Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

WADAU VYAMA VYA SIASA WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MATAKWA YA SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI

$
0
0

Wakati tukielekea kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kata 77 utakaofanyika tarehe 12 Agosti, 2018, nachukue fursa hii kuwakumbusha wadau wote hususani vyama vya siasa, wagombea na Asasi za kiraia kuzingatia matakwa ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa.

Sheria ya Gharama za uchaguzi inamtaka kila Mgombea wa Ubunge na Udiwani kuweka wazi mapato na matumizi ya gharama anazotarajia kuzitumia wakati wa uchaguzi husika kwa kujaza fomu maalumu ( EE1 & EE2) ambazo hujazwa na kuwasilishwa kwenye mamlaka husika ndani ya siku saba, kuanzia siku ya uteuzi wa wagombea. Hivyo ninasisitiza ujazaji sahihi wa fomu hizo maalumu ili kukidhi matakwa ya Sheria.

Pia, ninawakumbusha wagombea, vyama vya siasa na umma kwa ujumla kuepuka kufanya vitendo vinavyokatazwa na Sheria za nchi hususani Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na wa haki na pia unaendeshwa katika hali ya Amani na utulivu.
Nichukue nafasi hii pia kuwatakia Wadau wote maandalizi na uchaguzi Mwema.

Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.



ACACIA WATOA MSAADA WA SHILINGI MIL NANE KWA ATFGM MASANGA TARIME

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime
KAMPUNI ya uchimbaji wa mawe yenye dhahabu ya Acacia North Mara wametoa msaada wenye thamani zaidi ya Sh.milioni nane katika Kituo cha kuifadhi wahanga wa ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji cha ATFGM Masanga wilayani Tarime mkoani Mara.

Akisoma risala Meneja Miradi Shirika la Associatio for the Termination of Female Genital Mutilation ATFGM Masanga Valerian Mgani ametoa shukrani kwa niaba ya shirika hilo na kufafanua vifaa vilivyotolewa vina thamani ya Sh. 8,823,000 kwa lengo la kusaidia mabiti ambao watapokelewa kipindi cha Kambi Desemba mwaka huu.

"Kwani huenda ukeketeaji ukawepo licha ya wazee wa vila kupiga vita,"amefafanua.Pia mbali na watoto hao kukimbia ukeketaji uenda katika kituo hicho kwa ajili ya kupata elimu ya makuzi, hivyo mahitaji na kwamba msada uliotolewa una muhimu mkubwa.

Vitu vilivyotolewa na ACACIA ni Godoro 20, shuka 100,shuka za imasai 100, blanketi 100, taulo za kike(pedi) 1000,sabuni katoni 300, mafuta kopo187 na vitu vingine kadhaa.Pia Meneja huyo ameiomba Kampuni ya ACACIA kusaidia kujenga nyumba za wafanyakazi na wahanga wa matukio hiyo ambapo amesema fedha zinazohitajika ni Sh.488,804,400.

Huku akieleza mafanikio yao tangu kuanzisha kambi hiyo na suala la kutoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike ambapo wameokoa mabinti wengi.Ameongeza pia wamepeleka shule mabinti 102 shule ambao wamekataliwa na wazazi wao kwasababu walikataa kukeketwa na kuunga vikundi kwa Mangariba waliacha kukeketa na kuendelea kutoa elimu hiyo.
  Mkurugenzi wa Ushirika wa ATFGM Masana Sister Stella Mgaya akiongea katika hafla hiyo fupi ambapo ameiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wale ambao watakeketa Mwaka huu.
 Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga Valerian Mgani akitaja mafanikio ya Ushirika huo na kuomba Kampuni ya ACACIA Kusaidia katika ujenzi wa Nyumba za wafanykazi na wahanga wa ukatili kias cha Shilingi488,804,400 ili kukamilisha ujenzi huo.
Kaimu Jamii Endelevu ACACIA Reuben Ngusaru akiongea katika haflya hiyo ya makabidhiano ya msaada huo ambapo amesema maombi lazima ayafikishe kwa Viongozi wake ili kuyafanyia kazi.
   Kaimu Jamii Endelevu ACACIA Reuben Ngusaru akikabidhi baadhi ya vifaa kwa Wasichana hao ambao ni wahanga wa ukatili wa kijinsia Ukiwemo Ukeketaji.
 Baadhi ya vifaa vilivyotolewa katika Ushirika wa ATFGM Masanga na kampuni ya Uchimbaji wa Mawe ya dhahabu ACACIA North Mara Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAMWA, MASHIRIKA YA CANADA,ULAYA WAZINDUA FILAMU INAYOHUSU KUPINGA UKEKETAJI

