Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

CCM YAPITA BILA KUPINGWA UCHAGUZI MDOGO KATA YA KIMARA


KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI, KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR WALA KIAPO CHA UADILIFU

$
0
0
 Katibu Mkuu Wazira ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akisalimiana na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dr. Eliezer Feleshi, wakati alipoenda kuapishwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi Jeshi la Polisi, Magereza pamoja na Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu WazirI ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akila kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dk. Eliezer Feleshi kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Magereza, pamoja na Uhamiaji. Kiapo hicho kilifanyika katika ofisi za Mahaka Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wazira ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akisaini karatasi la kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Magereza, pamoja na Uhamiaji, pembeni ni Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliyesimamia kiapo hicho katika Ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohamed Haji Hassan akila kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dr. Eliezer Feleshi kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Mageereza, pamoja na Uhamiaji. Kiapo hicho kilifanyika katika ofisi za Mahaka Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam alipofika ofisini hapo kwaajili ya kula kiapo cha uadilifu kama mjumbe wa tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji. Wa kwanza (kulia) ni  Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania akifuatiwa na Mohamed Haji Hassan, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akifafanua jambo kwa Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakati alipoenda kula kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji, katikati ni Mohamed Haji Hassan Kamishna wa jeshi la Polisi Zanzibar. (Picha na Mambo ya Ndani)

H-TOWN OLD SCHOOL REUNION 2019, HOUSTON, TEXAS KUWAKA MOTO

$
0
0
Image result for old school reunion
H-Town Old School Reunion 2019 kufanyika March 22 na 23  mjini Houston, Texas, unaambiwa kaa mkao wa kula maana pia kutakuwa na Bonanza la mpira wa kikapu la Pazi vs Vijana 'City Bulls'  pamoja na soka la Simba na Yanga inayosubiliwa kwa hamu Houston na vitongoji vyake.
 Timu ya Yanga
Timu ya Simba
Image result for OLD SCHOOL OHIO VIJIMAMBO
Timu ya mpira wa kikapu

MISS TANZANIA USA PAGEANT KUFANYIKA AGOSTI 11, 2018 SILVER SPING MD

MAMA WA MITINDO ASYA IDAROUS-KHAMSIN AWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAONESHO YA VIVAZI NORFORK, VIRGINIA, MAREKANI

$
0
0
Mama wa mitindo Asya Idarous akiwa mwakilishi pekee wa Tanzania kwenye maonyesho ya mavazi yaliyofanyika Jumamosi Julai 14, 2018 huko Norfork,  Virginia, nchini Marekani
Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini katika picha
Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini akiwa katika picha ya pamoja na wan mitindo wengine walionogesha  tamasha hilo

FAHAMU KUHUSU HIFADHI YA MSITU WA ASILI,AMANI.

WELCOME TO THE TANZANIA PHOTOGRAPHERS GROUP

$
0
0
TANZANIA PHOTOGRAPHERS
Facebook Group · 10 members
Join Group
This page is for Tanzanian photographers all over the globe to share experiences, news, views, create unity, share expertise and have fun with the cam...

RC Iringa awaomba wadau wa utalii kuwekeza Nyanda za juu Kusini

$
0
0

MKUU wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza ametoa wito kwa wadau wa utalii na maendeleo nchini kuwekeza zaidi kwenye sekta ya Utalii katika Ukanda wa Nyanda za juu Kusini ili kuunga mkono adhma ya serikali ya kufungua na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.

Bi. Masenza ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayoenda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu.

Alisema kwa sasa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imejipanga kimkakati kuhakikisha kwamba inatangaza na fursa na vivutio vya kiutalii vinavyopatikana katika mikoa hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli alilolitoa hivi karibuni wakati wa kilele cha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Iringa ambapo aliitaka mikoa hiyo kufunguka kiutalii.

