ya marehemu yanafanyika leo katika Makaburi ya Kisutu,jijini Dar.

BREAKING NEWS: MSANII WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam leo imemtia hatiani na kumhukumu msanii Wema Sepetu kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Shilingi milioni mbili baada ya kupatikana na hatia  katika kesi ya kukutwa na  kutumia dawa za kulevya. 

Wema amelipa faini na kuachiwa huru. 

Mahakama imewaachia huru wafanyakazi wake Wema, Matrida Abbas na Angelina Msigwa,  aliokuwa akishtakiwa nacho baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Akisoma hukumu hiyo leo Hakimu Mkuu  Simba amesema, upande wa Mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa, mshtakiwa Wema alitenda kosa la kutumia na kukutwa na dawa za kulevya. 

Kabla ya kusomwa kwa Hukumu hiyo leo Julai 20 mwaka 2018, mashahidi upande wa mashtaka kupitia Wakili wake, Constantine Kakula waliwasilisha mashahidi 5 ambao wameweza kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa Wema ametenda kosa.

Upande wa washtakiwa walitoa utetezi wao wakiongozwa na Wakili Albert Msando  na walipomaliza walifunga ushahidi wao na kufunga kesi yao. Pande zote ziliwasilisha hoja za majumuisho za mwisho na hatimaye kesi ikapangiwa tarehe ya hukumu, huku watuhumiwa wakijitetea wenyewe.
Wema na wafanyakazi wake hao walikuwa wakishtakiwa na kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha madawa ya kulevya chini ya kifungu cha sheria namba 17 (1)(b) cha sheria inayodhibiti matumizi ya dawa za kulevya.

Walidaiwa kutenda kosa hilo Tarehe 4 February mwaka jana huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio
 Pichani kulia Wema Sepetu akiwa na Mama yake wakiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya 
 Wema Sepetu akiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.Wema Sepetu aliambatana na Mama yake pamoja na Ndugu,jamaa na marafiki zake.
Wema Sepetu akiwa na mama yake, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu 

SSRA YAHIMIZA VIJANA KUJENGA DESTURI YA KUJIWEKEA AKIBA

$
0
0
“Kesho ya Mtu hujengwa leo na Tofali la kujengea kesho hufyatuliwa leo” hii ni kauli ya Sarah Kibonde Msika, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii – SSRA akizungumza na vijana waliotembelea banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya 13 ya Elimu ya Juu na Taasisi za Kitafiti na wadau wa elimu ya juu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Akifanunua kauli hiyo, Mkuu huyo wa Kitengo kutoka SSRA anasema, Taifa linakabiliwa na kiwango kikubwa cha umaskini wa kipato hasa kwa baadhi ya makundi kama ya wazee, jambo linalotokana na watu wengi kutokuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba na maandalizi ya kufikia uzee, hivyo kuwahimiza vijana wenye nafasi ya kurekebisha hali hiyo kuanza maandalizi mapema kwa kujiwekea akiba kwa njia mbalimbali ikiwemo Mifumo ya Hifadhi ya Jamii .

Kwa kutambua changamoto hiyo ya umaskini wa kipato hasa wakati wa uzee, SSRA inajukumu la kuhakikisha watanzania wanapata kinga kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya majanga ya kiuchumi na kijamii. Mpaka sasa imefanya juhudi ya kuanzisha mipango ya kupambana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo utakaoruhusu kila kundi katika jamii kufaidika na huduma za Hifadhi ya Jamii. Miongoni mwa mipango hiyo ni pamoja na mfumo wa hiari/ziada (Supplementary Schemes), wenye lengo la kukabiliana na mahitaji mahususi ya nguvukazi katika sekta isiyo rasmi ambayo kwa hakika inajumuisha sehemu kubwa zaidi ya nguvukazi nchini, anasema Sarah Kibonde.

Akifafanua kuhusu Mpango huo, Sarah anasema chini ya usimamizi wa SSRA, nguvukazi kutoka katika wa sekta isiyo rasmi na hata wanafunzi wa vyuo vikuu sasa ina fursa ya kuchagua na kuchangia kiasi chochote wanachomudu kila mwezi au kila mara kadiri watakavyoweza. Katika mfumo huo inahimizwa zaidi kuwa fao litakalopatikana litategemea kiasi cha michango kitakachotolewa.

Kiasi cha michango kinavyokuwa kikubwa zaidi ndivyo fao linavyokuwa kubwa zaidi. Kuhusu utaratibu na namna ya kujiunga na mfumo huu wa hiari, Sarah anawashauri vijana kutembelea katika ofisi za Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii.