$
0
0


Na Khadija Seif , Globu ya jamii   .

CHAMA cha Wanawake Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kutoka nchini Canada na mataifa ya Ulaya wamefanya uzinduzi wa filamu inayohusu maisha ya binti wa kike inayojulikana kama  In the name of your daughter.

Uzinduzi wa filamu hiyo umefanyika jana katika ukumbi wa Alliance Francie's jijini dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa  ndani na nje ya nchi.

Filamu hiyo inazungumzia maisha ya watoto wa familia zenye utamaduni wa ukeketaji hasa mkoani Mara wakiwa bado wanaendelea na mila hiyo potofu inayowakandamiza  watoto wa Kike kwakuwa  hawajapata elimu ya kutosha kuhusu athari zake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwakilishi kutoka Serikalini   Grace Mwangwa  amesema jamii bado zinahitaji elimu ya kutosha ili kupiga vita dhidi ya ukeketaji na kwamba Serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirika ili kumkwamua mtoto wa kike kufikia malengo yake.

Mwangwa amesema baadhi ya jamii  wameichukulia  desturi hiyo kama  sheria kwao na watoto wengi hunyanyasika pindi wanapokataa kufanyiwa kitendo hicho na hata kutengwa na jamii kabisa .

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA  Edda Sanga  amesema  chama chao kimefanya juhudi na jitihada na kuona kwa namna moja au nyingine kushirikiana na vyombo vya habari kutokomeza vita hiyo ya ukatili wa kijinsia.

"Kwani kwa kiwango kikubwa mpaka sasa ndoa za utotoni zimepungua kutokana na elimu kufika sehemu mbalimbali pamoja na madhara yake kubainishwa  na kuwepo kwa Sheria kali kwa wanaojihusisha na uhalifu huo wa kumnyima haki za msingi mtoto wa kike,"amesema.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA  Edda Sanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa filamu ya "In The Name of Your Daughter" inayohusu ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike katika Ukeketaji.
Baadhi ya waalikwa wakifuatilia filamu hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAMISEMI Yakabidhiwa Gari Kuboresha Ufanisi Huduma za Afya

