Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara na Kumteua Bw. William Erio

$
0
0
Mkurugenzi Mteule wa NSS Bwa.William Erio


RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UFUNGUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.


RAIS Dk.John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitaifa wa tamasha la maalum la Mwezi wa Urithi kuenzi utamaduni wa Mtanzania ambalo litafanyika nchini nzima kwa kuaza na Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala amesema Serikali kupitia wizara hiyo wameaandaa tamasha hilo ambalo linalenga kuenzi utamaduni na urithi wa Mtanzania na kwamba tamasha hilo linaitwa Urithi Festival ambalo litakuwa likifanyika kila fikapo Septemba ya kila mwaka kuanzia mwaka huu.

"Dhumuni la tamasha ni kuenzi na kunadi kiutalii hazina kubwa ya utamaduni ,mila na desturi za makabila yote nchini ambayo ni zaidi ya 128.Hatua hii inaenda sambasamba na juhudi za Serikali za kuongeza wigo wa mazao ya utalii nchini hususan kukuza matumizi endelevu ya malikale,kutangaza utamaduni , vyakula vya asili , michezo ya jadi na kazi za sanaa mbalimbali.

"Tamasha litaisaida pia kukuza utalii wa ndani na kuongeza wastani wa watalii wa kimataifa kukaa nchini , hatua itakayoleta matokeo chanya kwenye mapato yatokanayo na sekta ya utalii na malikale.Wadau wa mwezi wa Urithi wa Tanzania ni Watanzania wote chini na waliopo ughaibuni .

"Aidha tamasha linawalenga raia wa mataifa mengine wanaoishi Tanzania na watalii wa kimataifa na kwamba tamasha litawashirikisha wadau wote wa utalii,"amesema Dk.Kigwangala.

Kuhusu namna ya kushiriki Dk.Kingwangala amesema Urithi Festival itasheherekewa Septemba yote na kwamba tamasha litafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri ambapo patakuwepo na matukio mbalimbali yakiwamo maonesho ya ubunifu wa sanaa na tamaduni , kazi za wajasiriamali na wadau wa utalii.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA CHA GAKI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha GAKI na kusema amevutiwa na uwekezaji uliofanywa na wamiliki wa kiwanda hicho ambao ni Watanzania.

“Ninawapongeza wazawa walioamua kujenga kiwanda hiki kwa sababu viwanda kama hivi vinasaidia kukuza kilimo hapa nchini, kiwanda hiki kinachambua pamba na kusindika mafuta,” alisema.

Ametoa pongezi hizo jana jioni (Ijumaa, Julai 13, 2018) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya GAKI Investment pamoja na wananchi waliofika kumsikiliza mara baada ya kukagua utendaji kazi wa kiwanda hicho kilichopo Manispaa ya Shinyanga.

Waziri Mkuu alisema amevutiwa na ujenzi wa kiwanda hicho kwa sababu kinatoa uhakika wa soko la pamba ikizingatiwa kwamba mikoa yote inayolima zao hilo, mwaka huu imezalisha pamba kwa wingi kuliko kawaida.

“Mwitikio wa wakulima wa zao la pamba unaonyesha kwamba bado wana imani na Serikali yao na ndiyo maana nimewaonya wajumbe wa bodi ya SHIRECU kuwa wajihoji kama kweli wameomba nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi,” alisema.

“Msije mkadhani kuwa SHIRECU ni mahali pa kuganga njaa. La hasha! Ni mahali pa kukuza soko la pamba. Tunataka viongozi wa sasa watambue kuwa hawajaenda SHIRECU ili kushiba, lazima walete mabadiliko kwenye ushirika na kama hawawezi waachie ngazi,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwangongo wilayani Kishapu, Julai 13, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pamba inayosubiri kuchambuliwa wakati aliootembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Gaki kilichopo mjini Shinyanga Julai 13, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda, Gaspar Kileo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kuchambua pamba wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Gaki Invesiment cha mjini Shinyanga, Julai 13, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendanji , Gaspar Kileo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mbengu za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Gaki Investment kilichopo mjini Shinyanga Julai 13, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho, Gaspar Kileo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DStv wanakuambia hivi, moto hauzimwii

$
0
0
Utakuwa ni wakati wa burudani ya aina yake ,kuanzia Julai 13 hadi 31, kila mteja wa DStv ambaye akaunti yake iko hewani atazawadiwa chaneli zote za michezo na za Watoto buree kabisa!