Hivyo basi, SSRA inatumia maonesho haya ya Elimu ya Juu kuelimisha Umma juu ya masuala ya Hifadhi ya Jamii hususani kukutana na vijana waliopo vyuoni na wanaotarajiwa kuingia vyuoni, lengo likiwa ni kuwaelimisha na kuwaimiza kuweka akiba jambo litakalowajengea tabia ya kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadae na kuwaepusha na changamoto ya umaskini wa kipato wakati wa uzee. “Majuto ya kesho huandaliwa leo” anasisitiza Bibi. Sarah Kibonde
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika akifafanua jambo wakati kwa wadau waliotembelea banda la SSRA wakati wa Maonyesho ya Taasisi za Elimu ya Juu yanaendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa Matekelezo wa SSRA, David Lyanga akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA lililoko kwenye Maonyesho ya Taasisi za Elimu ya Juu yanaendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye banda la SSRA wakati wa Maonyesho ya Taasisi za Elimu ya Juu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijni Dar es Salaam.

Wabunge wa Kigoma wakutanishwa mradi wa pamoja na UN

$
0
0
Na Mwandishi wetu
WABUNGE wa mkoa wa Kigoma walipata nafasi ya kutaarifiwa mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa ambao umejikita katika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Maendeleo na pia kutekeleza shughuli mbali mbali zinazolenga kufikia malengo endelevu ya dunia.
Akifungua mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliwataka washiriki wa mkutano huo kufuatilia kwa makini hatua iliyofikiwa ya mradi huo na kutoa mapendekezo yao.
Baadhi ya shughuli za mradi huo zimeanza kutekelezwa hususan katika maeneo ya Kilimo, uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi, kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na kina mama pamoja na elimu.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waheshimiwa wabunge kutumia fursa waliyoipata kupokea taarifa kuhusu mradi na kutoa ushauri wa namna ya kufanikisha malengo yaliyowekwa ili kuwaletea maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma.
“Mkoa wa Kigoma ni Mkubwa na tunatamani kuona mradi huu unapanuka kujumuisha wilaya zote na pia sekta nyingine muhimu kama afya. “ alisema Maganga ambaye alisema kama serikali wako tayari kushirikiana na wadau wote wenye mapenzi na mkoa wa Kigoma wataliona hilo.
Katika mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez na wadau  wengine wa maendeleo, misingi imara ya ushirikiano kwa ufanikishaji wa maendeleo ya mkoa wa Kigoma kwa ujumla yalizungumzwa na kuafikiwa.  

 Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga (kulia) akifungua mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma juu ya mradi wa pamoja na Umoja wa Mataifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho kutoka Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma juu ya mradi wa pamoja mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa (UN-KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo na kushoto ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha.
 Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini-CCM,  Daniel Nsanzugwanko akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa mkoa wa Kigoma wakati mkutano ulioandaliwa kwa Wabunge hao juu ya mradi wa pamoja na Umoja wa Mataifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha (kulia) akiwasilisha muhtasari wa mradi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma wakati wa mkutano maalum ulioandaliwa juu ya mradi huo wa pamoja uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akifafanua jambo wakati wa majadiliano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Faith Shayo (kulia) akielezea kuhusu mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UN Women pamoja na UNFPA unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA) katika eneo la elimu wakati wa mkutano juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano maalum na Wabunge wa mkoa huo ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.
 Picha ya pamoja ya Waheshimiwa Wabunge wa mkoa wa Kigoma na Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kumalizika kwa mkutano maalum juu ya mradi wa pamoja wa Kigoma na Umoja wa Mataifa na Wabunge hao ulioandaliwa na UN na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wadau wa Sekta ya Filamu Mkoa wa Songwe waipongeza Serikali