Mikoa inayounda kanda hiyo ni pamoja na Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Ruvuma, Rukwa na Katavi. 
“Mikoa ya nyanda za juu Kusini inasifika kuwa na hifadhi zenye sifa za kipekee ikiwemo Taifa ya Ruaha yenye makundi makubwa ya tembo na wanyama wengine. Hifadhi nyingine ni Kitulo yenye aina mbali mbali za maua ambayo hayapatikani mahali pengine Duniani; na Udzungwa yenye wanyama adimu duniani kama vyura wa Kihansi na mengine mengi,’’ alitaja. 

Akizungumzia maonesho hayo Bi Masenza alisema tofauti na miaka miwili iliyopita maonesho ya mwaka huu yataambatana na nyongeza ya matukio kadhaa ya kimichezo, kitaaluma na kiutamaduni ili kuongeza tija zaidi katika kufikia malengo ambayo hasa ni kuongeza mazao ya utalii katika kanda hiyo. 
MKUU wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa Septemba 26 hadi 30 mwaka huu. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Iringa Bw. Robert Masunya. Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela (kushoto) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ernest Mwamwaja (kulia) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Maonesho ya Utalii Karibu Kusini 2018 kutoka Kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI) Bw Clement Mshana (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo. Kampuni hiyo inashirikiana na Mkoa wa Iringa kuratibu maonesho hayo.


UVCCM MKURANGA WAJADILI NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO, KUCHANGAMKIA FURSA

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii 

BARAZA kuu la Umoja wa Vijana kupitia Chama Cha CCM(UVCCM)Wilaya ya Mkuranga limefanya kikao kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili vijana.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Baraza Kuu la umoja wa vijana Wilaya ya Mkuranga Mbwera amesema vijana wanachangamoto nyingi lakini CCM kina mikakati mbalimbali ya kuzitatua. 

Amefafanua tayariasa Mbunge wao amewatafutia fursa ya kutoa mikopo kwa ajili ya vijana .Pia amesema Mwenyekiti wa wauza ya pikipiki nchini tayari amezungumza na vijana kujitokeza kukopeshwa kuanzia bodaboda 50 ikiwa ni fursa ambayo imetafutwa na Mbunge wa jimbo la Mkuranga na kuhaidi kuwa vijana hawatomuangusha na marejesho yatarejeshwa kwa wakati.

Amefafanua kwa vijana ambao hawakufika katika mkutano huo wafahamu kuwa maendeleo yataletwa na CCM. Hivyo wajitokeze kwenye mikutano hiyo kwani ndio fursa peke yakujua matatizo ya jimbo hilo .Kwa upande wa Mjumbe wa Baraza Kuu la umoja huo Taifa Mkoa Ramadhani Mwishehe amewaomba wana CCM na wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli za kuleta maendeleo.

Mwishehe amesema kuwa "vijana kimsingi tuige na kumuunga mkono kwani dhamira yake ni njema katika kutukomboa na kuleta maendeleo katika nchi yetu kwani kwa hali ya sasa ni tofauti na hapo wali."Ameongeza kuwa Sera ya kwanza ambayo alihimiza Rais pindi atakapoingia madarakani ni pamoja na elimu bure ambayo sasa itatolewa bure.

Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao akizungumza na vijana mara baada ya kufungua kutano wa Baraza kuu uliofanyika wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.

Mwenyekiti wa Baradha kuu la umoja wa UVCCM wilaya Mkuranga,Ally Mohammed Mbwera akifafanua juu ya mikakati ya chama hicha kwa upende wavija Katika mkutano uliofanyika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Mkutano wa Baraza kuu la umoja wa UVCCM wilaya Mkuranga ukiendelea.

DED UBUNGO AFANYA UKAGUZI KATIKA UJENZI WA MADARASA MANNE YA KIMARA SEKONDARI

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akizungumza jambo na kaimu Mwamlimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimara wakati alipofika kukagua ujenzi wa Madarasa Manne yanayojengwa katika Sekondari hiyo Mpya, leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo, akikagua ubora wa Zege linalotumika katika ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari Kimara.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akisaidiwa kupanda  juu ya Msingi na Afisa Mtendaji wa kata Kimara.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akitoa maelekezo kwa mkandarasi aweze kumaliza ujezni huo kwa wakati.