Amini usiamini…., utashuhudia mieleka na mbio za magari za langalanga(Formula 1) kupitia Supersport 1,2,3,4,5,6,7 na 8.

Ofa hii haijawaacha Watoto kwani nao wataweza kushuhudia katuni mpya za peppa pig/munki and trunk na cloudy with a chance of meetballs kupitia Cartoon network, Disney, Nickleodeon na Cbeebies.

Hii si ya kukosa…….. au vipi?

Hakikiksha tu akaunti yako haijakatika na kama imeatika wahi kulipia akauti yako leo usipitwe na ofa hii ya aina yake!

Kumbuka ni chaneli zote za Supersport na katuni (Watoto) bila kijali kifurushi ulichopo.Unangoja nini?

#KamaSioDStvPotezea

BREAKING NYUUUUZZZZZZ.....: MBUNGE WA TUNDUMA ATIWA MBARONI MCHANA HUU

$
0
0
Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka amekamatwa na Polisi muda huu na kuwekwa rumande katika kituo cha Polisi Tunduma mchana huu, taarifa kamili juu tukio hilo zitakujia hapa hapa.

WATU WAWILI WADAIWA KUPOTEZA MAISHA AJALI YA GARI LA HALMASHARI YA WILAYA YA MEATU

$
0
0
 Gari la halmashauri ya Meatu limepata ajali eneo la mkiwa Ikungi likitokea Dodoma lilikuwa na madiwani na mkurugenzi wa halmashauri ya Meatu, inadaiwa kuwa ndani ya gari hiyo kulikuwa na watu 8 watu wawili wamefariki dunia ila bado haithibitishwa majina yao. Globu ya jamii inaendelea kufuatilia tukio hilo na tutaendelea kuwajuza kadri taarifa zitakavyotufikia.

POLISI WASTAAFU WAPATIWA ELIMU YA MIKOPO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Askari Polisi Wastafu(TAPOA) Kamishna mstaafu Suleiman Kova akizungumza katika ufunguzi wa semina ya wastaafu hao ambapo walipatiwa elimu ya kupata mikopo ya kustaafu na benki ya Azania.
Meneja wa huduma za mikopo kutoka benki ya Azania Thobias Samwel akizungumza na wanachama wa Chama cha Askari Polisi Wastafu(TAPOA) wakati wa semina maalum ya kuwapatia elimu ya kupata mikopo ya kustaafu.
Wanachama wa Chama cha Askari Polisi Wastafu(TAPOA) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina maalum ya kuwapatia elimu ya kupata mikopo ya kustaafu iliyotolewa na benki ya Azania wakati wa kikao chao jijini Dar es Salaam.(Picha na Jeshi la Polisi)

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAFUTA YA KULA CHA JIELONG CHA SHINYANGA NA KUKUTA SHEHENA KUBWA YA MAFUTA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ndoo za mafuta ya kula yaliyotokana na mbegu za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya mbegu cha JIELONG, nje kidogo ya mji wa Shinyanga Julai 14, 2018. Wapili kushoto ni Meneja wa kiawanda hicho Gemin Shoo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ndoo za mafuta ya kula yaliyokamuliwa kutokana na mbegu za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya mbegu cha JIELONG nje kidogo ya mji wa Shinyanga Julai 14, 2018. Kushoto ni Meneja wa kiwanda hicho, Gemin Shao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mafuta ya kula yaliyotokana na mbegu za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya mbegu cha JIELONG kilichopo nje kidogo ya mji wa Shinyanga, Julai 14, 2018.


WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA WAWEKEZAJI SEKTA YA UTALII

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dr. Joseph Chilongani. 
RC Mtaka (kulia) akizungumza na askari wa FCF. 
Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Siasa ya mkoa wa Simiyu na wilaya ya Meatu wakianza ziara kukagua Ranchi ya Wanyamapori ya Mwiba na Makao WMA. 
Hafla hiyo ikiendelea. 