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akitiliana saini hati ya makabidhiano ya msaada wa gari aina ya Toyota Landcruser kwa ajili ya  ufuatiliaji wa shughuli za Ukimwi katika ngazi ya jamii na Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii (CHSSP), Dkt. Tulli Tuhuma wakati wa hafla fupi ya kukabidhiana msaada huo leo jijini Dodoma. Kulia ni Mwakilishi wa USAID, Bi. Linda Madeleka. Msaada huo umetolewa kwa TAMISEMI na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID) kupitia mradi wa CHSSP unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la John Snow Inc (JSI).
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Zainab Chaula (kushoto) akakipokea hati ya makabidhiano msaada wa gari aina ya Toyota Landcruser kwa ajili ya  ufuatiliaji wa shughuli za Ukimwi katika ngazi ya jamii leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mwakilishi wa USAID, Bi. Linda Madeleka na Mkurugenzi wa Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii (CHSSP), Dkt. Tulli Tuhuma. Msaada huo umetolewa kwa TAMISEMI na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID) kupitia mradi wa CHSSP unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la John Snow Inc (JSI).
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Zainab Chaula (katikati) akipokea ufunguo wa gari na Mwakilishi wa USAID, Bi. Linda Madeleka wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa gari aina ya Toyota Landcruser kwa ajili ya  ufuatiliaji wa shughuli za Ukimwi katika ngazi ya jamii leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afya toka Tamisemi, Rasheed Maftah. Msaada huo umetolewa kwa TAMISEMI na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID) kupitia mradi wa CHSSP unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la John Snow Inc (JSI).
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Zainab Chaula akiwasha gari mara baada ya kukabidhiwa ufunguo wa gari hiyo na Mwakilishi wa USAID, Bi. Linda Madeleka (hayupo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa gari aina ya Toyota Landcruser kwa ajili ya  ufuatiliaji wa shughuli za Ukimwi katika ngazi ya jamii leo jijini Dodoma. Msaada huo umetolewa kwa TAMISEMI na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID) kupitia mradi wa CHSSP unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la John Snow Inc (JSI).
 Muonekano wa gari aina ya Toyota Landcruser lilolokabidhiwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya  ufuatiliaji wa shughuli za Ukimwi katika ngazi ya jamii leo jijini Dodoma. Msaada huo umetolewa kwa TAMISEMI na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID) kupitia mradi wa CHSSP unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la John Snow Inc (JSI).
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Zainab Chaula(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa gari aina ya Toyota Landcruser kwa ajili ya  ufuatiliaji wa shughuli za Ukimwi katika ngazi ya jamii leo jijini Dodoma. Msaada huo umetolewa kwa TAMISEMI na Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID) kupitia mradi wa CHSSP unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la John Snow Inc (JSI).(Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma).


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

LIVE: OBAMA AKIHUTUBIA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWA NELSON MANDELA

Watalii kutoka nchini Uswisi wakitalii Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli

$
0
0
Watalii kutoka nchini Uswisi Daniel Gehring na Andre Luethi wakitalii Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa muda wa siku saba na kufanikiwa kufika kilele cha juu kabisa cha Uhuru. 

Mawaziri watano wajadili Bomba la Mafuta

$
0
0
Mawaziri kutoka Wizara Tano zinazohusika na utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanzania, wamekutana na wataalam wa Tanzania walio katika Timu ya Kitaifa ya Majadiliano ya mradi ili kupata taarifa ya  utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2020.
Kikao hicho  kilichoongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma ambapo Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba,  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt. Angeline Mabula,  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji.
Viongozi wengine  waliohudhuria ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua,  Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi wa Bandari, Mhandisi Karim Mataka na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo  ya Petroli Tanzania (TPDC),Mhandisi Kapuulya Musomba.
Pamoja na  kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka katika Timu hiyo ya Taifa ya Majadiliano (GNT), Mawaziri hao pamoja na wataalam mbalimbali walijadili changamoto  mbalimbali pamoja na utatuzi wake lengo likiwa ni kutekeleza mradi huo kwa ufanisi ndani ya muda uliopangwa.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( wa Nne kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (wa Tatu kushoto),  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt. Angeline Mabula (wa Tatu kulia),  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde (wa kwanza kulia) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji (wa Pili kulia) wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili mradi wa Bomba la Mafuta jijini Dodoma.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( katikati), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia kwa Waziri wa Nishati),  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt. Angeline Mabula (kushoto kwa Waziri wa Nishati),  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde (haonekani pichani) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji (haonekani pichani) wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili mradi wa Bomba la Mafuta jijini Dodoma. Wengine ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( katikati), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (kulia kwa Waziri wa Nishati),  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dkt. Angeline Mabula (kushoto kwa Waziri wa Nishati),  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira,  Antony Mavunde (haonekani pichani) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji (haonekani pichani) wakiwa katika kikao kilichokuwa kikijadili mradi wa Bomba la Mafuta jijini Dodoma. Wengine ni Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi mbalimbali za Serikali.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MGOMBEA UDIWANI KIMARA KWA TIKETI YA CCM APITA BILA KUPINGWA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam John Kayombo amemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Pascal Manota kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo ulioitishwa nchini katika Kata ya Kimara.