TAGLA, ICDL KUNUFAISHA WANANCHI KIUCHUMI KUPITIA TEKNOLOJIA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAKALA wa mafunzo kwa Njia ya mtandao nchini (TaGLA) kwa kushirikiana na Wakala wa masuala ya teknolojia Afrika (ICDL) wamekutana na kujadili namna wanavyofanya kazi na changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kazi sambamba na kuzitafutia suluhisho.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa ICDL Afrika Etinick Mutinda ameeleza kuwa nchi 17 ni mwananchama wa ICDL ambapo makao makuu yapo Kigali nchini Rwanda na bado wanashawishi nchi nyingine kujiunga kwa maendeleo zaidi.

Ameeleza kuwa lengo la ICDL ni kusaidia na kushirikiana na Serikali katika masuala ya kiteknolojia na namna ya kutumia teknolojia kwa manufaa ya kujenga taifa na wanashirikiana na Serikali pamoja na taasisi binafsi katika kuhakikisha teknolojia inasaidia katika kukuza uchumi na katika mkutano huo wataangalia changamoto na namna ya kuzikabili katika masuala ya tehama.

Akiiwakilisha wakala ya mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) meneja habari na mafunzo Dickson Manyika ameeleza kuwa malengo ya teknolojia hasa matumizi ya kompyuta na mitandao yawe ya manufaa katika kushirikishana mawazo ambayo yataleta mabadiliko na maendeleo katika jamii.

Ameeleza kama wakala wana vipindi maalumu wanavyofanya kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na nchi mbalimbali na hujadili masuala ya kusaidia serikali na jamii kwa ujumla kama vile kukua na upangaji wa miji na masuala ya kielimu.

Baadhi ya washiriki wameeleza kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda hatuwezi kubaki nyuma katika suala la teknolojia kwani njanja nyingi kama kilimo, elimu na viwanda huhitaji matumizi ya teknolojia bora katika kufikia malengo.
 Meneja habari na mafunzo wa Wakala wa mafunzo kwa njia ya Mtandao,Dickson Manyika akizungumza na Globu ya jamii kuhusu matumizi ya mitandao iwe ya manufaa katika kushirikisha mambo mbalimbali ya maendeleo katika jamii.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ICDL Afrika,Etinick Mutinda akizungumza na wadau mbalimbali wa mitandao katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Semu ya wadau mbalimbali wa mitandao wakiwa katika mkutano huo.

NEWS ALERT: Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma aanza matibabu nchini India

$
0
0
Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma, ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili,  leo amenza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India.

Kwa mujibu wa binti yake, Bi. Asha Ngoma, mgunduzi huyo ameamua kusaka matibabu zaidi  baada ya kufanyiwa matibabu ili kuona kama anaweza kupona kwa uharaka zaidi.
“Mzee amekuwa akipatiwa matibabu tokea wakati ule Rais Magufuli  alipomzawadia pesa shilingi milioni 100 mwezi wa Aprili mwaka huu  ya matibabu wakati  uzinduzi wa ukuta unaozunguka machimbo ya madini Mirerani mwezi April mwaka huu.
“Tunamshukur sana Rais Magufuli kwani pesa hiyo tulipewa mara moja nasi tukaanza matibabu hapo nyumbani  na kwa kweli amemsaidia sana sana  na hapa India tunatarajia matibabu yatamsaidia zaidi”, alisema Bi. Asha ambaye ameongozana  na mjukuu wa Mzee Ngoma, Khalifa. 
 Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akipokewa na muuguzi leo tayari kupelekwa kuanza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. Pamoja naye ni bintiye, Asha Ngoma na mjukukuu, Khalifa
 Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akiwa kwa daktari baada ya kupokelewa katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. Pamoja naye ni bintiye, Asha Ngoma na mjukukuu, Khalifa
 Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma akiingizwa wodini tayari kuanza matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. 
Daktari wa zamu akimpima Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma mara tu baada ya kufikishwa wodini katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India. 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WAGONJWA 300 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA MACHO WILAYANI MUHEZA