Na Joachim Mushi, Arusha

WAKAZI wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani, wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotokana na uwekezaji wa kampuni ya Kitalii ya Mwiba Holding Ltd ambayo imewekeza katika pori la akiba la Meatu linalopakana na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro. Akizungumza katika ziara ya kamati ya ulinzi na Usalama mkoa wa Simiyu na kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Simiyu na wilaya ya Meatu katika eneo la mwekezaji huyo, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema uwekezaji wa kampuni hiyo umekuwa na faida kubwa kwa wananchi na taifa.

Mtaka alisema, kampuni hiyo ambayo imewekeza katika eneo la hifadhi ya Jamii ya wanyamapori (WMA) ya Makao na eneo la Ranchi kijiji cha Makao, licha ya kutoa malipo ya vijiji saba vinavyozunguka hifadhi hiyo kiasi cha sh 610 milioni kila mwaka pia anachangia misaada mingine ikiwepo kutoa ajira. Alisema kampuni hiyo, pia imekuwa ikichangia shughuli za maendeleo na hivi karibuni, imetoa saruji mifugo 3000, mabati 1000 na zaidi ya sh 115 milioni kwa ajili ya kuchangia mfuko wa elimu wa mkoa.

"kama kulikuwa na mahusiano mabaya baina ya vijiji na serikali na wawekezaji hawa ambayo yalitokana na makosa ya watu wachache miaka ya nyuma sasa tumeanza ukurasa mpya," alisema.

Awali Mmoja wa Wakurugenzi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo kampuni zake ndizo zimewekeza katika wilaya hiyo ya Meatu, Abdulkadir Mohamed, alisema hadi sasa kampuni zao, Mwiba Holding, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) na Wingert Safaris wamewekeza zaidi ya bilioni 670 na mwaka huu wataongeza sh 227 bilioni.

"tunatarajia kuongeza uwekezaji ila tunachoomba mazingira bora ya uwekezaji kuondolewa migogoro katika maeneo yetu, ikiwepo uvamizi wa mifugo na kama kuna mapungufu tuelezwe," alisema.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo, alisema chama cha mapinduzi kwa sasa hakina mgogoro na wawekezaji kwani mapungufu yaliyokuwepo yamekwisha na mafanikio yanaonekana. Hata hivyo, Mwenyekiti huyo, alishauri Mwekezaji huyo, kusaidia ujenzi wa mabweni kwa wanawafunzi wa kike katika shule ya Sekondari ya Makao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha wafugaji taifa, Jackson Yuma alitaka uongozi wa serikali kutokubali eneo la makao liharibiwe kwa kuruhusu mifugo kwani ndani ya mwaka mmoja hali itakuwa mbaya. Yuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa CCM mkoa wa Simiyu, alitaka serikali kwa kushirikiana na wawekezaji kuhakikisha maeneo yaliyotengwa katika uhifadhi yanatunzwa kwa gharama zote kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga Kata ya Kisanga wilaya ya Sikonge tarehe 12 Julai, 2018. Wengine wanaoshuhudia ni Viongozi Waandamizi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Sikonge, REA, TANESCO, Wakandarasi pamoja na wananchi.

NA RHODA JAMES - SIKONGE 

WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, jana tarehe 12 Julai, 2018 amewasha rasmi umeme katika kijiji cha Kisanga kata ya Kisanga wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora.  Waziri Kalemani amewasha umeme huo baada ya kufanya uzinduzi wa mradi husika mwaka jana wilayani Sikonge. 

“Leo nimekuja kuwasha umeme, kukagua utekelezaji wa mradi wa REA hapa Sikonge na kuwakabizi Wakandarasi ili kumalizia vijiji vilivyobakia,” alisema Waziri Kalemani. 

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Kalemani alisema kuwa Wilaya ya Sikonge ina jumla ya vijiji 71 na hadi sasa vijiji 30 tayari vina umeme ingawa sio kikamilifu, vijiji 40 vilivyobakia vyote vitapelekewa umeme. Aliongeza kuwa, mradi huu wa REA III awamu ya kwanza takriban vijiji 26 vitaletewa umeme, vijiji 4 vipo off gridi kwa hiyo vitapatiwa umeme wa Jua (Solar) na vijiji vingine 11 vilivyobakia vitaendelea kuunganishiwa umeme. 