Kayombo  amemtangaza Manota kuwa Diwani Mteule kutokana na madiwani wengine kutoka vyama upinzani kushindwa kujibu hoja za mapingamizi aliyowawekea kama mapungufu wakati wa ujazaji wa fomu.

“Vyama vilivyoweza kuchukua fomu ya kugombea Udiwani katika Kata ya Kimara ni , ACT-Wazalendo, Chadema, CUF na CCM lakini kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika ujazaji wa fomu Pascal Manota namtangaza kama Diwani Mteule aliyepita bila ya kupingwa,”amesema Kayombo.

Kwa Upande wake Manota ambaye ni Diwani Mteule katika Kata ya Kimara amewetaka wapinzani kuacha siasa za uongo za kuwasingizia watendaji kuwa ndio wanaharibu uchaguzi wakati wao ndio wa kwanza kuvunja taratibu za uchaguzi na sharia zilizowekwa.

Amesema wagombea wote walichukua fomu na zikajazwa na kubandikwa katika mbao ya matangazo katika Kata, hivyo baada ya kuona mapungufu ya wagombea wake aliamua kuwawekea mapingamizi.Kutokana na mapingamizi hayo wagombea wote wametupwa nje.


Amesema kuwa sasa anasubiri kuapishwa ili aendelee kuwatumikia wakazi wa Kimara na hatimaye wapate maendeleo ya kweli kupitia Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo , John Kayombo ambaye pia ndio Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri hiyo akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo kuwa Ndugu Pascal Manota kapita bila kupingwa.
Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akisaini kitabu cha kupokea barua ya kuwa Diwani Mteule aliyepita bila kupingw akatika kata ya Kimara.

Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akipokea barua ya kuwa Mshindi wa uchaguzi mdogo kwa kupita bila kupingwa mara baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa mapingamizi

Diwani Mteule wa Chama Cha Mapinduzi Pascal Manota akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kutangazwa mshindi

Wakazi wa Mbagala wapewa elimu kuhusu usaidizi wa kisheria

$
0
0

katika kuwafikia wananchi na kuwaelimisha kuhusu maswala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria , taasisi ya Peoples Development Forum(PDF) chini ya ufadhili wa Legal Services Facility imeendesha Tamasha la burdani na kutoa elimu mbagala mkoani Dar es saalam

katika tamasha hilo elimu juu ya haki katika ujasiriamali na maswala mbalimbali ya haki na sharia ilitolewa na vilevile watoa huduma za msaada wa kisheria (paralegal) kutoka Temeke walipata fursa ya kuongea na wananchi na kuandikisha matatizo yao yanayohitaji msaada wa kisheria

LSF kwa kushirikiana na wadau wake nchi nzima imekuwa ikiwawezesha watanzania kwenye kila wilaya Tanzania bara na Zanzibar kupata msaada wa huduma za kisheria kupitia watoa huduma za msaada wa kisheria bila gharama yoyote

kupitia mradi huu unaofadhiliwa na DANIDA na DFID , LSF imewawezesha wananchi kupata haki zao, utatuzi wa migogoro midogo midogo na msongamano mahakamani, imetoa elimu juu ya maswala mbalimbali ya kisheria na kuelimisha jamii umuhimu wa kulinda haki za binadamu, lakini pia imeshirikiana na serikali, kupitia wizara ya Katiba na Sheria, katika uandaaji na hatimaye kupitishwa kwa sheria mpya ya kutambua wasaidizi wa kisheria nchini (Legal Aid Act 2017).

Lengo kubwa la mradi huu ni kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa jamii maskini hususani wanawake na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuamasisha jamii kuheshimu haki za binadamu.


Bi Stella Singano, mtoa huduma za msaada wa kisheria (Paralegal) kutoka Temeke, akitoa elimu juu ya haki za ujasiriamali kwa wakazi wa Mbagala wakati wa Tamasha la uhamasishaji lililoandaliwa na Peoples Development Forum(PDF) chini ya ufadhili wa LSF.
Kikundi cha sanaa cha Machozi kikitumia sanaa kufundisha jamii kuhusu haki za binadamu na usaidizi wa kisheria katika tamasha lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.
 