$
0
0
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo waliofanyiwa uchunguzi wa  matatizo ya macho  wakati wa zoezi la kufunga kambi ya matibabu ya tiba ya macho iliyoendeshwa na Taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Medewell Health Centre kwenye kituo cha Afya cha Ubwari wilayani Muheza
 Mkurugenzi wa wa taasisi ya Medewell Munir Meral akizungumza katika ufungaji wa kambi hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
 Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga waliopatiwa matibabu ya macho. 

VYA NYUMBANI VIMEIVA, VINALIWA LEO, JE, UPO TAYARI?


MOJASPESHO YATOA MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 204

$
0
0
  Mchezo wa bahati nasibu wa Mojaspesho umetoa kwa mara ya kwanza mshindi wa kiasi kikubwa cha pesa cha shilingi Milioni 204 kwa ROSEMARY ONESMO LUHAMO, mfanyabiashara kutoka MPWAPWA DODOMA mwenye umri wa miaka 26.

Akuzungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi pesa kwa mshindi, Meneja biashara wa kampuni ya Lucy Games Patrick Salamouni ambayo ndio inajechezesha mchezo wa Mojaspesho alisema kuwa ushindi wa Rosemary umekuja baada ya kucheza Mojaspesho zaidi ya mara nyingi sana bila kukata tamaa, na hatimaye kulinganisha namba zake za tatu spesho ambazo zilikuwa 873 siku ya Jackpot ya Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Julai 2018.

Huu ni mchezo wa bahati nasibu. Unaweza ukacheza mara moja ukashinda lakini pia unaweza isishinde. Ninachoweza kuwaambia ni kuwa kila mtu anayecheza anayo nafasi ya kuwa mshindi. Naomba Watanzania kuwa huu ni mchezo halali na kila anayeshinda anapata zawadi yake, alisema Salamouni. Salamouni aliongeza kuwa huu ni ushindi mkubwa kuwahi kutokea tangu Moja Spesho ianze kuchezesha Droo zake na ni uthibitisho kuwa kila mtu anaweza kushinda Mojaspesho.

‘Unaweza kucheza MOJASPESHO kupitia simu yako ya mkononi kwa kuingia sehemu ya KULIPIA BILI kwa watumiaji wa AIRTEL MONEY, TIGO PESA, MPESA au HALOPESA, kisha ingiza NAMBA YA KAMPUNI/BIASHARA ya MOJASPESHO ambayo ni 123255 - kisha INGIZA NAMBA ZAKO 3 SPESHO ZA USHINDI’ aliongeza Salamouni.

Mshindi RoseMary Onesmo Luhamo (katikati) akikabidhiwa zawadi ya ushindi wake wa milioni 204 kutoka kwa Meneja wa Lucky Games Ltd, Patrick Salamouni, ambayo ni kampuni inayochezesha mchezo wa MojaSpesho pamoja. Kushoto ni Meneja wa tawi la benki ya CRDB Azikiwe Premier Fabiola Msula.
Mshindi RoseMary Onesmo Luhamo wa kwanza wa droo ya milioni 204 ya MOJASPESHO, akifurahi baada ya kukabidhiwa pesa za ushindi wake leo jijini Dar es Salaam. Kwa kucheza mchezo wa MOJASPESHO kupitia simu yako ya mkononi nenda sehemu ya KULIPIA BILI kwa watumiaji wa AIRTEL MONEY, TIGO PESA, MPESA au HALOPESA, kisha ingiza NAMBA YA KAMPUNI/BIASHARA ya MOJASPESHO ambayo ni 123255 - kisha INGIZA NAMBA ZAKO 3 SPESHO ZA USHINDI’

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CBE KUUNGURUMA KWENYE MAONESHO YA VYUO VIKUU KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUANZIA JUMATANO TAREHE 18 - 21/07/2018.