“Wakandarasi hawa watawaletea umeme Kijiji kwa Kijiji, Kitongo kwa Kitongoji, Nyumba kwa Nyumba bila kuruka nyumba yoyote” alisisitiza Waziri Kalemani. 

Pia, Waziri Kalemani aliendelea kuwahimiza Wafanyakazi wa Halmashauri kutenga pesa kwa ajili ya kuunganishia umeme Taasisi zote za Umma. Alisema kuwa, ikiwa suala la kutenga pesa hiyo itakuwa ngumu basi, Ofisi zenye chumba kimoja hadi vitatu wekeni kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho hakihitaji wiring ili taasisi zote za umma zipate nishati hii ya umeme. 

Aidha kwa upande wake, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakuda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge alimshukuru sana Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kwa ushirikiano mkubwa anaoendelea kumpa na kusema kuwa wananchi wa Sikonge wanahitaji umeme ili kuendelea kufungua Viwanda vidogo vidogo na hata kuboresha kipato cha kiuchumi katika miongoni mwao. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akijiandaa kukata utepe na kuwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakuda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sikonge.
Wananchi wa kijiji cha Kisanga wakisalimia viongozi waliofika katika kijiji hicho.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga akiwasalimia wananchi katika mkutano huo wa kuwasha umeme katika kijiji cha Kisanga Kata ya Kisanga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Gidion Kaunda akiwasalimia wananchi kabla ya zoezi la kuwasha umeme.

VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kunatarajia kufanyika mkutano wa kidunia wa vyama vya siasa pamoja na kikao maalum cha Afrika ambapo zaidi ya washiriki 130 wanatarajia kushiriki mkutano huo utakaofanyika jiini Dar es Salaam.

Akizungumzia mkutano huo katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema CCM imepata heshima kubwa ya mwenyeji wa mkutano huo wa kidunia.

Tunapenda kuujulisha umma wa watanzania kuwa tarehe 17-18 Julai 2018 kutafanyika Mkutano wa Kidunia wa Vyama vya Siasa, Kikao Maalum cha Afrika, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huu utaleta zaidi ya vyama vya siasa 38 kutoka Afrika na zaidi ya washiriki 130 kutoka nje ya Afrika,"amesema.

Amefafanua mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba mkutano huo ni sehemu ya matokeo mazuri ya utendaji kazi wa uongozi wa awamu ya tano ya Chama na Serikali chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk.John Magufuli.

Pia amesema mkutano huo wa kihistoria na wa kwanza kufanyika Barani Afrika ni wapili kufanyika baada ya mkutano kama huo wa kidunia kufanyika Jijini Beijing, China Desemba mwaka 2017. Mkutano huo wa Desemba mwaka 2017 uliandaliwa na Chama Cha Kikomunisti Cha watu China (CPC) na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu alikuwa ni Kamaradi Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.

Polepole amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa pamoja na wajumbe wengine wa mkutano ni Kamaradi Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China, Xu Luping Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu wa Kidunia wa Vyama vya Siasa ni Kamaradi John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NSSF KUTOA PENSHENI YA UZEENI KWA WALE WOTE WALIO SEKTA ISIYO RASMI PINDI WATAKAPOKUWA WANACHAMA

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadji ya Jamii(NSSF) limejipanga kutoa pensheni ya Uzeeni kwa watanzania wote walio katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi 

Hayo yalisemwa katika mkutano baina ya NSSF na viongozi wa vikundi vya uzalishaji mali Mkoani Morogoro jana. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe uliofanyika katika ukumbi wa NSSF Mafao Haouse 

Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Morogoro aliwaasa wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kama vile Mama Lishe, bodaboda, wafugaji, wakulima n.k kubadili mtazamo wa maisha ili kuepukana na changamoto za uzeeni kwa Kujiunga na NSSF kwani watapata pensheni ya uzeeni kama wale walio katika sekta rasmi 