MAFUNZO YA WAANDISHI WA HABARI ZA MAHAKAMA YAENDELEA MJINI MOROGORO

$
0
0

 Wakili wa Kujitegemea kutoka Haki Advocates,  Aloyce Komba akitoa Mada ya utoaji wa Habari za Kimahakama kwa waandishi wa Habari za Mahakama wanaoshiriki katika mafunzo ya Uandishi wa Habari za Kimahakama katika Ukumbi wa Magadu mkoani Morogoro. 
Naibu Msajili, Mahakama Kuu,  Augustino Rwizile akitoa mada ya ‘Hatua mbalimbali za Mashauri ya Jinai na Madai’, lengo ni kuwaelimisha zaidi Waandishi hao juu ya hatua/taratibu mbalimbali katika uendeshaji wa mashauri hayo. 
Afisa Tehama kutoka Mahakama ya Rufani-Tanzania, Allan Machella akitoa mada ya ‘Njia kuelekea Mahakama Mtandao, Mipango na Mafanikio.’
Mwandishi wa Nipashe, Hellen Mwango akichangia mada katika mafunzo hayo.
 Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini.
(Picha na Mary Gwera)

NCAA yaweka mikakati kuijaza Dreamliner

$
0
0
Na Ripota Wetu- Arusha
WAKATI Rais Dk. John Magufuli akitoa maelekezo ya kufikia watalii milioni 5 hadi ifikapo mwaka 2020, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeanza utekelezaji wa agizo hilo kwa kukutana na wawekeza katika sekta ya utalii.

Ili kuhakikisha mikakati hiyo inafikiwa Serikali tayari imeleta ndege kubwa Boeing 787 Dreamliner ambayo pamoja na mambo mengine itapanua wigo zaidi wa kubeba wageni wakiwamo watalii kutoka ndani na nje ya nchi.

Wakati mikakati hiyo ikiendelea kutekelezwa na Serikali, NCAA kwa upande wake nao imeanza utekelezaji huo wa kufikia watalii milioni 5 mwaka 2020 kupitia Jukwaa la Uwekezaji katika sekta ya utalii kwa eneo la Ngorongoro.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa hilo lililofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), mjini Arusha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga alisema malengo hayo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
 Naibu Mhifadhi wa NCAA Dk. Maurus Msuha akiwasilisha mada wakati wa Jukwaa la Wawekezaji katika sekta ya utalii kuhusu vivutio vipya vya utalii na uwekezaji kwenye eneo hilo la Ngorongoro.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro Edward Maura akizungumza wakati wa Jukwaa la Wawekezaji wa sekta ya Utalii lililoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mjini Arusha. 
  Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye Bangu akizungumza wakati wa Jukwaa la Wawekezaji katika Sekta ya utalii lilofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga katikati akifuatilia mada wakati wa Jukwaa la Wawekezaji wa Sekta ya Utalii mjini Arusha, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk. Aloyce Nzuki kulia ni Mwenyekiti wa TATO Will Chambulo. 
 Viongozi wa Chama cha Mawakala wa Utalii (TATO), kutoka kushoto Katibu wa TATO Cyril Ako na Makamu Mwenyekiti wa TATO Henry Kimambo wakifuatilia mada kwenye Jukwaa la wawekezaji katika sekta ya utalii lililoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AZINDUA FAO LA USHIRIKA AFYA LA NHIF

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua fao la Ushirika Afya ambalo linawalenga wananchi wanaojishughulisha na kilimo kupitia ushirika.

Amezindua fao hilo jana (Jumatatu, Julai 16, 2018) kwenye mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ulowa katika kijiji cha Kangeme, kata ya Ulowa, Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, Shinyanga.

Waziri Mkuu alikabidhi kadi 20 kwa niaba ya wanachama 259 ambao wamejiunga na mpango huo. Wanachama hao wanatoka katika vyama mbalimbali vya ushirika kwenye Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama.