$
0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM- Vwawa, Mbozi
Wadau wa Sekta ya Filamu Mkoa wa Songwe waishukuru serikali kupitia Bodi ya Filamu Tanzania kwa kuwapatia fursa ya mafunzo ya kujenga uwezo katika uandaaji wa kazi za filamu kwa lengo la kuboresha kazi za filamu zinazoandaliwa nchini.
Shukrani hizo zimetolewa leo Mjini Vwawa, Wilayani Mbozi na Katibu Mkuu wa Chama cha Wanatasnia wa Filamu Mkoa wa Songwe Bw.Tegemea Hasunga mara baada ya kuwasilishwa mada mbalimbali ikiwemo mada ya uandishi wa Miswada ya filamu na Utafiti ambazo zinawajengea uwezo wa kujua namna ya kuaanda miswada hiyo ambayo ndiyo roho ya kazi za filamu. 
“Kiukweli kabisa nimejifunza mengi sana kupitia warsha hii ya siku mbili kwanza nimepata kuelewa kuwa katika uandaaji wa kazi za filamu ni lazima kufanya utafiti wa kile unachotaka kuigiza na pili ni lazma kuandaa mswada kwani mswada ndiyo utakaonipa mwelekeo mzima wa filamu nitakayoandaa na pia miswada hii inatakiwa kuandaliwa katika mifumo ya kitekinolojia ambayo ipo mitandao ambapo hapo mwanzo sikuwa nafahamu haya,”alisema Bw.Hasunga.
Akiendelea kuzungumza kuhusu warsha hiyo Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa mafunzo haya yamemsaidia sana pia kufahamu namna ya kuboresha kazi zake na kulijua soko lake kulingana na utafiti aliyofanya na kile atakachotaka kuigiza.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alitoa pongezi kwa wadau wa filamu mkoa huo wa Songwe kwa kutoa ushirikiano katika mafunzo hayo na kutoa ahadi ya ofisi yake kuandaa mafunzo ya siku tano kwa halmashauri ya Tunduma kutokana na kuonekana kuwa na wadau wengi ambao wanajihusisha na uandaaji wa kazi za filamu.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiwaahidi wadau wa sekta ya filamu Halmashauri ya Tunduma (hawapo pichani) kuhusu kupokea maombi yao na kuwaahidi kuaanda mafunzo ya siku tano yatakayohusu uandaaji wa miswada na elimu juu ya upigaji picha wa filamu alipokuwa akizungumza katika warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa filamu Mkoa wa Songwe iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania yaliyofanyika leo Mjini Vwawa Wilayani Mbozi.
 Mmoja wa wezeshaji Bibi.Christa Komba akiwasilisha mada ya uhusiano kati ya mwigizaji na mwongozaji kwa kuwataka wadau wa filamu kuchagua wahusika wenye vigezo vya kuvaa uhusika badala ya kuangalia sura katika warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa filamu Songwe yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika leo Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi.
 Kamada wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe Bw.Damas Sutta (kulia) akizungumza na wadau wa sekta ta filamu mkoa huo (hawapo pichani) walipokuwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania yaliyofanyika leo Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Wadau wa sekta na filamu Mkoa wa Songwe wakimsikiliza kwa makini mtoa Mada ya elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka kwa Afisa wa TAKUKURU Bw.Audronicus Kivyiro katika warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau hao yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania na kufanyika leo Mjini Vwawa,Wilayani Mbozi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu jamii
CHUO cha Ustawi wa Jamii kilichopo Kijitonyama jijini Dar es salaam kimeanza kudahili wanafunzi kwa mwaka 2018/2019  katika maonesho al maarufu kama maonesho ya TCU yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Akizungumza na Michuzi blog Msajili wa Chuo hicho Nuru Kalufya ameeleza kuwa katika kupokea wanafunzi katika msimu huu na wanasajili kupitia mtandao (online) bure na kinachohitajika ni wanafunzi kuwa na vyeti vyao na namba zao za usajili (index number) na watapata huduma hiyo ya udahili na ushauri wa kitaaluma bure kabisa.

Kuhusu kozi zinazotolewa na Chuo hicho bi. Nuru ameeleza kuwa wanatoa kozi tano kwa gharama nafuu kabisa na hii ni kuanzaia ngazi ya cheti, stashahada, shahada, uzamili na post graduate ya kozi ya Health System Management ambayo ni mpya kabisa chuoni hapo.

Akizungumzia kuhusiana na usajili wa Chuo Nuru amesema kuwa wamesajili na wanatambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) pamoja na NACTE na Serikali kwa ujumla.Hivyo wazazi na  wadahiliwa wasiwe na hofu.

Aidha ameeleza kuwa watatoa huduma katika maonesho hayo hadi kesho majira na saa kumi na moja jioni na baadaye wataendelea kutoa huduma hizo katika chuo chao kinachopatika Kijitonyama hivyo wanafunzi waendelee kujitokeza kwa wingi zaidi.

Kwa upande wake Mshauri wa wanafunzi bi. Silvia Ngiga amewahakikishia wanafunzi usalama pindi wawapo shuleni na wanafunzi watokao mikoani watapata za malazi  na huduma nyingine za kijamii ni za kuaminika katika chuo hicho.
Msajili wa Chuo cha ustawi wa jamii Nuru Kalufya akizungumza na blogu ya jamii kuhusu mikakati walioweka katika kudahili wanafunzi wapya 2018/2019
 Mshauri wa wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa jamii Silvia Ngiga akizungumza na Michuzi blog kuhusiana na maonesho katika maonesho  ya TCU yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Introducing "Amen" Official Music Video by Maua X Ben Pol