Nae Mweneykiti wa Kamati ya kuratibisha Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi Bi Mariam Muhaji alisema, pensheni ya uzeeni ni haki ya kila Mtanzania hivyo ni wakati sasa kwa wale wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na NSSF ili kufaidika na Mafao mbalimbali yatolewayo ikiwemo pensheni ya uzeeni. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Stephen Kebwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Vikundi vya uzalishaji mali Mkoani Morogoro.
Meneja wa NSSF Shinyanga Ndugu Omary Mziya akizungumzia kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii wakati wa Mkutano na Viongozi wa Vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali Mkoani Morogoro
Viongozi mbalimbali wa Vikundi wakiwa katika mkutano ulioratibiwa na NSSF kwa ajili ya elimu kuhusu Hifdahi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi

MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha  Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Jenerali Ahmed anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo kwa kuwa msaidizi mkuu wa majeshi nafasi ambayo haikuwa kushikwa na mwanamke katika masuala ya ulinzi na usalama nchini humo.

Katika hafla hiyo Kenyata alieleza kuwa amemchagua ili awe kioo kwa wanawake nchini humo na kuthibitisha kuwa hakuna kinachoshindikana.

Aidha alieleza kufurahishwa na namna jeshi la Kenya linavyofanya kazi hasa katika kulihudumia taifa bila kujali dini, itikadi wala rangi, wamekuwa waaminifu katika kuhudumia taifa hilo lenye watu 42 milioni.

Naye Jenerali mteule amemshukuru Rais Kenyata kwa uteuzi huo na kueleza kuwa: "Ninafuraha sana kwa nafasi mpya niliyochaguliwa na inaonesha namna Rais anavyothamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu" alieleza Jenerali Fatuma.

Jenerali Fatma Ahmed alianza kushika kasi mwaka 2015  baada ya kuchaguliwa kuwa  brigedia wa jeshi nafasi ambayo haikuwahi kushikwa na mwanamke nchini humo.

Jenerali Fatuma ametumikia jeshi la ulinzi la Kenya kwa zaidi ya miaka 30 kuanzia miaka ya 1983.
 RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha  Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.
 RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha  Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

MZIGO MPYA WA ENGINE KUTOKA UK UMEINGIA

$
0
0
Tumeingiza mzigo mpya kutoka U.K tuna Engine zifuatazo....
DISCOVERY 3 ENGINE T.Sh.9.5 Milion
DISCOVERY 2 Td5 ENGINE T.Sh.4.5 Milion.
DISCOVERY 1 Tdi 300 AND Tdi 20O ENGINE T.Sh.4.5 Milion
DEFENDER ENGINE T.Sh.4.5 Milion.
LAND ROVER 110 ENGINE T.sh. 2 Milion
FREELANDER ENGINE T.Sh. 2 Milion
Kwa maelezo zaidi wasiliana na sisi 
Tell+255674616474
Tell+255779100064
On WhatsApp +447723550406



PADRI AUGUSTINO RAMADHAN AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MKE WA PROFESA SHABA

$
0
0
 Padri wa Kanisa la Anglikana, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Elizabeth Shaba mke wa Profesa James Shaba aliye patwa na mauti Julai Mosi mwaka huu na kuzikwa Julai 7, Chicago, Marekani. Ibada hiyo imefanyika leo kwenye Kanisa la St Albano Angilkana, jijini Dar es Salaam.

Marehemu ambaye alikuwa anaishi na mumewe nchini Marekani mpaka anakutwa na mauti alikuwa Muuguzi Mshauri wa Ubalozi wa Kanada. Alioana na Profesa Shaba mwaka 1963. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakishiriki kwenye Ibada hiyo
 Anna Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, akishiriki katika Ibada hiyo


Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake

$
0
0
 Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kushoto) akisaini taarifa ya makabidhiano ya ofisini na mtangulizi wake Bw. Kailima Ramadhani ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kushoto) akikadhiwa sehemu ya makabrasha ya ofisini na mtangulizi wake Bw. Kailima Ramadhani ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Baadhi ya Wakuu wa Idara za Tume ya Taifa ya Uchaguzi  wakishuhudia utiaji saini wa taarifa ya makabidhiano ya ofisini kati ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kulia) na mtangulizi wake Bw. Kailima Ramadhani ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


KANGI LUGOLA ATEMBELEA KITUO KIKUU CHA UZALISHAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA KIBAHA, MKOANI PWANI