Amesema katika kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za afya katika hospitali yoyote ile nchini, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, wameamua kuzindua mpango wa Ushirika Afya, ambao unahusisha wakulima walio katika vyama vya ushirika.

“Gharama ya kujiunga na fao hili kwa mwaka ni sh. 76,000 kwa mtu mmoja na sh. 50,400 kwa mtoto mmoja lakini unakuwa na uhakika wa kutibiwa katika hospitali yoyote ile hapa nchini,” amesema.

Amesema takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa Tanzania kuna vyama vya ushirika 10,522 vyenye wanachama 2,234,000 ambapo asilimia 35 ya wanaushirika huwa wanapata magonjwa ya dharura na wanakuwa hawana namna ya kupata fedha kwa haraka.

“Tunatambua wote kuwa fedha ya mkulima ni ya msimu, lakini mkulima ukiwa na kadi ya bima ya afya, utapata matibabu kokote kule hata kama huna fedha taslimu,” amesema.Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kijana aliyebuni mpango huo ambaye anatoka Taasisi ya Ukuzaji wa Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Mwombeki Baregu. 

“Huyu kijana si mwajiriwa wa NHIF, wala siyo mtumishi Serikalini, lakini kwa sababu ya uzalendo, alikuja na huu mfumo akauelezea na kuonesha manufaa yake kwa wananchi wa kawaida, na kwa sababu Serikali yenu ni sikivu, tukaufanyia kazi na leo ninauzindua,” amesema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya bima ya afya mmoja wa wakulima waliopo kwenye Ushirika huo ambapo wanachama 120 wamepatiwa kadi hizo na wanachama 200 wameshajaza fomu za kijiunga

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe mfano wa kadi ya bima ya afya kwa matibabu kwa vyama vya Ushirika wilayani Ushetu
 Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Ushirika Waziri  wa Afya Ummy Mwalimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bernad Konga akizungumzia Fao hilo ambalo litawanufaisha wakulima wa mazao waliopo kwenye vyama vya msingi.
 Wananchi wa kata ya Ulowa wakifuatilia uzinduzi huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Ipigie kura Ngoma Africa Band ishinde award ya kimataifa

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO KATI YA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
*Ahimiza hivyo kujikita kujenga uchumi imara ili wananchi wapate huduma bora.

Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
UKOMBOZI wa sasa kwa vyama tawala katika nchi za Afrika  ni vema wakajikita katika katika kujenga uchumi katika sekta mbalimbali ili wananchi wapate huduma bora.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.John Magufuli wakati akifungua Mkutano wa Vyama vya siasa ambavyo vilivyopigania ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika ambapo vina uhusiano na Chama cha Kikomonisti cha China (CPC) uliofanyika leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Rais Dk.John Pombe Magufuli amesema kuwa chama cha CPC kimekuwa na uhusiano ya muda mrefu na kilisaidia ukombozi katika Afrika kwa kutoa silaha lakini sasa wamekuwa na maendeleo ambapo lazima kujifunza kutoka kwao.

Amesema kuwa nchi za Afrika zitoke katika mnyororo wa unyonyaji na kuingia katika uchumi wa kujitegemea. Amesema kuwa nchi ya China imekuwa ikitoa msaada bila masharti na kwamba kinachofanyika maelewano na msaada unatoka.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika na Chama hicho cha CPC jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally akihutubia katika mkutano huo.
Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ST.ANNE MARIE YAONGOZA KITAIFA SOMO LA UHASIBU

$
0
0
SHULE ya Sekondari St. Anne Marie Academy imefanikiwa kuwa ya kwanza kitaifa kwenye somo la uhasibu katika matokeo ya kidato cha sita.


Pia shule hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya pili kitaifa kwenye masomo ya biashara katika matokeo yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki Zanzibar na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA).



 Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyretabura amesema wanafunzi wake wote 100 waliofanya mtihani huo wamefanikiwa kupata sifa za kujiunga na Vyuo vikuu mbalimbai nchini na nje ya nchi.