$
0
0
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kama mdau wa muhimu wa TCU kitashiriki katika maonesho hayo muhimu.  Pamoja na kutoa maelezo sahihi ya shughuli na huduma zinazotolewa CBE. Chuo kitapokea maombi ya kujiunga  katika ngazi za Masters, Bachelor Degree, Postgraduate Diploma  na Certificate.
1: MASTERS
a) Masters in IT Project Management 
b) Masters in ICT for Development 
C) Masters in Supply chain Management 
d) Masters in International Business Management 
2: BACHELOR,  DIPLOMA &  CERTIFICATE IN:-
a) Accountancy 
b) Business Administration 
C) Marketing 
d) Procurement and Supplies Management 
e) Information and Communication Technology 
f) Metrology and Standardization 
3: Bachelor of Business Studies with Education (BBSE)
4: Fika na vivuli vya vyeti vyako pamoja na Tshs 10,000/= gharama ya maombi. Mweye sifa atapewa Joining instruction . 
Pia, maombi ya kujiunga yanapokelewa katika Kampasi zetu za DSM, DODOMA, MWANZA  na MBEYA. Vilevile unaweza kuomba kupitia tovuti ya Chuo www.cbe.ac.tz 
Karibuni Ada zetu ni nafuu na zinalipwa kidogo kidogo.
KWA MAELEZO ZAIDI
TUPIGIE 0756 722 467
"ELIMU YA BIASHARA KWA MAENDELEO YA VIWANDA TANZANIA"
KARIBUNI SANA
Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano na Masoko
CBE

WAKAZI DODOMA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI BONANZA LA MICHEZO

WAZIRI MHAGAMA ATENGUA UTEUZI WA KAIMU MTENDAJI MKUU WA TaESA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Muhagama akisilikiliza hoja za baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Ajira (TaESA) wakati wa mkutano na wafanyakazi hao jinjini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wakala wa Huduma za Ajira (TaESA) wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Muhagama wakati wa mkutano na wafanyakazi hao jinjini Dar es Salaam.

Tanzania yafurahishwa na UN katika kutekeleza mradi wa KJP

$
0
0
MKUU wa mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga  amesema serikali ya Tanzania inafurahishwa na namna Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyofanya kila linalowezekana kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wa mkoa wa Kigoma ambao ndio wenyeji wa wenzao wanaokimbia matatizo nchi jirani.
Akizungumza katika mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP), alisema kazi kubwa inayofanywa na mashirika hayo ikiwamo ya kupeleka ushawishi kwa wadau wa maendeleo ya kusaidia wananchi wa Kigoma wakiwemo wageni wakazi na wakimbizi.
Akiwa Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo, Maganga alisema pamoja na juhudi hizo bado mkoa una changamoto nyingi zinazotakiwa kushughulikiwa japo serikali imeendelea na juhudi za kuboresha mazingira ya miundombinu ya kuwezesha shughuli za kiuchumi.
Alisema toka mkutano wa mwisho mwaka jana, kumekuwa na maendeleo makubwa katika kampeni za serikali za kuufungua mkoa huo kiuchumi kwa kutengeneza miundombinu mbalimbali kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara.
Alisema serikali inaendeleza miradi ya kimkakati hasa ya barabara zinazounga mkoa huo na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC)  na mikoa mingine ya Tanzania ya Shinyanga, Mwanza, Kagera na Tabora.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (wa pili kulia)akizungumza wakati akifungua mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford (kushoto).
 Kansela wa Ubalozi wa Norway, Britt Kjolas akitoa salamu kwa niaba ya wadau wa maendeleo wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Kigoma, Evance Siangicha akiwasilisha rasimu ya makubaliano ya utekelezaji wa Programu ya KJP wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mchambuzi  Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN Coordination Analyst )nchini, Kanali Rankho
 Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) nchini, Stephanie Shanler akiwasilisha hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi wa KJP eneo la kuzuia ukatili kwa wanawake na watoto wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Viola Kuhaisa akiwasilisha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa eneo la elimu wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) wakiwemo wadau wa maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images