$
0
0
 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimuuliza swali, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho, Alphonce Malibiche (kushoto), wakati wa ziara ya kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.Wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Andrew Masawe.
 Mkurugenzi  Mkuu wa Idara ya Uzalishaji Vitambulisho, Alphonce  Malibiche, akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.Wakwanza  kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida),Andrew Masawe
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Andrew Masawe  wakati wa ziara yake ya kikazi  kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(Nida), baada ya kuwasili  Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(Nida), baada ya kutembelea Kituo Kikuu cha Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa,kilichopo Kibaha,Mkoani Pwani.Wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Andrew Masawe Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


MAKAMBA ATOA MILIONI 46 ZA MFUKO WA JIMBO KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE

$
0
0
ZAIDI ya Sh.milioni 46 kutoka Mfuko wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoani Tanga zimegawiwa kwenye kata 18 za jimbo hilo ili kuweza kuchangia kasi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Bumbuli ni Jimbo linaloongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulia Mazingira na Muungano January Makamba. 

Kwa mujibu wa Katibu wa Mbunge wa Jimbo hilo,Hozza Mandia alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na miradi ya huduma ya maji, ujenzi wa madarasa, zahanati na matengenezo ya barabara. Mandia alitaja mchanganuo wa pesa hizo zilizotolewa kuwa kata ya Kisiwani imepata jumla ya sh. Milioni 4 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa mradi wa huduma ya maji, wakati ambapo kata ya Tamota itapatiwa Sh. Million 3 kwa ajili ya ujenzi wa zahanatati katika kijiji cha Ngwelo. 

Miradi mingine ni mradi wa zahanati katika kijiji cha Tekwa ambao mfuko umechangia Sh. Milioni 1.44, mradi wa zahanati kwemsambia aruji yenye thamani ya Sh 675,000, saruji ye thamani kama hiyo kwa mradi wa ujenzi wa darasa shule ya msingiya kivilu na saruji nyingine yenye thamani sh. 700,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ya kata ya Kwemkomole. 

Kata ya Dule B itapata mchango wa jumla ya Sh. Milioni 3.42 milioni kwa ajili ya miradi mbalimbali, , wakati ambapo kata ya Mamba imepata jumla ya Sh. Milioni 3.4, Bumbuli (Sh. 2.99 milioni), Vuga (Sh. 2.97 milioni) na Mponde (Sh. 2.25 million). 

Diwani wa Kata ya Vuga Jumaa Dhahabu alisema kuwa fedha hizo zitawasaidia kuweka lenta kwenye jengo la zahanati pamoja na kuweka sakafu kwenye chumba cha darasa kinacho tumika kwaajili ya maabara ya sayansi na kuweka miundombi katika darasa ,mabara hiyo ameongeza kwa kusema anamshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwanamna anavyoendelea kuwasaidia katiaka kata ya vuga Hata hivyo alisema kuwa serikali iliwapatia sh. Million 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kata ya kwemkomole , hivyo fedha hizo zitawasaidia kusafisha jengo hilo nakwamba kama viongozi wa kata hiyo tayari wamepokea mifuko 200 ya saruji kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo January Makamba ambayo itapelekwa kwenye madarasa naa zahanati .

DAWASCO TEMEKE KUMALIZA KERO ZA MIVUJO YA MAJI

$
0
0
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), limejipanga kuondoa kero ya mivujo ya Maji katika mitaa yote ya Wilaya Temeke ambayo imekuwa ikiripotiwa na wakazi pamoja na viongozi wa serikali za mtaa katika wilaya hiyo.

Hayo yamebainshwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Temeke Bw. Xavery Ndondole katika kikao chake na viongozi wa serikali za mitaa cha kujadili huduma ya Maji katika wilaya hiyo ambapo ameeleza kwamba mivujo mingi inatokana na miundombinu chakavu inayoshindwa kuhimili msukumo wa Maji yaliyoongezeka katika maeneo mengi.