 Amesema shule yake imefanikiwa kutoa wamnafunzi 54 kwa daraja la kwanza na la pili.Pia imetoa wanafunzi 45 wa daraja la tatu na kwamba hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyepata daraja la mwisho yaani 0.



 Amesema hiyo si mara yake ya kwanza kwa shule yake kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa kwani hivi karibuni Mkoa wa Dar es Salaam uliipatia Ngao Maalum shule hiyo kama sehemu ya kutambua mchango wake katika kuinua elimu hapa nchini na kuwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaaluma.



 Amesema shule yake ilipewa ngao inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba Best Performing Primary School in Tanzania.



 Ameongeza shule yake pia ilifanikiwa kuingia 10 bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana na kwamba nia yake ni kuwa namba moja kitaifa kwenye matokeo yanayokuja.



Amesema kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka jana walifanikiwa kuwa wa kwanza katika Wilaya ya Ubungo, wamekuwa wa pili Mkoa wa Dar es Salaam na walikuwa wanane kitaifa sasa.


"Hii haitufanyi tubweteke tutapambana kupata nafasi za juu zaidi,"amesema.
Mkuu wa shule ya Sekondari St Anne Marie Academy ya Mbezi kwa Msuguri Dar es Salaam,  Gladius Ndyetabura akiwasomea matokeo ya kidato cha sita wanafunzi wa shule hiyo ambapo shule hiyo imefanikiwa kuongoza kitaifa kwenye somo la uhasibu na kuwa ya pili kitaifa kwenye masomo ya biashara.
 Mkuu wa shule ya Sekondari St Anne Marie Academy ya Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, Gladius Ndyetabura akifurahia matokeo ya kidato cha sita na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutangazwa ambapo shule hiyo imeongoza kitaifa kwenye somo la uhasibu na somo la biashara.


NDC YAANDAA MAONESHO MAKUBWA YA KUKUZA UWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

KAMPUNI ya Phimona Ltd inayojihusisha na ushauri wa biashara na mawasiliano kwa kushirkiana na wadau waliobobea kuhamasisha uwekezaji imetangaza kufanyika kwa Maonesho ya kukuza uwekezaji Tanzania(TIPEC).

Uamuzi huo una lengo la kuitambua , kutengenezea andiko na kuitangaza miradi kwa ajili ya uwekezaji hasa kwa kutambua eneo hilo halijanyiwa kazi kikamilifu. Wakati wa kutangaza maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam mbali ya Phimona pia walikuwa wadau wengine wakiwamo TanTrade, TNBC, EPZA, TCCIA, NDC, TBC na TSN. 

Akizungumzi maonesho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Phimona Rodgers Mbaga amesema kupitia maonesho hayo yanayofahamika kwa jina la TIPEC yatawaleta pamoja wenye miradi inayotafuta wawekezaji na wenye mitaji.

Ameongeza na kwa upande mwingine inawaleta wawekezaji na wenye mitaji kuja kukutana ana kwa ana na wenye miradi. Amesema lengo la maonesho hayo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kutangaza na kukuza uwekezaji wameamua kuaandaa maonesho ili kukuza miradi na kutafuta wawekezaji na wenye mitji.

"TIPEC 2018 itaitambua , kutengenezea andiko na kuitangaza miradi isiyopungua 300 .Ingawa sekta nyingine itatangazwa pia.Mkazo utakuwa kwa miradi ya viwanda na kilimo,"amesema. Mbaga amesema maonesho hayo yatafanyika kuanzia Novemba 14 hadi 16 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Said Tunda akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kufanyika kwa Maonesho makubwa ya kukuza Uwekezaji kuanzia Novemba 14-16, mwaka huu jijini kwa udhamini wa makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN Ltd). Kutoka kushoto kwake ni Mchambuzi wa Mazingira ya Biashara (TNBC), Kabenga Kaisi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko TSN, Goodluck Chuwa, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Phimona Ltd, Rodgers Mmbaga, Meneja Ukuzaji Biashara wa TANTRADE, Stephen Koberou na Meneja Huduma na Uanachama wa TCCIA, Fatuma Hamis.

Madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchini China wafanya upasuaji kwa wagonjwa

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka nchini China wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo lililotobolewa katika paja (Catheterization) wa kuzibua mshipa wa moyo ambao haupitishi damu vizuri kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Kwa mwaka huu wa 2018 madaktari watatu wametolewa na Serikali ya China kwaajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo. 
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo lililotobolewa katika paja (Catheterization) wa kuzibua mshipa wa moyo ambao haupitishi damu vizuri . 
Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao kutoka nchini China wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto mwenye umri wa miaka 13 wa kuziba tundu la moyo na kufungua njia inayopeleka damu kwenye mapafu. Kwa mwaka huu wa 2018 madaktari watatu wametolewa na Serikali ya China kwaajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo. 
Picha na JKCI.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI

$
0
0
Tarime - Mara

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya ya Tarime mkoani Mara kumkamata na kumfungulia mashtaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Richard Tiboche kwa tuhuma za kuikashifu Serikali na kuchochea mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi ya Serengeti na vijiji jirani.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana majira ya saa tatu usiku baada ya kuhitimisha ziara yake wilayani humo iliyolenga kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani ikiwemo kijiji cha Kegonga.

Akiwa njiani majira ya saa tatu za usiku kwenye gari la wazi baada ya kukagua eneo hilo la mpaka kwa zaidi ya masaa sita, Waziri Kigwangalla na msafara wake walikuta lundo la mawe yakiwa barabarani ndani ya eneo la hifadhi hiyo, hali iliyosababisha taharuki kubwa na msafara wake kushuka na kuanza kuondoa mawe hayo ili kupata njia ya kupita.

Wakati zoezi hilo likiwa linaendelea, Kiongozi huyo wa UVCCM alisikika akiituhumu Serikali kwa kuweka mawe hayo na kwamba hayakuwekwa na wananchi wa eneo hilo, jambo lililozua mshangao mkubwa kwa viongozi wa Serikali waliokuwepo katika msafara huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima mtego wa misumari uliotegwa na watu wasiojulikana kwa lengo la kuzuia msafara wake wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Tarime John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa eneo lenye mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro huo mkoani Mara jana. Katikati aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma taarifa mbalimbali kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani vya wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji na hifadhi hiyo jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAANDALIA DHIFA YA KITAIFA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC)

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Dhifa ya kitaifa aliyowaandalia viongozi wa vyama vya siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na Chama cha Kikomunisti cha China cha CPC Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa vyama vya siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na Chama cha Kikomunisti cha China cha CPC wakiwa katika Dhifa hio ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wakiangalia burudani kutoka katika kikundi cha TOT katika Dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.
  Kikundi cha TOT kikitumbuiza katika dhifa hiyo ya kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Mshindi wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 kuchachangia milioni mbili ujenzi wa kituo cha Polisi Mbagala,Temeke.

$
0
0
 Katibu Tawala wilaya ya Temeke Ndugu Hashimu Komba (kwa niaba ya MKuu wa Wilaya),akimkabidhi Kombe la Tatu Mzuka kwa kijana mkazi wa Mbagala,Abeid Amir aliyejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 300,alipokwenda kutambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.Katika mazungumzo yake na Uongozi wa Wilaya mshindi huyo ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi kinachojengwa Mbagala.
 Mshindi wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 Abeid Amir akipokelewa kwa shangwe,nderemo na vifijo  mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Mbagala-Kilungule,ambapo pia alipokelewa vyema na viongozi wa serikali ya Mtaa kwa heshima kubwa.
  Mshindi wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 Abeid Amir akipokelewa kwa shangwe na Diwani wa Kata ya Kilungule Said Fella na akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kata ya Zomboko Ndugu Hemed Said Njiwa,mara alipowasili nyumbani kwao Mbagala-Kilungule
Diwani wa Kata ya Kilungule Said Fella akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kumpokea mshindi huyo wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images