MICHUZI TV: WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA DARAJA LA NYERERE

MICHUZI TV: VIONGOZI MBALIMBALI WASHIRIKI MAZISHI YA MKWE WA JK


ZIARA YA BABA WA TAIFA IKULU YA MAREKANI MWAKA 1963

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Kangi Lugola akisalimiana na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa pamoja na Maofisa wengine alipokuwa akiwasili Makao Mkauu ya Polisi kwa ajili ya kuzungumza na Maofisa Wakuu wa Polisi jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Kangi Lugola  akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa kikao chake na Maofisa Wakuu wa Polisi kilichofanyika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Kangi Lugola  akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa kikao chake na Maofisa Wakuu wa Polisi kilichofanyika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Picha na Jeshi la Polisi

TEAM MAPICHA: FUTURE WIFE

MAGEREZA NA JKT KUSHIRIKIANA KATIKA MIRADI YA UZALISHAJI MALI

$
0
0
Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa wameahidi kushirikiana katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kupitia mashirika yake ya Magereza Corporation Sole na SUMA-JKT.
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike  alipomtembelea Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Matin Busungu ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake  za kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa tangu ateulie kuwa mkuu wa Jeshi hilo Julai13, 2018.
Katika mazungumzo yao, wakuu hao wa taasisi hizo muhimu nchini wameonesha utayari wa ushirikiano katika miradi ya ujenzi pale taasisi moja inapokuwa na miradi mikubwa inayoweza kuhitaji utaalam au nguvu ya kuweza kushirikiana.
Aidha, Meja Jenerali Busungu amesema kuwa JKT  lipo tayari kulikopesha matrekta Jeshi la Magereza wakati litakapokuwa limekamilisha  mpango wake kilimo cha kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa kama ilivyoelekezwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
“Namshukuru sana  Meja Jenerali Busungu kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na Jeshi la Magereza, kilichobaki ni kujipanga na kuanza utekelezaji mara moja”. Amesema Jenerali Kasike.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akifuatilia kwa makini mazungumzo kati yake na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali, Martin Busungu(kulia) alipomtembelea Ofisini kwake leo Julai 20, 2018 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha rasmi tangu aapishwe rasmi kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa – JKT, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali, Martin Busungu.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa – JKT, Meja Jenerali, Martin Busungu mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake leo Julai 20, 2018 jijini Dar es Salaam(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza).

WACHEZAJI WA TIMU YA SIMBA WAFANYA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)

$
0
0
 Na Brighton James
Vilabu vya mpira hapa nchini vimeshauriwa kupima afya za  wachezaji wao kabla ya kuanza kwa mashindano ili kama watakutwa na matatizo waweze kupata matibabu mapema.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na wachezaji wa Klabu ya Simba waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Prof. Janabi alisema faida ya kufanya uchunguzi wa afya kutamsaidia  mchezaji kama atagundulika kuwa na matatizo ya moyo atapata matibabu mapema na kuepukana na kifo cha ghafla anachoweza kukipata awapo uwanjani.
“Vifo vya wachezaji vinavyotokea ghafla wanapokuwa uwanjani vinaweza kuzuilika iwapi wangefanya uchunguzi wa afya zao mapema. Nazishauri timu zinazocheza ligi kuu pamoja na mashindano ya kitaifa na kimataifa wajitahidi kupima afya za wachezaji wao ikiwemo uchunguzi wa magonjwa ya moyo”, alisisitiza Prof. Janabi.
Kwa upande wake Abasi Ally ambaye ni Mkuu wa msafara kutoka klabu ya Simba alisema wameamua kuwafanyia wachezaji wao uchunguzi wa magonjwa ya moyo  kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania inayotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi ujao.
Ally alisema kwamba kuwapima afya wachezaji hao kutawasaidia kujuwa afya zao ili kama mchezaji atakutwa na matatizo aweze kupata matibabu mapema na kushiriki mashindano akiwa na afya njema.
Jumla ya wachezaji 27 wa klabu hiyo wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa kuangaliwa jinsi mioyo yao inavyofanya kazi (ECHO), umeme wa  moyo (ECG) na  umeme wa moyo wakati mtu anafanya mazoezi (Stress ECG)
 Mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abuu Dalidali akimpima urefu Mchezaji  wa Klabu ya Simba Yussuf Mlipili wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo. 

 Muhudumu wa Afya wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Seleman Charles akimpima urefu Shiza Ramadhani Kichuya ambaye ni Mchezaji  wa Klabu ya Simba wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisimamia  upimaji wa magonjwa ya moyo ulivyokuwa unafanyanyika kwa wachezaji wa klabu ya Simba wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Picha na JKCI

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images