“Maji ni huduma ya msingi na hayana mbadala ni lazima tuzuie upotevu wa Maji ili wananchi wengine wasioyapata wapate kuyatumia hivyo nawaomba tushirikiane kwa kutoa taarifa muda wowote pale unapokutana na mivujo ya aina yoyote katika eneo lako na sisi Dawasco tutafika fika na mafundi wetu kwa wakati” alisema Ndondole

Hata hivyo mwenyekiti wa Kata ya Keko Bw. Shilingi S. Shilingi ameeleza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya Mafundi kutoka Dawasco kufanyia ukarabati mivujo mikubwa peke yake na kupuuzia taarifa za mivujo midogo midogo katika mitaa nakulekea madimbwi na mitaro kujaa.

“Mivujo imekuwa kero na hata gari zenu zinapita huko mitaani kwetu wanafika ila bado kuna mabwawa, mivujo ni mingi ila mafundi wenu wanafanyia kazi mivujo mikubwa lakini midogo wanaacha bila kufanya chochote nahii ndo mingi huko kwetu” alisema Shilingi.

Pia katika kikao hicho uongozi wa Dawasco Temeke umewaomba viongozi hao wa serikali za mitaa kutoa ushirikiano kwa wananchi wanaohitaji huduma ya Maji kwa kuwapa fomu za utambulisho ili waweze kuunganishiwa huduma ya Maji kwa wakati.

UTUNZAJI WA FUKWE KUTALETA WATALII WENGI NCHINI- TTB

$
0
0
 Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini(TTB) Ernest Mwamwaja akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Ramada Resort Dar es Salaam Barath Swarup wakifanya usafi kwa pamoja katioa fukwe ya Hotel hiyo uliofanyika kwa ushirikiano wa pamoja leo Jijini Dar es Salaam.
Usafi ukiendelea ndani ya fukwe Ramada Resort Dar es Salaam  wakiwa pamoja na Raia wa Ufaransa anayeishi katika Visiwa vya Reunion JeanMart Francois akishirikiana na Wafanyakazi wa TTB na Ramada kufanya usafi.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) pamoja na wafanyakazi wa Ramada Resort Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa usafi uliofanyika kwenye fukwe ikiwa na lengo la kuzitumia kama vivutio kwa watalii.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kutambua umuhimu wa vivutio vingi zaidi nchini mbali na wanyama pori wamekeza msisitizo zaidi katika utalii wa fukwe na majiji hususani Dar es Salaam. TTB wameanza na wadau wa mahoteli ya kitalii Jijini Dar es Salaam kwa kufanya usafi kwa pamoja kwenye fukwe ilyopo Hotel ya Ramada na fukwe za jirani. Kwa pamoja TTB na wadau wengine watakutana katika kikao kitakachofanyika Julai 19 mwaka huu kitalenga zaidi kutafuta njia mbadala ya kuzuia takataka zisiingie baharini.

Akizungumza baada ya kumaliza usafi, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Ernest Mwamwaja amesema lengo kuu la kufanya usafi huu ni katika kuhakikisha wanaboresha fukwe zote na majiji ili kuweza kuwa kivutio kwa watalii nchini. Mwamwaja amesema kuwa, ukiachilia mbuga za wanyama ambazo zipo nchini, fukwe za bahari kwa upande mwingine zinatakiwa ziwe safi ili kuvutia zaidi watalii pindi wanapokuja nchini.

Amesema kuwa, kama watalii watakuwa wanavutiwa na mazingira ya Fukwe ifikapo mwaka 2020 tunaweza kufikia wastani wa watalii Milioni 2 kwa mwaka pamoja na pato la taifa kuongezeka kutoka Dola Bilion 2.1 hadi 4.2 kwa mwaka.

 Kaimu Meneja wa Utalii Bodi ya Utalii Nchini Joseph Sendwa amesema kuwa kikao na wadau kitakachofanyika mwezi huu kitaleta maboresho makubwa sana katika sekta ya utalii kwakuwa kwa pamoja watatoka na azimio la kuhakikisha wanafanya usafi katika fukwe zote ikiwemo kwenda maeneo ya makazi ya watu yanayopita mkondo wa bahari ambapo kumekuwa na changamoto kubwa ya wananchi kutupa taka ovyo.

Mbali na hilo, Sendwa amesema wameanzia katika fukwe ya Ramada ila wataenda sehemu zote za Dar es Salaam ikiwemo pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utunzaji wa mazingira.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images